MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Semi]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ Mon, 29 Apr 2024 15:48:25 +0000 MyBB <![CDATA[MAANA YA METHALI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2794 Fri, 29 Jul 2022 04:04:13 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2794 MAANA YA METHALI
Wataalamu mbalimbali wamejaribu kutoa fasili ya maana ya methali. Mazrui na Syambo (1992), methali ni misemo mifupi yenye hekima fulani. Wamesisitiza kuwa methali hudhihirisha mkusanyiko wa mafunzo waliyopata watu wa vizazi vingi vya jumuiya wanayoishi katika maisha yao. Aidha, wameongeza kusem kuwa methali ni sehemu moja ya lugha inayoweza kubaini falsafa ya watu fulani kuhusu maisha kwa ujumla.
Ngole na Honero (1981), wamesema kuwa methali ni aina ya usemi mzito na ambao unakusudiwa kusema jambo maalumu kwa njia ya fumbo. Methali hukusudiwa kumuonya, kumuongoza na kumuadilisha mwanadamu katika maisha yake. Aidha, kwa umbile la nje methli huwa na muundo wa pande mbili. Upande mmoja wa methali hueleza mazoea au tabia ya watu au kitu katika utendaji wa jambo. Upande wa pili wa methali hueleza matokeo yaliyosababishw na mazowea au tabia iliyoelezwa katika upande wa kwanza.
Murega (2015), ameona kuwa methali ni semi fupi ya kimapokeo yenye muundo mahsusi na iliyo na fumbo amblo linapofasiliwa  hupata maana mbalimbali hutegemea muktadha na hali halisi ya maisha ya watumiaji.
Wamitila (2001), ameeleza kuwa methali ni msemo unaojitosheleza, wenye maana yenye nguvu au uzito, wenye muundo au sifa za kishairi, unaokusudiwa kuadibu au kuelekeza, kuelimisha, kushauri na kadhalika.
Kutokana na fasili za wataalamu hao, tunaweza kusema kuwa methali ni aina ya usemi mzito unaoelezea wazo pana kwa muhtasari ukiwa na umbo mahsusi na unaotumia uzowefu wa jamii kuonya, kuadilisha na kufunza kwa kuzingatia miktadha maalumu. Methali hutumia hekima, uficho wa kauli, usanii w kimsamiati, uzowefu wa matukio katika jamii na falsafa ya jamii katika mitazamo ya masuala mbalimbali ambayo huakisi maisha na utamaduni wa jamii husika.
]]>
MAANA YA METHALI

<![CDATA[METHALI NA MAANA ZAKE]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2447 Sun, 06 Mar 2022 09:50:14 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2447
  1. Aliye juu mngoje chini: Inatukumbusha kuwa na subira na kukubali pale ambapo mwenzio amekuzidi nafasi fulani basi hauna budi kumheshimu.
  2. Kamba hukatikia pembamba: Kamba ni kitu chochote kinachotumika kufungia vitu mathalani kuni n.k. Ili uweze kulitatua jambo fulani ni vyema ukaangalia penye udhaifu ili usitumie nguvu kubwa.
  3. Jungu kuu halikosi ukoko: Ni kawaida kuona chakula kikipikiwa kwenye vyungu vikubwa na masalia ya chakula hasa ukoko kubaki. Watu wenye hekima na wazee hawakosi neno la kutia kwenye mazungumzo. Watu wanapaswa kuomba ushauri kwa watu wazima wakati wowote ili wapate msaada wa mawazo kwa watu wazima au viongozi watakuwa na jambo la kusema.
  4. Akumulikaye usiku, mchana atakuchoma:Mzaha unaweza kusababisha jambo halisi kutokea. Katika maisha kuna watu wanaweza kukutishia halafu ukapuuzia, usipuuze kwa sababu anaweza kuwa anamaanisha au kama mtu ana uwezo wa kukusema vibaya mbele yako basi anaweza kukusema zaidi ukiwa ufahamu
  5. Kidole kimoja hakivunji chawa: Ushirikiano ni jambo la msingi katika kufanikisha jambo lolote lile. Ukifanya peke yako mambo yanakuwa magumu kama vile ambayo ni vigumu kumchukua chawa ukataka kumuua kumuua kwa kidole kimoja.
  6. Mwenda pole hajikwai: Kufanya jambo bila haraka kunasababisha jambo kufanyika kwa ufanisi zaidi kwa kuwa mawazo kufikiria vyema.
  7. Figa moja haliinjiki chungu: Figa ni jiwe kitu kinachotengenezwa ili kushikilia chungu au sufuria ikiwa jikoni. Huhitajika mafiga matatu na si moja. Hivyo, ili kufanya jambo ni sharti kuwe na ushirikiano wa watu. Ona pia methali kama; kidole kimoja hakivunji chawa
  8. Akiba haiozi: Methali inasisitiza umuhimu wa kuweka akiba ya kitu mathali fedha, chakula na vingine kwa matumizi ya baadaye.
  9. Aliyeshiba hamjui mwenye njaa: Njaa ni hali ya kuhitaji chakula au haja ya kufanya kitu fulani. Mtu asiye na haja ya jambo fulani haoni umuhimu wa kitu hicho kama ambavyo mwenye haja nacho aonavyo haja ya kukipata. Maana yake ni kwamba watu huwa hawajali haja na mahitaji ya watu wengi. Ni vyema kujali watu wengine.
  10. Sikio la kufa halisikii dawa: Hakuna awezaye kukizuia kifo, hivyo kikitaka kuja hakuna namna ya kukizua. Kuna mambo ambayo hufikia katika kiwango ambacho hayawezi kubadilika bila kujali nguvu itakayotumika, kwahiyo huachwa kama lilivyo.
  11. Lisemwalo lipo, kama halipo laja: Kuna maneno husemwa na wakati mwingine sio ya kweli. Hata hivyo ni vigumu kusema tu mambo ambayo hayapo, kwahiyo ni vyema kuyatilia maanani mambo yasemwayo kwani huwa na ukweli fulani ndani yake.
  12. Mwacha asili ni mtumwa: Ni vyema mtu akapathamini kwao kwa sababu ndipo alipotokea na kumemfanya kuwa vile alivyo. Ni vyema kuendelea kulinda yanayohusiana na wewe badala ya kukumbatia mambo yasiyo ya asili yako. Ni vyema kukumbuka kwenu.
  13. Ukitaka kuruka, agana na nyonga: Nyonga ni viungo muhimu katika ya miguu na kiuno. Viungo hivi hushirikiana katika jambo lolote mathalani kutembea, kukimbia n.k. Unashauriwa kufanya maandalizi ya kutosha kabla ya kufanya jambo au kitu chochote. Hakikisha umelichunguza jambo au maamuzi unayotaka kuyachukua ili baadaye usijutie uliyofanya.
  14. Adhabu ya kaburi aijua maiti: Hakuna mtu yeyote anayefahamu maswahibu ya kaburi isipokuwa maiti iliyozikwa mule. Kuna mambo ni vigumu mtu kuyafahamu kama si mhanga wa jambo hilo. Mathalani, kuna watu hupitia changamoto kama maradhi ambayo maumivu yake hakuna anayeweza kuyahisi zaidi yake kwa sababu yeye ndiye mhusika.
  15. Mficha uchi hazai: Uchi ni siri. Ni sehemu ambazo hazipaswi kuwa hadharani hivyo zinapaswa kuficha kama sehemu za siri. Hata uchi ni kuwa wazi kwa hiyo, ni vyema kuwa muwazi katika mambo mbalimbali ili uweze kupata msaada. Si vyema kuwa na jambo linakuumiza halafu usileweke wazi ili usaidiwe.
  16. Zimwi likujualo halikuli likamaliza: Ndugu au rafiki anaweza kukuonea katika jambo fulani hasa adhabu, kukudhulum na mengine kwa sababu anakufahamu.
  17. Ukubwa ni jalala: Jalala ni mahali ambapo uchafu na takataka za aina mbalimbali hutupwa. Ukiwa mtu mzima au mwenye mamlaka fulani kuna mambo mengi yatasemwa kukuhusu. Utapongezwa, wakati mwingine utalaumiwa, utakejeliwa na mambo yanayofanana na hayo. Usitetereke wala kukata tamaa, ni hali ya kawaida.
  18. Kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi: Uhunzi ni kazi ya kufua na kutengeneza vyuma na koleo ni kifaa kinachotumika kuchotea maka na kuweka kwenye tanuru. Kuna mambo, vitu na watu ambao huwezesha na kuwa mhimili shughuli au kazi fulani na yanapotoweka basi hudhaniwa kuwa ndiyo mwisho jambo ambalo si sahihi. Ikitokea changamoto ni vyema kuitatua na kusonga mbele. Mfano, katika kampuni au familia mtu muhimu akiondoka haimaanishi na shughuli zikome. Itafutwe namna nyingine ya shughuli na majukumu mengine kuendelea.
  19. Baada ya dhiki, faraja: Dhiki ni matokeo ya hali ngumu ya maisha au tukio fulani. Licha ya mambo magumu mtu anayopita hakuna shaka kwamba hayo yatapita na wakati wa furaha utafika. Kuna wakati unatafuta mafanikio katika mazingira magumu bila kupata, usikate tamaa kwani ipo siku utayapata na utakuwa katika wakati wa furaha.
  20. Dua la kuku halimpati mwewe: Kwa kawaida mwewe ni adui wa kuku kwa kuwa hula vifaranga. Inawezekana kuku humuombea mabaya mwewe ili asiwadhuru vifaranga lakini huwa ni vigumu yale anayoyaomba. Kuna mambo watu huwaombea wengine mabaya au wakati mwingine kuwalaani, ukweli ni kwamba mambo hayo hayawezi kutokea ikiwa Mungu hajapanga yakutokee.
  21. Mtegemea cha ndugu hufa maskini: Sio tabia nzuri kutegemea kusaidiwa kila wakati hasa na ndugu au rafiki au watu wengine. Ni vyema kuinuka na kufanya kazi au chochote kuwezesha kupata kipato au kitu chake kuliko kutegemea kupewa kila mara kwa sababu havutakusaidia sana.
  22. Usimwage mtama kwenye kuku wengi: Ni wazi kuwa ukimwaga mtama penye kuku wengine ni lazima kutatoka mtafaruku wa hali juu na pengine wasiweze kuufaidi huo mtama. Kuna mambo ambayo ni siri, hivyo si vyema kuyasema mahali penye watu wengi. Ikiwa kuna siri au jambo ambalo si la kuweka wazi mbele ya watu basi mtoe mhusika pembeni umwambie.
  23. Penye wengi pana mengi: Kila binadamu ana utashi wake na tabia yake humfanya afanye tukio au jambo fulani. Kwasababu kila mtu ana tabia yake, matukio pia yatatofautiana. Wakikutana watu wengi wenye tabia tofautitofauti, mambo mengi yanaweza kutokea mathalani, wizi, ugomvi, ushirikina, ulevi na mambo kama hayo.
  24. Haba na haba, hujaza kibaba: Haba ni kiasi kidogo. Ukikusanya kiasi kidogokidogo mwisho kitakuwa kikubwa. Methali hii inataka watu kuwa wavumilivu na kujiwekea akiba kidogokidogo mpaka pale ambapo kiasi kikubwa kitakapotokea.

<![CDATA[TUTEGUE KITENDAWLI : NENO MAITI IKO KATIKA NGELI IPI?]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1366 Mon, 25 Oct 2021 03:51:10 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1366 Mojawapo ya nomino ambazo ngeli zake zina kutokubaliana kwingi miongoni mwa
wanasarufi wa Kiswahili ni ‘maiti’. Walimu na wapenzi wengine wa sarufi ya Kiswahili
huchelea kuelezea kwa hakika mahali pa ‘maiti’ katika mfumo mpya wa uainishaji wa
ngeli uitwao upatanisho wa kisarufi.
MOJAWAPO ya nomino ambazo ngeli zake zina kutokubaliana kwingi miongoni
mwa wanasarufi wa Kiswahili ni ‘maiti’. Walimu na wapenzi wengine wa sarufi ya
Kiswahili huchelea kuelezea kwa hakika mahali pa ‘maiti’ katika mfumo mpya wa
uainishaji wa ngeli uitwao upatanisho wa kisarufi.
Binafsi, nimewahi kukabiliwa na swali lihusulo ngeli ya nomino ‘maiti’ ingawa
jawabu langu kwa kawaida huambatana na maelezo marefu ambayo dhamira yake
ni kujaribu kuutilia nguvu mwegemeo wangu. Ninadhani hata wewe umewahi
kukumbana na hali sawa na hiyo!
Kwa muhtasari, uainishaji wa ‘maiti’ kingeli una uambaji ngoma wa aina mbili
kama zilivyo ngeli nyingine kadhaa. Wanasarufi fulani hudai kwamba nomino hiyo
inapaswa kuingizwa katika ngeli ya ( I-ZI) ilhali wenye maoni tofauti hushikilia
kwamba inapaswa kuwa katika ngeli ya (A-WA ). Sababu zitolewazo na
wanasarufi hao kuhusiana na misimamo yao, ukisikiliza kwa makini, utaona
kwamba zina mashiko ya aina fulani.
Awali , nilieleza kwamba vipo vipengele vingine ambavyo vinaweza kuchukua
mkabala- kati ila si suala la ngeli! Haiyumkiniki kudai kuwa nomino moja inaweza
kuingia katika ngeli mbili tofauti. Kwa hivyo, kinachohitajika ni ukubalifu kuhusu
mahali pa nomino yenyewe katika mfumo mpya wa uainishaji wa ngeli bali si
maelezo marefu ya kushawishi.
Katika makala haya, ninadhamiria kuonyesha sababu mbalimbali zinazowafanya
wenye mikabala miwili tuliyoitaja kuliweka neno hilo katika ngeli mbili tofauti.
Baadaye, nitapendekeza njia ambayo kwayo utata huo unaweza kutatuliwa.
Wanaoshikilia msimamo wa A-WA wanatoa sababu kadha zinazoelekeza mtazamo
wao. Wanatumia methali za jadi zilizotumia nomino maiti pamoja na tamaduni
nyingine zinazohusiana na sherehe za matanga na mazishi ya Waswahili
kushadidia madai yao. Wanadai kwamba methali hizo zimetumia kirejeshi (ye) na
viwakilishi nafsi – ambata ‘u’ au ‘a’ kurejelea maiti. Viambishi hivyo hujitokeza
katika ngeli ya A-WA katika hali ya umoja. Baadhi ya methali hizo ni pamoja na:
(1) Adhabu ya kaburi aijuaye maiti.
(2) Maiti haulizwi sanda.
(3) Aibu ya maiti aijuaye mwosha.
Kwa mujibu wa mila na itikadi za Waswahili, inasemekana kwamba kisomo
anachosomewa maiti kaburini mara tu baada ya kuzikwa huitwa talkini. Hapa,
kiambishi ‘a’ katika neno ‘anachosomewa’ hurejelewa na kudaiwa kwamba kunayo
sababu maalumu iliyowafanya Waswahili kutotumia kiambishi kiwacho chochote
kile mathalan (i) ya upatanisho wa sarufi katika ngeli ya ( I-ZI), na badala yake
kutumia kiwakilishi nafsi-ambata ( a).
Sababu nyingine itolewayo kuunga mkono madai ya wanasarufi hao ni ile ya
heshima au uluwa. Wanasema kwamba ijapokuwa maiti hana uhai, heshima yake
bado ingalipo na ndiyo sababu hufanyiwa mazishi maalumu. Kwa mantiki
hiyohiyo, methali, ‘Mimi mbega nafa na uzuri wangu’ hutumiwa kushadidia suala
hilo la heshima ya maiti.
Aidha, majina ya heshima ambayo huendelea kutumiwa na walio hai kumrejelea
aliyeaga dunia miaka mingi baadaye ni ushahidi mwingine unaoelezea sababu ya
kuwekwa kwa nomino maiti katika ngeli hiyo. Majina hayo ni ‘marehemu’ na
‘hayati’. Tunasema, ‘Marehemu kakangu alikuwa muungwana sana au ; Hayati
Mwinyihatibu alitufanyia mambo mengi’. Ushahidi mwingine utolewao kuunga
mkono msimamo huo, ni ule wa kuwepo kwa kisawe cha maiti; mfu, ambacho
hutumia kiwakilishi nafsi-ambata ( a). Tunasema, ‘Mfu amezikwa’ wala si ‘mfu
umezikwa’
Wanasarufi wenye msimamo wa pili hudai kuwa maadamu hamna uhai na hisia
katika maiti; kigezo muhimu kielekezacho uingizwaji wa nomino katika ngeli ya
A-WA, basi nomino hiyo inapaswa kuingizwa katika ngeli ya (I-ZI) kama vilivyo
vitu vingine vingi ambavyo havina uhai. Wanasarufi hao wanaendelea kudai
kwamba haiyumkiniki kudai, ‘Maiti wake atazikwa kesho’ ila tutasema, ‘Maiti yake
itazikwa kesho.’ Maoni ya wanasarufi hawa ni kuwa maiti ‘inapaswa’ kuchukuliwa
kama nomino yenziwe mzoga ambayo iko katika ngeli ya U-I. Wanaendelea kudai
kwamba suala la heshima lina umuhimu mdogo likilinganishwa na ‘uhai’ na ‘hisia’.
Ipo haja ya kuafikiana kuhusu ngeli moja ya nomino ‘maiti’ na nyingine kadha
zenye utata. Ili kufanikiwa kufanya hivyo, jambo moja linapaswa kupewa kipau
mbele: Kuzibwaga imani na misimamo ambayo tumekuwa nayo kwa muda mrefu
kuhusiana na nomino husika na kuwa radhi, kukumbatia mjadala na kujifunza
upya.
]]>
Mojawapo ya nomino ambazo ngeli zake zina kutokubaliana kwingi miongoni mwa

<![CDATA[Matumizi ya Lugha Katika Vitendawili]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1232 Fri, 10 Sep 2021 13:30:02 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1232
.pdf   Matumizi ya Lugha Katika Vitendawili.pdf (Size: 80.52 KB / Downloads: 3) ]]>

<![CDATA[FAHAMU MAANA ZA MANENO HAYA]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1215 Fri, 10 Sep 2021 08:41:47 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1215
.pdf   FAHAMU MAANA ZA MANENO HAYA.pdf (Size: 206.36 KB / Downloads: 4) ]]>

<![CDATA[VITENDAWILI NA MAANA ZAKE]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1059 Sun, 29 Aug 2021 08:16:36 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1059 A
1. Adui lakini po pote uendako yuko nawe. Inzi
2. Afahamu kuchora lakini hajui achoracho. Konokono
3. Afuma hana mshale. Nungunungu
4. Ajenga ingawa hana mikono. Ndege
5. Ajifungua na kujifunika. Mwavuli
6. Akitokea watu wote humwona. Jua
7. Akitokea watu wote hunungunika na kuwa na huzuni. Ugonjwa
8. Akivaa nguo hapendezi, akiwa uchi apendeza. Mgomba
9. Alipita mtu ana bunda la mshale. Mkindu
10. Alipita mtu mwenye kibandiko cha nguo. Inzi
11. Aliwa, yuala; ala, aliwa. Papa
12. Amchukuapo hamrudishi. Kaburi
13. Amefunika kote kwa blanketi lake jeusi. Giza
14. Amefunua jicho jekundu. Jua
15. Ameingia shimoni akiwa uchi, akatoka amevaa nguo nzuri. Mbegu
16. Amejitwika mzigo mkubwa kuliko yeye mwenyewe. Konokono/Koa
17. Amekaa kimya na watoto wamemzunguka pande zote. Mgomba
18. Amekula ncha mbili. Wali
19. Amevaa joho kubwa kuliko yeye mwenyewe. Kaburi
20. Anakuangalia tu wala halali au kutembea. Picha
21. Anakula kila siku lakini hashibi na hatashiba. Mchanga
22. Anakula lakini hajashiba na hatashiba milele. Ardhi
23. Anakula lakini hashibi. Mauti
24. Anapendwa sana ingawaje ni mkali sana. Moto
25. Anatoka kutembea, anakuja nyumbani anamwambia mama, ‘Nieleke’. Kitanda
26. Ashona mikeka wala hailali. Maboga
27. Askari wangu wote wamevaa kofia upande. Majani
28. Askari wangu wote wamevaa mavazi meusi. Chunguchungu
29. Asubuhi atembea kwa miguu mine, adhuhuri kwa miwili. Fedha
30. Atapanya mbegu nyingi sana lakini hazioti. Mvua
31. Atolewapo nje hufa. Samaki
B
32. Baba alinipa mfupa, nikautunza ukawa fahali. Muwa
33. Baba ameweka mkuki nje nikashindwa kuukwea, mdogo wangu akaukwea. Sisimizi
34. Babako akojoapo hunung’unika. Mawingu
35. Babu amefunga ushanga shingoni. Mtama/Nazi
36. Babu anakula ng’ombe, analea fupa linakuwa ng’ombe. Muwa
37. Babu hupiga kelele akojoapo. Mvua
38. Babu mkubwa ameangushwa na babu mdogo. Mti na shoka
39. Babu, nyanya, mjomba, mama, baba na watoto, mna safari ya wapi? Siafu
40. Bak bandika, bak bandua. Nyayo
41. Bawabu mmoja tu asiyeogopa chochote duniani. Mlango
42. Bibi kikongwe apepesa ufuta. Kope za macho
43. Bibi yake hutandikwa kila siku, lakini hatoroMoyoKinu cha kutwangia

C
44. Chakula kikuu cha mtoto. Usingizi
45. Cha ndani hakitoki nje, cha nje hakiingii ndani. Nyama na mfupa
46. Chang’aa chapendeza, lakini hakifikiwi. Jua
47. Chatembea na hakijapata kupumzika hata nukta moja. Mwezi/Jua
48. Cheupe chavunjika manjano yatokea. Yai
49. Chumba change kina ukuta niondoa na kuusimika nitakapo. Pazia
50. Chungu change cha udongo hakipasuki kikianguka. Mjusi/Panya
51. Chungu kikubwa sana chenye kifuniko kikubwa sana. Dunia na mbingu

D
52. Dada yangu akitoka kwao harudi kamwe. Jani likwanyukapo
53. Dada yangu kaoga nusu. Jiwe mtoni
54. Drrrrrh1 Ng’ambo. Daraja la buibui
55. Dume wangu amelilia machungani. Radi

F
56. Fahali wa ng’ombe na mbuzi wadogo machungani. Mwezi na nyota angani
57. Fika umwone umpendaye. Kioo
58. Fuko kajifukia, mkia kaacha nje. Kata mtungini
59. Funga mizigo twende Kongo. Mikia ya mbwa

H
60. Hachelewi wala hakosei safari zake. Jua
61. Haina miguu wala mikono, lakini, yabeba magogo. Maji
62. Hakihitaji maji, wala udongo, wala chakula; lakini chamea. Nywele
63. Hakionekani wala hakishikiki. Hewa
64. Hakisimami, na kikisimama msiba. Moyo
65. Hakuchi wala hakuchwi. Kula
66. Halemewi wala hachoki kubeba. Ardhi
67. Hamwogopi mtu yeyote. Njaa
68. Hana mizizi, nimemkata mara nyingi lakini haachi kukua. Ukucha
69. Haoni kinyaa. Mvua
70. Hapo nje panapita mtu mwenye miguu mirefu. Mvua
71. Hasemi, na akisema hatasahaulika. Kalamu
72. Hasimamishwi akiwa na ghadhabu. Upepo
73. Hata inyeshe namna gani haifiki humu. Kwapani
74. Hata jua likiwaka namna gani hakauki wala kupata joto. Pua ya mbwa
75. Hata Mzungu ameshindwa. Mauti
76. Hauchagui chifu wala jumbe. Utelezi
77. Hausimiki hausimami. Mkufu
78. Hawa wanaingia hawa wanatoka. Nyuki mzingani
79. Hesabu haihesabiki. Nyota
80. Huitumia kila siku lakini haiishi. Miguu
81. Huku kutamu, huku kutamu, katikati uchungu. Jua
82. Huku unasikia ‘pa’ Huku unasikia ‘pa! Mkia wa kondoo
83. Hula lakini hashibi. Sindano
84. Hulala tulalapo, huamka tuamkapo. Jua
85. Humu mwetu tuko wanne tu, ukimwona wa tano mwue. Matendegu ya kitanda
86. Huna macho lakini wakamata wanyama. Ndoana
87. Hupanda mtini na mwenye kichaa wake. Kivuli
88. Hutembea watatu. Mafiga
89. Hutoka upesi sana lakini hasalimu. Kuku
90. Huwafanya watu wote walie. Moshi
91. Huwezi kukalia alipokalia msichana wangu mweusi. Chungu jikoni
92. Huzikwa mmoja, hufufuka mmoja, huzeeka wengi. Mbegu na matunda

I
93. Inaonekana mara mbili katika dakika moja na mara moja tu katika mwaka. Herufi "K"
94. Ini la ng’ombe huliwa hata na walioko mbali. Kifo

J
95. Jembe la Wangoni haliishi. Miguu/Nyayo
96. Je, unaweza, kukua ukampita mzee wako? Nywele kichwani
97. Jiwe litoalo maji. Macho

K
98. Kaburi la mfalme lina milango miwili. Kata ya kuchukulia Maji kichwani
99. Kaka yangu anapanda darini na fimbo nyuma. Paka na mkia wake
100. Kama kingekuwa mkuki, ungekuta kimekwisha kuua wote. Kizingiti cha mlango
101. Kama unapenda, mbona usile? Ulimi
102. Kanipa ngozi nikapikia, kanipa nyama nikala, kanipa mchuzi nikanywa, kanipa mfupa nikautumia. Nazi
103. Kapanda mti pamoja na uchawi wake. Tumbaku inaponuswa puani
104. Kidimbwi kimezungukwa na majani. Macho
105. Kikioza hutumiwa, kikiwa kichungu hakitumiwa. Maziwa
106. Kila linapofika kwetu hutanguliza makelele. Mvua
107. Kila mtu atapitia malango huo. Kifo
108. Kila mtu hata mfalme huheshimu akipita. Mlango
109. Kila siku hupita njia hiyo hiyo bali arudipo hatumwoni. Jua
110. Kileee! Hiki hapa. Kivuli
111. Kilimsimamisha chifu njiani. Chawa
112. Kina mikono na uso lakini hakina uhai. Saa
113. Kinaniita lakini sikioni. Mwangwi
114. Kisima cha Bimpai kina nyoka muwai, ndiye fisadi wa maji. Taa ya utambi
115. Kisima kidogo kimejaa changarawe. Kinywa na meno
116. Kitendawili change ukikitambua nitakupa hirizi. Mimba
117. Kiti cha dhahabu hakikaliwi na watu. Moto
118. Kiti cha Sulatni hukaliwa na mwenyewe. Kuku aatamiapo mayai
119. Kiti nyikani. Uyoga
120. Kitu changu asubuhi chatembea kwa miguu mine, saa sita kwa miguu miwili, jioni kwa miguu mitatu. Maisha ya binadamu
121. Kiwanja kizuri lakini hakifai kuweka mguu. Kipara
122. Kombe ya Sultani Ii wazi. Kisima
123. Kondoo wangu amezaa kwa paja. Mhindi
124. Kondoo wangu mnene kachafua njia nzima. Konokono
125. Kondoo za mtoto zamaliza mavuno. Jiwe la kusagia
126. Kufanya kwa ridhaa mojamoja. Kusuka mkeka
127. Kuku wangu aliangua mayai jana, lakini si kuku wala ndege. Nyoka au samaki
128. Kuku wangu amezalia miibani. Nanasi au chungwa
129. Kuku wetu hutagia mayai mikiani. Matunda
130. Kuna mlima mmoja usio pandika. Nafasi kati mdomo na pua
131. Kuna mtu mwenye tumbo kubwa aliyesimama nje. Ghala
132. Kuna ziwa kubwa ambalo limekauka na limebakiza mizizi. Chongo
133. Kunguru akilia hulilia mirambo. Mtoto akililia maziwa
134. Kwenye msitu mkubwa Napata mti mmoja tu, lakini kwenye msitu mdogo naweza kupata miwili. Watoto wa ng'ombe na mbuzi
135. Kwetu mishale na kwenu mishale. Mikia ya panya
136. Kwetu twalala tumesimama. Nguzo za nyumba

L
137. La mgambo limelia wakatoka weusi tu. Chunguchungu
138. Likienda hulia, likirudi halilii. Debe aka buyu
139. Likitoka halirudi. Neno
140. Liwali amekonda lakini hana mgaga. Sindano

M
141. Mama ametengeneza chakula lakini hakula. Chungu cha kupikia
142. Mbona kinakumeza lakini hakikuli? Nyumba
143. Mbona mwakunjiana ngumi bila kupigana? Mafiga
144. Mbona mwasimama na mikuki, mwapigana na nani? Katani
145. Mchana ‘ti’ usiku ‘ti’. Mlango
146. Mdogo lakini humaliza gogo. Mchwa
147. Mfalme amesimika mkuki wake hapa name nikausimika wangu kando yake, baadaye
           hatukuitambulisha tena. Kohozi
148. Mfalme hushuka kwa kelele. Mvua
149. Mfalme katikati lakini watumishi pembeni. Moto na mafiga
150. Mfalme wetu hupendwa sana, lakini wakati wa kumwona lazima umtoe nguo zote kwanza. Hindi
151. Mhuni wa ulimwengu. Inzi
152. Mkanda mrefu wafka mpaka pwani. Njia
153. Mke wangu mfupi, lakini huvaa nguo nyingi. Hindi
154. Mlango wa nyumba yangu uko juu. Shimo la mchwa
155. Mlima mkubwa wapandwa kuanzia juu. Sima/Ugali
156. Mlimani sipandi. Maji
157. Mlima umezuia kutazama kwa mjomba. Kisogo
158. Mlima wa kupanda kwa mikono. Mlima
159. Mlima wa kwetu hupandwa na mfalme. Nafasi kati ya mdomo na pua ya ngombe
160. Mlima wa mwenyewe hupandwa na mwenyewe. Buibui na utando wake
161. Mpini mmoja tu lakini majembe hayahesabiki. Mkungu wa ndizi
162. Msitu ambao haulii hondohondo. Mimba
163. Mti mkubwa, lakini una matawi mawili tu. Kichwa na masikio
164. Mti mnyanya mti kerekeche mti ah mti ah!. Ngoma na upatu
165. Mti wangu una matawi kumi na mawili na kila tawi lina majani kadiri ya thelathini. Mwaka
166. Mtoto asemea pangoni. Ulimi mdomoni
167. Mtu mdogo mwenye miguu mirefu ambaye aweza kutembea dunia nzima kwa dakika tano. Mawazo
168. Mvua hema na jua hema. Kobe
169. Mvua kidogo ng’ombe kaoga kichwa. Jiwe
170. Mwadhani naenda lakini siendi. Jua
171. Mwalimu analala na mwanafunzi wanamsomea. Kinyesi na inzi
172. Mwanamke mfupi hupiga kelele njiani. Kunguru
173. Mwanamke mfupi hutengeneza pombe nzuri. Nyuki
174. Mwanang’ang’a hulia mwituni. Shoka
175. Mwepesi, lakini aweza kuvunja nyumba za mji wote. Tufani
176. Mwezi wangu umepasuka. Kweme
177. Mzee Kombe akitoa machozi wote hufurahi. Mvua
178. Mzee Kombe akilia watu hufurahi. Mvua
179. Mzizi wa miti hutokea mbali. Siafu
180. Mzungu yuko ndani na ndevu ziko nje. Hindi

N
181. Naitumia ngazi hiyo kwa kupandia na kushukia. Mwiba
182. Nakikimbilia lakini sikikuti. Njia
183. Nakupa lakini mbona huachi kudai. Tumbo
184. Nakwenda msituni na mdogo wangu, lakini yeye namwacha huko.
185. Nameza lakini sishibi. Mate
186. Namkimbiza lakini simkuti. Kivuli
187. Namlalia lakini halii. Kitanda
188. Namwomba atangulie lakini hukataa kabisa. Kigino
189. Nanywa supu na nyama naitupa. Muwa
190. Napigwa na mvua na nyumba ipo. Matunda ya pua/Kwapa
191. Natembea juu ya miiba lakini hainichomi. Miiba
192. Natembea juu ya miiba lakini sichomwi. Ulimi
193. Natembea na wenzangu lakini tukifika kwenye nyumba mimi hukaa mlangoni. Mbwa
194. Natengeneza mafuta lakini nimepauka sana. Mzinga was nyuki kwa nje
195. Natengeneza mbono lakini alama hazionekani. Mzinga wa nyuki
196. Ndege wengi baharini. Nyota
197. Ndugu wawili wafanana sana, lakini hawatembeleani. Macho
198. Ngoja nikumbuke. Boga changa
199. Ng’ombe wa baba watelemka mtoni. Mawe mtoni
200. Ng’ombe wa babu huchezea miambani. Mijusi
201. Ng’ombe za babu zikienda machungani hulia, zikirudi hazilii. Vbuyu
202. Ng’ombe za babu zinalala na mkia nje.Viazi vitamu udongoni
203. Ng’ombe wamechanganyika nikakosa wa kwangu. Pesa/Nyayo
204. Ng’ombe wangu ni weupe kwatoni. Katani
205. Ng’ombe wangu wote hunywa maji isipokuwa mmoja. Fimbo ya kuchunga
206. Ngozi ndani nyama juu. Firigisi
207. Nguo ivaliwayo kila siku isiyoingiwa na chawa. Nyusi
208. Nikicheka kinacheka, nikinuna kinanuna. Kioo
209. Nikienda arudi, nikirudi aenda. Kivuli majini
210. Niiita ‘baba’ huitika ‘baba’. Mwangwi
211. Nikija kwenye ndege wananifukuza, na nikienda kwenye wanyama hawanitaki. Popo
212. Nikimpiga huyu huyu alia. Utomvu wa papai
213. Nikimpiga mambusu. Puliza kidole wakati unapojikwaa
214. Nikimwita hunijibu nani. Mwangwi
215. Nikipewa chakula nala bali natema. Shoka
216. Nikitembea walio wafu huniamkia na walio hai hukaa kimya. Majani makavu na mabichi
217. Nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayupo. Kivuli
218. Ni kitu gani ambacho kutoa ni kuongeza? Shimo
219. Nikitupa mshale wangu mchana huenda mbali sana, lakini niutupapo usiku hauendi mbali. Jicho
220. Nikiwaambia ondokeni hukataa, lakini mjomba akitokea wote hukimbia. Umande na jua
221. Nilijenga nyumba yangu nikaiacha bila kuiezeka majani; lakini niliporudi nilikuta imekwisha ezekwa majani. Mahindi machanga
222. Nilijenga nyumba yangu yenye mlango mmoja. Jani la mgomba la nchani
223. Nilimkata alafu nikamridhia. Kupanda mbegu
224. Nilimtuma askari vitani akaniletea kondoo mweusi. Fuko
225. Nilipandia majanini nikashukia majanini. Mwiba
226. Nilipigwa na tonge la ugali la moto nilipopita msituni. Manyigu
227. Nilipitisha mkono wangu chini la ardhi, nikamshika beberu mkubwa sana. Kiazi kikuu
228. Nilipoangalia kwenye magereza ya Wazungu, nikaona wameketi juu ya mabati. Pelele
229. Nilipofika msituni nilikuta chungu cha pure kinachemka. Mzinga wa nyuki
230. Nilipoingia Rumi, alitoka mtu na wake kumi; kila mke na tundu kumi, kila tundu na kuku
           kumi; kila kuku na mayai kumi. Mayai, kuku, tundu, wake, kumi kumi kumi. Wangapi
           walikwenda Rumi? Hakuna
231. Nilipo, juu kuna miiba na chini vivyo hivyo; lakini sichomwi. Ulimi kinywani
232. Nilipokuwa mchanga nilikuwa na kijikia lakini sasa sinacho. Chura
233. Nilitembea na mwezangu naye hupita vichakani. Kivuli
234. Nimechoma fimbo yangu pakabaki pa kushikia tu. Njia
235. Nimefyeka mitende yote kiungani isipokuwa minazi miwili tu. Masikio
236. Nimejenga nyumba babu akaihamia kabla mimi sijahamia. Mjusi
237. Nimekata mti, akaja samba mwekundu akaukalia. Utomvu
238. Nimekata mti bara ukaangusha matawi pwani. Nzige
239. Nimekwenda na rafiki yangu kwa jirani, yeye akafika kabla yangu. Sauti ya nziga
240. Nimemtahiri binti wangu akatoa damu mchana kutwa. Kivuli
241. Nimempeleka kondoo wangu akatoa damu mchana kutwa. Mgomba
242. Nimemtuma mtu kumwamkua mtu, yeye amekuja, Yule aliyetumwa hajaja. Kuangua tunda Ana nazi
243. Nimemwacha mzee kikongwe mtoni anangojea mgeni kulaki. Mtego
244. Nimempandikiza mti wangu ukapeleka matawi ng’ambo ya mto. Kivuli
245. Nimesimama mbali nyikani lakini naonekani. Moto
246. Nimetembea kitambo, kukumbuka sikufunga nyumba. Dirisha Ana ufa
247. Nimetoka kutembea kutembea, nikashika ng’ombe mkia. Kata
248. Nimetupa mshale angani wala sitambui utateremsha ndege wa namna gani. Mimba
249. Nimeweka ndizi yangu, asubuhi siioni. Nyota
250. Nimezaliwa na mguu mmoja. Uyoga
251. Nimezungukwa na adui wengi, lakini siumizwi. Ulimi na meno
252. Nina kijiti change, nizidivyo kukikata ndivyo kizidivyo kuwa kirefu. Maisha
253. Nina kitu changu kitumiwacho na wengine kuliko mimi. Jina
254. Nina kitu kizuri sana nyumbani, lakini siwezi kukichukua. Dada
255. Nina kitu nipendacho ambacho hata baba, mama, dada, kaka hata na mgeni nimpendaye sana siwezi kumwazima. Mke
256. Nina mwezi ndani ya bakuli. Maziwa
257. Nina ng’ombe wangu nisipomshika mkia hali majani. Jembe
258. Nina nyumba yangu imezungukwa na mifupa. Mdomo
259. Nina pango langu lilojaa mawe. Kinywa
260. Nina watoto wangu hamsini na wote nimewavisha visibau vyeupe. Kunguru
261. Nina watoto watatu, mmoja akitoka kazi haifanyiki. Mafiga
262. Nina badilika umbo langu baada ya kila muda mfupi. Kivuli
263. Ninachimba mizizi ya mti usio na mizizi. Jiwe
264. Ninacho, nakitumia, lakini kila nikitumiapo, sikiharibu ila nakipa rangi. Maji na mkojo
265. Ninakula vitu vyote vinono lakini sikui wala sinenepi. Chungu cha kupikia
266. Ninakwenda naye na kurudi naye. Kivuli
267. Ninao mlima ambao una msitu kileleleni tu. Kichwa
268. Nitokeapo kila mmoja asema namtazama yeye tu. Jua au mwezi
269. Njia yapitwa siku zote lakini haina alama. Njia ya jua au mwezi
270. Njoo hapa nije hapo. Kiraka
271. Nne nne mpaka pwani. Matendegu
272. Nusu mfu nusu hai. Sungura alalapo
273. Nyama ndogo imewashibisha wengi wala isiishe. Kinoo
274. Nyama ya Reale haijai kikombe. Mkufu
275. Nyanya yako ana huruma kukubeba ulalapo. Kitanda
276. Nyumba yangu ina makuti tele, lakini mvua ikinyesha huvuja. Mwembe
277. Nyumba yangu ina milango mingi. Kichuguu
278. Nyumba yangu ina nguzo moja. Uyoga
279. Nyumba yangu kubwa, haina mlango. Yai
280. Nyumba yangu kubwa, haina taa. Kaburi
281. Nyumba yangu kubwa hutembelewa mgongoni. Konokono

O
282. Oh! Mwanamke aliyevunja chungu mshangao wake
283. Ondoka nikae. Maji ya mfereji

P
284. Paa alipenga hata pua ikapasuka. Mbarika
285. Palikuwepo watu watatu wakivuka mto. Mmoja alivuka pasipo kukanyaga maji wala kuyaona; wa pili aliyaona maji lakini alivuka bila kuyakanyaga; wa tatu aliyaona na kuyakanyaga alipovuka.
Ni nani hawa? Was kwanza in Mtoto tumboni mwa mamake, was pili ni Mtoto aliyebebwa mgongoni, was tatu ni mama mwenyewe
286. Panda ngazi polepole. Sima ya ugali
287. Para hata Maka. Utelezi
288. Pete ya mfalme ina tundu katikati. Kata ya kuchukulia mizigo
289. Poopoo mbili zavuka mto. Macho
290. Po pote niendako anifuata. Kivuli

R
291. Rafiki yangu ana mguu mmoja. Uyoga
292. Reli yangu hutandika ardhini. Siafu
293. Ruka Riba. Maiti

S
294. Shamba langu kubwa lakini mavuno hayajazi kiganja. Nywele kichwani
295. Shamba langu miti mitano tu. Mkono wa vidole
296. Shangazi yangu ni mrefu sana lakini hafikii tumbo la kondoo. Njia
297. Sijui aendako wala atokako. Upepo
298. Sijui afanyavyo. Nyoka apandavyo mtini
299. Sina dada wala kaka, lakini baba wa huyu jamaa ni mtoto wa babangu. Ni nani huyo? Mtoto wangu
300. Subiri kidogo! Miiba
301. Sultani alipiga mbiu watu waje kufanya kazi yake lakini wakashindwa. Maji

T
302. Taa ya bure. Jua au mwezi
303. Taa ya Mwarabu inapepea. Kilemba
304. Tajiri aniweka mfukoni na maskini anitupa. Makamasi
305. Tandika kitanga tule kunazi. Nyota
306. Tangu kuzaliwa kwake sijamwona asimame wala kukimbia. Mkufu
307. Tatarata mpaka ng’ambo ya mto. Utando wa baibui
308. Tatu tatu mpaka pwani. Mafiga
309. Tega nikutegue. Mwiba
310. Teke teke huzaa gumugumu, na gumugumu huzaa teke teke. Mahindi ama yai
311. Tengeneza kiwanja kikubwa kabila Fulani lije kupigania. Mbono
312. Tonge la ugali lanifikisha pwani. Jicho
313. Tukate kwa visu ambacho hakitakatika. Maji
314. Tulikaribishwa mahali na mdogo wangu, yeye akaanza kushiba kabla yangu. Kucha
315. Tuliua ng’ombe na babu, kila ajaye hukata. Kinoo
316. Tuliua ng’ombe wawili ngozi ni sawasawa. Mbingu na nchi
317. Tumvike mwanamke huyu nguo. Kuezeka nyumba
318. Tunajengajenga matiti juu. Mapapai
319. Twamsikia lakini hatumwoni. Sauti

U
320. Ukimcheka atakucheka, ukimwomba atakuomba. Mwangwi
321. Ukimwita kwa nguvu hasikii, lakini ukimwita polepole husikia. Fisi
322. Ukimwona anakuona. Jua
323. Ukitaka kufahamu ana mbio, mwonyeshe moto. Kinyonga
324. Ukitembea ulimwengu wote utakosa nyayo. Mwamba
325. Ukiukata haukatiki, ukiushika haushikiki. Moshi
326. Ukiwa mbali waweza kumwona Fulani umatini. Tundu LA sindano
327. Ukoo wa liwali hauna haya. Wanyama
328. Ule usile mamoja. Kifo
329. Umempiga sungura akatoa unga. Funds LA mbuyu
330. Unatembea naye wote umjiao atakuona. Bakora
331. Upande wote umjiao atakuona. Kinyonga
332. Ushuru wa njia wKujikwaa Kujikwaa
333. Utahesabu mchana na usiku na hutamaliza kuhesabu. Nywele

V
334. Viti kumi nyumbani, tisa vyakalika lakini kimoja hakikaliki. Moto

W
335. Wake wa mjomba kimo kimoja. Vipande vya kweme
336. Wako karibu lakini hawasalimiani. Nyumba ama kuta zinazoelekeana
337. Wanakuja mmoja mmoja na kujiunga kuwa kitu kimoja. Matone ya mvua
338. Wanameza watu jua linapokuchwa. Nyumba
339. Wanamwua nyoka. Watu wanaotwanga
340. Wanangu wawili hugombana mchana, usiku hupatana. Mlango
341. Wanao wakati wao wa kuringa, nao ni weupe kama barafu. Nyota
342. Wanapanda mlima kwa makoti mazuri meusi na meupe. Vipepeo
343. Wanastarehe darini. Panya
344. Wanatembea lakini hawatembelewi. Macho
345. Watoto wa mtu mmoja hulala chini kila mwaka. Maboga
346. Watoto wangu wana vilemba, asio kilemba si mwanangu. Fuu
347. Watoto wangu wote nimewavika kofia nyekundu. Jogoo
348. Watoto wangu wote wamebeba vifurushi. Vitovu
349. Watu ishirini walipanda juu ya mti, wawili wakaona chungwa, watano wakalichuma, kumi wakalimenya, wote wakaridhirika mtu mmoja alile. Je, ni watu gani hao? Waliopanda ni vidole vya miguu na mikono, walioona ni macho mawili, waliochuma ni vidole vitano vya mikono, waliomenya ni vidole vya mikono yote miwili, na aliyelila ni mdomo
350. Watu waliokaa na kuvaa kofia nyekundu. Kuku, katani au mahindi
351. Watu wamehama askari wekundu wakazidi nyikani. Viroboto
352. Watu wawili hupendana sana; kati ya mchana hufuatana ingawa mmoja ni dhaifu. Usiku mdhaifu
           haonekani tena. Kivuli
353. Watu wote ketini tumfinye mchawi. Kula ugali
354. Wewe kipofu unaenda wapi huko juu? Mkweme

Y
355. Yaenda mbali lakini haiondoki ilipo. Njia

Z
356. Zilitazamana na mpaka sasa hazijakutana. Kingo za mto
357. Ziwa dogo linarusha mchanga. Chungu jikoni
358. Ziwa kubwa, lakini naogelea ukingoni tu. Moto]]>
A

<![CDATA[FAFANUA SIFA BIA ZINAZOBAINISHA TANZU ZA METHALI NA VITENDAWILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=973 Sat, 21 Aug 2021 06:24:13 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=973
.docx   FAFANUA_SIFA_BIA_ZINAZOBAINISHA_TANZU_ZA.docx (Size: 20.93 KB / Downloads: 5) ]]>

<![CDATA[VITENDAWILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=961 Sat, 21 Aug 2021 04:24:33 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=961 Vitendawili ni tungo fupi ambazo huwa na swali fupi lisilo wazi na jibu kwa makusudi ya kupima ufahamu wa hadhira kuhusu mazingira yake. Anayetoa kitendawili huulizia swali lake kwa kutoa maelezo mafupi yanayorejelea umbo la kitu hicho, sauti, harufu au kukifananisha na kitu kingine. Anayejibu huhitajika kufikiria haraka na kutoa jawabu ambalo huwa la neno moja au maneno mawili hivi. Vitendawili huwa na mianzo maalum kulingana na jamii yake.

Sifa za Vitendawili

  1. Vitendawili huwa na mwanzo maalum : Kitendawili  "tega"

  2. Hupitishwa baina ya watu wawili  anayetega na anayetegua

  3. Vitendawili huwa na muundo maalum wa kuendelezwa (utangulizi, swali, (majaribio ya) jibu; wanaotegua wakishindwa anayetega huwa ameshinda, huitisha apewe mji/zawadi na kisha kutoa jibu)

  4. Huwa na vipande viwili “ swali na jibu. Mfano: Kila niendapo ananifuata “ kivuli.

  5. Hutumia mbinu ya jazanda, kufananisha vitu viwili moja kwa moja. K.v. Nyumba yangu haina mlango “ yai (yai limelinganishwa moja kwa moja na nyumba isiyo mlango)

  6. Hurejelea vitu vinavyopatikana katika mazingira na vinavyojulikana sana

  7. Vitendawili vilitegwa wakati maalum, hasa wa jioni

  8. Vitendawili hutumia tamathali za usemi (mbinu za lugha) kama istiara, tashihisi, tashbihi, jazanda, chuku, tanakali za sauti, n.k

  9. Vitendawili huwa na jibu maalum.

Aina za Vitendawili
a) Vitendawili sahili

ni vifupi na huwa na na muundo mwepesi kueleweka. K.v.

b) Vitendawili mkufu

huwa na vipande vinavyofuatana na kila kipande huwa na uhusiano na kipande kilichotangulia. Mfano “ nikisimama anasimama, nikiketi anaketi, nikiondoka huondoka pia

c) Vitendawili vya tanakali

hutumia tanakali za sauti Mfano: Prrrrrrh mpaka ng'ambo “ buibui; huku ng'o na kule ng'o.

d) Vitendawili sambamba

huwa na maelezo marefu (kama hadithi fupi) halafu jibu lake huwa ni refu pia (kama mafumbo)

Umuhimu wa vitendawili

  1. Vitendawili huburudisha kwani hutegwa kwa njia ya uchangamfu na ushindani.

  2. Huwaleta watu pamoja (huunganisha jamii) kwani vinapotegwa watu hukusanyika pamoja.

  3. Vitendawili huhamasisha watu kuhusu mazingira yao kwani hulenga vitu vinavyopatikana katika jamii hiyo.

  4. Vitendawili hukuza uwezo wa kufikiria/kukumbuka kwani anayetoa jibu huhitajika kukumbuka jibu la kitendawili.

  5. Vitendawili hukuza na kuhifadhi tamaduni kwa maana hupokezanwa kutoka kizazi hadi kizazi.

  6. Vilitumika kupitisha wakati na kuwafanya watoto wasilale mapema kabla ya chakula kuwa tayari.
]]>
Vitendawili ni tungo fupi ambazo huwa na swali fupi lisilo wazi na jibu kwa makusudi ya kupima ufahamu wa hadhira kuhusu mazingira yake. Anayetoa kitendawili huulizia swali lake kwa kutoa maelezo mafupi yanayorejelea umbo la kitu hicho, sauti, harufu au kukifananisha na kitu kingine. Anayejibu huhitajika kufikiria haraka na kutoa jawabu ambalo huwa la neno moja au maneno mawili hivi. Vitendawili huwa na mianzo maalum kulingana na jamii yake.

Sifa za Vitendawili

  1. Vitendawili huwa na mwanzo maalum : Kitendawili  "tega"

  2. Hupitishwa baina ya watu wawili  anayetega na anayetegua

  3. Vitendawili huwa na muundo maalum wa kuendelezwa (utangulizi, swali, (majaribio ya) jibu; wanaotegua wakishindwa anayetega huwa ameshinda, huitisha apewe mji/zawadi na kisha kutoa jibu)

  4. Huwa na vipande viwili “ swali na jibu. Mfano: Kila niendapo ananifuata “ kivuli.

  5. Hutumia mbinu ya jazanda, kufananisha vitu viwili moja kwa moja. K.v. Nyumba yangu haina mlango “ yai (yai limelinganishwa moja kwa moja na nyumba isiyo mlango)

  6. Hurejelea vitu vinavyopatikana katika mazingira na vinavyojulikana sana

  7. Vitendawili vilitegwa wakati maalum, hasa wa jioni

  8. Vitendawili hutumia tamathali za usemi (mbinu za lugha) kama istiara, tashihisi, tashbihi, jazanda, chuku, tanakali za sauti, n.k

  9. Vitendawili huwa na jibu maalum.

Aina za Vitendawili
a) Vitendawili sahili

ni vifupi na huwa na na muundo mwepesi kueleweka. K.v.

b) Vitendawili mkufu

huwa na vipande vinavyofuatana na kila kipande huwa na uhusiano na kipande kilichotangulia. Mfano “ nikisimama anasimama, nikiketi anaketi, nikiondoka huondoka pia

c) Vitendawili vya tanakali

hutumia tanakali za sauti Mfano: Prrrrrrh mpaka ng'ambo “ buibui; huku ng'o na kule ng'o.

d) Vitendawili sambamba

huwa na maelezo marefu (kama hadithi fupi) halafu jibu lake huwa ni refu pia (kama mafumbo)

Umuhimu wa vitendawili

  1. Vitendawili huburudisha kwani hutegwa kwa njia ya uchangamfu na ushindani.

  2. Huwaleta watu pamoja (huunganisha jamii) kwani vinapotegwa watu hukusanyika pamoja.

  3. Vitendawili huhamasisha watu kuhusu mazingira yao kwani hulenga vitu vinavyopatikana katika jamii hiyo.

  4. Vitendawili hukuza uwezo wa kufikiria/kukumbuka kwani anayetoa jibu huhitajika kukumbuka jibu la kitendawili.

  5. Vitendawili hukuza na kuhifadhi tamaduni kwa maana hupokezanwa kutoka kizazi hadi kizazi.

  6. Vilitumika kupitisha wakati na kuwafanya watoto wasilale mapema kabla ya chakula kuwa tayari.
]]>
<![CDATA[METHALI ZA SHAABAN ROBERT]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=741 Mon, 02 Aug 2021 11:51:51 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=741
“Methali ni lugha nyepesi ipenyayo moja kwa moja katika mioyo ya wasikilizaji. Aidha, methali au misemo huondoa wingu au ukungu katika mawasiliano ya kisayansi na ya teknolojia nzito za kitaaluma. Pia, methali ni kielelezo cha utashi wa uhai wa jamii husika, historia na falsafa ya utu wa binadamu, hekima na busara. Mwanafasihi mashuhuri katika Afrika, Chinua Achebe, katika kitabu chake Things Fall Apart (1959: 7) anaandika, “Methali ni mafuta ya mawese ambayo kwayo maneno huliwa.” Kauli hii ikizingatiwa barabara huyafanya maandishi kukubalika kuwa ni fasihi, maana, matumizi ya methali na fani nyingine hukoleza simulizi kama tui la nazi na viungo mbalimbali kama vile vitunguu, nyanya, zinavyoifanya mboga iwe na riha na ladha tamu zaidi.
Dhima ya methali katika jamii. Mbonde anaendelea kufafanua dhima/umuhimu au nafasi ya methali katika jamii “Methali ni njia ya mkato ya kuelimisha, kuadilisha, kukosoa na kuelekeza jamii, hususani vijana katika kuzingatia tunu za jadi kwa kina ndani ya mazingira ya asili ya jamii”.
Vilevile Ngole na Honero wanafasili kuwa “methali ni aina ya usemi mzito na ambao unakusudiwa kusema jambo maalumu kwa njia ya fumbo. Usemi huu mzito mara nyingi hukusudiwa kumuonya, kumuongoza, na kumuadilisha mwanadamu. Kwa umbile la nje methali huwa na muundo maalumu, muundo wenye baadhi (pande) mbili. Upande mmoja wa methali huwa unaeleza mazoea au tabia ya mtu au kitu juu ya utendaji wa jambo; na upande wa pili unaeleza matokeo yatokanayo na mazoea hayo au tabia hiyo ambayo imeelezwa katika upande wa kwanza.
UCHAMBUZI WA METHALI ZA SHAABAN ROBERT
     1.            Cha mjinga huliwa na mwerevu.
–         Asiyejua mara nyingi hudhulumiwa na mtu anayejua.
–         Hutumiwa kuwatanabaisha watu wasiojua kwamba, haki zao siku zote hudhulumiwa na wale wanaojua, wajanja au wasomi.
    2.            Cha mlevi huliwa na mgema. (Tazama:1)
    3.            Cha mwivuo hulishwa na mgema.
–         Ubaya hubainishwa kwa wema.
–         Hutumika kuelezea kuwa daima watu wema ndiyo ambao hubainisha maovu katika jamii.
–         Cha mwovuo hulishwa na mwemao.
–         Sawa na “Cha mwivuo hulishwa na mwemao.” (tazama 3)
    4.            Cha nini kitu hiki kizuri? Punje moja ya mtama bora mara elfu.
–     Si kila kisifiwacho ni kizuri kwani vipo visivyosifiwa ambavyo ni vizuri zaidi ya hivyo vinavyosifiwa.
–   Hutumiwa kuonesha kuwa vitu vizuri (watu) siku zote havijibainishi kwamwonekano wake au umbile lake.
–         Sawa na “Wamo lakini hawavumi.”
    5.            Cha kichwa kitamu, na cha mkia kitamu.
–         Kila mtu anafurahia nafasi yake katika maisha.
–    Hutumika kuonesha kuwa kila hali (cheo, uchumi nk.) inauzuri wake katika maisha.
    6.            Cha shina kitamu, cha kati kitamu na cha ncha kitamu. (tazama: 5)
    7.            Chachu ikichachuka, watu watatafutana.
–         Amani itapotea punde mnyonge atakaposimama na kudai haki yake.
–   Hutumiwa kwa lengo la kuwatahadharisha wale wawanyonyao wanyonge kuwasiku watakapotambua haki yao hapatatosha.
     8.            Chafi rasilimali yake utumbo.
–  Kitu chochote chenye thamani hakiachwi/hakionekani waziwazi. Au tunaweza kusema uzuri wa mtu si umbo wala sura (mwonekano wa nje) bali ni tabia.
–  hutumika kuwatahadharisha wale wanaoshadidia au kupapatikia vitu kwakuangalia umbile lake bila kujua undani wake.
     9.            Chafi rasilimali yake matumbo. (tazama: 8)
10.            Chagua dogo katika maovu mawili.
–  Heri kutenda kosa dogo kuliko kuliko kutenda kosa kubwa. Au ni afadhali kupata hasara kidogo kuliko kupata hasara kubwa.
–  Hutumika kufariji endapo mtu anapatwa na tatizo dogo, hivyo anambiwa methali hii ili aone kwamba tatizo alilolipata huenda Mungu kamwepusha na janga kubwa zaidi ya hilo.
 11.            Chakula bora ni ukipendacho.
–         Uzuri au ubora wa kitu anaujua mtumiaji au mlaji.
– Methali hii hutumika kueleza kuwa, katika maisha si vizuri kumlazimisha mtu kutenda jambo bila yeye mwenyewe kuridhia.
12.            Chakula bora ni ulichonacho.(tazama:11)
13.            Chakula ni wali, kiungo ni samli na mke ni mwanamwali.
–         Kitu chenye thamani huthaminiwa na watu.
–  Methali hii hutumika kuonesha kwamba katika maisha daima vitu vyenye thamani ndivyo vinavyothaminiwa na watu. Pia hata watu wazuri au wenye sifa nzuri ndiyo wanaopendwa na wengi.
14.            Chanda na pete, ulimi na mate, uta na upote.
–    Chanda: kidole; Uta: upinde wa kupigia mshale; Upote: kamba ya upinde.
–         Kila kitu hutegemeana.
–         Hukuna kitu ambacho kimekamilika katika maisha.
15.            Cha ndugu hakiwi chako sharti upewe.
–         Using’ang’anie vitu visivyo vyako.
–         Methali hii hutumika kwa ajili ya kuwaonya na kuwakosoa wale wenye tabia ya kudhani kwamba kitu cha ndugu ni sawa na chakwake. Hivyo katika maisha haupaswi kijivunia vitu ambavyo si mali yako hata kama ni vya ndugu yako wa damu.
16.            Changilizi ya chungu huua hata nduvu.
–         Changilizi: kazi ya pamoja.
–  Umoja au ushirikiano wa wanyonge huweza kufanya mapinduzi makubwa.
–         Hutumiwa kuwa hamasisha watu hasa wa tabaka la chini (duni) kuwa endapo wataungana na kushirikiana wanaweza kutenda mambo makubwa katika maisha yao.
Changu si chetu.
–         Kitu ambacho ni changu mwenyewe hakiwezi kuwa cha wote.
– Hutumika kuwa hamasisha watu kupenda kujishughulisha katika maisha iliwajipatie vitu vyao wenyewe badala ya kutegemea vitu vya wengine. Pia inawafundisha watu kutopenda kuishi kwa kutegemea migongo ya wengine.
17.            Chatu anamvuto kwa mbwa na paka kama fedha kwa mtu.
–         Jinsi fedha ilivyo na mvuto vivyo hivyo wabaya au wakorofi wana uzuri pia kwa watu wao.
–         Methali hii hutumika kuwatanabaisha watu watambue kwamba katika maisha hakuna mtu asiye na rafiki hata kama mbaya kupita kiasi.
18.            Chawa si nzito lakini husumbua.
–  Matatizo madogo madogo yasipodhibitiwa tangu awali huweza kusumbua na kusababisha matatizo makubwa zaidi.
–    Hutumika kuwatahadharisha wale wenye tabia ya kudharau matatizo madogo madogo kwani huweza kuongezeka na kushindwa kutatulika.
–  Sawa na “mdharau mwiba guu huota tende, usipoziba ufa utajenga ukuta.”
19.            Cheche huzaa moto.
–         Kitu kidogo huweza kuleta madhara makubwa.
– Hutumika kuwatahadharisha wale wanaodharau mambo madogo kwani huweza kusababisha madhara makubwa yasiyotegemewa.
–         Sawa na “mazoea hujenga tabia”
20.            Cheche ndiyo moto.
–         Tabia ya mtu huonekana kupitia matendo yake.
–      Hutumika kuwatahadharisha watu katika maisha wanapaswa kufanya mambo kwa umakini kwani kupitia kwayo huweza kutambulika haraka.
21.            Chechema utafika wendako.
–         Hata ukitembea polepole utafika tu.
–         Hutumika kuwafariji watu waliokata tamaa katika mambo mbalimbali kuwa na uvumilivu katika yote kwani uvumilivu ndiyo msingi wa mafanikio katika maisha.
22.            Cheka uchafu, usicheke kilema.
–         Usimdhalilishe binadamu mwenzako kwa lolote lile.
–   Hutumika kuwaasa watu wenye tabia ya kuwanyanyapaa walemavu kwani hawakupenda kuwa hivyo na hata wao watambue kwamba wanaweza kupata ulemavu wakati wowote.
–   Usimcheke mtu mwenye shida kwani hata wewe siku moja unaweza kupata shida kama hiyohiyo.
23.            Chema chajiuza, kibaya chajitembeza.
– Siku zote kitu kizuri (watu wazuri) hujulikana tena bila hata kutangazwa. Lakini kitu kibaya hulazimu kutangazwa tena hata ikibidi kutia chuku ili kionekane kizuri.
–         Methali hii hutumika kuwaambia watu wasio na wema katika jamii.
24.            Chema hakikai, hakina maisha.
–         Daima katika maisha kitu chema hakidumu kwa muda mrefu.
–  Hutumiwa kuwafariji wale waliofiwa na wapendwa wao. Pia huweza kutumika wakati watu wanazungumza juu ya habari za mtu aliyekuwa mwema ambaye huenda amefariki dunia.
–         Sawa na “Wema hauozi.”
25.            Chema hakikai, hakina maisha.
–         Daima kitu kizuri katika maisha hakiwezi kuishi kwa muda mrefu.
–   Hutumika kuwatia moyo na kuwafajiri wale wote waliondokewa na ndugu, jamaa na marafiki zao.
26.            Chema hujiuza, kibaya hujitembeza.  (tazama: 23)
27.            Chema hutakwa na Mungu na watu.
–         Kitu kizuri hupendeza machoni mwa kila mtu pamoja na Mungu pia.
–         Huasa watu kuwa na tabia nzuri kwani hupendeza mbele jamii na hata kwa Mungu pia.
28.            Cheupe dawa, cheusi dalili hawa.
–   Tabia na sifa nzuri huongeza utu na thamani ya mtu, lakini tabia mbaya huondoa utu na thamani ya mtu huyo pia huondoka katika jamii.
29.            Chini kwetu juu kwa Mungu.
–         Hakuna binadamu anayeweza kuingilia mamlaka ya Mungu.
–         Huonya watu kuacha tabia ya kuingilia mamlaka ya Mungu.
30.            Chini ya mdogo juu ya mkubwa.
–         Usijiamini kwa nafasi uliyonayo na kujifanya wewe ndio wewe katika maisha kwani wapo watu ambao wamekuzidi.
–    Hutolewa kwa watu ambao huringia nafasi na vyeo walivyo navyo katika maisha.
31.            Chini yetu Juu ya Mungu. (tazama: 29).
32.            Chipukizi ndio miti.
33.            Vijana ndio taifa la kesho.
–     Hutumika katika kuelimisha watu wasiwadharau vijana na kuwanyima haki zao kwa sababu vijana ndio taifa la kesho.
34.         Chombo cha kuvunja (kuharibika hakina rubani)
–         Kitu au jambo lililoharibika kamwe halina mwokozi.
–   Hutolewa kwa watu wanaostaajabu na kulaumu kwa nini jambo limetokea na kutaka wajue kuwa jambo likisha tokea limetokea.
35.            Chombo cha mwenye kiburi hakifiki bandarini.
–         Watu wasiopokea ushauri daima hawafanikiwi.
–   Hutumika kuonya watu wasiopenda kushauriwa ili wapende kufuata ushaurikwani si kila ushauri ni mbaya.
36.            Chongo kwa msangu, kwa mswahili rehema ya Mungu.
–         Kitu kisicho na thamani kwako kwa mwenzio kinathamani.
–         Hutolewa kwa wale wanaodharau vya wenzao.
37.     Chongo kwa mnyamwezi kwa mswahili rehema ya Mungu. (tazama: 36)
38.            Choyo huweka mali mpaka ikaoza.
–         Uchoyo husababisha uharibifu wa mali.
–         Huonya watu ambao hawapendi kutoa vitu vyao kwa wahitaji mapaka vinaharibika
39.            Chuchu mpya huangua chuchu ya zamani.
–         Kitu kipya husababisha maendeleo ya kile cha zamani.
–     huelimisha watu juu ya kutunza na kuthamini vya zamani kuwa vyote kwa pamoja ni sehemu ya maendeleo.
40.            Chombo mpya huangua chombo ya zamani. (tazama: 39)
     41.    Chuki hupotoa watu.
– Daima chuki hupoteza watu mpaka wakashindwa kuaminiana, kupendana na hatA kushindwa kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo.
–   Hutolewa kwa watu ambao wanachukiana na kuwatahadharisha kuwa hali hiyo huleta athari mbalimbali katika maisha.
    42.            Chuki hupotoa haki na watu.
–         Chuki hupoteza haki na huleta mfarakano baina ya watu.
–   Hutumika kuwaelimisha watu juu ya athari za chuki kuwa hupoteza haki za watu na pia kufarakanisha watu hao.
    43.        Chuma kimetawala dunua.
–         Watu wenye mamlaka wametawala dunia.
–      Hutumika kuonesha kuwa watu wenye mamlaka ndio waamuzi wa kila kitu.
    44.      Chuma kipate kingali moto.
–         Ni vyema kufanya mambo katika wakati mwaafaka.
–  Kuhamasisha watu kufanya mambo katika wakati unaofaa bila kusubiri.
    45.       Chumvi ikizidi chakula huaribika.
–         Uongo ukizidi hupoteza uaminifu.
–    Huambiwa watu wapendao kusema uongo, kutoa ahadi bila kutekeleza (hasa kwa viongozi kuwa hupelekea jamii au watu wanaowaongoza kushindwa kuamini kabisa)
    46.            Chumvi ilihadaa watu kuja pwani kama sukari.
–         Tamaa ya mali iliwashawishi wageni kuingia nchini mara kwa mara.
–         Hujuza watu kuhusu historia ya uvamizi wa wageni nchini na lengo la kuja kwao ambalo lilikuwa ni kujipatia utajiri.
–         Pia hutumika kutoa funzo kwamba ni vyema kutafiti jambo kabla ya kutenda.
    47.       Chungu huvunjika magae na mtu huharibika asifae.
–         Hakuna kitu ambacho hakina mapungufu.
–  Hujuza watu kuwa hata binadamu anaweza kuharibika na kupoteza thamani sawa na vitu vingine kama chumvi. Hakuna kitu ambacho kimekamilika.
     8.            Chungu kibovu kimekuwa magae.
–         Kitu kilichoharibika huweza kukosa thamani kabisa.
–   Hutahadharisha watu kuwa kilichoanza kuharibika kisipo chukuliwa hatua huharibika zaidi.
   49.      Chura hushangilia mvua wala hakina (hana mtungi).
–    Watu wengi hufurahia mafanikio fulani bila kujua sababu za mafanikio hayo.
–  Hutolewa kwa wale wote ambao hupenda kufurahia mafanikio bila kufuatilia hatima ya mafanikio hayo ikiwa wao ni sehemu ya jamii hiyo.
50.            Chururu si ndondondo.
–         Jambo kubwa si sawa na jambo dogo.
–         Kuhamasisha watu ambao wanajuhudi katika kufanya kazi ndani ya jamii kuwa waongeze juhudi.
 51.            Dalili ya mpumbavu hupumbaa.
–  Dalili ya mtu mwenye mienendo mibaya huonekana kutokana na matendo yake katika  jamii.
–         Hutumika kuwaonyesha watu ambao hawajali hususani mambo yaliyo ya msingi.
52.            Dalili ya mvua mawingu.
–       Mafanikio ya mtu katika maisha hutegemeana nay eye mwenyewe jinsi alivyoyaandaa.
–         Hufundisha watu kuchukua taadhari.
53.            Dalili ya vita matata.
–         Kila matatizo yanayotokea katika jamii kuna  chanzo chake.
–         Tuondokane na migogoro inayochangia vita.
54.            Damu nzito kuliko maji.
–      Ndugu ni ndugu tu hata kama wakigombana watapatana hawataweza kutengana kamwe.
–         Hutumika kuhamasisha ndugu kuthaminiana/kusaidiana.
55.          Dau la mnyonge haliendi joshi,likenda joshi ni mungu kupenda.
–       Shida au matatizo ya mtu hayawezi kumuathiri mtu mwingine
–         Hutumika kuwaonya
56.            Dawa ya deni kulipa
–         Uaminifu katika maisha ni muhimu ili kuweza kuishi na jamii pasipo shaka.
–         Huwaonya watu wanaokopa  wanatakiwa wawe wanalipa kwa wakati.
57.            Dawa ya moto ni moto.
–         Ubaya hulipwa kwa ubaya.
–         Usimwogope kumkabili mtu.
58.            Dawa za wakurugenzi ni mizizi na makombe.
–    Viongozi walio wengi ili waweze kutwaa madaraka au kushika nyadhifa, lazima wapitie katika mambo ya kishirikina.
–         Kuwakosoa watu waendekezao imani potofu.
59.            Dhahabu haina maana chini ya ardhi.
–         Kukosa maarifa katika kazi ni sawa na hujafanya chochote.
–         Maarifa yanahitajika katika kazi ili uweze kufanikiwa.
60.            Dhambi hukimbiwa ,haikimbiwi.
–         Kitu chochote chenye hatari na chenye kuleta madhara hakina urafiki.
–         Huwataadharisha watu wenye mienendo mibaya.
61.            Dhihaka ina ukweli nyingi.
–         Si kila jambo lisemwalo kiutani halina ukweli ndani yake.
–   Tusidharau mambo yoyote yanayokuwa yanasemwa na watu ili baadaye tusije juta.
62.       Dhihaka ina kweli ndani. (tazama: 62)
63.            Dhiki hukumbusha deni la zamani.
– Unapopatwa na matatizo au shida kwa mara nyingine lazima kukumbuka yaliyokufika kipindi cha nyuma.
–         Hukumbusha kulipa deni kabla ya wakati ili uaminiwe zaidi.
64.            Dini ni mali ya roho.
–    Kila jambo lina wakati wake katika kupenda ambapo husukumwa na roho.
–         Tupende vitu kutoka rohoni na wala tusilazimishwe.
65.            Dunia duara huzunguka kama pia.
–   Usimfanyie mwenzako ubaya pasi kutambua kwamba ipo siku huyo mtu atakusaidia.
–         Hutumika kuonyesha namna maisha ambavyo hayatabiriki.
66.            Dunia hadaa na walimwengu shujaa.
–         Maisha ya duniani yamejaa hila na yanahitaji werevu na ushujaa.
–         Dunia huitaji werevu na ujuzi kuikabili.
67.            Dunia haidawamu,hudumu nayo.
–         Mambo ya duniani ni ya kupita, hayadumu.
–         Hutoa funzo kwa watu wasihadaike na mambo ya duniani.
68.            Dunia haishi kupambwa na kuharibiwa.
–         Wajengao ndo waharibuo au akupendaye kwa leo kutokana na fadhila zako kesho aweza kukua pasipo kutegemea.
–         Huonyesha namna dunia inavyokuwa na vitu vibaya na vizuri.
69.            Dunia haishi kupendwa na watu.
–         Mambo mazuri hayaishi kupendwa na watu na hata kuharibiwa.
–         Kuwa makini na vitu vilivyoko duniani si vyote ni dhahabu.
70.            Dunia haishi upya ingawa ya zamani.
–   Utu uzima au uzee hauwezi ukawa kizuizi kwa mtu kutokuwa na mawazo yanayojenga katika jamii (hekima,busara).
–         Tuwaenzi watu wazima ili watupe mapya.
71.            Dunia huleta jema na ovu.
–         Kila binadamu anao wema wake na hata uovu pia.
–         Tusitegemee  mema maishani bali hata mabaya.
72.            Dunia huzunguka kama pia.
–         Dunia huitaji maarifa kuikabili na wala sio kuiamini moja kwa moja.
–         Tusikurupukie mambo pasipo kuwa na maarifa au uelewa nayo.
73.            Dunia ikupapo soni, kila utendalo huzuni.
–   Walimwengu wakikuacha au kukugeuzia shingo, kutoshirikiana mambo utajisikia vibaya.
–         Walimwengu twapaswa kuishi nao vyema.
74.            Dunia kitu dhaifu.
–         Hakuna mtu aliyemkamilifu katika dunia hii.
–     Hatuna budi kusameheana katika mapungufu na madhaifu tuliyonayo.
75.            Dunia kubwa  mtakwisha hamu na kiu.
–         Mambo ya dunia hii ni mengi huwezi kuyamudu yaliyo yote.
–    Kuwa na kiasi katika maisha kwa kufanya uchaguzi ulio sahihi ili kuondokana na tamaa zisizo za lazima.
76.            Dunia mapito haiweki alama wala nyayo.
–    Wanadamu na mambo yao yanapita kila wakati,na siku husogea na mambomapya huibuka.
–       Watu wanapaswa kujua kwamba hapa duniani mambo mengi yanapita, haina haja ya kushikilia sana yaliyopita hasa mabaya, twapaswa kuyasahau kwani hayaweki kumbukumbu yoyote nzuri katika maisha yajayo.
77.            Dunia mti mkavu kiumbe siulemee.
–    Dunia inafananishwa na kitu dhaifu kama mti mkavu ambao hauna nguvu hivyo mwanadamu hapaswi kutegemea sana.
–        Walimwengu si watu wa kutegemea katika maisha waweza kukupoteza.
78.            Dunia nzito kwa mtu mjinga.
–    Mambo huwa magumu kwa mtu mjinga asiyeweza kutumia akili katika kujikwamua kutika hapo alipo hadi kwingineko.
–      Inawafundisha watu kutumia akili katika kufanya mambo kwa bidii ili wasije wakalemewa na maisha .
79.            Dunia pana msilie ngoa.
–     Usilie na kuumia (wivu) unapoona mwenzako kapata kwani kila mmoja ana bahati yake.
–     Inatupasa kutokuwa na wivu juu ya maendeleo ya mtu bali tujifunze kwa waliofanikiwa ili nasi tufanikiwe.
80.            Dunia toto kwa mtaalamu.
–         Hakuna mtu anayeweza kushindana na dunia.
–   Huhamasisha watu kuwa makini na maisha ya duniani hususani katika kuzikabili changamoto zake.
81.            Dua la kuku halimpati mwewe.
–   Dharau na kiburi haviwezi kumuathiri mtu aliyeko juu yako katika maisha au laana ya mnyonge na malalamiko yake hayamtishi mwenye nguvu.
–         Kulalamika sio ndio suluhisho la matatizo.
82.            Eda ni ada yenye faida.
–   Mwanamke kukaa eda ni muhimu na yenye mafunzo makubwa na faraja pia.
–         Kuwaasa wanawake kuwa mila na desturi zinapaswa kuenziwa.
83.            Eda ya mke hakuna eda yam me.
–         Eda huwekwa wanawake waliofiwa na waume zao tu na sio wanaume.
–         Mwanamke anaonwa kama mlezi mkuu wa familia hivyo anapoachiwa jukumu la kulea anapaswa kufundwa.
84.            Ee huyu ana ndaro si ukali wa tumbili.
–   Mtu anayetishia na kujitapa hana uwezo wa kufanya lolote. Mara nyingi anayejitapa mno kabla ya kufanya jambo hafanikiwi.
–         Inatuasa kuwa ukitaka kutenda jambo onesha kweli kwa vitendo na sio matambo na vitisho.
85.            Egemeo la mnyonge ni Mungu.
–  Mungu ndiye muweza wa yote katika maisha ambapo mnyonge hukimbilia.
–  Tuishi kwa kufuata mienendo miema impendezayo mungu ambaye ndiye kama kimbilio la mnyonge.
86.         Elekeo la moyo hushindwa na la akili.
–         Akili ndiyo hutawala na ndio mwongozo wa kila jambo.
–   Kufundisha watu kuwa twapaswa kutumia akili kupambana na kuamua mambo.
87.            Elimu haina mwisho.
–         Elimu haina mwisho au haina kikomo.
–         Tujielimishe pasipo kuwa na mwisho wake.
88.            Elimu bahari haikaushiki. (tazama: 88)
89.            Elimu bahari haiishi kwa kuchotwa.
–  Penye maarifa na ujuzi hapaishiwi, watu hupenda kuchota pasipo kikomo.
–  Tusitosheke kwa mambo yenye manufaa maishani kama elimu.
90.            Elimu bila adabu ni uharabu.
– Unapokuwa na elimu na ukaitumia kinyume na ilivyotakiwa ni uharibifu
–         Tuyatumie vizuri maarifa tuliyoyapata.
91.            Elimu bila adili ni ujahili.
–         Elimu bila hekima ni kazi bure.
–         Hutumika kuhamasisha watu kuthamini elimu.
92.            Elimu hushinda nguvu.
–   Ukiwa na maarifa, weledi na ujuzi katika kazi utashinda nguvu ambazo ungezitumia.
– Tusipende kutumia nguvu nyingi katika kazi badala yake maarifa ndiyo yatumike.
93.            Elimu hutaka adabu.
–         Inamaana kuwa ili kufanya jambo zuri inatakiwa kuwa na uvumilivu.
–         Tunatakiwa kuwa na nidhamu katika kufanya mambo yenye tija.
94.            Elimu kidogo hatari.
–         Mwenye elimu ya chini mara nyingi huwa na matatizo.
–      Kuwa na kiwango fulani cha elimu husababisha usumbufu katika jamii hasa kwa yule aliyenayo elimu hiyo.
–   Huonya wale ambao wana kiwango fulani cha elimu kutojisikia kuwa wao ndio kila kitu kwani wapo ambao wamewazidi katika hilo.
–   Huhamasisha watu kujipatia elimu ya kutosha ili kuzikabili changamoto mbalimbali za maisha.
95.            Elimu kidogo wazimu.

96.            Elimu mwangaza
–         Elimu ndio njia ya kila kitu katika maisha.
–   Huhamasisha watu kuwa na bidii katika kutafuta elimu kwani ndio kila kitu katika maisha.
97.            Elimu ni nguvu kwa mwanadamu.
–         Elimu ndio mkombozi katika maisha ya mwanadamu.
–         Huhamasisha watu kuthamini elimu kwani ndio dira ya maisha.
98.            Enda mwanakwenda usirudi tena.
–         Nenda moja kwa moja usirejee tena.
– Hutumika katika migogoro baina ya watu huku wakijibizana lilikusisitiza kuwa hakuna haja ya kuonana tena.
99.            Endaye ya akhera si wa marejeo.
–         Mtu ambaye amepoteza kamwe harudi tena duniani.
– Hutumika katika kuhamasisha watu kupunguza masikitiko na kufanya shughuli nyingine, kwani mtu akishafariki hawezi kurudi tena.
100.            Endaye hufika atakakokwenda.
–         Kila mwenye juhudi ya kufikia mafanikio fulani daima hufanikiwa.
–         Kuhamasisha watu kutokata tamaa katika harakati za maisha.]]>

<![CDATA[MTOTO MWENYE KIPAJI CHA AJABU BINGWA WA METHALI MTAZAME]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=740 Mon, 02 Aug 2021 11:44:16 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=740
BOFYA HAPA KUTAZAMA >>>>>]]>

BOFYA HAPA KUTAZAMA >>>>>]]>
<![CDATA[MISEMO,NAHAU NA METHALI ZA KISWAHILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=739 Mon, 02 Aug 2021 10:45:59 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=739 Pia, misemo ni fungu la maneno ambalo hutumiwa na jamii tofautitofauti kwa lengo la kusisitiza maadili fulani.
 
Kwa mfano tukisema mtu amegonga mwamba hatumaanishi kwamba amepiga jiwe kubwa kwa kifaa chochote au kwa mkono, bali tunamaanisha kwamba ameshindwa kuendelea katika jambo fulani.
Ifuatayo ni misemo ya kiswahili na maana yake.
Kupata jiko
Huu msemo haumaanishi kununua au kuazimz jiko la kupikia. Una maana ya kupata mke au kuoa. Kwa hivyo, mtu anaposema nimepata jiko anamaanisha kuwa ameoa.
Kuangusha uso
Maana ya huu msemo ni kuona aibu au soni mbele ya watu kwa jambo mbaya ulilolitenda. Mfano wa matumizi ni kama: ukitenda mema hapatatokea haja ya kujishusha hadhi kwa kuangusha uso kila wakati.
Kuenda mbwehu
Maana yake ni kutoa hewa mdomoni. Naneno lingine lililo na maana sawa na kuenda mbwehu ni kuteuka. Mfano wa matumizi ya msemo huu ni kama vile: Kwenda mbwehu ugenini ni dalili ya ulafi.
Enda msobemsobe
Maana kamili ya msemo huu ni kuenda pasipo na utaratibu wowote. Pia huweza kumaanisha kuenda pasipo na hiari. Mfano katika sentensi: alipougua malaria alikuwa akienda msobemsobe.
Enda mvange
Kabla ya kutoa maana ya msemo huu, ni vizuri uelewe kuwa maana ya neno ‘mvange’ ni ‘kombo’. Kwa hivyo mesomo huu unaweza kuwa ‘enda kombo,’ na maana yake mambo kufanyika kwa namna isiyotarajiwa. Kwa mfano, namshukuru Mola kwa sababu biashara yangu haikuenda mvange.
Chokoza nyuki mzingani
Mzinga ni nyumba ya nyuki. Musemo huu unamaanisha kuenda palipo na hatari na kujaribu kuichokoza au kuikabili kijiga hatari hiyo. Mfano katika sentensi: kung’oa simba usinga wake wa shingoni ni mfano wa kumchokoza nyuki mzingani.
Bwaga wimbo
Maana yake ni kuanzisha au kuongoza wimbo. Msemo huu huwezeka kutumika katika sentinsi kama ifuatayao; mahadhi ya aliyeubwaga wimbo yalikuwa mazuri.
Anua majamvi
Maana ya msemo huu ni kutamatisha jambo au shughuli fulani uliyoanzisha. Pia kukunja jamvi ina maana sawa na kuanua majamvi. Kwa mfano, baada ya wanariadha kuanua majamvi yao, walirejea nchini.
Choma mkuki
Maana ya msemo huu ni ‘kufuma’ au ‘shambulia’ kwa kutumia mkuki. Kwa mfano, siku hizi vituko ni vyingi, aghalabu watoto wanawachoma mikuku wenzao kwa utesi wa mashamba.
Fanya ndaro
Neno ndaro linamaanisha sifa au sifu. Msemo huu unamaashisha kujisifu kwa jinsi mtu anavyozumgumza. Kwa mfanfo, ni vizuri uyaeleze yote uliyoyapitia bila ya kujifanyia ndaro na kumbe hamna lolote.
Fanya speksheni
Speksheni ni neno ambalo lina maana sawa na ukaguzi. Hivyo basi, msemo huu unamaanisha fanya ukaguzi au kagua. Kwa mfano, mkubwa wa kituo cha polisi hufanya speksheni ya nyumba zote za polisi kila jumapili.
Fanya udhia
Msemo huu unamaanisha kufanya usumbufu. Kwa mfano, hakudhamiria kufanya udhia kwa matamshi yake kwani aliyoyasema ni ya kweli.
Arusi ya mzofafa
Neno ‘mzofafa’ lina maana sawa na maringo au madaha. Arusi ya mzofafa ina maana sawa na arusi iliyonoga kwa mbwembwe na hoihoi. Kwa mfano, Bwana alituandalia arusi ya mzofafa hatutaisahau.
Kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa
Msemo huu una maana kuwa unapewa sifa usizostahili. Msemo mwingine ulio na maana sawa ni kuvalishwa kilemba cha ukoka.
Chezea unyango wa kima
Msemo huu huweza kutumika kuonya mtu dhidi ya jambo fulani. Kwa mfano, ” wewe, utakiona leo, nitakuchezesha unyago wa kima”. Inaaminika kuwa kima huacheza ngoma (Unyago) ili kuwatoa vigori (Wali). Tendo hili  hufantika kwa siri na endapo watagundua umewaona, lazma nawe uchezeshwe. Kwa hivyo, kuwa makini na mambo ya watu, usije ukachezeshwa unyago wa kima!
Bura yangu sibadili na rehani
Huu ni msemo ambao una maana lukuki, baadhi ya watu hutafsiri neno “bura’ kama kitu cha tunu kichakavu. Kwa hivyo msemaji wa msemo huu hunamaanisha kuwa hawezi badili kitu chake cha tunu kwa kipya.
Usiache “mbachao” kwa msala upitao
Katika msemo huu, wahenga wametumia neno “mbachao” linatamkwa “m-bachao,” yaani ni kifaa duni kinachotumiwa kufanyia ibada, Kwa mfano, mkeka au jamvi kuukuu (Kidukwa)..sasa wamesisitiza usije ukauacha kwa “Msala” upitao..msala nao ni sehemu ya kusalia lakini si duni kama ilivyo m-bachao. Pia, msemo huu un maana sawa na Usiyadharau madafu, maembe ni ya msimu.
Mwanya ni kilema pendwa
 Wengi hawafahamu kuwa hata kama mwanya ni kilema, lakini ni kilema kinachopendwa na wengi. Vilema vya aina hii hutambulika kama ‘vilema pendwa’, vipo vingi kwa uchache ni baadhi ya matege ya miguu, makalio makubwa, vifua, na misuli mikubwa.
Mungu hakupi kilema akakunyima mwendo
Msemu huu una maana kuwa mtu anapaswa kuridhika na alicho nacho. Funzo kuu ni kuwa haina haja kutamani vitu ambavyo vimepiku uwezo wetu.
Mlevi haukubali ulevi
Msemo huu una maana kuwa hata anywe vipi hakubali kuitwa mlevi. Msemo hu umewalenga mahasidi na mafisadi ambao hukataa chungu ya ukweli.
Chongo kwa mnyamwezi kwa mswahili amri ya mungu
Wengne hutumia neno ‘chogo’ badala ya ‘chongo’, yote kheri alimradi haipotosha maana ya usemi huu.
Ushikwapo shikamana, si wengi wa kupendana
Maana ya msemo huu ni, endapo atatokea mtu akakupenda na akaomba muwe marafiki usikatae, kwani hapa ulimwenguni watu wachache sana wanaopendana.
Maji! Ni kumbwe na kinyweo, matupu yasonga moyo
 Maana ya msemo huu ni kuwa, kunywa maji pekee bila ya kula chakula yaweza kusumbua tumbo. Ni vema upatapo mgeni umpe chakula kwanza halafu ndo umpe maji. Ni vizuri uelewe kuwa msemo huu unaweza kuwa na maana tofauti tofauti kulingana na muktadha uliotumika.
Akomelepo mwenyeji na mgeni koma papo
Msemo huu wa kiswahili una maana kwamba mgeni anapaswa fuatisha mipaka ya mwenyeji wake. Endapo atakushawish jambo fulani,usipinge.
Pema usijapo pema, ukipema si pema tena
Kaana ya msemo huu ni kuwa, mahala popote huwa pazuri endapo hujawahi kwenda. Ukishaenda mara kwa mara uzuri wake huisha. Hutumika kuonya mtu dhidi ya kuzoea jambo fulani kwa uzuri wake kwa sababu anaweza kuzoea ule uziri na pindi ukipotea hatakuwa na sababu ya kulipenda jambo hilo.
Mwanaharamu hata umtie kwenye chupa atatoa japo kidole ili ajulikane kama yupo
Msemo huu unamlenga mtu aliye na tabia mbaya. Maana yake ni kuwa, popote aendapo lazma atataka mtambue uwepo wake.
Afugae ng’ombe tume, mwenye ziwa la kujaza
Usemi huu una maana kuwa, fanya kazi kwa bidii na utafaidi matunda ya kazi ya mikono yako. Msemo mwinigine ulio na maana sawa ni ‘mwenye kisu kikali ndiye ataekula nyama.’
Usione ukadhani
Huu ni msemo ambao nafahamika na wengi. Una maana kuwa, usije liona jambo na ukaridhika na tafsiri ya awali. unapaswa ulichunguze kwa makini ili upate uthibitisho wake pengine lina maana tofauti. Msemo huu unatufunza umuhimu wa kuhakiki jambo fulani ili kuhepuka tafsiri hasi.
Punda afe mzigo wa bwana ufike
Msemo huu hautushawishi kuua punda ili kufikisha mzingo. Una maanana kuwa, weka lengo la kutimiza wajibu wako. Labda kutakuwa na vizuizi katika kutimiza wajibu, lakini ili kulinda hadhi na cheo chako iwe kazini au popote pale ulipopewa wadhifa,jitahidi utimize wajibu wako kwa gharama yoyote.
Usimlaumu mungu kwa kumuumba chui, mshukuru hakumpa mbawa
Maana kuu ya msemo huu ni kwamba, unapaswa kumshukuru mungu kwa hicho mungu alichokujaalia, wala usikosoe uumbaji wake. Funzo kuu kutokana na msemo huu ni kuwa mungu huumba au hutoa kwa makadirio maalum, hazidishi wala hapunguzi. Hebu fikiria kama chui andegukuwa na mabawa tungekuwa wapi.
Maji ya kifuu bahari ya chungu
Msemo huu una maana kuwa jambo dogo unalolidharau wewe, wenzako linawatoa jasho. (maji ya nazi mdudu chungu/sisimizi kwake sawa na bahari).
Mgala mwue na haki yake umpe
Maana  ya musemo huu ni kuwa, Hata kama umeamua kumkandamiza mtu kwa kumfanyisha kazi ngumu ama malipo duni, mtimizie ulichomwahidi ama iliyo haki yake.
Kutoa ni moyo usambe ni utajiri
Msemo huu unatufunza kwamba kuwasaidia wengine si kuonyesha utajiri mtu alionao bali ni ishara ya upendo na kujali maslahi ya wengine.
Bure huchosha
Msemo huu unadhamiria kutufunza kuwa si vizuri kuzoea kupenda kupokea vitu bila kufanya kazi. Tabia hii ya kupokea tu hukwaza wanaotupa, ama labda wao wakatusema vibaya na kutukera.
Ampaye shetani maana,hujipatisha ghadhabu za Rahamani
Msemo huu unamaanisha kuwa anayemsifu shetani au mtu mwovu humchukiza Muumba na kujiletea adhabu. Msemo huu unatuonya kama wanajimii dhidi ya kuwapa watu waovu sifa nzuri.
Bahati yenda kwa wawi wema wakalia ngoa
Maana ya msemo huu ni kuwa bahati ikiwaendea watu waovu, wema huwewaonea wivu iweje wamebahatika? Husistaajabishwe na hayo kwani bahati haibagui.
Akuchukiaye hakosi hila ya kukutia
Maana ya msemo huu ni kuwa, mtu asiyekupenda anaweza kukuzushia mabaya ilimradi tu, akuchafue, akuharibie sifa zako, au mambo yako.
Waja kufa na laiti na vyanda kinywani
Msemo huu unatufunza kuwa tusipozingatia ushauri ama makanyo tutaishia tukifikwa na mabaya na tujutie kutoyazingatia.
Afichaye ugonjwa hufichuliwa na kilio
Funzo kuu katika msemo huu ni kuwa anayefanya siri matatizo yake huumbuka pale yanapomzidi ama kumgharimu hadi kuonekana.
Utatumiaje mchuzi nyama usile
Msemo huu unawalenga watu ambao wnapenda kujinufaisha na mali ya watu wengine ilhali hawataki kuhusishwa na wao. Maana ya msemo huu ni iweje wamkataa mtu ilhali unajinufaisha na vilivyo vyake?
Hutendwaje ikafana shubiri ikawa tamu?
Msemo huu unatufunza kuwa haiwezekani mtu kubadili jambo hata likawa kinyume na lillivyoumbwa au linavyofahamika.
Midundo ikibadilika ngoma huchezwa vingine
Maana kuu ya msemo huu ni kuwa, mabadiliko yanapotokea katika mazingira yako, huna budi kubadili mbinu ili kukabiliana na mabadiliko hayo. Funzo kuu ni kuwa wanajamii wanapaswa kukubali mabadiliko badala ya kulalamika.
Bata mtaga mayai usichinje kwa tamaa ya wingi
Msemo huu una funzo nzuri sana kwa wanajamii. Maana yake ni kuwa tamaa za haraka za kukifaidi kitu zisituponze tukaharibu manufaa makubwa zaidi ya kitu hicho hapo baadae.
Samaki mkunje angali mbichi
Msemo huu ni muhimu sana katika jamii yetu. Unatufunza kwamba ni vinzuri kuwaonya watoto wetu tangu utotoni mwao ili kwafanya waelewe mambo na kujirekebisha kwa urahisi.
Bahati ikibisha hodi sharti ufungue mlango mwenyewe
Msemo huu unamaanisha kuwa unapopata fursa ama nafasi ya kutenda jambo yakupasa uitumie vema na si kuipuuzia au kukata usaidiwe kuipokea. Kwa hivyo, ni vyema wanajamii wajifunze kutumia fursa tofauti tofauti kama inavyohitajika.
Kipenda roho hula nyama mbichi
Msemo huu una maana kuwa, mtu hujitosa hata kuyatenda mambo yasiyo ya kawaida au magumu bora apate anachokipenda.
Dunia tambara bovu ukivuta utachana
Msemo huu untuonya dhidi ya kuwaamini sana wanadamu. Maana yake ni kuwa, usiwaamini sana walimwengu au  kuwategemea sana kwani wanaweza kukutenda.
Cha mchama huchama cha mgura hugura
Msemo huu una maana kuwa asiyekuwepo kulinda mali yake au kutunza mali yake huishia kutumiwa vibaya ama kumalizwa na wengine ambao labda hawana.
Akopaye akilipa huondokana na lawama
Huu ni msemo ambao una funzo nzuri sana kwa wanajamii. Una maana kuwa anyekopa akilipa hujiondolea lawama. Kwa hivyo, ni wajibu wate kuhakikisha tumeiondolea lawama kwa kulipa madeni yote yanayotukabili.
Achezaye na tope humrukia
Msemo huu una maana kuwa unaposhiriki kutenda uovu si ajabu mabaya hayo yakakudhuru mwenyewe. Kwa hivyo, msemo huu unatuonya dhidi ya kushiki katika kutenda uovu.
Waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba
Pemba ni mji fulani wa pwani na waswahili wanoishi huko huvalia vilemba. Msemo huu una maana kuwa watu a tabia moja hujuana kwa mambo wanyofanya.
Lenye mwanzo lina mwisho
Msemo huu unamaanisha kuwa jambo lolote lililo na mwanzo lina mwiso. Msemo huu una maana sawa na hakuna ndefu lisilokuwa na mwiaso.
Zunguo la mtukutu ni ufito
Msemo huu unatufunza kuwa njia ya kumfunza mtoto mkaidi ama asiyesikiliza ni kumpa adhabu.
Maji usiyoyafika hujui kina chake
Msemo huu unamaanisha kwamba jambo ambalo hujalifanya hujui ugumu wake. Pia, msemo huu una maaana sawa na kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.
Ukiwaona ni watu moyoni hawana utu
Msemo huu unamaanisha kuwa usifikiri kwamba kila uliyekuwa karibu naye anakupenda kwa dhati wengine ndio maadui zako namba moja na ni vigumu kuwatambua.
Afadhali jirani mbuge kuliko jirani mwenye mdomo mrefu
Msemo huu una maana kuwa mtu anayefitini wengine ni hatari kuliko hata mlafi.
Misemo ni muhimu sana katika jamii. Kwanza, ni njia ya kupitisha mafunzo kutoka kazazi kimaja hadi kingine. Pia, misemo huwafunza wanajamii kuhusu utamanduni wao, ni njia ya kujiburudisha na pia hutumika kuonya au kushauri.
Kwa hivyo, ni vyema wanajamii kuitumia misemo kila siku kwani itawajenga kielimu na pia kimaadili.]]>
Pia, misemo ni fungu la maneno ambalo hutumiwa na jamii tofautitofauti kwa lengo la kusisitiza maadili fulani.
 
<![CDATA[VITENDAWILI VYA KISWAHILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=738 Mon, 02 Aug 2021 10:28:34 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=738 miayo.
      Ni kawaida kwenda miayo baada ya kuamka.
      2. Abeba mishale kila aendako – Nungunungu
au hata Kalunguyeye.
  m.s. Kalunguyeye ni mnyama mdogo mwenye ngozi yenye miiba kama ya nungunungu. Nungunungu ni mnyama mkubwa mwenye mishale mingi mwilini      anayoitumia kujihami au kujilinda na adui zake. Hawa ni wanyama wenye ngozi yenye miiba.
      3. Abiria wote wamelipa ila hawa weusi – Nzi.
     Huwa hawakosekani popote pawapo na watu hata magarini.
      4. Adona wala hamezi – Mashine ya kupigia chapa.
    m.s. Kudona ni kupiga kitu kigumu au kugotagota. Kwa mfano, kuku hudona nafaka   zikitupwa chini. Mashine ya kupigia chapa hutoa sauti ya kugonga kama ya kuku kutokana na mpigo wa vidole vya mpiga mashine.
    5. Adui hatari; sote tumemzingira lakini hatuwezi kumshika – Moto na  wanaouota.
      m.s. Zingira  ni zunguka.
Sote tunaielewa hatari ya kuipeleka mikono karibu na moto. Ukijaribu kuushika moto utachomeka.
     6. Adui mpenzi –
Moto Moto huwa na manufaa makubwa ingawa unaweza kuleta maangamizo makubwa.
     7. Adui wa wengi lakini humwepuki popote uendapo – Nzi.
Nzi huwaletea madhara binadamu kwa kuyasambaza magonjwa na huwa kila mahali. Adui lakini popote uendapo yuko nawe.
     8. Adui yangu haniwahi –Handaki.
m.s. Handaki ni namna ya mfereji au shimo kubwa refu linalochimbwa kwa madhumuni ya kujilinda wakati wa vita. Askari hutumia handaki wakati wa vita kujifichia na huwa sio rahisi kuonekana walipo.
     9. Aenda mbio ingawa hana miguu – Nyoka.
Nyoka ana uwezo wa kutambaa au kujiburuza kwa wepesi wa ajabu.
     10.  Afahamu sana kuchora lakini hajui akichoracho – Konokono.
m.s. Konokono ni kiumbe mdogo anayetambaa na kuteleza na ambaye huacha athari ya utelezi wake kila apitapo.
     11. Afuma hana mshale  – Nungunungu.
m.s. Fuma ni kushambulia kwa kitu chenye ncha kama mkuki au mfumo. Nungunungu humshambulia adui kwa miiba yake ya mwilini.
    12.  Ajenga ingawa hana mikono – Ndege.
Kwa kawaida ndege hujenga kiota chake kwa kutumia mdomo wake.
    13.  Ajifunua na kujifunika –
Mwamvuli/ mwavuli
m.s. Mwamvuli ni fimbo iliyofungwa kitambaa kinachoweza kukunjwa na kukunjuliwa wakati wa jua au mvua. Sifa hii ya mwamvuli inaeleweka kwa urahisi.
    14. Akamatwapo mkiani hutii amri – Kata.
m.s. Kata ni neno lenye maana nyingi. Hapa lina maana ya chombo cha kuchotea maji na ambacho hutokana na kibuyu. Aghalabu watu hushika kata sehemu nyembamba iliyojitokeza kaza mkia.
      15. Akifa anajizomea – Kifuu.
m.s. Kifuu ni ganda tupu la nazi baada ya kukunwa. Ukiangalia kifuu kinachowaka moto utakiona au kukisikia kikitoa sauti ya mvumo wa moto wakati wa kumalizika.
      16. Akikaa hafi wala akilala hafi – Jiwe.
        Jiwe  halina uhai kama tujuavyo.
      17. Akikosekana maana inakosekana – Kamusi.
m.s. Kamusi ni
kitabu kinachohifadhi maneno yanayopatikana katika lugha fulani pamoja na maana
zake. Kamusi hutusaidia kuzijua maana mbalimbali za maneno.
      18. Akikuandama hupendwi – Ukoma
m.s. Ukoma ni ugonjwa mbaya wa mabatobato na ambao huharibu na kukata viungo vya mwili. Unaambukizwa na mtu mwenye ugonjwa huu huepukwa na wengine.
     19. Akila yeye na mimi hushiba – Mtoto
awapo tumboni.
Mtoto awapo katika tumbo la mama yake hupata chakula kutoka kwa mama yake.
     20. Akinishika tu, ninazaa – Bomba/mfereji.
m.s. Bomba ni chuma chenye uwazi ndani ambacho hupitisha maji. Bomba la maji linapofunguliwa maji hutoka kwa wingi.
     21. Akinyamaza hawezi kuongea tena – Maiti.
         m.s. Maiti ni mtu aliyekufa. Pia mfu au kimba. Mtu akifa huwa hawezi kusema tena.  Wengine husema hivi: Akinyamaza hawezi kusema tena.
    
     22. Akiona mwangaza wa jua yuafa – Samaki.
Samaki amezoea na anaweza kuishi majini tu, akitolewa nje ya maji hufa.
       23.Akiondoka hawezi kurudi –  Jani la mti.
Jani la mti likianguka haliwezi kurudi tena mtini. Huo huwa ndio mwisho wake.
      24. Akiongea kila mtu hubabaika – Radi.
m.s. Radi ni sauti kubwa inayotoka au kusikika mawinguni wakati wa mvua. Aghalabu radi inapopiga watu wengi hujiwa na hofu kubwa.
      25. Akishazaa yeye hufariki – Kinyonga.
   m.s. Kinyonga ni kiumbe mdogo wa jamii ya mjusi ambaye ana uwezo wa kubadili  rangi ya ngozi yake kupatana na mazingira yake. Inasadikika kuwa wakati wa kuzaa hupasuka watoto wakatoka na huwa ndio mwisho wake.
      26.  Akitambaa huringa hata akiwa hatarini – Jongoo.
m.s. Jongoo ni mdudu mdogo mweuzi mwenye miguu mingi. Hutambaa kwa mbwembwe na anapoguswa hujigeuzageuza au kujikunja.
  27. Akitoa sauti yake wote hutafuta pa kujificha – Mauti/kifo/radi.
Hamna kiumbe asiyetishwa na kifo. Vivyo hivyo radi nayo huwaogofya watu wengi.
     28.  Akitoka mkewe na watoto hulala – Jua.
Jua litokapo mwezi na nyota hazionekani; nyota na mwezi huonekana usiku wakati jua halipo. Katika mtazamo wa jamiinyingi, jua hulinganishwa na mwanamume na mwezi ni mwanamke na nyota ni watoto.
      29.  Akitokea watu wote humwona – Jua.
Jua linapotokeza huangaza dunia nzima kwa hiyo huonekana na takribban kila mtu.
    30.  Akitokea watu wote hunung’unika na kuwa na huzuni  – Ugonjwa.
m.s. Huzuni ni masikitiko au ukosefu wa furaha. Hamna anayependa ugonjwa kwa kuwa unaweza kuleta kifo.
     31.  Akivaa miwani hafanyi kazi vizuri – Mlevi.
m.s. Vaa miwani ni nahau yenye maana ya kulewa. Mlevi huwa hawezi kutegemewa kufanya lolote vizuri.

32. Akivaa nguo hapendezi akiwa uchi anapendeza – Mgomba
m.s. Mgomba ni mmea unaozaa ndizi. Mgomba hupendeza baada ya majani makavu kuondolewa.
       33.   Akopa na halipi – Kaburi.
m.s. Kaburi ni shimo anamolazwa maiti. Mtu akizikwa kaburini hawezi kurudi duniani.
    34. Alia pasipo kupigwa –  Mgonjwa wa macho.
Aghalabu mtu mwenye ugonjwa wa macho hutokwa na machozi mno.
      35. Alianika mpunga wake alipoamka haupo – Nyota.
m.s. Mpunga ni mmea unaozaa mashuke ambayo hukobolewa na kutoa mchele. Nyota huenea mbinguni usiku lakini ifikapo Asubuhi tu hutoweka; hazionekani tena kutokana na mwangaza wa jua.
      36. Akienda kwa mjomba harudi –  Jani la mti.
m.s. Mjomba ni ndugu wa kiume wa mama.
     37. Alimsimamisha jumbe njiani – Chawa.
m.s. Chawa ni mdudu mdogo anayeishi mwilini mwa binadamu hasa kutokana na uchafu wa mwili na mavazi. Chawa anapomuuma mtu huwa hawezi kutumia hadi ampate alipo.
    38. Alinipa ngozi nikaipika, akanipa nyama nikaila akanipa mchuzi nikaunywa –
Nazi.
Vifuu vya nazi aghalabu huchomwa moto na watu huila nyama ya ndani ya nazi na kunywa tui lake (mchuzi wake). Nyama ya ndani hutumiwa pia katika mapishi.
     39.  Alipita mtu mwenye kibandiko cha nguo – Nzi.
Nzi wanapotua juu ya nguo huonekana kwa mbali kama kibandiko.
    40. Alipita mtu na bunda la mishale –  Mkindu.
m.s. Mkindu ni mti unaozaa (kindu) majani ambayo hutumiwa kusukia kili; huwa ni marefu na membamba kama mishale. Bunda ni mkusanyiko wa vitu pamoja au furushi.
      41.   Aliwa, yuala; ala aliwa –  Papa.
m.s. Papa ni samaki mkubwa wa baharini anayeweza kula hata watu. Samaki huyu huwala samaki wengine naye huliwa na binadamu.
     42. Aliyechuma hakula, aliyekula hakumeza, aliyemeza hakushiba –
Mkono,  kinywa na Koo.
Mtu huchuma kwa mkono na kula kwa kinywa kisha kumeza kwa koo.
    43.  Aliyefuatwa amefika, aliyemfuata hajafika – Nazi na mkwezi.
m.s. Mkwezi ni mtu nayepanda na kuangua nazi. Nazi huanguka na kumtangulia mkwezi ambaye atashuka baadaye.
     44. Ana meno lakini hayaumi –  Kitana/Chanuo.
m.s. Kitana au chanuo ni kifaa chenye meno mengi kinachotumiwa kuchania nywele. Kitana huwa na njiti zilizopangana kama meno.
     45. Anaoga kila wakati lakini hatakati –  Chura.
Huyu ni kiumbe ambaye huishi majini; hata hivyo ngozi ya mwili wake huonekana chafu.
    46. Anaota moto kwa mgongo –  Chungu.
Chungu kinapowekwa motoni huchomwa upande wa nje ambao unalinganishwa na mgongo.
     47. Askari tele mzungu katikati –  Meno na ulimi.
Meno huwa yanauzunguka ulimi ambao kutokana na rangi yake unafananishwa na mzungu.
    48.  Baba kanipa sanduku bila funguo – Tumbo.
Binadamu hana uwezo wa kulizuia tumbo lisitamani chakula au kuzuia tumbo lisitoe chakula kilichomo.
      49. Baniani mweupe katupwa jaani –  Machicha ya nazi.
m.s. Baniani ni mhindi wa jamii ya Kihindu aghalabu myanyabiashara. Machicha ni mabaki au masazo. Masazo haya hutupwa baada ya kukamuliwa.
     50.  Hunioni lakini nakupikia – Gesi
m.s. Gesi ni aina ya hewa isiyogeuka na kuwa majimaji katika joto la kawaida ambayo huwaka na hutumiwa kuwashia moto. Gesi ni kama upepo, haiwezi kuonekana. Tunachoweza kufanya ni kuinusa harufu yake na kuona moto unaotokana nayo.]]>
miayo.

<![CDATA[METHALI ZINAZOHUSU MKONO]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=737 Mon, 02 Aug 2021 10:19:23 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=737
Mkono mmoja hauchinji ng’ombe.
Mkono mmoja haufungi kuni.
Mkono mmoja haulei mwana.
Mkono mmoja haujioshi.
Mkono mmoja haupasui kuni.
Mkono mtupu haurambwi.
Mkono na mkono ndio kitu huwa.
Mkono ni wako japo kuwa umelemaa.
Mkono ukinyewa na Mtoto haukatwi.
Mkono ushike kazi,na moyo ushike Mungu.
Mkono wa muungwana ni mizani.
Mkono utoao ndio upatao.
Mkono wa mpewaji daima hukaa chini.
Mkono wa mwenzako huwezi kukunia
Mkono na vidole ndio ngumi.]]>

Mkono mmoja hauchinji ng’ombe.
Mkono mmoja haufungi kuni.
Mkono mmoja haulei mwana.
Mkono mmoja haujioshi.
Mkono mmoja haupasui kuni.
Mkono mtupu haurambwi.
Mkono na mkono ndio kitu huwa.
Mkono ni wako japo kuwa umelemaa.
Mkono ukinyewa na Mtoto haukatwi.
Mkono ushike kazi,na moyo ushike Mungu.
Mkono wa muungwana ni mizani.
Mkono utoao ndio upatao.
Mkono wa mpewaji daima hukaa chini.
Mkono wa mwenzako huwezi kukunia
Mkono na vidole ndio ngumi.]]>
<![CDATA[METHALI ZA MGUU]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=736 Mon, 02 Aug 2021 10:13:53 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=736 Mguu mmoja hauchezi ngoma.
Mguu mmoja ni afadhali kuliko mikongojo miwili.
Mguu usiotulia huchomwa mwiba.
Mguu wa kutoka haurudi tupu.
Mguu wako ni daktari wako.]]>
Mguu mmoja hauchezi ngoma.
Mguu mmoja ni afadhali kuliko mikongojo miwili.
Mguu usiotulia huchomwa mwiba.
Mguu wa kutoka haurudi tupu.
Mguu wako ni daktari wako.]]>
<![CDATA[METHALI ZA MDOMO]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=735 Mon, 02 Aug 2021 10:01:42 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=735 Mdomo wa mnafiki hauna likizo.
Mdomo uliponza kichwa.
Mdomo uliofungwa haungiwi nzi.
Mdomo ni kioo cha akili ya mtu.
Mdomo ndio ponza.
Mdomo uliofumba unanuka.
Mdomo ni jumba la maneno.
Mdomo ni haupumziki ni kisima cha maneno.
Mdomo mtindi, maziwa kwa mwenye ng’ombe.
Mdomo wa kunya hauachi kujamba.]]>
Mdomo wa mnafiki hauna likizo.