Kuna mfanano mkubwa kati ya maudhui katika fasihi andishi na fasihi simulizi.
Maudhui katika fasihi simulizi na fasihi andishi yanafanana. Masuala mengi yanayoshughulikiwa na fasihi andishi yamekwisha jadiliwa na fasihi simulizi. Kile ambacho fasihi andishi hufanya ni kuongezea masuala mapya kutokana na jamii ya kisasa.
Kwa mfano, asasi ya ndoa na nafasi ya mwanamke katika jamii ni maudhui katika fasihi simulizi . Maudhui haya pia yameangaziwa katika kazi mbalimbali za fasihi andishi.
Kwa mfano, riwaya ya utengano yake Said Mohammed imeangazia suala la nafasi ya mwanamke katika jamii ambapo mwanamke amesawiriwa kama chombo cha starehe, asiye na sauti mbele ya mwamamme na amekandamizwa.
Aidha, dhana ya majaaliwa hujitokeza sana katika kazi za kinathari za fasihi simulizi. Katika baadhi ya ngano, kuna watu ambao, kupitia kwa majaaliwa wanatajirika kimiujiza baada ya kuwa maskini.
Majaaliwa ni uwezo wa mungu. Wazo la majaaliwa katika tamthilia kama vile mfalme Edipode, ambapo Edipode anajaribu sana kukimbia utabiri kwamba angemuua babake na kimuoa mamake mzazi.
Mwishoni mwa tamthilia, utabiri huu unatokea na hivyo majaaliwa yanatimia
Jukumu kubwa la kijamii la fasihi simulizi ni kuadilisha. Ngano, semi , nyimbo na mawaidha ni baadhi ya tungo za fasihi simulizi zilizotumiwa kuadilisha.
Kwa mfano, ngano inayohusu kisa cha fisi kumkosa ndama kwa kuila kamba iliyokuwa imemfunga ndama, ni mfano wa ngano inayotahadharisha kujiepusha na tamaa na ujinga.
Dhamira hii ya kuadilisha inajitokeza katika tungo za fasihi andishi kama vile katika riwaya ya Adili na nduguze ya Shabaan Robert ambapo ndugu zake Adili wanageuzwa kuwa nyani kama adhabu kwa kumdhulumu Adili.
Nyenzo na malighafi
Fasihi simulizi na fasihi andishi hutumia lugha kuwasilisha mawazo ya binadamu.Fasihi simulizi ndiyo ya kwanza kutumia lugha kiufundi kama malighafi yake.
Lugha ilitumiwa kwa njia ya methali, na fani nyingine kama vile nyimbo na maghani.Vivyo hivyo, fasihi andishi kama vile tamthilia na riwaya iliibuka kimaandishi kutumia lugha kwa ufundi kama malighafi.
Tanzu za kimaandishi kama vile tamthilia ,riwaya, hadithi fupi na hata mashairi hutumia tamathali za usemi kama vile methali, nahau, tashbihi na jazanda.
Usimulizi
Msingi wa fasihi simulizi ni usimulizi.
Tanzu nyingi za fasihi simulizi huwasilishwa kwa masimulizi kama vile tendi, majigambo na rara. Riwaya kama vile lila na Fila na kipendacho roho zimeandikwa kwa mtindo wa ngano za kimapokeo; hali inayoonyesha athari za tanzu za fasihi simulizi.
Katika tungo za fasihi simulizi, fanani husimulia hadithi katika nafsi ya tatu.Kazi ya fasihi andishi pia hutumia nafsi ya tatu.
Utendaji
Fasihi simulizi ni tendi. Vivyo hivyo, upo uwezekano wa kutenda fasihi andishi.Kwa mfano, tamthilia huigizwa jukwaani, ngonjera huambatanishwa na vitendo.Tamthilia kama vile kifo kisimani na Mstahiki Meya zimeigizwa jukwaani kama ilivyo katika fasihi andishi.
Fani
Fani ni mbinu ambazo msanii hutumia kuwasilisha maudhui. Baadhi ya vipengele vya fani katika fasihi simulizi hupatikana katika fasihi andishi kama vile;
Ploti
Tanzu za kinathari za fasihi simulizi( ngano, visasili na mighani) huwa na ploti sahili. Sifa hii pia inajitokeza katika baadhi ya riwaya za Kiswahili kama vile siku njema yake Ken Walibora ambazo ni nyepesi kueleweka.
Wahusika na Uhusika
Fasihi simulizi imeathiri fasihi andishi katika upande wa wahusika.Fasihi simulizi hutumia wahusika wanyama, mizuka na binadamu. Fasihi andishi nayo hutumia wahusika wa aina mbalimbali kuwasilisha ujumbe.
Nyimbo
Mtambaji bora wa ngano za fasihi simulizi hutumia nyimbo katika usimulizi. Vivyo hivyo, baadhi ya kazi za fasihi simulizi kama vile tamthilia hutumia nyimbo.
Fantasia
Fantasia ni sifa ambayo hupatikana katika ngano na visasili. Sifa hii pia hupatikana katika baadhi ya tungo za fasihi andishi.
Baadhi ya riwaya za Kiswahili zina matukio ambayo yamekiuka uhalisia .
Kuwepo kwa wahusika wasio wa kawaida kama vile mazimwi katika fasihi simulizi na fasihi andishi ni mfano wa fantasia.
Kwa mfano katika riwaya ya Rosa Mistika yake E. Kezilahabi imesawiri wahusika Rosa na zakaria wakiwa mbinguni mbele ya hukumu ya mungu. Haya ni mandari yasiyo ya kawaida na hii ni fantasia.
]]>FASIHI Andishi imeathiriwa pakubwa na Fasihi Simulizi kimaudhui na kifani kadri inavyobainika katika vipengele vifuatavyo:
Dhamira

Linganisha na linganua riwaya pendwa na riwaya pevu kwa kurejeleaRiwaya ya Nyota ya Rehema na Kufa na Kupona .
Masebo (2008) anasema riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni yenye mawanda mapana ,lugha ya kinathari ,mchanganyiko wa visa na dhamira ,wahusika kadhaa na matukio yaliyosukwa Kimantiki yenye kufungamana na wakati na kushabihiana na maisha halisi.
Msokile (1992) ,anasema kuwa riwaya ni kazi ya sanaa ya kubuni yanye maandishi ya kinathari yanayosimulia hadithi ambayo ina uzito ,upana, na urefu wa kutosha ina wahusika mbalimbali wenye tabia za aina nyingi vilevile huwa na migogoro mingi ,mikubwa na midogo ndani yake.
Madumulla (2009) ,riwaya pendwa ni riwaya ambayo inajihusisha na masuala ya mapenzi ,upelelezi, na ujasusi ambapo mara nyingine katika ufuatiliaji wake kuna mapigano makali ya kimwili au kiakili kati ya mtu mmoja au wachache na watu wengi.
Masebo (2008) ; riwaya pevu ni riwaya yenye kuchimbua matatizo au masuala mazito ya kijamii ,kutafuta sababu zake ,athali zake na ikiwezekana ufumbuzi wake. Ni riwaya inayokusudiwa kumkera na kumfikirisha msomaji,sio kumstarehesha tu.
Riwaya pendwa ni kufa na kupona iliyoandikwa na E. Musiba na Riwaya pevu ni Nyota ya Rehema iliyoandikwa na iliyoandikwa na M.S Mohammed.
Riwaya pendwa na riwaya pevu hufanana na hutofautiana.Kwa kutumia kitabu cha riwaya ya “ Nyota ya Rehema” iliyoandikwa na M.S Mohammed na riwaya ya “Kufa na Kupona” iliyoandikwa na E .Musiba .
Ufuatao ni ufanano uliopo kati ya riwaya pendwa na riwaya pevu kwa kutumia riwaya ya “Nyota ya Rehema” na riwaya ya “Kufa na Kupona.”
Riwaya hizi zimetumia mandhari halisi ,mandhari kama eneo ambalo tukio la kifasihi kutendeka .riwaya pevu na riwaya pendwa waandishi wake mara nyingi hutumia mandhari ambazo ni halisi na zidhihilikazo katika mazingira halisi. Kwa mfano katika riwaya ya “Nyota ya Rehema “mwandishi ametumia mandhari kama vile Mwembeshomari (uk 31)
“Unakwenda mwembeshomari? Rehema aliulizwa.
‘Mwembeshomari’ aliitika upesi upesi.”
Vilevile katika riwaya ya “kufa na Kupona” mwandishi mandhari kama vile
“nikaingia kwenye gari langu huyoo upanga” uk 12
Riwaya hizi zinaelimisha jamii ;riwaya pevu na pendwa zote zinaelimisha jamii katika mambo mbalimbali kwa mfano riwaya ya “Nyota ya rehema “ mwandishi amewatumia Rehema na Sulubu kuelimisha jamii suala la kutokata tamaa, baada ya wahusika hawa kufukuzwa katika shamba la Ramwe wakapata kijieneo kidogo huko pakani ambapo hapakuwa na rutuba lakini hawakukata tamaa na jitihada za kilifanya shamba kuwa na rutuba kwa kulitilia moto na kuanza kulima kwa juhudi (uk -155 -159 ).
Pia katika riwaya ya Kufa na Kupona mwandishi amewatumia wahusika Sammy na Joe Masanja konesha suala la kutokata tama ambapo wapelelezi wenzao wanauwawa mmoja mmoja kwa vifo vya kutisha na kikatili lakini wao wanaendelea na upelelezi wa nyaraka za siri pasi kuto kukata tamaa mfano Wiilly Gamba anasema
“lazima mumkamate na kumuua mimi mwenyewe kama nitakuwa mzima wakati wote wa madhira kama yao………… (uk 24)
Zote zinaonyesha uhalisia wa matukio katika jamii, riwaya pendwa na riwaya pevu zote huonyesha uhalisia wa matukio yaliyo katika jamii . mfano katika riwaya ya “ kufa na kupona” mwandishi anaonyesha matukio ya rushwa,usaliti ,mauaji ya kiharifu na upelelezi ambapo mwandishi anamtimia mhusika piter mpigania uhuru aliyewasaliti wenzake kwa kuiba “nyaraka za siri “ Uk 91.
Pia DR Dikson Njoroge aliyeahidiwa kupewa rushwa na wareno ili kufanikisha wizi wa karatasi za siri (uk 99 ). Pia Benny anayefanya mauwaji ya kiharifu ili kulinda “nyaraka za siri walizoziiba (uk 53). Hivyo hivyo katika riwaya ya “Nyota ya Rehema” mwandishi anaonyesha matukio kama vile Dhuruma ambapo mwandishi anaonyesha rehema anadhurumiwa shamba la Ramwe aliyopewa na Baba yake (Fuad ) enzi za uhai wake na akina salma na karim (uk -150).
.Zifuatazo ni tofauti kati ya riwaya pevu ya “Nyota ya Rehema “ na ile ya “Kufa na Kupona” unadhihirika katika mambo yafuatayo ;-
Mtindo ,huu ni upekee wa mwandishi ambao hutofautisha kazi ya mwandishi mmoja na mwingine katika riwaya ya “Nyota ya Rehema”mwandishi ametumia mtindo wa wimbo. Kwa mfano pale Rehema alipoanza kukalili nyimbo za kubembelezea wototo.
“ukimpenda mwanao
Na wa mwenzio mpende,
Wako ukimpa chenga
Wamwezio chenjegere
Humjui akufaaye
Akupaye maji mbele……………”
“Nyamaa mama nyamaa
Nyamaa usilie ,
Ukilia waniliza
Wanikumbusha ukiwa
Ukiwa wa baba na mama” (uk 49 na 50)
Vilevile mwandishi ametumia mtindo wa nafsi ya tatu umoja na pia nafsi ya kwanza umoja, mfano “Mansuri alimtazama Rehema aliyekuwa akingojea jawabu kwa hamu “ (nafsi ya tatu umoja ) (UK 43). Na matumizi madogo ya nafsi ya nafsi ya kwanza mfano “ningependa kwenda huko rakwe nikakuona kulivyo “ alisema Rehema (uk 86). Na katika riwaya ya “Kufa na kupona” mwandishi ametumia matumizi ya simu.mfano ni pale polisi walipompigia willy kumjulisha Benny aliwasiliana na nani. Kama vile :
Hello ,Joe huyu “ “polisi stesheni hapa”
Basi hii simu ilikuwa inapigwa huko laving green ,kwenye nyumba ya Dr. Dickson Njoroge “ . uk 80.
Vilevile kuna matumizi ya nafsi ya kwanza umoja “nilipiga simu kwa chifu saa hiyohiyo nikimweleza kuwa awashauri maofisa polisi wasishugulike sana na mauaji mengi yatakayotokea “.
Katika riwaya pendwa mhusika mkuu ni mkwezwa ilhali katika riwaya pevu mhusika mkuu ni wakimapinduzi. Mfano katika riwaya yaKufa na kupona mhusika Willy Gamba amekwezwa na mwandishi kwa kumpalia sifa kama ,mwenye nguvu ,jasiri na mwenye uwezo mkubwa wa kupambana ,mfano mwandishi anamwinyesha mhusika Gamba akipambana na kundi la watu kumi na tatu na bado akawashinda anasema …
“..walipotaka kuanza kunifyatulia risasi haraka nikawafyatulia mfululizo.sita tayari chini nilipiga risasi mkono wa pita risasi ikaanguka chini bila ya kuwa nayo bastolla,ksha nikawamalizia wale wane waliobaki”………(uk 93). Pia katika riwaya ya “Nyota ya Rehema”mwandishi anamwonyesha mhusika mkuu Rehema kama mwanamapinduzi pale ambapo moja alipotoroka nyumbani kukataa mateso ya mama yake wa kambo (uk 22) pia kujiepusha kuingiliwa kimwili na mansuri kwa kumuuma meno na kupata nafasi ya kujiokoa (uk 65) tatu ,kupitia jitihada ya kufanya kazi kama ufugaji na kilimo ili kupambana na maisha yake na mmewe aliyemchagua kuishi naye (uk 104)
Riwaya imetumia lugha rahisi na inayoeleweka ilihali riwaya pevu imetumia lygha ngumu. Kwa mfano katika riwaya ya nyota ya rehema mwandishi ametumia misamiati ambayo si rahisi kuelewa maana yake mfano bigija,dhiyaa,ghila (uk 170) pia mwandishi ametumia mafumbo kama ubwebwe wa shingo haujamtoka………(uk 45) lakini, katika riwaya Kufa na kupona mwandishi ametumia lugha rahisi na inayoeleweka na iliyo na methali mfano mtaka cha sharti ainamen (uk 44).
Matumizi ya taharuki taharuki kama hamu ya msomaji kujua matokeo ya kitu Fulani katika riwaya pevu matumizi ya taharuki hutumika kwa kiasi kidogo mfano katika riwaya ya Nyota ya Rehema,taharuki imejitokeza ktika (uk 12) mwandishi anasema
“jina lako nani ? Faud alijisikia akiuliza kwa sauti iliyokuwa si yake
Adili ; alisikia jawabu akija
Aligeuka kumtazama na macho yao yakakutana ,roho zao zikaumana …………milele. Baada ya hapo hakuna chochote kilichoendelea baada ya hapo mwandishi ametuacha kwenye taharuki. Ilhali katika riwaya pendwa taharuki hujitikeza kiasi kikubwa mfano katika riwaya ya kufa na kupona wandiishi anathibitsha katika ukurasa wa 7 kama ifuatavyo “Amani lete madebe ya petrol na kiberiti”. Hii ni baada ya Sammy na willy kukamatwa na benny hivyo basi msomaji anapata hamu ya kujua nini kitatokea baadaa ya kuletwa petrol na kiberiti.
Pia katika ukurasa 45 taharuki imejitokeza pale willy aliposema “alinivuta akaanza kufungua tai yangu,kasha shati langu , halafu suruali yangu……….. tukajilaza . pia hapa msomaji atataka kuelewa kitu gani kiliendelea baada ya hapo.
Pia katika ( uk 67 ) ni pale ambapo willy anamkuta lina amechomwa kisu na mtu aliyemfahamu na anataka kumuuliza bila mafanikio. Hivyo msomaji Napata maswali je? Lina atakufa au atapona baada ya kujeruhiwa vibaya na mtu asiyefahamika
Vilevile taharuki nyingine imejitokeza pale ambapo willy Gamba alivyokamatwa na benny na akaambiwa asali sala yake ya mwisho kabla sijammiminia risasi kama mwenzake (uk 89 ).hivyo msomaji anapata taharuki kuwa je? Anaweza kufa au kunusulika? Lakini hata Gamba mwenyewe anakuwa yuko kwenye taharuki je? Anaweza kunusulika.
Wahusika katika riwaya pevu huakisi hali halisi ya maisha ilhali wahusika katika riwaya pendwa hupewa uwezo mkubwa usio wa kawaida wa kutenda matukio yanayosawiriwa Wahusika katika riwaya pevu huakisi hali halisi katika jamii riwaya hizi waandishi wametumia wahusika wao ambao ni tofauti dhidi ya uwakilishaji wao wa uhalisia wa mambo. Riwaya ya “Nyota ya Rehema” kama Rehema alipokuwa akipambana kupata mali yake ya urithi wa mali ya baba yake Faud, ambaye alifariki.hali hii ya urithi wa mali kwa mtu aliyefariki ni hali halisi kwa sababu yanatokea. katika jamii . mwandishi anathibitisha katika (uk 143) “ konde zilizomo na shamba lenyewe ni mali ya yangu bwana muridi na mimi ndiye motto wa maarehemu bwana Faud………………….. . Na katika riwaya ya “KUFA NA KUPONA “ mwandishi ameonyesha hali isiyo halisi kwa kumtumia mhusika Gamba aliyepewa uwezo mkubwa pale anapopambana na watu kumi na watatu na kuwashinda . hali hii si ya kawaida katika jamii.Katika (uk 93) walipotaka kuanza kunifyatulia risasi haraka nikawafyatulia mfululizo.sita tayari chini nilipiga risasi mkono wa pita risasi ikaanguka chini bila ya kuwa nayo bastola ,kisha nikawamalizia wale wakiobaki”
Katika riwaya pendwa mwanamke
amechorwa kama chombo cha anasa na katika riwaya pevu mwanamke amechorwa kama
mlezi na mzazi. Mwandishi wa riwaya ya Kufa
na Kupona anaonesha ambavyo Lina na Lulu wanavyojihusisha na masuala ya
anasa kama vile kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mhusika Benny aliyekuwa
mhalifu katika wizi wa nyaraka za siri (uk. 3) lakini mwandishi wa riwaya ya
Nyota ya Rehema, anamwonesha Bi. Kiza katika nafasi ya mlezi kwa kumlea Rehema
baada ya kifo cha mama yake (Aziza) pia Rehema anachorwa kama mzazi na mlezi wa
mwanae aliyeitwa Faud baada ya kuoana na Sulubu mume aliyemchagua mwenyewe (uk.
44)
Suluhu ya matatizo katka Riwaya pevu hutolewa hali ambayo ni tofauti na riwaya pendwa . suluhu ya matatizo katika riwaya ya “Nyota ya Rehema “ imedhihirika pale ambapo mhusika Rehema baada ya kupiia mikasa mingi katika maisha ambayo ilimfedhehesha, mfano kufa kwa mama yake (Aziza ) safari yake ya kutoroka nyumbani kwao ,maisha magumu aliyokuwa nayo mjini ,kudhurumiwa haki ya urithi lakini badi hakukata tama,hatimaye akampata sulubu ambaye kwake alimuona ni mume mchapakazi na chaguo lake katika maisha. Ilhali katika riwaya pendwa, suluhisho la matatizo haijaonyeshwa , kwani mwandishi wa riwaya ya kufa na kupona anaonyesha mwisho wa riwaya kuwa Lulu anawapigia simu
Tofauti nyingine ni riwaya pevu imejikita katika mkondo wa kihalisia ilihali riwaya pendwa imejikita katika mkondo wa kipelelezi, mkondo wa kiuhalisia ni aina ya mkondo ambao hueleza jambo katika uhalisia wake. Katika riwaya ya nyota ya rehema mwandishi amejaribu kueleza matatizo mbalimbali yanayoakisi jamii zetu. Mfano; ugumu wa maisha ,watu kunyimwa haki zao mwandishi katika (uk 143) anathibitisha
“ Konde zilizomo na shamba lenyewe ni mali yangu bwana Mudiri na mimi ndiye mototo wa marehemu bwana Faud……………” . Hapa mhusika Rehema alikuwa akijitetea pindi alipokuwa anataka kudhurumiwa shamba wakati ni haki yake kabisa. Hivyo basi haya ni masuala ya kihalisia kabisa katika jamii zetu. Lakini mkondo wa kipelelezi ni aina ya mkondo ambao hujikita kuzungumzia masuala ya mapenzi, upelelezi na ujasusi katika riwaya ya Kufa na kupona tunaona mwandishi ameeleza na kuonyesha vya kutosha masuala ya upelelezi na mapenzi mfano katika (uk 66) mwandishi anasema
“ kwa hiyo kazi kubwa sasa ni kutafuta kwa kila njia tumjue huyo “ bosi mi nani. Na habari nilizozipata kwa James hizo karatasi zinabadilishwa kesho usiku………. .Hapa ni Willy alikuwa anazungumza na Sammy.hivyo basi hapa inasibitisha kuwa hawa wanajihusisha na vitendo vya upelelezi. Pia masuala ya mapenzi katika riwaya hii pia yapegusiwa kama sifa mojawapo mwandishi katika (uk 105)
“Oh Willy,nilikuwa nakuota sasa hivi umenikumbatia ,kumbe ni kweli .Oh ,sasa nimepona kabisa ,nibusu Willy nirejewe na uhai”. Hapa ni lina baada ya kukutana na Willy.hivyo basi hii inathibtisha riwaya pendwa imejikita katika mkondo wa kipelelezi.
Kwa kumalizia riwaya pendwa na riwaya pevu zote kwa ujumla hubeba dhima za fasihi nia na madhumuni ni kufikisha ujumbe mzito uliokusudiwa kwa jamii lengwa ,mfano wa dhima hizo ni kuelimisha ,kukosoa ,kuburudisha kuonya ,kutunza historia ya jamii hivyi basi fasihi ya riwaya inamchango mkubwa katika jamii.
Madumulla, J.A. (2009),Riwaya ya Kiswahili,Nadharia Historia na Misingi ya Uchambuzi Dar-es-Salaam:Mture Education Publishers.
Masebo, J.A.(2007), Nadharia ya Fasihi (Fasihi kwa Ujumla).Dar-es- Salaam: Nyambari Nyangwine Publishers.
]]>Swali :

JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU A : UFAHAMU NA UFUPISHO
SWALI LA 1
Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata.
Tendawili: Tega: Mtalitegua leo?
Oneni mazinge ya njia, enyi mbele mwendao,
Msizimwe macho na vumbi la pofuo,
Msizibwe masikio na upepo uvumao,
Msizibwe pua na mnuko unukao,
Oneni majani ya upepo huu uvumao.
Tafiti chanzo na midundo ya yote yapitayo:
Anzia kijijini huko kwa mtu – kwao,
Watu huko watakwambia hali yao,
Huko, utenzi wa dhiki ndio uimbwao,
Utawaona wamekabwa koo zao,
Ngoma si ya furaha ichezwayo leo,
Bei ya vitu hupanda, sio bei ya mazao,
Na maisha yamepanda, sio maisha yao.
Njoo kwa wafanyakazi – mali wazalishao,
Watakweleza haki ikabwavyo koo,
Ukemi umezidi – ahaa! Siyo vilio,
Bei ya vitu hupanda, siyo mshahara wao,
Wafaidio ni wale wenye vyeo,
Yasikilize kidogo mazungumzo yao:
“Tutakutana wapi – New Afrika – leo?
“Palm Beach. New Afrika pamechosha, siyo?
Hizi ni enzi za wenye nafasi zao,
Asiye na fedha katu hana bao,
Na wasio na bao hulia kikwao.
Au tuyamulike mashule tuliyo nayo,
Wanafunzi – habari zafika kila leo,
Kiboko cha nidhamu ni halali yao,
Kila wapazapo sauti zao,
Hupigwa konzi na walimu wao,
Na wengine hurudishwa kwao.
Enyi wenye kuona, yapi yale muonayo,
Kulikucha, kulikucha au uongo huo?
Walenge, walengao, wafume wafumao,
Lugha ya mata itasemwa, siyo?

Uko wapi mwanga wa mwenge umulikao,
Tariki ya ndoto yetu tuiotayo?
Hata hivyo, washairi tunao,
Na kila siku hupaza sauti zao,
Tendawili hili litateguliwa leo?
MASWALI
(a) Andika kichwa kifaacho kwa shairi ulilosoma
(b) Toa maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi.
(i) Tariki
(ii) Ukemi
(iii) Vumbi la pofuo
(iv) Konzi
(v) Katu
(d) Mwandishi ana maana gani anaposema “utenzi wa dhiki ndio uimbwao” katika ubeti wa pili?
SWALI 2
Fupisha shairi ulilosoma kwa maneno yasiyozidi mia na hamsini (150) na yasiyopungua mia moja (100).
MAJIBU YA SWALI LA 1
(a) Kichwa cha shairi kiandikwe kwa herufi kubwa na kisizidi maneno matano (5)
Mf: – KITENDAWILI
(b) Maana ya maneno
(i) Tariki – njia
(ii) Ukemi – ukulele, sauti ya juu sana ya mtu au kitu, yowe, maneno makali ya kukaripia anayosema mtu
(iii) Vumbi la pofuo – vumbi linalomfanya mtu kupoteza uwezo wa macho yake kuona.
(iv) Konzi – vidole vya mkono uliokunjwa pamoja kwa lengo la kumpiga mtu kichwani
Kitenzo cha kupigwa
(v) Katu – neno linalotumika kuelezea ukanushi wa kitu au jambo fulani.
wafanyakazi kukosa haki yao wakati wao ndio wazalishaji.
hakuna uwiano kati ya bei ya vitu inavyopanda na mishahara ambayo haijapandishwa.
Wenye vyeo ndio wenye pesa na wanaofaidi maisha kwani hata wanabadilisha sehemu za kustarehe.
Wasio na nafasi hata kukosa fedha hawana la kufanya
Ubeti wa tano
Mwandishi anazungumzia yafuatayo:
Anawasemea wananchi wanaoona uozo unaoendelea katika jamii na hawawezi kusema
Anajua mwenge wa uhuru uliwekwa ili kumulika waovu sasa maovu yapo ndani ya jamii. Mwenge ufanye kazi yake, yaani viongozi wenye dhamana wasimame kwenye nafasi zao kuondoa maovu hayo
Anawaasa washairi wawe wazi kusema kweli ili jamii iwe huru
(d) Mwandishi anamaanisha yafuatayo:
– Kutokana na hali ya maisha basi kila lisemwalo na jamii huwa limebeba hali halisi ya maisha ya shida yanayoikabili jamii husika.
SWALI LA 2
Hapa unapaswa kufupisha shairi hilo kinathari kwa kuzingatia yafuatayo:
Mawazo makuu
Kutegua kitendawili kuhusu maisha
Watu/wananchi wawe macho kulingana na maisha ambayo si mazuri
Chanzo cha maisha magumu – ni bora kuangalia/kufanya utafiti kuanzia vijijini. Watu wanaishi maisha ya dhiki
Mijini wafanyakazi ndio wanaozalisha lakini hawana haki
Kupanda kwa bidhaa na huku mishahara ikidumaa huongeza adha ya maisha
Wenye navyo wanafaidi maisha kuliko wasio navyo
Maisha ya shuleni – wanafunzi hawana nafasi ya kutoa mawazo yao
Mwenge wa uhuru umulikao ufanye kumulika na kuondoa uozo wote.
ZINGATIA PIA
Mpangilio mzuri wa hoja wenye ufasaha wa lugha
Tumia maneno yako mwenyewe bila kupotosha maana ya msingi
Zingatia taratibu za uandishi na mpangilio wa aya
Zingatia idadi ya maneno uliyopewa
NB: Ufupisho huwa theluthi moja (1/3) ya habari ya awali.]]>

https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1102
Thu, 02 Sep 2021 03:22:22 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1102
Kwa kutoa mifano, onesha maumbo mbalimbali ya kitenzi kishirikishi. (onesha
maumbo matano).
MAJIBU
(i) Kishirikishi –li-
Mfano:
Embe li bicho
Gari li bovu
(ii) Kishirikishi –u-
Wewe u mdogo
Baba u mkubwa
(iii) Umbo –i-
Mikono i mirefu
Shule i porini
(iv) Umbo –ki-
– Kisu ki kikali
– Kisahani ki kidogo
(v) Umbo –ndi- ambalo haliwezikusimama peke yake bali huambishwa kirejeshi kulingana na nomino husika.
– Tumaini ndiye mkubwa
– Watoto ndio wakorofi
– Ndizi ndizo mbivu
(vi) Umbo –ngali-
– Amani angali mtoto
– chakula kingali kibichi
(vii) Umbo -wa-
– Wazee wa wakali
– vijana wa wakorofi
(vii) Umbo –si- (huongezwa kiambishi rejeshi kulingana na nomino husika.
Yeye si mwanangu
Yeye ndiye mwanangu
(viii) Umbo –kuna-/ – hakuna-
Mbagala kuna mvua
Mbagala hakuna mvua
(viii) Umbo –yu-
Huyu yu mgonjwa
-Mzee yu hospitali
(ix) Umbo –ya-
– Maembe ya mabichi
– Mashati ya machafu
2. (a) Eleza maana ya kishazi na utoe mifano.
MAJIBU
Kishazi ni tungo inayotawaliwa na kitenzi na yenye kutoa taarifa kamili au isiyo kamili. Kitenzi chenye kutoa taarifa kamili huzalisha kishazi huru na kile chenye taarifa isiyo kamili huzaaa kishazi tegemezi (K/Tg).
Mfano:
Baba analima (K/Hr)
Mtoto anayelia (K/Tg)
Fafanua sifa nne za kishazi tegemezi na utoe mifano kwa kila sifa.
Sifa za kishazi tegemezi
– Hakitoi taarifa kamili bila kuambatana na kishazi huru
Mfano:
Mtoto aliyeiba jana
Chumba kilichovunjwa
– Hutambulika kwa kuwa na viambishi rejeshi
Mfano:
Shule inayouzwa
Nyumbu aliyepigwa risasi
– Huweza kufutwa katika sentensi bila kuathiri maana
Mfano:
Mtoto anayelia amenyamaza
Mtoto amenyamaza
– Huweza kutokea kabla au baada ya kishazi huru
Mama aliondoka aliponiona
Mama aliponiona aliondoka
3. Kwa kutoa mifano miwili kwa kila kazi bainisha kazi tano za “kwa” katika tungo za Kiswahili.
MAJIBU
Kuonesha mahali
Juma alienda kwa mwalimu
Sisi tutaenda kwa dada
Kuonesha namna au jinsi
Mgonjwa alikula kwa tabu
Vijana waliimba kwa madaha
Kuonesha uwiano
Walifunga magoli matatu kwa mawili
Watashindana wazee kwa vijana
Kuonesha sababu
Alifeli mtihani kwa uzembe
Utachelewa kwa uvivu
Kuonesha matumizi ya kitu
Tutaenda kwa basi
Utakula kwa kijiko
Kuonesha thamani
Alinunua kwa bei ghali
Atauza kwa gharama kubwa
4. Nini maana ya mtindo wa lugha ya kiofisi/kikazi? Fafanua kwa mifano sifa nne (4) za mtindo wa lugha ya kiofisi/kikazi.
MAJIBU
Mtindo wa lugha ya kiofisi/kikazi ni mtindo unaotumika katika mawasiliano rasmi ambayo hupatikana katika ofisi au mahali popote pa kazi, mikataba, matini za kisheria, matangazo ya vikao, ripoti za mikutano, mahakamani, n.k.
Sifa za mtindo wa lugha ya kiofisi/kikazi ni kama vile:
Usahihi wa mambo yanayojadiliwa (ushahidi)
Matumizi ya istilahi maalumu zinazohusu mambo ya kiofisi
Hakuna matumizi ya misimu, mafumbo, tafsida (hutumia lugha sanifu)
Matumizi ya vifupisho hasa majina ya mashirika ya kimataifa kama vile UNO, ILO, UNICEF, IMF, UNESCO, n.k (Majina ya watu hayaruhusiwi kufupishwa)
]]>

Wewe ni mhitimu wa fani ya elimu na umekusudia kuomba kazi Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI). Andika wasifu kazi utakaouambatanisha kwenye barua yako ya kuombea kazi.
2006-2009: Shahada ya Sanaa katika Elimu. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
2004-2006: Cheti cha Elimu ya sekondari ya juu. NECTA
2000-2003: Cheti cha Elimu ya sekondari ya kawaida. NECTA
1993-1999: Elimu ya Msingi. Shule ya Msingi Mto wa Mbu
Uzoefu na historia ya kuajiriwa
2013-2015: Mwandishi wa Habari za Mazingira, Mwananchi Communications
Ltd
Ujuzi na weledi
Katika sehemu hii onesha aina ya ujuzi na weledi uliowahi kuupata kupitia warsha, semina na makongamano yalivyokusaidia kuongeza ujuzi mwepesi unaoweza kukusaidia kuzalisha, kukuza, kubuni, kuanzisha, kusababisha, kubadili, kuchangia mabadiliko na kuwezesha.
Onesha mahali, mwaka, shughuli husika na malengo yake kwa mtiririko wa kuanzia hivi karibuni mpaka yale ya zamani.
Mapendeleo
Ninapendelea kuogelea, kusoma magazeti na habari habari mbalimbali za kijamii, kusogoa kwenye mitandao ya kijamii.
Tuzo au heshima
Mwajiri huvutiwa na mtu anayeweza kuonyesha namna jitihada zake zilivyotambuliwa na wengine. Onesha namna bidii, na ari yako ya kazi ilivyowahi kutambuliwa katika ajira zilizopita.
Siyo lazima iwe kazini tu, inawezekana kuwa katika masomo, lakini ziwe tofauti na zile tuzo za kitaaluma moja kwa moja.
Maneno kama, nilishinda, nilituzwa na nilitambuliwa, kwa sababu ya shughuli, majukumu, jitihada zilizowahi kufanywa, yanakuongezea nafasi ya kukubalika.
Orodha ya wadhamini
MAJURA KAMAZI
S.L.P 1020
TANGA
SIMU: 0717104507
CHARLES MAZIKU
S.L.P 1045
DAR ES SALAAM
0684104507
TAMKO
Mimi…………………ninatamka kuwa taarifa zilizotolewa kwenye wasifu kazi huu ni zangu na sahihi kwa mujibu wa uelewa wangu.]]>
SWALI:

https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1100
Wed, 01 Sep 2021 12:40:36 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1100
1. Lugha ya Kiswahili ni lulu ya Taifa la Tanzania, barani Afrika na duniani kote. Toa sababu tano zenye mifano kuthibitisha dai hilo.
MAJIBU
UTANGULIZI
Lulu ni kitu cha thamani, Kiswahili kinafananishwa na kito cha thamani kutokana na umuhimu wa lugha yenyewe na historia yake kwa jamii.
KIINI (Sababu tano)
Kiswahili hutumika kama lugha rasmi bungeni, mahakamani, serikalini
Kiswahili hutumika kufundishia shule za msingi na kama somo kwa shule za sekondari na elimu ya juu (Tanzania)
Nchi za nje nyingi zimeanzisha mifumo ya elimu inayohusisha somo la Kiswahili. Baadhi ya nchi hizo ni Marekani, Canada, China, Sudani na Botswana
Matumizi ya Kiswahili katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania mfano: Televisheni (Channel Ten,TBC, ITV, Clouds)
Redio (TBC, Radio One, Efm, Magic Fm)
Magazeti (Mwananchi, TanzaniaDaima, Uhuru)
Nchi za nje – mfano BBC, Sauti ya Amerika, Redio Vatican, Redio France International, Deutsche Welle
Kiswahili hutumika kwenye mitandao ya kijamii kama ‘Facebook, Twitter, WhatsApp, n.k
Matumizi ya Kiswahili katika mfumo wa kibiashara kimataifa na kitaifa mfano mikataba ya kibiashara, vituo vya kibiashara kama Beijing China, New York Marekani, Moscow Urusi, Dubai Uarabuni, London Uingereza. Hutumia lugha ya Kiswahili kuwasiliana.
Kiswahili kimepewa hadhi ya kimataifa kufikia kuwa lugha ya tano katika umoja wan chi huru za Afrika. Kiliteuliwa kuwa moja ya lugha za kiafrika itakayotumika pamoja na lugha za kigeni kama Kiingereza, Kireno, Kifaransa na Kiarabu.
Kiswahili hutumika kama lugha ya Taifa nchini Tanzania, vilevile nchi za Kenya, Uganda na Rwanda.
Kiswahili hutumika katika shughuli za maisha ya kawaida ya kila siku kama vile majumbani, sehemu zenye mikusanyiko kama kanisani, misikitini, n.k
HITIMISHO
Toa hitimisho zuri linaloendana na swali.
2. Dini inasaidiaje katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili nchini Tanzania? Toa hoja tano (5)
MAJIBU
UTANGULIZI
Dini ni miongoni mwa taasisi za kijamii zenye mchango mkubwa sana katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili hapa nchini Tanzania. Mchango wa dini katika kukuza na kueneza Kiswahili unajipambanua kama ifuatavyo:
KIINI
Mahubiri na mawaidha ya kidini hutolewa kwa lugha ya Kiswahili
Madrasa na shule za dini za watoto (Sunday schools) hufundisha kwa kutumia lugha ya Kiswahili
Uanzishwaji wa vyombo vya habari vya kidini kama redio, magazeti na televisheni ambavyo hurusha na kutoa habari kwa lugha ya Kiswahili mfano: Redio Maria, Redio Imaan, Agape Televisheni, Magazeti kama Al-Noor, Mwangaza, n.k
Uanzishwaji wa shule pamoja na vyuo vya taasisi za kidini ambavyo hufundisha kwa lugha ya Kiswahili. Vilevile hufundisha walimu wa somo la Kiswahili mfano wa vyuo ni kama St. Augustine, Tumaini, TEKU, Mum, n.k
Pia taasisi za kidini zinamiliki shule nyingi za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu
Nyimbo za kidini kama kwaya na hata tenzi za rohoni, huimbwa kwa lugha ya Kiswahili mfano wasanii wa injili kama Rose Muhando, Christina Shusho, n.k huimba nyimbo zao kwa lugha ya Kiswahili na husikilizwa na watu wengi
Vilevile kanda na santuri za Kaswida nazo huuzwa na kusikilizwa na watu wengi ndani na nje ya nchi.
HITIMISHO
Toa hitimisho zuri lenye kuafiki mchango chanya wa dini katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili.]]>

https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1081
Tue, 31 Aug 2021 04:58:38 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1081
MAJIBU
(a) Muda mfupi baada ya kupata uhuru.
(e) Kipindi cha hali ngumu ya maisha baada ya vita vya Kagera.
Ukata
Ulanguzi
Kabachori
(f) Kipindi cha kuanzia 1985 hadi sasa
Ruksa
Ngangari
Ngunguri
Wapambe
Wafurukutwa
Wakereketwa
]]>
https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1055
Sat, 28 Aug 2021 06:23:34 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1055
Eleza maana ya ‘kiimbo’
Kiimbo ni sauti maalum inayojitokeza unapotamka maneno fulani. (kupanda na kushuka kwa sauti)
Tunga sentensi mbili zinazodhihirisha uamilifu wa aina mbalimbali wa kiimbo.
Mama ameenda sokoni? -swali
Mama ameenda sokoni. -kauli
Tunga sentensi ya hali timilifu ukitumia kiunganishi cha kibantu
Mwalimu na mwanafunzi wameenda nyumbani.
na- kiunganishi cha kibantu
wameenda – hali timilifu
Kazi hii imekuwa ngumu kwangu. (maliza kwa ….ngumu)
Kwangu, kazi hii imekuwa ngumu.
Andika sentensi hii kwa hali ya ukubwa, wakati uliopita
Ningepelekewa huyu ndama nyumbani ningefurahi.
Nilipelekewa hilo dama jumbani nikafurahi.
Tunga sentensi kutumia kirejeshi cha tamati.
Kiti wakitumiacho kimevunjika.
Kirejeshi tamati ni ‘cho’
Taja yambwa za sentensi ifuatayo :
Mjomba hakupikiwa mlo wa leo kwa bidii.
Mjomba – Yambwa tendewa:
Mlo- Yambwa tendwa
Tunga sentensi kanushi kutumia kiambishi ‘a’
Mtoto asipolishwa vizuri, hawezi kulala.
Andika miundo yoyote miwili ya nomino katika ngeli ya U-ZI huku ukitoa mifano
U-ny uzi-nyuzi
u-nd ulimi-ndimi
w-ny wembe-nyembe
u- ukuta -kuta
Bainisha vitate vifuatavyo kwa kutunga sentensi moja. (alama 2)
kaza, kasa.
Mvuvi alikaza kamba alipomuona kasa akiwa ndani ya wavu.
Taja ala za kutamkia vitamkwa vifuatavyo.
/v/g/j/t/
v- Midomo + Meno
g – Kaakaa Laini
j- kaa kaa ngumu
t- Ufizi
Bainisha shamirisho katika sentensi: (alama 3)
Mwalimu atawasimulia wanafunzi hadithi kwa kipaza sauti
Mwalimu-shamrisho kitondo,
Hadithi- shamrisho kipozi,
kwa kipaza sauti- shamrisho ala
Toa mifano miwili ya matumizi ya ritifaa(’)
Kuonesha king’ong’o kwa mfano ng’ombe
Kuonyesha nambari iliyoachwa kwa mfano ’99
Walipokuwa wanasoma mgeni wa heshima alifika (andika kwa wakati ujao)
Watakapokuwa wakisoma mgeni wa heshima atafika.
Tunga sentensi yenye ni uundo ufuatao:
S KN(N+U+N+V)+KT(T+E+E)
Mama na mtoto wake wanatembea haraka sana.
Tunga sentensi mbili kutofautisha vitate hivi kimaana. (alama 2)
(i) Hawara
(ii) Hawala
Hawara alifukuzwa nyumbani kwa kuwa mzembe.
Alipomaliza kazi, alilipwa kwa hawala.
Kanusha bila kutumia ‘amba’
Nitavaa nguo ambayo ni safi.
Sitafaa nguo iliyo safi.

https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1053
Sat, 28 Aug 2021 05:48:40 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1053