MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Nukuu]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ 2024-04-27T08:55:22Z MyBB MwlMaeda]]> 2023-01-15T13:06:14Z 2023-01-15T13:06:14Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2882 <![CDATA[NADHARIA ZA UHAKIKI WA FASIHI]]>
.pdf   Nadharia Za Uhakiki Wa Fasihi.pdf (Size: 296.97 KB / Downloads: 1) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2022-05-28T10:29:28Z 2022-05-28T10:29:28Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2584 <![CDATA[AINA ZA ALOMOFU]]>
.pdf   Aina za Alomofu.pdf (Size: 79.2 KB / Downloads: 9) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2022-05-24T05:31:30Z 2022-05-24T05:31:30Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2579 <![CDATA[MATUMIZI YA ALAMA ZA KIFONETIKI KATIKA KAMUSI]]>

.pdf   3136-9356-1-PB.pdf (Size: 354.12 KB / Downloads: 9) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2022-01-04T04:10:04Z 2022-01-04T04:10:04Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1987 <![CDATA[‘MGOGORO’ KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI]]> ‘MGOGORO’ KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI
Mgogoro” katika ushairi wa Kiswahili umekuwapo kwa zaidi ya miaka kumi sasa. Una misingi yake katika utata wa mambo mawili:
(i) Maana ya jumla ya shairi
(ii) Maana ya shairi la Kiswahili.
Mvutano huu, sawa na uk tulioutaja katika nchi za Ufaransa, Uingereza na Marekani, una pande kuu mbili. Upande mmoja wapo wanamapokeo ambao wanasisitiza kuwa vina na urari wa mizani ni roho ya ushairi wa Kiswahili.2 Upande wa pili wako wanamabadiliko, washairi wa kisasa, ambao wanaeleza na kuthibitisha kuwa si lazima shairi liwe na vina na urari wa mizani ndipo liitwe la Kiswahili.
“Tatizo” lilianza rasmi katika miaka ya mwisho ya sitini na mwanzoni mwa miaka ya sabini walipotokea “watundu” watatu: Ebrahim Hussein, Euphrase Kezilahabi na Jared Angira. Hawa waliandika na kusoma mashairi kwa lugba ya Kiswahili bila kujali kanuni zilizo “uti wa mgongo” wa ushairi wa Kiswahili kwa wanamapokeo. Baadaye waliungwa mkono na washairi wengine kama akina M.M. Mulokozi, K.K. Kahigi, na hivi karibuni Henry Muhanika na Theobald Mvungi. Baadhi ya wanamabadiliko hawa hali kadhalika wameandika nadharia za ushairi za kuonyesha kuwa si lazima shairi la Kiswahili libanwe na kanuni na sheria hizo. Jambo ambalo wanamapokeo kama vile Jumanne Mayoka na Abdilatif Abdalla hawakuzingatia katika vita vya maneno baina yao na wanamabadiliko ni kwamba akina Kezilahabi, Kahigi, Mulokozi na wenzao hawana vita na ushairi wa Kiswahili unaofuata hizo sheria. Kwa mfano, katika diwani ya Mulokozi na Kahigi ya Malenga wa Bara3 zaidi ya nusu ya mashairi yao ni ya kimapokeo yafuatayo “sheria” za vina na mizani! Jambo walilolisisitiza watundu hawa ni kuwa kila kitu na kila kiumbe duniani daima kiko katika mwendo wa mabadiliko; na kuwa fani ya ushairi wa Kiswahili pia isingesimama tisti tu katika mzingo wa “sheria” daima dumu. Walilotilia mkazo basi, ni kuwa uwanja wa ushairi wa Kiswahili uyakubali mabadiliko ya fani zilizotumiwa na washairi kueleza maudhui mapya.
Kwa kueleleza kiini cha mgogoro huu, tutatoa maana za ushairi zilivyoelezwa na wanamapokeo na zile za wanamabadiliko. Baada ya hapo tutazichuja zote na kutoa maana tuonayo kuwa inafaa zaidi.
Shaaban Robert, ambaye tunaweza kumchukua kuwa kielelezo cha waumini wa ushairi wa kimapokeo, alitoa maana ifuatayo ya ushairi:
Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Zaidi ya kuwa sanaa ya vina ushairi una ufasana wa maneno machache au muhutasari… Wimbo ni shairi dogo, sbairi ni wimbo mkubwa na utenzi ni upeo wa ushairi… kina ni mlingano wa sauti za herufi. Kwa maneno mengine huitwa mizani ya sauti, na ufasaha ni uzuri wa lugha. Mawazo, maono na fikira za ndani zinapoelezwa kwa muhtasari wa ushairi huvuta moyo kwa namna ya ajabu.4
Kabla ya kuichambua maana hii ya ushairi, tuangalie maana zingine zilizo na welekeo sawa na wa hiyo ya Shaaban Robert.
Mathias Mnyampala, ambaye aliishi enzi za Shaaban Robert pia, aliueleza ushairi hivi:
Ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kaie. Ndicho kitu kilicho bora sana katika maongozi ya dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa mizani na vina maalumu kwa shairi.5
Nayte Abdilatif Abdalla kaueleza ushairi kuwa:
Utungo ambao katika kila ubeti wake kuna ulinganifu wa vina vitukufu vilivyopangwa kimoja baada ya chenziye; wenye vipande vilivyo na ulinganifu wa mizani zisizo pungufu wala zilizo zaidi; na vipande hivyo viwe vimetandwa na maneno ya mkato maalum na yenye lugha nyofu, tamu na laini, lugha ambayo ni tetelezi kwa ulimi kwa kuitamka, lugha ambayo ina uzito wa fikra, tamu kwa mdomo wa kuisema, tumbuizi kwa masikio ya kuisikia na yenye kuathiri moyo uliokusudiwa na kama ulivyokusudiwa.*
Katika maana hizi za ushairi kuna mambo kadhaa yanayoibuka. Kwanza kabisa, kipengele cha lugha kinatiliwa mkazo na washairi wote hao waliojaribu kueleza maana ya ushairi japo kwa mitazamo tofauti tofauti. Shaaban Robert anasisitiza kuwa shairi zuri halina budi kuwa na ufasaha wa lugha. Naye Mathias Mnyampala anakieleza kipengele hiki kwa kusema kuwa ushairi lazima utumie “maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata.” Abdilatif hatofautiani na wenawe kwani naye pia kasisitiza kuhusu “maneno ya mkato maalum na yenye lugha nyofu, tamu na laini.”
Kwa jumla basi, wanamapokeo hawana ugomvi wowote na washairi wa kisasa kuhusu kipengele cha lugha. Wote wanakubaliana kuwa lugha ya ushairi haina budi iwe ya mkato na ya ufasaha.
Jambo hili tunaliona tujaribupo kuchunguza maana za ushairi kama zilivyotolewa na wanamabadiliko. Tutadondoa maana hizo kama zilivyotolewa na M.M. Mulokozi na E. Kezilahabi, ambao tunaweza kuwachukulia kama wawakilishi wa wanamabadiliko. Kezilahabi anasema:
Ushairi ni tukio, hali au wazo ambalo limeonyeshwa kwetu kutokana na upangaji mzuri wa maneno ya fasihi yenye mizani kwa kifupi ili kuonyesha ukweli fulani wa maisha.7
Naye M.M. Mulokozi ametoa maana ya ushairi kuwa ni:
… mpangilio maalumu wa maneno fasaba yenye muwala, kwa lugha ya mkato, katika usemi, maandishi au mahadhi ya wimbo, ili kueleza wazo au mawazo, kufunzaau kuelezajambo au hisi fulani kuhusu maisha ya binadamu kwa njia inayoburudisha na kugusa moyo. 8
Mgogoro uko katika matumizi ya urari wa mizani na vina, kwam wanamapokeo wanashikilia kuwa vipengele hivi ni vya lazima; kuwa ni sheria za kutumiwa katika ushairi, hususan ule wa Kiswahili. Kwao vina na urari wa mizani ni uti wa ushairi wa Kiswahili. Haya yamepigiwa muhuri na mfuasi mkuu wa tapo hili Jumanne M. Mayoka, ambaye akiwa kajawa na jazba alisema haya kuhusu mashairi ya kitabu chake cha Mgogoro Wa Ushairi na Diwani ya Mayoka:
Katika kitabu hiki, tungo kama za Kezilahabi, Kahigi, Mulokozi na wengineo watungao tungo tutumbi zisizokuwa na sanaa yoyote nimezitupa pembeni… Mwundo wa mashairi yote yaliyomo kitabuni humu ni wa asili ya Kibantu. Kila utungo wa shairi umefungika upande wa mistari: ni lazima kila ubeti wa shairi uwe na idadi maalumu ya mistari; umefungika upande wa vina: ni lazima mistari iwe na vina; umefungika upande wa mizani: ni lazima kila mstari uwe na idadi sawa ya mizani. Mashairi yote yaimbwa; yawcza pia kusomwa au kusemwa tu. Tungo zisizotimiza yote hayo si mashairi.9
Tumemdondoa Mayoka kwa kirefu kwa sababu matamko yake, na hasa lazima alizozisisitiza ni mfano mzuri wa sheria za kirasimi10 ambazo akina Kezilahabi, Kahigi, Mulokozi na wengineo wanaeleza kuwa si za lazima.
Labda kabla ya kuuingilia “mgogoro” huo, tuangalie vipengele vingine vijitokezavyo katika maana za ushairi tulizoziorodhesha.
Vina na urari wa mizani ni vipengele vya ushairi vilivyo na asili yake kama itakavyodhihirika baadaye. Ni udhaifu wa kianazuoni kusisitiza juu ya kipengcle kimoja au viwili vya fani ya kazi ya fasihi na kuviita ni uti wa kazi hiyo. Mathalani, ni wazi kuwa kuna mashairi na nyimbo mzo mzo katika fasihi andishi na simulizi ya Kiswahili ambazo hazifuati hivyo vipengele alivyoviwekea ulazima mtaalamu Mayoka, na ambazo hazina vina wala urari wa mizani, na bado – tupende au tusipende – ni kazi nzuri sana za sanaa.
Katika maana ya kwanza tuliyoiangalia, kwa kutaroka kuwa “wimbo ni shairi dogo” Shaaban Robert anaweza kumtatanisha mwalimu na mwanafunzi wa ushairi. Tujuavyo, si kila wimbo ni shairi. Sifa ya “udogo” ambayo kaitumia Shaaban Robert ina utata pia, le udogo huo ni wa kifani au kimaudhui?
Shaaban Robert aelezapo kuhusu “maono na fikra za ndani (ambazo) huvuta moyo kwa namna ya ajabu” anaungana na wengine kama Abdilatif anayeongelea juu ya nguvu ya ushairi katika kuathiri moyo uliokusudiwa, na hata Mulokozi ambaye amesisitiza kuwa ushairi unatoa maudhui yake “kwa njia inayoburudisha na kugusa moyo.”
Nadharia hizi zina udhaifu wake kwani katika ushairi hakuna maajabu yoyote yale. Ijapokuwa huenda wataalamu hawa walikusudia tu kueleza juu ya umuhimu wa ushairi kujaribu kunasa hisia za watu, unasaji huo si lazima uwe kwa upande wa ushairi tu bali, kwa hakika, ni unasaji wa lazima kwa kazi zote za sanaa.
Ziko nadharia dhanifu zilizopandikizwa kuhusu uwezo wa mshairi. Nadharia hizi humweka mshairi juu ya watu wengine, juu ya jamii; nazo humgeuza kuwa Mungu-mtu mwenye visima vya hekima na zamzam za mawazo na maeneno mazito yanayovuta mioyo ya watu “kwa namna ya ajabu.”
Imani hii ambayo imeenea basa katika nchi za kibepari ambako mwanasanaa ni mtu maalumu asiye mmoja wa watu anaoandika juu yao, imepata nafasi kubwa sana katika kuipotosha nadharia yote ya ushairi wa Kiswahili. Kwa kufuatana na nadharia hii, baadhi ya washairi wa Kiswahili wameshikilia kutumia maoeno magumu magumu-hasa ya Kiarabu katika mashairi yao. Kwao hao mapambo ya sheria za vina na urari wa mizani ni ya lazima kafika ushairi. Wasioweza kuzitimiza sheria hizo kali basi wasijitie kuwa ni washairi! Kuhusu msisitizo huu wa matumizi ya “mapambo”, M.M. Mulokozi kasema:
… Uozo na ubaradhuli wa maisha ya kiumwinyi, hasa wakati mfumo huo unapoanza kutetereka kutokana na mabadiliko ya nguvu za jamii na uchumi, huwafanya mamwinyi, katika maisha yao ya kizembe na kifasiki, wapendelee sana mambo ya kuvutia macho na kuliwaza pua, kama vile mapambo aina aina, wanawake wazuri, nakshi na marembo ya rangi za kuvutia katika makazi na malazi yao… marashi na manukato, udi na ubani, (nakadhalika…)11
Ni wazi kuwa baadhi ya washairi wetu wa Kiswahili wanaosisitiza mno kuhusu mapambo katika maana ya ushairi wanasisitiza tu mtazamo wa kimwinyi waliorithi na kuuchukua vivi hivi tu bila kutambua asili yake.
Mtazamo huo pia – kwa vile unahusu tabaka hilo nyonyaji la kimwinyi – huwania kuweka sheria na kanuni mbalimbali za kuulinda utamaduni wake. Ni mtazamo unaoumba sanaa na wanasanaa wenye kujitenga na janui, wajionao wao kuwa ndio tu wamejawa na hekima katika bongo zao – hekima na uwezo ambao ni siri yao tu. Ili kusisitiza kuhusu upekee wa wanasanaa wenye mtazamo huo, wengi wao huanza kazi zao kwa kumwita Mungu na kuongea naye. Twaelezwa kuwa huyu, huwaongezea hekima na vipawa. Haishangazi kuona kuwa washairi wetu wengi waliopokeatu “ada” hii ya kinafiki ya kujiona kuwa na kipaji na hekima yenye asili ya uwezo wa Mungu, daima huanza mashairi yao kwa dua. Leo hii hili jambo la kuanza shairi au utenzi kwa kumwita Mungu ni dhahiri kuwa ni njia dhaifu mno ya kuanzia kazi yoyote ya fasihi; ni kujidanganya kuwa ni mkongojo wa mpingo kumbe ni “wa bua” tupu!
Kwa Mayoka, maana ya “shairi” imeishia tu katika idadi ya mistari, vina, urari wa mizani na kule kuimbika kwa utungo. Utungo usiofuata “sheria” hizo basi kwa mtaalamu huyu haufai kwani hauna “sanaa yoyote.” Lakini labda swali la kuuliza hapa ni je, sanaa ni nini? Sanaa ni uoanishaji mzuri wa fani na maudhui katika kazi ya mwigo aifanyayo mtu. Tanzu za sanaa hukua, hubadilika, na hata wakati mwingine hupigwa vikumbo na nguvu za kijamii ikabaki kuwa historia katika kumbukumbu za nyaraka za kale. Tanzu hizi basi, daima huwa katika mwendo wa mabadiliko, na ijaribupo kusimama tu bila kuguswa na mwendo huo hujikuta imechacha. Hii ina maana kuwa mtu aiwekeapo sanaa sheria na kuziita takatifu zisizoguswa na wakati na aina ya jamii, anadunisha na hata kuudharau uhai wa sanaa hiyo!
Katika maana aitoayo Kezilahabi utata unajitokeza katika sehemu mbili: kwanza anapotaja ulazima wa mizani katika shairi, halafu pia anapotamka kuwa kila shairi linaonyesha “ukweli fulani wa maisha.”
Kuhusu mizani, inabidi kuzingatia kuwa Kezilahabi anaongelea kipengele ambacho ni tofauti na kile cha urari wa mizani. Urari wa mizani ni kulingana kwa silabi za kila mstari wa ubeti katika shairi, kila silabi moja ikiwa ndio mizani moja. Urari wa mizani hupambanuliwa na mizani tu katika msisitizo wa idadi sawa za silabi. Mizani aisisitizayo Kezilahabi ni mapigo (rhythm) ambayo ni muhimu katika kila shairi ijapokuwa si lazima yaws ya kufanana kwa kila mstari. Mapigo haya hujulikana pia kama wizani. Ni mapigo yanayosaidia kuainisha mwendo wa shairi. Kwa mfano, iwapo shairi linahusu kifo, lazima mwcndo wake utakuwa wa polepole na mapigo yake yataonyesha huzuni na majonzi. Vile vile, iwapo shairi linahusu mapenzi ni wazi kuwa litakuwa na wizani laini na nyororo inayooana na maudhui ya kimapenzi. Wizani pia huainishwa na mambo kama vile urefu wa mstari au sentensi, ucbaguzi wa maneno na jinsi hayo maneno yanavyohusiana yenyewe kwa yenyewe katika kujenga mstari, ubeti au hata shairi zima.
Kufaulu ama kushindwa kwa shairi kutoa maudhui yanayoeleweka vizuri akilini mwa msomaji au msikilizaji hutokana na ufundi wa mshairi wa kuchagua mwendo na mapigo yanayolandana na maudhui anayoyashughulikia katika shairi lake.
Wizani inajitokeza katika hali mbalimbali, na wala siyo lazima ibebwe na mizani minane au kumi na sita kama ambavyo yaelekea wanamapokeo wanataka iwe. Hali kadhalika siyo lazima wizani iletwe na vina vya kati na vya mwisho, na hata siyo lazima kuwepo na vina katika shairi ili kuleta wizani. Wakati mwingine msisitizo uletwao na marudiorudio ya maneno fulani fulani katika shairi huleta mapigo mahsusi katika mtiririko wa hilo shairi. Yako mashairi mengi katika fasihi ya Kiswahili ambayo yanatumia mbinu hii ya matumizi ya maneno yenye kurudiwarudiwa.
Kwa kifupi basi, tunaweza kusema kuwa wizani ni mpangilio wa urudiaji wa mapigo au mwendo tunaosikia katika tungo. Hata hivyo haimaanishi kuwa lazima wizani ijitokeze tu katika ushairi. Sentensi ifuatayo imedondolewa kutoka katika nathari (Rosa Mistika ya Kezilahabi) na bado ina wizani utokanao na ufupi na usambamba ndani yake. “Jualikatua. Gizalikaingia. Mwezi ulitokea.”
Wizani husaidia sana wasomaji au wasikilizaji wa shairi kwani hufungamana oa yale maudhui akusudiayo kuyatoa mshairi. Mathalani, katika shairi la “Wimbo wa Kunguni” tulilolidondoa katika Kitangulizi, mshairi kaamua kuwa mstari wa 12 uwe na neno moja tu, tena wa mizani mbili tu: “sasa.” Inambidi msomaji ajiulize kwa nini mshairi kafanya hivyo. Ielekeavyo, hapa mshairi alitaka kuwekea mkazo neno hili, na kulipa nguvu ya msisitizo kuwa mambo yote hayo yahusuyo matatizo na migogoro ya ndoa yanatokana na usasa kwani hayakuwapo zamani. Ni wazi kuwa neno hili lingepoteza nguvu yake ya kusisitizwa kama lingewekwa na maneno mengine.
Kwa hiyo basi, sheria za kuifunga wizani katika mapigo ya aina hiyohiyo na ya idadi hiyohiyo ya silabi kwa kila mstari zinaweza kuifanya sanaa ivie, na shairi kama hilo la “Wimbo wa Kunguni”, lisingeleta athari hiyo ya kimaudhui kama lingefungwa na sheria hizo.
Tamko la Kezilahabi alitoalo katika maana yake ya shairi, kuwa katika kila shairi mna ukweli fulani wa maisha linatatanisha, kwani hata maana ya “ukweli” ina utata pia. Labda kwa vile baadhi ya wanafalsafa wamesema kuwa kila uongo ni ukweli fulani wa maisha; lakini tamko la Kezitahabi linaibusha swali moja muhimu: Je, huu “ukwell wa maisha” ni kwa macho ya nani? Kwa mtano, ni wazi kuwa shairi au kazi yoyote ya fasihi ya kipinga maendeleo – tuseme fasihi iliyoandikwa na kaburu anayeabudu ubaguzi wa rangi – itajaa wongo mtupu kuhusu hali za wanaobaguliwa; na itanuia kuuimarisha uongo huo ili kuendeleza unyama wa ubaguzi wa watu kufuatana na rang zao. Yako mashairi mengi sana yaliyojaa wongo mwingi ndani yake!!
Tamko la Kezilahabi halitotautiana na lile la Jumanne Mayoka ambaye, kati ya mengi aliyoyasema, kahitimisha juu ya ushairi kwa kusema: “kamwe ushairi hauwezi kuwa na uhusiano wowote na ujinga wa binadamu. Kazi ya ushairi ni kuuzindua na kuuelimisha umma wa binadamu.”13
Tatizo kubwa la Mayoka ni kuwa ametoa matamko ya jumla jumia mno kutokana na imani yake ya “utakatifu” wa usbairi. Kazi ya ushairi ya “kuuzindua na kuuelimisha umma wa binadamu” hutegemea masuala mbalimbali ya kijamii, hasa ya maslahi ya kitabaka. Katika jamii za mfumo wa kibepari, kazi ya ushairi mara nyingi ni ya kuwalaza na kuwapumbaza watu ili waendelee na ujinga wao kuhusu hali zao. Kazi za namna hii ni zile zinazoeleza uzuri wa maua na machweo ya jua; utamu wa nyimbo za ndege na za mawimbi ya bahari; pamoja na mambo mengine ya kindotondoto wakati ambapo mamilioni ya watu katika jamii hiyo hiyo wanaendelea kuteswa na kugandamizwa. Kazi za namna hii za ushairi katika jamii hizi husiflwa sana na vyombo vya habari, majarida na wahakiki; na zile zinazojaribu kuwazindua oa kuwaelimisha wanyonge zinapigwa vita vikali. Ijapokuwa kwa Mayoka shairi ni lile tu linalozindua na kuuelimisha umma, lakini tujuavyo yamejaa mashairi chungu ozima ya kupumbaza na kuuzubaisha umma.
Mayoka angeihusisha nadharia yake ya ushairi na mifumo mbalimbali ya kijamii, pamoja na nguvu za kitabaka katika mifumo hiyo, angelupatia nadharia sahihi zaidi.14
Sehemu ya mwisho ya maana aitoayo Mulokozi nayo ina matalizo kidogo. Siyo lazima kila shairi lieleze mambo yake “kwa njia inayoburudisha moyo,” kwani yako mashairi mengi mno yanayotoa maudhui vake kwa niia inayokasirisha na hata kukera moyo.
Abdilaut Abdalia naye atuelezapo juu ya “lugha nyofu, tamu na laini,” tena lugha “tetelezi kwa ulimi kuitamka” anatetereka kwani matumizi ya lugha hutegemea maudhui ya shairi. Lugha “nyoofu, tamu na laini” huweza kutumiwa kwenye maudbui kama yale ya mapenzi; wakati ambapo iwapo shairi linahusu vita au hasira lugha itakayotumika ni kali, chungu, na ya kukatakata.
Baada ya kuchunguza kwa kifupi kuhusu maana za ushairi kufuatana na mawazo ya wataalamu wa fasihi ya Kiswahili, sasa tunaweza kutoa maana tuonayo inasadifu kuueleza ushairi.
Ushairi ni utanzu wa fasihi utumiao mpangilio wa lugha ya mkato, ya kipicha na iliyopangwa kwa njia iletayo mapigo mahsusi kufuatana na maudhui yahusikayo.
USHAIRI WA KISWAHILI
Zamani sana lugha ya Kiswahili ilikuwa ya watu wa pwani ya Afrika ya Mashariki tu. Lakini leo hii hutumika Afrika ya Mashariki yote pamoja na nchi za jirani kama vile Zaire, Burundi, Somalia na Malawi. Kwa hiyo ni wazi kuwa wakati tukiongelea kuhusu ushairi wa Kiswahili mara nyingi tunamaanisha ule ushairi uliotungwa kwa lugha ya Kiswahili, na ambao unawahusu watu watumiao lugha ya Kiswahili maishani mwao.
Kwa sababu tunajua wazi kuwa historia ya ushairi wa Kiswahili haianzi na matumizi ya vina na mizani – kwam tuna ushairi mwingi wa Kiswahili kutoka katika fasihi simulizi ambao haufuati “sheria” za vina na mizani15 – sisi hatutachukulia vina na mizani kuwa ni uti wa ushairi wa Kiswahili. Pia tunajua wazi kuwa kuita vina na mizani kuwa ni roho ya ushairi wa Kiswahili ni kosa kwani ushairi wa Kiarabu na mataifa mbalimbali ya Ulaya pia una mizani na vina kama atuelezavyo mtaalamu Lyndon Harries:
…kwa mujibu wa arudhi ya Kiarabu ilishikiliwa kuwa, bila kujali urefu wa shairi, vina vya mwisho katika kila ubeti lazima vipatane tangu mwanzo hadi mwisho wa shairi. Kwa hiyo, hata katika tungo zenye vina vya kati, mtunzi akishaamua tu kutumia kina fulani katika kipande cha kwanza, ilibidi akitumie kina hicho hicho hadi mwisho… utaratibu wa namna hii bado unafuatwa katika mashairi mengi ya Kiswahili…16
Kumbe basi hicho wakntacho “roho” ya ushairi wa Kiswahili kipo katika ushairi wa Kiarabu na mataifa mengine. Je, ushairi wa Kiarabu ni ushairi wa Kiswahili kwa sababu kote ipo “roho” hiyo?
Si nia ya kitabu hiki kujaribu kupuuza sanaa ya urari wa vina na mizani katika ushairi wa Kiswahili. Ni wazi kuwa sanaa hii ikitumiwa vizuri ni pambo zuri sana katika ushairi. Hata hivyo jambo linalosisitizwa hapa ni kuwa vina na mizani sio yipengele pekee katika sanaa ya ushairi wa Kiswahili; wala sio lazima vina na urari wa mizani utumiwe katika utungaji wa ushairi wa Kiswahili.
Usanii katika kazi ya fasihi huamuliwa na mambo yaliyomo katika kazi hiyo. Yaani kutumia au kutotumia mambo kama vile tamathali, vma, mizani, na kadhalika, hutegemea jambo linaloongelewa katika kazi ya fasihi. Kwa kifupi fani ya kazi ya fasihi huamuliwa na nwudhui ya kazi hiyo. Sasa basi, ushairi wa Kiswahili ni upi?
Mwanzoni tulitaja uhusiano wa fasihi na utamaduni wa jamji inayohusika. Uhusiano huu utatusaidia hapa katika kueleza ushairi wa Kiswahili. Tutaamua kuwa kazi fulani ni ya fasihi ya Kiswahili au la kutokana na jinsi ilivyojitambulisha na ilivyojihusisha na utamaduni wa Waswahili. Hapa neno Waswahili halimaanishi kabila la Waswahili kwani kabila la namna hiyo halipo leo. Waswahili hapa ni wananchi wa Afrika ya Mashariki na Kati kwa ujumla na wala si wale tu wanaoishi katika pwani ya nchi hizi.
Sasa basi, utamaduni huo wa Waswahili ni upi? Huu ni ule unaohusu mila na jadi za Waswahili; sanaa zao, siasa, sayansi na uchumi wao; pamoja na mambo mengineyo yanayokamilisha maisha ya watu hao. Kwa hiyo ushairi wa Kiswahili ni dhahiri kuwa utakuwa na wahusika, mawazo, maudhui, falsafa, historia, dhamira na mambo mengineyo yanayoambatana na maisha ya Waswahili. Kutokana na mambo yote haya, hata kama shairi lina vina na mizani, kama halitekelezi mambo hayo ya kiutamaduni, basi hatuwezi kuliita la Kiswahili!
Maelezo
  1. Wazo hili la kuwa chanzo cha ushairi ni uchawi limcelezwa kwa kirefu na mtaalamu George Thomson katika Studies in Ancient Greek Society: The pre-historic Aegean (Lawrence and Wishart, London, 1961). Katika Kiswahili wazo hili limeendelezwa na wahakiki kama vile K.K. Kahigi katika makala yake “Ushairi (Mtazamo wa Kisayansi)” katika Kiswahili, Tol. 411, (Machi 1975). Baadhi ya wataalamu wa ushairi wa Kiswahili wameligusia jambo hili – labda bila wao wenyewe kuwa na habari – kwa kuupa ushairi Sifa ya kuuathiri moyo kwa “namna ya ajabu,” ijapokuwahawakulipanua. Ila Jumanne Mayoka, katika kitabu chake cha Mgogoro wa Ushairi na Diwani ya Mayoka, (Dar es Salaam, TPH, 1986), ameielewa vibaya nadharia hii akadhania kuwa akina George Thomson na Kahigi waongeleapo “uchawi” wana maana ya “tunguli za kichawi” na uramali. Nguvu za kishairi zinazoweza kumfanya mtu alie, ahuzunike, apate moyo wa ujasiri, na kadhalika, ndizo zilizokusudiwa hapa na wataalamu hawa; kwa hiyo “uchawi” ni neno ambalo limetumiwa kishairi zaidi kuliko kwa maana ya ulozi.
  1. Dai hili la kwamba vina na mizani ni uti wa ushairi wa Kiswahili linajitokeza katika matamko mengi ya wanamapokeo. Mathalani, katika kitabu cha Jumanne Mayoka, Mgogoro wa Ushairi na Diwani ya Mayoka, (uk. 28), mwandishi anadai hivi:
Vina na urari wa mizani ni uhai, roho na uti wa ushairi wa Kiswahili. Iwapo vitaepukwa au kubezwa hatutaweza kutambua kuwa hili ni shairi au la.
Dai kama hili linalochukua vipengele viwili au vitatu vya fani na kuviita kuwa ni robo na uhai wa kazi fulani ya saoaa linaua sanaa!!
Yakaenda na kwa kasi
Ni kukanda bila rasi
Na mikanda kuiasi
Hebu basi pigilia.
Utungo huu nimeutunga harakaharaka tu kwa kutumia maneno ya Kiswahili yaliyojipanga katika vina vya kati oa urari mzuri wa mizani. Lakini maneno yenyewe hayana maana wala mantiki, ijapokuwa hiyo roho na uhai audaio Mayoka upo. Huu ni ubeti kibudu, hauna ubai wowote! Uhai wa kazi yoyote ya sanaa hutokana na uwiano mzuri baina ya fani na maudhui, na kamwe hauwezi kutokana na vipengele viwili au vitatu tu vya fani!
  1. M.M. Mulokozi, na K.K. Kahigi: Malenga wa Bara, (Dar es Salaam/Kamnala/Nairobi: East African Literature Bureau, 1976).
  1. Shaaban Robert, “Hotuba Juu ya Ushairi,” Journal of The East African Swahili Committee, 28/1 (1958).
  1. Mathias Mnyampala, Diwani ya Mnyampala, (Dar es Salaam Kampala/Nairobi: East African Literature Bureau, 1970); “Dibaji.”
  1. A. Abdalia, “Tanzu za Ushairi na Maendeleo Yake.” Makala, (Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, 1974).
  1. E. Kezilahabi, “Ushairi wa Mapokeo na Wakati Ujao,” katika kitabu cha J.P. Mbunda (Mhariri), Uandishi wa Tanzania: Insha, (Nairobi/Kampala/Dar es Salaam: East African Literature Bureau, 1975), uk. 23.
  1. M.M. Mulukozi, “Ushairi wa Kiswahili ni Nini?” Lugha Yetu, Na. 26 (1975), uk. 12
  1. J. Mayoka, Mgogoro wa Ushairi, uk. x
  1. Ili kuelewa zaidi kuhusu matapo ya fasihi za Ughaibuni na yale ya fasihi ya Kiswahili ya urasimi mkongwe, urasimi mpya, ulimbwende na uhalisia, soma sura za 1 na 2 za kitabu cha F.E.M.K. Senkoro, Fasihi na Jamii (Das es Salaam: Press and Publicity 1987).
  1. Mulokozi, “Ushairi na Kiswahili ni Nini?” uk. 12
  1. Yafuatayo ni baadhi ya marejeo kwa wenye nia ya kusoina zaidi KUHUSU wizani: C. Kugh Holman (Mhariri), A Handbook to Literature (Indianapolis: Odyssey, 1975), hasa kurasa za 4456-457; William R. Bascon na Melwile J. Herskovits (Wahariri), Continuity and Change in African Cultures (Chicago & London: The Univ, of Chicago Press, 1959); Ruth Finnegan, Oral Poetry (Cambridge: Cambridge Univ. Press, 1977); Desmond Graham, Introductin to Poetry (London: Oxford Univ. Press, 1968); na A.M. JONES, African Rhythm.” Africa 24 (1954)
  1. Kezilahabi, “Ushairi wa Mapokeo.” uk. 5
  1. Nimejaribu kuainisha fasihi katika mifumo tofauti ya jamii tangu jamii ya mwanzo hadi ya sasa katika Sura ya Kwanza (“Fasihi Katika Mifumo Tofauti ya Jamii”) ya Fasihi ya Jamii.
  1. Huu ulikuwa katika umbo la cyimbo za ngoma, za kazi, majigambo, na kadhalika. Kuhusu jambo hili, Mnyampala alisema haya: “… Mashairi ya Kiswahili, kabla ya watu hawajajua kuandika, yalikuwa yanatungwa na kuimbwa katika ngoma, majando, nyago, harusi na kadhalika; kwani mashairi si kitu kingine, ni nyimbo, na waliokuwa wakizitunga nyimbo hizo au kuziimbisha katika ngoma waliitwa ‘Manju’ au ‘Malenga’, nazo ziliendelea kuimbwa na kukumbukwa namna hiyo…” (Waadhi wa Ushairi, East African kuwa “mashairi si kitu kingine ni nyimbo” kwani si lazima kila shairi liimbike – na tujuavyo bila kuimbika maneno hayaitwe wimbo – hata hivyo Mnyampala anapoelezea kuhusu ushairi wa Kiswahili kabla ya maandishi anatudhihihshia wazo letu la awali kuhusu vina na nuzani. Kwani, si kila wimbo ulikuwa na vina na mizani kati ya hizo za majaodo, oyago, ngoma, na kadhalika.
  1. Lyndon Harries, Swahili Poetry, (London, 1966) uk. 186. Msisitizo wangu.
TANBIHI: Kutoka kitabu cha Ushairi – Nadharia na Tahakiki (Dar Es Salaam University Press, 1988, 168 p.) cha F.E.M. K. Senkoro
]]>
false
MwlMaeda]]> 2022-01-04T03:48:05Z 2022-01-04T03:51:26Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1985 <![CDATA[NUKUU ZA USHAIRI]]>
.docx   NUKUU ZA USHAIRI.docx (Size: 221.6 KB / Downloads: 4) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2022-01-03T07:32:13Z 2022-01-03T07:32:47Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1973 <![CDATA[DHANA NA DHIMA YA UMAPOKEO KATIKA USHAIRI]]> Kwa Muhtasari
MKABALA wa kimapokeo ndio ulioanza katika kutoa fasili ya ushairi kutokana na ukweli kwamba watetezi wake waliupokea tu kutoka kwa wazee bila kuhoji ikiwa kweli mambo yalivyoelezwa ndivyo yalivyo au la.
Wao waliurithi tu. Dhana hii ya umapokeo ni tafsiri ya ile dhana ya Kiingereza “ Traditional approach.”
Gituma (2010) anafasili shairi kuwa ni mtungo wa kisanaa wenye mpangilio maalumu wa lugha ya mkato katika usemi, maandishi au wimbo unaoelezea wazi kuhusu mawazo, hisi au tukio kuhusu maisha na ambao hufuata utaratibu wa urari na muwala maalumu uliosheheni kanuni za utunzi wa mashairi.
Fasili hii inasisitiza kwamba “shairi ni wimbo, shairi huwa na urari (bila shaka wa vina na mizani), shairi huwa na kanuni mbalimbali.”
Maelezo haya bila shaka yametokana na athari za Abedi (1954:1) ambaye imani hiyo ilimfanya kuandika kitabu alichokiita ‘Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri’.
Jambo la dhahiri hapa ni kwamba utunzi wa mashairi una kanuni maalumu na kwamba kama shairi haliimbiki basi halina maana. Mtazamo huu kwamba shairi ni wimbo ndio unaotawala sana miongoni mwa wanamapokeo wengi.
Hili lina maana kwamba shairi linatungwa ili liimbwe na hadhira husika. Wazo hili linapewa nguvu na fasili ya Uvetie (1976) anaposema kwamba, “napenda kuwafafanulieni kwamba mashairi ni usemi usemwao kwa namna ya mafumbo na pia ni nyimbo.”
Zaidi ya kusisitiza ushairi kuwa ni wimbo, dhana nyingine kwamba shairi lazima liwe fumbo ni kusema kuwa kama shairi si fumbo basi si shairi.
Aidha, Mnyampala (1964:4) anabainisha kwamba mashairi ni nyimbo zenye maghani ya mvuto wa madoido na vingorimbo bora. Anachokisema hapa ni kwamba ushairi lazima utumie lugha tamu yenye madoido ya kuupamba. Dhana ya ushairi kama utamu wa lugha inaonekana pia kwa Uvetie (1976) ambaye anachagua kukiita kitabu chake cha mashairi ‘Utamu wa Lugha’.
Ingawa hivyo, fasili hizi zinaweza kuonekana kuwa sahihi zaidi katika fasihi simulizi ambapo utanzu wa ushairi (na hasa ushairi simulizi) unachukuliwa kuwa ni wimbo.
Kimsingi, tunapozungumzia utanzu wa ushairi katika fasihi simulizi tunazungumzia nyimbo za aina mbalimbali za makabila ya Kiafrika.
Ushairi kama wimbo ulionekana sana katika miaka ya awali ya maendeleo ya taaluma ya ushairi wa Kiswahili (kabla ya miaka ya 1960).
Baada ya hapo, dhana ya ushairi kama wimbo ilipingwa vikali. Hadi sasa inakubaliwa miongoni mwa wanazuoni na katika fasihi ya Kiswahili kwamba, shairi si lazima liimbike. Shairi linaweza kughaniwa, kutongolewa au hata kusemwa.
Kwa kusema kwamba shairi lazima liimbike, ina maana kwamba shairi lazima liwe na urari wa vina na mizani. Mashairi yanayopishana sana kivina na mizani ni vigumu kuyaimba.
Dhana hii ya urari wa vina na mizani kama sifa kuu ya shairi imepingwa vikali na hatimaye kubainika kwamba shairi linaweza kuwa na urari wa vina na mizani au lisiwe nao lakini bado likabaki kuwa shairi.
Jambo la kukumbuka ni kwamba shairi linapokosa urari wa vina na mizani kuna uwezekano mkubwa wa shairi husika kutoimbika.
Hivyo basi, dhana ya shairi kama wimbo si ya msingi japo hatuwezi kuipuuza kabisa kwani inajaribu kutupa upande mmoja wa sarafu ya shairi.
Zaidi ya msisitizo katika kanuni na uimbikaji, fasili nyingine za ushairi zimejikita zaidi katika dhima ya ushairi. Mnyampala (1975) anaufasili ushairi kwa kuzingatia nguvu ya shairi kuiasa, kuiongoza jamii kwa pamoja licha ya kusheheneza uzuri na utamu wa lugha.
Anauona ushairi kuwa ni utungo wenye maneno ya hekima na kwamba ndio utungo ulio bora sana katika maongozi ya dunia.
Anafafanua kwamba kuna aina tano za mashairi kwa kuzingatia maongozi na mafunzo yanayotoa. Aina hizo ni mashairi ya kawaida, mashairi ya furaha, mashairi ya huzuni, mashairi mazito na mashairi ya kuadibu.
Mashairi ya kawaida ni yale ambayo yana mawaidha ya dunia, visa na mikasa ya kawaida na mengine ya aina hiyo wakati mashairi ya furaha hushangilia tamasha iliyopo, kutakia heri na mafanikio, ombi la kudumisha furaha hiyo na waadhi kwa ajili ya tafrija hiyo.
Kwa upande wa yale yaliyomo katika mashairi ya huzuni, anayataja kuwa ni rambirambi, maombezi kwa Mungu kwa ajili ya marehemu, maombezi kwa wale waliobaki, historia ya marehemu na kumbukumbu itakiwayo.
Nayo mashairi mazito huwa ni mashairi ya kuzama (kufumba), mashairi ya tambo, pigo kuu la ushairi, furaha ya ushairi na taaluma zake na kuonyesha mbinu za lugha ya mshairi yule.
Aina nyingine ni mashairi ya kuadibu ambayo humwonya mtu kinagaubaga bila kutumia utusi, kumtanabahisha ya hatima, mashairi yanayohusu maandiko matakatifu na yale yahusuyo uungwana.
Wakati ambapo tunakubaliana na wazo kuwa shairi linaweza kumwongoza mwanadamu, tunaona kwamba ushairi unapaswa kufasiliwa kwa kuzingatia nduni bainifu na si nduni jumuishi kwani tanzu zote za fasihi huwa na jukumu hilo la kumwongoza mwanadamu.
Moja ya dhima kuu za fasihi ni kuelimisha, na huko ni kusema tanzu zote za fasihi huelimisha. Hata hivyo, izingatiwe kwamba si kila shairi hubeba mawazo ya hekima na linakusudia kutoa maongozi kwa jamii.
Yapo mashairi mengi ambayo yanapotosha jamii. Zaidi ya uwezo wake mkubwa wa kuielimisha jamii, fasihi inaweza pia kuipotosha jamii hiyo.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-27T09:56:19Z 2021-12-27T09:56:19Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1851 <![CDATA[FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI: MUHADHARA WA KUMI]]> MUHADHARA WA KUMI
Kumbo za ushairi wa Kiswahili
Ushairi wa Kiswahili unaweza kuwekwa katika kumbo za aina tatu za kimtindo ambazo ni; Ushairi wa kijadi (kimapokeo), Ushairi wa Kisasa/mlegezo/masivina/mauve/mapingiti na Ushairi wa maigizo.
  1. Ushairi wa kimapokeo; Haya ni mashairi yenye kuzingatia urari wa vina na mizani.
  2. Ushairi wa mlegezo; Ni mashairi yasiyofungwa na kanuni za kimapokeo.
  3. Ushairi wa maigizo; Ni ushairi unaotumia vitendo na hugawanyika katika aina mbili ambazo ni ngonjera na ushairi wa kidrama.
(i)         Ngonjera; Ni ushairi wa majibizano ulioanzishwa na Mathias Mnyampala 1960 na ulitumika sana katika kueneza siasa ya ujamaa. Katika ngonjera huwa kuna pande mbili, kuna upande uliopotoka na upande uliosahihi. Kila upande hujenga hoja za kushawishi upande mwingine kishairi.
Mwisho wa majibizano ya kingonjera huwa ni suluhisho ambalo kwa kiasi kikubwa upande uliopotoka huthibitisha kuzidiwa kwa hoja.
Mfano: ngonjera za UKUTA.
(ii)       Ushairii wa kidrama; Ni ushairi unaotumiwa katika baadhi ya tamthiliya kama sehemu ya mchezo wa kuigiza na ni moja wapo ya mitindo itumiwayo katika tamthiliya. Mfano; Tamthiliya ya Mfalme Edipode na Mabepari wa Venisi (mfarisi: J.K. Nyerere)
–   Ngonjera hupaswa kuwa na Mwanzo wa kingonjera.
            Bahari za ushairi kijadi
Bahari ya ushairi ni aina mahususi ya ushairi yenye sifa     fulani kiumbo zinazojipambanua na aina nyingine za ushairi.
(i)         Shairi; wanajadi walisema shairi ni utungo wenye mishororo minne kila ubeti na vipande viwili vya mizani nane kila kipande. Maudhui yanaweza kuhusu suala lolote linalomkuna mtunzi.
(ii)       Wimbo; Ni utungo wenye mishororo mitano kila ubeti na una vipande viwili na maudhui yanaweza kuwa ya mapenzi yaliyochepuka.
(iii)     Bahari ya utenzi; Ni shairi la masimulizi,mawaidha au maelezo marefu. Tenzi nyingi zina mizani nane kila mstari na vina hubadilika kila ubeti isipokuwa mstari wa mwisho. Maudhui ni ya kawaida, masimulizi, mawaidha ambayo huelezea wasifu au tawasifu, ushujaa, utendi, nk.
–   Wasifu ni historia inayomhusu mtu fulani na ambayo huandikwa na mtu mwingine.
–   Tawasifu ni historia ya mtu ambayo huandikwa na mtu mwenyewe.
Inkishafi/Dura Mandhuma; Ni aina ya ushairi ambayo imepata jina lake kutokana na utenzi wa Al-Inkishafi na Dura Mandhuma. Utenzi huu ulikuwa pamoja kwa sababu ya nafanana na pia zina maudhui ya kidini ingawa zinaweza kutumika kwa maudhui ya kidunia. Mpangilio wake ni mishororo minne na mizani kumi na moja kwa mgawanyo wa sita na tano jumla yake ni kumi na moja yaani 6 + 5 = 11.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-27T09:36:42Z 2021-12-27T09:36:42Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1849 <![CDATA[FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI: MUHADHARA WA TISA]]> MUHADHARA WA TISA
HISTORIA FUPI YA USHAIRI WA KISWAHILI
Wataalamu wengi wanakubaliana  kwamba asili ya ushairi wa Kiswahili ni tungo simulizi hasa ngoma na nyimbo. Kabla ya karne ya 10BK ushairi wa Kiswahili ulikuwa ukitungwa na kughaniwa kwa ghibu (sanaa za asili) bila kuandikwa.
Ø Baadhi ya tanzu za ushairi zilihusu masuala ya dini hasa ya Kiislamu na taaluma ya uandishi kwa hati ya kiarabu.
Ø Miongoni mwa watunzi mashuhuri wa ushairi wa mwanzo wa Kiswahili ni Fumo Liyongo.
Ø Uandishi wa ushairi uliendelea kuwa wa ghibu hata baada ya karne ya 15 na kusawiri mabadiliko ya mifumo mbalimbali ya kimaendeleo katika maisha mfano: kipindi cha waarabu kiliambatana na migogoro mingi ya vita,upinzani,mizozo kati ya madola ya miji ya Pwani na kati ya watwana na mabwana.
Ø Vilevile wasomi wa kidini waliibua fasihi ya ushairi uliotafakari theolojia na falsafa ya maisha mfano: Utenzi wa Al-Inkishafi.
Ø Tendi za Kiislamu zilizungumzia pia matukio ya uarabuni enzi za Mtume Muhammad.
Mfano:
–   Utenzi wa Shufaka (kuomba rehema)
–   Utenzi wa Ngamia na Paa (dua kutegemea aendako muombaji)
–   Utenzi wa Mikidadi na Mayasa (namna ya kuwaasa watoto wa kike na kiume)
–   Utenzi wa Ras L’ Ghuli
TUNGO ZA KITAMADUNI, MAWAIDHA NA TUMBUIZO
(a)    Tungo za kitamaduni (mawaidha na tumbuizo)
Mfano: utenzi wa Mwanakupona ulitungwa na Bi. Mwanakupona akimuasa binti yake juu ya nidhamu, heshima na utii kwa mumwe wake.
MASHAIRI YA SIASA
Watunzi mashuhuri wa kundi hili ni Muyaka bin Haji, Suud bin Said na Kibabina. Hawa ni baadhi ya watunzi wa mashairi ya kisiasa na walifungwa jela na kuuawa. Pia kulikuwa na mashairi ya kukataa kutawaliwa na wakoloni.
Mfano:
–   Potugezi Afala
Mzungu Migheli
KARNE YA ISHIRINI
Ushairi karne ya 20 hadi sasa.
Maendeleo ya ushairi wa Kiswahili yaliathiriwa na mambo matatu ambayo ni:
–   Elimu ya kizungu
–   Hati ya maandishi ya kirumi
–   Taaluma ya uchapaji
Haya yote yaliletwa na wazungu.
ATHARI ZA UJIO WA WAARABU KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI
(a)    Hati za kiarabu
(b)    Maudhui yalilenga elimu akhera zaidi ya siasa na mawaidha
©    Fani; kanuni zilianza kutumika kwa kuzingatia vina na mizani. Mwanzilishi wa kanuni za utunzi wa mashairi ni Plato kutoka Ugiriki.
(d)    Elimu;mashairi yalieneza elimu ya Kiswahili maeneo ya bara kupitia shule. Maarifa ya kusoma na kuandika,maarifa ya arudhi (kanuni ) za utunzi zilipewa kipaumbele katika kutunga mashairi.
(e)    Hati za kirumi; zilienea kupitia elimu ya shule,makanisani kwa kutumiwa na watunzi wengi badala ya hati za kiarabu.
–   Kipindi hiki ushairi ulianza kusomwa na watu wengi zaidi na hata wasio waislamu na baadhi yao wakaanza kutunga mashairi mfano: Mathias Mnyampala.
–   Utunzi huu uliingia magazetini na kuhamasisha watu wengi kusoma magazeti mfano: gazeti la Mambo Leo (1923).
–   Kuanzishwa kwa shirika la uchapaji nako kulichochea utunzi wa mashairi ya Kiswahili kwa sababu watunzi wengi walipata mahali pa kuchapa kazi zao (shirika la uchapaji la Afrika Mashariki : The East African Literature Bureau, 1948) lilichapa kazi mbalimbali za watunzi mashuhuri.
Mfano:
–   Mathias Mnyampala
–   Akilimali Snow-White
–   Amri Abeid.
SHUGHULI ZA KISIASA ZA KUDAI UHURU (1950-1960)
  1. Ushairi ulipamba moto ukihamasisha wanajamii kudai uhuru mfano: Mashairi ya Saadan Kandoro
  2. Baada ya uhuru ushairi ulisambaa zaidi kutokana na msukumo wa kisiasa na fani mpya mfano; Ngonjera na Mavue ni mashairi yasiyo na kanuni. Mashairi huru yaliyoanzishwa ili kuzingatia mahitaji mapya ya kisiasa na kisanii.
HISTORIA YA USHAIRI KIFASIHI
Historia ya ushairi kifasihi inaweza kubainishwa katika mihula mbalimbali kama alivyofanya Kezilahabi. Mihula minne aliyoianzisha Kezilahabi ni:
(i)         Muhula wa urasimi mkongwe; hiki ni kipindi ambacho ushairi ulitawaliwa na kanuni na mitazamo ya kidini na kimwingi.
(ii)       Muhula wa utasa (kipindi cha mpito); ni kipindi cha mabadiliko ya kiutamaduni na kielimu kulikoleta mabadiliko ya hati za maandishi. Kipindi hiki mashairi machache yalitungwa kwa lugha ya kiarabu na kanuni kubadilika.
(iii)     Muhula wa urasimi mpya; huu ulikuja wakati wa kufufua kanuni za utunzi ambapo palitungwa kitabu cha sheria na kanuni na kusambaza kwa watunzi. Kitabu hicho kilitungwa na Amri Abeid na kuchapishwa 1954.
(iv)       Muhula wa sasa (ulimbwende,1967); ni muhula wa mtazamo mpya kimawazo na kisanaa. Muhula huu umeibua mgogoro mkubwa kati ya uwanja wa ushairi baina ya wanamapokeo na wanausasa.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-27T09:35:34Z 2021-12-27T09:35:34Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1848 <![CDATA[FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI : MUHADHARA WA NANE]]> MUHADHARA WA NANE
   USHAIRI
Ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Ushairi una ufasaha wa maneno machache au muhtasari wa mawazo, maono na falsafa za ndani zenye kuvuta moyo kwa namna ya ajabu.
       Sifa za ushairi
–   Wimbo sharti uimbike,ughaniwe na kutongoleka
–   Maneno ya hekima yenye kufunza, kuonya na kuadibu
–   Lugha ya mkato, vina na mizani mf: mfanowe, mefumbata, nk
–   Lugha nzito au lugha ya kunata
Hisiya (lugha inayovuta moyo
Vijenzi vya ushairi wa Kiswahili
Fani na Maudhui
Muwala ni uwiano mzuri kati ya mtiririko wa fikra na umbo la shairi. Mawazo ya shairi yakifuatana kimantiki ubeti hadi ubeti na mstari hadi mstari hufikisha bara bara maudhui yaliyokusudiwa na hapo husemwa kuwa shairi lina muwala.
Muundo ni msuko,mwingiliano na uwiano wa vipengele vyote vinavyojenga shairi au kazi ya sanaa. Vipengele vya kimuundo hudhihirika katika umbo la shairi.
–   Idadi ya beti kwa shairi zima
–   Idadi ya mistari kwa kila ubeti
–   Vipande (ukwapi-utao-mwandamizi)
–   Kituo kila ubeti
–   Mizani
–   Vina
Maudhui ni wazo au mawazo yaliyomsukuma mtunzi wa kazi ya fasihi kutunga kazi ya sanaa. Maudhui huhusisha mtazamo, shabaha na ujumbe.
Umbo hutumika kwa maana ya sanaa ya nje ya shairi au kazi ya sanaa.
Mtindo unakuwa na uteuzi wa maneno; lugha ya Kiswahili huteua maneno maalumu yenye kuleta athari au matokeo yaliyokusudiwa.
–   Takriri- ni mbinu ya kurudiarudia neno au sehemu ya neno kwa lengo la kutia msisitizo.
–   Wizani- ni kiimbo yaani kupanda na kushuka kwa sauti kunakoleta mapigo ya kimuziki.
–   Mchezo wa maneno – ni mbinu ya kutumia maneno ya kiufundi ili kutanua maana ya kile kinachosemwa na kuongeza utamu wa usemaji mfano: wale wali wale wali wao (Mulokozi)
Wale wale ndio wao
Bado wapo palepale
Wao wale wenye vyao
  Na vya kwao vile vile
Wala kale wala leo
Kula huko kura kule
Mwendo huu ndio huo
Bado tupo palepale
–   Lugha ya mkato – shairi huzungumza mambo kwa ufupi kuliko ilivyo katika maongezi ya kawaida. Mfano: shairi la Hila zina maulaya (Amri Abeid)
Nijapotendwa ubaya na wabaya kuwajua
Mwenzi huona haya ubaya kuwatendea
Japo moyo una waya hufanya kuuzuia
Nacheka hali najua hila zinamaulaya
Hila zinamaulaya na wananishambulia
Nyama iliyooza mbaya mbesi hufurahia
–   Taswira – ni mbnu ya kuumba picha ya jambo katika mawazo ya msomaji au msikilizaji kwa kutumia maneno. Mfano: Amina (Shaaban Robert)
Amina umejitenga,kufa umetangulia
Kama ua umefunga,baada ya kuchanua
Nakuombea mwanga,peponi ukubaliwe
Mapenzi tuliyofunga,hapana wa kufungua
          Tamathali za semi
v Sitiari- ni mbinu ya kulinganisha vitu bila kutumia viunganishi linganishi.
Mfano:
–   Elimu ni bahari
–   Misitu ni uhai
–   Kilimo ni uti wa mgongo
v Tashibiha – ni mbinu ya kulinganisha vitu kwa kutumia maneno kama: mfano wa,mithili ya,kama,nk
Mfano:
–   Mrefu kama twiga
–   Mweusi mithili ya kiatu cha jeshi
–   Ananata mfano wa nta
v Tashihisi – ni mbinu ya kuvipa uhai na uwezo wa kutenda kama binadamu vitu au viumbe visivyo na uwezo huo.
Mfano:
–   Misitu ikatabasamu
–   Mawimbi yakapiga makofi
–   Kaburi likamkumbatia
v Tafsida – ni maneno yatumiwayo kwa lengo la kupunguza au kuficha utusi na ukali wa maneno.
Mfano:
–   Ametutoka (kufariki dunia)
–   Kupiga simu ( kwenda haja)
–   Kujifungua (kuzaa)
Ø Mdokezo – ni mbinu ya kumshirikisha msomaji kwa kumuachia akamilishe wazo fulani.
     Mfano:
–   Alipomtazama akamwambia ………… lakini nakupenda.
Ø Ishara – ni matumizi ya maneno yanayoashiria mambo au matukio katika jamii.
Mfano:
–   Mwezi – Baada ya kuona mwezi alirudi nyumbani akiwa na furaha.
Ø Balagha/mubalagha – ni mbinu ya kutia chumvi kwenye habari kwa lengo maalumu.
Mfano:
–   Alikuwa mweusi kama buti la jeshi.
–   Alikuwa mrefu mithili ya twiga
 Mbinu ya kikufu– Ni mbinu ya kukifanya kipande cha mwisho cha ubeti kiwe kipande cha mwanzo cha ubeti au mstari unaofuata.
Mfano:
Kutafuta hali njema, maana ya mapinduzi
Unyonge kuusukuma, uonevu wa majizi
Na kuonewa lazima, tung’owe yote mizizi
Maana ya mapinduzi, Kutafuta hali njema.
 Mbinu ya pindu- Neno pindu katika ushairi lina maana mbili.
(i)         Kufanya neno au sehemu ya neno la kipande au mstari lianze katika kipande cha mstari unaofuata.
Mfano: (Zuko)
Tika kitupu hutika,TIKA upya unafuka
UKA huko ukaleni,LENI mapya kulaFUKA
FUKAra wa mzaMANI, MANI MAPYA hutaKA
TUKATAKA mawazoni,ZONI huna kukuSHIKA
SHIKAmimi sishiKANI,KANIzo zapukutika
(ii)       Mbinu ya kugeuza silabi za neno mwanzo kuwa za mwisho.
Mfano:
Saadan chambilecho, chambilecho humenyeka
Kinyume ni kiambacho,chomba akini hakina
Hila tatu chekecho,chokeche huzipinduka
Kwa wenye chongo kufika,mwe fumba lako jicho
Mbinu ya kidato – Ni mbinu ya kufupisha mshororo mmoja au zaidi kila ubeti kwa lengo maalumu. Malengo maalumu ni pamoja na kupata vina na mizani, kuuliza swali, n.k
Mfano: Nimeamka la S. A. Mohamed
Sidanganywi kwa hotuba na mahubiri matupu
Hata wanakula riba,wanaongoza vikapu
Nimeamka
Nawaambia wahubiri,wanaodanganya watu
Moyo umejaa ari,sizugiki tena katu
Nimeamka
Mbinu ya tungo mchoro – mbinu hii hutumika katika shairi la mchoro ambapo shairi hupangwa katika umbo lenye kufanana na kile kinachozungumziwa hivyo mada ya shairi hilo huonekana machoni licha ya kusikia masikioni.
Mfano: Tafakari tesi
Masikini
Haya ambayo
Mawe yalifinyangwa
na                      maumbile
mawe                          ambayo
yalisongwa                          na
matambara                        maskani
haya                                ambayo
yalimiminishwa                           kwa
saruji                              itokanayo
HISIYA ZA KISHAIRI
Hisiya za kishairi hutokana na msukumo wa ndani ya moyo alionao mshairi wakati anatunga shairi lake.
Aina za hisiya za kishairi
(i)         Hisiya ya furaha
Mfano wa shairi la Cheka kwa furaha
Dhiki ni kama mzaha,asiyecheka nani?
Haya cheka kha kha kha,ndio ada duniani
Basi cheka kwa!kwa!kwa!,usafike moyo wako
 
(ii)       Hisiya za chuki
Mfano shairi la Manzese mpaka Ostabei, 
Unaishi ostabei unapata mchumba/mpenzi Manzese, je atakula nini ilhali hali ya maisha ya manzese yajulikana?
(iii)     Hisiya za kimapinduzi
Mfano shairi la Tohara.
Linahamasisha jamii ya kinamama kuachana na mila za tohara kwa wanawake au wasichana.
(iv)       Hisiya za kichochezi
Mfano: shairi la “Hatumwoni” katika diwani ya Karibu Ndani mwandishi katika shairi lake anasema:
Miungu waliosimama kama vichaka
Waambieni wakae chini warefu
Kaeni chini! Wengi nyuma hatuoni!
Hatutaki vyenu visogo kuona.
Kaeni chini miungu, kaeni chini ndiyo amri!

Mlipewa uongozi ukawapaka rangi
Na madaraka madaraka yakawalevya
Sasa vueni wapisheni wenye nia!

Kokeni mioto mashujaa wa uonevu tuwabanike
Kamwe hapatakuwa na kilio wala matanga
Bali hoihoi za ushindi na madaraka kwa umma

(v)         Hisiya za huzuni
Mfano: Utenzi wa Hayati Sokoine katika diwani ya Mloka.
Ilikuwa redioni
Saa kumi za jioni
Mwenyekiti kwa uchungu
Umma kautangazia

]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-27T09:28:52Z 2021-12-27T09:28:52Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1847 <![CDATA[FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI: MUHADHARA WA SABA]]> MUHADHARA WA SABA
MAGHANI NA NGOMEZI
Maghani ni ushairi unaoghaniwa au kutambwa hadharani. Sauti ya mghani aghalabu huwa kati ya mazungumzo na kuimba (hazungumzi wala haimbi).
Maghani hutambwa hadharani pamoja na ala za muziki au bila ala na huzungumzia masuala mazito ya kijamii au ya kibinafsi.
        Tanzu za maghani
(i)         Ghani nafsi; Ni ushairi simulizi wa kinafsi unaoelezea hisiya, matatizo na fikra za mtunzi mwenyewe. Mashairi ya mapenzi yanaingia katika kundi hili.
(ii)       Ghani tumbuizi; Ni ushairi wa kuliwaza, kufurahisha na kuburudisha na hughanwa badala ya kuimbwa.
(iii)     Ghani sifo; hili ni kundi mahususi la maghani ambalo hubeba tungo za kusifu hasa watu,wayama,mimea au vitu.
Tanzu za ghani sifo
(a)    Vivugo/kivugo; ni ghani la kujisifu ambalo hutungwa na kughaniwa na mhusika mwenyewe. Muundo wake hutegemea sababu za mtunzi na jadi ya utunzi. Mathalan jamii ya wahaya kivugo huwa na mambo yafuatayo:
–   Jina halisi au jina la sifa ya mtunzi
–   Sifa za nasaba yake ya kuumeni
–   Sifa za nasaba ya kikeni
–   Maelezo ya matendo makuu aliyoyatenda au matendo matukufu yanayozidi wengine wote
–   Ahadi ya kutenda makubwa zaidi kwa ajili ya mkubwa wako
–   Tamati- kujikabidhi rasmi kwa mkubwa.
(b)    Tondozi; Ni tungo za kusifu watu, wanyama au vitu vya kawaida. Pembezi ni aina moja wapo ya tondozi ambayo husifu watu wakubwa au watawala. Tondozi zinazohusu wanadamu moja kwa moja ndio nyingi zaidi. Watu husifia wapenzi wao,adui zao au wake zao.
Ghani simulizi; Ni ghani za kihadithi zenye mtiririko wenye msuko wa matukio uliojengwa ili kuleta taharuki na ujumbe fulani.
Tanzu za ghani masimulizi ni:
(a)    Rara; Ni ghani zinazotambwa ili kusimulia hadithi, historia au tukio fulani na mara nyingi huambatana na muziki wa ala. Mtambaji huitwa Yeli/Manju na huwa ni mtaalamu wa kupiga ala fulani za muziki. Ala mashuhuri ni zeze, marimba, ngoma na njuga.
                      Sifa za rara
–   Huweza kuwa tenzi au tendi
–   Lazima ziwe ni tungo za kishairi
–   Isirudie hadithi au tukio kwa kirefu
–   Matini yake hutungwa papo kwa papo
(b)    Tendi; huu ndio utanzu mashuhuri zaidi katika kundi la ghani simulizi, utendi ni utungo mrefu unaosimulia matukio ya kishujaa yenye uzito wa kijamii au matukio ya kitaifa. Huweza kuwa ya kihistoria au yaliyochanganya historia na visakale au visasili.
Sifa za tendi
–   Muundo wa kinudhumu (kishairi)
–   Huwa na beti nyingi kati ya 700/800
–   Upatanifu au muunganiko
–   Maudhui kuhusu maisha na matendo ya kishujaa.
Ngomezi/ngoma;Ni fasihi ya ngoma ambapo baadhi ya makabila hupeleka habari kwa njia ya ngoma kupitia midundo fulani ambayo huwakilisha kauli fulani katika lugha ya kabila hilo. Utunzi wa ngoma hutumia kanuni na kaida za kimapokeo zinazofahamika kwa watu wengi katika jamii husika.
Umbo la ujumbe wa ngoma huwa ni la kishairi. Matukio ya dharura kama vita, hutangazwa kwa njia ya ngoma.
Sanaa ya ngoma haijachunguzwa kiasi cha kutosha na huenda ugunduzi huu ukapotea bila kuacha kumbukumbu za kuridhisha kama hazitachunguzwa kwa kina.

]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-27T09:26:36Z 2021-12-27T09:26:36Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1846 <![CDATA[FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI: MUHADHARA WA SITA]]> MUHADHARA WA SITA
   NYIMBO
Zinaelezwa na baadhi ya wataalamu kuwa ni chochote kinachoimbika. Katika nyimbo tunapata ushairi simulizi na ngomezi.
(a)    Ushairi simulizi
Ni tungo za kinudhumu zinazotungwa kwa kufuata kanuni au kutofuata kanuni za urari wa sauti, mapigo ya sauti na mpangilio wa vipashio vya lugha. Lugha ya kishairi katika fasihi simulizi hupambanuliwa na lugha ya kawaida kwa namna inavyopagiliwa na jinsi inavyoingiliana na muktadha wa utendaji. Kanuni za kishairi hupambanuliwa kwa kufuata wizani (rithimu) maalumu na mawimbi ya sauti,mara nyingi lugha huwa ya mkato, tamathali na mafumbo hutumika.
Ushairi simulizi una tanzu nyingi lakini tunaweza kuzigawa zote katika makundi mawili ambayo ni nyimbo na maghani.
Mgawanyo huu ni kwa ajili ya uchambuzi tu kwani nyimbo nyingi pia ni maghani na maghani mengi ni nyimbo.
Nyimbo – ni kila kinachoimbika; dhanna hii inajumuisha tanzu nyingi baadhi zikiwa za kinathari pia huingia kwenye kundi hili pale zinapoimbwa.
Mambo muhimu yanayotambulisha nyimbo
–   Muziki wa sauti ya mwimbaji au waimbaji
–   Muziki wa ala
–   Matini au maneno yanayoimbwa
–   Hadhira inayoimbiwa
–   Muktadha (mazingira) yanayofungamana na wimbo mf: sherehe, Ibada,tanzia,kazi,n.k
Nui au tanzu kuu za nyimbo za Afrika Mashariki
Mashairi
Kundi hili linaundwa na vipengele mbalimbali kama vile:
(i)         Tumbuizo ; hizi ni nyimbo za kuliwaza au kufurahisha watu kwenye matukio mbalimbali kama msiba, ngoma au haruzi.
Tanzu za tumbuizo
(a)    Bembea/pembejezi; ni nyimbo za kubembeleza watoto na hupatikana katika kila kabila.
(b)    Mbolezi; ni nyimbo za kilio au maombolezo na hutumika kuliwaza wafiwa na kuwaondolea machungu.
©    Nyiso; ni nyimbo za jando au unyago na huimbwa na makabila yenye mila na desturi ya kupeleka watoto unyagoni au jandoni, nyimbo hizi hukusudiwa kuwaasa wari kuhusu majukumu ya kiutu uzima pindi watakapohitimu jando au unyago.
(ii)       Nyimbo za siasa
Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa kwenye shughuli za kisiasa kwa lengo la kuelewesha,kuhamasisha,kubeza na kutumbuiza kwenye tukio husika. Mf: ccm… nambari wani, Tumejipanga…….mwaka huu wataisoma, Sasa kumekucha……jogoo limekwishawika Dodomaaa……n.k
(iii)     Tukuzo
Ni nyimbo zinazoimbwa kutukuza au kudhihirisha utukufu na ufahari wa taifa,mtawala,mtu au kitu fulani. Mf: Tazama ramani utaona nchi nzuri…….
Yenye mito na mabonde mengi ya nafakaa…nanenaa kwa kinywa halafu kwa kufikiri nchi iliyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaaa…….majira yetu hayaaaa… yangekuwaje sasa…
Tanzu za tukuzo ni:
(a)    Kongozi; Ni nyimbo za kuaga mwaka au kuadhimisha mwandamo wa mwezi. Nyimbo hizi ni maarufu sana unguja na huchezwa kipindi cha sherehe za kuaga mwaka na huambatana na ngoma ijulikanayo kama Shindwe. Wachezaji huzunguka nyumba hadi nyumba na kupewa chochote wakati wakiimba.
(b)    Nyimbo za dini; Ni nyimbo za kidini ambazo huimbwa na kumtukuza Mungu.
Mfano:
–   Kaswida za kumsifu Mungu
–   Nyimbo za Kikristo kama Tenzi za rohoni, Tumwimbie Mungu na kwaya. Nyimbo za aina hii huwa na maudhui yanayooana na mafunzo ya dini zinazohusika hasa kuhusu Mungu,ibada,dhambi na mapatilizo ya jehanamu na akhera. Nyimbo hizi zinabeba maudhui yanayohusiana na dini zaidi.
©    Nyimbo za taifa; Ni nyimbo za kusifia taifa na huimbwa katika matukio maalumu. Kwa mfano mataifa mengi ya Afrika wimbo wa taifa ni mmoja na asili yake ni wimbo wa Afrika Kusini. (Nkosisikeleeeeliiii Afrikaaa ……. Mumgu ibariki Afrikaaaaa …….Almight God bless Afrikaaaa …….)
(iv)       Chapuzo
Ni nyimbo za kuchekesha na kuhamasisha shughuli au kuwahamasisha watendaji wasichoke wala wasikate tamaa.
Tanzu za chapuzo ni:
Tanzu za chapuzo hugawanywa katika makundi mbalimbali kama vile:
(a)    Kimai; Ni nyimbo zinazoimbwa katika shughuli za uvuvi. Huimbwa ili kuwaondolea wavuvi hofu hasa iwapo ni usiku na vilevile kuwatia ari ya kuvuta makasia.
(b)    Wawe; Ni nyimbo zinazoimbwa wakati wa kazi ya kulima na huimbwa kwa kufuata mapigo ya kupanda na kushuka kwa jembe kadiri walimaji wanavyoinua na kushusha majembe yao kuisakama ardhi.
©    Wimbo wa kutwanga; Wimbo huu huimbwa na wasichana au wanawake wanapopura (kupwaga) ulezi au nafaka yoyote na huimbwa kwa kupokezana wakishindana kupura nafaka. Wimbo huu huleta hamasa na kuwafanya wasichoke mpaka kazi imalizike.
(d)    Nyimbo za vita; nyimbo hizi huimbwa vitani na askari ili kuwahamasisha na kuwaondolea uwoga kwa kuwapandikiza hisia za kizalendo. Mf: ….. Iddi Amini akifa …… mimi siwezi kuliaaa … nitamtupa Kageraaa …… awe chakula cha mambaaa …piga magoti Amini … Amini … piga magoti Aminiiii ….. aaakija toboa … toboa … toboa ….. toboa …  Nyimbo hizi huwasahaulisha kama kuna kufa na hujikuta wakisonga mbele na kumkabili adui.
(e)    Nyimbo za watoto; Nyimbo hizi huimbwa na watoto wakati wa michezo yao,hukusudiwa kunogesha michezo yao. Nyimbo hizi kwa kiasi kikubwa zinasetiri itikadi na falsafa ya jamii kuhusu mahusiano, ndoa na tabia mbalimbali za kibinadamu.
Tenzi au Tendi
Haya ni masimulizi ya kishairi yanayohusu matukio ya kihistoria au kishujaa. Hizi ni nyimbo ndefu za kimasimulizi au kimawaidha ambazo zinahusiana na matukio ya kihistoria, nyimbo hizi zinaitwa tenzi na zinapohusu visa vya mashujaa huitwa tendi.
Mfano: Nyimbo za Issa Matona ni Tenzi, nyimbo za ngoma ya chakacha halikadhalika. Mfano wa tendi ni utendi wa Fumo Liyongo.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-27T09:16:39Z 2021-12-27T09:16:39Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1845 <![CDATA[FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI: MUHADHARA WA TANO]]> MUHADHARA WA TANO
          DUA
Haya ni maombi ya kawaida kwa mizimu mahususi kwa ajili ya kupata mafanikio yanayotegemewa na muombaji.
Mfano:
–   Dua fulani au kuomba mtu fulani apate rehema
(i)         TABANO
Ni manuizo ya maneno kama ya kiganga yasemwayo wakati wa shughuli ya kuzindika au kwa ajili ya kutaka mizimu au miungu ibariki uganga huo.
Mfano:
–   Wazee wetu…mwanenu kaja leo na hiki kidogo kuwataka radhi zenu….nawaomba mumpokee na kumkubalia maombi yake.
(ii)       MASIMULIZI
Ni fasihi yenye kusimulia habari fulani. Masimulizi huwa na sifa zifuatazo:
–   Mpangilio mahususi
–   Wahusika
–   Mandhari
–   Lugha ya kimaelezo
–   Utambaji
–   Maudhui ya kweli au ya kubuni yenye funzo fulani
Masimulizi yanaundwa na tanzu mbalimbali kama vile:
v Hadithi za kubuni; Hadithi hizi huweza kuwa:
(i)         Ngano au vigano
Hadithi za kimapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama,mazimwi na watu katika kuonya na kuadibu kuhusu maisha.
(ii)       Ishara
Ni hadithi ambazo maana yake ya wazi huwakilisha maana ingine iliyofichika.
Mfano:
–   Kusadikika ni ishara kuhusu utawala wa mabavu wa kikoloni.
(iii)     Mbazi
Hadithi itolewayo kama kielelezo cha kufafanulia hadithi inayosimuliwa.
Mfano:
–   Mafundisho ya Yesu katika Biblia aliyafafanua
kwa kutumia hadithi ndani ya masimulizi.
Ipo mbazi kuhusu kisa cha mtego wa panya, mbazi hii inasimuliwa hivi; …. siku moja katika nyumba fulani panya aligundua kuwa ametegewa mtego na kwa kuwa hakuweza kuutegua alienda kuomba msaada kwa ng’ombe lakini ng’ombe alikataa akidai kuwa huo ni mtengo wa panya yeye haumuhusu. Panya hakuchoka akapiga hodi kwa mbuzi na kumlilia shida yake, mbuzi naye akamjibu kama alivyojibu ng’ombe kuwa huo ni mtego wa panya wala haunihusu. Hatimaye panya akamwendea jogoo na kueleza yote lakini jogoo naye alimkataa panya na kumkejeli kuwa huo mtego hamhusu yeye jogoo. Baada ya kugonga mwamba panya akakosa amani akihofia mtego ulioitwa.. “ …wa panya..” kwa kweli siku nzima ile panya hakuweza kujipatia riziki akihofia mtego. Usiku ulipofika baba mwenye nyumba alishituliwa na mkewe akiambiwa kuwa mtego umefyatuka na bila shaka panya atakuwa amenaswa. Baba yule akakurupuka na kuuendea mtego huku akipuuza hadhari ya mkewe kuwa asiende giza giza, alienda huku akijifariji kuwa panya hawezi kumdhuru chochote……alipoufikia mtego ule akapeleka mkono ili auchukue na kumsulubu panya aliyewasumbua kitambo. La haula! Kumbe hakuwa panya, mzee yule akarudi nyuma haraka huku akiagiza mkewe amletee taa haraka. Baada ya taa kuletwa ikabainika mtego ulinasa nyoka na hivyo mzee yule aliumwa na nyoka yule…..ghafla hamkani ikaingia ndani ya nyumba kutafuta dawa ya kumponya mzee mwenye nyumba. Muda si muda mzee yule alikata roho kwa kuzidiwa na sumu ya nyoka na nyumba ikawa na msiba. Siku ya kwanza wageni wachache ikabidi achinjwe jogoo kupata kitoweo. Siku ya pili wageni ni wengi kiasi ikabidi achinjwe mbuzi ili kukidhi mahitaji. Baada ya maziko siku ya tatu na kumaliza tanga akachinjwa ng’ombe.
Funzo:
Hivi ule mtego ulikuwa wa panya,ng’ombe,mbuzi,kuku au baba mwenye nyumba? Mbazi hii inasadifu umuhimu wa kushirikiana kuokoa mambo ambayo yakiharibika yataathiri wengi.
(iv)       Mchapo
Ni hadithi fupi aghalabu husimuliwa kwa watu wanaofahamu historia ya jambo linalotolewa mchapo huo.
Mfano:
–   Kawawa alipoambiwa afunike kikombe ughaibuni ili asiendelee kutiliwa chai hali ametosheka.
–   Mchapo wa kuchapwa viboko kwa Samwel Sitta baada ya kuongoza wanafunzi wenzake kudai siagi akiwa chuo kikuu.
(v)         Hekaya
Ni hadithi ndefu na yenye kuzingatia matukio machache ya kusisimua na ya kustaajabisha. Msuko wake hauchangamani na wahusika huwa ni wachache na bapa.
Mfano:
–   Hekaya za Abunuwasi, Alfu-lela Ulela
Moja wapo ya hekaya za Abunuwasi ni hii:
“ Abunuwasi baada ya kutofurahishwa na utawala wa mfalme wake aliamua kupanga njama za kumpa adhabu mfalme wake huyo, basi siku moja Abunuwasi akapika wali wake na ulipoiva akaufunua ili upoe naye akaendelea na shughuli zingine,baada ya muda akarudi na kukuta nzi wamejaa kwenye chakula chake. Hapo abunuwasi akazua kisa kuwa nzi wamekula harufu yote ya wali wake hivyo akamwendea mfamle ampe waraka utakaomruhusu (Abunuwasi) kuwaua nzi popote atakapowaona. Mfalme bila kujua akampa Abunuwasi waraka huo. Abunuwasi kisha kupata waraka huo akachonga rungu kubwa maalumu kwa kazi ya kuwasaka na kuwaua nzi. Siku moja mfalme akawa na karamu nyumbani kwake iliyohusisha wananchi wake wote akiwemo Abunuwasi. Katika karamu hiyo Abunuwasi alihudhuria na akaketi karibu kabisa na mfalme huku akiwa na rungu lake. Muda si muda huku sherehe ikiendelea ghafla Abunuwasi akainua lile rungu lake na kulishusha kwa nguvu kichwani kwa mfalme, mfalme alianguka palepale na kupoteza maisha. Walinzi wa mfalme walipomshika Abunuwasi akawatolea waraka wenye saini ya mfalme ukisomeka kuwa Abunuwasi ameruhusiwa kuua nzi popote atakapowaona. Basi hapo Abunuwasi akawaambia kuwa lengo lake halikuwa kumdhuru mfalme bali kumsulubu nzi aliyetua kichwani kwa mfalme huyo.”
(vi)       Salua
Ni kipengele cha kimasimulizi kinachojumuisha tanzu za kihistoria zenye kusimulia habari za zamani. Baadhi ya tanzu zake ni:
v Visakale
Ni masimulizi yanayohusu matukio yaliyopita ya kale/zamani kuhusu mashujaa wa kabila au taifa yenye kuchanganya chuku na historia.
Mfano:
–   Hadithi za Liyongo,Mkwawa,n.k
v Mapisi
Ni maelezo ya historia bila kutia maneno ya kubuni. Ni historia halisi ya mtu au kitu au jambo pasipokutiwa chuku.
Mfano:
–   Mapisi ya Tanganyika- mapisi ya historia ya kweli.
v Tarihi
Ni maelezo au jedwali la matukio muhimu na tarehe zake. Hutokea zaidi katika maandishi na huhusu matukio ya kihistoria.
v Nasaba/shajara/potifolio
Ni orodha ya wazee au wahenga wa mtu kuanzia baba,babu na wengine waliotangulia. katika baadhi ya makabila kila mtu hupaswa kufahamu majina ya wahenga wake hadi kizazi fulani.
Mfano:
–   Prof. Sengo anaweza kutaja orodha ndefu ya wahenga wake tangu kizazi cha kwanza hadi cha sasa alichopo yeye. (Tigiti-Yusuf-kibwana-Semindu-Mnyagatwa-Sengo)
–   Watu wengi wenye kuendeleza historia za makabila yao hupenda kutumia majina zaidi ya mawili (mf; John-Joseph-pombe-magufuli)
v Kumbukumbu
Ni maelezo ya matukio muhimu yanayohusu mtu binafsi au jamii ya watu. Fani za wasifu ni aina ya kumbukumbu.
Mfano:
–   Wasifu wa Siti Binti Saad
–   Dereva wa kwanza Tanganyika
–   Uhuru wa watumwa.
(vii)     Visasili
Ni hadithi za kale zenye kuwakilisha imani na mtazamo wa jamii unaohusiana na asili ya ulimwengu na mwenendo wake.
AINA ZA VISASILI
v Visasili vya usuli
Hivi ni visasili vinavyojaribu kuelezea asili ya chimbuko la taifa fulani au wanadamu kwa ujumla.
Mfano:
–   Hadithi ya wayahudi ya kuumbwa kwa ulimwengu na kutokea kwa mwanadamu (Adam na Hawa) ni mfano mzuri wa kisasili cha usuli. Baadhi ya visasili vya usuli hasa Afrika huelezea asili ya mila na desturi fulani ya jamii.
v Visasili vya ibada na dini
Visasili hivi huhusu matendo ya ibada na imani mbalimbali za dunia na mara nyingi hutungwa kisanaa (kuigizwa) katika ibada hizo.
Mfano:
–   Katika ibada za kikristo Ekaristi (kula pamoja chakula cha bwana) ni maigizo ya chakula cha mwisho alichokula Yesu Kristo na wanafunzi wake kabla ya kusulubiwa.
NB:
– Madhehebu ni makundi ya watu wanaoongozwa
na imani fulani.
–     Dini-ni kikundi cha waamini wenye
kufuata utaratibu fulani katika
kumuabudu mungu wao.
v Visasili vya miungu na mizimu
Hivi hupatikana zaidi katika mataifa yenye miungu wengi kama vile Asia, Ulaya ya kale na Misri ya kale.
Hapa Afrika visasili hivi hupatikana kwa wingi katika lugha ya Wayoruba (Nigeria) na katika falme zinazozunguka ziwa victoria (Nyanza).
  1. Maigizo (Drama)
Ni utendaji unaohusisha uigaji wa tabia na matendo ya watu au viumbe uli kuburudisha na kutoa ujumbe kwa njia ya sanaa. Drama za ki-Afrika huambatana na ngoma, utambaji, hadithi, nyimbo na matendo ya kimila kama jando na unyago. Drama nyingi hutumia maleba maalumu (mavazi maalumu) yanayovaliwa na waigizaji ili kuficha uhalisia wao.
AINA ZA MAIGIZO
(i)         Maigizo ya watoto
Watoto wanapocheza mara nyingi huigiza matendo ya kimaisha wanayoyaona katika jamii zao kama vile kulima,kupika,harusi,vita, n.k
Maigizo ya aina hiyo ni sanaa za maonesho zenye kuburudisha na kuwaelimisha watoto pamoja na kukuza vipaji vyao vya ubunifu.
(ii)       Maigizo ya misibani
Maigizo haya hufanywa na watani au wajukuu wa marehemu na huhusiana na maisha, matendo na tabia za marehemu. Maigizo haya hufanywa ili kuwapunguzia wafiwa huzuni na kutoa mafundisho kwa watu waliopo msibani kuhusiana na tabia za marehemu.
Mfano:
–   Kama marehemu alikuwa na tabia mbaya waigizaji/ watani wanaweza kuigiza kwa njia ya kejeli au dhihaka juu ya tabia hiyo.
(iii)     Maigizo ya kwenye sherehe/kidini
Sherehe nyingi za kijadi na kidini huambatana na maigizo mfano; kusimika viongozi huweza kuambatanishwa na kuvishwa aina fulani ya mavazi na kukalishwa katika viti vya asili,kusemewa baadhi ya maneno,kutemewa mate ya Baraka pamoja na kupewa vinywaji fulani kama ishara ya jambo husika.

]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-27T09:15:35Z 2021-12-27T09:15:35Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1844 <![CDATA[FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI: MUHADHARA WA NNE]]> MUHADHARA WA NNE
   SEMI
Semi ni mojawapo kati ya kumbo za fasihi simulizi. Semi hutawaliwa na sifa tambulishi mahususi. Semi hufafanuliwa kama tungo au kauli fupi fupi za kisanaa zenye kubeba maana au mafunzo maalumu ya kijamii. Kumbo hili lina tanzu zifuatazo.
–   Methali
–   Vitendawili
–   Mafumbo
–   Misimu
–   Lakabu
–   Kauli tauria (tafsida)
(a)    Methali
Ni semi fupi za kimapokeo zinazodokeza fikra au funzo zito linalotokana na tajiriba (uzoefu wa maisha ya jamii).
Mfano:
–   Haraka haraka,haina Baraka
–   Mwenda pole,hajikwai
Mara nyingi falsafa ya methali huelezwa kwa kutumia tamathali hasa sitiari au mafumbo. Methali hubeba hekima na busara ambazo aghalabu hutumika kuonya, kuasa, kutia moyo, kuadilisha na kuadibu.
(b)    Vitendawili
Kitendawili ni usemi uliofumbwa wenye kuchochea fikra na udadisi wa mambo. Vitendawili ni sanaa inayotegemea uwezo wa mtu kutambua, kuhusisha na kulinganisha vitu vya aina mbalimbali katika mazingira yake.
Mfano:
–   Wanangu wawili hushabihiana sana- (maziwa na tui la nazi)
–   Ikiwa ya moto hainyweki ikipoa hainyweki –(supu)
©    Mafumbo
Mafumbo ni kauli zenye kuchemsha bongo. Kauli hizi humtaka anayeulizwa atumie akili na udadisi kufumbua fumbo. Mafumbo ni hatua ya juu ya vitendawili.
AINA ZA MAFUMBO
Kuna mafumbo ya kuchemsha bongo na mafumbo majina.
(i)         Mafumbo ya kuchemsha bongo
Ni maswali yenye kutaka kutumia akili na ujuzi ili kujibu .Baadhi ya mafumbo ni ya kimapokeo na mengine hubuniwa na msemaji kwa lengo maalumu.
Mfano:
–   Nina kilo moja ya pamba na kilo moja ya mawe je, kipi ni kizito zaidi? (Jibu: vyote vina uzito sawa)
–   Mtu mmoja alikuwa na ng’ombe fahali wawili akitokea Kenya kuja Tanzania akiwa mpakani ng’ombe mmoja akazaa je, maziwa watakunywa watu wa wapi? (Jibu: Fahali hazai)
(ii)       Mafumbo majina
Huwa ni majina ambayo yamebeba maana fulani inayofungamana na tukio au hali iliyojitokeza kipindi cha kupatikana kwa mwenye jina hilo. Aghalabu hutumika kama njia ya kuhifadhi kumbukumbu inayohusiana na mhusika.
Mafumbo jina huweza kuwa mepesi au mazito kulingana na maana ya fumbo lenyewe lililobebeshwa kwenye jina la mhusika.
Baadhi ya mafumbo jina huwa ya kikabila.
Mfano:
–   Tabu,shida- alipatikana kwa hali hiyo
–   Mwanjaa –alizaliwa msimu wa njaa
–   Mwamvita – msimu wa vita
–   Majuto,riziki,bahati – hali husika
–   Tenahuvo – hana makuu (kipare)
–   Mwendwa – mpendwa (kibena)
–   Gumbo – njaa (kizigua)
–   Aimbora – Baraka (kimachame)
(d)    Simo/misimu
Ni semi za muda na mahali maalumu ambazo huzuka na kutoweka kutegemea mazingira maalumu. Misimu ikipata mashiko husanifishwa na kuingizwa katika msamiati, methali au vitendawili.
Mfano:
–   Tamutamu mahonda ukinila utakonda- (msimu uliozuka baada ya kuanzishwa kiwanda cha pombe kali cha Mahonda huko Zanzibar)
–   CCM – Chukua Chako Mapema
–   UPE – Ualimu Pasipo Elimu
–   SU – Soma Ule
(e)    Lakabu
Ni majina ya kupanga ambayo mtu hupewa au hujipa kutokana na sifa au tabia alizonazo. Majina haya hubeba maana iliyofumbwa.
Mfano:
–   Kifimbo,mchonga – Nyerer,J.K
–   Mzee Ruksa – Ali-Hasan Mwinyi
–   Simba wa vita – Kawawa
–   Mkuki uwakao – Jomo Kenyatta
(f)    Kauli tauria/tafsida
Hizi ni kauli zenye mchanganyiko au mfuatano wa sauti zinazotatanisha kuzitamka ambazo hutumiwa kupunguza utusi na ukali wa baadhi ya maneno.
Mfano:
–   Wauwao wawe wao wauwa wewe wauawa
–   Wale wali wale wali wao
–   Pema ujapo pema ukipema si pema tena
–   Ukiona neno usitie neno ukitia neno utapatwa na neno.

]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-27T09:09:52Z 2021-12-27T09:09:52Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1843 <![CDATA[FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI :MUHADHARA WA KWANZA NA WA PILI]]> FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI
MUHADHARA WA KWANZA
FASIHI NI NINI?
Dhanna ya fasihi imekuwa ikijadiliwa kwa karne nyingi na wataalamu mbalimbali huko ulaya. Dhanna hii imekuwa ikihusishwa na neno la Kilatini Litera lenye maana ya herufi au maandishi. Neno hilo ndilo limefasiriwa kwa Kiingereza kama Literature.
Mitazamo iliyotawala dhanna hii ni mingi kama ifuatavyo:
(a)    Mtazamo wa kwanza ni ule unaodai kuwa literature ni jumla ya maandishi yote katika lugha fulani. Wellek na Warren wanauelezea mtazamo huu kwa kusema kuwa, “ One way is to define Literature as everything in Print. Wellek na Warren (1986:20)
        Udhaifu wa mtazamo huu:
(i)         Mtazamo huu unapanua sana uwanja wa fasihi na kuingiza vitu vyote ambavyo kwa kawaida watu hawavifikirii kuwa ni fasihi kwa sababu tu vimeandikwa.
Mtazamo huu unabagua sehemu kubwa ya fasihi ya ulimwengu ambayo haikuandikwa au kupigwa chapa (Ambayo ndiyo chanzo cha maandishi ya kifasihi mf. Matambiko, ngoma, majigambo, n.k).Katika taaluma ya fasihi katika Kiswahili neno Literature lilitafutiwa namna ya kuitwa na kupewa maneno kama adabu ya lugha na fasihi.
Hatimaye neno fasihi likashinda na kupewa ufafanuzi kuwa ni sanaa ya lugha bila kujali kama imeandikwa au la.
(b)    Mtazamo wa pili ni ule unaodai kuwa Literature ni maandishi bora ya jamii ya kisasa yenye manufaa ya kudumu. Hollis Summers anafafanua kuwa; The word literature in its strictness sense means more than printed words, is one of the fine arts. Mtazamo huu unaupa uzito usanii na uwezo wa kubaini fasihi kwa kuihusisha na maandishi na maandiko bora tu.
©    Mtazamo wa tatu; unaitazama Literature kama sanaa ya lugha yenye ubainifu bila kujali kama imeandikwa au la. Kwa mtazamo huu nyimbo na masimulizi ya kisanaa ni fasihi.
Mtazamo huu uliambatana na kuzuka kwa tapo la ulimbwende huko ulaya mwishoni mwa karne ya 18. Tapo hili liliathiriwa na falsafa za watu kama Kant na Hegel (Eagleton 1983:120-21). Mtazamo huu ndio unaotawala kwa sasa na unadai kuwa neno fasihi limetokana na neno la kiarabu lenye maana ya Ufasaha au uzuri wa lugha. Kwa hiyo istilahi Literature (fasihi) katika taaluma ya Kiswahili inatofautiana na istilahi Literature katika Kiingereza. Neno fasihi halihusiani na maandishi wala vitabu bali ufasaha wa kauli. Dhanna hii katika Kiswahili inazingatia aina zote za fasihi, iliyoandikwa na ile ya mdomo.
(d)    Mtazamo wa nne; ulizuka hapa Afrika Mashariki na kuenea miaka ya 1970. Mtazamo huu unadai kuwa…..Fasihi ni hisi ambazo zinajifafanua kwa njia ya lugha….. Waumini wa mtazamo huu ni John Ramadhan, Balisidya,A na Sengo na Kiango katika Hisi Zetu. Mtazamo huu unachanganya mambo matatu ambayo ni fasihi yenyewe, mambo yaelezwayo na fasihi na mtindo wa fasihi ya Kiswahili. Fasihi huweza kuelezea hisi, kadhalika mtindo wa kifasihi mara nyingi ni wa kihisiya bali fasihi yenyewe si hisi.
–   Vivyo hivyo fasihi huweza kuelezea mapenzi lakini fasihi yenyewe si mapenzi.
(e)    Mtazamo wa tano; ni wa karne hii ulioanzishwa na wafuasi wa nadhariya ya umbuji (formalism). Mtazamo huu ulianzishwa na wanaisimu wa Kirusi mwanzoni mwa karne hii miongoni mwao akiwa Boris, Tomashevski, Roman Jakobson na Victor Shklovski. Hawa wanadai kuwa fasihi ni tokeo la matumizi ya lugha kwa njia isiyo ya kawaida ili kuleta athari maalumu. Kwa mujibu wa watu hawa, fasihi hukiuka taratibu za kawaida za matumizi ya lugha katika sarufi ili kumvutia msomaji au msikilizaji.
Lugha ya kifasihi humfanya msomaji aitafakari lugha yenyewe badala ya kutafakari tu ujumbe unaowasilishwa na lugha hiyo.
  Udhaifu wa mtazamo huu
(i)         Unaelemea mno upande wa fani na kupuuza maudhui
(ii)       Unasadifu zaidi ushairi kuliko fani nyingine za fasihi
Kwa maelezo yote yaliyotolewa tunaweza kuhitimisha kuwa fasihi ni sanaa itumiayo maneno teule ya lugha yenye ubunifu inayojaribu kusawiri vipaji vya maisha, mahusiano na hisiya za watu katika miktadha mbalimbali.
CHIMBUKO LA FASIHI
Kuhusu chimbuko la fasihi wataalamu mbalimbali wametoa hoja zao na kuibua nadhariya kadhaa:
  1. Nadhariya ya kidhanifu; nadhariya hii hujiegemeza kwenye dhanna zisizoweza kuthibitishwa kisayansi. Nadhariya hii inadai kuwa chimbuko la fasihi niMungu.
Nadhariya hii ndiyo kongwe na ilikuwepo tangu kabla ya Kristo na ilitumiwa sana na Wayunani wa huko Ulaya ambao waliamini sana miungu kama wa Ushairi na Muziki ambao waliwaita Muse.
Miungu hawa waliaminika ndio waliowapa watunzi Muhu au Kariha (Msukumo) wa kiroho, nafsi na kijazba wa kutunga kazi zao.
Wanaounga mkono nadhariya hii wanadai kuwa Mungu ndiye msanii mkuu na wa kwanza. Wasomi wa kale waliounga mkono nadhariya hii ni Hesiod, Plato, Aristotle na Socrate.
Udhaifu wa nadhariya hii:
(i)         Nadhariya hii inakataa kuwepo kwa dhanna ya ubunifu kwa watunzi
(ii)       Haichochei kujiamini kwa wasanii na huwafanya wajione kama waigaji tu wa mambo yaliyofanywa na Mungu
(iii)     Huwafanya wasanii waonekane ni watu waliokaribu sana na Mungu kuliko binadamu wengine
(iv)       Huibua dharau miongoni mwa wasanii na kusababisha wajitenge na jamii ya kawaida
     DHIMA YA FASIHI
Fasihi ni sanaa itumiayo maneno teule ya lugha kufikisha ujumbe kwa jamii. Hivyo fasihi ina dhima (wajibu/majukumu) mbalimbali kwa jamii kama ifuatavyo:
v Kuelimisha jamii kupitia vipengele mbalimbali kama nyimbo,hadithi,ngoma,nk
v Kuhifadhi na kurithisha amali za jamii katika vizazi mbalimbali vya jamii.
v Kuburudisha jamii na kuifanya ijisahaulishe madhila mbalimbali yanayoikuta jamii
v Kukuza na kuendeleza lugha ya jamii.
Hata hivyo unapojadili dhima ya fasihi huna budi kuzingatia dhanna ya utabaka na itikadi.
Tabaka; ni makundi ya watu yanayounganishwa na uhusiano wao na njia za uzalishaji mali na mfumo wa mamlaka katika jamii.
Itikadi; inafafanuliwa kuwa ni imani juu ya yale yasemwayo na jamii na kuyaamini yale yanayohusiana na mahusiano ya kiutamaduni ya jamii tunamoishi.
Dhanna ya utabaka na itikadi zinajitokeza katika fasihi kwa sababu zifuatazo:
(i)         Kwanza fasihi hufungamana na muktadha (mazingira maalumu ya kijiografia), kiutamaduni, kiuchumi, kisiasa na hivyo kila kazi ya fasihi ni zao la muktadha ulioizaa kazi husika.
(ii)       Pili, fasihi hudhihirisha aina fulani ya urazini (kujitambua kibinadamu/kuwa na utashi) na utambuzi wa hali ya maisha alionao mtunzi pamoja na wale anaowawakilisha.
(iii)     Tatu; zipo jamii za aina mbili nazo ni jamii zenye usawa na mshikamano ambazo hazina matabaka nazo huitwa jamii zenye utabaka usio wa kinyonyaji mfano jamii za wavuvi, wafugaji, wakulima, n.k. katika jamii hizo fasihi zao zitabeba dhima tofauti.
Kwa ufafanuzi huo waweza kubaini kuwa kwa ujumla dhima ya fasihi inajikita katika mambo yafuatayo:
–   Itikadi, utamaduni, falsafa, uchumi, siasa, nk.
(a)    Dhima ya itikadi
Kila jamii hutawaliwa na itikadi fulani ambayo ndiyo huzalisha misimamo ya jamii husika katika uzalishaji mali. Kila mtunzi wa fasihi mtiifu kwa jamii yake lazima ataathiriwa na itikadi ya jamii yake na hatimaye utunzi wake kuwa na mwelekeo wa utetezi wa itikadi iliyommeza.
 Mfano:
–   Kipindi cha ukoloni watunzi wengi walibanwa na itikadi za kikoloni na kujikuta wakitetea tabaka la wakoloni. Mifano ya kazi za fasihi kama Mashimo ya Mfalme Suleman, Uhuru wa Watumwa, Hekaya za Abunuwasi, n.k.
Maandishi hayo yalijaribu kutetea itikadi ya ukoloni kwa kuwaonesha wakoloni wa kizungu kama watu wenye uwezo wa hali ya juu, wema na wachapakazi, wenye akili nyingi waliojua kukomboa na kumuendeleza mwafrika. Pia maandishi hayo yalisisitiza maadili ya utii ambao ulisaidia watawala kuwadhibiti watawaliwa kimawazo.
(b)    Dhima ya kiuchumi
Dhima ya fasihi katika uchumi huonekana zaidi kupitia nyimbo za kazi ambazo hutungwa ili ziimbwe wakati wa kufanya kazi ngumu. Mfano: kazi kama kulima, kutwanga,kuvua samaki,kuwinda na shughuli nyingine.
Katika uchumi wa kibepari dhima ya fasihi ilijikita zaidi kwenye kuburudisha,kutafuta pesa kwa kurekodi na kuuza kazi za fasihi. Ni katika kipindi hiki palizuka fasihi pendwa iliyojikita kwenye kujipatia pesa zaidi na kusahau maadili ya jamii.
©    Dhima ya kiutamaduni
Katika dhima hii fasihi ina majukumu yafuatayo:
–   Kuhifadhi na kurithisha amali za jamii
–   Kuburudisha
–   Kukuza lugha
–   Kuelimisha,kuasa na kurekebisha jamii.
Amali za jamii ni pamoja na mila, desturi, mtindo wa maisha, imani, jiografia, visasili, maarifa ya kijadi n.k.
Amali hizi huweza kuendelezwa na kuhifadhiwa katika fasihi na kurithishwa vizazi vijavyo. Kwa mfano; Tamthiliya ya Kinjeketile imehifadhi mengi kuhusu hali ya maisha wakati wa ukoloni wa kidachi. Kurwa na Doto hali kadhalika, Bwana Muyombekere na Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulihwali, Mirathi ya Hatari na Mashetani ni kazi za fasihi zilizohifadhi amali nyingi sana za jamii za kiafrika hasa Tanzania.
Fasihi hasa nyimbo na visasili hutumika kukoleza shughuli za kijamii kama ibada,matambiko,sherehe, n.k. Nyimbo licha ya kuburudisha pia hubeba ujumbe kuhusiana na tukio husika.
Kinafsiya fasihi pendwa kwa mfano ile ya masaibu na vituko vya ujambazi na uhalifu humpa msomaji imani kuwa anashuhudia na kushiriki katika matukio ya ushujaa yanayosimuliwa na hivyo kusisimua mwili na kuridhisha ari yake ya kujihusisha na matendo ya kishujaa.
Malighafi ya fasihi ni lugha, kwa kadiri lugha inavyotumiwa na kufinyangwa na watunzi ndivyo inavyokua na kupanuka. Maneno mengi yanayotumika katika utunzi wa mashairi, riwaya, nyimbo na tamthiliya hufanya lugha ikue. Kwa mfano: katika sanaa ya ushairi maneno kama vina na mizani, mshororo, muwala, tathilitha, takhmisa, tarbia, n.k huchochea ukuaji wa lugha katika jadi ya ushairi ambao huchukuliwa kama ghala la maneno.
Fasihi hubeba elimu za kila aina, baadhi ya watunzi ni mabingwa wa kuonesha ufundi katika maandishi. Mfano: maandishi ya Ngugi wa Thiong’o kama vile Petals of Blood na Nitaolewa Nikipenda vilevile Alamin Mazrui katika: Kilio cha Haki, na F. Katalambula katika Simu ya Kifo husawiri vizuri mandhari ya kijiografia na maneno yaliyokuza watunzi na ujuzi wao katika kumudu lugha.
Hadithi za kisayansi kwa mfano: Jina langu ni Sifuri na Kipeo na Kipeuo na Mahakamani zimekusudia kuwafundisha watoto dhanna hizo za kisayansi kwa njia ya kisanaa.
Elimu ya ukweli sharti iambatane na tabia ya uchunguzi, uchambuzi na udadisi. Tabia hiyo ni usomaji wa uhakiki wa fasihi ya msomaji ambayo humsaidia msomaji kupanua upeo wa kudadisi na kukosoa.
Fasihi hutoa maonyo, huasa na kuiadilisha jamii ili iendane na mila na desturi za jamii husika mfano: hadithi kama vigano vyenye kuhusu tabia za fisi husaidia watoto kujirekebisha kitabia.
(d)    Dhima ya kisiasa
Fasihi imetumika sehemu nyingi sana kuendeleza au kudumaza harakati za kisiasa nchini Tanzania kwa mfano; fasihi imetoa mchango mkubwa sana kupitia ngonjera za Azimio La Arusha. Nyimbo za kizalendo kama Tanzania, Tanzania na Tazama ramani, ni miongoni mwa kazi za fasihi ambazo zimetoa mchango katika siasa. Hadi sasa nyimbo za kizazi kipya zinaendelea kushughulika na siasa mifano ipo mingi ila kwa uchache tu: Ndio Mzee na Sio Mzee (Joseph Haule/Prof.Jay), Tanga Kunani Pale? (Wagosi wa Kaya), Muungano CCM na CUF (Juma Kassim/Juma Nature) n.k
(e)     Dhima ya kifalsafa
Baadhi ya kazi za fasihi hujaribu kuelezea falsafa fulani kuhusu maisha. Falsafa hiyo watunzi wengine huita ukweli wa maisha ingawa si kila wakati ukweli huo hukubalika kwa wote.
Kazi za fasihi za kifalsafa huchambua masuala mazito kuhusu maisha ya mwanadamu duniani na hatima yake. Fasihi hii huchochea wasomaji na wasikilizaji kutafakari masuala hayo kwa umakini na undani zaidi.
Mifano ya fasihi za kifalsafa ni Utenzi wa Al-Inkishafi, Nagona, Mzingile, Karibu Ndani, Kusadikika, Kufikirika, Rosa Mistika, n.k
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-03T12:36:33Z 2021-12-03T12:36:33Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1669 <![CDATA[FASILI YA NENO KILEKSIKA, KIMUUNDO NA KISARUFI]]> DHANA ZA MSINGI
(a)  Mofimu
Kwa mujibu wa Matinde (2012:101) mofimu ni maana inayowakilishwa na mofu. Pia mofimu ni dhana ambayo ni sehemu ya umilisi kwa watumiaji wa lugha husika.
Mofimu ni vipashio vidogo vya msingi vinavyotumika katika kuunda maneno ya lugha. Mofimu ni vipashio vinavyoonyesha uhusiano uliopo kati ya sauti msingi za lugha yaani fonimu na maana maalumu katika sarufi ya lugha (Besha, 1994:52).
Aidha Massamba na wenzake (2013:13) wanaeleza kuwa mofimu ni kipashio kidogo kabisa katika umbo la neno kilicho amilifu (yaani kilicho na kazi ya kisarufi au kileksika) na ambacho hakiwezi kuvunjwa au kugawanywa katika vipande vingine vidogo bila kupoteza uamilifu wake.
Kwa ujumla mofimu ni kipashio kidogo cha lugha chenye maana kisarufi au kileksika.
Aina za MofimuMatinde (2012) ameainisha na kuelezea aina kuu mbili za mofimu yaani mofimu huru na mofimu tegemezi.
Mofimu huru. Ni silabi moja au zaidi yenye maana kamili ya neno na inaweza kujisimamia yenyewe bila msaada wa viambishi au silabi nyingine. Aghalabu mofimu huru huwa nomino, vivumishi au vielezi visivyochukua viambishi vya ngeli mfano daktari, ndoa, nyumba.
Mofimu tegemezi. Ni mofimu ambazo huhitaji viambishi ili kukamilisha maana iliyokusudiwa. Mofimu hizi hujumuisha mzizi wa neno au shina la kitenzi, kivumishi, nomino au vielezi ambavyo vinahitaji viambishi viwakilishi vya ngeli ili kutoa maana iliyokusudiwa.
Kwa ujumla mofimu inaweza kujidhihirisha kwa namna kuu tatu tofautitofauti ambazo ni;(i) mzizi. Mfano; ruk-   ruka                             Kop-  kopa                             Pig-    piga                            Lim-   lima                             Chez- cheza                       (ii) kiambishi. Mfano; a-na-temb-e-a                                      a-na-lim-a                                   kop-esh-a                                   a-na-chez-a(iii) Neno yaani neno sharti liwe linajitosheleza kimaana  mfano Baba, Dirisha, Mama, Kaka, Babu, Asha, Juma na maneno mengineyo mengi ya namna hiyo.
(b) AlomofuMatinde (2012:100) Alomofu ni maumbo mawili au zaidi yanayowakilisha mofimu moja na hutokea katika mazingira maalum ya utokeaji.
Besha (1994:55) anaeleza kuwa Alomofu za mofimu ambazo zinatokea katika mazingira maalumu ya kifonolojia ya utokeaji wake unaweza kutabirika.
Hivyo basi, Alomofu ni maumbo mawili au zaidi yanayowakilisha mofimu ileile moja na ambayo huweza kutokea katika mazingira maalum.
Kanuni za alomofu katika kauli ya kutendeka.
Matinde (2012:192) anasema kuwa alomofu {-ik-} hutokea katika shina likiwa na irabu mojawapo kati ya a, i au u na mzizi huo huishia na konsonanti ambayo huonyesha ubora wa jambo fulani au uwezekano wa kitu kufanyika.Mfano;  {imb-} + //-ik-// + {-a} = imbika              {umb-} + //-ik-// + {-a} = umbika              {fany­-} + //-ik-// + {-a} = fanyika              {pit-} + //-ik-// + {-a} = pitika              {tup-} + //-ik-// + {-a} = tupikaHabwe na Karanja (2007:110) anasema alomofu /-ek-/ hutokea iwapo mzizi wa kitenzi ndani yake una irabu e au o na mzizi huo huishia na konsananti na huonyesha ubora wa kitu/jambo kufanyika au uwezekano wa jambo fulani kufanyika.Mfano;   {jeng-} + //-ek-// + {-a} =jengeka               {pony-} + //-ek-// + {-a} = ponyeka                  {chom-} + //-ek-// + {-a} = chomeka               {tosh-} + //-ek-// + {-a} = tosheka               {som-} + //-ek-// + {-a} = someka               {tek-} + //-ek-// + {-a} =tekeka© MofuMatinde (2012) akiwanukuu TUKI (1990) wanaeleza kuwa mofu ni kipashio cha isimu maumbo kiwakilishacho mofimu.
Matinde (2012) Mofu ni umbo kamili ambalo huwakilisha mofimu. Umbo hilo hudhihirika kifonolojia na kiothografia (uwezo wa kutamkwa na kuandikwa).
Katika lugha ya kitaalamu umbo linalowakilisha mofimu hujulikana kama mofu (Massamba na Wenzake, 2013:14).
Kwa ujumla mofu ni umbo au maumbo yanayowakilisha mofimu na ambayo yanaweza kudhihirika kwa kutamkwa au kimaandishi.
Aina za MofuMatinde (2012) ameainisha mofu kwa kuzingatia vigezo viwili ambavyo ni:          (i) kigezo cha isimu maana          (ii) kigezo cha isimu maumboKatika kigezo cha isimu maana tunapata aina kuu tatu za mofu ambazo ni;        (i) Mofu huru        (ii) Mofu funge        (iii) Mofu tata
(i) Mofu huruNi mofu ambazo zinaweza kukaa peke yake kama maneno kamili yenye maana inayoeleweka bila kusaidiwa na mofu nyingine. Mofu huru zinaweza kuwa nomino,  kivumishi,  kiwakilishi, kielezi, kitenzi au kiunganishi.
(ii) Mofu funge au tegemeziNi mofu ambayo haiwezi kukaa peke yake kama neno lenye maana kamili. Mofu hizi huhitaji kuambatanishwa na mofu nyingine ili kupata maana sawa au neno kamili. Mfano: M-toto – w-atoto             Ki-su – vi-su             M-ti – mi-ti             Ji-tu – ki-ji-tuWakati mwingine mofu funge inaweza ikatokea katika mizizi ya vitenzi: Mfano: {-l-} katika neno kula              {-f-} katika neno kufa              {lim-} katika neno lima              {-j-} katika neno kuja              {-nyw-} katika neno kunywa
(iii) Mofu tataNi mofu ambayo huwa na maana zaidi ya moja yaani kuanzia mbili na kuendelea. Mofimu tata hutokea katika vitenzi vilivyopo katika kauli ya kutendea.Mfano:        Alimpigia = a-li-m-pig-i-a.                   Alimchezea = a-li-m-chez-e-a.                   Alimchomekea = a-li-m-chom-ek-e-a.Hivyo mofu {-i-} na {-e-} ni mofu ambazo zinaonyesha kauli ya kutendea na ndizo zinaleta utata katika vitenzi hivyo.
 Kigezo cha isimu maumboMatinde (2012) anaeleza kuwa katika kigezo hiki cha isimu  maumbo kuna aina kuu mbili za mofu. Aina hizo za mofu ni;            (i) Mofu changamani            (ii) Mofu kappa
(i) Mofu changamaniNi mofu inayoundwa kutokana na mwambatano wa mizizi miwili ambayo inaweza ikawa ni mizizi sahihi miwili kama vile;             {Askari} + {Kanzu} = Askarikanzu             {Gari} + {Moshi} = Garimoshi             {Fundi} + {Chuma} = FundichumaPia inaweza ikawa mofu funge + mofu huruMfano: {Mw-} + {-ana} + {nchi} = Mwananchi             {Mw-} + {-ana} + {hewa} = Mwanahewa


(ii) Mofu kapaNi mofu za pekee ambazo hazina umbo. Mofu kapa hazitamkwi wala kuandikwa. Mofu kapa hazionekani katika neno lakini athari zinazotokana na mofu kapa hueleweka.Mfano;    Umoja           wingi              U-kucha   –    ⱷkucha             U-kuta      –    ⱷkuta             U-funguo –     ⱷfunguo
Nomino zilizo na kiambishi cha wingi tu cha umoja hakipoMfano; umoja        wingi              ⱷkasha        Ma – kasha               ⱷdebe         Ma – debe               ⱷjembe       Ma – jembe
(b) Fasili ya neno kileksika, kimuundo na kisarufi  (i)  Fasili ya neno KileksikaNeno ni kipashio kidogo cha lugha chenye maana. Kwa maana hiyo neno ni lazima liwe na maana inayoeleweka kwa jamii inayotumia lugha hiyo. (Mdee, 1977).Mfano:   Mama- Mzazi wa kike               Ndama- Mtoto wa ng`ombeDhana hii ina mashiko kwa sababu maneno mengi katika lugha yana maana ya kueleweka kwa watumiaji wa lugha.
Udhaifu wa fasili hiiSi kila neno linalotumika linaweza kuwa na maana ya wazi au ya kileksika. Mfano baadhi ya maneno hasa  viunganishi na vihusishi  kama  vile ya, kwa, na, wakati ambapo yanakua hayana maana ya kileksika lakini yana uamilifu kisarufi.
  (ii) Fasili ya neno kimuundoNeno ni kipengele kidogo kabisa cha sentensi ambacho kinaweza kuhamishwa kutoka nafasi moja hadi nyingine bila kuathiri sarufi ya lugha katika tungo au sentensi hiyo (cruse, 1986) akinukuliwa na (Mdee, 1997).  Kwa ujumla hapa kinachotazamwa zaidi ni kategoria za maneno na mpangilio wake katika tungo.
Mfano: Ali   alimuua     Ahmed              N          T               N            Ahmed    alimuua   Ali
                 N            T          NHapa N ni nomino na T ni kitenzi japo nomino zimebadilishana nafasi lakini sarufi hiyo haijaathirika. Utaratibu huu husaidia katika kujifunza sarufi ya lugha hasa miundo ya tungo kama kirai, kishazi na sentensi na pia kujua sehemu za tungo kama kiima na kiarifu.Udhaifu wa fasili hii·         Sio maneno yote yanaweza kuhamishwahamishwa bila kuvuruga sarufi ya lugha
Mfano;   Ali alisimama kando ya mto                        Amesimama kando ya mto Ali                        Kando ya mto Ali amesimama                        *Mto Ali amesimama kando ya                        *Mto ya kando amesimamaHivyo sentensi mbili za mwisho hazikidhi haja ya usahihi wa kisarufi.·         Vilevile unapohamisha maneno basi maana ya neno pia hubadilika.
Mfano;      Zubeda anampenda Zawadi                        Zawadi anampenda Zubeda
Nomino zimebadilishana nafasi hazijaathiri sarufi ya lugha lakini kimaana imebadilika kwa sababu katika sentensi ya kwanza Zubeda ndiye anatenda tendo na katika sentensi ya pili Zawadi ndiye anatenda tendo.
(iii) Fasili ya neno kisarufi Kwa mujibu wa Katamba (1993:19) ili neno litambulike lazima liwe katika muktadha wa matumizi. Katamba anasema neno moja linaweza kuwa na dhima mbalimbali na dhima hiyo itagundulika tu litakapokuwa ndani ya muktadha wa matumizi kwenye sentensi. Anatoa mfano wa neno la kiingereza “cut” kwamba likiwa kipwekepweke mtu hawezi kutambua linarejelea nini pamoja kwamba neno hilo katika lugha ya kiingereza ni kitenzi yaani ‘kata’ lakini kuna wakati linaweza kutumika kurejelea nomino. Mfano I need my cut na I have cut my fingure. Ukichunguza vizuri mifano hii ‘cut’ katika sentensi ya kwanza hurejelea nomino na katika sentensi ya pili hurejelea kitenzi. Sentensi ya kwanza ilikuwa na maana ‘nahitaji stahiki yangu’ na ya pili ina maana ya ‘nimekata kidole’.
Kigezo hiki huenda mbali kwa kufafanua kuwa pia maneno kama ‘na’, ‘tu’, ‘si’ katika Kiswahili na maneno kama ‘and’, ‘an’, ‘the’ ‘on’ katika kiingereza nayo hayawezi kutambulika yanarejelea nini, lazima yawe katika muktadha wa matumizi ndio tunaweza kusema ni aina gani za maneno na kutambua maana zake.
Udhaifu wa fasili hii     Si lazima maneno yote yawe katika muktadha wa matumizi ndipo tuweze kubaini maana zake kwani kuna baadhi ya maneno huweza kutambulika kuwa yana maana gani  hata yasipokuwa katika muktadha wa matumizi katika sentensi. Kwa mfano nomino za mahali kama vile Dodoma, Mwanza na Morogoro na majina ya watu kama vile Amina, Omari, Magreth na Ali.
HITIMISHOHivyo basi katika kufasili dhana ya neno ni vyema kuzingatia vigezo vyote vya kisarufi kama vile fonolojia, maana, sarufi ili kupunguza changamoto zinazojitokeza katika kufasili dhana hii kama ilivyobainishwa hapo juu.
 
MAREJELEO:
Besha, R.M. (2007). Utangulizi wa Lugha na Isimu. Dar es Salaam: Macmillan Aidan Ltd.
Habwe, J. & Karanja, P. (2007). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers.
Katamba, F. (1993). Morphology. London: Macmillan Press Ltd.
Massamba, D.P.B  na Wenzake. (2013).  Fonolojia ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: TUKI.
Matinde, R.S. (2012). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia: Kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu. Mwanza: Serengeti Educational Publishers (T) Ltd.
Mdee, D. (2007). Nadharia za Leksikografia. Dar es Salaam: TUKI.
TUKI. (1990). Kamusi ya Isimu na Lugha. Dar es Salaam: TUKI
]]>
false