MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI.doc (Size: 527.5 KB / Downloads: 8)
]]>falseMwlMaeda]]>2021-12-05T16:40:16Z2021-12-05T16:46:43Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1681 NGAZI ZA UTAMBUZI NA VITENZI VYA UPIMAJI.pdf (Size: 9.46 KB / Downloads: 20)
]]>falseMwlMaeda]]>2021-08-10T07:55:33Z2021-08-10T07:55:33Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=817 Shajara ya Somo.pdf (Size: 11.7 KB / Downloads: 15)
]]>falseMwlMaeda]]>2021-08-01T10:47:31Z2021-08-01T10:47:31Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=708 Mtindo hujitokeza katika maandishi na pia mazungumzo.pdf (Size: 161.26 KB / Downloads: 2)
]]>falseMwlMaeda]]>2021-08-01T10:04:36Z2021-08-01T10:04:36Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=706
Mtaala una vifaa vyake maalumu ambavyo vinatakiwa vitumike kwa usahihi ili kutekeleza mtaala kwa ufaninsi. Vifaa hivyo ni;
Muhtasari
Vitabu vya kiada
Kiongozi cha mwalimu
Kitabu cha mwalimu na
Rejea.
MATAYARISHO YA UFUNDISHAJI
Matayarisho ya ufundishaji ni ile hali ya mwalimu kuandaa zana na vifaa muhimu kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia
UMUHIMU WA MATAYARISHO YA UFUNDISHAJI
Kazi ya kufundisha ni kazi ya kitaalamu hivyo inahitaji maandalizi wakati wote. Hivyo basi mwalimu anapaswa kufanya maandalizi ya kutosha kabla ya kuingia darasani kufundisha na kwa mantiki hiyo mwalimu analazimika kujiandaa ili kuepuka matatizo yafuatayo wakati wa kufundisha na kujifunza.
Kukosa mtiririko unaofaa wa ufundisahaji
Kufundisha kwa kubahatisha au kubabaisha
Kuchosha wanafunzi katika kujifunza
Uwezekano wa kupotosha maudhui
Kushindwa kutunza muda
Kushindwa kukidhi matarajio ya somo na ya wanafunzi
Kujiamini au kutojiamini kusiko na misingi dhahiri
Kumbuka:
Ili Mwalimu aweze kukamilika katika maandalizi yake ya ufundishaji wa kila siku ni muhimu awe na baadhi ya vifaa ambavyo ndivyo msingi muhimu na muongozo muhimu wa kazi yake. Miongoni mwa vifaa hivyo ni:
Muhtasari wa somo
Azimio la Kazi
Andalio la Somo
Shajara la somo nk.
]]>falseMwlMaeda]]>2021-08-01T07:54:41Z2021-08-01T07:54:41Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=699
(Angalizo: Hivi ni lazima viwe vimepishana kwa wiki kadhaa )
Kabla ya kusoma
Umeshafikiri kuhusu kile kitabu tangu tulipokisoma kwa mara ya mwisho?
Ungependa kukisoma tena?
Nisimulie unachokumbuka zaidi kuhusiana na kile kitabu.
Wakati wa kusoma
Uliza tena maswali kuhusu muundo wa hadithi na jinsi maneno na picha vinavyochangia katika muundo huu.
Baada ya Kusoma
Umegundua kitu chochote wakati huu ambacho hukukigundua kabla?
Unajisikiaje kuhusiana na hadithi hii baada ya kuisoma tena?
Unapofikiria kitabu hiki sasa, ni kitu gani muhimu kuliko vyote kwako kuhusiana na kitabu?
Baada ya kuwa umekisoma kitabu hiki zaidi ya mara moja, je, ungependekeza wanafunzi wengine pia wakisome zaidi ya mara moja na mwalimu wao?
Imechukuliwa kutoka: Swain, C. Gazeti Msingi la Kiingereza (The Primary English Magazine)
Nyenzo-rejea 3: Hadithi
Nyenzo-rejea ya mwalimu kwa ajili kupanga au kurekebisha ili kutumia na wanafunzi
Andika hadithi ubaoni, lakini usiandike kichwa cha hadithi wala sentensi mbili za mwisho (‘Alitoa shuti – chini kuelekea kulia. Goli zuri!’) ubaoni mpaka sehemu ya mwisho kabisa ya somo lako.
[Kukimbilia utukufu na Mark Northcroft (umri miaka 12 )]
Alikimbia tena na tena. Miguu yake iliuma kama tindikali. Aliweza kusikia waliokuwa wanamfukuzia wakiwa wanamkaribia. Alihisi kuwa asingeweza kukaa nao sana na kwa muda mrefu lakini alijua lazima afanye vile. Hatua zilikuwa zinamkaribia. ‘Haraka! Haraka!’alilia. ‘Siwezi! Siwezi!’ alijibu. Alijisikia nguvu kutoka sehemu fulani ndani ya mwili wake. Sasa alijua kuwa atafanikiwa.
Ghafla mtu alitokea kusikojulikana. ‘Nipate sasa au nisipate kabisa,’ alifikiri.
[Alipiga shuti – chini kuelekea kulia. Goli zuri!]
Tanbihi
‘Miguu yake iliuma kama tindikali’ – Tashbiha hii au ulinganisho huu si rahisi kuueleza lakini unaweza kusema kuwa mwanaume au mvulana huyu alijisikia maumivu katika miguu yake kana kwamba kulikuwa na mchanganyiko wa kemikali iliyokuwa inachemka.
Maswali ya kuwauliza wanafunzi katika maandalizi ya uandishi wa mwanzo na mwisho mbadala wa hadithi hii
Unafikiri ‘A’ ni nani?
Unafikiri yuko wapi?
Unafikiri nini kitamtokea?
Nani ‘mwanamume’?
Watu gani wengine wanaweza kuwa sehemu ya hadithi hii?
Kutakuwa kumetokea nini kabla ya sehemu hii ya hadithi?
Nini kinaweza kutokea baadaye?
]]>falseMwlMaeda]]>2021-08-01T07:45:22Z2021-08-01T07:47:04Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=698MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI
1.0 UTANGULIZI
Somo la Kiswahili ni miongoni mwa masomo ambayo yameonekana kuwa na changamoto katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Katika kukabiliana na changamoto hizi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu wamefanya jitihada za kuandaa miongozo ya masomo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwongozo wa Ufundishaji wa Walimu Kazini wa Somo la Kiswahili.
Mwongozo huu umeandaliwa ili kuweza kuziba mapengo ya ufundishaji na ujifunzaji wa baadhi ya mada za somo la Kiswahili kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Mwongozo umekusudiwa kutumika katika mzunguko wa kwanza kwa mafunzo ya walimu wa sekondari wa somo la Kiswahili.