MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

https://jifunzekiswahili.co.tz/2024-12-21T18:26:51ZMyBBMwlMaeda]]>2022-12-19T03:41:28Z2022-12-19T03:41:28Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2875
Wasomi na wasomaji, tujadili hili jambo,
Tusibaki waigaji, kukimbilia mikumbo,
Lisilo na mfumbaji, la mavazi hili fumbo,
Dhima ya kwanza mwilini, yatusitiri mavazi.
Pengine twajivalia, kuona kama urembo,
Vile tukishika njia, kuyaonesha maumbo,
Tuanze kuwasumbua, wenzetu waende kombo,
Dhima ya kwanza mwilini, yatusitiri mavazi.
Wazazi wametwambia, nasaa zao ni wimbo,
Hakuna wa kusikia, kuacha mambo ya ng'ambo,
Viwalo twajitupia, Kwa wengine huwa fimbo,
Dhima ya kwanza mwilini, yatusitiri mavazi.
Fumbuka nakufumbua, mavazi hubeba nembo,
Mvaaji akivaa, twajua ni mwendakombo,
Vema akijivalia, tutasema hiki chombo,
Dhima ya kwanza mwilini, yatusitiri mavazi.
Mitindo tumeizua, kuweka wazi matumbo,
Yatatoka kwenye pua, kuigaiga wa mombo,
Laiti tungalijua, tungalivaa masombo,
Dhima ya kwanza mwilini, yatusitiri mavazi.
Mitindo ikiingia, twanata kama ulimbo,
Bila ya kufikiria, thamani ya letu umbo,
Hapo tunang'ang'ania, na kuleta majigambo,
Dhima ya kwanza mwilini, yatusitiri mavazi.
Uzungu watuzuzua, kwa mitumba yenye shombo,
Jambo ninaloshangaa, hivi tumelewa tembo?
Maungo kujiachia, wanzuki ama zarambo?
Dhima ya kwanza mwilini, yatusitiri mavazi.
Mtu aliyetimia, kichwa, mabega na tumbo,
Akili akatumia, kung'amua haya mambo,
Hawezi kuangukia, pasipo kuramba bambo,
Dhima ya kwanza mwilini, yatusitiri mavazi.
Siwezi kuendelea, nanga nakitia chombo,
Jambo hilo shikilia, acha kuiga wamombo,
Mbona wewe twakujua, umezaliwa Matombo?
Dhima ya kwanza mwilini, yatusitiri mavazi.
Kwa tatizo yake dawa, uanze kulisakama,
Mwishowe kulitatatua, kwa busara na hekima,
Wako moyo utapowa, furaha ukiifuma,
Halina thamani chozi, aliniusia mama.
Wakati tukifiliwa, mfano baba na mama,
Moyo hutaki kutuwa, machozi hujaa pima,
Vipi wanafufuliwa? mwisho vichwa vyatuuma,
Halina thamani chozi, aliniusia mama.
Tupatapo mitihani, ya mabonde na milima,
Mikono huwa kichwani, tulie olele mama,
Mwisho tunapata Soni, kulia mtu mzima,
Halina thamani chozi, aliniusia mama.
Nilikuwa bado kinda, alipofariki mama,
Kilio sikukishinda, nililia Kama kinda,
Huku kule nilikwenda, yani aamke mama,
Halina thamani chozi, aliniusia mama.
Siku niliyoamini, chozi halina salama,
Yangu hapo sithamini, kulivisha koja jema,
Machozi ni kitu duni, aminj ninayosema,.
Halina thamani chozi, aliniusia mama.
Kwa heri wanazuoni, ndugu zangu maulama,
Nimefika ukingoni, ndiyo yangu kaditama,
Kulialia ya nini, bure kujitia homa?
Halina thamani chozi, aliniusia mama.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704]]>falseMwlMaeda]]>2022-07-30T10:16:09Z2022-07-30T10:16:09Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2796
haloo!hanii halo, Rwaka hani wasikia?
Ndio hapo sawa halo, vipi unaendelea?
Tatizo nililonalo, lazizi ninaugua,
Hani nipo kitandani, taabani hali yangu.
Wala sijahama njia, nitafika huko Rwanda,
Ikinijia afia, na wangu mwili kuwanda,
Basi huko nitatua, unione mie kinda,
Sasa nipo kitandani, taabani hali yangu.
Ila ninayo pumzi, bado moyo unahema,
Bora nikweleze wazi, kinifanyacho kukwama,
Matatizo ya uzazi, ndiyo yaloniandama,
Jua nipo kitandani, taabani hali yangu.
Ina machungu dunia, na mie yamenikuta,
Nusu niage dunia, kwa tumbo kunikeketa,
Japo nimeamkia, bado najivutavuta,
Ila nipo kitandani, taabani hali yangu.
Maradhi yanaghasia, Karagama sikiliza,
Yakishakuangukia, dira unaipoteza,
Mwilini nimelegea, vile nimepata siza,
Love nipo kitandani, taabani hali yangu.
Nitahama nikipona, Tanzania sitarudi,
Na wewe tukionana, itatulia fuadi,
Ila sasa raha sina, Darling I feel bad,
Vile nipo kitandani, taabani hali yangu.
Namshukuru Karima, ningali hai mpenzi,
Ninaungoja uzima, japo kutwa nakuenzi,
Ningelikufa mapema, ungelipata simanzi,
Hapa nipo kitandani, taabani hali yangu.
Na mie napata ganzi, nikikukosa kijana,
Heri kunipiga konzi, utosini nitapona,
Sitahimili majonzi, na wewe tukikosana,
Japo nipo kitandani, taabani hali yangu.
Maumivu yamezidi, yanikataza kutunga,
Kuacha imenibidi, utungo huu kufunga,
Ila ninakuahidi, huko Rwanda nitatinga,
Nikitoka kitandani, iwe njema hali yangu.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704]]>falseMwlMaeda]]>2022-07-27T18:17:07Z2022-07-27T18:17:07Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2793
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi,
Huko awako gizani, mbona ya Mana hayawi,
Pasi na nguo mwilini, lake baridi mchawi,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Mchawi hupenda tabu, hapendi mambo rahisi,
Kona anaziharibu, apite kwa wasiwasi,
Mlangoni hajaribu, apite kwa urahisi,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Yake kazi kuharibu, akageuza kizazi,
Ili unapojaribu, huoni chako kizazi,
Hapo hawana sababu, mambo yao ni ushenzi,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Japo yu mtu mkubwa, chamani kuheshimika,
Tabiaye kama mbwa, anapotaka kuruka,
Na baridi atakumbwa, hana nguo kujivika,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Juzi nilipata kesi, mtu katiwa kifafa,
Matabibu na manesi, wakadhani amekufa,
Mwisho katoa kamasi, tukagundua hajafa,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Mchawi akifahamu, una kitu kumzidi,
Jua umejipa sumu, kukuroga hana budi,
Utateswa kwa awamu, ukuishe ukaidi,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Msiwaone vichaa, kidhani yote ya Mumba,
Wengine tukashangaa, ovyo waanza kuimba,
Wachawi walishakaa, kuchanganya mitishamba,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Mtu umesoma sana, Mara vyeti huvioni,
Kumbe walishagawana, watandike kaburini,
Miaka kazi hauna, uchawi ni ushetani,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Machawi yake hasara, ulie yeye acheke,
Wala haimpi fora, hadharani asifike,
Kiumbe mwenye mikwara, japo asifaidike,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Mchawi mtu wa ila, mambo yake ni kinyume,
Usiku sie twalala, yu uchi atutazame,
Na hawi tajiri wala, kiwa wongo na aseme,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Sasa ninafunga beti, utungo siendelezi,
Msijenishika shati, ati nimewapa kazi,
Naona bora niketi, kuandika nimesizi,
Jamani niambieni, akipatapacho mchawi.
Usidhani nalalama, nijinadani mnadani,
Moyo wangu unauma, Mimi nicheze na nani?
Au simu ulizima, upo kwea kitandani?
Naingoja simu yako!
Sio mwingi wa lawama, nakuomba samahani,
Kwakowe nimetuama, kama somba mtungoni,
Haki kwako nimekwama, mithili mwiba kooni,
Naingoja simu yako!
Basi uamke vema, pasi mavune mwilini,
Nakungoja mtu mwema, unijuze hali gani,
Hamu bado hijakoma, kukusubiri mwendani,
Naingoja simu yako!
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704]]>falseMwlMaeda]]>2022-07-22T02:23:03Z2022-07-22T02:23:03Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2787
Mwenzenu nipeni rai kwa haya yalonifika
Moyo wangu haukai, kwa hapa nilipofika
Japo naona nishai, moyoni nimewatika
Kati ya hawa wawili, Nipende nani zaidi?
Huyu wa kwanza mpole , tena si muongeaji
Kama simba mwenda pole, kwenye ufatiliaji
Hutembea polepole ,amdake mwiwindwaji
Kati ya huyu nayule jama nimpende nani?
Huyu wa pili mweusi , kapanda juu kidogo
Mwenye pua ya kitusi, mwili mwembamba kidogo
Mtalamu wa kukisi,utadhania mgogo
Kati ya huyu na yule ,jama nimpende nani?
Akili inanituma , wa pili awe mwandani
Ninategemea mema ,sitotoka asilani
Kama ikiwa salama ,nitasota uvunguni
Kati ya hawa wawili Nimpende nani?
Nilikuwa na furaha,nimefika maskani
Nikayaanza madaha, nikavipata vya ndani
Nilishazika karaha,ninapokuwa chumbani
Alivyokuja wa pili , Moyo wangu umeshindwa
Wa pili yeye mcheshi , muda wote tabasamu
Ni kweli kuwa achoshi ,twacheka kama binamu
Kwangu hamu haiishi, jama mpeni salamu
Kati ya Hawa wawili nimpende nani?
Wa kwanza ananijali, kwa pesa nayo mahaba
Nikimuuzi hajali, hunilea kama baba
Na hunijulia hali, upendowe sio haba
Wanagenzi mnijuze nimpende yupi?
Rama karibu javini , unipe jibu murua
Na wengine karibuni, jibu nataka kujua
Nitomuweka moyoni, kofuli kumfungia
Kitendawili tegua Yupi kwangu anafaa?
DINNA ( MOM J )
21/7/22
KUWA TAYARI KUHESABIWA
MPE USHIRIKIANO KARANI WA SENSA??]]>falseMwlMaeda]]>2022-06-13T03:21:04Z2022-06-13T03:21:04Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2598 KUJUWA NI MATATIZO
Lugha yangu ya asili, niijuavyo si haba, najivuniayo sana Lakini hii ya pili, ni Kizungu chanikaba, uwelevu nayo sina Ndipo juzi Jumapili, akanitanza swahiba, tukaanza kuvutana Aliniambia: Silly!, nikadhani anshiba, kumbe yuwanitukana! Kuelewa ni kuzuri, hukukinga na kujuta, ukawa hutazozana Hukupunguza kiburi, ukadharau kuteta, ukapenda kushikana Ja vile kaka Saburi, alivyonitia tata, mpaka nikadangana Na nilipomshauri, aliponambia: Better, hapo hapo nikakona Si mjinga kama gude, huzitumia fikira, nawambia muelewe Bao latezwa kwa ndude, na kazi ni za majira, yakupasa uyajuwe Nenda skuli 'sidode, ujinga una izara, yasikufike na wewe Naliambwa: Hey dude!, nikajibu kwa hasira:, Na wewe dude mwenyewe! Kujiweka nyumanyuma, jambo hilo likataye, usiwatwe mkiani Utafanyiwa hujuma, wenzako wakukimbiye, uulize: Kulikoni? Jana mimi nilikwama, nikasema nimwambiye, hanong'ona sikioni Akasema: Don't murmur, hasema: Mama nnaye, sijui wateka nini! Kimombo tulokikopa, kina sisi chatuuma, chatukutisha madhila Kisa hiki ningakupa, japokuwa chanitoma, kina funzo la sahala Sima twali twaichapa, akaingia Fatuma, akatuona tukila Akanita: Juma's papa, hamba: Papa si wa Juma, lakini waweza kula Mohamed Khamis. Takaungu, Kenya 12.6.2022]]>falseMwlMaeda]]>2022-05-05T06:48:50Z2022-05-05T06:48:50Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2542
Usifurahi mwanzoni, kauli huikumbuki?
Yule mtunga diwani, alisema kitu hiki,
Sasa umekuwa nyani, umezua taharuki,
Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila.
Kutunga nimekawia, kwa shibe sitamaniki,
Juzi ulisimulia, una wengi marafiki,
Sifuri umeambua, na nyumbani hubanduki,
Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila.
Yalizidi maakuli, jambo hili liafiki,
Tukajaziwa bakuli, pilau nyama na siki,
Na ule mweupe wali, ukaliwa kwa samaki,
Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila.
Wale wapenda mtindi, hawakukosa wanzuki,
Tulikesha kama bundi, hadi mida ya mswaki,
Watu vikundi vikundi, tukaisahau dhiki,
Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila.
Mdomo waacha wazi, kwa hili unahamaki,
Wajawe wanakuhizi, vile unavyojinaki,
Na ujuwe siku hizi, marafiki wazandiki,
Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila.
Sasa wakuna sharubu, kimepita kitu hiki,
Imekufika taabu, hakuna wakukulaki,
Njaa ilikuadhibu, na kwako vile hupiki,
Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila.
Kijiko umenunua, ukiwa mwenye mithaki,
Kesho wenda kujilia, kula kwako hukumbuki,
Mee! sasa unalia, umenuna haucheki,
Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila.
Lifika kukusalimu, na hapa kwako sibaki,
Ilivyonifika hamu, viporo vilivyobaki,
Nikale mbuzi kwa ndimu, na leo kwangu sipiki,
Idd tumekula sisi, pole yako Makanyila.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704]]>falseMwlMaeda]]>2022-04-15T19:18:53Z2022-04-15T19:18:53Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2512
Ngoma hizi mchezazo, hali wazi maungoni,
Zinaleta angamizo, mnadhani hatuoni?
Basi zitiwe katazo, hivi mwatufunza nini?
Vikemeeni vigoma.
Kina mama hususani, lawama nawangushia,
Nauliza mwafanyani, ngomani mkisogea?
Kujitia fedhehani, nasi tukiangalia,
Hivi twajifunza nini?
Enyi wapiga vigoma, kina baba maarufu,
Sikieni ninasema, acheni huo uchafu,
Mnatutia kilema, tusiwe waadilifu,
Acheni hiyo tabia!
Serikali Mtukufu, uliye chombo imara,
Ondoeni usumbufu, maadili wanopora,
Taifa hulikashifu, adabu ikose dira,
Kamateni wachezaji.
Wachezavyo ni hatari, sikia habari hizi,
Vyote viungo vya Siri, twaviona siku hizi,
Hata nyie mtakiri, walikofika walezi,
Sheria zichukuliwe.
Yanatufika madhila, watoto tutazameni,
Tunalala bila kula, walezi wapo ngomani,
Ndoani amani Wala, tunabaki madharani,
Watoto tunateseka.
Taona barabarani, wameunda misafara,
Watoto nao njiani, hujiunga misafara,
Hivi wanapata nini, kiongezacho fikira?
Washitakini Wazazi.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704]]>falseCosmas shukuru]]>2022-04-07T21:35:13Z2022-04-07T21:35:13Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2504falseMwlMaeda]]>2022-04-04T02:04:34Z2022-04-04T02:04:34Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2497
Ni usiku saa nne,
Huu ni mwezi wa nne,
Tumefunga goli nne,
Simba Robo Fainali.
Ndege tutazidi panda,
Jinsi tunazidi shinda,
Hata dau linapanda,
Simba Robo Fainali.
Wachezaji hongereni,
Na makocha hongereni,
Viongozi pongezini,
Simba Robo Fainali.
Katika ukanda huu,
Simba ndiyo timu kuu,
Katika mpira huu,
Hiyo Robo Fainali.
Siyo Kombe la Azam,
Hiyo pokea salam,
Huko kwa wataalam,
Simba Robo Fainali.
Ni Simba ya Tanzania,
Robo imeshaingia,
Heri tunaitakia,
Izidishe kwenda mbali.
Robo fainali CAF,
Simba timu maarufu,
Ni mpira maradufu,
Chaenea Kiswahili.
Na Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602]]>falseMwlMaeda]]>2022-04-02T14:18:48Z2022-04-02T14:18:48Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2494
Mapenzi anayejua, kwa hili simshangazi,
Haya yakishakutua, kukung’uta hauwezi,
Vile hukung’ang’ania, kama chawa kwenye vazi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.
Miaka imekimbia, tutengane na lazizi,
Fikirani hunijia, kumkataza siwezi,
Picha inanirudia, m atukio ya miezi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.
Heri angekuwa Tanga, Shinyanga kwenda siwezi,
Uchumi unanizinga, huko mbali sikatizi,
Sasa nimebaki bunga, sioni lenye tatuzi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.
Niliapo ni msiba, hayakatiki machozi,
Uso wangu nauziba, nizuie michirizi,
Haki nimekuwa zoba, mwenyewe ninajihizi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.
Jambo linaniumiza, mtu huyo ni mzazi,
Ameoa naeleza, na watoto kwa mashazi,
Ijapo najikataza, kufanya makumbukizi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.
Nikiona zake picha, mimi chali sijiwezi,
Nawaza kila kukicha, nimezidi siku hizi,
Roho yanambia ‘acha’, ila moyo mchokozi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.
Tatizo wake upole, kufoka huyu hawezi,
Nakumbuka siku zile, mweledi wa mapepezi,
Basi ilikuwa vile, bila yeye sijilazi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.
Bwana huyu mtalamu, mithili kaenda kozi,
Yake mabo ni matamu, hadharani sielezi,
Ni kama mbuzi kwa ndimu, alikuwa mganguzi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.
Yana ajabu mapenzi, yakianza hayasizi,
Marefu kama utenzi, wenye beti jozi jozi,
Na ukiwa mwanafunzi, hutaweza piga mbizi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.
Nilidhani Mjaluo, kwa urefu mchokozi,
Weusi wenye vutio, afaa kwa matumizi,
Nikakiweka kituo, kwake sikupitilizi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.
Kijana wa Kimanyema, kiliko chake kizazi,
Ni mkoani kigoma, Tabora yake makazi,
Kwa sasa ameshahama, yupo Shinyanga kikazi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.
Kweli mahaba huua, kwa hili sibishilizi,
Nimekonda hadi pua, sijisifu siku hizi,
Heri zirudi hatua, hadi kwenye mwakajuzi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704]]>falseMwlMaeda]]>2022-03-02T02:03:37Z2022-03-02T02:03:37Zhttps://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2418
1. Mwendani wako mwendani, ukitaka umjuwe
Ngia naye safarini, mwenende mwendo wa kuwe
Au muate nyumbani, ukatembee ukawe
Akosapo kuwa mwewe, huyo ni wako mwendani
2. Mwendani wako mwendani, ukitaka mjuato
Mpishe ndia zenye mwani, zenye miba na tototo
Au mbwagie zani, ambayo kwamba ni nzito
Akuonyapo mapito, huyo ni wako mwendani
Kwa tatizo yake dawa, uanze kulisakama,
Mwishowe kulitatatua, kwa busara na hekima,
Wako moyo utapowa, furaha ukiifuma,
Halina thamani chozi, alinihusia mama.
Wakati tukifiliwa, mfano baba na mama,
Moyo hutaki kutuwa, machozi hujaa pima,
Vipi wanafufuliwa? mwisho vichwa vyatuuma,
Halina thamani chozi, alinihusia mama.
Tupatapo mitihani, ya mabonde na milima,
Mikono huwa kichwani, tulie olele mama,
Mwisho tunapata Soni, kulia mtu mzima.
Nilikuwa bado kinda, alipofariki mama,
Kilio sikukishinda, nililia Kama kinda,
Huku kule nilikwenda, yani aamke mama,
Halina thamani chozi, alinihusia mama.
Siku niliyoamini, chozi halina salama,
Yangu hapo sithamini, kulivisha koja jema,
Machozi ni kitu duni, aminj ninayosema,.
Halina thamani chozi, alinihusia mama.
Kwa heri wanazuoni, ndugu zangu maulama,
Nimefika ukingoni, ndiyo yangu kaditama,
Kulialia ya nini, bure kujitia homa?
Halina thamani chozi, alinihusia mama.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704]]>false