MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Uhakiki wa kazi za fasihi]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ Sun, 28 Apr 2024 17:52:33 +0000 MyBB <![CDATA[FALSAFA YA MAISHA KATIKA MASHAIRI YA MULOKOZI NA SHAABAN ROBERT]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2849 Fri, 21 Oct 2022 05:16:37 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2849
.pdf   FALSAFA YA MAISHA KATIKA MASHAIRI YA MULOKOZI NA SHAABAN ROBERT.pdf (Size: 7.89 MB / Downloads: 6) ]]>

<![CDATA[JARIDA LA FAHARI YA KISWAHILI la Chuo Kikuu Ruaha (RUCU)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2839 Wed, 28 Sep 2022 13:43:55 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2839
.pdf   JAFAKI, JUZUU 1, TOLEO 1, 2022.pdf (Size: 1.56 MB / Downloads: 3) ]]>

<![CDATA[Uhakika wa Fani katika tamthiliya ya KILIO CHA HAKI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2511 Wed, 13 Apr 2022 10:06:16 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2511
.docx   FANI_KILIO_CHA_HAKI.docx (Size: 50.25 KB / Downloads: 8) ]]>

<![CDATA[UHUSIANO WA FANI NA MAUDHUI KWA MUJIBU WA WATAALAMU MBALIMBALI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2408 Fri, 25 Feb 2022 11:53:34 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2408 UHUSIANO WA FANI NA MAUDHUI KWA MUJIBU WA WATAALAMU MBALIMBALI
Uhusianoa wa fani na maudhui umekuwa ukiangaliwa na wanazuoni wa fasihi katika mitazamo tofauti, mtazamo mkuu unaoangaliwa na wanazuoni katika uhusiano wa fani na maudhui umo katika makundi makubwa mawili ya kimtazamo. Makundi hayo ni ya mtazamo wa KIYAKINIFU na mtazamo wa KIDHANIFU.
A: Mtazamo wa kidhanifu.
 Wanazuoni wanaoegemea katika mtazamo huu hudai kuwa fani na maudhhui havina uhusiano wowote. wanaagalia uhusiano wa vijenzi katika utengano ambao fani inaweza kujikamilisha bila ya kutegemea maudhui na maudhui pia huweza kujikamilisha bila ya kutegemea fani.
Wanaeleza uhusiano wa fani na maudhui kuwa ni sawa na ule wa kikombe na maji au chai iliyomo ndani ya kikombe hicho. Baadhi ya wananadharia hao wanahusisha mahusano haya na yale ya sehemu ya ganda la chungwa lililo nje ya nyama ya chungwa. Wanazuoni wanaoungana mkono na nadharia na mtazamo huu ni hawa.
Fr.F.M.V NKWERA
Nkwera anadai kuwa fani na maudhui havina uhusiano wowote kwa kufananisha na maziwa na kikombe. Kikombe anakiona na kukichukulia kama chombo kinachotumika kuhifadhi maziwa. Hivyo kikombe anakifananisha na fani kuwa ni umbo la nje la kazi ya fasihi. Maziwa anayafananisha na maudhui kuwa ni umbo la ndani la kazi ya Fasihi. Kwa madai yake ni kuwa maziwa yanaweza kutenganishwa na kikombe na kila kimoja kubaki peke yake.
S.D. KIANGO NA T.S.Y. SENGO.
Wanazuoni hawa pia wanaunga mkono mtazamo wa kidhanifu, wanadai kwamba fani na maudhui havina uhusiano wowote katika kazi ya fasihi.Wanazuoni hawa wanafananisha fani na maudhui sawa na chungwa kwa madai kwamba chungwa linaweza kutenganishwa na nyama ya ndani ya chungwa inayoliwa ambayo inafananishwa na maudhui ambalo ndilo umbo la ndani la kazi ya Fasihi. Aidha wanafananisha maganda ya chugwa yanayomenywa ili kupata  nyama ya ndani ya chugwa  sawa na fani ambalo ni umbo la nje la kazi ya Fasihi.
Madai hayo ni kwamba kwa kuwa magamda ya chugwa yanaweza kutenganishwa na nyama ya ndani ya chugwa basi hata fani na maudhui katika kazi ya fasihi vinaweza kutenganishwa na kila kimoja kusimama katika upekee wake. Hivyo, wanadai fani na maudhui havina uhusiano.
PENINA MUHANDO NA NDIYANAO BALISIDYA
Wanazuoni hawa nao wamo kwenye kundi hili la wenye mtanzamo wa kidhanifu, madai yao makubwa kuhusu mahusiano ya fani na maudhui ni kwamba fani katika  kazi ya fasihi ni umbo la ndani basi kwa hali hiyo fani na maudhui vinaweza kutenganishwa kwa hiyo fani na maudhui havina uhusiano kwa vile kila kimoja kinaweza kusimama peke yake.
UDHAIFU WA MTAZAMO HUO
Udhaifu unaojitokeza katika mtazamo huu ni ule wa kutazama fani na maudhui kwa mtazamo wa utengano hili ni kosa kubwa sana kwa kutenganisha vile ambayo havitenganishwi.
B : Mtazamo wa kiyakinifu
Wanazuoni wa fasihi wanaoegemea katika mtazamo huu wanadai kwamba fani na maudhui hutegemeana, huathiriana na kukamilishana. Wanazuoni wanaounga mkono mtazamo huu ni kama vile;
M.M.MULOKOZI NA K.K.KAHINGI
Wanazuoni hawa wanadai kuwa fani na maudhui haviwezi kulingana na kuathiriana unaposoma kazi ya fasihi kwa kupata miundo, matendo, madhari, wahusika na matumizi ya lugha. Hivi ni vipengelele vilivyomo ndani ya fani ndipo msomaji anaweza kupata maudhuni ya kazi ya mwandishi kama vile dhamira, ujumbe (fundisho), falsafa ya mwandishi, msimamo na mtazamo wake kwa hivyo basi huona kwamba fani hutegemea maudhui na maudhui ya fasihi hutegemea fani hivyo, fani  na maudhui haviwezi kutenganishwa kwani hutegemeana na kuathiriana kama tulivyoona hapo juu.
 F .E.SENKORO.
Mwanazuoni huyu pia anaungana na wanazuoni wa mtazamo wa kiyakinfu wanaodai kwamba fani na maudhui haviwezi kutenganishwa. Senkoro katika madai  yake anafananisha uhusiano wa fani na maudhui kama sarafu yenye sura mbili mfano wa sarafu ya shilling 200 yatanzania ili iweze kukamilika na kuwa yenye matumizi halali katika serikali halali ya tanzani inalazimika kuwa na picha ya karume na kuwa upande wa pili kuwa na picha ya simba na mtoto wake kutokuwepo au kukamilika sura moja ya sarafu hiyo basi sarafu hiyo haziwezi kutumika kama sarafu halali.
Kwa hali hiyo inamaanisha kwamba upande mmoja wa sarafu huwa ni sawa na kufananisha na maudhui katika kazi ya Fasihi. Hivyo basi ili sarafu ikamilike ni lazima pande mbili zikamilike na hiyo ndiyo hali iliyopo katika fasihi kwamba ni lazima fani na maudhui kukamilishwa ndipo kazi ya fasihi hukamilika na huwezi kutenganisha fani na maudhui.
Mambo muhimu yanayojitokeza katika fani ni.
  • Muundo – mtiririko wa mawazo na matukio.
  • Wahusika
  • Mtindo –  mbinu za kiuandishi
  • Uteuzi wa maneno
  • Picha za ishra
Wakati katika maudhui vitu vinavyojitokeza huwa ni:-
  • Dhamira
  • Ujumbe
  • Falsafa
  • Migogoro
  • Mtazamo
  • Msimamo wa mwandishi.
Kwa kuhitimisha basi fani na maudhui haiwezi kutenganishwa kwani hutegemeana, huathiriana na kukamilishana. Fasihi kama tunavyoona inajegwa na maumbo mawili ambayo ni fani na maudhui.
]]>
UHUSIANO WA FANI NA MAUDHUI KWA MUJIBU WA WATAALAMU MBALIMBALI

<![CDATA[Dhana ya mtindo na nafasi yake katika fasihi]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2403 Fri, 18 Feb 2022 14:51:50 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2403 Dhana ya mtindo na nafasi yake katika fasihi
Kabla hatujaangalia dhana ya mtindo ni vema tukajua kwanza dhana ya fasihi.
Wataalamu wengi  akiwamo Wamitila (2003) wanakubaliana kuwa fasihi ni sanaa inayotumia lugha na ambayo hujishughulisha na binadamu pamoja na maisha yake na huathiri, hugusa, au huacha athari fulani na hupatikana katika umbo ambalo linatambuliwa na jamii. Kwa ujumla fasihi ni sanaa inayotumia lugha na yenye maudhui katika jamii husika.
Baada ya kuangalia dhana ya fasihi kwa ujumla sasa tuangalie dhana ya mtindo na nafasi yake katika fasihi.
Senkoro (1982) anasema mtindo katika kazi ya fasihi ni ile namna ambayo msanii hutunga kazi hiyo na kuipa sura ambayo kifani na kimaudhui huainisha kanuni au kawaida zilizofuatwa (za kimapokeo) ama ni za kipekee. Anaendelea kusema, mtindo ni upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi kwa njia ambayo hutokeza au huonyesha nafsi na labda upekee wa mtungaji wa kazi hiyo.
Katika fasili hii tunaweza kuona anachokieleza mtaalamu huyu ni kwamba mtindo huhusisha upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi ambapo upangaji huu hutegemea upekee alionao msanii. Kwa maana nyingine, unaposoma kazi fulani ya fasihi unaweza kumwona mtunzi wa kazi hiyo kulingana na jinsi alivyoiandika, kwa maana kwamba jambo moja linaweza kuongelewa na wasanii wawili tofauti lakini namna linavyowasilishwa likatofautiana, na hii ni kulingana na upekee wao.
Wamitlia (2003) naye anasema ‘mtindo ni jumla ya mbinu au sifa zinazomwezesha mwandishi kuwasilisha ujumbe  wake, huelezea mwandishi anavyounda kazi yake’. Anaendelea kusema, dhana ya mtindo hurejelea sifa maalumu za mwandishi au mazoea ya mwandishi fulani ambayo hujionyesha kwenye fani yake, mazoea hayo ya mwandishi ya kuandika, kuteua msamiati, tamathali za semi, taswira, uakifishi, sentensi na kadhalika ndio yanayompambanua mwandishi huyu na mwanzake.
Kitu anachokisema hapa Wamitila hakitofautiani na Senkoro, kinachoongelewa hapa ni upekee wa mwandishi husika lakini Wamitila kasema kitu kimoja zaidi,  kwamba msanii anaonekana kuwa na mtindo fulani kwa sababu amezoea kutunga kazi zake za fasihi kwa namna fulani ambayo inadhihirisha upekee wake. Kwa kauli hii ya Wamitila tunaweza kusema kwamba mtindo wa mtunzi huonekana baada ya kuandika kazi zake kadhaa na kimsingi hii ndio huleta maana halisi ya mazoea.
Nakubaliana na kauli hii, kwani hata hivyo huwezi ukahitimisha kuwa mtunzi fulani mtindo wake ni huu kama umesoma kazi yake moja tu, kwa hiyo mtindo (upekee) wa mwandishi huweza kubainishwa baada ya kupitia kazi zake kadhaa na ndipo tunaweza kuona mazoea ya mwandishi huyo katika kuandika kazi zake.
Kwa  sentensi fupi tunaweza kusema kuwa mtindo ni ule upekee alionao mtunzi wa kazi ya fasihi katika kuipa kazi yake sura fulani kifani na kimaudhui ambapo mtunzi mwingine hawezi kufanya hivyo hata kama kitu kinachoongelewa ni kilekile.
Sasa mtu anaweza kujiuliza, nitawezaje kubainisha mtindo wa mtunzi katika kazi ya fasihi? Swali hili linaweza kujibiwa kwa kuangalia vipengele fulanifulani.
Tunapotaka kujua mtindo wa msanii katika kazi husika, kwa mfano katika  riwaya tunaangalia vipengele vifuatavyo:
  •  Matumizi ya lugha; je, lugha ni rahisi au ngumu, je kuna matumizi ya maneno ya kiufundi na kadhalika
  • Matumizi ya daiolojia; je, ni kwa kiasi gani mtunzi ametumia dailojia, ni kwa kiasi gani daiolojia husimulia hadithi?
  • Namna ya usimulizi; je, anatumia nafsi ya kwanza, ya pili au ya tatu na kadhalika.
  • Ukuaji wa wahusika; kwa vipi mtunzi anawatambulisha wahusika na kwa vipi wanabadilika katika hadithi.
  • Hisia za mwandishi; je hisia zake zinaonekanaje katika hadithi? Je, anaonekana ni mwenye dhihaka? Mwenye mapenzi, mwenye matumaini, mkali, mwenye kejeli na kadhalika.
  • Namna anavyopanga sura au matukio katika hadithi. Je, sura ni fupifupi au ndefu? Ni nyingi kiasi gani, zimepangwaje? Na kwa nini imepangwa hivyo?
  • Tamathali za semi; je, mwandishi katumia kwa kiasi gani tashibiha, sitiari, tashihisi au alama?
  • Mandhari; je mandhari yaliyotumika ni halisi au ya kubuni?
  • Uteuzi wa msamiati; je, ni kwa jinsi gani msamiati uliotumika unaleta mvuto kwa msomaji.
Kwa ujumla hivi ni baadhi tu ya  vipengele vya mtindo vinavyoweza kujitokeza  katika riwaya.
Baada ya kuangalia dhana ya mtindo ni vema sasa tukaangalia nafasi yake katika fasihi. Kwa ujumla mtindo una nafasi kubwa tu katika kazi ya fasihi.
Mtindo humtambulisha mtunzi wa kazi ya fasihi; watu hupenda kazi ya mtunzi fulani kwa sababu mtindo anaoutumia huwavutia wasomaji wake.
Mtindo ndicho kipengele kinachotenganisha  kazi nyingine za kisayansi au za kawaida, bila mtindo kazi za kifasihi zisingepata mashabiki wengi. Kwa hiyo mtindo ndio huibua hisia na kuwafanya wasomaji wapende zaidi kusoma kazi za msanii husika.
Kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa, tunapozungumzia dhana ya mtindo tunakuwa tunarejelea mwandishi husika, kwa maana kwamba ubinafsi wake ndicho kile kinachoonekana kwenye kazi yake. Tunaposema hadithi fulani ina taswira nyingi, ina sitiari nyingi au lugha yake ni rahisi au lugha yake inavutia na kadhalika tunakuwa tunarejelea mtindo wa mtunzi husika. Kwa mantiki hiyo dhana ya mtindo kama ilivyokwisha jadiliwa inaonekana kwa namna mtunzi anavyopangilia kazi yake kifani na kimaudhui, yaani namna anavyotumia lugha, anavyopanga visa na matukio, uteuzi wa mandhari, falsafa anayoiwasilisha,ujumbe dhamira na kadhalika.
 Marejeo
Senkoro, F.E.M.K (1982) Fasihi. Dar es salaam: Press and Publicity Centre.
Wamitila, K.W. (2003) Kichocheo cha Fasihi Simulizi na Andishi. Naiobi: Focus Publishers.
]]>
Dhana ya mtindo na nafasi yake katika fasihi

<![CDATA[TENDI TATU ZA KALE]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2103 Tue, 11 Jan 2022 04:17:06 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2103
Ikisiri
Tangu Finnegan (1970:108) alipodai kwamba, katika fasihi simulizi ya Afrika Kusini mwa Sahara ni nadra sana kupata Tendi, dai hili limeibua mjadala mrefu wa kitaaluma miongoni mwa wataalam mbalimbali wakiwamo: John William, Thomas A. Hale na Stephen Belcher ambao ndio waliodondoa baadhi ya beti katika tendi za Kiafrika na kuziweka pamoja katika kitabu kinachojulikana kwa jina la Oral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent. Mbali na hao, mtaalam mwingine ni Mulokozi (1999) ambaye naye anathibitisha upo wa tendi katika Afrika Mashariki kwa kukusanya pamoja tenzi tatu za kale katika kitabu cha Tenzi Tatu za Kale. Pia kuna mtaalamu mwigine Belcher (1999) ambaye naye alizungumzia tendi za Kiafrika katika kitabu chake kinachojulikana kwa jina la Epic Tradition of Afrika. Hivyo basi, ni wazi kwamba uchapishaji wa vitabu hivi ni matokeo chanya ya tafiti zilizofanywa na wataalamu mbalimbali na kuamua kukusanya na kuziweka pamoja kama mifano ya uwakilishi wa utamaduni wa tendi Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa lengo la kufungua milango ya kutambulika zaidi.
1.0     Utangulizi
Makala hii itajishughulisha zaidi na mapitio-hakiki ya vitabu viwili ambavyo ni, Oral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent na Tenzi Tatu za Kale. Katika mapitio hayo vipengele mbalimbali vitajadiliwa kama vile: fasili ya tendi, mpangilio wa tendi katika vitabu hivyo, waandishi wa vitabu husika, uhakiki: usuli wa yeli/manju, usuli wa kijamii-kihistoria, utendaji-uwasilishwaji, udhaifu/mapungufu, ubora wa kazi, ulinganisho na tendi nyingine, hitimisho na marejeo. Kwa kuanza na fasili ya tendi;
[url=https://www.blogger.com/null][/url]
1.1  Fasili ya Tendi
Miongoni mwa wataalam waliofasili dhana ya utendi ni pamoja na Bowra (1930) yeye anatumia fomula kuelezea maana ya utendi kuwa ni E = M + Ms yaani, (Epic = Mars + Muse/music). Hii ina maana kamba utendi ni mungu, muziki na vita (U = M + V). Hivyo basi, maana ya maelezo ya Bowra ni kuwa utendi ni tukio la kimuziki linalozungumzia vita kwa njia ya ushairi ulioandikwa.
Mulokozi (1996) anasema, Tendi ni nyimbo ndefu za kimasimulizi au za mawaidha, nyimbo hizo zinahusu visa vya mashujaa.
Wamitila (2006) anasema, Tendi ni aina ya utenzi ambao unazungumzia maisha na matendo ya shujaa au mashujaa wa jamii fulani.
Kwa hiyo, kutokana na fasili hizi tunaweza kusema kuwa, utendi ni kama Saiklopidia au maktaba ya jadi ya historia ya jamii fulani ambayo kupitia tendi mbalimbali jamii inatambua historia yake katika vipindi mbalimbali, chimbuko lake, mashujaa wao pamoja na kujua mila na desturi zao pamoja na utamaduni.
2.0     Mpangilio wa tendi katika vitabu

Johnson na wenzake (1997) katika kitabu chao cha Oral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent wanajaribu kukigawa katika sehemu kuu tatu. Sehemu ya kwanza wameweka tendi mbalimbali za Afrika Magharibi, sehemu ya pili wameweka Tendi za Afrika ya Kaskazini na sehemu ya tatu wanamalizia kwa kuweka tendi za Afrika ya Kati. Je mpango huu ni wakinasibu au kuna uzingativu wa jambo fulani? Je tendi za Afrika Mashariki zinatambulika miongoni mwa tendi za Kiafrika? Kwa nini hazijitokezi katika kitabu hiki?
Wataalamu hawa wanadai kuwa, tendi hazipatikani kila mahali, kuna matokeo ya muunganiko wa jamii na mazingira ya kihistoria pamoja na utendaji wa namna mbalimbali. Tendi zilizokusanywa katika ukanda huu zina sifa zinazoingiliana/zinazohusiana miongoni mwazo ingawa si lazima ziwe na utamaduni pamoja na historia inayofanana.
Pia hata katika Tenzi Tatu za Kale mwandishi naye amekigawa katika makundi makuu matatu au sehemu kuu tatu ambazo ni: sehemu ya kwanza inahusu Utendi wa Fumo Liyongo, sehemu ya pili mwandishi amehakiki Utenzi wa Al-Inkishafi na sehemu ya tatu ni Utenzi wa Mwanakupona.
2.1     Waandishi wa vitabu husika
Oral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent ni kitabu kilichoandikwa na kuhaririwa na John William Johnson (Indiana University), Thomas A. Hale (The Pennsylvania State University) na Stephen Belcher (The Pennsylvania State University).
Pia Mulokozi (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) ameandika na kuhariri kitabu cha Tenzi Tatu za Kale. Wataalam hawa katika kukusanya na kuhariri tendi mbalimbali za Kiafrika walibaini nduni bainifu za tendi za Kiafrika na masuala majumui yanayopatikana katika tendi za Afrika na tendi za Ulaya kama tutakavyoona hapo baadaye.
Johnson na wenzake wanasema kuwa, koja/diwani hii yenye dondoo 25 za tendi za Kiafrika ni ya kwanza na ya aina yake kutokea duniani na ni toleo la tatu katika mkururo wa tendi za Kiafrika zilizozinduliwa na “Indiana University Press”. Hii ni hatua muhimu sana iliyofikiwa katika kubadili fikra za kimagharibi kuhusu tendi katika muktadha wa kiulimwengu.
Hegel (1963) akinukuliwa na Johnson na wenzake (kashatajwa) anadai kuwa, Waafrika hawanaLiterature, hivyo ni wazi kamba hata historia hawana. Dai hili halina mashiko, kwani leo hii tunaona kwa kupitia tendi uibukaji wa vyote viwili historia na Fasihi ya Kiafrika ambavyo vilifunikwa na ujinga wa wazungu kwa muda mrefu sana. Lakini pamoja na hayo, bado wanahoji juu ya fasili ya fasihi simulizi.
3.0     Usuli wa manju/yeli
Kwa ujumla tendi ni tungo ndefu ambazo huimbwa na mafundi fulani wanaojulikana kama mayeli na huwahusu mashujaa walioishi au wanaosadikiwa kuishi katika jamii fulani. Mfano mzuri ni utendi wa Sundiata/Sunjata wa jamii ya Wamande nchini Mali ambao uliimbwa na mayeli wa jamii hiyo kama vile Fa-Gigi Sisoko. Pia utendi wa Fa-Jigi ambao yeli wake ni Seydou Camara akisaidiana na mkewe ambaye alikuwa akipiga narinya-kifaa cha muziki, utendi wa Sonsan of Kaarta ulisimuliwa kwa kuimbwa na Mamary Kuyate’, huku wimbo ukiambatana na muziki, utendi wa Almami Samori Toure’ yeli alikuwa ni Sory Fina Kamara.

Pia wasimulizi au mayeli wa utendi wa Wagadu ni Diarra Sylla ambaye aliandika mistari 257 na Jiri Silla ambaye naye aliandika mistari 800. Kwa pamoja waliweza kupata simulizi moja linaloeleza mambo yaliyowatokea watu wa Wagadu.
Aidha utendaji katika tendi za Kiafrika huweza kutofautiana kutoka yeli mmoja kwenda mwingine. Sababu za utofauti huo huweza kuwa masuala ya mila na desturi za jamii husika, hivyo huweza kukuta yeli/manju husimulia hadithi yake ya kiutendi kwa kuzingatia taratibu za jamii hiyo. Licha ya hayo, vilevile yeli huyohuyo huweza kusimulia hadithi ileile ya kiutendi kwa namna tofauti tofauti kulingana na muktadha.

Katika tendi za Kiafrika mayeli walikuwa ni watu walioheshimika sana katika jamii husika, kwani wao ndio waliojua historia na tamaduni za jamii na ndio wanaopitisha historia ya jamii kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Mfano, Johnson na wenzake wanatuambia kuwa, katika jamii ya Wamande yeli (Sara) alikuwa mwanamke wa heshima sana na hata alipokufa mwaka 1989 ng’ombe 15 walitolewa sadaka wakati wa sherehe za maziko yake.
3.1     Usuli wa kijamii-kihistoria
Kama tulivyosema hapo awali utendi ni kama saiklopidia ya jamii fulani kwani umesheheni masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo historia pamoja na mila na desturi za jamii mbalimbali. Mfano, tendi zote za Kiafrika kama vile wa Bamana Segu, Sonsan of Kaarta, Almami Samori Tuure’, Musadu, Fa-Jigi na Son-Njara kwa kuzitaja chache, zote zinaelezea masuala ya kijamii-kihistoria kama vile: matukio ya kivita, kidini-hija, asili ya koo mbalimbali, mila na desturi za jamii ya Wamande kama vile: masuala ya matambiko, salamu nk. Ndio maana utendi kama waSundiata umesimuliwa katika nchi za Ghana, Sudan, Gambia, Ivory Coast, Mali na Mauritius nk. kama njia mojawapo ya kurithisha amali za jamii hiyo.
Vilevile utendi wa Wagadu ni simulizi maarifu sana katika historia ya Soninke’kuanzia wakiwa wamoja kabla ya kuanguka kwa ufalme na kusambaratika katika maeneo mbalimbali ya Sahel, Senegal na Ghana.
4.0     Utendaji-uwasilishwaji
Tendi nyingi za Kiafrika hutumia mbinu mbalimbali katika uwasilishaji wake. Mfano huweza kusimuliwa kwa njia ya kinadhari au kwa njia ya ushairi/nudhumu yaani kuimbwa kama vile utendi wa Hambodedio and Saigalare,  Fa-Jigi huwasilishwa kwa kuimbwa na manju pamoja na mkewe ambaye husaidia kupiga kifaa kiitwacho narinya (nanga), pia utendi wa Sara wa jamii ya Maninka uliimbwa na Sara pamoja na kaka yake Yamuru Jabate’. Katika utendi huu unajitokeza urudiaji rudiaji wa korasi, mfano;
5. Chorus:       Ah! Sara is sung for those of one voice.
Don’t you see it?
Sira Mori: Sara! Sara is sung for those with promises.
Don’t you see it?
Pia mwandishi anafafanua kuwa, tendi simulizi za Afrika mara nyingi katika uwasilishwaji wake huambatana na uigaji wa matendo ya watu pamoja na muziki kutoka kikundi cha waimbaji na hadhira.
Vilevile, mwandishi anaibua hoja juu ya mjadala ulioongozwa na Lucy Duran juu ya uwepo wa suala la ujinsia katika tendi. Japokuwa anakiri kwamba, mjadala haupo wazi sana kutokana na vyanzo visivyorasmi kushindwa kutofautisha kati ya sifa ziimbwazo na wote wanaume na wanawake na simulizi za kitamaduni katika utawala wa wanaume. Duran anadai kwamba, wanawake wataimba utendi mzima kama hakuna wanaume wa kuimba. Hata hivyo hakuna utendi wa mwanamke ulioonekana katika machapisho. Hoja hii inahitaji ushaidi wa kitafiti zaidi.
Aidha katika mapitio haya inajibainisha wazi kuwa, tendi simulizi za Kiafrika hazina mpaka halisi unaotenganisha tendi, visasili, ngano, visakale, maghani, nyimbo, n.k. Kwa mfano Utendi wa son-Jara, una kisakale cha Biblia; masimulizi ya uumbaji wa Mungu kwa Adamu na Eva. Lakini katika tendi za kimagharibi tunaona mpaka uliodhahiri.
Hivyo tunaona kwamba, tendi nyingi zinazohusu mashujaa huingiza sifa nyingi za visasili, visakale, maghani au hata ngano ndani yake. Kwa mfano, utendi wa Fumo Liyongo, Wagadu, Lihanja, Mwindo, nk. sifa hii huonesha kwamba, tendi huchota visa vya sanaa jadi nyingine kutoka tamaduni zenye tendi simulizi. Kwa mfano, Fumo Liyongo, Mwindo, Rukiza, Sundiata, n.k. ni miongoni mwa mashujaa wenye sifa sawa na mashujaa wengine wa kiutendi ulimwenguni kama vile, Gilgameshi na wengineo.

Tenzi Tatu za Kale ni kitabu cha fasihi chenye baadhi ya tungo mashuhuri za zamani, zilizokusanywa na kuhifadhiwa pamoja. Tungo hizo ni pamoja: Utendi wa Fumo Liyongo, uliotungwa na Muhamadi Abubakar Kijumwa mwaka 1913, Utenzi wa Al-Inkishafi uliotungwa na Sayyid Abdallah bin Ali bin Nasiri na Utenzi wa Mwanakupona uliotungwa na Mwanakupona Binti Mshamu kwa ajili ya binti yake aliyeitwa Mwana Hashima binti Mataka.
Mwandishi wa kitabu hiki amebainisha vipengele mbalimbali vya utendi vinavyojitokeza katika Utendi wa Fumo Liyongo. Anaeleza kwamba, Fumo Liyongo ni utendi unaohusu matukio muhimu ya kihistoria na kijamii, hueleza kuhusu ushujaa wa shujaa. Anamwona Fumo Liyongo kama shujaa anayependwa na watu. Sifa hii pia tunaiona hata katika tendi nyingine za Kiafrika. Kwa mfano: Utendi wa Sundiata unaakisi historia na utamaduni wa jamii, huelezea matukio ya kishujaa na mashujaa. Pia hata Utendi wa Lihanja nao anawakilisha chimbuko la taifa la Wamongo.
Aidha, mwandishi anadondoa baadhi ya sifa za tendi za Kiafrika kwa kuhusianisha na shujaa Liyongo. Anamwelezea shujaa huyu kuwa, ni mtu mwenye nguvu za kimwili. Mfano kitendo cha kubeba mizigo ya kujaza chumba kiliwashangaza Wagalla, kupuliza panda na kusua nk. Pia ni rijali. Mfano, Wagalla walimwomba sultani awaruhusu wapate mbegu yake. Licha ya nguvu za kimwili pia alikuwa na nguvu za kisirihi. Mfano, udhaifu wake ulikwa kitovuni, hivyo haikuwa rahisi kudhurika kwa namna yoyote ile isipokuwa kwa kuchumwa sindano kitovuni. Vilevile alikuwa na mshikamano na jamii yake ndio maana hata aliweza kusaidiwa na mama yake pamoja na kijakazi Saada pindi alipokuwa kifungoni. Hatimaye alifaulu kutoroka.
Sifa hizi alizonazo Liyongo pia zinajitokeza hata katika tendi nyingi za Kiafrika, kwa mfano Mwindo anasaidiwa na shangazi yake, mjomba pamoja na watu wengine kwenda kulipiza kisasi kwa baba yake. Pia mbali na sifa hizi, mashujaa wengi wa Kiafrika huzaliwa kwa njia isiyo ya kawaida. Kwa mfno, katika Utendi wa Jeki la Njambe’ Inono shujaa Njambe’ Inono kabla ya kuzaliwa anaongea tumboni akielekeza mahali atakapozaliwa. Baada ya kuzaliwa anarudi tena tumboni, halafu baadaye anataka kuzaliwa kwenye chupa. Mfano,
…So they began to go back with waves. It was then that a voice spoke from Ngrijo Epee Tungum’s womb: “Ina! Sit down in the water and give birth to me!”
Mulokozi (2002) katika utafiti wake kuhusu tendi za jamii ya Wayaha hasa Utendi wa Rukiza anaungana mkono na mawazo ya Johnson japokuwa anaongeza kuwa, shujaa wa Kiafrika sharti awe ni msaada kwa watu wake na hivyo: (USHUJAA: Ushakiri+Sihiri+Watu) Hivyo basi, tunaweza kusema kuwa, Utendi wa Fumo Liyongo una sifa fawafu kama ilivyo katika tendi nyingine za Kiafrika. Kwanza ni masimulizi ya kinadhari yenye uunganifu, pili nudhumu, yaani ni utungo wa kishairi, tatu ni simulizi linalohusu matukio muhimu ya kijamii-historia na mwisho huelezea kuhusu ushujaa.

Fauka ya hayo, mwandishi wa Tenzi Tatu za Kale amejadili pia Utenzi wa Al-Inkishafi kuwa ni miongoni mwa tenzi mashuhuri sana katika lugha ya Kiswahili na ulichipuka kutokana na jadi ndefu ya tenzi za Kiswahili mjini Pate. Utenzi huu ulitungwa na Sayyid bin Ali bin Nasiri mwaka 1800-1820 unahusu matukio mbalimbali yaliyotokea katika jamii ya Waswahili wa Pwani ya Afrika Mashariki, kwa mfano, mgogoro hasa wa kuanguka kwa mji wa Waswahili kulikosababishwa na uvamizi wa Wareno.

Kihalisia ni kweli mambo hayo yametokea. Kwa hiyo utenzi huu una dhima ya kihistoria katika jamii ya watu wa Pwani ya Afrika Mashariki. Pia unawakilisha utamaduni wa jamii ya Waswahili wa Pwani ya Afrika Mashariki kutokana na lugha iliyotumika ambayo ni Kiswahili kilichochanganyika na Kiarabu kwa kiasi fulani, utamaduni wa watu hao, miji iliyotajwa ambayo ni Pate, Kilwa, Lamu na  Mombasa.

Vilevile katika Tenzi Tatu za Kale kuna Utenzi wa Mwanakupona ni utenzi wa kimawaidha uliotungwa na Mwanakupona Binti Mshamu kwa ajili ya binti yake aliyeitwa Mwanahashimu binti Mataka mwaka 1858. Utenzi huu unaonekana kuwakilisha vyema tungo za utamaduni na maonyo ya wakati huo. Lakini pia aligusia kwa vijana wengine wa kike wapate kuusoma utenzi huu ili nao wapate maonyo hayo (Ubeti wa 94 na 95). Utenzi huu unaonekana kuibadilisha jamii ya uswahilini baada ya kuona kuwa unafaa hasa kwa malezi ya kijadi kwa watoto wa kike kwa kuwafunda. Yawezekana Jambo hili ndilo linaloufanya utenzi huu uonekane kuwa msaada wa jamii hata leo hii.

Kihistoria, tunaelezwa kuwa huu ni utenzi wa kale uliokuwa unaendana na mazingira ya wakati huo. Mwandishi aliuandika kwa kuilenga jamii ya wakati ule hasa kwa kufuata mila na desturi za jadi za wakati huo kama vile: heshima ya ndoa, wanawake kuwekwa utawani, kutoonesha sura zao mbele ya watu, kumtukuza mume kama Mungu wao wa pili. Pia unaonekana kuwa ulikuwa ni utenzi wa tabaka tawala.

5.0     Udhaifu katika kitabu cha Tenzi Tatu za Kale na Oral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent.

Pamoja na kwamba, Utenzi wa Mwanakupona una baadhi ya sifa za utendi kama vile: unudhumu, uunganifu, unahusu masula ya kijamii mfano, mafundisho katika jamii, mianzo na miisho ya kifomula, nk. bado hatuwezi kuuingiza kwenye kumbo la tendi kwani unakosa baadhi ya sifa za msingi za kitendi kama vile: masuala ya kishujaa na mashujaa, matendo ya kivita nk. Vivyo hivyo hata katika Utenzi wa Al-Inkishafi pia unakosa sifa hizo za msingi.

Kimsingi Utenzi wa Inkishafi na Mwanakupona hazizungumzii suala la ushajaa wala shujaa zaidi ya kumwona mwandishi akitamalaki kwa kiasi kikubwa kama kwamba yeye ndiye shujaa. Swali la kujiuliza Mwandishi anawezaje kuwa shujaa? Kama ni shujaa ruwaza yake ni ipi? Anafuata kanuni za shujaa wa namna gani? Wa Kijadi/Kiafrika au Kimagharibi, au Kiarabu? Hoja hii haihusiani na kitabu cha Tenzi Tatu za Kale lakini inafaa kujiuliza maana wengine huweza kufikiri kwamba, mwandishi ni shujaa kutokana na tajiriba aliyonayo, mfano mtunzi wa Utendi wa Mwanakupona.

Pia katika Tenzi Tatu za Kale, mwandishi amechanganya pamoja Tendi na Tenzi na kuziita zote kwa pamoja TENZI TATU ZA KALE, yaani Utendi wa Fumo Liyongo na Utenzi wa Al-Inkishafi pamoja na Utenzi wa Mwanakupona. Je, kigezo gani kimetumika? Kama mwandishi alilenga kuzishughulikia kazi zote tatu ndani ya kitabu kimoja, basi angepaswa kukwepa neno hilo ili kuepuka kuchanganya dhana mbili zinazotofautiana, badala yake angeziita TUNGO TATU ZA KALE. Nadhani msamiati huu ungekuwa fawafu kabisa kwa kazi zote tatu.

Mkanganyiko mwingine tunaouona ni kwamba, mwandishi hakuweka bayana kuwa Utenzi wa Inkishafi ni utendi au ni utenzi, maana baadhi ya sehemu ndani ya kitabu ameita Utenzi na sehemu nyingine ameita Utendi. Mfano, ukurasa wa 73 anasema; “Utenzi wa Inkishafi unapata nguvu yake kutokana na lugha tukufu na taswira anazotumia mtunzi…” ilhali katika ukurasa wa 77, mwandishi anasema; “Inkishafi ni Utendi wa Kiafrika…” Hivyo tunaona kwamba, hapa mwandishi anawaweka wasomaji katika hali ya sintofahamu kipi ni kipi!

Pia suala jingine la kujiuliza kuhusu Tenzi Tatu za Kale ni kwamba, je huo ukale anaousema mwandishi unaanzia wapi na unaishia wapi? Je tunawezaje kubaini mipaka ya ukale na usasa? Kwani ukale unaanza lini na unaisha lini?

Aidha, mwandishi hajaonesha bayana mkabala au nadharia iliyomwongoza katika ubatizaji wa tungo hizi na kuziita TENZI TATU ZA KALE? Je ameangalia lugha iliyotumika au mambo yalisheheni katika tungo hizo?

Suala la udhaifu pia linajitokeza hata katika Oral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent. Inaonekana kuwa, mwandishi hakufanya utafiti wowote katika Afrika Mashariki ndio maana hakuna chochote kilichoelezwa kuhusu tendi za Afrika Mashariki. Hii inawapa picha wasomaji kwamba, Afrika Mashariki hakuna tendi ilhali tunajua kuwa, Afrika Mashariki kuna tendi na wapo watafiti wabobevu waliofanya tafiti za tendi sehemu mbalimbali za Afrika Mashariki kama vile: Mulokozi, Mbele, Kagame, nk.

Kosa kama hili tunaliona pia hata kwa Belcher (1999) katika Epic Traditions of Africa. Belcher amechunguza baadhi ya tendi za Afrika hasa tendi za Afrika Magharibi na Afrika ya Kati na kugundua kuwa zinamfanano katika baadhi ya vipengele. Hii inadhihirisha kwamba, katika ukanda wa Afrika Mashariki wataalamu wa tafiti katika uwanja huu ni wachache sana, hivyo kuna haja ya wataalamu chipukizi kumakinikia katika uwanja huu.
6.0     Ubora wa kazi hizi
Mbali na mapungufu ya hapa na pale, pia tutakuwa wachoyo wa fadhila kama hatutaona ubora uliosheheni katika kazi hizi. Kwa mfano, Johnson na wenzake katika kitabu chao cha Oral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent wamefanya kazi nzuri sana katika kuzitambulisha tendi mbalimbali za Kiafrika kwa ulimwengu mzima ili hata wale waliopotoshwa na Finnegan waweze kubadili mtizamo wao.

Pia wamesaidia kuonesha ufanano mkubwa uliopo katika tendi za Kiafrika hasa katika baadhi ya mambo kama vile manju au mayeli, japokuwa kuna utofauti za kimsamiati lakini dhima yake ni ileile. Kwa mfano wanajulikana kwa majina kama: gewel, gawlo, jali, jeli, mabo, gesere, jesere, nk.

Vilevile mwandishi wa Tenzi Tatu za Kale amefaulu sana katika kutoa maana mbadala za maneno au msamiati mgumu uliotumika ili kuwarahisishia wasomaji kuelewa kwa urahisi ujumbe unaokusudiwa katika tungo zote tatu.
Licha ya hayo, utangulizi na maelezo ya mwandishi wa Tenzi Tatu za Kale yamenisaidia sana kama mwanafasihi chipukizi hasa kujua maudhui ya tungo hizi tatu na pia kujua namna bora ya kujenga hoja zenye mantiki na maelezo yenye mtiririko fawafu.
7.0        Hitimisho
Kwa ujumla tunaweza kuhitimisha makala haya kwa kusema kuwa, wataalamu hawa wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kutuonesha namna tendi simulizi za Kiafrika zinavyoakisi historia ya jamii husika katika utamaduni, mila na desturi, mahusiano na mshikamano wa kijamii. Vilevile wote kwa pamoja wametuonesha kuwa, utendi pamoja na hadithi mbalimbali za mashujaa huwa na ruwaza inayofanana ambayo hutuwezesha kupata muundo wa msingi wa tendi ambao ni wa kimajumui.

Mulokozi (kashatajwa) ameainisha sifa za shujaa wa tendi za nanga kama ifuatavyo: Anatoka tabaka la juu au la kawaida, shujaa huwa ni jasiri, anatumia sihiria, anakuwa rijali, hutegemea nguvu za wahenga au mizimu na anahitaji msaada wa umma. Ukiangalia tendi nyingi katikaOral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent ruwaza za mashujaa wa Kiafrika kwa kiasi kikubwa zinalandana na ruwaza za mashujaa Gilgamesh na Enkidu katika utendi waGilgamesh. Mwandishi Sandars (1960), haoneshi kuzaliwa kwa Gilgamesh na Enkidu. Utendi huu unawaonesha mashujaa hawa wakiwa tayari watu wazima kama vile kwa Fumo Liyongo. Gilgamesh ameanza kuelezewa tayari akiwa kiongozi wa mji wa Uruk wakati Enkidu ameanza kuelezewa tayari akiwa anaishi porini na wanyama. Maelezo haya yanajidhihirisha katika kigae/kibao cha I & II na katika kitabu uk. 61.
                Kigae/kibao cha I na kitabu (uk. 61)
 I WILL proclaim to the world the deeds of Gilgamesh. This was a man to whom allthings were known; this was the king who knew the contries of the world. He was wise, he was misteries and knew secret things, he broughy us a tale of the days before the flood

Kibao/kigae cha II Then he, Enkidu, offspring of the mountains,
who eats grasses with the gazelles,
came to drink at the watering hole with the animals,
with the wild beasts he slaked his thirst with water.
 
8.0        MAREJEO
Belcher, S. (1999), Epic Traditions of Africa, Bloomington, Indiana University Press.
Finnegan, R. (1970), Oral Literature in Africa. Oxford. Clarendon Press.
Johnson, J. W. na wenzake, (1997), (Ed.), Oral Epics from Africa: Vibrant Voices from a VastContinent, Bloomington, Indianapolis University Press.
Mulokozi, M. M. (1996), Fasihi ya Kiswahili, Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
                              (1999), (Mha.), Tenzi Tatu za Kale, Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi                                 wa Kiswahili.
                           (2002), The African Epic Controversy:  historical, Philosophical and
                Aesthetic Perspectives on Epic Poetry and Performance. Dar es salaam,                 Mkuki na Nyota Publishers.
Wamitila (2006) Kamusi ya Ushairi, Nairobi: Vide-Muwa Publishers Ltd.
Sandars N. K (1960), The Epic of Gilgamesh. Cox & Wyman Ltd: Great Britain.]]>

<![CDATA[TASWIRA YA KIFO CHA SHUJAA KATIKA UTENDI: SHUJAA LIYONGO NA EMANUEL KATIKA BIBLIA]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2102 Tue, 11 Jan 2022 03:58:29 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2102 TASWIRA YA KIFO CHA SHUJAA KATIKA UTENDI:  SHUJAA LIYONGO NA EMANUEL (YESU) KATIKA BIBLIA

.pdf   SEHEMU YAKWANZA.pdf (Size: 144.72 KB / Downloads: 1) ]]>
TASWIRA YA KIFO CHA SHUJAA KATIKA UTENDI:  SHUJAA LIYONGO NA EMANUEL (YESU) KATIKA BIBLIA

.pdf   SEHEMU YAKWANZA.pdf (Size: 144.72 KB / Downloads: 1) ]]>
<![CDATA[UHAKIKI WA UTENZI WA MAPENZI BORA]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1997 Tue, 04 Jan 2022 05:36:02 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1997
.docx   MAPENZI BORA.docx (Size: 28.06 KB / Downloads: 4) ]]>

<![CDATA[MADAI YA WANAMAPOKEO NA WANAMAPINDUZI KUHUSU USHAIRI WA KISWAHILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1994 Tue, 04 Jan 2022 05:20:44 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1994 MADAI YA WANAMAPOKEO NA WANAMAPINDUZI KUHUSU USHAIRI WA KISWAHILI
Dai la msingi la wanamapokeo (wanajadi) ni kuwa urari wa vina na mizani ni roho na uti wa mgongo wa shairi la Kiswahili.Wengi wa wanamapokeo hawakiri kuwa kinachotungwa na wanamapinduzi ni mashairi. Wanauchukulia ushairi wa kisasa kuwa si ushairi bali ni insha au nathari tu. Kwa upande wa wale wachache wanaokiri kuwa ni ushairi, wanauona kuwa ni ushairi usio bora na ushairi wa kigeni.Wanauchukulia kuwa ni ushairi uliotokana na kuiga ushairi wa Kiingereza. Aidha, wanawachukulia wanamapinduzi (wanausasa/ wanamamboleo) kuwa ni watu walioshindwa kutunga mashairi ilhali wanatamani kuwa watunzi wa mashairi. Matokeo yake ni kutunga vitu visivyokuwa mashairi na kudai kuwa ni mashairi ya kisasa, jambo ambalo wao wanamapokeo hawalikubali.Wanazuoni wanaounga mkono chapuomkabala huu ni pamoja na Said Karama, Jumanne Mayoka, S.Kandoro, Amiri A. Sudi, Haji Gora,Nassir, Abdilatif Abdalla, Shihabuddin Chiraghdin, Mathias Mnyampala, Shaaban bin Robert, Amri Abedi, Amiri A.S. Andanenga, Wallah bin Wallah.
Kwa upande wao, wanamapinduzi wanawalaumu wanamapokeo kwa kuzuia maendeleo ya ushairi wa Kiswahili kwa kutoutambua ushairi ‘mpya’ ulioibuka.Wanamapinduzi wanabainisha kwamba ushairi simulizi wa Kibantu, ambayo ndiyo chimbuko la ushairi wa Kiswahili, kama wanavyokiri piawanamapokeo, haukufuata kanuni za urari wa vina na mizani. Kanuni ya urari wa vina na mizani kama uti wa mgongo wa ushairi wa Kiswahili wanaiona kama kanuni iliyotokana na athari za Waarabu katika ushairi huo wala si kanuni ya jadi ya ushairi wa Kiswahili.
Hivyo, wanamapinduzi nao, kama ilivyokuwa kwa wanamapokeo, wanalaumu ujio wa wageni kama chimbuko la athari mbaya kwa ushairi wa Kiswahili.Wanamapinduzi wanaenda mbali na kukazia kwamba shairi liamuliwe na kufungamana na mawazo, mtiririko wa hisia na makusudio ya mtunzi na si mbinu ya kifani.
Kwa jumla, wanausasa hawapingi uhalali wa urari wa vina na mizani katika ushairi wa Kiswahili bali wanataka aina ‘mpya’ ya ushairi, ushairi usiofuata urari wa vina na mizani utambuliwe kuwa ni mashairi ya Kiswahili pia. Kwa hivyo, wanamapinduzi wanatambua mashairi yenye urari wa vina na mizani kuwa ni mashairi ya Kiswahili lakini hawaoni kuwa huo ndio uti wa mgongo wa ushairi wa Kiswahili; mashairi ya Kiswahili yanaweza pia kutokuwa na urari wa vina na mizani.Watetezi wanaopigia chapuo maoni haya ni Fikeni Sonkoro, Euphrase Kezilahabi, Kulikoyela Kanalwanda, David Massamba, M.S.Khatibu, Theobald Mvungi, Kithaka wa Mberia miongoni mwa wengine wengi.
Ulinganishi na ulinganuzi wa mashairi ya arudhi na mashairi huru.
Mlingano:
  • Maumbo: Kimaumbo, yote hujigawa katika beti, mishororo, vipande na mizani.
  • Hutumia lugha ya mvuto, ya kimafumbo, ya kishairi, tamathali za usemi.
  • Hutumia uhuru wa kishairi kama inkisari, mazida, tabdila, kufinyanga au kuborongasarufi na kadhalika.
  • Uakifishaji:Yote hutumia alama za kuakifisha kama koma, kiulizi(o), kituo kikuu, kibainishi (ritifaa).
  • Maudhui :Maudhui yote huwa na ujumbe muhimu wa mtunzi. Huzungumzia mambo  yanayomhusu binadamu na mazingira yake.
Ulinganuzi:
  • Maumbo hubadilika katika mashairi huru lakini katika mashairi ya arudhi (wanamapokeo) hayabadiliki.
  • Katika mashairi ya arudhi, viwakilishi hutumiwa kwa kusudi maalumu ilhali katika mashairi huru havitumiwi sana ila kiulizi,kipumuo kifupi na alama ya hisi.
  • Mashairi huru hutumia lugha sanifu. kwa kiasi kikubwa. Mashairi ya kimapokeo huboronga sarufi kwa kusudi la kutosheleza vina na mizani.
  • Idadi ya mistari kutoka ubeti hadi ubeti hutofautiana katika mashairi huru.
  • Katika mashairi ya arudhi, idadi ya mizani, vina na vipande huzingatiwa sana lakini katika mashairi huru jambo hili halitiliwi uzito hata kidogo.
  • Mashairi ya arudhi huzingatia kanuni za kijadi katika utunzi wake, lakini mashairi huru hayazingatii kanuni hizi za kijadi za utunzi wa mashairi.
]]>
MADAI YA WANAMAPOKEO NA WANAMAPINDUZI KUHUSU USHAIRI WA KISWAHILI

<![CDATA[VIPERA VYA USHAIRI SIMULIZI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1993 Tue, 04 Jan 2022 05:14:02 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1993 VIPERA VYA USHAIRI SIMULIZI
(1) Nyimbo
Nyimbo ni tungo za kishairi zenye mahadhi ya kupanda na kushuka kwa sauti, muwala maalumu na mapigo ya kimuziki na huwasilishwa kwa kuimbwa. Hutumia lugha yenye uwezo wa kuleta picha akilini. Msingi mkubwa wa nyimbo ni kuwako kwa sauti. Nyimbo huweza kuimbwa na mtu mmoja au kikundi cha watu. Nyimbo ndio asili ya ushairi. Kuna aina mbalimbali za nyimbo ambazo hutegemea mambo kadha: malengo, umri, jinsia, maudhui, wakati wa kuimba na mahali pa kuimba nyimbo hizo.
Sifa za nyimbo
  • Kuwapo kwa watu wanaoimbiwa au hadhira inayosikiliza uimbaji huo.
  • Muktadha wa kuimbwa kwenyewe, yaani wimbo unawasilishwa wapi na katika muktadha gani. Kwa mfano harusi, ibada na kadhalika.
  • Kuchezwa au miondoko ya kucheza ya mwili ya mwimbaji au hadhira yake.
  • Maneno yanayoimbwa au matini yenyewe.
  • Wimbo unaweza kumlenga mtu au hadhira iliyopo au isiyokuwepo.
  • Sauti ya mwimbaji au waimbaji : mmoja huwaongoza wengine.
  • Huandamana na matumizi ya ala za muziki kama ngoma, baragumu, siwa, zumari au chochote kile ambacho hutegemea jamii husika.
  • Hugusa na kuibua hisia kwa njia mbalimbali.
  • Waimbaji wanaweza kuwa na maleba ingawa si lazima.
  • Nyimbo hutumia lugha nzito yenye kuibua taswira na hisia nzito za furaha, huzuni,mapenzi.
  • Hutolewa kwa mahadhi ya kupanda na kushuka kwa sauti.
  • Nyimbo hutumia lugha ya mkato yenye mpangilio maalum wa silabi, mishororo na beti zenye mapigo ya kimuziki.
  • Huwa na takriri.
  • Huweza kuwa na kiitikio kinachokaririwa.
Umuhimu wa nyimbo katika jamii
  • Huhifadhi matukio muhimu ya kihistoria.
  • Hutumiwa kama burudani ya kutumbuiza waimbaji na hadhira.
  • Hutumiwa kuliwaza na kufariji wenye majonzi.
  • Hudumisha na kuwasilisha usanii wa tamaduni za jamii mbalimbali.
  • Hutumiwa kuhamasisha watu kushiriki katika kutenda mambo fulani.
  • Hutumiwa kama chombo cha kupitisha utamaduni wa jamii.
  • Huelimisha, hukejeli na kuonya.
  • Hutumiwa kuongoa watoto walale ama hata wapende kitu.
  • Hurithisha sanaa yenyewe kwa vizazi kwa kupokeza kizazi hadi kingine.
  • Hutumiwa katika vipera vingine kama vile ngano kuhusisha hadhira.
  • Huchangia katika kukuza uzalendo, kwa mfano wimbo wa taifa na mengine ya kisiasa.
  • Hukuza utangamano. Nyimbo za kazi (hodiya) zinapoimbwa hufanya watu kutangamana katika kundi moja.
  • Hutia ujasiri. Wimbo kama vile nyiso na ule wa kivita huwapa wahusika ujasiri kukabiliana na yanayowaka bili au yatakayowakabili.
  • Huweza kutumiwa kuwazindua watu walioko katika hali fulani (nyimbo za kisiasa)
  • Hutumiwa kuonyesha ustadi wa msanii. Wimbo bora huonyesha ubora wa msanii husika.
  • Ni mojawapo wa njia za kujipatia riziki.
Muundo wa nyimbo
  • Nyimbo hugawika katika mafungu (beti)
  • Beti au mafungu huwa na mistari inayoitwa mishororo.
  • Mishororo huwa na silabi zenye mdundo wa kimuziki.
  • Huweza kuimbwa kwa kupokezana baina ya kiongozi na waimbaji ambao huimba kiitikio.
  • Mafungu au mistari yanaweza kurudiwarudiwa kama kiitikio.
  • Lugha huwa nzito na fiche.
  • Hutumia lugha ya mkato.
  • Waimbaji wanaweza kubuni maneno ya ziada na kuongezea kulingana na hafla.
  • Baadhi ya nyimbo huwa na vina.
Sifa zinazofanya nyimbo ziwe mashairi
  • Huwasilisha ujumbe kwa kutumia lugha ya mkato.
  • Kifungu kimoja au kadha huweza kukaririwa sawa na kibwagizo katika ushairi.
  • Beti za mashairi hulinganishwa na stanza au vifungu vya nyimbo.
  • Baadhi ya nyimbo huzingatia urari wa vina n ahata mizani katika mishororo na vifungu.
  • Mishororo inayounda ubeti inalinganishwa na mistari inayounda vifungu katika vya nyimbo.
Umuhimu wa nyimbo katika masimulizi ya hadithi
  • Nyimbo hutumiwa kurefusha masimulizi ili kujenga hali ya taharuki
  • Hujenga uhusiano wa karibu kati ya mtambaji na ha dhira yake.
  • Nyimbo hutumiwa kuibua hisia kwa msimulizi kama vile hisia za furaha, huzuni na kadhalika.
  • Nyimbo hutumiwa kuelezea jambo la siri kati ya wahusika, kwa mfano, mhusika aliye kwenye taabu fulani huweza kuomba msaada aokolewe kisirisiri kwa kutumia nyimbo.
  • Husisimua hadhira na kuondolea ukinaifu wa masimulizi makavu.
  • Huangazia maadili katika hadithi.
  • Hutenganisha matukio yanayojumuisha hadithi.
  • Ni kama kipumuo.
  • Nyimbo huburudisha wakati wa utambaji hadithi.
Athari hasi za nyimbo
  • Kuna ukosefu wa maadili katika baadhi za nyimbo.
  • Huweza kutumika kueneza propaganda kwa kutoa ujumbe au picha isiyo ya kweli kwa nia ya kufaidika kwa mwimbaji huku wakipotosha wasikilizaji.
  • Huweza kuibua hisia za ukabila au utabaka na kwa hivyo kuchangia kuleta au kukoleza uadui au kutoelewana kwa wahusika.
  • Nyimbo zinalevya; zinapumbaza.
  • Baadhi ya nyimbo huwa na mawaidha mabovu,
hivyo, huwapotosha watu katika jamii. Kwa mfano, nyimbo zinazowapotosha vijana kuhusu kushiriki mihadarati.
Vibainishi vya nyimbo
(i) Vigelegele
Vigelegele ni mlio wa sauti ifanywayo kwa kutembeza ulimi mdomoni upesiupesi. Katika wimbo, vigelegele hutumika kuonyesha upeo wa juu wa furaha. Vigelegele huweza kupigwa pia kumpongeza mchezaji ambaye amecheza vizuri au mwimbaji kwa uimbaji wake muruwa.
(ii) Mkarara
Huu ni ule msitari au ubeti ambao hurudiwarudiwa mara nyingi na washiriki. Mkarara hasa ndio huwafanya wasikilizaji kushiriki.Husaidia kuondoa  udhia wa kumsikiliza mshiriki mmoja.Aidha, huondoa usingizi na kumpa mwimbaji fursa ya kupumzika kidogo.
(iii) Mshindo
Ni mapigo ambayo hupigwa kwa mwendo ule ule katika nyimbo zetu, hususa zile za kucheza.Mapigo haya hufanywa kwa mguu mmoja au miwili. Katika baadhi ya jamii, miguu ya wachezaji hufungwa njuga, msewe au makopo.Njuga husababisha mlio ambao huleta uzuri au utamu wa aina yake.
(iv) Makofi
Makofi hutumika kumtia hamasa mchezaji aliye katikati yao na kadiri makofi yaongezekavyo ndivyo mchezaji huchangamka.
Aina za nyimbo
Nyimbo huainishwa kutegemea wahusika, sherehe au shughuli zinazohusishwa. Zipo aina nyingi sana za nyimbo za fasihi simulizi
Ifuatayo ni mifano ya aina hizo:
(a) Bembelezi/ bembea/ pembejezi
Ni nyimbo za kuwafariji au kuwabembeleza watoto walale au waache kulia.
Huimbwa taratibu kwa sauti ya kuongoa. Huwa fupi na zinazoonyesha kuliwaza. Kuna kurudiwarudiwa kwa maneno. Hutumiwa lugha shawishi na
wakati mwingine hutolewa ahadi za kununuliwa watoto zawadi.
(b) Mbolezi/ tahalili
Huimbwa wakati wa matanga au kifo.Hutegemea jamii inayohusika
na hata umri wa anayehusika. Huimbwa kwa nia ya kuwafariji waliofiwa. Huwatoa woga kwani   hueleza kuwa kila mtu atafariki. Hukikashifu kifo na kukibeza kwa kuwachukuawapendwa. Aidha, mbolezi huweza kuimbwa katika hafla ya kuadhimisha makumbusho ya mtu.Mbolezi huimbwa kwa toni ya huzuni na pengine uchungu, hivyo kuibua hisia za ndani za mwombolezaji.
© Nyimbo za watoto / chekechea
Mtoto mchanga anapokua, akaweza kwenda, kukimbia na kusema, naye huanza kuimba pamoja na wenzake. Nyingi katika nyimbo hizi huimbwa katika michezo ya watoto; baadhi huimbwa kwa kujibizana.
(d) Sifo / tukuzo
Nyimbo za aina hii huweza kupatikana katika miktadha tofauti kama kwenye sherehe za kitamaduni, uwanja wa kisiasa, arusi na kwingineko. Hujaza maneno ya sifa na aghalabu  matumizi ya chuku, istiari (kwa mfano, kuwalinganisha wanaosifiwa na wanyama wakali).
(e) Nyimbo za kisiasa
Huimbwa katika hadhara ya kisiasa au kwingineko. Ni nyimbo za kawaida sana katika jamii zetu. Nyimbo za kisiasa huwa na maudhui mapana kama vile kuzindua, kuhamasisha, propaganda, mapambano, kutia ari, kukejeli.
(f) Nyiso
Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa jandoni. Hutumiwa kuwaandaa kihisia
Wanaotahiriwa kwa kuwapa ari ya kupitia kijembe cha ngariba. Nyiso huhimiza ujasiri na kukebehi woga. Huwaambia kuwa wameingia katika hatua nyingine ya maisha, yaani hatua ya utu uzima.
 (g) Nyimbo za mapenzi / chombezi
Huimbiwa wapenzi. Hizi ni nyimbo ambazo huwa na maudhui ya kimapenzi. Huelezwa kwa maneno matamu yenye hisia nzito nzito. Huenda ukaimbwa na mtu  kumsifu mpenziwe, kuomba msamaha au hata kuomba uchumba.
(h) Kimai
Ni nyimbo zinazoimbwa katika shughuli mbalimbali za baharini. Hizi hujumuisha  nyimbo za mabaharia, wavuvi na wasafiri wa vyombo vyombo vya baharini. Nyimbo hizi hazina idadi kamili ya vina na mizani na pia swala la vina na mizani si lazima.
(i) Tumbuizo
Tumbuizo ni nyimbo ambazo huimbwa ili kuwafurahisha watu katika sherehe mbalimbali kama vile kwenye ngoma au kwenye harusi. Husifia wahusika wakuu katika sherehe husika. Huweza kuwa na sehemu zinazorudiwarudiwa.
(j) Nyimbo za migomo
Huimbwa na watu wanapoandamana na hukashifu serikali au shirika kwa
kutoshughulikia haki za wafanyikazi. Aidha, huwasifu viongozi wa wafanyikazi au kundi fulani. Nyimbo za migomo hunuiwa kuwashinikiza viongozi kuyatatua matatizo ya wagomaji.
(k) Nyimbo za vita
Hizi ni nyimbo zinazoimbwa au kuimbiwa watu wanaokwenda vitani kuwapa hamasa na moyo wa kuitetea hadhi na heshima ya taifa lao kwa matu mizi ya silaha.
(l) Hodiya / chapuzo
Hizi ni nyimbo ambazo huhusishwa na kazi kama vile kutwanga nafaka,
kufua nguo, kuvuna, kupalilia, kuinua gogo na kadhalika. Huimbwa wakati watu wanapofanya kazi. Huimbwa na kundi la wafanyikazi au mtu mmoja wakati anapofanya kazi.
(m) Nyimbo za harusi
Nyimbo hizi huimbwa katika sherehe za harusi, kuwatakia mema maharusi katika uhusiano wao wa kindoa zinazoimbwa kumsifu Mtume Muhammad zinazoimbwa katika Maulidi.
(n) Jadiiya
Hizi ni nyimbo za kitamaduni ambazo zinaimbwa na kupokezwa kwa mdomo kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Nyimbo hizi husimulia mambo mengi hasa yaliyotukia katika historia ya jamii fulani kama vile majanga, ucheshi.
(o) Kijapuzi
Ni wimbo unaoambatana na hadithi.
(p) Kongozi
Nyimbo za kuaga mwaka mkongwe na kualika mwaka mpya hususa katika jamii ya Waswahili.
(q) Wimbo wa taifa
Ni wimbo unaotambulisha taifa fulani. Nyimbo hizi huimbwa na watu wa taifa moja kuonyesha mapenzi yao na uzalendo kwa nchi yao.
® Vave / wawe
Ni nyimbo zinzoimbwa na wakulima wakiwa katika shughuli za kilimo (kufyeka, kulima, kupalilia, kupanda mbegu, kukata magugu, kuteketeza moto na kadhalika) Baadhi ya wawe huwa na mtu anayewaongoza wengine katika uimbaji.
(s) Taarabu
Muziki wa mahadhi yenye asili ya mwambao wa Afrika Mashariki unaotumia ala za Mchanganyiko wa Kiarabu, Kihindi na Kizungu.
(t) Nyimbo za uwindaji
Huimbwa na wawindaji wakiwa katika usasi.
(u) Nyimbo za kidini
Nyimbo hizi huimbwa maabadini wakati wa ibada za sala / swala.
(v) Nyimbo za siku ya kuzaliwa
Nyimbo za aina hii huimbwa kuadhimisha ukumbusho wa siku ya kuzaliwa.
(w) Nyimbo za kishujaa
Huimbwa kusherehekea ushindi wa tukio fulani kama vita au kupata uhuru.
(2) Maghani
Maghani hutumiwa kuelezea ushairi ambao hutolewa kwa kalima, yaani kwa njia ya maneno badala ya kuimbwa au kughaniwa kama mengineyo. Sauti ya juu au ya chini katika neno hutilia uzito maana ya anayeghani. Kimsingi,huu ni ukariri wa nusu kusemwa na nusu kuimbwa. Kuna aina mbili kuu za maghani:
  • maghani ya kawaida
  • maghani ya masimulizi (maghani simulizi)
(a)  Maghani ya kawaida
Hutumiwa kuelezea aina ya tungo ambazo hupatikana katika fasihi simulizi na ambazo hugusia maswala mbalimbali kama mapenzi, siasa, harusi, dini, kazi na maombolezo. Mashairi yanayogusia maswala haya yanapoghaniwa (kukaririwa kwa kalima) basi huwa maghani ya kawaida. Maghani ya kawaida ni pamoja na kivugo /majigambo, tondozi na pembezi / pembejezi.
(b) Maghani simulizi
Haya ni maghani ambayo husimulia hadithi, tukio, kisa au historia. Usimulizi unaohusika hapa unaweza kuambatanishwa na muziki wa ala kama zeze, njuga, marimba au hata ngoma. Maghani ya aina hii hupatikana katika jamii nyingi Afrika na uhusishwa na wasimulizi ambao hujulikana kama yeli au manju. Mifano ya simulizi ni rara, tendi / utenzi, ngano.
Sifa za maghani
  • Maghani ni tungo za kishairi, kwa hivyo zina mapigo ya kimuziki au maneno mateule yenye muwala.
  • Huwa katika umbo la shairi.
  • Huzungumzia mashujaa na ushujaa.
  • Muundo huwa na utaratibu fulani.
  • Hueleza mambo ya kiutenzi.
  • Tamathali za usemi hutumika kwa wingi kujenga taswira.
  • Huweza kutolewa na mtu mmoja au kundi la watu.
  • Hutungwa papo hapo na kutongolewa mbele ya watazamaji / hadhira.
  • Hutumia tamathali za usemi kwa wingi.
Dhima ya maghani
  • Huwatukuza mashujaa
  • Hutumiwa kukejeli au kukashifu sifa mbaya katika jamii.
  • Kufurahia fanaka ya watu binafsi na jamii kwa jumla.
  • Hutumiwa kueleza sifa maalumu za mashujaa.
  • Hukuza uhusiano bora miongoni mwa wanaojigambia wenzao.
Kipera cha maghani kinaweza kuainishwa katika vijipera vifuatavyo:
(i) Kivugo/ majigambo
Haya ni mashairi yanayohusu majisifu ambayo hutungwa na mtu anayehusika. Hutungwa kwa namna ambavyo hujenga taswira ama picha ya anayehusika kwa hadhira yaje kwa kuonyesha ubingwa wake katika jambo fulani kama vile vita, masomoni, michezoni, ucheshi na kadhalika.
Majigambo huwa ni ya papo hapo na huelekezewa wale wanaomjua na kumtambua anayejisifuna hivyo huwa vigumu kwa wale wasiomjua kuelewa. Katika jigambo hilo anaweza kujieleza jina lake, ukoo wake na lakabu zake.
(ii) Tondozi
Haya ni maghani ambayo huwasifu watu, wanyama au vitu. Tondozi inaweza Kumsifu mtu kwa mambo kama umbo, kimo, tabia, sura, wema, na kadhalika. Pia mnyama wa mwitu anaweza kusifiwa kwa ukubwa wake, ujasiri, ukali kama ambavyo mti unaweza kusifiwa kwa umbo ama manufaa yake. Msingi hapa ni kuwa kinachosifiwa kinapewa sifa fulani. Lugha ya kuvutia na yenye kuvuta taswira hutumika katika tondozi.
(iii) Pembezi / pembejezi
Hizi ni tungo za kusifu kama zilivyo tondozi. Pembezi hutumiwa kuwasifu watu mashuhuri ambao wametenda matendo maarufu kama ya ushujaa, uongozi  namaendeleo ya jamii husika.Watu hawa husifika pia kutokana na nafasi au nyadhifa walizonazo katika jamii.
(iv) Simango
Ni maghani ambayo dhima yake kuu ni kumsimanga mtu fulani juu ya mambo aliyoyafanya au anayoaminiwa kuyafanya na sifa alizonazo mtu au  anazoaminika kuwa nazo. Kwa kawaida, anayosimangiwa mtu huwa ni mambo mabaya na hayakubaliki katika jamii ya binadamu.
(v) Tendi /utenzi
Tendi ni tungo ambazo hutumiwa kusimulia matukio ya kihistoria yanayohusishwa na watu maarufu katika jamii. Mara nyingi wahusika wa tendi huwa mashujaa au majagina wanaodhaniwa waliishi katika jamii na walifanya matendo ya kijasiri. Tungo hizo huyaeleza maisha ya mashujaa hao kuanzia kuzaliwa hadi kufa kwao. Wahusika wanaopatikana katika tendi huwa na sifa zinazokiuka uwezo wa binadamu wa kawaida. Huwa na sifa zinazofanana na mashujaa wa mighani.
(vi) Rara
Rara ni hadithi fupi na nyepesi za kishairi zinazosimulia tukio la kuvutia.Tukio hilolaweza kuwa la kweli kama sherehe za uhuru au liwe tukio la kubuni tu. Rara hutongolewa ukiandamanishwa na ala za muziki.
(vii) Rara nafsi
Huu ni ushairi wa kinafsi ambao hutungwa na mtu kuelezea hisia, matatizo na fikra zake mwenyewe kama vile kuhusu mapenzi, usaliti, talaka, kifo. Rara nafsi huwasilishwa kwa njia ya uimbaji unaoandamana na ala za muziki.
(viii) Ngano
Hizi ni tungo ambazo hutokea katika muktadha wa utambaji wa ngano lakini huwa pia zinaandamana na ala za muziki kama marimba, njuga na mengineyo.
(3) Ngonjera
Ngonjera ni tungo za kishairi ambazo huwa na muundo wa kitamthilia. Mazungumzo katika ngonjera ni kulumbiana au kujibizana. Mhusika mmoja husema au huuliza jambo na mhusika mwingine hujibu au kuendeleza mazungumzo. Mazungumzo yanaweza kuwa baina ya watu wawili au zaidi. Ngonjera huanza na fikra kinzano yakiwa na azma ya kutatua utata fulani kuhusu jambo fulani. Suluhisho la utata huo hupatikana hatimaye mwishoni mwa ngonjera.
]]>
VIPERA VYA USHAIRI SIMULIZI

<![CDATA[VIPENGELE VYA FANI KATIKA HADITHI FUPI ZA KISWAHILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1896 Wed, 29 Dec 2021 14:48:15 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1896
.pdf   VIPENGELE VYA FANI KATIKA HADITHI FUPI ZA KISWAHILI.pdf (Size: 305.22 KB / Downloads: 4) ]]>

<![CDATA[UCHAMBUZI WA RIWAYA YA MFADHILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1895 Wed, 29 Dec 2021 14:35:01 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1895
.pdf   UCHAMBUZI WA RIWAYA YA MFADHILI.pdf (Size: 156.56 KB / Downloads: 5) ]]>

<![CDATA[MISINGI YA UHAKIKI KATIKA FASIHI YA KISWAHILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1894 Wed, 29 Dec 2021 14:20:05 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1894
.pdf   Misingi ya Uhakiki katika Fasihi ya Kiswahili.pdf (Size: 45.1 KB / Downloads: 5) ]]>

<![CDATA[FALSAFA YA KIAFRIKA]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1892 Wed, 29 Dec 2021 13:26:24 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1892 Mpaka sasa tumekwishaona maana ya Falsafa ya Kiafrika katika mitazamo miwili, yaani mtazamo wa falsafa kama mtazamo na falsafa kama taaluma. Aidha, tumekwishaona kazi ya kwanza iliyochukuliwa kama kazi ya kwanza na ya msingi kuhusu Falsafa ya Kiafrika, hapa tunazungumzia kitabu cha Placide F. Tempels kinachoitwa Bantu Philosophy (La philosophie bantoue kwa Kifaransa), kitabu hiki kinaweza kusomwa katika wavuti hii www.scribd.com/doc/27632044/Placide-Tempels-Bantu-Philosophy-English. Baadaye tukaangalia kazi ya John S. Mbiti katika kitabu chake kiitwacho African Religions and Philosophy. Kwa upande wetu tuliangalia hasa dhana ya mtu, kifo, muda kwa juujuu ili tuunganishe vizuri na dhana zilizozungumzwa na Placide Tempels. Baadaye tumeangalia mikondo ya Falsafa ya Kiafrika ambapo tuliona mikondo minne kama ilivyoainishwa na Odera Oruka (1990) ambapo tuliona mikondo ifuatayo: ethnofilosofia, mkondo wa siasa na jamii, mkondo wa falsafa ya kitaaluma, falsafa ya watu wenye hekima.
Kwa kifupi, wanaethnofilosofia wanatazama falsafa kama mawazo ya jamii nzima ambayo yanapatikana katika kazi mbalimbali za fasihi simulizi kama vile methali, visasili, visakale, simulizi mbalimbali, na nyimbo. Wanakosolewa kwa kuwa wanachokitilia mkazo si falsafa bali ni mila na desturi za jamii. Suala wanalopaswa kuchambua falsafa kutoka katika vyanzo hivyo. Kwa hiyo mkondo huu wa falsafa una umuhimu wa kutambua vyanzo vinavyoweza kutumiwa kama chanzo cha falsafa ya Kiafrika lakini hawajaweza kuchambua mawazo ya kiafalsafa.
Mkondo wa Siasa na jamii ni mkondo unaohusisha kwa lugha rahisi wapigania uhuru. Wengi wao walianzisha mawazo yao ya Kifalsafa kama nyenzo ya kuwasaidia kupata uhuru katika nchi zao au kujenga mitazamo mipya katika nchi mpya tofauti na mitazamo iliyojengwa na wakoloni. Katika kundi hili tunawaona watu kama vile Nyerere, Nkrumah na Kaunda.
Nyerere akisimamia “Ujamaa” kama msingi wa maisha ya Mwafrika na kwamba Wazungu wamebomoa misingi ya Ujamaa wa Kiafrika na kuleta mifumo yenye unyonyaji ndani yake ilhali huu sio mfumo uliozoeleka kwa Waafrika. Kwa hiyo, Nyerere anadai ni vema turudi katika mfumowa Ujamaa wa Kiafrika ili tujenge jamii itakayoondoa mifumo ya kinyonyaji. Kwa Mwalimu Nyerere, mfumo wa Ujamaa wa Kiafrika ni mfumo mzuri unaowafaa Waafrika.
Kwame Nkrumah kwa upande wake anaona mfumo uliokuwa ukitumika Afrika kabla ya ukoloni ni mzuri kuliko mfumo wa ubepari. Anaamini kuwa ili Afrika isonge mbele inahitaji kuachana kabisa na mfumo wa kibepari. Hata hivyo, tofauti na Mwalimu Nyerere Nkrumah hashauri Waafrika warudie kwenye mifumo yao ya awali, (yaani baada ya kuondoka wakoloni) badala yake Waafrika waunde mfumo utakaokuwa na mseto wa mawazo mbalimbali ikiwemo yale ya Kiislamu, Kikristu yaliyotoka Ulaya na mawazo ya Kiafrika. Tukumbuke kuwa Nkrumah kama Nyerere ni watu waliokuwa wasomi na waliathiriwa kiasi fulani na falsafa za kisoshalisti za Karl Marx, Vladmir Lenin na Mao. Kwa hiyo wote walikuwa na mtazamo wa kijamaa, kinyume na ubepari. Kwa kifupi, mtazamo wa Kwame Nkurumah ni kama vile umekaa kinadharia zaidi kuliko ule wa Nyerere.
Kwa upande wake Kenneth Kaunda, ambaye yu hai hadi hivi sasa anatazama Afrika inayojengwa kwa misingi ya utu. Kaunda anadai kuwa utu wa ndio silaha pekee iliyowasaidia Waafrika kuondokana na ukoloni. Utu ni kitu kinachoviweka pamoja dini na siasa; vyote vinahitaji utu ili vilete matokeo yanayohitajika katika jamii. Kaunda alikuwa Mkristu hivyo anaingiza wazo la Mungu katika mtazamo wake akidai kuwa ili kuwa na taifa lenye upendo, uelewano na amani, ni lazima watu wake wawe na nia thabiti ya kumfuata Mungu, kujitahidi kufanana na Mungu. Kama Nyerere na Nkrumah, Kaunda pia alikuwa na mawazo ya Kijamaa lakini aliyachanganya na na Ukristu lakini pia aliingiza misingi ya maadili ya Kiafrika. Kwa kifupi wanasiasa hawa walizungumzia masuala mengi, lakini hapa tunadokeza tu mawazo ya msingi.
]]>
Mpaka sasa tumekwishaona maana ya Falsafa ya Kiafrika katika mitazamo miwili, yaani mtazamo wa falsafa kama mtazamo na falsafa kama taaluma. Aidha, tumekwishaona kazi ya kwanza iliyochukuliwa kama kazi ya kwanza na ya msingi kuhusu Falsafa ya Kiafrika, hapa tunazungumzia kitabu cha Placide F. Tempels kinachoitwa Bantu Philosophy (La philosophie bantoue kwa Kifaransa), kitabu hiki kinaweza kusomwa katika wavuti hii www.scribd.com/doc/27632044/Placide-Tempels-Bantu-Philosophy-English. Baadaye tukaangalia kazi ya John S. Mbiti katika kitabu chake kiitwacho African Religions and Philosophy. Kwa upande wetu tuliangalia hasa dhana ya mtu, kifo, muda kwa juujuu ili tuunganishe vizuri na dhana zilizozungumzwa na Placide Tempels. Baadaye tumeangalia mikondo ya Falsafa ya Kiafrika ambapo tuliona mikondo minne kama ilivyoainishwa na Odera Oruka (1990) ambapo tuliona mikondo ifuatayo: ethnofilosofia, mkondo wa siasa na jamii, mkondo wa falsafa ya kitaaluma, falsafa ya watu wenye hekima.
Kwa kifupi, wanaethnofilosofia wanatazama falsafa kama mawazo ya jamii nzima ambayo yanapatikana katika kazi mbalimbali za fasihi simulizi kama vile methali, visasili, visakale, simulizi mbalimbali, na nyimbo. Wanakosolewa kwa kuwa wanachokitilia mkazo si falsafa bali ni mila na desturi za jamii. Suala wanalopaswa kuchambua falsafa kutoka katika vyanzo hivyo. Kwa hiyo mkondo huu wa falsafa una umuhimu wa kutambua vyanzo vinavyoweza kutumiwa kama chanzo cha falsafa ya Kiafrika lakini hawajaweza kuchambua mawazo ya kiafalsafa.
Mkondo wa Siasa na jamii ni mkondo unaohusisha kwa lugha rahisi wapigania uhuru. Wengi wao walianzisha mawazo yao ya Kifalsafa kama nyenzo ya kuwasaidia kupata uhuru katika nchi zao au kujenga mitazamo mipya katika nchi mpya tofauti na mitazamo iliyojengwa na wakoloni. Katika kundi hili tunawaona watu kama vile Nyerere, Nkrumah na Kaunda.
Nyerere akisimamia “Ujamaa” kama msingi wa maisha ya Mwafrika na kwamba Wazungu wamebomoa misingi ya Ujamaa wa Kiafrika na kuleta mifumo yenye unyonyaji ndani yake ilhali huu sio mfumo uliozoeleka kwa Waafrika. Kwa hiyo, Nyerere anadai ni vema turudi katika mfumowa Ujamaa wa Kiafrika ili tujenge jamii itakayoondoa mifumo ya kinyonyaji. Kwa Mwalimu Nyerere, mfumo wa Ujamaa wa Kiafrika ni mfumo mzuri unaowafaa Waafrika.
Kwame Nkrumah kwa upande wake anaona mfumo uliokuwa ukitumika Afrika kabla ya ukoloni ni mzuri kuliko mfumo wa ubepari. Anaamini kuwa ili Afrika isonge mbele inahitaji kuachana kabisa na mfumo wa kibepari. Hata hivyo, tofauti na Mwalimu Nyerere Nkrumah hashauri Waafrika warudie kwenye mifumo yao ya awali, (yaani baada ya kuondoka wakoloni) badala yake Waafrika waunde mfumo utakaokuwa na mseto wa mawazo mbalimbali ikiwemo yale ya Kiislamu, Kikristu yaliyotoka Ulaya na mawazo ya Kiafrika. Tukumbuke kuwa Nkrumah kama Nyerere ni watu waliokuwa wasomi na waliathiriwa kiasi fulani na falsafa za kisoshalisti za Karl Marx, Vladmir Lenin na Mao. Kwa hiyo wote walikuwa na mtazamo wa kijamaa, kinyume na ubepari. Kwa kifupi, mtazamo wa Kwame Nkurumah ni kama vile umekaa kinadharia zaidi kuliko ule wa Nyerere.
Kwa upande wake Kenneth Kaunda, ambaye yu hai hadi hivi sasa anatazama Afrika inayojengwa kwa misingi ya utu. Kaunda anadai kuwa utu wa ndio silaha pekee iliyowasaidia Waafrika kuondokana na ukoloni. Utu ni kitu kinachoviweka pamoja dini na siasa; vyote vinahitaji utu ili vilete matokeo yanayohitajika katika jamii. Kaunda alikuwa Mkristu hivyo anaingiza wazo la Mungu katika mtazamo wake akidai kuwa ili kuwa na taifa lenye upendo, uelewano na amani, ni lazima watu wake wawe na nia thabiti ya kumfuata Mungu, kujitahidi kufanana na Mungu. Kama Nyerere na Nkrumah, Kaunda pia alikuwa na mawazo ya Kijamaa lakini aliyachanganya na na Ukristu lakini pia aliingiza misingi ya maadili ya Kiafrika. Kwa kifupi wanasiasa hawa walizungumzia masuala mengi, lakini hapa tunadokeza tu mawazo ya msingi.
]]>
<![CDATA[UHAKIKI WA TEUZI ZA NAFSI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1891 Wed, 29 Dec 2021 13:13:06 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1891 Francis H.G. Semghanga: Teuzi za Nafsi
SURA YA SITA
Diwani ya Teuzi za Nafsi ni mkusanyo wa tenzi tano: “Ewe Mama Mpenzi”, “Kidani cha Huba”, “Ewe Mwana”. “Siasa Yetu” na “Ujamaa Vijijini.” Kwa vile kwa namna moja ama nyingine tenzi hizi zote zinaingiliana hapa na pale kifani na kimaudhui, tutaziangalia kidhamira kwa jumla badala ya kuzichambua moja moja.
DHAMIRA KUU
Dhamira kadhaa zinajitokeza katika tenzi za diwani hii. Kati ya hizo, kuu ni kama saba hivi:
1. Mapenzi
2. Mila na desturi za jadi
3. Umuhimu wa elimu
4. Ukamilifu wa mtu na ulu wake
5. Ndoa katikajamii
6. Nafasi ya mwanamke katika jamii
7. Siasa.
Mapenzi
Mshairi anajaribu kujibu swali ta maana yu mapenzi halisi. Katika “Ewe Mama Mpenzi,” tunaonyeshwa mapenzi ya mtoto kwa mama yake. Mapenzi haya yamejikita katika “deni” alilonalo mtoto kwa mama yake hasa kutokana na uchungu wa kumbeba tumboni na hatimaye kumzaa na kumlea. Hapa mshairi anaonyesha kuwa mapenzi ya mama hayawezi kulipwa kwani hayakadiriki.
Katika “Kidani cha Huba” mapenzi baina ya mwanamume na mwanamke yanaonyeshwa katika sura zake mbalimbali. Kwa kupitia katika ndoto (beti za 34-61) mwpndishi anatuonyesha mapenzi mabaya yanayofuata sura na vitu kama ile nguo na umbo. Kinyume chake mshairi anascma kuwa mapenzi mazuri ni yale ya labia njema:
63 Ni wewe nakuwazja,
Tabiayo ni murua,
Tena u mwenye kujua,
Wa akili na busuri.
64 Huna ndeo huna hila,
Unenayo ni aula,
Ningakuwa ni muila,
Hunifanyii ghairi.
Katika “Ewe Mwana” tunaonyeshwa mapenzi baina ya baba na mwana; mapenzi ambayo yamejengwa juu ya malezi mema na mawaidha kuhusu umuhimu wa kushika dini (beti za 1-143), umuhimu wa kuwaheshimu wazazi (beti za 144-160), kuheshimu kazi (beti za 144-160), kuepuka uvivu, ulevi, uzembe na ufasiki, na kuwa na heshima kwa watu.
Tenzi za “Siasa Yetu” na “Ujamaa Vijijini” zinaonyesha aina tofauti ya mapenzi: mapenzi ya kijamii na kitaifa yaletwayo na siasa ya ujamaa na kujitegemea. Katika “Siasa Yetu” tumepewa nguzo kuu nane za mapenzi hayo:
1. Usawa wa binadamu
2. Heshima baina ya watu
3. Haki ya kushiriki katika uongozi
4. Uhuru wa kufuata dini yoyote aitakayo mtu
5. Haki ya kuwa na makazi mazuri
6. Haki ya kuwa na kazi na kupata ujira utokanao na jasho la mtu
7. Umuhimu wa kujitegemea
8. Umuhunu wa Serikali kumiliki njia zote kuu za uchumi pamoja na kulinda usawa katika mgawanyo wa mali.
Kwa jumla dhamira hii ya mapenzi imepanuliwa sana katika diwani hii kwa kupewa nyuso hizo tulizozitaja. Hata hivyo, msomaji wa “Ewe Mama Mpenzi” na wa “Kidani cha Huba” huweza kuchoshwa sana na marudiorudio mengi ya kauli zenye kumaanisha jambo moja; na hasa katika “Kidani cha Huba” ambamo kumejaa mapenzi ya “sili silali” pamoja na wingi wa sala ambazo sio za lazima.
Mila na Desturi za Jadi
Baadhi ya tenzi katika diwani hii zinaibusha masuala fulanifulani ambayo yaha umuhimu wa kisosholojia. Mathalani, katika utenzi wa kwanza wa “Ewe Mama Mpenzi,” beti za 72-77 zinaonyesha imani za jamii ya mwandishi kuhu.su “kinga” itokanayo na tunguri, pembe, hirizi na chanja. Baadaye katika beti za “4-181 mila na desluri za jadi kumhusu mtoto mara baada ya kuzaliwa zinajitokeza, na baada ya baba kufariki tunaiona mila imhusuyo mama kuhamia kwa mjomba. Kwa jumla beti hizi zinatuonyesha nguvu za utamaduni wa jadi japokuwa tunaweza kuuliza kama mila na desturi hizi zina nafasi gani katika maisha ya leo.
Utenzi wa mwisho wa “Ujamaa Vijijini” nao unatupa taswira ya mila, desturi na imani za mababu zetu wa zamani:
1. Jamaa zetu zamani
Waliishi na vijijini
Kwa ujamaa yakini
Na bila kujitambua.
Utenzi unatoa picha ya ujima wa awali uliowashirikisha wanajamii wote katika kufanya kazi. Ufanyaji kazi huu uliambatana na haki na usawa wa kugawana mapato:
13. Hitaji za hao watu,
Ziwile “chakula chetu,
Ardhi na ng’ombe wetu.”
‘Ansu’ hawakuiiua.
Katika maisha haya ya ujamaa wa asili tunaonyeshwa kuwa watu waliishi kwa kupendana na kushirikiana (ubeti wa 20); waligawana mali kiusawa (ubcti wa 29); hapakuwa na wizi (ubeti wa 32); na njia kuu za uzalishaji mali zilimilikiwa na umma wote kama ielezwavyo katika beti za 33 na 34. Pia, kaiika jamii hii ya awali kila mtu alifanya kazi, hakuna aliyeishi kwa jasho la mwingine.
Mshairi, hata hivyo, anaikosoa jamii hii ya awali kwa kumgandamiza mwanamke. Hili tutalichambua vizuri zaidi wakati wa kuichunguza dhamira ya nafasi ya mwanamke katika jamii.
Mshairi anatuonyesha, sawa na Mwalimu Nyerere alivyofanya katika andiko lake la Ujamaa Vijijini, kwamba maisha haya ya mababu zetu ndio msingi mkubwa wa siasa ya Tanzania ya ujamaa.
Umuhimu wa Elimu
Katika diwani hii mwandishi anatuonvesha aina mbili kuu za elimu:
1. Elimu itokanayo na shule na vitabu
2. Elimu ya kurithishwa.
Katika beti za 209-213 za “Kidani cha Huba,” mshairi anaonyesha jinsi vitabu vinavyoyapanua mawazo ya mtu, na piajinsi vilivyo “ngazi” ya kumpandisha daraja. Elimu hii imeonyeshwa kuwa ni silaha ya ukombozi wa mtu kikazi, kicheo na pia katika upande wa mapato. Kutokana na elimu aliyo nayo mshairi ya utaalamu wa kilimo, tunaonyeshwa pia faida zake kwa mkulima ambaye huutumia utaalamu huu na kuongeza ufanisi wa kazi yake.
EIimu ya kurithishwa tunaiona ikielelezwa katika sehemu mbalimbali zinazohusu desturi na mila za jadi ambako mtoto anafunzwa na wazazi wake juu ya maisha bora katika jamii.
Ukamilifu wa Mtu na Utu Wake
Mshairi anatupatia taswira ya ukamilifu wa mtu na utu wake kwa kutuorodheshea sifa azionazo kuwa ni muhimu katika maisha ya mtu.
Kwanza, katika tenzi zote Semghanga anasisitiza kuwa ukamilifu wa mtu hutokana na kufuata mafunzo ya dini pamoja na “amri” za Mungu. Wakati ambapo “ukamilifu” huu unakubalika kwa wale ambao bado wanaweka mategemeo na matumaini yao katika nguvu zilizoko nje ya uwezo na mazingira ya mwanadamu hapahapa duniani, kwa wale ambao maisha ya mtu yanaanza na kumalizikia duniani “ukamilifu” huo utaonekana kuwa si wa maana yoyote.
Katika utenzi wa “Kidani cha Huba” tunapewa taswira nyingine ya ukamilifu wa mtu. Zaidi ya kwamba heshima na unyenyekevu ni sehemu ya kukamitika huko, mwandishi pia anaonyesha ukamilifu wa kimaumbile. Mathalani, katika beti za 35 na 36 za “Ewe Mama Mpenzi” twaelezwa haya:
35. Awe mwana sio jitu,
Ambalo halina utu,
Nimzae mwana mtu,
Nisimzae kitishia.
36. Awe mtu wa kamiti,
Aleumbika muili,
Na kuchongoka kauli,
Mengine nipishilia.
Sifa za “kuumbika muili” tunazikuta pia katika utenzi wa “Kidani cha Huba” ambamo mshairi anajieleza kwa mpenzi wake kuhusu ukamilifu wa maungo yake:
171. Umbo langu kawaida,
Kwangu mie laakida,
Sikia hayo muwada,
Uyajue ukariri.
172. Kichwa si kikubwa sana,
Tena kimenilingana,
Wala hakikupitana,
Kimewekwa barabari.
173. Kina sikio za kingo,
Tamthili vile ungo,
Yamekaa kwa mpango,
Kwenye panja za kadiri.
Baada ya sifa zihusuzo viungo mbalimbali vya mwili, mshairi anasema kuwa kakamilika kwani:
186. Muili wote mzima,
Sina mie ukilema,
Ninaketi ninaima,
Tembeo natasawari.
187. Ni wa Manani mpango,
Kunipa hivyo viungo,
Viwe kwangu ni ukingo,
Kuniambaza fakiri.
Labda swali liwezalo kuzuka kuhusu hii dhana ya “kukamilika” kwa mtu kama aitoavyo mshairi ni: je, mazingira ya jamii ya kiuchumi, kisiasa na kitamaduni yana nafasi gani katika dhana hii? Hili ni swali muhimu kwani “kukamilika” kwa mtu na utu wake hutegemea wakati na mahali. Katika jamii ya kibepari kama ya Marekani, kwa mfano, mtu huonekana kakamilika kama ana malimbikizo ya mali nyingi za kibinafsi na pesa nyingi, wakati ambapo dhana ya “ukamilifu” wa mtu si hivyo katikajamii za kijamaa.
“Ukamilifu” mwingine wa mtu ni ule wa kiwango cha jamii ambao unamhitaji ayafuate maadili na amali mbalimbali za wanajamii wenzake. Huu ni wa kisiasa, nao tutaujadili vizuri katika dhamira ya mwisho.
Ndoa Katika Jamii
Kwa mawazo ya Semghanga, taasisi ya ndoa ni jambo la lazima na muhimu katika jamii. Mshairi anatuonyesha kuwa kuoa au kuolewa si jambo la hiari bali ni wajibu wa kila mtu afikiapo makamo yanayoruhusu.
Mshairi anaonyesha jinsi ambavyo kutokana na ndoa mapenzi yanapatikana, kwani katika ndoa kuna kusaidiana, kuheshimiana, kuzaa, pamoja na kulea watoto.
Umuhimu wa ndoa umeonyeshwa hasa katika utenzi wa “Kidani cha Huba’ ambamo beti za 74-99 zinapinga ukapera na upweke wa kutooa au kuolewa:
75. Kupwekeka si auta,
Kwasababisha madhila,
Hata mtu angekula,
Hana raha na sururi.
76. Kupwekeka nuksani,
Alisema Shaabani,
Hukutia aibuni,
Ukavunjiwa suturi.
79. Ujane kitu dhalili,
Kasema Akilimali,
Nayo ndoa nafttdhili,
Ashirafu na fahari.
Majina ya Shaaban (Robert) na Akilimali (Snowhite) yametajwa kwani katika ushairi wao washairi hawa walitetea sana ndoa na kupinga ujane.
Katika kuisifu ndoa mwandishi anatumia tamathali mbalimbali ambazo anatutaka tuzilinganishe na kuzilinganua na zile zinazoonyesha ubaya wa ujane. Kwa hiyo-basi upweke na ujane kauita “nuksani”, “una misiba”, “hauna heba”, “ni mkatili” na ni “kitu dhalili”; wakati ambapo tunaeiezwa yafuatayo kuhusu ndoa:
80. Ndoa pambo la unasi
Ni kidani cha nafsi
Ni kifao kwetu sisi
Kukikosa takiriri
81. Ndoa ni kitu cha hadhi
Hutoa shaka na udhi
Na tena hukuhifadhi
Penye tabu na usiri.
Twaambiwa pia kwamba ndoa ni fadhila ambayo imetoka kwa Mungu.
Wakati ambapo baadhi ya wasomaji watamuunga mkono Semghanga kuhusu ndoa katika jamii, huenda baadhi wasikubaliane naye. Inaelekea kuwa mshairi huyu anaamini kuwa ndoa hutatua matatizo yote baina ya wawili wanaooana. Lakini, hata hivyo ingembidi mshairi ajiulize maswali kuhusu talaka zinavyozidi kuongezeka leo hii si katika jamii za Ulaya tu bali pia katika jamii za Afrika.
Ndoa, kama taasisi zingine zote, ni zao la jamii. “Ukamilifu” na mabadiliko katika taasisi hii hutegemea mfumo mzima wa Jamii pamoja na mtazamo wa wanajamii kiutamaduni, kisiasa na kiuchumi. Leo hii yametokea mabadiliko mengi katika jamii kiasi ambacho taasisi hii si kama ilivyokuwa zamani. Imeingiliwa na nguvu mbalimbali za kijamii kama vile uchumi wa kifedha, kuzuka kwa miji ambayo inavutana na vijiji, na madaraka ya watawala kiasi kwamba wazazi hawana tena kauli juu ya nani amuoe au aolewe na mtoto wao – vjjana wanaweza kwenda kwa mkuu wa wilaya na kuoana bila idhini ya wazazi wao, na mengi mengineyo. Yote haya yameibadili taasisi hii kiasi ambacho kiuhalisi mawazo ya Semghanga yanaeleza ndoa inavyotakiwa iwe na siyo ilivyo. Kulikuwa na haja kwa mshairi kuzingatia athari za kimazingira juu ya taasisi hii ili atupatie taswira sahihi ya ndoa badala ya ile ya “mito ya asali na maziwa” aliyotupatia.
Nafasi ya Mwanamke Katika Jamii
Suala la nafasi ya mwanamke katika jamii limeshughulisha sana kalamu za waandishi wengi wa Kiswahili. Wengi wao wameiona nafasi hii kuwa ni duni ya kuonewa na kunyanyaswa.
Katika diwani hii, mshairi anaangalia masuala matatu kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii. Kwanza kamwangalia mwanamke kama mama. Hili tunaliona katika utenzi wa “Ewe Mama Mpenzi” ambamo jukumu la kubeba mtoto tumboni kwa miezi tisa likiambatana na uchovu na maumivu, halafu uchungu wa kujifungua mtoto huyo – yote haya yanaonyeshwa na mwandishi asemapo:
32. Miezi tisa wandani,
Kijusu bila amani,
Nakanyaga na mbavuni,
Wewe umevumilia.
33. Uchovu kila namuna,
Na umivu na sonona,
Ukivumilia nina,
Huku unaniombea.
Pili, kamwona mwanamke kama pambo au ua zuri – taswira ambayo aghalabu hujitokeza sana katika baadhi kubwa ya kazi za fasihi na hata nyimbo za bendi zetu – kama ionekanavyo katika ubeti wa 161 wa utenzi wa “Kidani cha Huba”
61. Awe kama ua safi,
La urembo na usafi,
Livutivu na nadhifi,
Na nukioja ambari.
Tatu, kama ionekanavyo katika utenzi wa mwisho, mshairi ameikosoa jamii ya zamani kwa kumdunisha mwanamke. Anasema:
56. Japo tulihusiana,
Pia tukaheshimiana,
Mwanamke tunakana,
Hakupata afudhaa.
57. Hakuthaminika mke,
Kwa hali na umbo lake,
Heshima kuwekwa kwake,
Ni ajabu na ajaa.
58. Walifanya kazi mama,
Kama watumwa na uma,
Huku wakishika tama,
Pasina kufurahia.
Beti hizi na zingine zinazoongelea suala la nafasi duni ya mwanamke katika jamii hii ya ujima wa awali, zinafanya kosa moja kubwa la kihistoria. Kosa hilo ni lile la kumpa mwanamke nafasi ambayo hakuwa nayo katika jamii ya awali kabisa ya mtu. Utengano anaouongeiea Semghanga baina ya mwanamume na mwanamke haukuwapo enzi za ujima wa awali. Tujuavyo, bistoria ya jamii ya watu ina hatua kuu tano: ujima wa awali, utumwa, umwinyi, ubepari, na ujamaa ambao hatima yake ni ukomunisti. Mfumo wa jamii ya kiujima haukuwa na matabaka ya watu. Mazingira ya wakati huo yaliyokuwa ya kiuhasama kwa mtu hayakuruhusu “anasa” za mgawanyiko wa watu kwa kufuata tabaka au jinsi ya kike au ya kiume. Yalihitaji watu wote washirikiane kwa pamoja kupambana na mazingira hayo. Ni baadaye sana, baada ya jamii kuanza kuwa na mifumo ya kitabaka na mali au milki za kibinafsi, ndipo suala la kugandamizwa na kuonewa kwa mwanamke linapojitokeza. Hili liliambatana na mambo ya mahari pamoja na kumwona mwanamke kuwa ni moja ya milki hizo za kibinafsi. Hali za namna hii hazikuwapo katika jamii ya ujima wa awali.
Siasa
Katika mkusanyo huu wa tenzi, tenzi mbili za mwisho zinashughulikia masuala ya kisiasa. Kama tulivyokwishaonyesha, “Siasa Yetu” ni utenzi mfupi unaoorodhesha nguzo muhimu za siasa ya Tanzania. Nguzo hizi ndicho kiini cha siasa ielezwayo katika “Ujamaa Vijijini.”
Kama alivyosema mwandishi katika Utangulizi, utenzi wa “Ujamaa Vijijini” ni “kama tafsiri ya kitabu cha Mwalimu Julius K. Nyerere UJAMAA VIJIJINI (uk. iii). Humu, baada ya k’uiangalia jamii ya zamani ilivyoishi kijamaa, mshairi, sawa na Nyerere, ameikosoa jamii ya leo hasa kuhusu maadui kama vile ujinga (ubeti wa 74), tamaa ya kujilimbikizia mali (beti 84-89), kupenda miji na kuchukia vijiji (ubeti wa 90), kukosekana kwa usawa baina ya watu (ubeti wa 106), na kukosekana uongozi bora (ubeti wa 202). Hayo yote mwandishi anahubiri kuwa hatuna budi kuyarekebisha ili kujenga jamii ya ujamaa kamili.
Njia anazozipendekeza mshairi kuwa zitatuletea maendeleo hazitofautiani na za Nyerere, nazo zinahusu mambo kama vile kuwa na usawa wa binadamu, kuunda vyama imara vya ushirika (beti za 109-117), kilimo bora cha shirika (ubeti wa 118), ujenzi wa ujamaa kwa kuzingatia tofauti za mazingira (beti za 141-144), kutumia mali asili ya jamii kwamanufaa yajamii nzima (ubeti 146), kutunza vizuri mahesabu ya mapato na matumizi (ubeti wa 163), uongozi bora (beti za 200-206), kuwa na demokrasia (beti za 235-237), Chama na serikali kuwa na mipango madhubuti ya kusimamia ujenzi wa jamii, pamoja na kujitegemea.
Labda ingefaa ieleweke tu kuwa mshairi hakukusudia kutathmini na kuhakiki siasa ya ujamaa vijijini, bali nia yake kubwa ilikuwa kunakili yale yaliyoelezwa katika kijitabu cha Nyerere. Kwa hiyo, kwa msomaji ambaye alikwishasoma kitabu hicho cha Mwalimu Nyerere, utenzi huu hautoi lolote jipya kimaudhui.
Utatuzi wa Migogoro
Mwandishi ameibusha migogoro ambayo pia amejaribu kuipendekezea masuluhisho. Hata hivyo, mengi ya masuluhisho hayo ni ya kimaadili na kimahubiri, na yamejikita katika udhanifu wa kidini. Kwa mfano, katika Utenzi wa “Ujamaa Vijijini,” baada ya kueleza njia sahihi ya ukombozi wa wanawake mshairi anatoa tu maonyo:
68. Si vyema hata kidogo,
Wake kuwafanya gogo,
La kukalia mzigo,
Huku wakivumilia.
69. Hilijambomnukusi,
Kudunisha mzima nusi,
Ya Tanzania unasi,
Si vyema hili sikia.
Baada ya mahubiri haya, mshairi anadhani amekwishaiteka mioyo ya wanaume wanaowadunisha wanawake, kwa hiyo anatoa utatuzi:
72. Tukitaka wendeleo,
Tuwape wake ufao,
Uhuru na haki zao,
Hapo tutaendelea.
Ni dhahiri kwamba ni kosa kufikiria kuwa kwa kuhubiri tu tutaibadili mioyo ya watu, nao wataziacha dosari zao. Hivi ni kukwepa uhalisi wa nguvu mbalimbali za kimazingira zilizozizaa dosari hizi. Huu ni udhaifu unaojitokeza karibu katika kila dhamira aliyoishughulikia mshairi wa Teuzi za Nafsi. Katika tenzi mbili za mwisho ndimo tu mlimo na utatuzi wa migogoro katika kiwango cha mfumo wa janui, ijapokuwa hapa pia hatuwezi kumsifu mshairi kwani haya si mawazo yake ila kayanakili tu.
Dhamira nyinginezo
Tulizozishughulikia ni baadhi tu ya dhamira muhimu zijitokezazo katika diwani hii. Ziko dhamira zingine ndogo ndogo ambazo msomaji huweza kuzichambua sambamba na hizo tulizoziangalia. Kwa mfano dhanura ya umuhimu wa kazi inaweza kuchambuliwa kipekee na kuonyeshwa jinsi mshairi alivyoiangalia. Kazi za aina zote – za sulubu na za akili zimeonyeshwa zinavyohitaji kuthaminiwa na kuheshimiwa kwani kazi ni msingi wa mapenzi na hata wa ndoa. Mshairi kaonyesha basi, kuwa kazi ni wajibu kwani ndiyo chanzo cha heshima kwa mtu.
Dhamira nyingine ambayo msomaji huweza kuichunguza kipekee ni ile ya nafasi ya dini au Mungu katika maisha ya mtu. Hii imejitokeza sana katika tenzi tatu za mwanzo ambazo zinatuonyesha jinsi mshairi anavyoamini kuwa mtu ni kiumbe dhaifu ambaye hawezi kuishi bila msaada na baraka za Mungu. Ndiyo sababu mshairi ameona heri azinakili Amri Kuu za Mungu pamoja na Amn Sita za Kanisa ili kukamilisha mahuhiri yake. Ni dhahin kuwa katika jamii ya leo ambapo dini inaelekea kupoteza nafasi muhimu iliyokuwa imeishikilia hapo awali, dhamira hii huweza kuzusha mjadala mkubwa wa kuuliza kama dini inayo nafasi yoyote katika maendeleo ya jamii iliyotawaliwa na elimu, sayansi na teknolojia za hali ya juu.
FANI KATIKA TEUZI ZA NAFSI
Kwa msomaji ambaye amekwishasoma kazi nyingi za washairi wengine wa Kiswahili kama vile za akina Muyaka bin Haji, Abdilatif Abdalla, Shaaban Robert. Mathias Mnyampala, Saadani Kandoro, Amri Abedi, Akilimali Snowhite, E. Kezilahabi, M.M. Mulokozi na K.K. Kahigi, miongoni mws wengi wengineo, itadhihirika wazi kuwa Francis HJ. Semghanga bado hajaiva kwa upande wa ufundi wa kisanaa.
Mara nyingi fani ya Teuzi za Nafsi imeonekana kuwa chapwa. Japokuwa mshalri kajitahidi kuzingatia kanuni za tenzi’ za kimapokeo za vina, ulinganifu wa mizani na mpangilib wa beti; kanuni na minyororo hii ya “sheria” imemfunga mno ikamletea matatizo. Kwa vile ilimbidi afuate kanuni za vina na mizani, mara nyingi kutokana na upungufu wa maneno mshairi amerudiarudia msamiati uleule katika beti mbalimbali hadi unamchosha msomaji.
Kurudiarudia huku si kuie tukukutapo katika ubeti wa 110 wa “Ewe Mama Mpenzi” au ule wa neno “mtwae” katika beti za 135-138, kwa mfano. Hapa inajulikana wazi kuwa mshairi anafanya hivyo kama mtindo wa kusisitiza. Mtindo huu wa kusisitiza umejitokeza hata katika beti za 176-181 za utenzi huo huo, beti za 164-167 za “Kidani cha Huba” zinazolirudia neno “japo”, na beti za 78-81 za “Ujamaa Vijijini” zenye kurudia bahari ya “shabaha itatimia.”
Kule kurudiwarudiwa kwa maneno mengi ya hapa na pale ambayo yangeweza kupatiwa mengine ya maana na mizani sawa na yenyewe ndiko kunakomchosha msomaji. Kwa mfano, katika beti za 19 na 20 za “Ewe Mama Mpenzi,” mshairi katumia maneno “na kwisha” ambayo angeweza kuyatumia katika ubeti mmoja tu na kutumia neno kama “baada,” katikaubeti mwingine. Pia, katika beti za 196 na 198 za utenzi wa “Ujamaa Vijijini” tunaona jinsi mshairi alivyokosa msamiati wa kuundia tamathali zake kwa hiyo akatumia ile ya “taji” kwa mambo mawili. Msomaji anaweza kugundua mifano mingine mizun zaidi ya udhaifu huu wa Semghanga.
Pia, mara nyingi mizani imezidi ile ya kanuni za kimapokeo na ni dhahiri kuwa mshairi hakuikusudia iwe hivyo. Mathalani, mstari wa mwisho wa ubeti wa 180 wa “Ewe Mwana,” na wa tatu wa ubeti wa 181 wa utenzi huo huo; mstan wa pili wa ubeti wa 196 wa “Ujamaa Vijijini,” na wa kwanza wa ubeti wa 219 wa utenzi huo huo – yote maonyesha kuwa katika kupungukiwa na msamiati, mshairi alijikuta katumia mizani 9 badala ya 8. Na hata wakati mwingine mshairi katumia mizani kumi katika baadhi ya mistari. Mfano ni mstan wa mwisho wa ubeti wa 252 wa utenzi wa “Ujamaa Vijijim.”
Kwa Jumla, mtu asomapo tenzi hizi, hasa tenzi tatu za kwanza, ataona kuwa mshairi amezirefusha tu bila sababu maalumu. Maudhui ya mawaidha na sala pamoja na dua mzomzo yangeweza kupunguzwa sana, labda kvva zaidi ya nusu, na bado yakaleta maana ile ile aliyoikusudia mwandishi
Ushairi husemwa umeiva kwa matumizi yake ya iugha ya mficho, y kipicha (taswira) na ishara. Lugha ya namna hii ndiyo aghalabu huutofautisha ushairi na tanzu zingine za fasihi kama vile riwaya, hadithi, au tamthilia. Hata hivyo lugha ya aina hii imetumika kwa nadra sana katika Teuzi za Nafsi. Mara nyingi lugha aliyoitumia mwandishi ni ya moja kwa moja ambayo haina ubunifu wa kisanaa ndani yake.
Sehemu tuwezazo kuzitaja kuwa rimetumia lugha kisanaa ni kama vile ubeti wa 26 wa utenzi wa “Ewe Mama Mpenzi” unaotoa taswira ya “zigo” kuwakilisha kazi kubwa ya kumshukuru mama; ubeti wa 126 wa utenzi huohuo utumiao tamathali ya sitiari ya kumwita mama “nyota ya hudumu;” mtindo wa lugha ya majigambo tuuonao katika beti za 244-249 za utenzi huohuo; tamathali zieiezazo maana ya maisha katika beti za 257 na 258 za utenzi huohuo; tamathaii ya kumwita mkosa dini kuwa ni “safura” katika ubeti wa 130 wa “Ewe Mwana;” na ile ya kuuita usawa kuwa ni “taji” ya watu.
Mwisho wa utenzi wa ”Ewe Mwana” ni wa ghafla mno, na kwa baadhi ya wasomaji huu ni udhaifu kwani yaelekea mshairi aliukatisha tu utenzi huu baada ya yeye mwenyewe kuchoshwa nao.
Japokuwa katika utenzi mfupi wa “Siasa Yetu” mshairi kaonyesha mtindo tofauti na ule wa idadi ya vina na hata wa mizani katika mistari ya beti, na japokuwa huenda mshairi akapata sifa za kuwa miongoni mwa “‘wanamapinduzi” wa mwanzo walioutoa utenzi wa Kiswahili kutoka katika silisila za maadili, dini na historia tu na kuungiza katika masula ya mapenzi na mahaba, uzito wa sifa hizo hupungua hasa tuzingatiapo udhaifu wa ufundi wa kisanaa na hata wa kimaudhui kama tulivyouonyesha; udhaitu uonyeshao uchanga wa mshairi huyu katika bahari kubwa ya ushairi wa Kiswahili.
Maswali
1. Ichambue dhana ya “mapenzi halisi” kama ilivyojitokeza katika diwani ya Teuzi za Nafsi.
2. Jadili jinsi mwandishi alivyoiibusha na kuishughulikia dhamira ya mila na desturi za jadi katika jamii katika Teuv za Nafsi. Je, unadhani dhamira hii ina nafasi gani katika jamii ya Tanzania ya leo?
3. Chagua dhamira mbili kati ya zifuatazo ujadili zilivyojitokeza katika diwani ya Teuzi za Nafsi:
1. Umuhimu wa elimu
2. Ukombozi wa mwanamke
3. Nafasi ya dini katika maisha ya mtu
4. Siasa.
4. “Kazi ya fasihi haina budi iwe na uwiano mzuri baina ya maudhui yake na fani”. Ijadili kauli hii ukiihusisha na diwani ya Teuzi za Nafsi.
]]>
Francis H.G. Semghanga: Teuzi za Nafsi