MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Kiswahili Kimataifa]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ 2024-04-27T23:55:54Z MyBB MwlMaeda]]> 2022-07-08T12:24:42Z 2022-07-08T12:24:42Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2682 <![CDATA[Je wafahamu misingi iliyowezesha Kiswahili kuadhimishwa 7/7?]]> siku ya Kiswahili duniani.

SOMA KWA KINA HAPA &t&t&t&t&t&t&t&t]]>
false
MwlMaeda]]> 2022-07-07T17:00:40Z 2022-07-07T17:02:19Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2669 <![CDATA[Kwa nini 7/7 na si tarehe nyingine?]]>
Tarehe iliyopendekezwa ya siku ya Kiswahili duniani ni tarehe 7 mwezi Julai kwa kuwa katika tarehe hiyo mwaka 1954 ni siku ambayo chama cha Tanganyika African National Union, TANU chini ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilipitisha Kiswahili kama lugha ya kuunganisha harakati za ukombozi. Bila shaka, Rais wa zamani na pia Baba wa Taifa la Kenya, Hayati Mzee Jomo Kenyatta, pia alitumia lugha ya Kiswahili kupitia kauli yake maarufu, “Harambee” ya kuhamisha watu wakati wa harakati dhidi ya ukoloni. Zaid iya hapo tarehe 7 mwezi Julai mwaka 2000, jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, ilianzishwa tena kurejesha ushirikiano na utangamano baina ya wananchi wa Kenya, Tanzania na Uganda ambako Kiswahili kinazungumzwa zaidi. Rwanda, Burundi na Sudan Kusini zimejiunga baadaye na ni wanachama wa EAC.]]>
false
MwlMaeda]]> 2022-02-03T02:27:33Z 2022-02-03T03:26:12Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2385 <![CDATA[KISWAHILI BIDHAA KUBWA DUNIANI]]>
.jpg   e0fde1ac-7899-4653-ac85-f4933d015491.jpg (Size: 252.81 KB / Downloads: 1)

KISWAHILI BIDHAA KUBWA DUNIANI

Watanzania wana rasilimali adhimu

Gazeti la Alhuda Alhamisi  Februari 3, 2022 linaandika kwamba:

Kiswahili ni bidhaa yenye thamani kubwa inayohitaji kuthaminiwa ili iipatie nchi tija na kueneza mila na tabia zake za kiungwana kwa wengine nje ya nchi.

Aidha bidhaa hiyo haina budi kuuzwa na wamiliki wenyewe ili sanjari na kupata faida wafunze matumizi, miiko na mila zake ili lugha hiyo iathiri tabia zake kwa watumiaji hasa wageni.

Hayo yamesemwa na Nguli wa Kiswahili Profesa Tigiti Mnyagatwa Sengo akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Manzese jijini Dar es Salaam.

“Mimi siafiki kuwa Tanzania tuna makabila 120, ni zaidi ya hapo, lakini Kiswahili kimeweza kuchomoza na kuathiri maisha ya watanzania wote, lazima tukubali tuna tofauti kihulka na kimienendo kulingana na makabila yetu, wako wakali walio tayari hata kutoa uhai wa wengine na wako wengineo, lakini wote hao wamejikuta wakidhibitiwa na mila na tabia zinazotokana na lugha ya Kiswahili katika kuamiliana kijamii ambako kumeleta Amani na utulivu usiopatikana Taifa lingine  Afrika na sehemu kubwa ya dunia”, amesema Profesa Sengo.

Amewataka watanzania waichukulie lugha ya kiswahili kama neema inayopaswa kushukuriwa kwa kumtukuza mwenye lugha yake, Mwenyezi Munga Muumbaji ambaye hakuwajalia wengine ila waishio kipande hiki cha dunia kinachoitwa Tanzania.

“Tunasikia yanayoendelea kwa majirani zetu na nchi nyingine, tujaribu kulinganisha na hali iliyopo nchini, kama isingelikuwa mila na dasturi zinazoedana na lugha yetu adhimu ya kiswahili, hapa penye makabila zaidi ya 120 hali ingekuwa mbaya zaidi”, amekumbusha Profesa Sengo ambaye ni mmoja wanafunzi Waalimu walioasisi idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwanzoni mwa miaka 1970.

Profesa Sengo ambaye kabla ya kustaafu amefundisha Vyuo vikuu kadhaa ndani na nje ya nchi  amewaasa Watanzania na hasa vijana kuzungumza lugha yao kama inavyotakiwa kuzungumzwa badala ya kuchanganya lugha yao na ama lugha nyingine kwa namna isiyoakisi ufahamu au kutumia maneno yasiyozalikana nayo.

“Ninakerwa ninaposikia neno ‘Mtalaa’ linatamkwa ‘mtaala’, neno ‘hakunaga’, ni budi na uwekaji wa ‘R’ kwahala kwa ‘L’ na kinyume chake, neno Mrabaha kutamkwa mrahaba, hatujui hata neno umilisi(fluency) badala yake tunatohoa neno la kigeni bila sababu za msingi”, ametahadharisha Profesa Sengo.

Amesema zama za RTD, uhariri na matumizi ya lugha uliwezesha Kiswahili kuenea na kuathiri watumiaji wa lugha nyingine, badala yake kukosekana kwa umakini huo hivi sasa kumehatarisha hadhi  na nafasi ya lugha hiyo miongoni mwa watumiaji hasa wageni.

“Tujitahidi kuzungumza Kiswahili na kukifunza kitaalamu kwa kuzingatia asili na jadi ya lugha hiyo ili kizungumzwe na kuambukiza tabia na miiko yake kwamba mtu akiweza kuzungumza Kiswahili aondokane na tabia za ukakasi zinatokana na lugha yake mama”, ameasa.

Amesema kwenye Kiswahili kuna maneno ‘naomba’, tafadhali, upole, uungwana na ukarimu hata kwenye kuuza na kununua, hata kwenye magomvi na mivutano kuna aina ya maneno yanayotumika yanayosuluhisha magomvi kimya kimya, lakini pia kuna masuala ya utani baina ya makabila yaliyosigana na kupigana huko nyuma.
Kwa ajili hiyo amewaasa watanzania na hasa wizara husika ya Sanaa na Utamaduni kuhakikisha fursa ya kukifunza Kiswahili na tabia zake nje ya nchi itumiwe vema ili iweze kunufaisha Tanzania kiuchumi na kijamii kwa mataifa ya kigeni badala ya fursa hiyo kubebwa na wengine wasio na asili nacho kwa tamaa ya chumo peke yake.

Hata hivyo Profesa Sengo ameshauri kuwa Wizara ya Utamaduni ingewekwa peke yake kwa kuwa ndiyo Wizara mama iliyozaa Elimu ikikusanya mila, jadi, dasturi, Miiko na Imani za Watanzania zinazohitaji miongozo maalum na umakini mkubwa badala ya kuchanganywa na Sanaa na michezo na hasa mpira wa miguu ambao umebeba utendaji mkubwa wa wizara hiyo.
Profesa Sengo amesifu upenzi wa Simba na Yanga nao umesaidia sana kukuza lugha ya Kiswahili ambapo amefichua matangazo ya RTD ya mpira wa Yanga na Simba zama hizo yalisikilizwa nchi nzima na kwamba lugha iliyotumika ni Kiswahili.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-10T02:26:30Z 2021-12-10T02:26:30Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1697 <![CDATA[MIAKA 40 YA MKUKI NA NYOTA- SOAS (KISWAHILI KIMATAIFA)]]> ]]> false MwlMaeda]]> 2021-11-10T08:21:50Z 2021-11-10T08:21:50Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1430 <![CDATA[MIAKA 30 YA UJERUMANI KUFUNDISHA KISWAHILI]]> MBALAMWEZI YA KISWAHILI: Miaka 130 ya Ujerumani kufundisha Kiswahili
Kwa ufupi
  • Mtazamo wa wengi wetu umejikita katika kuvibeza vilivyo vyetu na kuvitukuza vya wenzetu.
Na. Erasto Duwe
Hivi karibuni Profesa Clarisa Vierke wa kutoka Chuo Kikuu cha Bayreuth, Ujerumani aliyeshiriki katika Kongamano la Chama cha Kiswahili cha Afrika Mashariki lililofanyika jijini Dar es Salaam, aliwashtua wengi alipopewa nafasi ya kutoa neno katika kongamano hilo.
Akiongea kwa Kiswahili, katika maelezo yake alisema kwamba mwaka 2017 Chuo Kikuu cha Bayreuth, kinataraji kusherehekea miaka 130 ya ufundishaji wa Kiswahili.
Kauli hiyo ya kusherekea miaka 130 ya ufundishji wa Kiswahili Ujerumani na umahiri wa profesa huyo katika kutumia Kiswahili, vilionekana kuibua picha ya aina yake akilini mwa baadhi ya washiriki.
Mbalamwezi ya Kiswahili ilisikia sauti za minong’ono kutoka kwa washiriki waliokuwa wameketi karibu, “Daa aise, kumbe Kiswahili si mchezo! Miaka 130 …Kiswahili… Ujerumani!…” Jambo hilo lilionekana geni kwa wahusika hao.
 Yumkini kauli hizo za kuonyesha mshangao uliochanganyika na furaha ya aina yake, zilitolewa kutokana na mazoea na mitazamo ya baadhi ya Waswahili wazawa ambao hukichukulia Kiswahili katika mtazamo dufu badala yake huzishadidia zaidi lugha za kigeni.
Profesa Vierke aliendelea kusema, “Lugha ni ufunguo wa utamaduni. Ajuaye lugha ni tajiri. Tukuze Kiswahili na kukisherehekea… Kuna wazungumzaji wengi zaidi wa Kiswahili duniani ukilinganisha na wazungumzaji wa Kijerumani…
‘‘Tutambue pia kuwa kila lugha ni bora kwa watumiaji wake. Lakini pia tusisahau kwamba aliye na lugha moja ni maskini…”  Kwa ujumbe huu wa Profesa Vierke tunayo mengi ya kujifunza na kuyafanyia tafakuri.
Mintarafu ufundishwaji wa Kiswahili duniani, vipo vyuo vikuu vingi vinavyofundisha Kiswahili. Katika vyuo hivyo kuna idara na taasisi za masomo ya Kiafrika kama ilivyo katika Chuo Kikuu cha Bayreuth ambako Profesa Vierke ni mhadhiri. Miongoni mwa masomo hayo ya Kiafrika ni somo la Kiswahili ambacho kitovu chake ni Afrika Mashariki.
Mtazamo wa wengi wetu umejikita katika kuvibeza vilivyo vyetu na kuvitukuza vya wenzetu. Ni kinyume cha mambo, wenzetu kila jambo hulipa umuhimu, huvienzi vyao na kuvishikilia vya wengine kwa kuangalia umuhimu ya thamani yake.
Nchini Ujerumani pekee, vipo vyuo vingi vifundishavyo Kiswahili. Miongoni mwa hivyo ni Chuo Kikuu cha Kolon, Leipzig, Bayreuth, Humbolt, Berlin na Hamburg. Kwa nini vyuo vikuu vyote hivyo? Ni kutokana na dhima na thamani waionayo katika lugha hii adhimu ya Kiswahili.
Sherehe hiyo ya maadhimisho ya miaka 130 ya ufundishaji wa Kiswahili ni ya Ujerumani nzima. Tunaweza kujiuliza walianza lini kufundisha Kiswahili hata washerehekee miaka yote hiyo?
Tukiirejelea historia ya Kiswahili na wageni waliopata kukita guu nchini mwetu, yaani wamisionari, wakoloni na wafanyabiashara, tutapata majibu.
 Kiswahili kilianza kufundishwa huko Ujerumani katika karne ya 19 kwa ajili ya kuwaandaa wale ambao walipaswa kuja kufanya kazi nchini Tanganyika. Kituo kikuu cha ufundishaji wa Kiswahili kwa wakati huo kilikuwa  katika mji ujulikanao kwa jina la Kolon.
Ikiwa wenzetu wanakienzi Kiswahili kwa namna hiyo kiasi cha baadhi yetu kuwashangaa, basi sisi wenye lugha tunawiwa mengi na lugha hii. Tunapaswa kufanya hivyo maradufu, kwa kuwa Kiswahili ni lugha yetu na ndiyo ufunguo wa utamaduni wetu.
Mbalamwezi ya Kiswahili, katu haipingi watu kujifunza lugha nyingine na chambilecho Profesa Virke, kujua lugha nyingi ni utajiri. Kinachosisitizwa na makala haya ni mtu kukipenda na kukithamini kilicho chake.
Kiswahili ni chetu Watanzania, kabla ya kuthamini wa nje ya mipaka ya nchi, tuanze sisi kukithamini.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-10-27T04:01:23Z 2022-09-02T04:11:34Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1399 <![CDATA[Lugha 6 za Afrika zinazotumika zaidi]]>


1) Kiarabu 200 Million
2) Kiingereza 150 Million
3) Kiswahili 140 Million
4) Kifaransa 115 Milliion
5) Kihausa 50 Million
6) Amharik 25 Milion]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-09T03:13:59Z 2021-09-09T03:13:59Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1200 <![CDATA[Mzee Mwinyi ahutubia wadau wa Kiswahili Washington DC]]> Ifuatayo ni hotuba ya Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Ali Hassan Mwinyi alipohutubia mkutano wa nne wa Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) uliofanyika tarehe 23 Aprili 2015 katika Chuo Kikuu Cha Howard jijini Washington DC

]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-07T13:51:25Z 2021-09-07T13:52:02Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1183 <![CDATA[FAIDA YA KUTUMIA KISWAHILI KWA MATAIFA YA AFRIKA]]> 1. Kusaidia kuleta umoja wa bara zima.
2. Kudumisha utamaduni wa Kiafrika kuliko kufuata kasumba.
3. Kufanya Waafrika waamini zaidi mambo yao kuliko kutegemea tu ya kigeni.
4. Kurahisisha upatikanaji wa ajira kwa watumiaji wa lugha hiyo hata nje ya Afrika.
5. Kukuza sekta ya utalii.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-08-31T02:58:47Z 2021-08-31T02:59:49Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1072 <![CDATA[Kiswahili kinavyozidi kupaa na kukubaliwa kimataifa]]> ]]> false MwlMaeda]]> 2021-08-01T05:18:39Z 2021-08-01T05:20:04Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=690 <![CDATA[Athari za Kimofosintaksia za Ngeli za Luganda katika Matumizi ya Kiswahili Sanifu]]>

.pdf   Athari za Kimofosintaksia za Ngeli za Luganda katika Matumizi ya Kiswahili.pdf (Size: 238.57 KB / Downloads: 2)


CHANZO &t&t&t&t&t&t]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-07-30T06:02:58Z 2021-07-30T06:05:16Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=676 <![CDATA[Lugha 5 zinazozungumzwa zaidi Afrika]]>
Kwa mujibu wa mtandao wa AnswersAfrica hizi ndizo lugha tano zinazozungumzwa zaidi Afrika.


1. KIARABU
  • Kiarabu ndiyo Lugha inayozungumzwa zaidi barani Afrika ni Lugha inazongumzwa zaidi katika nchi za Afrika ya kaskazini na Baadhi ya maeneo karibu na Jangwa la Sahara, Kiarabu huzungumzwa kwenye nchi kama Tunisia, Misri, Morocco, Algeria na Sudan Kaskazini,Chad, Djibouti  na Libya salamu ya Kiarabu kwa kusema Mambo Au Hello  ni AL SALAAM A’ALAYKUM
 
2.KISWAHILI
 
  • Lugha yetu ya ASILI kabisa Hii ambayo karibu kila mtanzania huzungumza maana ndiyo lugha ya Taifa, Kiswahili ni Lugha ya pili kuzungumzwa zaidi barani Afrika ni Lugha ambayo tafiti mbalimbali zinaonyesha ni Lugha inayokuwa kwa kasi.
  • Kiswahili huzungumzwa zaidi katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na nchi nyingine kama Rwanda, Burundi, kaskazini mwa msumbiji, kusini mwa somalia na Congo mashariki.Kiswahili ndiyo mama wa maneno maarufu kama Hakuna matata, Simba na safari. mambo ya kwataunit.com Tunakupa Unachohitaji.
 
3.HAUSA
 
  • Ni Lugha ya tatu kuzungumzwa zaidi Afrika inazungumzwa zaidi Afrika ya Magharibi  inajulikana pia kama Haoussaa,Habe, abakwariga Kihausa kinazungumzwa kwenye nchi kama Nigeria, Chad, Togo, Niger, Ghana, Benin na Burkinafaso,. Kusema Hello kihausa ni SANNU.
 
4.KIINGEREZA
 
  • Kiingereza ni Lugha ambayo inashika nafasi ya 4 kuzungumzwa zaidi Afrika ni Lugha ambayo ilienea zaidi Afrika kutokana na Ukoloni ila kwasasa imekuwa Lugha ya Kufundishia kwenye Taasisi mbalimbali za Kielimu Afrika.
 
5.AMHARIC
 
  • Ni Lugha Ngeni kidogo kwa watu wengi ila ndiyo Lugha ya 5 kuzungumzwa zaidi Afrika, Ni Lugha ambayo kwenye eneo kubwa la Janga la Sahara Huzungumzwa, ni lugha ya pili kuzungumzwa baada ya kiarabu Kaskazini mwa Afrika inajulikana pia kama amarigna, amarinya, kuchumba, hii ndiyo lugha ya taifa ya Ethiopia,  Kusema Hello Kwenye luha ya AMHARIC ni SALAM.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-15T12:42:23Z 2021-06-15T12:42:23Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=36 <![CDATA[Kiswahili katika utangamano wa kimataifa]]>
  • Hatuna budi kuwapongeza vijana wanajiotokeza kutafuta fursa za ajira kwa kufundisha Kiswahili katika asasi na taasisi ambako wapo wageni wanaotaka kujifunza Kiswahili.
  • Ijapokuwa baadhi ya walimu hawa hawana kiwango cha kuridhisha cha kufundisha na wala hawapati usaidizi wa kutosha kutoka katika Serikali zetu, ni dhahiri kuwa wanajitahidi.
  •  
    Juhudi zinafanywa na watu binafsi katika kufundisha na kutangaza lugha ya Kiswahili katika ngazi mbalimbali za kimataifa.
    Hatuna budi kuwapongeza vijana wanajiotokeza kutafuta fursa za ajira kwa kufundisha Kiswahili katika asasi na taasisi ambako wapo wageni wanaotaka kujifunza Kiswahili.
    Ijapokuwa baadhi ya walimu hawa hawana kiwango cha kuridhisha cha kufundisha na wala hawapati usaidizi wa kutosha kutoka katika Serikali zetu, ni dhahiri kuwa wanajitahidi.
    Hizi ni juhudi binafsi za vijana wetu za kujipatia ajira. Inafaa asasi na taasisi zenye jukumu la ukuzaji lugha ziongeze juhudi za kusaidia wimbi kubwa la vijana wenye elimu ya kutosha ya lugha ya Kiswahili kwa kujipatia ajira. Mfano mzuri ni viongozi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (Tataki), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) za kuanzisha mawasiliano na Chuo Kikuu cha Harare nchini Zimbabwe.
    Taasisi hii ilifanya na mawasiliano na Chuo Kikuu cha Harare na hatimaye kufanikiwa kuwapeleka wahadhiri weledi wa Kiswahili waliokuwa tayari kwenda kufundisha Kiswahili.
    Hatuna budi kuwapongeza wote walioanzisha mpango huu kwani ni sifa kwa taifa letu na faida kwa wahadhiri hawa ambao watakuwa ni mabalozi wetu katika nchi za nje kutokana na uzoefu wao.
    Mpango huu wa kuwapeleka walimu huko Zimbabwe ulihitaji maandalizi ya kutosha ambapo hapo awali walianza kutayarisha mtalaa wa somo la Kiswahili nchini humo kwa kuzingatia stadi nilizotaja hapo juu na baadaye kuandaa vitabu, vielelezo na matini kwa ajili ya ufundishaji.
    Walimu wanatakiwa kuwa wavumilivu kwani hii ni misingi waliyotakiwa kuandaa kwa wengine watakaokuja siku za baadaye.
    Kwa kuanzia, somo lilianza kufundishwa katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe kwa lengo la kupata walimu ambao watasaidia kufundisha Kiswahili nchini humo kuanzia shule za msingi na sekondari.
    Hivyo, darasa la wanafunzi 80 lilianzishwa mwaka 2012 likisimamiwa na walimu wenye uzoefu kwenye taaluma ya Kiswahili. Miongoni mwa walimu hao ni Titus Mpemba ambaye amewahi kufundisha darasa maalumu kwa wahariri, wahakiki na waandishi wa Kiswahili wa gazeti la Mwananchi na Mwanaspoti katika Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).
    Hata hivyo, licha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya kufundishia kwenye ngazi ya shule za msingi, bado wanafunzi na wananchi wa kawaida wanapenda kujifunza lugha hiyo kutoka kwa wenyeji wa Kitanzania.
    Kutokana na mahitaji haya, gazeti la Mwananchi lina nafasi ya kuwa mojawapo ya marejeo wakati wa kujifunza, huku wakipata habari mbalimbali za kimataifa ikiwamo za Zimbabwe.
    Njia mojawapo ya kuwaunganisha wanafunzi wa Zimbabwe na wenzao wanaojifunza Kiswahili ni kwa kutumia mtandao wa mawasiliano unaomilikiwa na Kampuni ya Nation Media Group ambayo ni kampuni mama ya MCL. Mtandao huu unajulikaka kama Swahili Hub na tovuti inafahamika kama www.swahilihub.com. Huu ni mtandao ambao umelenga kuwaunganisha watumiaji wa Kiswahili ulimwenguni kote.
    Zaidi ya hayo, mtandao huu unatayarisha benki ya kuhifadhia majina ya vituo, vyuo shule na pia watafiti na wahadhiri wa Kiswahili duniani kote kwa lengo la kukusanya kazi zao za uhariri na uchapishaji wa makala, vitini na vitabu vya Kiswahili.
    Wazungumzaji wa Kiswahili nchini Zimbabwe wanaweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwamo kukuza uelewa wa matumizi sanifu ya lugha ya Kiswahili kupitia makala za kitaaluma zinazopatikana katika mtandao wa Swahili Hub.
    Stephen Maina anapatikana kwa baruapepeConfusedmaina@mwananchi.co.tz

    ]]>
    false