MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Nukuu]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ Sat, 27 Apr 2024 14:45:52 +0000 MyBB <![CDATA[KITABU CHA MWANAFUNZI-KIDATO CHA PILI (TET)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2532 Fri, 29 Apr 2022 03:19:27 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2532
.pdf   KIDATO CHA PILI.pdf (Size: 35.27 MB / Downloads: 44) ]]>

<![CDATA[KIDATO CHA PILI: MATAMSHI NA LAFUDHI YA KISWAHILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1662 Fri, 03 Dec 2021 10:27:35 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1662 Matamshi na Lafudhi ya Kiswahili Matamshi ni namna ambavyo mtu anatamka neno au jinsi mtu anavyozungumza lugha. Unaposema fulani ana matamshi mazuri ya Kiswahili utakuwa unamaanisha anazungumza Kiswahili fasaha.
Neno moja linaweza kuzungumzwa/kutamkwa kwa namna tofauti na watu mbalimbali kutokana na sababu mbali mbali, sababu hizo ni pamoja na eneo la kijiografia anakotoka huyo mtu, kabila lake, kundi lake la kijamii mfano msanii au mwanasiasa, na elimu aliyonayo. Hizi zote zinaweza zikawa ni sababu za kufanya watu watofautiane katika matamshi.
Lafudhi Mbalimbali za Kiswahili
Dhana ya matamshi huhusisha
Sauti za lugha husika
·
Mkazo
·
Kiimbo
Sauti za lugha ya Kiswahili
Sauti za lugha ya Kiswahili hujumuisha irabu na konsonanti, ambazo kwa ujumla huunda sauti 24, irabu tano na konsonanti 19 (konsonanti x na q hazipo katika matamshi ya kiswahili). Sauti za Kiswahili hutamkwa kama zilivyoandikwa, kwa mfano maneno “data” au “dengue” wewe unayatamkaje? Wengi huyatamka kama yalivyo hata
kama wakiwa wanazungumza kiingereza, hii ni kwa sababu maneno ya Kiswahili hutamkwa kama yalivyoandikwa.
Kwa hiyo unapotamka maneno ya Kiswahili ni sharti uzingatie sauti asilia za lugha ya Kiswahili. Kuna watu huwa wanaandika hivi “xaxa”, hii huwa unaitamkaje? Au “ucjal” huwa unaitamkaje? Kwa kufuata matamshi asilia ya Kiswahili “ucjal” itatamkwa “uchijal” sijui itakuwa ina maana gani sasa. Na pengine umekuwa
ukitumia maandishi ya namna hii hata kwenye insha zako ukidhani upo sahihi au ni kwa mazoea tu, sasa kwa kuwa umejua matamshi sahihi ya Kiswahili ni yapi, utajifunza kuyatumia kwa usahihi katika maandishi rasmi na yasiyo rasmi.
Mkazo
Katika lugha ya Kiswahili kuna namna ya kutamka maneno ili kuleta maana mbali mbali, kwa mfano neno “barabara” litaleta maana husika kulingana na jinsi lilivyotamkwa. Hivyo, mkazo ni pale silabi inapotamkwa kwa kukazwa. Maneno ya Kiswahili huwa na silabi moja ambayo hutamkwa kwa nguvu zaidi kuliko silabi nyingine. Unapotamka silabi iliyotiwa mkazo, sauti hupandishwa juu kiasi. Maneno mengi ya Kiswahili, hasa yale yenye asili ya Kibantu hutia mkazo katika silabi ya pili kutoka mwisho.
Kwa mfano:ba’bu, maya’i, rama’ni (mimi nilikuwa nikitamka ra’mani), baraba’ra (njia). Baadhi ya maneno yenye asili ya kigeni, huwa na mkazo katika silabi nyingine. Kwa mfano: bara’bara (sawa sawa), Alha’misi
Kiimbo
Ni utaratibu maalum wa upandaji na ushukaji wa mawimbi ya sauti unaojitokeza katika utamkaji wa lugha fulani.
Katika utaratibu wa utamkaji, dhana ya Kiimbo huandamana pia na dhanna ya kidatu ( yaani , kiwango cha juu, cha chini au cha kati cha sauti katika usemaj), Kwa hivyo ni muhimu hapa kueleza tofauti zilizopo baina ya kiimbo na kidatu. Wakati kiimbo kina maana ya kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti ya lugha, kidatu kina maana ya kiwango cha sauti isikikayo, wakati wa utamkaji ama kuwa juu, kuwa katikati au kuwa chini.
Aina za viimbo
·
Kiimbo cha maelezo: Kiimbo cha maelezo ni kile ambacho kwa kawaida msemaji wa lugha akiwa kwenye kidatu chochote kile mawimbi sauti ya usemaji wake yanakuwa takriban katika mstari ulionyooka. Mfano, Mwalimu anafundisha.
·
Kiimbo cha maulizo: Kiimbo cha kuuliza hujitokeza kwa kutumia viwango tofauti vya kidatu kutegemeana na aina ya swali linaloulizwa. Mfano, mwalimu anafundisha?
·
Kiimbo cha amri: kiimbo cha amri hakitofautiyani sana na kiimbo cha maulizo. Kiimbo cha amri, mzungumzaji hutumia kidatu cha juu zaidi kuliko ilivyo katika kiimbo cha maelezo. Mfano, njoo hapa!
Lafudhi ya Kiswahili
Lafudhi ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani ambayo yanatokana na athari za kimazingira. Mazingira hayo yanaweza kuwa eneo atokalo mtu, mahali alikosomea, kiwango chake cha elimu, tabaka lake la kijamii na kadhalika.
Lugha ya Kiswahili ni lugha ya pili kwa watumiaji wengi wa afrika mashariki, kwa hiyo hii inafanya kuwatambua wazungumzaji wa Kiswahili kulingana na makabila yao au maeneo wanakotoka. Kwa mfano, kwa hapa Tanzania tunaweza kuwatambua watu wa mwanza kwa lafudhi yao, watu wa mtwara kwa lafudhi yao, watu wa pemba kwa
lafudhi yao au watu wa Musoma kwa lafudhi yao.
Mifano
1.      Usiniretee maswara ya ubaguzi wa kikabira hapa (Wakuria)
2.      Amemupiga mutoto ya watu juu amemuibia mfaranga makumi mawili (Wakongo)
3.      Ukikaa nchale, ukichimama nchale (Wamakonde)
4.      Wewe unakamuaga mang’ombe tu moja kwa moja (Wasukuma)
5.      Mbona unakuwa kinganganizi, nilishakwambia sikupendi lakini wewe bado unaningangania tu! (Wahaya)
ZOEZI  
Neno lipi kati ya haya linaonesha lafudhi ya mzungumzaji wa Kiswahili kutoka jamii ya Wapare?
A Sasa
B Thatha
C N’toto
D Thelathini
 “Twende tukarare” ni sentensi ya Kiswahili inayoonesha lafudhi ya kabila gani?
A Wakurya
B Wahaya
C Wajita
D Wamasai
___ni tofauti ya matamshi ya wasemaji wa lugha ambayo husababishwa na athari ya mazingira.
A Mkazo
B Lafudhi
C Utata
D Mtindo wa lugha
 ‘Hifi ni fiatu fyangu’ hii ni lafudhi ya watu wa jamii gani?
A Wanyakyusa
B Wapare
C Wayao
D Wamakua
___ ni tungo ya Kiswahili yenye lafudhi ya Kimakonde.
A Juma amemupiga mutoto.
B Riereze riondoke.
C We mitu kabila gani?
D N’toto amekuja.
]]>
Matamshi na Lafudhi ya Kiswahili Matamshi ni namna ambavyo mtu anatamka neno au jinsi mtu anavyozungumza lugha. Unaposema fulani ana matamshi mazuri ya Kiswahili utakuwa unamaanisha anazungumza Kiswahili fasaha.

<![CDATA[KISWAHILI KIDATO CHA PILI (KENYA)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1602 Sun, 28 Nov 2021 08:36:24 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1602
.pdf   KISWAHILI KIDATO CHA PILI.pdf (Size: 309.08 KB / Downloads: 1) ]]>

<![CDATA[UUNDAJI WA MANENO (VIDEO)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1348 Thu, 21 Oct 2021 08:10:18 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1348 ]]> ]]> <![CDATA[UTATA KATIKA MAWASILIANO (VIDEO)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1347 Thu, 21 Oct 2021 08:07:26 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1347 ]]> ]]> <![CDATA[USIMULIZI WA HABARI (VIDEO)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1346 Thu, 21 Oct 2021 08:04:27 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1346 ]]> ]]> <![CDATA[UHIFADHI WA FASIHI SIMULIZI (VIDEO)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1345 Thu, 21 Oct 2021 08:00:40 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1345 ]]> ]]> <![CDATA[SIMU YA MAANDISHI (VIDEO)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1344 Thu, 21 Oct 2021 07:52:55 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1344 ]]> ]]> <![CDATA[MATUMIZI YA LUGHA KTK MIKTADHA MBALIMBALI (VIDEO)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1343 Thu, 21 Oct 2021 07:10:09 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1343 ]]> ]]> <![CDATA[MASHAIRI YA KIMAPOKEO (VIDEO)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1342 Thu, 21 Oct 2021 07:07:38 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1342 ]]> ]]> <![CDATA[UHIFADHI WA FASIHI SIMULIZI (SLIDES)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1226 Fri, 10 Sep 2021 12:41:42 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1226
.pdf   UHIFADHI-WA-FASIHI-SIMULIZI.pdf (Size: 910.86 KB / Downloads: 10) ]]>

<![CDATA[MAMBO YA MSINGI YANAYOJENGA MAANA YA LUGHA (UFASILI WA DHANA YA LUGHA)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=670 Wed, 28 Jul 2021 14:36:11 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=670
.pdf   Maana ya lugha.pdf (Size: 90.13 KB / Downloads: 16) ]]>

<![CDATA[LUGHA YA MAZUNGUMZO NA LUGHA YA MAANDISHI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=669 Wed, 28 Jul 2021 14:20:54 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=669
.pdf   Sifa ya Lugha ya Kimazungumzo.pdf (Size: 31.27 KB / Downloads: 4) ]]>

<![CDATA[KIDATO CHA PILI: REJESTA]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=659 Tue, 27 Jul 2021 12:10:32 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=659 Rejesta
Kwa ujumla tunaweza kufasili rejesta kama mtindo wa lugha kutegemeana na kazi fulani, muktadha wa matumizi, lengo na uhusiano wa wanaowasiliana. Katika muktadha rasmi rejesta hurejelea upande mmoja kama vile, msamiati wa kiufundi, adabu maalum na matumizi ya lugha fasaha, mfano katika elimu, mahakamani na kadhalika.
Kuwasiliana kwa kutumia Rejesta
Rejesta za Mitaani
Haya ni mazungumzo yanayozungumzwa magengeni nayo hueleweka na wazungumzaji wenyewe. Ni lugha ambayo huchipuka kutokana na kikundi cha watu ambacho ni kidogo. Mfano wa maneno yanayotumika sana mitaani ni kama vile “Mshikaji” (rafiki) Demu” (mwanamke)n.k. Kwa ujumla lugha ya mitaani ni lugha isiyo sanifu, ni lugha iliyojaa maneno ya mitaani ambayo yanaeleweka kwa wazungumzaji wenyewe.
Mazungumzo ya Kwenye Shughuli Maalum (Rejesta za Mahali)
Mazungumzo ya kwenye shughuli maalumu hayafanywi kiholela, bali yanafuata taratibu na kanuni maalum zinazojitokeza katika mazingira haya. Kutokana na kutumiwa kwake kwa muda mrefu kwenye mazingira yale yale.
Mazungumzo ya kwenye shughuli maalumu ni kama vile mazungumzo ya:
  • Maofisini au mahali popote pa kazi
  • Mahakamani
  • Hotelini
  • Hospitalini
  • Msikitini
  • Kanisani n.k
Mazungumzo ya mahotelini yana utaratibu wake ambao katika hali ya kawaida inaweza isieleweke.
Nani wali kuku?
B: Mimi
Chai moja wapi?
B: Hapa
Katika mazungumzo haya A anapouliza “Nani wali kuku”, ana maana kuwa nani anahitaji kula wali na nyama ya kuku”. Hapa hana maana ya kumwainisha mtu aitwaaye “wali kuku”.
Kwa upande wa lugha ya mahakamani ni tofauti na lugha ya hotelini. Lugha ya mahakamani inasisitiza usahihi ili kuondoa migongano miongoni mwa wanaohusika.
Mfano 1
Mfano:
Wakili wa Utetezi: Nakuuliza jaribio la kutaka kupindua serikali litakuwa kosa la namna gani katika sheria za Tanzania?
Kamishna Msaidizi: (Baada ya kupewa kitabu cha sheria za Tanzania na kukisoma) Ni kosa la uhaini.
Wakili wa Utetezi: Ulichukua muda mrefu kufikia jibu hili. Washitakiwa wawili hawahusiani na makosa haya?
Kamishna Msaidizi: Sijui.
Kimsingi hii ni hali ya kawaida kabisa katika mahojiano ya mahakamani. Mara nyingi mahojiano katika mahakama hayaendi haraka sana. Kila mtu anayehusika – hakimu, mwendesha mashtaka, wakili, mdaiwa, shahidi, n.k. hujieleza kwa wazi wazi bila kujali urefu wa maelezo.
Rejesta Zinazohusu Watu
Rejesta zinazohusu watu ni yale mawasiliano yasiyo rasmi, ni yale maongezi ya kawaida ya kila siku au mazungumzo rasmi; kwa mfano mazungumzo kati ya:
  • Vijana wenye rika moja,
  • Wazee wenyewe,
  • Wanawake wenyewe,
  • Wanaume wenyewe,
  • Mwalimu na mwanafunzi,
  • Meneja na wafanyakazi wake,
  • Mtu na mpenzi wake, n.k.
Mazungumzo miongoni mwa marafiki wa rika moja huzungumza lugha ambayo wao wenyewe wanaielewa na sio rahisi kwa mtu wa rika lingine kuielewa lugha hiyo.
Mfano 2
Mfano:
‘Basi, Master jana wikiendi ilikuwa kibaridi sana. Basi nilizamia infoo kwenye zinga la mnuso huko saiti za upanga. Nilifika getini nikakuta baunsa kanyuti chedro likisubiri kumtoa noma kila mzamiaji. Alikuwa mnoko kishenzi. Akatema mkwara mbuzi, nikajibu kwa mkwaradume….akabloo mimi ndani’.
Maana ya Maneno
  • Wikiendi – Mwisho wa wiki
  • Kibaridi –tulivu
  • Kuzamia infoo – Kuingia mahali bila kualikwa
  • Zinga la Mnuso –sherehe kubwa
  • Saiti –sehemu
  • Baunsa limenyuti chedro – Ni mlinzi wa mlangoni ametulia pembeni
  • Noma – Hatari
  • Mnoko kishenzi – kinaa sana
  • Mkwara mbuzi – Vitisho dhaifu (Sani, Toleo Na 49).
Mtu asomapo maelezo hayo, mara moja unaona jinsi vijana hawa wa rika moja waishio mjini wanavyozungumza Kiswahili. Si rahisi kwa mzungumzaji wa Kiswahili sanifu kuielewa kirahisi lugha hiyo.
‘Chai moja wapi?’ hii ni rejesta inayotumika katika muktadha gani?
A Hotelini
B Dukani
C Hospitalini
D Darasani
___ni mazungumzo ya kwenye shughuli maalumu yanayofuata taratibu na kanuni.
A Rejesta za mitaani
B Rejesta za kitarafa
C Rejesta za mahali
D Rejesta za watu
 ‘Je mshtakiwa una utetezi wowote?’ rejesta hii hutumika wapi?
A Msikitini
B Kanisani
C Mahakamani
D Shuleni
___hutumika kuwasiliana katika muktadha maalumu.
A Lahaja
B Rejesta
C Misimu
D Istilahi
Ni rejesta gani zinahusu mazungumzo ya kawaida ya kila siku?
A Rejesta zinazohusu watu
B Rejesta za kitarafa
C Rejesta za mahali
D Rejesta za mitaani
Dhima za Rejesta
Katika kipengele cha utambulisho wa kijamii tunaangalia namna aina ya lugha ya mazungumzo inavyoweza kujidhihirisha miongoni mwa watumiaji wake au kuwatambulisha na kuwatofautisha wanajamii husika. Pia katika utambaulisho wa kijamii tunaangalia vile ambavyo mtu hutambulika katika jamii kulingana na namna anavyoongea kulingana na hadhi, tabaka, na jinsi ambavyo mtu huyo anavyoweza kusababisha mshikamano au mwachano katika mazungumzo. Kwa mfano jamii itamtambua mwanajamii kuwa ni msomi kulingana na mtindo wa lugha ya mazungumzo anaoutumia, au ni mtu wa mtaani kulingana na lugha anayotumia.
Rejesta, ina nafasi kubwa sana katika maendeleo ya kiuchumi kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Hii ni kutokana na kwamba, madhumuni makuu ya mawasiliano katika biashara ni kuwavutia wateja na kuwafanya kuamini kuwa bidhaa ama huduma wanazouziwa ni za kiwango cha juu na ni thamani bora kwa pesa zao. Hivyo lugha ya biashara (rejesta), kwa kawaida ni lugha ya kutangaza uzuri wa bidhaa au huduma, huwa na sentensi au vifungu vifupi, mfano “Okoa mapesa chungu mbovu” pia huwa na lugha ya kupumbaza na kuaminisha, mfano “Kunywa XYZ kufumba na kufumbua afya yako itakurudia”.
Pia rejesta inasaidia sana kurahisisha mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji katika masuala mbalimbali ya kibiashara na hata katika huduma mbalimbali za kijamii. Mfano hospitalini “mbili mara tatu”, hotelini “kuku wali tafadhali”, sokoni “kata nusu” na maeneo mengine.
Baadhi ya rejesta hutumika kupunguza idadi ya maneno hivyo kufanya mazungumzo yawe mafupi na yanayoeleweka kwa urahisi mfano rejesta za hotelini kama vile:- Muuzaji: wapi ng’ombe? Mteja: hapa Muuzaji: wapi chai chapati? Mteja: hapa.
Pia katika kutolea elimu ya dini kanisani na msikitini rejesta ina nafasi kubwa katika kujenga maadili.
Vilevile rejesta ina nafasi ya kupamba mazungumzo, wazungumzaji wengi wanapozungumza hapa na pale hupenda kutumia maneno tofautitofauti ili kufanya mazungumzo yawe ya kuvutia. Mfano mazungumzo miongoni mwa vijana:
Kijana 1: Niaje? Nakuona umechili
Kijana 2: mzuka jembe. Kama kawa… kama dawa!]]>
Rejesta

<![CDATA[UFAHAMU NA UFUPISHO]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=657 Tue, 27 Jul 2021 06:41:05 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=657
.pdf   Ufahamu na Ufupisho.pdf (Size: 127.44 KB / Downloads: 5) ]]>