MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Wasifu/Tawasifu]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ 2024-12-21T13:20:51Z MyBB MwlMaeda]]> 2021-12-18T16:03:09Z 2021-12-19T04:22:35Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1765 <![CDATA[SHAJARA YA MWANA MZIZIMA]]>
.doc   KIGOGOTO_-_Abdilatif_Abdalla.doc (Size: 46.5 KB / Downloads: 0)

*Shajara ya Mwana Mzizim
*Ali*Shajara ya msomea Dua Nyerere, Nyota Yake Ikang’ara*
*Jumbe Muhammad Tambaza*

*JUMBE Muhammad Tambaza,* ni mmoja katika wapigania uhuru mashuhuri wa nchi hii ambao, historia inawataja kama ni watu waliotoa mchango mkubwa sana katika kufanikisha kumng’oa Mkoloni Mwingereza, katika ardhi yetu tukufu.

Hayati Mzee Tambaza, ambaye alifariki mnamo mwaka 1978 hivi, anaingizwa katika kundi moja la watu wa mwanzo kabisa waliompokea kwa furaha na upendo kijana Julius Nyerere kutoka Butiama, alipofika jijini Dar es Salaam kwa kumuunga mkono ‘mia kwa mia’, katika harakati zake za kupigania uhuru wa Tanganyika kwenye miaka ya 1950s.

Wanaharakati wengine aliokuwa nao ni pamoja na Mzee Mwinjuma Mwinyikambi wa Mwananyamala; Mzee John Rupia wa Mission Quarters; Sheikh Suleiman Takadir; Sheikh Haidar Mwinyimvua (Kisutu); Mzee Max Mbwana (Kariakoo); Zubeir Mwinshehe Mtemvu (Gerezani) pamoja na familia ya Mzee Azizi Ali (Mtoni) na ile ya Kleist Sykes (Gerezani), Dar es Salaam.

Ukoo wa Diwan Tambaza Zarara bin Mwinyi-Kitembe, ndio waliokuwa wenyeji wa maeneo ya katikati ya jiji wakati huo, wakihodhi eneo la ardhi yote ya Upanga, iliyosambaa kuanzia Daraja la Selender kuelekea Palm Beach Hotel, hadi Ikulu ya Magogoni kwa upande mmoja; na kwa upande mwengine maeneo yote kutoka Aga Khan Hospital, Ocean Road Hospital, Kivukoni Front (makaburi ya asili ya wanandugu wengine yako pale Wizara ya Utumishi, Magogoni) kwenda Mnara wa Saa pale Uhuru Street na vilivyomo ndani yake.

Habari zinasema kwamba, katika siku za mwanzo tu za kupambana na Mwingereza, wazee mashuhuri wa hapa Dar es Salaam walikutana na kuamua kumfanyia ‘zindiko’ na ‘tambiko’ la kijadi, pamoja na kumwombea dua maalumu kijana mdogo, Julius Nyerere, ili kumkinga na waovu na pia kuifanya nyota yake ing’are juu ya wote wenye nia mbaya naye; wakiwamo watawala wa Kiingereza, hasa Gavana Twinning.

Katika moja ya hotuba zake za kuaga aliyoitoa mnamo Novemba 5, 1985, Nyerere alilikumbumbuka tukio hilo na hapa chini anasimulia:

“…Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania…na mambo makubwa kama haya kama hayana baraka za wazee hayaendi… huwa magumu sana. Wanasema ngoma ya watoto haikeshi! Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani; tangu awali kabisa.

“Sasa siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (nyumbani kwake) akasema: ‘Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.”

Anahadithia Mwalimu na kuendelea:

“Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilipomalizika… zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee… za jadi, “…walikuwa na beberu la mbuzi… wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama beberu akachinjwa huku anaambiwa Twinning ‘umekwisha’… nikaambiwa tambuka… nikavuka lile shimo na baada ya hapo nikaambiwa …basi nenda zako kuanzia leo Twinning amekwisha!”

Mwalimu alimaliza kusimulia namna alivyofanyiwa dua na tambiko nyumbani kwa Mzee Tambaza, Upanga jijini.

(Picha ya Baraza la Wazee wa TANU kutoka kitabu cha Saadan Abdu Kandoro, ''Wito wa Uhuru'')

Kutawaliwa na Wazungu kuliwakera na kuwakasirisha watu wengi sana, kutokana na kule kudharauliwa ndani ya nchi yao wenyewe na watu wengine; hasa pale walipominywa katika kupatiwa huduma muhimu kama elimu bora, matibabu na mahala pazuri pa kuishi.

Pamoja na mambo mengi mengine yaliyokuwa mabaya kutokana na kutawaliwa, yamo pia na yale ya kuwekwa kwa madaraja katika utoaji huduma muhimu. Sisi, wana wa nchi hii, hatukuwa na shule za maana hata kidogo; watu wote sisi tukasomee shule moja tu (Mchikichini) mpaka darasa la nne; kwa nini hasa kama siyo dharau?

Nyumba zetu za kukaa zilikuwa za ovyo zilijengwa kwa miti na kukandikwa udongo na juu ni makuti, tena hapa hapa mjini Dar es Salaam, sikwambii vijijini; umeme uko kwenye taa za barabarani na siyo majumbani mwetu. Tukiwasha vibatari na taa za ‘chemli za Aladin’ kwa wenye uwezo kidogo kila siku.

Hospitali ziliishia kutoa kama huduma fulani ya mwanzo tu (First Aid). Haikuwapo hospitali ya Amana, Temeke, Mnazi Mmoja, Mwananyamala wala Mbagala. Tuliponea kibahatibahati tu kwa mizizi na majani ya porini. Ukiwa na homa kali basi chemsha mwarobaini; tumbo la kuendesha chemsha majani ya mpera au mpapai nani akupe ‘antibiotic wewe’.

Hospitali ya Muhimbili, yenye maabara na vipimo pamoja na madaktari bingwa, ilijengwa mwaka 1957 - ni juzi tu - kwa heshima ya Binti Mfalme Margareth II, aliyekuwa na ziara ya kutembelea makoloni ili aje kufungua rasmi hospitali hiyo. Kiwanja kilitolewa kwa hisani ya familia ya Mzee Jumbe Tambaza, ambapo miembe ile mikubwa inayoonekana mpaka leo pale ilikuwa shambani kwa kina Tambaza.

Kwa hivyo basi, ukiacha labda homa na vidonda, magonjwa mengine yote kwetu ilikuwa ni kifo tu. Umri mkubwa wa kuishi kwa wastani ulikuwa ni miaka 30.

Mzee Jumbe Tambaza, ambaye jina lake linanasibishwa na shule maarufu ya Sekondari ya Tambaza ya jijini - hana uhusiano wowote na shule hiyo - shule ilipewa jina lake kutokana na eneo iliyopo na kwa kuthamini mchango wake katika kupigania uhuru.

Kabla ya hapo, wakati huo wa ubaguzi wa rangi na matabaka, shule hiyo na ile ya msingi iliyo jirani nayo inayoitwa Muhimbili Primary, zilikuwa mahsusi kwa vijana wa Kihindi tu – hasa Ismailia - zikijulikana kama ‘Aga Khan Schools’ na kamwe hawakuwa wakisoma Waswahili na Kiswahili pale.

Shamba la Mzee Jumbe Tambaza pale Upanga, lilianzia mbele kidogo ilipo Shule ya Jangwani Wasichana (ambayo wakati wa ukoloni ilijengwa na serikali wasome watoto wa kike wa Kihindi tu, na ile Shule ya Azania ilikuwa kwa watoto wa Kihindi wa kiume), na kutambaa moja kwa moja mpaka lilipo Daraja la Selender pale baharini.

Eneo la Majengo ya Hospitali ya Muhimbili ilikuwa mali ya Jumbe Tambaza na marehemu nduguze (Msakara, Kudura na Mwamtoro Tambaza). Kutokana na kukosekana kwa hospitali ya maana ya rufaa kwa ajili ya Waafrika (kwa sababu ya ubaguzi tu), hayati Mzee Tambaza alitoa eneo lote lile la Muhimbili ijengwe hospitali ya Waafrika ili kupunguza vifo vilivyotokana na kukosa tiba sahihi.

Kijihospitali kidogo kwa ajili ya watu Weusi kilikuwapo pale jirani na Kituo cha Kati cha Polisi (Central Police Station) jijini, ikiitwa Sewa Haji Hospital, kwa heshima ya mfadhili aliyeijenga kusaidia jamii masikini. Sewa Haji alikuwa mkazi wa Bagamoyo mwenye asili ya Kibulushi kutoka Persia. Baada ya kujengwa hospitali ya Muhimbili, jengo moja katika yale matatu makuu, likaitwa Sewa Haji kama kumbukumbu yake.

Mjini Dar es Salaam wakati huo wa kibaguzibaguzi, serikali ya kikoloni haikutenga sehemu ya kuzikia watu weusi ambao walikuwa daraja la nne. Yale makaburi mashuhuri ya Kisutu, wakati huo yalikuwa ni ya watu wenye asili ya Kiarabu tu! Mwengine yoyote, ilibidi apelekwe kijijini kwao tu nje ya mji – Kunduchi, Mbweni, Msasani, Bagamoyo, Kisarawe, Maneromango na mikoani pia.

Sasa, ili kuondoa adha hiyo na usumbufu, Babu Mzee Tambaza, alitoa bure sehemu kubwa ya eneo lake itumike kwa watu wenye kuwa na shida ya kuzika ndugu zao jijini. Makaburi ya Tambaza siku hizo yalikuwa maarufu sana kuliko yalivyo yale ya Kisutu kwa sasa. Kamwe watu weusi hawakuwa wakizikwa Kisutu, kama ilivyo wakati huu.

Kufuatia hali hiyo, Jumbe Tambaza aliwashawishi binamu zake wawili, Mwinyimkuu Mshindo na Diwan Mwinyi Ndugumbi na wao wakatoa sehemu watu waweze kuzikana kule maeneo ya Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa na Ndugumbi, Magomeni Makuti; makaburi ambayo mpaka leo yameendelea kutumika kuzikia watu wote.

Neno, ''Tambaza,'' limetokana na neno ''kutambaa,'' au ''kusambaa,'' eneo kubwa. Diwan Tambaza na nduguze walikuwa watawala wa sehemu mbalimbali za hapa Mzizima siku za nyuma kabla Waarabu, Wajerumani wa Wangereza kufika hapa. Nduguze wengine ni Diwan Uweje; Diwan Uzasana; Diwan Mwenye-Kuuchimba na Diwan Mwinyi Ndugumbi.

Majina hayo walijipachika wenyewe kiushindani, kujigamba na kujitukuza kuliko ndugu wengine; hivyo kimafumbo mafumbo, huyu akajiita hivi na yule akamjibu mwenzake vile; mwengine akajiita naye atakavyo, kutokana na uhodari na tawala thabiti walizoziongoza.

Majina hayo pandikizi, hata hivyo yalikuwa na maana yake kila moja; kama vile mtu aseme mimi ‘Mobutu Sese Seku Kuku Mbenju wa Zabanga’, ikiwa na maana ya ushujaa kwa ‘Batu ba Kongo na fasi ya Zairwaa!’

Sasa Diwan Tambaza alipojiita vile, nduguye Diwan Uweje akamjibu na kumwuliza hata ukiwa umesambaa ndio uweje? Mwengine naye akasema, ‘’Ah! Uliza sana wewe uambiwe.’’ Hivyo yeye akajita Diwan Uzasana. Diwan Mwenye-Kuuchimba, yeye alikuwa akitawala maeneo ya Mtoni Kijichi na Mbagala yake, akasema, ‘’Nyie wote mnacheza tu, ‘mimi ndiye mwenye kuuchimba!’’ Kwa maana ya kwamba ndio kiboko ya wote. Ilimradi hali ikawa ndiyo hiyo; na hizo ndio zama zao, kwani husemwa kila zama na kitabu chake.

Mwandishi wa makala haya, jina langu naitwa Abdallah Mohammed Saleh Tambaza. Babu yangu Mzee Saleh bin Abdallah Tambaza wa Zarara, anakuwa binamu wa Mzee Jumbe Muhammad Tambaza, yaani baba zao walikuwa ndugu.

Shamba la babu yangu mimi pamoja na kaka yake Kidato Tambaza, linasambaa kuanzia Don Bosco, Makao Makuu ya Jeshi, Diamond Jubilee, Msikiti Maamur (kaburi la babu na babake babu yamo ndani ya Msikiti wa Maamur unapoingia mkono wa kulia pale ukutani), kuelekea kwenye Jamat la Wahindi mpaka Mahakamani kule Kisutu.

Miembe, minazi na mizambarau ile ya asili inayoonekana Upanga, ilipandwa na babu yangu kwa ajili ya urithi wa wajukuu zake, itakapofika zamu yao kumiliki maeneo yale.

Kwa bahati mbaya sana, Wazungu Waingereza, wakaona mandhari ile nzuri ya Upanga, hawakustahili watu weusi kuishi pale na wakawaamuru babu zangu wahame wawapishe Wahindi raia daraja pili. Hii ni baada ya wao Wazungu daraja la kwanza kuchukua eneo lote la Oysterbay (sasa Masaki). Maeneo yote hayo mawili yenye upepo mwanana ni karibu kabisa na bahari.

Kitendo cha kumhamisha mtu nyumbani kwake kwa namna ile, halafu kumpa fidia uitakayo wewe, ni dharau, dhuluma na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Wazee wale wastaarabu na wajanja hawakuwa na haja ya kuyauza maeneo yale, kwani ukiyaangalia utaona waliyapangilia ili vizazi na vizazi vya kwao viishi hapo.

Hii haihitaji mjadala wala maelezo marefu, lakini ni ushahidi tosha kwamba inaweza ikawa ndiyo sababu kubwa iliyomfanya Mzee Jumbe Tambaza awe mstari wa mbele kabisa katika kuwachukia watawala wa Kizungu na kumuunga mkono Nyerere kwa nguvu kubwa kama ile.

Mchango wa Mzee Jumbe Tambaza katika ukombozi wa nchi yetu haukutetereka hata kidogo, kwani hata pale rafiki yake mpenzi Sheikh Suleiman Takadir, alipotahadharisha watu kuwa makini na Nyerere maana ameonyesha kwamba siku za usoni angependelea zaidi jamaa zake, Mzee Jumbe hakumuunga mkono na akakubali Sheikh Takadiri atengwe na jamii kwa manufaa ya umoja wa kitaifa.

Jumbe Tambaza pia hakumuunga mkono Zubeir Mtemvu, kwenye suala la Kura Tatu ambalo ilibaki kidogo tu chama cha Tanu kingesambaratika na kuwa vipande viwili; lakini yeye alibaki na Nyerere wake mpaka dakika ya mwisho kule Tabora hadi kukasainiwa waraka wa ‘Uamuzi wa Busara’ ambao uliwapeleka TANU kwenye Uchaguzi wa Kura Tatu.

Katika picha ya pamoja iliyopigwa baada ya kutangazwa ushindi wa kuingia kwenye Kura Tatu kwa chama cha TANU, anayeonekana nyuma ya Mwalimu Nyerere pale Tabora ni Mzee Jumbe Tambaza. (Rejea kitabu Mohammed Said, ‘’Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes… uk 275).

Kutokana na uaminifu wao usiotetereka kwa chama chao, Mzee Jumbe Tambaza na mwenziwe Mzee Mwinjuma Mwinyikambi; wazee wale wawili wa Kimashomvi kutoka Mzizima, kwa muda mrefu wamekuwa wajumbe wa kudumu (permanent seats) kwenye Kamati Kuu ya TANU bila kupigiwa kura; achilia mbali ule uwepo wao kwenye Baraza la Wazee wa TANU.

Mnamo mwanzo wa miaka ya mwanzoni 1950, Mzee Tambaza alitumbukizwa tena kwenye mgogoro mkubwa na serikali pale ilipokuwa inajenga upya Barabara ya Umoja wa Mataifa kutokea Faya kuelekea Daraja la Selander, ilipoamuliwa kwamba sehemu ya eneo la makaburi iondoke kupisha ujenzi huo.

Hayati Mzee Tambaza, alifungua kesi mahakamani dhidi ya serikali, kesi ambayo inatajwa kama moja ya kesi nzito (landmark cases) sana kutokea hapa nchini na Afrika Mashariki iliyogusa imani ya Dini ya Kiislamu; kwamba je, ni halali au si halali kufukua makaburi ya watu waliokufa?

Kesi ya Makaburi, kama ilivyokuja kujulikana, iliunguruma kwa muda mrefu na kujaza kurasa za mbele za magazeti wakati huo, kutokana na mabishano makali ya hoja (cross examinations) mahakamani baina ya mawakili wa pande mbili hasimu.

Wakati serikali ikiwatumia masheikh wazawa wa hapa waliosema kwamba inakubalika kufukua makaburi, Jumbe Tambaza aliwatumia masheikh wakubwa kutoka Mombasa na Zanzibar, akiwemo aliyekuwa Kadhi wa Zanzibar Abdallah Saleh Farsy kupinga hoja hizo.

Kwa kishindo kikubwa, Mzee Tambaza alishinda kesi ile na ikabidi barabara ile ipindishwe pale kwenye mteremko wa kutokea Faya na kuyaacha makaburi na vilivyo ndani yake kama yalivyo. Haraka haraka, Hayati Mzee Tambaza akafanya maamuzi ya kujenga msikiti ambao haukuwapo mahala hapo kabla ya tukio hili, kuepusha kujirudia.

Huyo ndiye Mzee Jumbe Muhammad Tambaza, mwanaharakati wa kupigania uhuru wa taifa hili wa kupigiwa mfano, aliyetetea na kutoa vyake kusaidia wanyonge wenziwe katika jamii yetu katika kipindi cha manyanyaso ya utawala dhalimu wa Malkia wa Uingereza. Alimfanyia madua na matambiko ya jadi Mwalimu Nyerere ili nuru yake ing’are kama mwezi na jua!

Ewe Mola Mghufirie madhambi yake – Ameen.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-11-19T03:12:08Z 2021-11-19T03:12:08Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1503 <![CDATA[HISTORIA YA WALLAH BIN WALLAH: GURU WA KISWAHILI]]> ]]> false MwlMaeda]]> 2021-11-12T06:02:47Z 2021-11-12T06:07:13Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1479 <![CDATA[MAKIWA MAMA - KISWAHILI!]]> MAKIWA MAMA - KISWAHILI!
Mama yetu - Kiswahili anayetulea kwa hali na mali amepata pigo kwa kufa mmoja wa watoto wake - Profesa Pete Mhunzi.
Nilifahamiana na Profesa Pete Mhunzi, aliyelibadili kuwa la Kiswahili jina Peter Smith zaidi ya miaka 30 pale alipozuru Tanzania na kutembelea ofisi ya Waswahili - Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania (UKUTA), eneo la Anartoglo, Mnazimmoja, Dar es Salaam mwishoni mwa miaka ya 80.
Hiyo ilikuwa ni mara ya pili kumuona Mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyempenda Mama Kiswahili na kumtendea haki baada ya kukutana na John Mtembezi (Bwana Punda).
Profesa Pete Mhuzi alipenda sana kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Kiswahili na Taaluma zake na tulikuwa  na vikao maalum, tukiwa na gwiji la Kiswahili Marehemu Mzee Hamis Akida (Allaah Amrehemu), pale nyumbani kwa mwanadada (bila shaka sasa ni Bibi mwenye wajukuu) Irene (aliyekuwa mfanyakazi wa Kampuni ya TPH - Tanzania Publishing House, eneo la Kota za Misheni, Kariakoo, Dar es Salaam.
Anapofika Profesa Pete Mhuzi huwa ni hekaheka nguo kuchanika kwa waswahili waliokuwa na raghba ya kufanikisha ziara yake ya utalii wa Kiswahili.
Hapa namkumbuka Kaka Mswahili Mohamed Mwinyi (Bwana Jasho), Marehemu Ramadhani Stumai (Allaah Amrehemu), Marehemu Sihiyana Swalehe Mandevu (Mtenda Mema) na mradi wake wa alfabeti za Kiswahili zinazowakilisha vinavyopatikana Uswahilini kama upawa, mwiko, chungu na kadhalika.
Huchoki unapomsikiliza Mswahili Pete Mhunzi na juhudi zake za kumuenzi Mama Kiswahili.
Kuondoka kwake ni pigo kubwa kwa Mama yetu na ukoo mzima wa Mama Kiswahili.
Mama Kiswahili ana huzuni kubwa anapokumbuka maumivu ya tumbo la udele linalouma mno.
Makiwa Mama Kiswahili!
Makiwa watoto wa Mama Kiswahili!
Tunamuomba Mola wetu Ampokee.
Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, jina la  Bwana lihimidiwe.
Na:
Khamis Mataka
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-11-10T06:43:12Z 2021-11-10T06:43:12Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1427 <![CDATA[Wasifu wa Julius Nyerere]]> [Image: wasifu.jpg]
[Image: Julius_Nyerere_cropped.jpg]
Mwalimu Julius Nyerere
Muda wa Utawala
26 April 1964 – 5 November 1985
Waziri Mkuu
Rashidi Kawawa (1972–77)
Edward Sokoine (1977–80)
Cleopa Msuya (1980–83)
Edward Sokoine (1983–84)
Salim A. Salim (1984–85)
Makamu wa Rais
Abeid Karume (1964–72)
Aboud Jumbe (1972–84)
Ali Hassan Mwinyi (1984–85)
aliyemfuata
Rais wa Tanganyika
Muda wa Utawala
9 December 1962 – 25 April 1964
Waziri Mkuu
Waziri Mkuu wa Tanganyika
Muda wa Utawala
1 May 1961 – 22 January 1962
Monarch
mtangulizi
Ofisi iliundwa
aliyemfuata
Waziri Kiongozi wa Tanganyika
Muda wa Utawala
2 September 1960 – 1 May 1961
Monarch
tarehe ya kuzaliwa
13 Aprili 1922
tarehe ya kufa
14 Oktoba 1999 (umri 77)
mahali pa kuzikiwa
utaifa
chama
ndoa
Maria Nyerere
watoto
7
mhitimu wa
Chuo Kikuu cha Edinburgh
Fani yake
Mwalimu
dini
tovuti
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Butiama, mkoani Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza13 Aprili 1922 – LondonUingereza14 Oktoba 1999) alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania, na mara nyingi anatajwa kama “baba wa taifa”. Kwa hakika aliiathiri kuliko yeyote yule. Ndiye mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliyotangazwa hasa katika Azimio la Arusha.
Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimuKazi hiyo ndiyo iliyompatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la “Mwalimu.”
Kwanza aliongoza Tanganyika toka mwaka 1961 hadi 1964 kama waziri mkuu, halafu kama rais; baada ya muunganowake na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1985 kama rais.
Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi.
Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Hata hivyo aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.
Kwa ruhusa ya makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Jimbo Katoliki la Musoma linashughulikia kesi ya kumtangaza mwenye heri na hatimaye mtakatifu. Kwa sababu hiyo anaitwa pia “mtumishi wa Mungu“.
Maisha yake
Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musomamkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika).
Alikuwa mmojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki.
Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba yake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma.
Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusomea shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora.
Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa Mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.
Mapadri wakiona akili yake kubwa walimsaidia kusomea ualimu huko MakerereKampalaUganda kuanzia mwaka 1943hadi 1945.
Akiwa Makerere alianzisha tawi la Umoja wa Wanafunzi Watanganyika, pia alijihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).
Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary.
Mwaka 1949 alipata [[skolashipu[[ ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha EdinburghUskotiUfalme wa Muungano, akapata M.A. ya historia na uchumi (alikuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanganyika).
Aliporejea kutoka masomoni, alifundisha Historia, Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam.
Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.
Mwaka 1954 alibadilisha jina la chama cha TAA kwenda chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ambacho pia kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kikawa tayari chama cha siasa kinachoongoza nchini Tanganyika.
Uwezo wa Nyerere uliwashtua viongozi wa kikoloni akalazimika kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.
Alijiuzulu ualimu na kuzunguka nchi nzima ya Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta umojakatika kupigania uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship Council na Fourth Committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York.
Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu.
Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo, Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.
Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960.
Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9 Desemba 1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru; mwaka mmoja baadaye akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika.
Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.
[Image: Julius_Nyerere_1977.jpg]
Julius Nyerere akiwa mzee mnamo mwaka 1977.
Tarehe 5 Februari 1977 aliongoza chama cha TANU kuungana na chama tawala cha Zanzibar Afro Shirazi Party na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake wa kwanza.
Nyerere aliendelea kuongoza taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi rais wa pili, Ali Hassan Mwinyi.
Aliacha kuongoza Tanzania ikiwa ni mojawapo kati ya nchi maskini zaidi duniani, ingawa yenye huduma za elimu na afya zilizoenea kwa wananchi wengi.
Hata hivyo aliendelea kuongoza CCM hadi mwaka 1990 na kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.
Kwa mfano, inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamin W. Mkapa kama mgombea wa urais mwaka 1995, ambaye alichaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi.
Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima shamba lake. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.
Tarehe 14 Oktoba 1999 aliaga dunia katika hospitali ya St Thomas mjini London baada ya kupambana na kansa ya damu.
Mafanikio na kasoro
[Image: 250px-Muungano.JPG]
Nyerere akichanganya udongo wa Zanzibar na Tanganyika wakati wa muungano mwaka 1964.
Mafanikio[hariri | hariri chanzo]
Kati ya mafanikio makubwa ya Nyerere kuna: kujenga umoja wa taifa kati ya watu wa makabila na dini tofauti, na hivyo kudumisha amani ya muda mrefu tofauti na hali ya nchi jirani, iliyofanya Tanzania iitwe “kisiwa cha amani”.
Pia kustawisha utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa taifakatika vita dhidi ya mvamizi Idi Amin wa Uganda.
Kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za Kusini mwa Afrika kama vile: Zimbabwe (ZANU), Afrika Kusini(ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo).
Ukosoaji dhidi yake
[Image: 170px-Nyerere_2.jpg]
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Nyerere analaumiwa kwa siasa yake ya kiujamaa kuwa ilichelewesha maendeleo ya kiuchumi wa Tanzania. Siasa yake ya ujamaa ilishindikana kwa kiasi kikubwa baada ya mwaka 1976 kwa sababu mbalimbali za nje na za ndani ya nchi.
Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa ya kijamaa na kuwa hataweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa nyingine ambazo yeye hakuwa na imani nazo, Nyerere kwa hiari yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais kuanzia uchaguzi wa mwaka 1985 na kumwachia usukani Ali Hassan Mwinyi, aliyetawala kwa siasa ya uchumi wa soko huria.
Katika hali ya kukubali ukweli, Nyerere katika tafrija ya kumwaga alitamka juu ya siasa yake upande wa uchumi: “Nimefeli. Tukubali hivyo.”
Kosa lingine ambalo wengine wanaona Nyerere alilifanya ni kumhadaa aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mzee Abeid Amaan Karume kwa kuziunganisha Tanganyika na Zanzibar, na kuanza kupora mamlaka ya Zanzibar kidogokidogo. Kwa hivi sasa Wanzanzibari wengi wamechoka na Muungano huo, na wanataka uhuru wa nchi yao ili wapumue. Hata upande wa bara wananchi wengi wanalalamikia kutoweka kwa Tanganyika na serikali yake.
Pia kuna makundi ya Waislamu wanaomtuhumu kwa kuendesha kwa siri vita dhidi ya dini yao na kupendelea Wakristo katika utoaji wa elimu na madaraka,japo wasomi wengi kwa kipindi cha utawala wake walikuwa Wakristo.
[Image: 250px-Nyerere_bao_butiama.jpg]
Nyerere akicheza bao kwake Butiama, akitazamwa na mwandamizi wake katika urais Ali Hassan Mwini, mke wake Mama Maria, na kaka yake, chifu Burito.
Sifa zake
Pamoja na hayo, Nyerere bado anakumbukwa na Watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu. Pia ataendelea kukumbukwa na Waafrika barani kote hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.
Ni mmoja wa viongozi wachache waadilifu waliokwepa kujilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.
[Image: 220px-Nyerere_grave.jpg]
Kaburi la Nyerere kijijini Butiama.
Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama. Alipatwa na kansa ya damu (leukemia) akafariki Uingereza wakati wa kutibiwa katika mji wa London tarehe 14 Oktoba 1999.
Alizikwa mahali pa kuzaliwa kwake, kijiji cha Butiama.
Heshima na Tuzo
Nishani[hariri | hariri chanzo]
Nishani
Nchi
Mwaka
Ref
[Image: 80px-Ribbon_jose_marti.png]
Nishani ya José Marti
1975
[Image: 80px-MEX_Order_of_the_Aztec_Eagle_1Class_BAR.png]
Nishani ya Tai ya Kiazteki (Ukosi)
1975
Nishani ya Amílcar Cabral
1976
Nishani ya Eduardo Mondlane
1983
Nishani ya Agostinho Neto
1985
[Image: 80px-Order_of_the_Companions_of_O.R._Tam...bar%29.gif]
Nishani ya Masahaba wa O. R. Tambo (Dhahabu)
2004
Nishani ya Kifalme cha Munhumutapa
2005
[Image: 80px-Order_of_the_Pearl_of_Africa_%28Uga...on_bar.gif]
Nishani Ubora wa Lulu ya Afrika (Bwana tukufu)
2005
[Image: 80px-Order_of_Katonga_%28Uganda%29_-_ribbon_bar.png]
Nishani ya Katonga
2005
[Image: 80px-National_Liberation_Medal_%28Rwanda...on_bar.png]
Medali ya Ukombozi wa Kitaifa
2009
[Image: 80px-Campaign_Medal_Against_Genocide_%28...on_bar.png]
Medali ya Kampeni Dhidi ya Mauaji ya Kimbari
2009
[Image: 80px-Order_of_the_Most_Ancient_Welwitsch...on_bar.gif]
Nishani ya Kikale cha Welwitschia Mirabilis
2010
[Image: 80px-Order_of_Mwalimu_Julius_Kambarage_N...on_bar.png]
Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
2011
[Image: 80px-National_Order_of_the_Republic_%28B...on_bar.png]
Nishani ya Kitaifa cha Burundi
2012
[Image: 80px-Order_of_Jamaica.gif]
Nishani ya Jamaika
[url=https://sw.wikipedia.org/wiki/Julius_Nyerere#cite_note-10][10]
Tuzo
Kisha kufa
Machapisho ya mwl.Julius K. Nyerere
  • Freedom and Unity (Uhuru na Umoja): Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1952–1965 (Oxford University Press, 1967)
  • Freedom and Socialism (Uhuru na Ujamaa). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1965-1967 (1968)
    • Ndamo zimo: “The Arusha Declaration”; “Education for self-reliance”; “The varied paths to socialism”; “The purpose is man”; and “Socialism and development.”
  • Freedom & Development (Uhuru na Maendeleo). Mkusanyiko wa maandiko na hotuba, 1968-73 (Oxford University Press, 1974)
    • Ndani zimo mada za elimu kwa watu wazima; uhuru na maendeleo; kujitegemea; na miaka kumi ya uhuru.

  • Ujamaa – Essays on Socialism’ (1977)
  • Crusade for Liberation (1979)
  • Julius Kaisari, Tafsiri ya mchezo wa William Shakespeare unaoitwa Julius Caesar
  • Mabepari wa Venisi, Tafsiri ya mchezo mwingine wa William Shakespeare, The Merchant of Venice
  • Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Mathayo, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya Mathayo
  • Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Marko, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya Marko
  • Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Luka, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya Luka
  • Utenzi wa Enjili Kadiri ya Utungo wa Yohana, Tafsiri ya kishairi ya Injili ya Yohane
  • Utenzi wa Matendo ya Mitume, Tafsiri ya kishairi ya Matendo ya Mitume
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-11-09T09:52:43Z 2021-11-09T09:54:43Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1421 <![CDATA[WAZANZIBARI SITA MAARUFU]]>
[Image: Tippu.jpg]
Akiwa ametiwa ila sana na “magazeti ya wavumbuzi,” shujaa huyu jasiri wa kizanzibari ambaye jina lake hasa aliitwa Hamed bin Mohammed Marjebi alijulikana zaidi kama Davy Corocket au Francis Drake wa Afrika ya Mashariki kuliko mfano wa mwanafunzi mtundu ambaye tabia zake zilizompa umaarufu zaidi ni vile kuwa na ugomvi wa mara kwa mara na wavumbuzi wa kidini kutoka Ulaya wa wakati ule.Aliwatumikia Sultani wake kwa zaidi ya miaka 50, huku akibeba bendera na ustaarabu wao katika kila pembe ya mipaka yao.
 

Katika nyakati tafauti, alifanya kazi kama mvumbuzi, kiongozi, mfanyabiashara, askari mwanadiplomaisa, hakimu na gavana. Aliwatumikia jumla ya Sultani 8 wakati wa maisha yake baadaye akastaafu na kubakia nyumbani kwake katika Mji Mkongwe. Alifariki mwaka 1905 akiwa hakuwahi kuhalifu kazi zote alizopewa na watawala wake.





        SITI BINTI SADI.

[Image: Siti_Binti_Sadi.jpg]
Akiwa Nyota wa kwanza mkubwa wa kurikodi Taarab tokea miaka ya mwanzo ya santuri, Siti aliweza kuifanya Taarab kuwa maarufu kutokana na muziki wake mtamu na nyimbo za mapenzi zilizobeba ujumbe wa nguvu za kijamii na uchambuzi wakisiasa. Jambo moja lililoifanya kazi yake kuwa ya kiharakati ni vile kuimba kwake kwa kutumia lugha ya watu wa kawaida. Baada ya kuishi kwa muda mrefu katika mitaa ya Ng’ambo mjini Zanzibar, baadaye Siti alitembelea nchi mbali mbali za Afrika ya Mashariki akiimba na kuuza rekodi zake. Lililompa umaarufu zaidi miongoni mwa watu ilikuwa ni muziki mpya uliorekodiwa katika lugha yao wenyewe. Baada ya wasomo wanadai kuwa rekodi hizi za zamani zilichangia sana kuieneza lugha ya Kiswahili.
 

Akiwa mtoto wa watumwa, Siti alianza maisha kwa akali ya kitu, lakini kwa juhudi yake mwenyewe na sauti yake ya ajabu, aliweza kwanza kuimba taarabu ya kawaida, baadaye katika makasri na kumsifu Mfalme, na hata kuimba kwa Kiarabu. Baadaye aliigeuza midundo na mifumo ile ya kishairi na kuwa katika vinanda vya kawaida. Matokeo yake, Taarab ya Kiswahili ilimfanya awe Nyota na yeye kuifanya taarab iwe aina ya sanaa ambayo bado ni maarufu visiwani na isiyokosekana katika harusi na sherehe zote za Kizanzibari ..


BARGHASH BIN SAID

[Image: Barghash.jpg]
Huyu ni Mfalme wa Tatu wa Zanzibar, aliyetawala kuanzia mwaka 1870 mpaka 1888. Mama yake alikuwa mtumwa (aliyewachwa huru kwa kuzaliwa yeye), Sultani wengi wa Zanzibar walikuwa watoto wa wanawake watumwa. Baba yake, Seyyid Said bin Sultan, alikuwa mfalme mlowezi wa Sultan wa mwanzo wa Zanzibar. Barghash anasifika kwa ujenzi wa miundo mbinu ya Mji Mkongwe, ikiwemo maji ya bomba, vituo vya polisi, barabara, bustani, hospitali na majumba mengi ya kiutawala kama vile Beit el Ajaib.
 
Pengine alikuwa Sultan wa mwisho kuweka kipimo cha uhuru wa kweli dhidi ya udhibiti wa Wazungu.Alishauriana na “Washauri” kadhaa wa kizungu ambao walikuwa na ushawishi mkubwa, lakini alibaki kuwa mtu imara waliyepambana naye kumdhibiti alipambana na wanadiplomasia kutoka Uingereza, America, Ujerumani, Ufaransa na Ureno na mara kwa mara aliweza kuiangusha kitaalau nchi moja baada ya nyengine katika kinyang’anyiro cha kabla ya Ukoloni. Ni mtoto wake, Khalid, ambaye katika mchuano wa kurithi ufalme, alishindwa katika Vita vifupi kabisa katika histora.



SHEIKH ABDALLA SALEH FARSY

[Image: SHEIKH_ABDULLAH_SALEH_AL-FARSY2.jpg]
Alikuwa ni mfano wa karne ya Ishirini, katika safu ndefu ya Ulamaa wa Kiislam kutoka Zanzibar. Mchango wake maarufu katika uislamu ni kuchapisha QUR’AN TAKATIFU, yenye kurasa 807, ambayo ni tafsiri ya mwanzo kamili inayokubalika katika lugha ya Kiswahili Sheikh Abdulla Saleh Farsy vile vile alikuwa kabobea katika sarufi ya Kiarabu. Akiwa katika umri wa miaka ya ishirini, alikuwa anaandika mashairi kwa kiarabu, jambo linaashiria ukubwa wa kiwango cha elimu ambacho ulamaa wa Zanzibar walikuwa wanasambaza nyakati zile.
 

Sheikh Abdulla aliteuliwa kuwa Mkaguzi Mkuu wa shule za msingi za Unguja na Pemba mnamo mwaka 1949, Mkuu wa Shule ya Lugha ya Kiarabu mwaka 1957 na Kadhi Mkuu wa Zanzibar mwak 1960. Aliondoka visiwani baada ya Mapinduzi ya 1964 na akafia Omani Novemba 9 mwaka 1982.



TARIA TOPAN

[Image: Taria_Topan2.jpg]
Mfanya biashara, “mwana mfalme” wa kihafidhina, ambaye alijipatia utajiri wa mailioni kutokana na biashara ya karafuu na mamilioni mengine zaidi wakati alipokuwa anafanyakazi kama mkusanyaji Ushuru wa Forodha katika bandari ya Unguja na Pemba. Katika dhamana ile, alitakiwa kumlipa Sultani kiwango kikubwa kisichobadilika cha ada kila mwisho wa mwaka, kutokana na fursa aliyopata kwa kuteuliwa mkusanyaji mapato. Alipiga mahesabu na kuona kuwa angeliweza kukusanya pesa nyingi zaidi kuliko zile ambazo angelilipa, kama ikiwa biashara ingekwenda vyema. Na kwa wakati ule, biashara Zanzibar ilikuwa nzuri. Bei ya karafuu na viungo vyengine ilikuwa juu, mahitaji yalikuwa makubwa na bidhaa za viwandani ambayo vitu hivi zilifanyiwa biashara zilionyesha kushuka kupungua kila mwaka, kwa vile vitendea kazi na mbinu za kutendea kazi vilikuwa rahisi katika nchi za Magharibi.
 
Kwa utajiri wake huu, Topan aligeuka kuwa mfadhili Mkuu wa mji. Aliweka Wakfu na kujenga Kituo cha Afya kilichonakishiwa ambacho kipo Kaskazini kabisa mwa Bandari ya Mji Mkongwe. Vile vile alitoa “Wakf” vikataa vya ardhi vilivyokusudiwa kuwanufaisha wazee wasiojiweza.


NAHODHA “SMITH WA ZANZIBAR”

[Image: Capt_Zanzibar_Smith.JPG]
Yeye hakuwa Mzanzibari, lakini alikuwa rafiki wa mwanzo wa Kimarekani kuja Zanzibar. Alifanya biashara kwa mapana katika mwambao wa Afrika Mashariki kwenye miaka ya 1800. Akiwa mfanyabaishara kutoka Salem, Massachussets, aligundua kitu kilichomuunganisha na wafanyabiashara wa Zanzibar ambao Utajiri wao ulitokana na mfanya biashara mwerevu na wa kuaminika. Pamoja na manahodha wafanya biashara hawa, alifanyanao mapatano ya bei na kuweza kuwa marafiki haraka sana.
 
Wamarekani wao waliuza nguo za pamba (Mrekani) na kununua vipusa, viungo na sandarusi ambayo ilitumika kutengeneza vanishi kwenye viwanda vya New England. Kwa kufanya biashara na Marekani, kuliifanya Zanzibar kuwa kituo Kikuu cha Biashara katika maeneo haya.. Hata kufikia mwaka 1830, katika kipindi cha miezi 18, jumla ya vyombo 32 kutoka Amerika vilishatia nanga katika bandari ya Zanzibar.Mnamo mwaka 1836 kiwango cha biashara baina ya nchi mbili hizi ilihakikisha kuanzishwa Balozi za Amerika za kudumu katika Mji Mkongwe. William Smith alisafiri “kuzunguka pembe” ya Afrika mara nyingi katika safari ndefu za kutoka Amerika na visiwani kiasi cha kujulikana kama Smith wa Zanzibar katika pande zote za ikweta.

Chanzo &t&t&t&t&t]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-10-09T02:13:48Z 2021-10-09T02:14:36Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1302 <![CDATA["MEMORY OF DEPARTURE " ya ABDULRAZAK GURNAH]]> Nimemaliza kusoma Riwaya ya Kitawasifu ya  AbdulRazak Gurnah Mshindi wa Tuzo ya Nobel katika Fasihi 2021 inayoitwa  "Memory of Departure".

Wakati wengine wakiendelea na mijadala yao ya ima yeye ni Mtanzania au Mwingereza,mimi nikaona nijikite kutazama yaliyompa hedaya duniani kote.Makubwa na machache niliyoyabaini ni yafuatayo katika Falsafa yake:

1.Nimeishuhudia nguvu kubwa ya Utamaduni katika kujenga aina ya kizazi tutachokitaka ama Utamaduni unavyoweza kuifuta jamii moja au hata Taifa moja na likabaki historia tu katika ndimi za watu.

2.Nimeshuhudia kuanzia mwanzo mpaka mwisho nguvu kubwa ya mama.Kwa namna mama anavyoweza kumfinyanga mwana na akawa vile atakavyo.Mama anavyoweza kuilinda familia.Mama anavyoweza kuifariji familia.

3.Nimeshuhudia kuwa AbdulRazak kifalsafa ni Mmajumui wa Afrika na haya hana katika hilo.Wanaobishana wabishane lakini yeye anaililia Afrika.

4.Nimeishuhudia safari inayoakisi kama yakwake.Laiti angalipata "Scholarships" za Serikali ambazo zilikuwa zinatolewa kwa upendeleo kipindi hiko,katu asingaliondoka Zanzibar kama mkimbizi.Mitihani alifaulu vizuri,alikuwa na malengo ya kusoma nje kama alivyomshawishi Mwalimu wake wa Kiingereza,alifanya harakati za kupata "passport" n.k.

5.Nimeishuhudia namna uchungu nao unavyoweza kumsukuma mtu katika maendeleo.Kwasababu kwa maoni yangu ukiniuliza hasa kilichomkimbiza AbdulRazak Zanzibar nitakwambia ni matendo ya kiutamaduni,kwa maana tabia za watu binafsi wachache,hali ya maisha ya kifamilia (umasikini) kuliko hata hizo vuguvugu za kisiasa zinazotajwa kwamba labda ni hofu ya kuuawa ama vinginevyo.

6.Nimeona jitihada na athari ya kukitambulisha Kiswahili kwa maneno tele ambayo angalitaka angaliyapata tu katika lugha ya Kiingereza.Utaona humo maneno kama:
a)Voti mpeni Jongo.
b)Mbatata
c)Mzambarau.
d)Rizki.
e)Buibui.
f)Khitma.
g)Muadhin.n.k.

Kwa hakika,ninaweza kusema kuwa, kwa uandishi wake na kwa namna nilivyowahi kuwaona waandishi wengine wa Kiswahili,laiti ingalikuwa kazi zetu za Kiswahili za waandishi wetu nguli hapa Tanzania hutafsiriwa katika lugha za kimataifa kama Kiingereza, basi huenda tuzo zenyewe za Nobel zingelikuwa zinatiririkia hapa kwetu tu na hivi sasa ingelikuwa tumeshazizoea huku tukiwashuhudia wenzetu wa nchi jirani zinazotuzunguka wakizimezea mate.Wasalam!.

Mudhihiri Njonjolo.
Lindi.

+255 620 207 336]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-07-24T03:14:37Z 2021-07-24T03:17:02Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=624 <![CDATA[BURIANI PROFESA EUPHRASE KEZILAHABI]]> [Image: euphrase-kezilahabi.jpg]
Kumbe ni kweli kwamba kilichoandikwa kimeandikwa. Wakati ninamlilia mwandishi huyu ambaye amekuwa kioo changu katika fasihi, wakati ninatafuta niandike nini juu yake, nikagundua kwamba kumbe linifanya uhakiki wa kitabu chake cha Nagona.
Labda, nitoe siri ya Kitabu cha Nagona na Mzingile. Hivi ni vitabu viwili vya Profesa Kezilahabi, ambavyo si vitabu vyepesi kuvisoma. Mimi nilivisoma zaidi ya mara tatu bila kufanikiwa kuelewa kilichoandikwa. Nilipokutana na Profesa Mulokozi, nikalalamika, yeye akaniambia vinaeleweka tu. Nikajipa moyo, nikasema kama Profesa Mulokozi, anaamini vitabu hivi vinaeleweka, kwa nini mimi nisivielewe? Ndipo nikaendelea kuvisoma hadi nikafanikiwa kuvielewa na kugundua kwamba hivi ni vitabu viwili tofauti ingawa watu wengi wanafikiri ni kitabu kimoja. Hivyo ninamshukuru sana Profesa Mulokozi, kwa kunipatia moyo wa kuendelea kuvisoma vitabu hivi hadi nikafanikiwa kuvielewa.
Na sioni namna nyingine ya Kumlilia Profesa Kezilahabi, kama kurudia uhakiki wangu wa Nagona. Ninauweka hapa, nikimlilia na kusherehekea maisha yake ambayo yalikuwa kioo cha fasihi katika taifa letu la Tanzania, Afrika na dunia nzima.
Mungu, amlaze mahali pema peponi marehemu Profesa Euphrase Kezilahabi.
UHAKIKI WA KITABU: NAGONA
1. Rekodi za Kibibliografia.
Jina la kitabu kinachohahikiwa hapa ni Nagona, Kimeandikwa na Profesa Euphrase Kezilahabi. Mchapishaji wa kitabu hiki ni Dar es salaam University Press na amekipatia namba ifuatayo katika sekwensia ya vitabu duniani (ISBN): 9976 60 071 2. Kitabu kina kurasa 62 . Na anayekihakiki sasa hivi katika safu hii ni mimi Padri Privatus Karugendo.
II. Utangulizi
Nagona, ni hadithi ya kubuni. Imetungwa kwa mtindo wa uhalisiamazingaombwe. Ni mtindo wa kuandika unaofanana sana ule wa mwandishi Garcia Marquez wa Kolombia, Kyallo Wadi Watimila wa Kenya, Juan Rulfo wa Meksiko, Gunter Grass wa Ujerumani na Said Ahmed Mohamed wa Zanzibar. Waandishi hawa ambao kwa kiasi kikubwa wanatoka mataifa tofauti na lugha tofauti wanaunganishwa na uamuzi wao wa kuandika riwaya kwenye mtindo usiokuwa kawaida.
Kwa kuzingatia kazi hizi za fasihi, twaweza kusema kwamba
waandishi wote hawa wamo kwenye tapo moja kwani wametunga sanaa zao hizi, kusawiri uhalisia kama ulivyo hasa lakini kwa kujumuisha
vipengele vya kimazingaombwe .Masimulizi ya mambo ya kawaida na masimulizi ya matukio yasiyokuwa ya kawaida inakaribiana na Istilahi ya ‘uhalisiamazingaombwe’, ambayo mwanzoni ilitumika kuwahusu
wachoraji katika miaka ya 1920, inatumika kufasili kazi za bunilizi za kinathari za waandishi niliowataja hapo juu na Jorge Luis Borges wa Argentina. Waandishi hawa wanasukanisha uhalisia uliochongwa kwa njia maalum katika ruwaza inayobadilikabadilika daima, huku wakiwakilisha matukio ya kawaida na maelezo ya kina sambamba na vipengee vya kifantasia na kindoto, na kwa kutumia mambo yaliyotokana na visaasili na hekaya.
Nagona, ni riwaya ya kumfanya mtu kutafakari. Ujumbe mzima ni juu ya maisha! Lakini mwandishi anatufanya kutafakari juu ya maisha kwa njia ya uhalisiamazingaombwe. Kwa upande mmoja anatuelezea mambo ya kueleweka kwa hali ya kawaida, na kwa upande mwingine anatuingiza kwenye ndoto na mazingaombwe. Kuna mambo yasiyokuwa ya kawaida. Mfano mtu anakuwa kijana, lakini kuna hali fulani ikimwingia anakuwa mzee! Maana yake ni kwamba hekima na busara vinamfanya mtu kuwa mzee. Mwili unabaki ni wa kijana, lakini roho yake na akili vinakuwa vya mzee!
Nagona ni riwaya inayothibitisha upevu wa falsafa ya Kezilahabi kuhusu dhana ya maisha. Katika riwaya hii, maisha yanasawiriwa katika mtazamo wa dhihaka na kejeli. Ndiyo maana mwandishi anatega kitendawili kwamba waliobahatika kuishi, “…. Walikufa katika rumani. Walikufa wakicheka hali wameshikilia mbavu zao kwa vichomi. Baadhi walikanyagwakanyagwa, wakafa wakicheka. Wengine… walitumbukia katika kisima cha ndoto zao wakafa kwa uwingi wa ndoto walizokunywa…”
Nagona, ni hadithi inayotaka kufanana sana na ile nyingine ya Kezilahabi iitwayo Mzingile. Wachambuzi wengi wamekua wakichambua hadithi hizi kama moja. Lakini kuna tofauti kubwa. Nitaonyesha tofauti hizi kwa kuvichambua vitabu hivi viwili tofauti.
Nagona, ni kitu kinachotafutwa. Wamekitafuta wengi lakini wameshindwa kukipata. Mashujaa wengi wamejitahidi lakini wameshindwa. Nagona, anatafutwa kama mnyama, anawindwa! Na shujaa ni lazima awe na upinde na mshale. Hatimaye Nagona, anajitokeza kama msichana mzuri. Lakini shujaa anayefanikiwa kumpata anashindwa kufanya naye mapenzi. Hatimaye Nagona, anaelekea kuwa ni Hekima, busara, mkombozi au ni Mungu mwenyewe?
“Nagona ni mwanga. Ni kama jua lililopatwa na mwezi. Ukitazama kwa muda mrefu unaweza ukapofuka na usione chochote wakati wote wa uhai wako. Lakini ajabu ni kwamba unavutwa kumtazama bila kinga licha ya hatari zake. Ukishamwona hamu ya kuendelea kumwona haishi. Akitoweka utaendelea kumsaka kila mahali bila woga”
“Nikimwona nitamtambuaje?”
“ Penye mwanga hukosi kupaona. Alipo, uwongo umejitenga, ni yeye peke yake aliyepo pale. Utajikuta umevutwa kuelekea kwake. Lakini hataruhusu umshike awe wako peke yako, maana ni wa kila mtu. Kila mtu anamtambua na ndiyo maana anavuta na anaambaa, sisi tunavutika na tunamwambaa. Hakuna awezaye kuepukana na mvuto wake” (Uk 45).
Mwokozi wa pili ndiye atakaye uokoa ulimwengu. Mwokozi huyu atakuja wakati wa Ungamo kuu au wakati wa Ngoma kuu. Kizee mwenye fimbo, ambaye kwa namna nyingine ndiye kama Mungu mwenyewe, anasababisha vurugu katika ngoma na inatokea maangamizi makubwa. Wanaopona ni pamoja na mhusika mkuu Anayepewa kazi ya kumleta mtoto Nagona, anayezaliwa siku hiyo ya Ngoma Kuu na huyu ndiye analeta ukombozi wa pili!
Kabla ya kufanya uhakiki wa kitabu hiki ningependa kuelezea mazingira yanayokizunguka.
III. Mazingira yanayokizunguka kitabu
Profesa Euphrase Kezilahabi, amezaliwa wakati wa ukoloni. Amesoma shule ya msingi na sekondari wakati wa ukoloni. Amepata elimu ya juu wakati wa uhuru, amekulia kwenye vuguvugu la Azimio la Arusha. Ni wakati ambapo taifa lilitegemea zaidi fikra na uongozi wa Mwalimu. Mawazo mbadala ilionekana kama msaliti. Lakini pia ni wakati ambapo kila maandishi lalichujwa ili kulinda maadili. Kitabu kama Rosa mistika cha Kezilahabi, ambacho kilizungumzia mahusiano ya kimapenzi, kilipigwa marufuku; na labda huu ukawa mwanzo wa Kezilahabi kufikiria kuandika kwa mafumbo. Mpaka mtu agundue kwamba Nagona, inaongelea mapenzi ni hadi karne nyingine. Kezilahabi pia ameshuhudia Azimio la Arusha likitupwa nyuma na kuanzishwa kitu kingine ambacho hakijulikani vizuri.
Nagona, ni hadithi ambayo imetungwa wakati huu wa kuyumba kwa nchi yetu. Mwelekeo ukiwa haujulikani vizuri tunakwenda wapi? Hivyo mtu anaposoma Nagona ambayo iko kwenye mtindo wa uhalisiamazingaombwe, ni lazima kuweka maanani mwandishi anaandika akiwa katika mazingira gani.
Ni wakati ambapo watu walianza kutupilia mbali utamaduni wa Tanzania na kukumbatia utamaduni wa magharibi. Ni wakati ambapo fikra haikutawala tena, fedha ilianza kuzungumza. Rushwa iliota mizizi hadi kwenye chaguzi na watu kuuza huru wao. Ni wakati ambapo wasomi na wenye kutaka kufikiri walionekana kama vichaa.
“Basi hayo ndiyo yalikuwa maktaba ya taifa. Walikata shauri kutupa vitabu vyao vyote huko. Vimeoza na miti imeota juu yake. Waliopata kupita humo wanasema kuna mizungu. Waandishi wanalilia kusomwa wasife” (Uk 5)
Pia tukumbuke kwamba Kezilahabi, amesoma kwenye shule za seminari. Yeye ni Mkatoliki ambaye anaona wazi hasara kubwa waliyoipata wale wote walioziacha dini zao za jadi na kuingia dini mpya za Ukristu na Uislamu. Hili analiongea kwa uangalifu mkubwa na kwa mafumbo ya hapa na pale.:
“Mimi nahubiri habari za Kristo. Wewe unahubiri upagani”
“Wewe ni mcheza ngoma ya twiga nje ya duara. Twiga hawezi kuhimili ngoma yenye vurumai, vurugu, na ghasia katika gharika la hisia na fikra” (Uk 10).
Hapa mwandishi anatuchorea mabishano kati ya babu mwenye imani yake ya jadi na Padri ambaye alikuwa anahubiri neno la Mungu. Na ukweli kwamba imani hizi za kigeni zilileteleza watu waanze kuishi bila kufikri, bila kuhoji: “ Katika mkono mmoja alikuwa amepakatishwa Biblia Takatifu na mwingine Korani Tukufu. Mdomo wake uliwa umefungwa kwa kitambaa cheupe na juu ya kitambaa hiki kwenye mdomo palionekana maandishi yaliyosema “Kimya ni hekima” (Uk 3).
“Watu wa mji huu hawasemi. Anayezungumza katika mji huu ni mmi, na labda mzee mmoja karibu na mto. Sisi sote wawili tunaitwa vichaa katika mji huu. Wanatuona wendawazimu. Wakituona tu wanakimbia” (Uk 5).
Kwa kifupi ni kwamba Mwandishi, aliandika hadithi hii fupi, lakini yenye fikra nzito akiwa kwenye mazingira ya vita, mazingira ya mapambano: Ni kupambana na ukoloni, ukoloni mambo leo, utandawazi, siasa uchwara, dini za kigeni, hadi mtu anapopata Uhuru wa kweli. Nagona ni kujitambua, kujikubali na kuendeleza kizazi. Ndo maana mwisho wa hadithi yake mtoto anazaliwa.
Euphrase Kezilahabi alizaliwa 13 Aprili 1944 huko Namagondo kisiwani Ukerewe kilichopo ndani ya Ziwa Viktoria. Babake Vincent Tilibuzya alikuwa msimamizi wa kijiji na Euphrase alikuwa na ndugu 10 yaani wavulana 5 na wasichana 5. Alisoma shule ya msingi ya Nakasayenge halafu tangu 1957 Seminari ya Kikatoliki ya Nyegezi aliyomaliza mwaka 1966.
1967 alijiandikisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akasoma ualimu na fasihi hadi digrii ya B.A. katika mwaka 1970. Mwaka uleule 1970 akawa mwalimu wa shule ya sekondari Mzumbe (Morogoro) halafu kwenye shule ya sekondari ya Mkwawa (Iringa).
1971 alirudi chuoni Dar es Salaam akawa mhadhiri msaidizi wa chuo alipoandika pia tasinifu ya M.A. kuhusu riwaya za Shaaban Robert, tangu 1974 mhadhiri kamili na 1978 mhadhiri mwandamizi. Akaendelea na masomo ya Ph.D. huko Marekani kwenye Chuo Kikuu cha Wisconsin Madison alipotoa tasinifu yake mwaka 1985 kuhusu “African Philosophy and the Problem of Literary Interpretation”. Sasa ni profesa wa lugha za Kiafrika kwenye Chuo Kikuu cha Botswana.
Euphrase Kezilahabi ni mwandishi ambaye ametoa mchango mkubwa katika fasihi ya Kiswahili. Yeye ndiye anatambuliwa kama mwanzilishi wa ushairi huru (free verse) katika Kiswahili alipoandika Kichomi na baadaye Karibu Ndani.
Kezilahabi anajulikana kwa ushujaa wake wa kujaribu mitindo mipya katika uandishi wake na ukisoma vitabu vyake kama Rosa Mistika, Dunia Uwanja wa Fujo, Kichwamaji, Gamba la Nyoka na Kaptula la Marx utakutana na chembechembe za upya katika nyanja mbalimbali na hasa matumizi ya falsafa.
Baadhi ya maandiko yake ni:
Riwaya:Rosa Mistika (1971),Kichwamaji (1974), Dunia Uwanja wa Fujo (1975),Gamba la Nyoka (1979),Nagona (1987/1990),Mzingile (1991)
Mashairi: Kichomi (1974),Karibu Ndani (1988) Dhifa (hakijatolewa bado).
Tamthiliya: Kaptula la Marx (1978/1999)
Baada ya maelezo haya sasa tuone kitabu chenyewe kwa muhtasari.
IV. Muhtasari wa Kitabu
Kijana shujaa, akiambatana na mashujaa wengine ambao ni Nabii, Mtume, Mfuasi na Mtenzi, wanasafiri kumtafuta Nagona. Hawa walijulikana kama askari wa mwanga. Huyu Nagona, anatafutwa kama paa! Anawindwa. Safari ya kumfikia ni ngumu sana. Mwandishi, ndipo anapoonyesha ukomavu wa uandishi wake. Safari hii ya kumsaka Paa, inakuwa ya karne – ingawa kwa kutafakari kwa kina ni safari ya mtu ndani mwa nafsi yake. Ni safari ya kutafuta ukweli!
Njiani mashujaa wa mwanga wanakumbana na vikwazo vingi. Watu wengi walijaribu kumtafuta Paa huyu bila ya mafanikio. Na wengi walishindwa masharti na kukatwa vichwa. Mashujaa wa mwanga wanaonyeshwa vichwa vilivyokatwa. Pamoja na vitisho vyote, bado walitaka kuendelea kumsaka Paa hadi wampate!
Babu alitoa ushuhuda jinsi ilivyo vigumu kumkamata Nagona: “ Ahaa! Nagona! Kwa muda wote wa uhai wangu alinipiga chenga. Mara nyingi nilimwona kwa mbali. Mara chache sana nilikaribiana naye. Sikupata nafasi ya kumweka mikononi mwangu nilipokuwa karibu naye. Daima alirudi kinyumenyume, nami niliendelea kumfuata nikiongozwa na nguvu fulani. Nilipokuwa mvivu wa kufikiri alinipotea kabisa lakini alitokea tena nilipoanza kufikiri kwa makini. Nawaonea wivu waliopata kumweka mikononi mwao ingawa daima aliwaponyoka. Yote haya shauri ya maluweluwe. Hatuoni tena kilichowekwa wazi. Tumekuwa vichaa kwa kutafuta kilicho wazi na kwa kujaribu kufichua kilicho wazi. Wewe mjukuu wangu nyota yako nzuri. Huenda ukabahatika kumwona na kumshika mikononi mwako” (Uk 44).
Na kweli mashujaa wa mwanga walifanikiwa kuvishinda vikwazo vyote na kumfikia Paa huyo ambaye alikutwa ni msichana mzuri kupindukia. Hata hivyo aliwaponyoka! Ni nani awezaye kumkamata? Babu anaendelea kuelezea kwamba hata ukimkamata, Nagona ni wa watu wote!
Safari ya kumsaka Nagona, inatufunulia mengi: “ Wanaishi kwa matumaini. Wanakula matumaini yao wenyewe ambayo wanasema huzaliana siku hadi siku’
“Hayo matumaini hutoka wapi?”
“Ndotoni”
“Hizo ndoto wanazitoa wapi?”
“Katika kisima cha ndoto ambacho wanasema hakikauki kamwe”
“Hicho kisima kiko wapi?”
“Yeyote afikirie hawezi kukiona”
“Kwa nini?”
“Wanasema fikra hufumba mboni za urazini”
“Hao watu wamekufa au wazima?”
“Kama kufa ni kutokuwepo basi wazima. Zaidi ya hayo maisha tuyajuayo yaweza kuwa ndoto za mtu mmoja mwenye vichwa vingi. Hakuna jibu rahisi” (Uk 6).
Katika safari hii ya kumsaka Nagona, tunafunuliwa pia kizazi kisichopenda kusoma. “ Watu wa mjini waliitupa miswada yangu yote ya kitanzia wakanibakizia komedi. Walipoanza kukaa kimya na kuchekacheka, hata hizo komedi wakazitupa msituni. Walisema kucheka ni ushindi…” (Uk 7).
Safari ya kumsaka Nagona, inapotoka ndotoni, tunafunuliwa viwanda vyetu vingi ambavyo sasa hivi vipo tu havifanyi kazi. Hata hivyo vingine bado vina meneja na walinzi. Meneja wa viwanda visivyofanya kazi bado wanaamini wako kazini na wao ni muhimu sana kwenye viwanda hivyo;
“ Wataalamu gani! Mimi ndiye niliyesimamia mradi wa kujenga kiwanda hiki tangu jiwe la kwanza la msingi hadi mwisho wake. Wao wanajua nini! Na kwa nini Serikali isiniulize mimi matatizo ya kiwanda hiki! Mapendekezo mangapi nimekwisha andika! Yote yalitupwa kapuni! Waambie waondoke”(Uk 22).
Viwanda vimekufa lakini bado vinalindwa. Wanaovilinda wanajua wafanyacho. Wanapoulizwa wanalinda nini wakati viwanda vimekufa, wanajibu: “ Tunalinda maiti asifunuliwe”… “Sisi ni waosha!”… “ Aibu ya maiti aijuaye mwosha”.(Uk22). Ni sawa na kusema la kuvunda lina ubani? Viwanda vimekufa, bado kuna watu wanalinda ili aibu isitoke nje? Hapo kuna maendeleo?
Lakini pia katika safari ya kumsaka Nagona, tunafunuliwa kwamba: “Katika bonde hili kuna imani kuwa ajali ni mwanzo tu wa kitu au wazo jipya. Bila ajali hakuna ambacho kingekuwako. Kuzaliwa kwenu ndiyo ajali kubwa iliyopata kutokea katika uhai wenu. Wakati huo hamkuwa na utashi..” (Uk 23).
Tunaambiwa pia kwamba: “ Hakuna maumivu katika kufa. Kuna masikitiko na huzuni. Masikitiko kwa mali na watu uwaachao nyuma na kwa yale ambayo hukupata nafasi ya kuyatekeleza. Lakini mimi nimeacha mali gani nyuma! Hakuna. Labda maneno yangu. Nimeacha nani nyuma ! Hakuna isipokuwa wewe, baba yako na mama yako. Ninyi nyote mlinielewa vyema na mko imara. Hamtanisaliti. Niliyotaka kutekeleza nimeyatekeleza. Muda nilikuwa nao wa kutosha” (Uk 42).
Babu, ambaye anaonekana kuwa na hekima kubwa katika simulizi hii ya Nagona, anaonyesha wazi wazi kwamba yeye haogopi kufa na wala hana wasi wasi wowote:
Anasema: “Anayeogopa ni yule aliye na tamaa ya kuishi maisha ambayo hajayaishi”
“Maisha ambayo hajayaishi?”
“ Maisha baada ya kifo. Mimi sina tamaa hiyo. Maisha kitu cha ajabu. Nyuma hakuna nyayo na mbele hakuna nyayo, nyayo ziko katikati tu. Kama hujui ulikotoka na hukumbuki, ya nini kutaka kujua uendako!”.
Ndo maana ngoma ni lazima ichezwe katikati mwa duara. Ukicheza nje ya dura wewe uko nje, wewe uko nje maisha. Katikati ni leo, ni maisha ya hapa hapa na wala si ya jana au ya kesho. Ni maisha ya leo ni maisha ya Nagona!
Hadithi inafikia mwisho kwa maangamizi makubwa. Hilo ungamo kuu au ngoma kuu, inaleta vurumai. Watu nakanyagwa na kufa. Hata hivyo kwenye vurumai na vifo hivyo anazaliwa mtoto, tena binti wa kuendeleza kizazi: Binti huyu anapewa jina la Nagona! Inakuwa ni simulizi ya matumaini mapya!
V. TATHIMINI YA KITABU.
Nianze kwa kumpongeza Profesa Kezilahabi, kwa kazi hii nzuri sana aliyoiandika. Kusema kweli hadithi hii inaburudisha na kufikirisha. Ingawa si hadithi ya kueleweka upesi kama Rosa Mistika, bado inaburudisha kwa mtu anayesoma kwa kutafakari.
Ingawa mtindo alioutumia wa uhalisiamazingaombwe, unaonekana kuwa mpya na wengi wanafikiri alijifunza mtindo huu alipokwenda kusoma Amerika, maana ni mtindo unaotumika Amerika ya kusini, bado ukweli unabaki kwamba mtindo huu wa simulizi ni wa Kiafrika. Bibi zetu na babu zetu walikuwa wakitusimulia hadithi za mazimwi na uhalisiamazingaobwe. Simulizi hizi zilitumika kama njia moja ya kujenga maadili, kujiamini na ushujaa.
Ukerewe kama ilivyo kwa Mwanza na Kagera, kuna hadithi za Mungu wa Maji “Mugasha”, Mungu wa misitu “Ilungu”, Mungu wa kilimo na mavuno “Nyakalembe”. Hadithi za miungu hawa zinaelezwa kwa mtindo wa uhalisiamazingaombwe. Hivyo Nagona, si kwamba ni kitu kipya. Labda ni kwa vile tunasahau haraka. Mwandishi anaonyesha tabia hii ya kusahau katika simulizi yake.
Hata hivyo ni ukweli kwamba Waafrika tunapenda miujiza, tunapenda miujiza hadi kuamini kwamba kila kitu kinaweza kutokea kwa miujiza. Tunachoma moto na kuharibu mazingira na bado tunategemea mvua inyeshe! Isiponyesha tunakwenda kwenye nyumba za ibada kuomba mvua inyeshe. Ipo mifano mingi inayoonyesha jinsi Waafrika tunavyopenda miujiza. Hivyo ujumbe mzito kama wa Profesa Kezilahabi, ukipitia kwenye uhalisiamazingaombwe, unaeleweka haraka.
Vitabu vya Nagona na Mzingile vilileta kizaazaa katika Fasihi ya Kiswahili kwa wasomaji pamoja na wahakiki kwani si rahisi kuelewa hasa anazungumzia nini. Inabidi kwanza uwe na uelewa mpana wa matapo makuu ya falsafa za Kimagharibi (mf. Existentialism, Epistemology, Metaphysics, Psychoanalysis, Aesthetics na Phenomenology) na pia falsafa za Kiafrika kama unataka kuelewa cho chote kinazungumziwa katika vitabu hivi.
Kutokana na ugumu wa kueleweka wa vitabu hivi, wahakiki wengi wamemlaumu Kezilahabi kwamba pengine ameuleta mtindo huu wa uandishi katika fasihi ya Kiswahili wakati riwaya ya Kiswahili bado haijakomaa sawasawa. Wahakiki wengine wamefikia hata kumhukumu kwamba pengine ameiua riwaya ya Kiswahili. Ukweli ni kwamba Profesa Kezilahabi, anazifufua riwaya za Kiswahili. Ukoloni, ulifuta simulizi zetu na zilipachikwa majina ua ushenzi na upagani:
“Wewe ndiye kiongozi wa kundi hili la wapagani?”
Babu alimtazama kwa jicho kali. Wazee walimwangalia babu kwa makini wakisubiri neno litakalomtoka.
“Mbona unacheza ngoma yako nje ya duara? Bila njuga hupendezi”.
Padri alimtazama kwa njia iliyoonyesha kutoelewa vizuri. “Nimekuja kukuona wewe”
“Kuhusu?”
“Nimesikia habari za mazungumzo yako. Yanapingana na yangu”
“Mimi si mhubiri. Na mazungumzo yako sijayasikia”
“Na hawa hapa wanafanya nini?”
“Ni askari wa mwanga. Wawindaji”
“Mimi nahubiri habari za Kristo. Wewe unahubiri upagani”
“Wewe ni mcheza ngoma ya twiga nje ya duara. Twiga hawezi kuhimili ngoma yenye vurumai, vurugu, na ghasia katika gharika la hisia na fikra” (Uk 10).
Kutokana na kutoelewa simulizi za Kezilahabi, wahakiki wanafikiri Nagona Na Mzingile ni kitabu kimoja? Ni wazi kuna namna ya kufanana, lakini hivi ni vitabu viwili tofauti. Vinaongelea maisha na umuhimu wa Waafrika kupambana kwa nguvu zote na utandawazi wa kimagharibi unaokuja na kutuvamia. Wale wanaoupinga utandawazi huu, wanaonekana kama vichaa.
Profesa Kezilahabi, amefanikiwa katika Nagona, kuonyesha jinsi maisha ya Waafrika yanavyozunguka ardhi, mito, misitu, wanyama. Haya anayaonyesha vizuri na kwa mtindo wa kutomchosha msomaji. Ameonyesha umuhimu wa Wazee, vijana na wanawake katika jamii zetu.
Lakini hasa ni kuonyesha umuhimu wa Mkombozi wa pili. Anamalizia simulizi lake kwa matumaini mapya. Utafikiri ukombozi huu ni muhimu leo hii; maana kama kuna kipindi cha historia ya taifa letu kilichohitaji Mkombozi wa pili na maisha mapya ni wakati huu tuliomo sasa hivi. Sote tunamhitaji Nagona!
VI. HITIMISHO.
Ni wazi ningependa kuwashauri wasomaji wangu kukinunua kitabu hiki na kukisoma. Pamoja na ukweli kwamba si kitabu chepesi kueleweka kwa uvumilivu mtu anaweza kukisoma na kuelewa. Hata hivyo maisha nayo hayaeleweki haraka; tunapanda milima na mabonde katika maisha na wakati mwingine hatufiki sehemu ya kupumzika na kustarehe.
Na,
Padri Privatus Karugendo.
+255 754 633122
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-07-20T02:12:22Z 2021-07-20T03:15:00Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=594 <![CDATA[MALIKA "MWANAKUPONA ALIYEFANIKIWA KUKATA RUFAA YA KIFO]]>

.jpg   5005b360-ac54-44b9-962d-ed4c7b0dbf0d.jpg (Size: 22.9 KB / Downloads: 0)

Na. 
HEMED KIVUYO

"Wangu muhibaka sikuhizi sikuoni,tangu kuondoka moyo upo msibani,sijui hakika ilokuudhi Ni Nini,naomba tamka unijuze kwa yakini ,Mimi nakutaka Wewee,nakupenda weweee"

Ni baadhi ya mashairi yaliyopo katika wimbo wa Malika yaani Taarab. Malika Ni Nani,yupo wapi ,na kwanini kafanikiwa kukata rufaa ya kifo?

AISHA ABDULY MAARUFU KWAJINA JINA LA MALIKA . Ni mzaliwa wa Kismayuu Somalia .

Kumuelezea bi Malika yahitaji wigo mpana mno,lakini nitakufafanulieni kwa ufupi.

Malika Ni Mwimbaji hodari wa Taarab zenye kulalamikia Mapenzi ,na hata kushajihisha Mapenzi,Nk.

Nakosa lugha ya kumwelezea Mwanakupona huyu ambaye haishi kunitoa matozi kila nisikiapo sauti yake kupitia tungo zake ,Hana kifani.

Siwezi kuelezea sauti yake kupitia maandishi yangu,labda nikusihi usikize tungo zake.

Malika ameimba nyimbo nyingi mno za Taarab,baadhi ya ametunga na kuimba na baadhi ametungiwa na kuimba yeye mwenyewe .

Katika upeo wa mato yangu,bi Malika Ni Mwanamke mwenye sauti yenye kutibu maradhi yangu Mengi mno . "Napohisi uchovu sauti ya Malika imekuwa Nguvu kwangu,napodhihakiwa ,sauti ya Malika imekuwa tiba kwangu" Mwenyezimungu azidi kumpa Umri .

Baadhi ya Tungo zake maarufu Ni "WAPEWAPE VIDONGE VYAO" ZABIBU,YALAITI,NDUGU WAFAZA,NINGEULALIA MTO,STAKI STAKI,MWANAWAJINI
MR.MAHMOUD NK.

Hali ya usalama Nchini Somalia imekuwa hamkani kwa muda mrefu,Malika aliiacha Nchi yake kutokana na machafuko hayo na kuweka Kambi kwa muda mfupi Tanzania Kisha Mambasa Nchini Kenya .

Wakati Aliitwa Aisha Abduly jina lake halisi

Alipokelewa Kenya kwa shangwe na kuishi vyema,kutokana na Sauti yake si tu yakumtoa nyoka pangoni Bali hata Mamba MTO rufiji,Wakenya walimpa jina la Malika .

Na wakati anakaribia kuondoka Kenya akawaimbia " Metembea Nchi nyingi,lakini Kenya kufika kwangu ndiyo namba wani,siwati kuwakumbuka nyumbani kwetu kirudi" tawaombea wadudi"

Alitunga pia wimbo kuomba Vita simame Nchini Somalia na warejee Kama zamani.

"Ni Nchi yangu Somalia,nilozaliwa nikalelewa na maisha nikayajua,leo yamekuwa hayaa mola atatunusuru,Leo yamejiri haya"

Kama ilivyokuwa kwa Siti Bint Saad,hakukosa wasompenda. Baadhi walimwita majina mabaya Malika nakumtaka arejee kwao..

Akawajibu kwa Wimbo ,Wimbo uliitwa staki staki na baadhi ya mashairi yalisema hivi

"Staki staki stakiii japo kuwa sinachangu Mimi kunyanyaswa staaakii..staki stakii stakii japo Ni mnyonge Mimi kuonewa staakii"

Wimbo huu ulipendwa hata na maadui zake kwakua mwiba wa samaki humchoma hata mnunuzi.

Wimbo Zabibu pia ulikuwa maarufu Sana,na wengine hudhani uliimbwa na Bi Kidude laa hasha!

"Hiyo yako si Zabibu Ni tunda lililo na sumu,mempa mwenye imani roho ilomtulia,hiyo siyo kazi yangu Mimi kwenda uchawini ninaye mpenzi wangu wewe nikuroge Nini , huyu tenaa!!!!

Kuna wimbo uliitwa halohalo. Kulitokea kisa kimoja  kwa Alhanisa Malika kupigiwa simu na mtu asiyemfahamu,akimsihi mtu huyu kujitambulisha lakini wapiii!

Malika akatunga wimbo "haloo haloo jina lake alifitaa hajulikani Ni nanii haloo haloo".

NINGEULALIA MTO.Wimbo huu mpaka hii leo umekuwa miongoni mwa nyimbo zenye kunitibu "kwa wakubwa na watoto wakubwa pambano mwao,kuna Mengi ya uzito,yangu hayawi nishanii..NINGEULALIA mtooo ningeulaliaa mto".

Jina la Malika lilikuwa maarufu mno Afrika na Ulaya,kila akitaka kurejea Somalia Basi Hali ya machafuko ilipamba Moto.

Aliendelea kuishi Kenya akiendelea kuimba Taarab ambayo nakiri huyu Mwanakupona wa ajabu ameletwa na Allah kwa kazi hiyo.

Alikutana na misukosuko  kiasi Cha kutunga wimbo na kuuita misukosuko,hakuacha kitu Mwanakupona huyu .

Alitumia fasihi kuelezea umri wa kuoa na kuolewa,rejea wimbo "shebe nampenda shebe nampenda ntakula nishibe.

Malika ambaye alikoma kurejea Somalia kwasababu za dhahiri aliendelea kuomba Dunia iiisaidie Somalia irudi Kama zamani na warejee nyumbani.

Mwanamama huyu amekuwa maarufu Duniani,na miaka mingi iliyopita alipata makazi ya Kudumu Michigan Marekani anapoishi mpaka sasa.

Manju wa Mazuki Masou Masoud takribani miaka5 iliyopita alifanya naye mahojiano kupitia Radio Tanzania Sasa TBC.

Niliposkia mahojiano hayo nilihamaki Sana na dhahiri hayakuwa mahojiano ya simu Bali Ni ana kwa ana.

Nilidokezwa kuwa alikuja  Dar es salaam kuhudhuria Harusi maeneo ya Kariakoo.

Kisha alirejea Marekani.Manju wa Mazuki Masou Masoud usirejee Tena dhambi hii yakutokunijuza ujio wa Bila Malika hata ukisikia yupo Kenya unijuze nimfuate angalau nimshike mkono tu .

Huyu ndiye Aisha Abduly maarufu Malika . Ambaye haotokufa fofofo Bali ataendelea kuishi kupitia tungo zake ambazo zitaishi dahari na DAHARI .

Malika amefanikiwa kukata rufaa ya kifo kwakuweka alama ya Taarab Duniani,wakati ambapo sura yake itakapotoweka Duniani ,sauti na tungo zake zitaendelea kutamalaki chini ya Jua .]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-07-09T04:05:28Z 2021-07-09T04:05:28Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=469 <![CDATA[KUHUSU MUHAMMED SAID ABDULLA (BW. MSA)]]> KUHUSU MUHAMMED SAID ABDULLA
MAISHA YAKE
Muhammed Said Abdulla alizaliwa huko Makunduchi kisiwani Unguja. Elimu yake ya sekondari alipata katika shule ya misioni ya kikristo. Baada ya kumaliza masomo mwaka 1938 aliajiriwa na serikali idara ya afya. Hapo alihamishwa kwa idara ya kilimo alipokuwa mhariri wa jarida la Swahili Bulletin.
Kutoka hapa aliendelea kuwa mwandishi wa habari na kuanzia 1948 akawa mhariri wa gazeti la Zanzibari. Baadaye alikuwa mhariri msaidizi wa majarida ya Al-Falaq, Afrika Kwetu na Al Mahda. Tangu 1958 hadi kustaafu mwaka 1968 alikuwa mhariri wa jarida la Mkulima. Katika kipindi hiki kilitokea mapinduzi ya Zanzibar ambako mke na watoto wake waliuawa.
RIWAYA
Mwaka 1958 Abdulla alishiriki kwenye mashindano ya utunzi wa tungo za Kiswahili (“Swahili Story-Writing Competition”) yaliyoendeshwa na Ofisi ya Fasihi ya Afrika ya Mashariki (East African Literature Bureau). Riwaya yake Mzimu wa Watu wa Kale ilishinda tuzo la kwanza ikachapishwa kitabu 1960. Hapa alimbuni mhusika Bwana Msa aliye mpelelezi wa binafsi anayeshirikiana na polisi na kudhihirisha siri ya uuaji wa mtu tajiri. jina la “msa” ni akronimi ya herufi za kwanza za majina yake mwenyewe Abdulla yaani M-S-A.
Abdulla aliendelea kutunga kwa jumla riwaya ya upelelezi sita ambako Bwana Msa ni mhusika mkuu. Mhusika huyu anafanana katika tabia kadhaa na Sherlock Holmes, mhusika wa riwaya za mwandishi Mwingereza Conan Doyle. Sawa na Sherlock Holmes Bwana Msa anavuta kiko, anapata usulihisho wa kesi kwa kutumia akili yake akishirikiana na msaidizi na rafiki yake Najum (anayefanana na Dr. Watson wa Sherlock Holmes) na kusaidia kazi ya polisi inayowakilishwa na Spekta Seif.
Wahakiki walimshambulia Abdulla kwa kutumia mfano wa kigeni. Hata hivyo hata akitumia nukuu za Conan Doyle aliweka masimulizi kabisa katika mazingira na utamaduni wa Unguja na jamii ya Waarabu na Waafrika kabla ya mapinduzi.
Wahakiki wengine wameona ya kwamba muundo wa kesi katika hadithi za Abdalla ni tata mno, hata hivyo wamemsifu kwa uwezo wake wa kuchora tabia za wahusika kikamilifu katika lugha na imani ya Kiunguja.
KATI YA RIWAYA ZAKE ZA KIPELELEZI NI;
Mzimu wa Watu wa Kale (1966)
Kisima cha Giningi (1968)
Duniani Kuna Watu (1973)
Siri ya Sifuri (1974)
Mwana wa Yungi Hulewa (1976)
Nje ya riwaya za upelelezi aliandika pia Mke Mmoja Waume Watatu (1975) kinachohusu ulaghai katika ndoa na mkusanyo wa hadithi fupi katika “Hekaya za Kuburudisha”.
WASIFU
Abdulla alikuwa ni mhariri na mwaandishi wa vitabu tofauti ambavyo viliinyanyua lugha ya kiswahili katika daraja la juu na kuiongezea umaarufu mkubwa eneo la afrika mashariki. Alifanikiwa kuowa mke na kupata wawili katika maisha yake. Vile vile ni miongoni mwa watetezi wakubwa walifanya utetezi katika kuikomboa nchi ya Zanzibar kutoka mikononi mwa Watanganyika. Na hii ndio ilikuwa sababu ya yeye kuwa katika hatari ya maisha yake. Miongoni mwa beti zake za kuwatupia watanganyika ujumbe utakaoweza kuwapotezea nguvu ya kutaka kuinyakuwa Zanzibar. Njama ilianza kupangwa na watanganyika ili kumuondoa Bwana Msa Katika hii dunia
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-07-09T03:12:42Z 2021-07-09T03:12:42Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=462 <![CDATA[SITI BINT SAAD AMEIFARIKI DUNIA HII LEO JULAI 8]]>

.jpg   cc257895-2dee-43bf-8834-8a4b64ecd598.jpg (Size: 15.65 KB / Downloads: 0)

HEMED KIVUYO

"Tazameni tazameni eti alichofanya kijiti,kumchukua mgeni ,kumchezesha foliti,Kenda naye maguguni ,kamrejesha maiti"  Ni baadhi ya Maneno yaliyopo katika moja ya nyimbo za Siti Bint Saad ambao kisa chake nicha kweli.

Kilitokea kisa kimoja Zanzibar ambapo Mwanamama mmoja kutoka Bara alihadaiwa na Mwanaume mmoja Kisha kuuawa.

Vijana wengi hudhani baadhi ya nyimbo za Taarab zilizovuma ziliimbwa na Marehemu Fatma Baraka "Bi Kidude"mfano wimbo huo "kijiti" ambao bi Kidude aliuimba ka ufasaha.

Ndu zangu,Siti Bint Saad ameifariki Dunia leo Julai 8.

SITI NI NANI?

SITI alizaliwa Fumba Zanzibar 1880,na alipewa jina la "Mtumwa kwakuwa alizaliwa kipindi Cha utumwa.

Babake alikuwa Mnyamwezi wa Tabora na Mama alikuwa Mdigo kutoka Yanga .

Mamake alikuwa akiuza Nyungu huku Siti akimsaidia hiyo Ni baada ya kupata umriwakujifahamu.

Mwanzo wangoma nilele,Siti alianza kuonesha kipaji Cha uimbaji angali mdogo mno,kiasi Cha mapafu take kufananishwa na Simba kwakuvuta sauti muruwaa..

1911,Siti alindoka kijijini kwao na kuhamia mjini ndipo alipokutana na kundi la Taarab la Nadi ikhwan safaa"

Kundi hili lilianzishwa na Sultani Seyyid barghashy Said. Said anatajwa kuwa Sultani mpenda starehe".

Kundi hili lilikuwa na wanaume tupu kwakuwa miaka hiyo ,Mwanamke hakuruhusiwa kuimba,ilionekana Ni anasa kwao.

Safaa ilivutiwa na uimbaji wa Siti,hapo akaanza kufananishwa na Ummy Kulthum wa Misri.

Kundi hili lilimpa Siti nafasi akawa mwanamke wa kwanza kuimba Taarab katika Hadhira,umma ukahamanika baadaye ukasisimka na Siti hakuwa nawakufananishwa naye.

SITI alivuma ulimwenguni kote,si Afrika hata Ughaibuni. 1928 kampuni ya Columbia And hs masters voice ya Mumbai India ikamtafuta Siti kwa udi na uvumba.

Hatimaye Kampuni hiyo ikajenga studio visiwani Zanzibar kwaajili ya Siti.

Kwakuwa mwiba wa samaki humchoma hata mnunuzi Basi wasompenda Siti wakaanza "chokochoko".

Wakasema "Siti kawa mtu lini,kaja mjini na Kaniki chini ,Kama si sauti angekula Nini"

SITI hakukaa kimya naye akajibu kwa ubeti " Si hoja uzuri ,na sura jamali,kuwa mtukufu najadi kebeli ,hasara ya mtu kukosa akili" .

Mshairi maarufu Shaaban Robert alikutana na Siti siku kadhaa kabla Siti hajaaga Dunia ,

Alimwandikia Fasihi Bora kuwahi kutokea ulimwenguni "wasifu wa Siti Bint Saad". Wengi walizidi kumjua Siti kwa andiko Hilo.

Miaka ya hivi karibuni kulikuwa na Gazeti linaitwa "SAUTI YA SITI" sijui Kama bado lipo ama laa"

SITI aliaga Dunia tarehe 8 mwezi 7 mwaka 1950.

SITI ndiye aliyefungua ndiya kwa waimbaji wengine wakike wa Taarab,watilia mbali Hawa wajuzi akina Malika na wengineo .

Mola azidi kumrehemu Siti Bint Saad (Mtumwa)]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-14T15:42:05Z 2021-06-14T15:42:05Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=20 <![CDATA[WASIFU WA SITI BINTI SAAD]]> Siti binti Saad alizaliwa katika kijiji cha Fumba, Zanzibari mwaka 1880. Alipozaliwa alipewa jina la ‘Mtumwa’ hii ni kwa vile alizaliwa katika kipindi cha utumwa wa Kiarabu. Jina la Siti alipewa na mkabaila mmoja wa kiarabu.Baba yake bwana Saadi alikuwa ni Mnyamwezi kutoka Tabora na mama yake alikuwa ni Mzigua toka Tanga, lakini wote wawili walizaliwa Zanzibari. Hali ya maisha ya familia yao ilikuwa ni duni sana na walijishughulisha zaidi katika shughuli za kilimo na ufinyanzi kazi ambazo Siti alijifunza na kuzimudu vizuri pia.Kama waswahili wasemavyo ‘kuzaliwa masikini si kufa masikini’ Siti alibarikiwa kuwa na kipaji cha pekee cha uimbaji. Kipaji hiki kilimsaidia sana tangu siku za awali za maisha yake kwani alitumia uimbaji wake kuuza vyungu vya mama yake alivyokuwa akimsaidia kuvitembeza. Siti alipoimba sauti yake iliweza kupaa na kusafiri kwa umbali wa maili nyingi na hii ndio ilikuwa ishara ya watu kujua kwamba vyungu vya kina Mtumwa vinapita leo. Alifananishwa kuwa na mapafu yenye nguvu kama ya simba kutokana na alivyoweza kupaza sauti yake mbali na bila kuachia pumzi.Kutokana na wakati huo elimu kwa watoto wa kike kutotiliwa mkazo, Siti hakuwahi kwenda shule wala kuhudhuria mafunzo ya Kurani. Hivyo mnamo mwaka 1911 aliona ni bora ahamie mjini ili kubooresha maisha yake zaidi. Ujio wake wa mjini ulikuwa wa neema kwani alikutana na bwana mmoja wa kundi la muziki wa Taarabu la “Nadi Ikhwani Safaa” aliyeitwa Muhsin Ali. Katika kipindi hicho hilo ndilo lilikuwa kundi pekee la muziki wa taarabu lililoanzishwa na Sultani mpenda starehe na anasa bwana Seyyid Barghash Said. Kundi hili lilikuwa ni la wanaume peke yake , wanawake hawakuruhusiwa kujiunga na vikundi vya muziki kwa vile ilikuwa ikichukuliwa kama ni uhuni. Bwana Muhsin alikiona kipaji cha pekee cha Siti na hivyo akajitolea kumfundisha kuimba kwa kufuata vyombo vya muziki na lugha ya kiarabu. Baada ya hapo alikwenda kumtambulisha kwa wanamuziki wenzie wa “Nadi Ikhwani Safaa” ambao bila kusita wakaanza kufanya naye maonyesho mbalimbali katika jamii. Walipata mialiko mingi hasa kutoka kwa Sultani na matajiri wengine wa Kiarabu, pia katika maharusi na sherehe zingine mbalimbali, inasemekana ulifika wakati ambapo sherehe ilishindwa kufana kama Siti binti Saadi hakuwepo kutumbuiza. Siti alikuwa ni moto wa kuotea mbali na jina lake lilivuma kwa haraka sana hadi nje ya mipaka ya nchi na bara la Afrika. Na punde Siti alianza kufananishwa na ‘Umm Kulthum’, mwimbaji mahiri wa kike aliyetamba wakati huo kutoka Misri.Kama nilivyosema moto wa Siti ulikuwa si wa kuusogelea karibu, mwaka 1928 kampuni ya kurekodi muziki ya Columbia and His Master’s voice yenye makazi yake Mumbai Indiailisikia umaarufu wa Siti binti Saadi na hivyo ikamwalika yeye pamoja na kundi lake kwenda kurekodi kwa lugha ya Kiswahili ili kujaribu kama muziki wake utauzika. Kampuni ile haikuweza kuamini jinsi muziki ule ulivyouzika kwa kasi kubwa kwani wastani wa santuri 900 ziliweza kuuzika katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo, na hadi kufikia 1931 santuri 72,000 zilikuwa zimeuzwa. Kutokana na kusambaa kwa santuri hizi, umaarufu wa Siti ulizidi mara dufu watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia walikuwa wakija Zanzibari kuja kumwona. Mambo yalizidi kuwa mazuri kwa Siti hadi ikafikia hatua kampuni ya kurekodi ya Columbia kuamua kujenga studio ya kurekodi muziki palepale Zanzibar maalumu kwa ajili ya Siti binti Saadi.Hatua hiyo ya hadi kujengewa studio iliwaumiza wengi wenye wivu, hivyo wakaanza kumtungia nyimbo za kumkejeli ili kumshusha na hasa walitumia kigezo kwamba hana uzuri wa sura, nyimbo nyingi ziliimbwa lakini huu ndio uliovuma sana:-
    Siti binti Saad kawa mtu lini,
    Kaja mjini na kaniki chini,
    Kama si sauti angekula nini?
Na yeye kwa kujua hila za wabaya wake, akaona isiwe taabu akajibu shambulio namna hii:-
   Si hoja uzuri,
   Na sura jamali,
   Kuwa mtukufu,
   Na jadi kebeli,
   Hasara ya mtu,
   Kukosa akili.
Kwa kujibu shambulio hilo kwa namna yake aliwafunga midomo wale wote waliokuwa wakifumatafuata. Siti pia alikuwa ni mwanamke wa kwanza mwanaharakati katika kipindi chake, alitetea wanawake na wanyonge kwa ujumla, kwani katika kipindi chake watu matajiri walikuwa wakiwaonea masikini na walipofikishwa mbele ya haki waliweza kutoa hongo na kuachiwa huru halafu wewe uliyeshitaki ndiye unayefungwa.Utunzi wake wa wimbo wa Kijiti ulimpatia sifa kubwa kwani ulikuwa ukielezea kisa cha kweli kilichomkuta mwanamke mmoja mgeni kutoka bara, mwanamke huyu alipofika alikutana na Tajiri mmoja ambaye alijifanya amempenda, hivyo akamchukua na kulala naye halafu baadaye akamuua. Tajiri yule alishitakiwa na bahati nzuri walikuwepo mashahidi wawili walioshuhudia tukio lile, lakini kwa vile ni Tajiri alitoa pesa na kesi ikawageukia wale mashahidi na kufungwa.Siti akatoa wimbo huu :-
    Tazameni tazameni,
    Eti alofanya Kijiti,
    Kumchukua mgeni,
    Kumcheza foliti,
    Kenda naye maguguni,
    Kamrejesha maiti.
Siti aliendelea kumwambia katika nyimbo zake kwamba asijethubutu kwenda Dar er Salaam kwa maana watu wenye hasira wanamsubiri na wameapa kwa ajili yake.Siti aliendelea na shughuli yake ya muziki hadi uzeeni, muda mfupi kabla ya kifo chake alikutana na mwandishi maarufu na mwanamashairi Shaaban Robert ambaye alimhoji na kuweza kuandika wasifu wake katika kitabu alichokiita ” Wasifu wa Siti binti Saadi.” Wasifu huu unaonekana kuwa ndio bora zaidi uliowahi kuandikwa katika fasihi ya Tanzania. Kitabu hiki kinatumika kufundishia shule za sekondari za Tanzania.Tarehe 8 Julai 1950 Siti binti Saadi alifariki dunia na kuacha pengo kubwa katika fani ya Taarabu. Ingawa pengo hilo haliwezi kuzibika lakini kuna watu wengi walioweza kuibuka na umaarufu wa kuimba taarabu kupitia kwake, mfano hai ni Bi Kidude.Hata baada ya kifo chake jina lake bado linatumika sana kama kielelezo cha ushujaa wake, Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA), kimetumia jina lake kulipa jina gazeti la chama chao “Sauti ya Siti”. Hadi leo hii Siti hutumika kama kipimo cha kufundishia uimbaji wa Taarabu. Na anakumbukwa katika historia yake ya kuwa mwanamke wa kwanza Afrika mashariki kurekodi muziki katika santuri.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-14T15:25:57Z 2021-06-14T15:25:57Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=18 <![CDATA[TAWASIFU YA SHAABAN ROBERT]]> KATIKA kitabu chake cha tawasifu “MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA HAMSINI” Shaaban Robert anasimulia dhiki, adha na udhalili alioupitia, pengine kwa sababu ya Uafrika wake, kipindi cha ukoloni akiwa katika safari ya kikazi kama mtumishi wa serikali;
ABIRIA CHEO CHA PILI
DARAJA yangu katika kazi sasa ilikuwa imeniwezesha kusafiri kama abiria wa cheo cha pili katika gari moshi. Mapendelea haya yanayotamaniwa yalinijia baada ya miaka kumi na nne ya kazi serikalini. Julai 13, 1944, nilichukua tikiti, na baada ya kuagana na marafiki, nikasafiri kwenda Mpwapwa. Nilishuka Korogwe kungoja safari ya lori. Karibu ningalilala nje Korogwe kwa ukosefu wa malazi kwa abiria Waafrika., lakini mtu mmoja aliyenijua zamani alinichukua kwake akanipa malazi mema. Asubuhi nilionyesha tikiti zangu za safari kwa msimamizi wa safari. Mtu huyu alinitupia jicho kwa haraka kisha akaamuru nijipakie katika lori.
Palikuwa na malori manne tayari kwa safari siku ile. Nilikwenda nikajipakia katika lori la abiria cheo cha pili. Mimi nilikuwa msafiri wa kwanza kujipakia. Dakika chache baadaye loro letu lilijaa abiria. Abiria Waafrika tulikuwa mimi na watoto wangu tu. Wengine wote walikuwa ni Wahindi. Karibu na dakika ya mwisho kusafari pakaja Wahindi wanne wengine. Kuwapa watu hawa wanne nafasi katika lori nililojipakia mimi ilipasa watu wanne waliokuwa wamekwisha kuingia washuke. Msimamizi wa safari, Mhindi vilevile, hakuona mtu mwingine wa kushuka ila mimi. Baridi ina mzizimo siku zote kwa kondoo mwenye manyoya haba. Kwa maneno ya karaha alinilazimisha kushuka chini nikajipakie katika lori la abiria wa cheo cha tatu au la mizigo. Nilimkumbusha msimamizi wa safari kuwa mimi ni abiria wa cheo cha pili ambaye nilikuwa nikisafiri kwa kazi ya serikali; nilitangulia kujipakia mahali nilipostahili kukaa; alikuwa hana haki ya kuniteremsha; iwapo ililazimu kutenda atakavyo ililazimu vilevile yeye kunipa stashahada ya kuonyesha namna ilivyosafiri kutoka Korogwe. Kwa maneno hayo ulimi wa msimamizi wa safari ulianza kupotoka akadai kuwa aliweza kuzuia kusafiri lori nililoingia.
Kundi kubwa la watazamaji lilikuwepo. Karibu watu wengi katika kundi lile walicheka kwa maneno ya msimamizi wa safari. Kivumo cha kicheko kilichemsha hasira yake akaamuru niteremshwe chini kwa nguvu. Matarishi waliokuwa chini ya amri yake walitii wakawa tayari kunijia wanikamate na kunitupa chini kama mtumba, lakini kitu gani sijui kiliwafanya kusita kutimiza amri ya bwana wao. Halafu nilisikia kuwa desturi ya matarishi wale ilikuwa kutii na kutimiza kila amri njema waliyopewa, na kuacha mbali kila amri mbaya hata katika hatari ya kutolewa kazini mwao. Nilifurahi sana kusikia habari hii. Idadi ya watu wema ni kubwa siku zote kuliko jumla ya watu wabaya.
Siku zangu zilikuwa zikihesabiwa. Sikutaka kuchelewa bure pale Korogwe. Niliita watu kuja kushuhudia mwamale niliotendewa na tabia ya msimamizi wa safari. Watu wengi walikuwa tayari kunipa sahihi za mikono yao kuwa walishuhudia yote yaliyotokea. Kisha mimi na watoto wangu tulishuka na kujipakia katika gari jingine. Nafasi iliyokuwa imebaki mle garini ilikuwa si kubwa. Basi tulikaa juu ya mizigo yetu. Kutoka Korogwe tulikwenda Morogoro. Mchana wote ulituishia njiani. Hii ilikuwa siku ya pili ya safari yangu, nikafurahi kushuka katika gari.
Saa mbili na nusu usiku nilijipakia katika gari moshi lililotoka Dar es Salaam hata saa tisa usiku nikashuka Gulwe. Kutoka Gulwe nilichukuliwa na lori la Idara ya Utunzaji wa Wanyama kwenda Mpwapwa. Saa kumi alfajiri nikawa Mpwapwa. Mwisho wa safari yangu ilikuwa ni Kikombo, lakini niliambiwa nikae juu ya gari hata saa moja asubuhi wakati mwendeshaji wetu alipoingia nyumbani kwake kulala. Nje kulikuwa kukizizima sana kwa baridi na umande na lori letu lilikuwa wazi. Taya za watoto wangu zilitingishika na meno yakagongana kwa kipupwe. Julai ni mwezi wa kipupwe kikali pande zile za dunia. Mbwa hafi maji akiona ufuko, na sisi kwa kuwa sasa tulikuwa karibu kufika mwisho wa safari yetu jaribu la baridi halikutufadhaisha sana. Tulikuwa na mablanketi yaliyoweza kuzuia mzizimo wake kutudhuru. Tulijifunika mablanketi yetu tukasaburi kuche polepole.
Saa moja na nusu asubuhi nilikuwa mbele ya msimamizi wa Afisi ya Idara ya Utunzaji wa Wanyama. Huyu alikuwa ni Mzungu. Hakuwa tayari kushikana mikono na mimi kama nilivyozoea kuona Wazungu wengine. Labda mimi nilikuwa si kitu mbele yake lakini tuliongea vema. Alisema kuwa nitapata nyumba lakini kwa namna maneno yalivyotamkwa niliweza kufahamu kuwa idara ilikuwa na dhiki ya makao mema. Dhiki hii ilikuwa imeenea duniani wakati ule. Bati na simenti vilikuwa adimu kupatikana kwa sababu ya Vita Kuu Na. 2. Hii ilikuwa ni Jumapili, siku ya tatu ya safari yangu. Nilipewa ruhusa nikapumzike nihudhurie kazini Jumatatu asubuhi.
*** Vitabu vya sheikh Shaaban Robert vimerejewa kuchapwa upya, na sasa vinapatikana kwa wingi madukani, hususani jijini Dar es Salaam. Ni uzalendo wa kujivunia kwa kila Mswahili kumiliki na kuzisoma nakala za vitabu vya gwiji huyu na “baba wa Kiswahili”.
ORODHA YA KAZI ZA FASIHI ALIZOANDIKA SHAABAN ROBERT

1. MWAFRIKA AIMBA (1969), Nelson. Nairobi

2. ALMASI ZA AFRIKA (1971), Nelson, Nairobi

3. KOJA LA LUGHA (1969), Oxford, Nairobi

4. INSHA NA MASHAIRI (1967), Nelson, Nairobi

5. ASHIKI KITABU HIKI (1968), Nelson, Nairobi

6. PAMBO LA LUGHA (1968), Oxford, Nairobi

7. KIELEZO CHA FASILI (1962), Nelson, Nairobi

8. MASOMO YENYE ADILI (1959), Art&Literature, Nairobi

9. MAPENZI BORA (1969), Nelson, Nairobi

10. TENZI ZA MARUDI MEMA NA OMAR KHAYYAM (1973), TPH, Dar-es- salaam

11. UTENZI WA VITA VYA UHURU (1961), Oxford, Nairobi

12. ALMASI ZA AFRIKA NA TAFSIRI YA KIINGEREZA (1960), Art&Literature, Nairobi

13. MASHAIRI YA SHAABAN ROBERT (1971), Nelson, Nairobi 14. SANAA YA USHAIRI (1972), Nelson, Nairobi. Na vitabu vya nathari vya Sheikh Shaaban Robert ni:

15. KUFIKIRIKA (1968),Oxford, Nairobi

16. WASIFU WA SITI BINTI SAAD (1967), Art&Literature, Nairobi 17. MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA HAMSINI (1949), Nelson, Nairobi

18. KUSADIKIKA (1951), Nelson, Nairobi

19. ADILI NA NDUGUZE (1977), TPH, Dar-es- salaam

20. UTU BORA MKULIMA (1968), Nelson, Nairobi

21. SIKU YA WATENZI WOTE (1968), Nelson, Nairobi

22. KIELELEZO CHA INSHA (1954), Witwatersand, Nairobi

23. BARUA ZA SHAABAN ROBERT 1931- 1958, (2002), TUKI, Dar- es- salaam

24. MITHALI NA MIFANO YA KISWAHILI (2007), TUKI, Dar-es- salaam
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-14T15:20:48Z 2021-06-14T15:23:28Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=17 <![CDATA[WASIFU WA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE]]> Aprili 13, mwaka 1922, safari ndefu ya maisha ya Mwalimu Kambarage Nyerere iliyochukua miaka 77 na miezi 6 ilianza Mwitongo kijijini Butiama, kilomita takribani 30 kutoka mji wa Musoma, mashariki mwa Ziwa Victoria lililoko kaskazini mwa Tanzania. Siku hiyo mvua kubwa ilionesha. Mama Mgaya Nyang’ombe, aliyekuwa mke wa tano kati ya 23 wa Chifu Nyerere Burito wa Zanaki, alijifungua mwanae wa pili. Kwa desturi za kabila la Wazanaki, mtoto wa kike ama wa kiume aliyezaliwa siku ya mvua alipewa jina la KAMBARAGE (mzimu wa mvua).
Kambarage alikuwa mtoto wa maskini kama walivyokuwa watoto wengine kijijini. Ingawa baba yake alikuwa Chifu (Mtemi), cheo hicho alichopewa wakati wa utawala wa Kijerumani hakikuwa na maslahi yoyote ya maana. Kwa desturi za makabila mengi, watoto walilelewa na kutunzwa na mama zao.  Kwa hiyo, Mama Mgaya alijitegemea mwenyewe katika kuwalea wanawe 6 alioishi nao kwenye kibanda cha udongo, na paa la nyasi. Kambarage alipofikia umri wa kuelewa mambo, alimuhurumia sana mama yake na kumsaidia kazi kwa kadri alivyoweza.
Eneo la Mwitongo lilikuwa na mandhari ya kupendeza ya kilima kidogo kilichozungukwa na vichaka na mawe. Mtoto Kambarage alicheza michezo ya kujificha kwenye vichaka na kukimbiza pimbi na tumbili kwenye mawe.  Alichunga mbuzi za mamaye na alipofikia umri wa kutosha, alienda na vijana wenziwe kuwinda porini. Pamoja kumsaidia mamaye alipata muda wa kuwa karibu na babaye na kujifunza utamaduni wa kizanaki.
Siku moja, akiwa na miaka 10 baba yake alimtuma afuatane na mama yake wa kambo kwenda kwenye kijiji kingine kuhudhuria msiba wa jamaa wa mama huyo. Wakati wa kurudi walipewa mbuzi. Kambarage alimfunga kamba mbuzi na kumwelekeza njia. Mbuzi akagoma. Wakati wanakukurushana naye mzee mmoja akamwambia atamrahisishia kazi. Mzee yule akang’oa nywele kidogo kutoka kichwa cha Kambarage na manyoya kidogo toka kichwa cha mbuzi akachanganya na mizizi fulani, akatafuna na kumpa mbuzi akala. Yule mbuzi akamfuata Kambarage mpaka wakafika nyumbani Mwitongo bila kumsumbua!
Akiwa na umri wa miaka 11 baba yake akamtolea Kambarage mahari kwa binti mmoja kijijini. Kwa desturi za Kizanaki mzazi alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo ili kuwa na uhakika kwamba hata akifa wanawe wa kiume watakuwa na uwezo wa kuoa.
Kambarage hakutegemea kwamba angeliweza kupata nafasi ya kwenda shule kwa sababu baba yake alikuwa hana uwezo wa kuwasomesha wanawe wote.  Hata hivyo, alidhihirisha kuwa na akili nyingi zilizo muwezesha kujifunza mambo haraka. Alijifunza kucheza bao kutoka kwa baba aliyependa kucheza bao na mama yake aliyekuwa hodari wa mchezo huo. Kila alipopewa nafasi ya kucheza bao na marafiki wa baba yake Kambarage aliweza kuwafunga!  Akili alizozidhihirisha katika mchezo huo ndizo zilizomuwezesha kupata bahati ya kwenda shule. Mmoja wa wazee hao alimshauri Chifu Nyerere amuingize mwanawe shule kwa kuwa alionekana kuwa na akili sana. Ilimuwia vigumu Chifu kuamua lakini mwanawe mkubwa Edward Wanzagi alimshawishi akakubali.
Hatimaye, siku moja ya mwezi Aprili mwaka 1934, Kambarage akiwa na umri wa miaka 12 aliamka mapema kwa furaha kwenda kuanza darasa la kwanza katika shule ya Mwisenge, Musoma mjini. Kambarage aliingia shule akiwa hajui Kiswahili sawasawa. Hata hivyo, haikupita muda akajua Kiswahili, akili alizooonesha kwenye bao zilidhihirika darasani pia.  Ingawa wakati alipoanza shule alikuwa amechelewa kwa miezi mitatu, aliweza kuelewa mambo kwa kasi kuwashinda wengine walioanza mapema. Alipoingia darasa la tatu walimu waliamua kumrusha hadi la nne, akasoma masomo ya miaka minne kwa miaka mitatu tu. Mwaka 1936 alifanya mtihani wa nchi nzima wa kuingia darasa la tano, akawa mtu wa kwanza Tanganyika nzima.  Alichaguliwa kuingia shule ya bweni Tabora ambayo ilikuwa na darasa la tano hadi la kumi.
KIJANA KAMBARAGE
Mwaka 1937 Kambarage akiwa kijana wa miaka 15 alianza masomo ya darasa la tano akiwa na ari ya kusoma kwa bidii.  Waalimu wake Tabora walimpenda kwa akili zake. Wanafunzi wenziwe nao walimpenda sana kwa sababu alikuwa mcheshi na mwema sana.  Waliosoma naye waliwahi kueleza kwamba ingawa alikuwa akienda shule na fedha kidogo sana za matumizi, alikuwa radhi kutoa fedha zote alizokuwanazo kuwasaidia wanafunzi waliokuwa na shida.  Pamoja na wema, alioonesha tabia ya kupenda kutetea HAKI. Hakukubali kuona uonevu uliokuwa ukifanywa na ma-kaka dhidi ya wanafunzi. Aliwahi kwenda kwa Mwalimu Mkuu kulalamika kuhusu adhabu ya kufungwa miguu na mikono aliyopewa mwanafunzi mmoja na kaka wa bweni.
Kwenye kuamua shauri hilo Mwalimu Mkuu alimpendelea kaka na alimpa mwanafunzi huyo adhabu nyingine ya viboko. Kambarage aliamuriwa kumchapa, ilibidi amchape ingawa hakupenda kabisa kufanya hivyo! Hata hivyo, Kambarage hakuuacha msimamo wake wa kuwatetea waliokuwa wakionewa.  Hatimaye, Waalimu waliamua kumpa naye cheo cha ‘Kaka’ lakini hiyo haikuwa dawa. Haikupita muda, alianzisha mgomo wa kupinga mtindo wa ma-kaka kupata upendeleo wa kujigawia chakula kingi kuliko wanafunzi wengine ingawa naye alikuwa kaka!
Pamoja na kutetea haki za wanafunzi wenziwe, alidhihirisha uhodari wa kutetea kile alichoamini. Siku moja wakati wa kipindi cha majadiliano, mada ya “Tanganyika iendelee kuwa chini ya utawala wa Waingereza” ilikuwa ikijadiliwa.  Katika kuchangia, bila woga wowote mbele ya Mwalimu Mkuu (Mwingereza) Kambarage alipinga kwa nguvu hoja ile na kuelezea waziwazi uovu mwingi uliokuwa ukifanywa na Serikali ya Uingereza katika kuitawala nchi kwa mabavu na kwa misingi ya ubaguzi wa rangi.  Mwalimu Mkuu alimkatisha na kumwamuru akae chini asiendelee kuzungumza.  Kambarage alihamaki na kuamua kutoka kwenda bwenini kubeba sanduku lake ili akapande gari moshi (treni) kurudi kwao Butiama!  Ilibidi Mwalimu Mkuu atume watu kumshawishi arudi shuleni.
JULIUS KAMBARAGE
Akiwa shuleni Tabora Kambarage aliweza kubatizwa na kuwa Mkatoliki akajipa jina la ‘JULIUS’. Mwalimu aliwahi kusimulia kwamba ingawa alianza kuingia kwenye mafundisho ya dini akiwa shuleni Mwisenge, hakuweza kubatizwa kwa sababu mapadri walidhani kwamba angeweza kumrithi baba yake uchifu na hatimaye kuwa na wake wengi! Wamisionari walijaribu sana kumhubiria Chifu Nyerere Burito ajiunge na ukristo bila mafanikio. Mara nyingi mapadri walipomfuata kumhubiria aliishia yeye kuwahubiria wao! Kambarage aliweza kubatizwa baada ya baba yake kufariki mwaka 1942. Wasiwasi wa mapadri ulikuwa umeisha kwa sababu aliyerithi u-chifu alikuwa Edward Wanzagi.
Baada ya masomo shuleni Tabora, Julius Kambarage alifanikiwa kwenda Chuo Kikuu cha Makerere. Akiwa  huko kidogo kidogo alianza kujihusisha na mambo ya kisiasa. Alianzisha tawi la chama cha TAA kilichokuwa kimeanzishwa Dar es Salaam kama chama cha kutetea maslahi ya Watumishi wa Serikali waliokuwa wakinyanyaswa na kudhulumiwa na Wakoloni.
MWALIMU JULIUS KAMBARAGE
Mwaka 1945 Julius Kambarage Nyerere alifaulu masomo yake na kupata Diploma ya ualimu.  Akarudi kijijini Butiama na kumjengea mama yake nyumba kabla ya kwenda kuanza kazi Tabora. Uamuzi wake wa kutaka kuajiriwa kwenye shule ya misheni ya Mtakatifu Maria Tabora ni kielelezo kimoja cha msimamo wake kuhusu HAKI. Alikuwa amepokea barua mbili za ajira – moja kutoka Serikalini ikimpa nafasi ya kufundisha kwenye shule ya Sekondari ya Tabora na nyingine kutoka kwenye shule ya misheni ya Mtakatifu Maria (St. Marys).  Barua kutoka Serikalini ilimweleza juu ya mshahara atakaopata na marupurupu ya malipo ya pensheni na kwamba shule za misheni hazikuwa na marupurupu yoyote. Julius hakupendezwa na utaratibu wa marupurupu ya walimu wa serikali na misheni kutofautiana. Akaamua kwenda kufundisha shule ya Sekondari ya misheni isiyo na marupurupu yoyote.
Tabia yake ya kupenda haki iliendelea kujidihirisha katika shughuli mbalimbali alizofanya akiwa Tabora. Aliendelea kujihusisha na chama cha TAA akawa katibu wa tawi la chama hicho mjini Tabora. Alishiriki kwenye midahalo ya shule za Sekondari na hoja alizotoa zilivutia sana. Katika mdahalo mmoja uliokuwa na mada “Mali ni bora kuliko Elimu” Julius alipinga vikali hoja. Akasema kwamba alichagua kazi ya ualimu ili iwawezeshe watu kuelewa mambo na kwamba wakielewa wanakuwa na furaha, si kwa sababu wana mali. Unaweza kuwa mtu mwenye mali lakini huna furaha!
Mwalimu Julius alikuwa na hamu sana ya kwenda ng’ambo kwa masomo ya juu lakini kutokana na msimamo aliokuwanao dhidi ya Serikali, wakoloni hawakutaka kumpa nafasi hiyo. Hatimaye kwa kutetewa na rafiki yake aliyekuwa padri wa kizungu (Father Walsh) aliweza kupewa scholarship na Serikali kwenda Chuo Kikuu cha Edinburgh kuchukua masomo ya historia na uchumi. Akalipenda sana somo la filosofia. Mawazo ya kuingia kwenye siasa yalianza kujengeka wakati huo.
Akiendelea na msimamo wake wa utetezi wa haki aliweza kuandika makala mbali mbali. Mbili alizopeleka kwenye mashindano alipata zawadi ya kwanza. Makala moja ilihusu ‘kuonewa wanawake’ akielezea kuhusu unyonge wa wanawake katika maisha ya makabila nchini. Ya pili ilikuwa na kichwa cha habari “Matatizo ya Ubaguzi wa Rangi katika Afrika Mashariki”. Katika makala hiyo alisema Wazungu alikuwa anatawala kudumisha umaarufu wao kwa njia ya unafiki…. Bepari Mhindi alikuwa anapata chakula chake kwa wizi mtupu au ujanja-ujanja na unafiki… Mwafrika naye alikuwa mnafiki alijipendekeza kwa Mzungu wakati moyoni anapasuka kwa wivu na chuki!
Alimaliza vema masomo yake huko Edinburgh na kuwa Mwafrika wa kwanza nchini Tanzania kupata Stashahada ya Juu. Aliporudi nyumbani alipokelewa na mchumba wake Maria Magige aliyemchagua mwenyewe si yule aliyetolewa mahari na baba yake. Ikambidi afanye tena zoezi la kujenga nyumba kwa ajili yake na Maria watakapofunga ndoa. Wanakijiji walimshangaa walipomuona msomi kama yeye akichanganya simenti na mchanga kufyatua matofali kwa ajili ya kujengea. Wasomi hawakupaswa kufanya kazi kama hizo! Julius na Maria walifunga ndoa tarehe 24 Januari 1953 kwenye kanisa Katoliki Musoma. Katika maisha yao ya ndoa waliweza kuwapatia watoto 7, watatu wa kike na wanne wa kiume.
AWA KIONGOZI
Baada ya mapumziko yake Butiama Mwalimu Nyerere alienda kuanza kazi ya kufundisha katika shule aliyopangiwa ya Pugu Sekondari, Dar es Salaam. Mwaka huo wa 1953 akiwa Pugu alianza kujihusisha kikamilifu na shughuli za chama cha TAA. Aliitembea kwa miguu na wakati mwingine kwa baiskeli ya kua zima umbali wa maili 12 kwenda mjini Dar es Salaam kuhudhuria mikutano na shughuli za chama hicho. Haikupita muda akili na uwezo mkubwa aliokuwanao ulidhihirika akachaguliwa kukiongoza. Kutokana na uongozi wake mahiri chama cha TAA kikabadilishwa kuwa chama kamili cha siasa tarehe 7 Julai 1954, kikaitwa TANU.
Chini ya uongozi wake baada ya kuanzishwa kwa chama cha TANU zilianza rasmi harakati za kupigania Uhuru. Pamoja na juhudi zote za Wakoloni kuchelewesha kupatikana kwa Uhuru hatimaye mwaka 1960 nchi ya Tanganyika ilifanikiwa kupata Serikali ya Madaraka. Desemba 9 1961 ikapata Uhuru kamili ,Mwalimu akawa Waziri Mkuu. 1962 nchi ya Tanganyika ikawa Jamhuri akawa Rais wa Kwanza wa Tanganyika Huru.
Simulizi kuhusu uongozi uliotukuka miaka 24 wa Mwalimu Nyerere akiwa Rais wa Tanzania unahitaji makala nyingine nyingi. Hakuna maelezo mafupi yanayoweza kutosheleza historia ya uongozi wake. Itoshe kusema alikuwa kiongozi shupavu sana aliyepigania uhuru wa nchi yake na wa nchi zingine za Afrika. Alijishusha na kuwa pamoja na wananchi aliowaongoza – shida zao aliziona ni zake, zilimgusa na kumnyima usingizi!  Akaondoa ubaguzi na kufuta matabaka ya walionacho na wasionacho. Akafuta ukabila na udini nchini. Watanzania wakaishi kidugu. Akafanikiwa kujenga AMANI, UMOJA NA MSHIKAMANO akiongozwa na dira ya MAENDELEO  YANAYOLENGA WATU WOTE. Akafanya Tanzania ijulikane kuwa kisiwa cha AMANI duniani.
HITIMISHO
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipendwa na kuheshimika sana ndani na nje ya nchi. Mwaka 1985 aliamua kwa hiari yake mwenyewe kuacha uongozi wa Taifa ili apumzike.  Alizunguka nchi nzima kuwaaga Watanzania. Kwa mapenzi makubwa wakampa zawadi za kila aina. Wananchi walioonesha wazi huzuni waliyokuwanayo kwa uamuzi aliouchukua. Walimuaga wakilia machozi!
Yote aliyoyaanza tangu utoto wake yalifikia kikomo tarehe 14 Oktoba 1999 alipoaga dunia kwenye kitanda cha hospitali ya Mtakatifu Thomas mjini London alikokwenda kwa matibabu. Kabla hajafariki dunia aliwakumbuka Watanzania wake akasema: “Najua nitakufa sitapona ugonjwa huu. Ninasikitika kuwaacha Watanzania wangu, najua watalia sana. Lakini nami nitawaombea kwa Mungu.”  Naam, Watanzania wake walilia sana walipopata taarifa za kifo chake. Mwili wake ulipoletwa nchini waliomboleza kwa uchungu mno. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizikwa kijijini kwake Mwitongo Butiama kwa heshima zote na wananchi wa Tanzania, na wa mataifa mbalimbali wakiwemo viongozi mashuhuri waliokuja kwa ajili hiyo.
Ni dhahiri msingi wa yale yote aliyoyaamini na kuyasimamia utaendelea kudumu ndani ya mioyo ya kizazi chake, kizazi hiki na vizazi vijavyo kutokana na mchango mkubwa alioutoa akiwa Muasisi na Baba wa Taifa katika kujenga taifa la Tanzania. Huyo ndiye mtoto aliyezaliwa siku ya mvua na kupewa jina la mzimu wa mvua KAMBARAGE; mwana wa Chifu Nyerere Burito na Mgaya wa Nyang’ombe.  Ni dhahiri, tarehe  aliyozaliwa – 13 Aprili mwaka 1922, Mgaya hakujua kwamba alikuwa amejifungua mtoto ambaye angekuja kuwa kiongozi maarufu sana nchini na duniani, aliyewapenda binadamu wote na kuwatumikia Watanzania kwa moyo wake wote, akili na nguvu zake zote! MUNGU Ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi. Amin.
]]>
false