MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Hadithi]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ 2024-12-21T17:49:04Z MyBB MwlMaeda]]> 2022-01-13T09:25:54Z 2022-01-13T09:25:54Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2216 <![CDATA[KIMYA CHENYE KELELE NYINGI]]> KIMYA CHENYE KELELE NYINGI
Akulumbale huwa hapendi kupuuzwa hata kidogo, kwa sababu hiyo,  alikata shauri la kurudi huko pasipojulikana .  Kwa hakika, kusikojulikana ndiko pahala waishipo watu wasiojulikana pia. Watu hao aghalabu huwa hawana sio tu anwani za makazi  lakini pia hata  majina yao hayatambuliki kiwepesi.
Hata hivyo,  pamoja na yote hayo, huko kusikojulikana ni tofauti kabisa na kule kimya, ambako huenda watu walioharibikiwa mambo yao.
Utasikia,  hivi bwana fulani siku hizi yuko wapi?  Iwapo bwana fulani mwenyewe anayezungumziwa  atakuwa ameharibikiwa na mambo yake, majibu huwa, '  bwana yule, yupo kimya ' ikisemwa hivyo mara nyingi huwa inaeleweka kuwa,  ingawa mambo ya huyo bwana fulani yapo msegemnege lakini uhakika uliyopo  ni kwamba, walau  huko aliko yuko hai.
Hii ni kinyume kabisa na kule kusikojulikana. Huko ikiachiliwa mbali kutojulikana kwake na kwenda bila utayari wala hiyari hakuna kikingine kinachojulikana na wengi.
Ni muhimu kufahamu kuwa,  si kila mtu aliyeharibikiwa ama kuharibiwa mambo yake huchagua kwenda huko kimya.  Kuchagua kuishi huko hutegemea ubora wa ama busara na hekima au silka na hulka zilizomkuza mtu mwenyewe.
Jambo muhimu kuliko yote katika muktadha huu,  ni kule kuweza kung'amua nyakati za mapito ya kimaisha ya mwanadamu. 
Hivyo, ni muhimu kabisa kujua, ni wakati gani  mtu aende huko kimya na muda gani achague kwenda pasipojulikana kama itaonekana inafaa.
Akichagua kwenda kimya huenda akavikwa nguo upya siku za usoni. Hata hivyo,  uamuzi wowote baina ya hiyari hizi mbili ni mgumu.  Ingawa ni bora katika mazingira fulani kupoteza pua ili kuulinda wajihi. Kwani! Kama hapana budi lisilobudi hufanywa! Uamuzi wa mithili hii ndiyo hasa huitwa uamuzi wa kukata jongoo kwa meno.  Wakati fulani kimya ni kelele lakini si kila kiza ni shari.
Si budi kuzipima vizuri nyakati ili ifanyike itihari sahihi ya mtindo wa maisha kwa kuzingatia mazingira ya wakati unaohusika. Hata kiza si shari tupu na si kila kilichopinda ni kibaya.
soma_useme
********
A. A. Majid Mswahili
Chang'ombe,  Kisarawe_ Pwani
Usipitwe na Hadithi Fupi kwa Ufupi za Majid Mswahili,  kuanzia Februari Mosi, 2022, In Shaa Allah.
Anuanipepe: majidkiswahili@gmail.com
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-17T16:40:12Z 2021-12-17T16:40:12Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1758 <![CDATA[KISA CHA MVUVI NA SAMAKI]]> Wakati anarudi na wafuasi wake ndipo akakutana na Mvuvi mmoja tu alie bahatika kupata samaki watatu 3 Mfalme akataka kuwanunua Mvuvi akakataa kuwauza samaki wake.

Mfalme akaomba auziwe japo mmoja Mvuvi akamwambia Mfalme huyu samaki mmoja naenda kumkopesha sijui kama nitalipwa,
Na huyu mwengine naenda kulipa deni sijui kama nitalimaliza na huyu wa tatu naenda kumtupa.

Mfalme akachukizwa kwa majibu yale akaamuru anyang'anywe wale samaki nae atupwe gerezani,Akiwa kwenye Kasri Mfalme akaamuru yule mvuvi aletwe mbele yake ili amuhoji.Kwanini umekataa kuniuzia mimi samaki wakati unaenda kumkopesha tena hujui kama utalipwa,,? Wapili unaenda kulipa deni na hujui kama utalimaliza,,? Kisha mwengine unaenda kumtupa wakati mimi nina shida na samaki,,?

Mvuvi akamjibu Mfalme
Huyu ninae kwenda kukopesha sijui kama nitalipwa naenda kuwapa wanangu
Kwani kuwaudumia watoto hujui kama na wao watakuhudumia.

Na huyu ni nae kwenda kulipa deni sijui kama nitalimaliza nawapelekea wazazi wangu,
Kwa waliyo nitendea siwezi kuwalipa hata niwape nini.

Na huyu ninae kwenda kumtupa naenda kumpa Mkewangu,Kwani hao hawajui kushukuru wala kutosheka, hata uwape nini siku akicharuka tu atasema hujamfanyia chochote tokea umuoe.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-10T02:32:15Z 2021-12-10T02:32:15Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1698 <![CDATA[NGANO YA "MSAFIRI NA NGAMIA"]]> Msafiri mmoja aliamua kupumzika kutokana na upepo mkali na vumbi la jangwani. Aliamua kukaa ndani ya hema yake hadi hali hiyo ya hewa ibadilike ndipo aendelee na safari yake. Ngamia wake pale nje alikumbwa na baridi kali hivyo akaamua kumuomba hifadhi ndani ya hema la bwana wake. “Bwana nakuomba uniruhusu nitie kichwa ndani ya hema nijiepushe na athari za upepo na mavumbi yaliyoko hapa nje”. Yule msafiri alikataa na kumweleza kuwa haingewezekana kwani hema lilikuwa dogo. Lakini ngamia alimrairai hadi bwana wake alipokubali. Ngamia alipoona kuwa kichwa chake kiko ndani aliomba aingize shingo yake, akidai kuwa shingo haitachukua nafasi kubwa, naye msafiri alikakubali. Baadaye akakubaliwa kuingiza hata nundu yake na hatimaye akaingiza wote mzima. Msafiri kutanabahi, alikuwa amerushwa nje, huku ngamia akidai kuwa wasingeweza kuenea pamoja kwani hema lilikuwa dogo. Basi msafiri akaumia nje huku baridi inamzizima ingawa hema lilikuwa lake. Hali ya hewa ilipobadilika, msafiri alimwambia ngamia kuwa wangeendelea na safari. Baada ya siku kadhaa hali ya hewa ilibadilika, mvua kubwa ikanyesha naye msafiri akatafuta hifadhi ndani ya hema lake. Licha ya kuwa ngamia alimbembeleza angalau aijiepushe na baridi, msafiri alikuwa ameapa kutorudia kosa lake la awali.
 
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-11-23T03:22:53Z 2021-11-23T03:22:53Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1547 <![CDATA[MFANO WA SOGA]]> KIFENGE NA BARUA KWENDA KWA BWANA MUNGU
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Kifenge alikuwa maskini sana. Yeye na familia yake waliishi kwa kuombaomba chakula, mavazi na mahitaji mengine.
Siku moja wazo la kuomba msaada kutoka kwa Bwana Mungu lilimjia. Kifenge alienda dukani akanunua karatasi,bahasha na stempu akaamua kumwandikia Bwana Mungu barua.
Barua ilipofika posta wafanyakazi wa posta wakashangaa kuona  barua inatakiwa kutumwa kwa Bwana Mungu. Wakaifungua wakaisoma,wakamhurumia sana Bwana Kifenge. Wakaamua kuchanga fedha hadi zikafika laki tano,wakazituma katika anwani iliyokuwa kwenye barua.
Baada ya wiki moja fedha zikafika kwa Kifenge. Alifurahi sana na akamwambia mke wake, “Mke wangu sasa dhiki imeisha. Tununue mahitaji yote, tukae, tustarehe.”
Mke wake alifurahi sana akamuuliza mume wake, “Hivi siku zote tulikuwa wapi mume wangu? Kumbe ndiyo maana watu wanatajirika lakini hawasemi kama Bwana Mungu huwa anawatumia fedha?”
Wakanunua magunia ya mchele, sukari, unga, mafuta na nguo na mahitaji mengine mpaka fedha zote zikaisha.
Fedha zilipoisha na mahitaji yakaisha wakaandika barua ingine kwa Bwana Mungu kuomba msaada. Wafanyakazi wa posta walipoiona wakajua mwandishi ni yuleyule. Wakamjibu, fedha ulizopata kama hukuweka mtaji, hakuna fedha tena.
Bwana Kifenge alipoipata akazunguka kila mahali akitangaza kuwa atawashitaki wafanyakazi wa posta kwa sababu wameiba fedha zake alizotumiwa na Bwana Mungu. Hata hivyo wenye akili wakasema kweli wajinga ndio waliwao. “Hivi Kifenge hakujua kuwa ule ulikuwa ni msaada uliotoka kwa watu wema ambao alitakiwa kuutumia vizuri?”
Kelele za Kifenge hazikuzaa matunda, akarudia umaskini wake kama zamani.
Kutokana na hadithi ya Kifenge tunaona kuwa Soga ni hadithi fupi za kuchekesha au kukejeli. Mara nyingi wahusika wake ni watu wa kubuni, na huwa na kisa kimoja tu.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-11-23T03:18:26Z 2021-11-23T03:18:26Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1546 <![CDATA[MFANO WA KISASILI]]> KISASILI
Kisasili ni hadithi fupi zinazoelezea asili ya jambo au maumbile fulani. Wahusika wake huwa ni wadudu, wanyama, binadamu, miungu na vitu visivyo na uhai, lakini huwa na hadhi ya kibinadamu. Mara nyingi kisasili huanza na “paukwa!”  mfano ni Kisa cha Nguruwe kukosa mkia. 
Paukwa! (Aliuliza bibi)
Pakawa! (Waliitikia wajukuu zake)
Hapo zamani za kale, palitokea ubishi kati ya nguruwe na ng’ombe. Kila mmoja akawa anatamba kuwa ana nguvu kuliko mwenzake. Bahati nzuri akatokea sungura akawauliza, “Kulikoni mbona mnabishana hivyo?” Nguruwe na ng’ombe wakamweleza chanzo cha ubishi wao.
Nguruwe akaanza kumkashifu mwenzake ng’ombe, “Huyu hanijui mimi! Ananisikia tu, nitamvunjavunja mbavu asahau hata njia ya kurudi kwao” Ng’ombe naye akadakia, “Wewe ni bwana mdogo tu, huo ufupi na unene wako hauwezi kunibabaisha.”
Sungura akasikiliza halafu akasema, “Hakuna sababu ya kubishana, mimi naona mshindane.” Wote wakakubali. Sungura akasema, “Nitawafunga mikia yenu pamoja. Nikihesabu moja, mbili, tatu muanze kuvutana. Yule ambaye mkia wake utakatika atakuwa ameshindwa.”
Basi wajukuu zangu, wote wakasema sawa. Nguruwe akamtahadharisha ng’ombe, “Mkia wako utakuwa halali yangu” Ng’ombe akaingiwa na woga, akatulia tuli kama maji mtungini, lakini akaamua kujikaza kisabuni.
Basi sungura baada ya kuwafunga mikia akahesabu moja, mbili, tatu wakaanza kuvutana. Wajukuu zangu mngekuwepo mngejionea kivumbi na jasho. Si mnajua wajukuu zangu, wapiganapo fahari wawili? Akauliza bibi. “Ziumiazo nyasi,” wakajibu wajukuu zake.
Punde si punde zilisikika kelele Guuuuu! Guuuuu! Guuuuu! na kishindo kikubwa puuu uu! Lahaula! Mkia wa nguruwe ulikatika, akaanguka chini puuuu na pua ikabonyea. Nguruwe akalia kwa uchungu, damu ikamtoka kwa wingi kama bomba la maji. Ng’ombe alikuwa mshindi.
Sungura kuona vile akakichukua kipande cha mkia; huyoooo! Akampelekea rafiki yake fisi. Nguruwe akajuta sana kwa nini alikubali ushindani.
Basi wajukuu zangu, hadi leo nguruwe na ukoo wake hawana mikia na pia pua zao zimebonyea. Wajukuu zake wakacheka na kusema, “Kumbe! Ndiyo maana nguruwe wana mikia mifupi”
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-11-21T11:54:55Z 2021-11-21T11:54:55Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1538 <![CDATA[KISA CHA PUNDA WA DOBI]]> [Image: pwd.jpg]
Hadithi za Esopo
Aliondokea kima akafanya urafiki na papa. Pana mti mkubwa, jina lake mkuyu, umeota katika kilindi, matawi yake nussu yako mjini, na nussu yako baharini. Yule kima kulla siku kwenda akila kuyu, na yule rafiki yake papa huwapo chini ya mti. Humwambia, utupie nami rafiki yangu vyakula; humtupia siku nyingi na miezi mingi.
Hatta siku hiyo papa akamwambia kima, fathili zako nyingi, nataka twende kwetu nikakulipe fathili. Kima akamjibu, ntakwendaje, nasi hatuingii majini, nyama wa barra. Akamwambia, ntakuchukua, tone la maji lisikupate. Akamwambia, twende.
Wakaenda zao hatta nussu ya njia. Papa akamwambia, rafiki yangu weye, ntakwambia kweli. Akamwambia, niambie. Akamwambia, huko kwetu tunakokwenda, Sultani wetu hawezi sana, na dawa tumeambiwa ni moyo wa kima. Kima akamjibu, hukufanya vema usiniambie kulekule. Papa akamwuliza, ginsi gani?
Akafikiri kima akaona, nimekwisha kufa; sasa ntanena uwongo, labuda utanifaa.
Papa akamwuliza, umenyamaza huneni? Akamwambia, sina la kunena, kwani usiniambie kulekule, nikapata kuchukua moyo wangu. Papa akamwuliza, hapa, kunao moyo wako?
Huna khabari yetu? Sisi tukitembea mioyo yetu huacha mitini tukatembea viwiliwili tu, wallakini hutanisadiki, utaniambia nimeogopa, sasa twende zetu hatta huko kwenu, ukanichinje kama utauona moyo wangu.
Papa akasadiki, akamwambia kima, turudi sasa, ukatwae moyo wako. Kima akamwambia, sikubali, ela twende kwenu. Akamwambia, turudi kwanza ukatwae moyo wako, tupate kuenenda.
Kima akawaza ni heri kumfuata hatta mtini, akili nnayo mwenyewe nikiisha fika. Wakaenda wakarudi hatta mtini, akapanda juu yule kima akamwambia, ningoje hapa, papa, naenda twaa moyo wangu, tupate kwenda zetu.
Akapanda mtini akakaa kitako kimya. Papa akamwita. Akanyamaza. Akamwita tena. Akamwambia, twende zetu. Kima akamjibu, twende wapi? Akamwambia, twende kwetu. Akamwambia, una wazimo? Papa akamwuliza, ginsi gani? Kima akamwambia, umenifanya punda wa dobi? Papa akamwuliza kima, ginsi gani punda wa dobi? Akamwambia, Ndiye hana moyo, wala hana mashikio. Papa akamwuliza, ginsi gani kisa cha punda wa dobi? Nambie, rafiki yangu, nipate kujua maana.
Akamwambia, Dobi alikuwa na punda wake, akimpenda sana mwenyewe. Akakimbia punda akaingia mwituni siku nyingi, hatta akamsahao mwenyewe dobi. Akanenepa sana kule mwituni.
Akapita sungura, akamwona yule punda, mate yakamtoka, akanena, nyama imenona hii. Akaenda akamwambia simba. Na simba atoka ugonjwani, amekonda sana. Sungura akamwambia, ntakuleta nyama kesho, tuje tule. Akamwambia, vema.
Sungura akaondoka, akaenda mwituni, akamwona punda, na yule punda mke. Akamwambia, nimetumwa kuja kukuposa. Na nani? akamwuliza. Akamwambia, na simba. Akakubali, akafurahi sana punda. Akamwambia, Twende zetu, bass.
Wakaenda zao, hatta wakafika kwa simba. Akawakaribisha simba. Wakakaa kitako. Sungura akamkonyeza simba, akamwambia, nyama yako hiyo imekwisha kuja, nami naondoka. Akamwambia punda, nnakwenda chooni mimi, zumgumzeni hapo na mumeo.
Simba akamrukia, wakapigana, akapigwa sana simba kwa mateke, naye akampiga makucha mengi. Akaangusha simba akakimbia punda, akaenda zake mwituni. Akaja sungura, akamwambia, Je! simba, umempata? Akamwambia, sikumpata, amenipiga kwa mateke amekwenda zake, na mimi nimemtia madonda mengi, sababu sina nguvu. Sungura akamwambia simba, tulia we.
Wakakaa siku nyingi, hatta punda akapona madonda yale, na simba akapata nguvu sana. Akaenda sungura kwa simba, akamwambia, waonaje sasa, nikuletee nyama yako? Akamwambia, kaniletea ntaikata vipande viwili.
Akaenda sungura mwituni. Punda akamkaribisha sungura, akamwuliza khabari. Akamwambia, na mchumba wako anakwita. Punda akamwambia, siku ile umenipeleka, amenipiga sana kwa makucha, naogopa sasa. Akamwambia, hapana neno yalio ndio mazumgumzo ya simba. Akamwambia, twende zetu, bass.
Wakaenda hatta wakafika. Simba alipomwona tu, akamrukia akamkata vipande viwili.
Hatta sungura alipokuja, akamwambia, chukua nyama hiyo ukaoke, wallakini sitaki kitu mimi, ela moyo na mashikio ya punda. Sungura akamwambia, marahaba. Akaenda akaoka nyama mahala mbali, simba hamwoni. Akatwaa moyo ule na mashikio akala yeye sungura, hatta akashiba. Na nyama ngine akaziweka.
Akaja simba, akamwambia, niletee moyo na mashikio. Akamwambia, yako wapi? Simba akamwuliza, kwa nini? Akamwambia, huyu punda wa dobi, huna khabari? Akamwambia, ginsi gani kutoa kuwa na moyo na mashikio? Akamwambia, wewe simba mtu mzima hayakuelei? Kama ana moyo huyu na mashikio, angalikuja tena hapa? Kwani marra ya kwanza amekuja akaona atakuuawa, akakimbia, marra ya pili amekuja tena, bassi kama ana moyo angalikuja? Simba akamwambia, kweli maneno yako.
Bassi kima akamwambia papa, nawe wataka unifanye mimi punda wa dobi, shika njia wende zako kwenu, mimi hunipati tena, na urafiki wetu umekwisha.
Kua heri.
—–
1. Umejifunza Nini Kwenye Simulizi Hii!
2. Nini maana ya neno Usiwe kama Punda wa Dobi?]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-11-21T10:41:10Z 2021-11-21T10:41:10Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1533 <![CDATA[KISASILI CHA JOGOO – KWANINI JOGOO HUWIKA?]]> Paukwa!
Pakawa!
Hapo zamani za zamani, siku moja palitokea mafuriko makubwa sana. Wanyama na ndege wote walipata taabu kubwa. Taratibu maji yalijaa nchini hata kufikia mahali ambapo jogoo alikuwa amesimama baada ya kuchoka mno. Jogoo alitweta na kuhangaika kabisa. Kwa bahati nzuri ndege wengine walioruka juu zaidi walimwona na kumwonea huruma. Hivyo wakakata shauri la kumsaidia.
Haraka sana ndege hao walikwenda juu ya mlima mrefu sana, wakaokota huko ufito na kuja nao mpaka alipokuwa jogoo. Wenyewe wakajigawa makundi mawili. Kundi moja likashika ncha moja ya ufito na jingine likashika upande wa pili. Kisha wakamwambia jogoo asimame katikati juu ya ufito, huku ameshikilia kwa nguvu. Kwa pamoja wakamwinua juu na kuruka naye hadi mlima mrefu mahali pasipoweza kufikiwa na mafuriko. Akawa ameokoka kabisa.
Jogoo alifurahishwa sana na kitendo hicho cha kumwokoa. Hata mafuriko yalipokwisha, jogoo aliwauliza ndege, “sasa rafiki zangu wapenzi, nilikuwa nimekufa, nanyi mmeniokoa. Je, nami niwafanyie nini mpate nanyi kufurahi?”
Ndege kwa pamoja wakamjibu, “Sisi hatutaki utulipe kitu. Ila sote tunapenda kuwahi kuamka. Lakini wakati mwingine tunachelewa. Kwa hiyo ukihiyari tunaomba uwe unatuamsha.” Jogoo akajibu, “Nimehiyari kabisa; nitajitahidi kuwaamsha mapema kila siku.”
Tangu hapo jogoo huwika kila siku: kokoikoo maana yake kumekucha, amkeni wapenzi; Ooo! yaani. Nilikufa, asanteni! Huwika asubuhi na mapema ili kuwaamsha wafadhili wake. Huwika na mchana ili kuzoeza sauti yake isikwame.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-11-20T18:28:43Z 2021-11-20T18:28:43Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1531 <![CDATA[KISASILI CHA JONGOO NA NYOKA]]> Tokiani!
Namchai!
Hapo kale mzee Jongoo na NYoka walikuwa marafiki wa kuaminiana sana. Siku moja Jongoo akamwambia Nyoka, “Rafiki yangu, leo kuna ngoma. Twende nasi tukaone jinsi wenzetu wanavyocheza.”
Nyoka akamjibu, “Ningependa sana kwenda huko. Lakini ujuavyo sina macho. Nitaonaje huo mchezo?” Jongoo akasema, “NItakuazimisha macho yangu, nawe utaniazimisha miguu yako kama dhamana.” Wakakubaliana. Basi wakabadilishana viungo: Jongoo alimpa Nyoka macho yake, naye Nyoka akampa Jongoo miguu yake mingi.
wakaenda ngomani. Baada ya ngoma kwisha, Jongoo alimtaka Nyoka macho yake. Lakini Nyoka akajibu, “La, rafiki yangu. Kumbe wenzangu mnafaidi sana kwa macho yenu. Leo nimeona ngoma na moyo wangu umeburudika sana. Kwa hiyo hupati macho haya tena. Jongoo akamjibu, “Lakini werevu siyo kupata!” Kwa hasira Jongoo akaondoka na miguu yake yote huku anapapasa njia kurudi kwake.
Ndicho kisa cha Nyoka kukosa miguu na Jongoo kuwa na miguu mingi bila macho. Ndicho kisa pia cha Jongoo na Nyoka kamwe hawaamkiani hata kama wangekutana njiani.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-11-20T18:20:09Z 2021-11-20T18:20:09Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1530 <![CDATA[KISA CHA MJANE NA MBWA WAKE]]> Hadithi hadithi!
Hadithi njoo!
Hapo zamani za zamani palikuwa na baba mjane na mbwa wake. Nao walipendana sana. Kwa siku nyingi walikaa katika kibanda chao kidogo mbali mwituni.
Ikaondokea siku moja katika zungukazunguka yake ya kutafuta chakula, baba mjane huyo aliokota kioo kizuri akakiweka kibandani mwake.
Mchana mmoja, wakati amepumzika kibandani mwao, mbwa akakiona kile kioo kimetundikwa ukutani. Kuchungulia zaidi akaona mbwa mwingine wa kimo chake na rangi yake amesimama mbele yake. Pale pale mbwa akaanza kubweka ili kumwogofya yule mbwa mgeni. Kumbe jinsi alivyobweka ndivyo na yule mbwa wa pili alivyoonekana kubweka pia. Asitake mshindani, mbwa alimrukia kwa makucha yule mbwa mgeni. Kumbe badala ya kumpiga mbwa mgeni makucha yalifikia ukutani. Makucha yakaumia. Hapo mbwa kwa hasira yote alitoa meno na kumrukia ili amwume. Lakini safari hii alikipiga kioo na kukivunja kabisa.
Baba mjane alipotahamaki alimwambia mbwa wake, “Unajisumbua, rafiki yangu. Mbona unagombana na kivuli chako, wala siyo mbwa!” Mbwa akaona haya sana.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-11-19T03:18:12Z 2021-11-19T03:18:12Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1504 <![CDATA[KISA CHA ABUNUWASI NA SUTI YA MFALME]]> Hapo zamani za kale Abunuwasi alimuendea mfalme akamwambia anaweza kumshonea suti ya thamani sana ambayo wenye dhambi watakuwa hawaioni na wasio na dhambi tu ndio watakuwa wanaiona. Mfalme akampa kazi Abunuwasi ya kutengeneza suti ya aina hiyo kwa ajili yake. Kwa siku kadhaa Abunuwasi alijifungia katika chumba akawa bize anashona suti ya mfalme. Baada ya siku tatu, mfalme akamtuma msaidizi wake akaangalie kazi inavyoendelea, yule msaidizi akaingia chumba alichokuwa akishonea Abunuwasi lakini hakuona kitu japo alimuona Abunuwasi akifanya vitendo kama vile yuko bize anashona nguo. Msaidizi akamwambia Abunuwasi, ‘Nimetumwa na mfalme niulizie umefikia wapi?” Abunuwasi akamjibu, “Kwani we huoni jinsi suti ilivyoanza kupendeza, ila bado namalizia nguo nyingine nataka kuanzia nguo za ndani ziwe ni hizi za kitambaa ambacho hakionekani kwa wenye dhambi”. Hakika yule msaidizi alikuwa haoni kitu lakini ili aonekane hana dhambi akaanza kusifu jinsi nguo zilivyoshonwa kwa ufundi. Akatoka na kurudi kumueleza mfalme kuwa Abunuwasi kamshonea nguo nzuri sana si za dunia hii kwa jinsi zilivyo nzuri. Mfalme alifurahi sana, kesho yake akamtuma msaidizi mwingine, nae kama yule wa jana akarudi kwa mfalme na ripoti nzuri sana ya maendeleo ya koti, pia akaleta taarifa nzuri kuwa kesho yake Abunuwasi angemaliza kazi na angeleta nguo ili mfalme azivae. Kesho yake mapema Abunuwasi akaingia katika kasri la mfalme akiwa kama kashika lundo la nguo, ambazo mwenyewe alisema wasio na dhambi tu ndio wataziona. Wasaidizi wa mfalme wote hawakuwa wanaona kitu lakini walianza kupiga makofi wakisifu jinsi nguo zilivyokuwa nzuri, hamna aliyekuwa anataka kuonekana ana dhambi. Hatimae Abunuwasi akamkabidhi mfalme nguo, mfalme nae hakuwa anaona kitu lakini ili asiambiwe ana dhambi akajidai eti nae anaziona akaanza kumsifu Abunuwasi kwa umahiri wake wa kuchagua rangi na hata ufundi wake mkubwa wa kushona. Abunuwasi akamuomba mfalme azivae zile nguo, wakaingia faragha mfalme akavua nguo zake na akaanza kuvaa nguo asizoziona kwa msaada wa Abunuwasi. Kwa vile alivua nguo zote na kuvalishwa mpya zisizoonekana, rohoni mwake alikuwa anajiona yuko uchi lakini akaona akitangaza haoni kitu wananchi wangemshangaa kuwa mfalme ana dhambi, hivyo akaendelea kusifia na kujiangalia kwenye kioo akisifu nguo zilivyompendeza. Kisha akalazimika kutoka nje ili wananchi waone nguo mpya za mfalme. Wote walikuwa wanamwona mfalme yuko uchi lakini wakawa wanaogopa kuonekana wana dhambi hivyo kila mtu akawa anashangilia na kusifu uzuri wa nguo za mfalme. Lakini ghafla mtoto moja mdogo kwa sauti kubwa akamuuliza baba yake, “Baba mbona mfalme yuko uchi?”. Minong’ono ikaanza mwishowe watu wakaanza kumuunga mkono mtoto, mfalme nae sasa aibu ikamshika kwani alijua sasa watu wote wanamuona yuko uchi, akatimka na kujificha kwenye kasri lake na hadithi yangu imeisha hapo.]]> false MwlMaeda]]> 2021-09-14T13:04:25Z 2021-09-14T13:04:25Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1242 <![CDATA[MFANO WA MBAZI]]> Siku moja Panya akiwa darini alichungulia chini na kumuona mkulima na mkewe wakiaanda mtego utakaotumika kumnasa, Kwa majonzi alisikitika na kujiona anasiku chache za kuishi duniani.
Siku hiyo panya alizunguka huku na kule kuomba msaada wa mawazo kwa wanyama wenzake ili aweze kunusurika na mtego alioandaliwa, lakini wanyama wenzake hawakuweza kumsaidia huku wakisema matatizo yako hayatuhusu.
Awali panya alitoka ndani na kwenda kuonana na mbuzi, akamwambia mbuzi, mkulima na mkewe wananiwinda, wameandaa mtego wa kuniangamiza, tafadhali naomba nisaidie, naomba nisaidie mwenzako niepukane na kifo nilichoandaliwa, Mbuzi akamjibu ” Samahani Mimi sihusiki na mambo ya huko ndani na hayo matatizo yako hayanihusu, tafadhali acha kunisumbua, mimi siwezi kukusaidia nakuomba uondoke hapa haraka sana, mkulima akikuona hapa utanisababishia matatizo. Panya akaondoka kwa huzuni wakati huo akapata wazo la kuonana na ng’ombe akiamini ng’ombe si mbuzi japo wote ni wanyama kama yeye.
Basi Panya alienda kuonana na Ng’ombe, alianza kwa kusema ” Samahani ng’ombe, najua wewe ni mnyama kama wanyama wengine, tunachotofautiana Mimi na wewe ni ukubwa wa umbo ila ukiangalia mambo mengine hakika tunaendana, wewe una mkia na Mimi pia nina mkia, unakula mahindi na mimi pia ninakula mahindi. Tafadhali bwana naomba nisaidie mwenzako ninawindwa na mwenye nyumba kwani jana usiku nimemuona akitoa mtego unaoweza ukaniangamiza ndani ya dakika chache, najua wewe unaweza kuukanyaga ule mtego na kuuvunja vunja kabisa, nitakachofanya mimi ni kukujulisha mara tu atakapotoka, ukiuvunja nitakuwa huru kula nitakavyo, ng’ombe naye alitoa majibu kama ya mbuzi basi panya akawa amekosa kwa kukimbilia, zaidi zaidi alijiwazia mwenyewe kuwa itabidi awe makini kwa kila hatua atakayo iendea.
Usiku ule panya akiwa amelala alisikia mtego umefyatuka, mke wa mkulima na mumewe wakafurahi wakiamini kuwa ni panya amenaswa, haraka sana waliufuata mtego ulipo na kukuta mtego umenasa nyoka badala ya panya. mke wa mkulima alipojaribu kumtoa ghafla aling’atwa na hali yake ikaanza kuwa mbaya, ikabidi yule mkulima amkimbize mkewe hospitalini, hali ya mke wa mkulima aliendelea kuwa mbaya kutokana na sumu ya nyoka, watu wakawa wanakuja kutoa pole kwa mke wa mkulima, chakula kikapungua, mkulima aliamua kumchinja mbuzi, Panya aliyaona haya alisikitika huku akiwa anayakumbuka majibu ya mbuzi na kujiuliza mwenyewe kuwa mbuzi angesaidia kuuharibu ule mtego wala asingechinjwa, baadaye mke wa mkulima alifariki, watu wengi walikuja kwenye msiba, yule mkulima aliamua kumchinja ng’ombe wake ili watu wapate kitoweo siku ya msiba.
Ndivyo ilivyo katika maisha tunayoishi. Watu wengi wanakuwa na uwezo wa kutatua shida za watu wasio na uwezo, lakini kwa sababu haziwahusu hata wakiombwa msaada wanaishia kutoa maneno ya dharau na matusi huku wakisema shida zako hazinihusu wasijue msaada wanaoweza kuutoa unaweza ukawasaidia au kuwaepusha na jambo baya lililopo mbele yao.
Mbuzi na ng’ombe wangeamua kumsaidia panya kuuharibu ule mtego hata wasingeangamia, lakini kwa jeuri zao na kuona matatizo ya panya siyo yao wala hayawahusu mwishowe walijikuta wao ndio wanaangamia.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-10T09:37:28Z 2021-09-10T09:37:28Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1220 <![CDATA[Visasili (Visa-asili)]]> Visasili ni ngano za kihistoria zinazoeleza chimbuko /asili ya jamii/kabila fulani; tamaduni mbali mbali katika jamii ile na namna jamii hiyo ilivyofika katika eneo lake la sasa. Visasili husaidia kuelezea asili ya mambo yasiyoelezekakama vile mauti, jando, tohara, ndoa na tamaduni/imani nyinginezo.
Tanbihi: Tofauti kati ya visasili na usuli(visaviini) ni kwamba visasili huhusisha jamii fulani, mila, imani na matukio ya kiada kama vile kifo, tohara n.k ilhali ngano za usuli huelezea kwa nini mambo fulani hufanyika bila kuhusisha jamii au imani.

Sifa za Visasili
  1. Huelezea chimbuko la jamii fulani
  2. Matokeo yake hufanyika mwanzoni (k.v mwanzo wa dunia)
  3. Aghalabu huhusisha miungu, malaika n.k
  4. Kuburudisha
Umuhimu wa Visasili
  1. Kutafuta jibu kwa maswali yanayotatiza
  2. Kuhifadhi historia na imani ya jamii
  3. Kuunganisha jamii
  4. Kuwasilisha mila na desturi za jamii

Mifano
  1. Asili ya jamii ya Wamaasai
  2. Asili ya Wagikuyu
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-10T09:30:52Z 2021-09-10T09:30:52Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1219 <![CDATA[NADHARIA ZA CHIMBUKO LA NGANO/MASIMULIZI]]>
.pdf   NADHARIA_ZA_CHIMBUKO_LA_NGANO_MASIMULIZI.pdf (Size: 396.69 KB / Downloads: 0) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-09T10:57:24Z 2021-09-09T11:55:02Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1210 <![CDATA[KISA CHA MFALME NA MVUVI WA SAMAKI]]> Wakati anarudi na wafuasi wake ndipo akakutana na Mvuvi mmoja tu alie bahatika kupata samaki watatu 3 Mfalme akataka kuwanunua Mvuvi akakataa kuwauza samaki wake
Mfalme akaomba auziwe japo mmoja Mvuvi akamwambia Mfalme huyu samaki mmoja naenda kumkopesha sijui kama nitalipwa, 
Na huyu mwengine naenda kulipa deni sijui kama nitalimaliza na huyu wa tatu naenda kumtupa
Mfalme akachukizwa kwa majibu yale akaamuru anyang'anywe wale samaki nae atupwe gerezani,
Akiwa Ikulu Mfalme akaamuru yule mvuvi aletwe mbele yake ili amuhoji 
Kwanini umekataa kuniuzia mimi samaki wakati unaenda kumkopesha tena hujui kama utalipwa,,? Wapili unaenda kulipa deni na hujui kama utalimaliza,,? Kisha mwengine unaenda kumtupa wakati mimi nina shida na samaki,,? 
Mvuvi akamjibu Mfalme
Huyu ninae kwenda kukopesha sijui kama nitalipwa naenda kuwapa wanangu
Kwani kuwaudumia watoto hujui kama na wao watakuhudumia
Na huyu nae kwenda kulipa deni sijui kama nitalimaliza nawapelekea wazazi wangu,
Kwa waliyo nitendea siwezi kuwalipa hata niwape nini,
Na huyu ninae enda kumtupa naenda kumpa Mkewangu
Kwani hao hawajui kushukuru wala kutosheka, hata uwape nini siku akicharuka tu I atasema hujamfanyia chochote tokea umuoe.

Siku njema]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-08-22T08:12:23Z 2021-08-22T08:12:23Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=983 <![CDATA[MFANO WA TARIHI]]> Kijana Kadenge ambwaga Jemedari Nyangumi
 
“Tuseme hii ndiyo hatima ya utawala wangu?” Alijiuliza Mfalme Ntire akiwa mwenye majonzi makubwa. Akatangaza katika milki yake kuwa yeyote atakayefanikiwa kumuua Jemadari Nyangumi atampa robo ya milki yake.
 
Wakatoka wanaume wa miraba minne, wakajaribu kupambana na Jemadari Nyangumi lakini wakateketea wote. Jemadari Nyangumi alikuwa anakaribia kabisa kuteka ardhi yote ya Mfalme Ntare.
 
Akatoka Kadenge kama walivyozoea kumwita. Miguu yake imeangalia kushoto na kulia. Macho yake ni madogo mithili ya macho ya mamba.
 
Akafika kwa Mfalme akamwambia, “Mtukufu Mfalme, naomba ruhusa yako nikamng’oe huyo nduli.” Mfalme akamjibu akasema, “Mfupa uliomshinda fisi wewe utauweza/” Kadenge akasema, “Nitauweza Mfalme Mtukufu.”
 
Mfalme akamwambia, “Nakuruhusu uende lakini siwezi kuruhusu jeshi langu kuongozana na wewe maana ni aibu tupu,” Mfalme akasema huku akibinua mdomo. Kadenge akatoka akachukua jiwe lililokuwa katika kombeo lake akamwendea Jemadari Nyangumi. Jemadari alipomwona akacheka, akasema, “Wewe ndiyo nani? Jeshi huna, silaha nazo huna, njoo uone. Nitakuvunjavunja mbavu zako a nyama yako itakuwa chakula cha tai.” akasonya huku akisogea mbele kwa mikogo.
 
Kadenge akamwangalia, akarusha jiwe lililokuwa katika kombeo lake, likamgonga Jemadari Nyangumi kwenye paji la uso; akaanguka chini puu! Damu zikaanza kumtoka mithili ya maji ya bomba. Mwisho akaaga dunia.
 
Askari wa chini yake walipoona Jemadari amekufa, wakakimbia. Watu wote katika ufalme wa Ntare wakashangilia, wakambeba Kadenge mpaka kwa Mfalme.
 
Mfalme akafurahi, akamgawia Kadenge nusu ya ufalme wake, wala siyo robo. Watu wote wakafurahi sana. Mzee mmoja akasikika akisema, “mdharau mwiba mguu huota tende.”
]]>
false