MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Nukuu]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ Tue, 30 Apr 2024 06:41:06 +0000 MyBB <![CDATA[ODC : MUHADHARA WA KUMI NA NANE : FANI NA MAUDHUI KATIKA FASIHI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1807 Sat, 25 Dec 2021 11:32:46 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1807
FANI NA MAUDHUI KATIKA FASIHI
18.1 Utangulizi
Katika muhadhara huu utasoma vipengele vya fani na maudhui na jinsi vinavyohusiana.
Madhumuni ya Muhadhara
Baada ya kumaliza kusoma muhadhara huu, utaweza :
  • Kufafanua vipengele vya fani na maudhui.
  • Kuhusianisha vipengele vya fani na maudhui
18.2 Fani na Maudhui
Fani katika kazi za fasihi ni ule ufundi wa kisanaa anaoutumia mwandishi kufikisha ujumbe kwa jamii aliyokusudia. Fani inahusisha mambo yafuatayo; Muundo, Mtindo, Matumizi ya lugha, Wahusika naMandhari. Maudhui katika fasihi ni yale mawazo yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu mawazo hayo. Nayo,yaliyomsukuma mtunzi kutunga na kusana kazi fulani ya sanaa. Pia katika maudhui kuna falsafa ya mwandishi.
Kuna mitazamo miwili inayojadili uhusiano wa fani na maudhui. Mitazamo hiyo ni mtazamo wa kidhanifu na mtazamo wa kiyakinifu.
Mtazamo wa kidhanifu ni ule unaoona kuwa fani na maudhui ni vipengele ambavyo havina uhusiano wowote, kwamba vinaweza kutenganishwa. Wataalamu kadhaa wanalinganisha fani na maudhui na kikombe cha chai. Kikombe kinachukuliwa kama ndiyo fani na upande mwingine chai iliyomo ndiyo maudhui. Mnywaji wa chai hiyo analinganishwa na wasomaji wa kazi ya fasihi.
Vilevile wanafafanua kuwa fani na maudhui hulinganishwa na chungwa ambalo lina sehemu ya nje na ndani. Maudhui ya kazi ya fasihi yanalinganishwa na nyamanyama za chungwa na fani ni sehemu ya nje (ganda). Kwa ufupi hawa wanaona kuwa fani ni umbo la nje la kazi ya fasihi na maudhui ni umbo la ndani.
Mtazamo huu una udhaifu wake (mkubwa) na unaweza kuwachanganya wasomaji. Kwa sababu hauonyeshi ama kuwakilisha ukweli wa mambo juu ya uhusiano uliopo kati ya fani na maudhui katika kazi ya fasihi.
Mtazamo wa kiyakinifu unaeleza vizuri ukweli wa mambo ulivyo. Ni kwamba vitu hivi viwili hutegemeana na kuathiriana na wala havitazamwi katika utengano.
Wanafasihi wenye mtazamo huu, wanalinganisha fani na maudhui na sura mbili za sarafu moja, na si rahisi wala sahihi huzitenga na kuzieleza katika upweke, bila kuhusisha upande mmoja na nyingine. Sura moja ya sarafu ikikosekana, basi sarafu hiyo haiwezi kuwa na hadhi ya kisarafu. Jambo la muhimu ni kuona jinsi kitu kimoja (fani) kinavyoweza kukikamilisha kingine (maudhui).
Wanafasihi hawa wanaonesha kuwa kila kimoja cha kigezo cha fani na maudhui kimo ndani ya chenziwe, kushirikiana na kuathiriana katika ama kijenga vizuri au kubomoa kazi ya sanaa.
Kama kazi ya fasihi itakuwa na fani duni, lakini maudhui yake ni mazuri basi hata maudhui yaliyokusudiwa hayatatoa ujumbe unaokusudiwa ipasavyo. Mfano mzuri ni riwaya ya kikasuku   zilizoandikwa baada ya Azimio la Arusha zinazojadili dhamira ya ujenzi wa jamii mpya kama vile Shida, Mtu ni Utu, Ufunguo Wenye Hazina, Njozi za Usiku, Ndoto za Ndaria n.k. zilisisitiza zaidi maiudhui na kuupuzia kipengele cha fani.
Vile vile kama maudhui ni duni na fani ni bora, pia jamii itapata hasara ya kufikiwa na maudhui yasiyo na maana. Mfano mzuri ni riwaya pendwa zote zimeweka msisitizo kwenye fani na kusahau kipengele cha maudhui. Katika riwaya pendwa kama vile riwaya za upelelezi , mapenzi na uhalifu, zina wahusika ambao hawaaminiki kwani wanapewa sifa ambazo si rahisi kuziona kwa binadamu wa kawaida. (Toa mifano ya riwaya hizo).
Fani na maudhui ni vitu viwili ambavyo huwiana, hutegemeana hatimaye kuathiriana. Uhusiano huo ndio unaojenga kazi bora ya fasihi. Msanii hutumia vipengele mbalimbali vya maudhui katika kuijenga fani na hutumia vipengele mbalimbali vya fani katika kujenga maudhui.
18.3  Vipengele muhimu vya fani na maudhui vijengavyo kazi ya fasihi andishi.
Katika fasihi andishi, fani hujumuisha vipengele vifuatavyo:
Kwanza ni muundo ambao  ni mpangilio na mtiririko wa matukio toka mwanzo hadi mwisho. Hapa tunaangalia jinsi msanii alivyounda na alivyounganisha tukio moja na linguine, kitendo  kimoja na  lingine sura na sura, ubeti na ubeti n.k.  Katika  hadithi na Tamthiliya  muundo unaweza kuwa wa moja kwa moja (Msago), wa Kioo (Rejeshi) au wa rukia. Katika ushairi muundo unaweza kuwa wa  Tathnia, Tathlitha, Tarbia au Sabilia.
Pili, Mtindo, ambao ni upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi andishi kwa njia ambayo hatimaye huonesha nafsi au labda upekee wa mtungaji wa kazi hiyo. Katika riwaya, mtindo unaweza kuwa na masimulizi, monolojia au doyolojia na katika tamthiliya mtindo wake ni dayolojia (majibizano). Katika ushairi mtindo unaweza kuwa wa kimapokeo au wa kisasa.
 
Kipengele cha tatu ni wahusika ambao hutumiwa na msanii kufikisha ujumbe kwa jamii yake. Katika hadithi na Tamthiliya kuna wahusika wakuu, wadodo (wasaidizi) na wajenzi. Wahusika wakuu na wadogo wanaweza kuwa wahusika bapa, mviringo (duara) au shinda (wafoili).
Kipengele kingine ni matumizi ya lugha, ambayo mwandishi hutumia kuyaibusha mawazo yake katika kazi hiyo. Vipengele vya lugha wanavyotumia sana ni:
  • Matumizi ya semi – Misemo, Nahau, Methali, Misimu, Mafumbo n.k.
  • Matumizi ya tamathali za semi
  • Matumizi ya mbinu nyingine za kisanaa
  • Matumizi ya taswira
  • Matumizi ya ucheshi
 
 Pia kuna Kipengele cha Mandhari hii ni sehemu ambapo matukio muhimu ya kazi ya fasihi hutokea. Mandhari inaweza kuwa ya kubuni au ya kweli. Katika masimulizi mengi ya kihistoria mandhari yake ni ya kweli na kazi za kubuni mandhari yake ni ya kubuni.
Kipengele kingine ni jarada kazi za fasihi huwa na michoro au picha na hata rangi kwenye majarada yake.Inawezekana majarada hayo yakawa na uhusiano na dhamira au maudhui ya kazi zinazohusika.Picha hizi huweza kuwa kielekezi muhimu cha fani kwenye uchambuzi wa kazi ya kifasihi.mfano picha za majarada ya Nyota ya Rehema ya M.S.Mohamed,Kufa Kuzikana ya K.Walibora,Babu alipofufuka ya M.S.Mohamed na Bina-Adamu ya K.W.Wamitila na nyingi nyinginezo Hata hivyo ni muhimu kutambua kuwa sio kazi zote za kifasihi ambazo zinaonesha uwiano kati ya majarada yake na yaliyomo.
 
Vipengele vya maudhui, kipengele cha kwanza ni dhamira.
Dhamira ni wazo kuu au mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi andishi. Dhamira hutokana na jamii. Katika dhamira, kuna dhamira kuu na dhamira ndogo ndogo.
 
Kipengele cha pili ni mtazamo wa mwandishi. Hapa ni hali ya kuyaona mambo katika maisha kwa kuzingatia mazingira aliyonayo msanii mwenyewe. Mtazamo wa msanii unaweza kuwa wa kiyakinifu au wa kidhanifu.
 
Kipengele kingine ni msimamo wa mwandishi ambayo ili  hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani. Jambo hili linaweza kuwa halikubaliki na wengi, lakini yeye atalishikilia tu.
Msimamo wa msanii ndio unaosababisha kazi ya sanaa iwe na  mwelekeo maalum na hata kutofautiana na kazi za wasanii wengine.
Kipengele cha nne ni falsafa ya mwandishi. Ambao huu ni mwelekeo wa imani ya msanii. Msanii anaweza kuamini kwa mfano “Mungu hayupo”.
Maadili na ujumbe ni kipengele kingine cha maudhui.Katika fasihi andishi, ujumbe ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazi Fulani ya fasihi andishi.
 
Mwisho, migogoro, ambayo ni mivutano na misuguano mbalimbali katika kazi ya fasihi. Katika migogoro tunapata migogoro kati ya wahusika ama vikundi vya wahusika, familia zao, matabaka yao n.k. na migogoro hii mara nyingi hujikita katika mahusiano ya jamii. Migogoro yaweza kuwa ya kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa na kinafsia.
18.4 Wahusika katika Fasihi ya Kiswahili
Wahusika ni watu, ama viumbe waliokusudiwa wawakilishe tabia fulani za watu katika kazi za fasihi ..
 Mitazamo mbalimbali juu ya Mhusika ni nani?
Jonathan Culler katika kitabu chake  cha Structural Poetics anasema kuwa uhusika ni kipengele cha msingi katika riwaya, kwani kila tukio lipo ili kumfafanua mhusika na maendeleo yake. Naye Barthes katika kitabu hichohicho anasema kuwa mhusika ni kitu kilichochorwa kwa fikra (maneno) kwa msingi wa vielelezo vya kitamaduni, kwa maana kwamba mhusika wa fasihi ya jamii fulani ataeleweka vizuri na kwa urahisi zaidi na jamii hiyo husika.
Nao Kasper na Wuckel wanasema kuwa mhusika ni picha ambayo huchorwa na fasihi, na ni kiini cha vyote vipya, dhamira na mada za fasihi: Wanaendelea kudai kuwa katika mhusika kuna uwili: kwanza kuna usawiri wa kisanaa na mtu kwa upande mmoja, na sura ya mtu kwa upande mwingine. Yaani, katika mhusika kuna hali ya welekeo binafsi (subject) na uhalisi (object). Aidha, dunia ni ghala ya wahusika wa namna mbalimbali kwa fikra, hisia na utendaji, na hayo ndiyo yanayosababisha maendeleo tofauti.
Aristole akizungumzia mwigo katika utanzu mkuu wa zama zake, yaani tanzia, alisema kuwa mhusika hufunua uadilifu na kuonyesha lipi zuri baya, kwani tanzua tanzia ni mwigo wa watu.
Naye Hegel, alisema kuwa mhusika ni kitovu katika usawiri wa kisanaa, na anapaswa kutazamwa katika utatu huu:
  1. Kama mtu binafsi mkamilifu;
  2. Kama mtu katika upekee;
  3. Kama mtu mwenye tabia maalum iliiliyojijenga ndani yake.
Karl Marx na F rederick Engels, kwa kutumia upembuzi wa kiyakinifu, walikubaliana na Hegel kuhusu umuhimu wa mhusika, isipokuwa utatu wake usiangaliwe katika ombwe, bali katika mazingira yake kama ifuatavyo:
  1. Kama mtu binafsi, kwa sababu ni zao la upekee usioweza kujirudia;
  2. Kama mtu tabaka, kwa sababu ni kiwakilishi cha kijamii kinachosimamia tabaka, au kikundi maalum na maendeleo maalum ya kipindi cha historia;
  3. Kama mtu jamii, kwa sababu ni mtu mwenyewe sifa za mtu na za kijamii.
Sifa mbili ni bayana, kwani hujionyesha kupitia matendeo. Lakini sifa ya tatu ni ya kidhahania, au ya kufikirika.
Kutokana na ufafanuzi huu mhusika, tunaona kuwa wahusika ni watu au viumbe katika kazi ya fasihi waliokusudiwa kuwakilisha tabia za watu katika maisha halisi. Wahusika katika hadithi za mapokeo na baadhi ya hadithi fupi, kwa kawaida huwa ni wanyama, wadudu, mimea, mashetani, miungu, n.k. kama ndio wahusika wakuu. Kitabia, wahusika hawa hugawika katika makundi makubwa ya ubaya na wema. Katika riwaya, hasa zile za mwanzomwanzo (za akina Shaaban Robert, Mathias Mnyampala na Faraji Katalambullah), uundaji wa wahusika uliathiriwa na ule wa hadithi za kimapokeo. Lakini wahusika katika riwaya halisi huwa ni wahusika halisi wanaoendana kwa karibu sana na maisha ya kila siku kwa sura yao, mavazi yao, lugha yao, na hulka yao kwa ujumla. Na kitabia, hawagawanyiki kwa urahisi katika makundi mawili, bali huwa na tabia mchangamano: hawana sifa za uungu na kuwa wazuri moja kwa moja, wala hawana sifa za shetani wakawa wabaya mia kwa mia.
Je, ni jambo gani huwezesha mabadiliko ya mhusika? Sababu ya msingi ni kule kujitokeza kwa wajibu mpya wa fasihi kutoka kipindi kimoja hadi kingine unaotelekezwa na ukweli wa maisha, kwa njia ya mahusiano ya kijamii. Mhusika wa kipindi cha ukoloni hawezi kuwa na wajibu sawa na mhusika wa kipindi cha baada ya Azimio la Arusha; wala kamwe hawezi kuwa sawa na Yule wa baada ya kufia kwa uchumi huria.
AINA ZA WAHUSIKA KATIKA FASIHI
  • Wahusika Wakuu
Hawa ni wale ambao wanajitokeza kila mara katika kazi ya fasihi tangu mwanzo hadi mwisho. Wahusika hawa hubeba kiini cha dhamira kuu na maana ya hadithi yote. Vituko na matendo yote hujengwa kuwahusu ama kutokana nao. Mara nyingi jambo hili limewafanya wahusika wakuu wa kazi za fasihi wawe “midomo” ua wasanii. Wawe vipaza sauti vya Watungaji. Wahusika Wakuu hasa wa riwaya na tamthiliya huchorwa na Wasanii kwa mapana na marefu ya maisha na tabia zao ili kuukamilisha unafsi wao.
  • Wahusika wadogo/wasaidizi
Hawa hujitokeza hapa na pale katika kazi ya fasihi ili kuukamilisha ulimwengu wa kazi hizo. Hawa husaidia kujenga dhamira flani katika kazi ya fasihi, lakini mradi dhamira hiyo ni ndogo, basi hata wahusika hao tutawaita kama ni wadogo. Wakati mwingine husaidia kuijenga dhamira kuu ya kazi ya kazi ya fasihi, lakini, kwa sababu nafasi yao  ni ndogo sana katika kuutoa msaada huo, basi hawa tunawaita wahusika wadogo.
  • Wahusika wajenzi
Hawa ni wahusika ambao wamewekwe ili kuikamilisha dhamira na maudhui fulani, kuwajenga na kuwakamilisha. Wahusika hawa wawili; yaani wahusika wakuu na wahusika wasaidizi.
Wahusika wakuu na wadodo tunaweza kuwaweka katika makundi makuu matatu:
  • Wahusika Bapa
Hawa ni wale wasiobadilika kitabia au kimawazo kulingana na mazingira au matumio ya wakati wanayokutana nayo. Wahusika bapa tunaweza kuwagawanya kwenye makundi mawili:
Wahusika Bapa – Sugu – hawa wanakuwa sugu katika hali zote, kiasi amacho hata tunapowaona mahali pengine hali zao ni zilezile, hawahukumiwa bali wao huhukumu tu, hawashauriwi bali wao  hushauri tu, madikteta, mfano Bwana Msa katika riwaya za  M.S. Abdalla ni mmoja wa wahusika hawa.
 
Wahusika Bapa – Vielelzo – Ni wale ambao pamoja na kutobadilika kwao, wamepewa majina ambayo humfanya msomaji aielewe tabia na matendo yao. Shaaban Robert alikuwa fundi sana katika kuwaumba wahusika wa aina hii, akina Majivuno, Adili, Utubusara n.k. Hapa msanii anatilia mkazo tabia moja inayotawala, kiasi ambacho anaondoa sehemu nyingine zote za sifa za mhusika huyo.
  • Wahusika Duara/Mviringo
Hawa ni wahusika ambao wana desturi ya kubadilika kitabia, mawazo au kisaikolojia. Maisha yao yanatawaliwa na hali halisi za maisha. Hivyo wanavutia zaidi kisanii, kwani wanasogeza hadithi ielekee kwenye hali ya kutendeka au kukubalika na jamii. Mfano ni: Rose (Rosa Mistika), Josina (Pepo ya Mabwege).
  • Wahusika Shinda/Wafoili
Hawa wako katikati ya Wahusika bapa na wahusika duara. Hawakuja kama wahusika duara, lakini ni hai zaidi kuliko wahusika bapa. Tofauti kubwa kati ya wao na wahusika wengine ni kwamba wahusika shinda wanawategemea wahusika duara au wahusika bapa zaidi ili waweze kujengeka. Wanaendeshwa na mawazo ya wahusika wengine. Kwa mfano, katika riwaya za M.S. Abdalla, Najum ni mhusika shinda.]]>

<![CDATA[ODC : MUHADHARA WA KUMI NA TISA: UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1805 Sat, 25 Dec 2021 11:26:54 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1805 ODC : MUHADHARA WA KUMI NA TISA: UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI
19.1 Utangulizi
19.2 Mhakiki ni nani?
Mhakiki ni mchambuzi na mfafanuzi wa maandishi ya sanaa hasa yale ya kifasihi. Ni jicho la jamii kwa vile katika kazi za fasihi anagundua mazuri pamoja na hatari iliyomo. Huyu ni bingwa wa kusoma na kuchambua maudhui, maadili na ujumbe uliomo katika maandishi ya fasihi.
19.3 Sifa za Mhakiki
Mhakiki anatakiwa ajue historian ya mazingira yaliyomkuza mwandishi. Mhakiki ili aweze kuifanya kazi yake anapaswa aelewe vema historia ya mwandishi na jamii yake inayohusika. Aelewe asili ya mwandishi, historia yake na utamaduni wake kwa ujumla. Kutokana na hali hii, mhakiki anaweza kuelewa kama mwandishi amefanikiwa kueleza ukweli wa maisha ya watu yaani jamii inayohusika.
Mhakiki anatakiwa kuelewa histori na siasa ya jamii inayohusika. Hii itamwezesha kuyaelewa matatizo ya jamii hiyo. Mhakiki lazima aifahamu barabara jumuiya ambayo mwandishi aliandika juu yake ili aweze kuandika uhakiki imara, ama sivyo atakwama na kuandika uhakiki dhaifu. Mhakiki anapaswa kuelewa historia ya watu ambao maandishi yao hayo yanawahusu, bila kuifahamu historia yao, itakuwa vigumu kwake kueleza bayana baadhi ya mambo ambayo mwandishi aliandika na kwa nini aliandika hivyo. Uhakiki wake ukisomwa na watu wanaoishi katika jamii hiyo si ajabu kusema yeye si mhakiki. Mhakiki, huangalia jinsi gani mwandishi ameiwakilisha hali halisi ya jumuiya na historia ya watu hao.
Mhakiki ni muhimu awe amesoma kazi mbalimbali za fasihi na siyo ile tu anayoifanyia uhakiki. Hii itamsaidia kuwa na ujuzi zaidi katika uwanja wa uhakiki.
Mhakiki anatakiwa asome tabakiki za wahakiki wengine katika uwanja wa fasihi na hata nje ya jamii yake ili kupata upanuzi zaidi katika kazi ya uhakiki. Hii itamsaidia kutoa tahakiki bora zaidi kwani atakuwa amejifunza yale yaliyo mazuri na kuepuka makosa waliyofanya wengine.
Mhakiki lazima awe na akili pevu sana ili aweze kung’amua mambo na akishayang’amua ayaandike kwa lugha rahisi ili mawazo yake yasomeke na kila mtu kwa urahisi, yaani atumie lugha ambayo itawatumika wasomaji wake.
 
Mhakiki lazima ajiendeleze katika taaluma mbalimbali ili aweze  kuwa na mawazo mengi ambayo yatamsaidia kuhakiki maandishi mbalimbali.Mhakiki hodari huichonga jamii yake kimawazo. Huiimarisha isitetereshwe au kupofushwa na waandishi wapotoshi.
 
Mhakiki anapaswa kuwa na uwezo wa kuchambua mambo kisayansi bila kutonesha hisia za wasomaji. Asiwe na majivuno na awaheshimu anaowahakiki na anaotaka wasome uhakiki wake, asichukie au kusifia tu kazi za waandishi kwa sababu zake binafsi bila kueleza ukweli wa kazi hiyo. Mhakiki ni rafiki wa mwandishi na wasomaji. Kwa hiyo, mhakiki lazima awe fudi katika kutoa hoja zake na lazima ziwe zinagonga, zenye kuibua udadisi na kuathiri.
Mhakiki anapaswa asiwe mtu wa kuyumbishwa na maandishi au maeneo ya wahakiki au watu wengine. Tunategemea asme kweli kuhusu kazi hiyo. Mahusiano baina ya mhakiki na mwandishi yasiathiri uhakiki wake.
Mhakiki anapaswa awe na uwezo wa kutumia mkabala sahihi kulingana na kazi anayoifanyia uhakiki. Mikabala humwongoza mhakiki kuchambua vema kazi za fasihi.
19.4 Dhima za Mhakiki
 
Kuchambua na kuweka wazi funzo linalotolewa na kazi ya fasihi. Hapa mhakiki anatoa ufafanuzi wa kimaudhui wa kazi ya  fasihi. Mhakiki husoma kwa uangalifu kazi ya fasihi, baada ya kusoma kwa makini, hutafakari na kuchunguza maudhui, Maadili , na ujumbe ambao mwandishi amekusudia kuwafikishia wasomaji wake na jamii inayohusika.
Kuchambua na kufafanua picha za kisanii zilizotumika katika kazi ya fasihi. Mhakiki huwasaidia wasomaji ili wasishindwe kuyaelewa maudhui barabara kutokana na kukakanganywa na usanii, matumizi, mathalani ya Ishara na baadhi ya mbinu ambazo zinaweza kumkanganya msomaji ambaye hajapata utaalamu mkubwa wa kuchambua. Mhakiki kwa kufichua ishara Fulani ina maana kuwa amemsaida msomaji kupata ujumbe kikamilifu.
Kuhusu matumizi ya picha, kwa kawaida, lugha ya picha ina mguso sana na huibua hisia aina na hata kuchekesha au kuwafanya watu walie machozi. Mhakiki sharti awambie kwamba, matumizi ya picha ni mbunu mojawapo inayosaidia maudhui kuwaganda wasomaji. Picha inayochekesha, kufurahisha, kukejeli n.k. haikomei pale tu kwani baada ya kucheka n.k. msomaji huathiriwa sana kinafsia na aghalabu huachiwa funzo fulani. Hivyo mhakiki lazima achambue na kuiweka wazi funzo ambalo linatolewa na picha hiyo.
Mhakiki ana dhima ya kumshauri mwandishi ili afanye kazi bora zaidi. Mhakiki anamfundisha mwandishi juu ya yale anayoyasema yanavyoweza kupokelewa na jamii. Humwonesha msanii uzuri na udhaifu wa kazi aliyosaini kitendo hiki humfanya anavyoelekezwa na mhakiki, na hivyo humfanya awe na nafasi nzuri ya kuirekebisha kazi hiyo atakapoishulikia kazi nyingine. Kwa msingi huo mhakiki anaweza kulaumu au kusifu/ kumpongeza mwandishi wa kazi yoyoe ya kisanaa.
 
Mhakiki ana dhima ya kumwelekeza msomaji ili apate faida zaidi kuliko yale ambayo angeweza kuyapata bila dira ya mhakiki. Mhakiki huifunza jamii (wasomaji) namna ya kupokea na kuifurahia kazi ya sanaa. Vilevile mhakiki huwasaidia wasomaji kuyabaini maandishi yaliyo sumu kwa jamii. Mhakiki lazima ayafichue maandishi hayo ili yasieneze sumu kwa jamii inayohusika.
 
Mhakiki ni kiungo muhimu kati ya jamii na msanii. Mhakiki ndiye anayeitambulisha na kuelezea kazi ya msanii kwa hadhira. Vile vile mhakiki huchukua mawazo ya wasomaji na kuyapeleka kwa mwandishi. Humtahadharisha msanii kuhusu makosa aliyoyafanya katika kuikabili kazi yake na wakati huo huo anaionesha jamii udhaifu uliomo katika kazi hiyo ya fasihi.
Mhakiki ana dhima ya kukuza kiwango cha utunzi na usomaji wa kazi ya fasihi. Kutokana na ushauri anaoupata mwandishi kutoka kwa mhakiki, humfanya awe makini zaidi wakati wa kushughulikia kazi nyingine. Vile vile wasomaji wanakuza kiwango chao cha usomaji kwa kufuata mawaida ya mhakiki.
Mhakiki ana dhima ya kusema wazi kuhusu kiwango cha maandishi anayoyahakiki.Akisema wazi kwamba maandishi hayo yako katika kiwango cha chini, mara mwandishi huyo asilia atakapoamua kutunga tena, atashawishika kuandika maandishi yaliyo kwenye kiwango cha juu zaidi. Na waandishi wengine watapatiwa msukumo wa kuandika maandishi yaliyo kwenye kiwango cha juu pia. Na hivi ndivyo mhakiki anavyosaidia kukuza na kuendeleza maandishi ya taifa lake.
Mhakiki ana dhima ya kumsaidia msomaji kuyabaini maandishi yaliyosumu kwa jamii. Mhakiki sharti aseme wazi ayafichue maandishi ya namna hiyo. Kuna maandishi ambayo huwachekesha na kuwaburudisha wasomaji sababu yameandikwa kwa namna hiyo, na kumbe yaneneza sumu, na maandishi haya yanazorotesha maendeleo ya jamii, hivyo mhakiki huyafichua maandishi kama haya.
 
Mwisho, mhakiki anatakiwa kuheshimu na kuthamini kazi za waandishi na kuzifanyia haki. Jambo la msingi (lazima) kuzingatia ni kwa mhakiki afayapo kazi yake huwa vitani. Mhakiki anapaswa kujua namna ya kuwanasa wasomaji bila wao kujitambua na kuwa na uwezo au kuchambua kisayansi mambo bila kutonesha hisia za wasomaji. Anatakiwa asiwe na majivuno na aheshimu anaowahakiki na anaowataka wasome uhakiki wake, awachukue hatu kwa hatua kifalsafa hata waone vigumu, na haiwezekani kupingana naye.
 
Kwa kuhitimisha, mhakiki ni mtu muhimu sana katika kazi za fasihi. Kazi ya sanaa ya uandishi ni kama chakula kilichokwishapikwa na kuungwa vizuri. Uhakiki ni sehemu mbalimbali za ulimi zenye kuifanya jamii ikubali utamu wa chakula hicho; uchungu au ukali wa chakula hicho na igundue uchungu wa chakula hicho au ukali wake.
19.5  Uhakiki wa Fasihi
Nkwera (2003) amechunguza na kuona kwamba mara nyingine mhakiki hulazimika kulinganisha kazi za kifasihi. Kazi hizo zinaweza kuwa zinafanana au zinatofautiana. Ulinganisho huo utazingatia vipengele vyote vya fani na maudhui. Mhakiki anatazamiwa aone ubora au upungufu katika kazi na jinsi zinavyozidiana.
Vigezo vinavyotumiwa katika kulinganisha kazi za fasihi ni vile vile vya ukweli, uhalisi na umuhimu. Vigezo hivyo vitapima dhamira, ujumbe, falsafa, wahusika na matumizi ya lugha.
Uhakiki wa kazi za fasihi unajumuisha kuzingatia kazi hiyo kwa kuisikiliza au kuisoma; kuchambua vipengele vya fani na maudhui vinavyoijenga kazi hiyo. Hatimaye mhakiki atatoa maoni kuhusu ubora au ubaya wa kazi hiyo na hukumu ya kazi ipi bora kuliko nyingine.
VIPENGELE VYA UHAKIKI  1. MAUDHUI
  1. FANI
    • Uhakiki wa Maudhui
 
            Katika kuyahakiki maudhui ya fasihi, zingatia yafuatayo:
(i) Soma na uielewe habari nzima, kisha uieleze kwa muhtasari.
(ii) Itambulishe hadhira au wazo kuu la mchezo husika kwa sentensi mbili au tatu.
(iii)Onesha mapendekezo au mawaidha ya mwandishi, msimamo na mtizamo wake wa mambo kutokana na mchezo huo.
(iv) Chunguza falsafa ya maisha ambayo mwandishi anaielezea: k.m. Je, mwandishi anaelezea hali halisi ya maisha au ni nadharia tu za uchawi au ni maisha ya njozi yasiyo na ukweli ndani yake?, nk.
(v) Ainisha matatizo na migogoro inayojitokeza katika mchezo huo na sababu zake.
(vi) Mtambulishe mhusika mkuu katika mchezo mzima.
(vii) Onesha njia/mbinu zilizotumika ili kumuinua au kumuangusha mhusika mkuu.
(viii)Onesha njia/mbinu zilizotumika ili kuyakabili na kuyatatua matatizo hayo na migogoro iliyojitokeza katika mchezo huo.
(ix)Onesha majibu/matokeo ya juhudi zote alizotumia mwandishi ili kulikabili suala au tatizo linalozungumziwa katika mchezo huo.
(x)Fanya tathmini ya kupima kama mwandishi amefanikiwa, katika maelezo yake, kulifikisha lengo alilokusudia kwa hadhira lengwa.
(xi)Na kama hakufanikiwa kulifikisha lengo lake kwa hadhira husika, eleza kwa nini kashindwa.
19.5.2  Uhakiki wa Fani: Wahusika
Uhakiki wa Fani Wahusika unatakiwa ushughulikiwe kwa kuzingatia na kuchunguza mambo mawili makubwa:
  • Wahusika
Yuko mhusika mkuu au wako wahusika wakuu.
Mhusika mkuu au wahusika wakuu hutambulishwa kwa maswali matatu:
(a)Hadithi imejengwa juu ya nini?
(b) Je, mhusika huyo hutokea mara nyingi akitenda mambo, kuongea au kuzungumziwa na wahusika wenzake?
 © Je, mhusika anatoa uamuzi unaofikisha mchezo kwenye kilele au upeo wa weledi wa hadhira yake?
Wahusika wadogo nao huunda makundi matatu:
(a)  Wahusika wadogo walio maarufu au muhimu.
(b) Wahusika wadogo walio maarufu kidogo.
©Wahusika-Wadogo wanaofanya mazingira katika mchezo   ambayo yanamsukuma Mhusika-Mkuu aamue au asiamue jambo kama alivyokusudia hapo awali.
Jinsi wahusika walivyoundwa na kulelewa mambo muhimu ya kuchunguza katika kipengele hiki ni:
 (a) Sura, tabia, kazi zao maishani katika jamii, na katika mchezo.
 (b) Uhusiano wao katika Jamii:
  • Je, wanaendelezana kimaisha, au kila mmoja kivyake?
  • Je, wanagongana kitabaka, kifikra, kiuchumi, kielimu, nk?
  • Je, wanasadikika na kupokeleka na jamii yao, au na hadhira kwa jumla?
19.5.3    Uhakiki wa Fani: Muundo
Kipengele hiki kinachunguza jinsi mchezo wenyewe ulivyotengenezwa. Maswali ya kujiuliza ni haya:
(a) Mwanzo wa mchezo ni wapi na unakomea wapi?
(b) Kilele cha mchezo ki wapi; kimeanzia na kuishia wapi?
© Sehemu za mchezo ni zipi? Yaani mchezo una vitendo vingapi (sehemu ngapi) na maonesho mangapi?
(d)Ni mandhari gani yaani sura ya mahali na mzingira ya wakati yanasawiriwa katika mchezo?
19.5.4  Uhakiki wa Sanaa: Kufaulu Kwa Mtunzi
Uamuzi wa kwamba mtunzi amefaulu ama hakufaulu katika utunzi wa mchezo wake, hatuna budi kuchunguza au kujiuliza mambo yafuatayo kuhusu sanaa aliyoitumia katika mchezo wake.
(a) Je, lugha aliyoitumia mwandishi ni fasaha, (yaani ni lugha sahihi kisarufi, na ni rahisi kueleweka kwa watu wengi waliokusudiwa wauelewe mchezo wake?
(b) Je, viashiria au ishara na mifano iliyotumika ili kulijenga wazo kuu; kuunda visa, mazingira ya wakati na mahali; kubainisha ukale dhidi ya usasa (mapinduzi); nk. yamechangia kufanikisha azma ya mchezo?
© Je, ukubwa wa hadhira au jamii inayoweza kufikiwa na ujumbe wa mchezo na ikauelewa fika na kuathirika nao vibaya au vizuri, unaridhisha?
 (d) Je, maudhui yatokanayo na mchezo huu yanatoa jawabu au suluhisho la kufaa kuhusu migogoro inayojitokeza katika jamii hiyo?  Je, yanachochea zaidi vurugu akilini  kuhusu mgogoro uliopo?
(e) Je, semi zimetumiwa katika mchezo ili kusisitiza au kukejeli mambo yanayosadikiwa na kufuatwa kama kanuni au desturi katika jamii?
(f) Je, suala linalojadiliwa linawagusa watu wa kiwango gani kielimu katika jamii hiyo?
(g) Je, suala la wachache katika jamii, yaani ni tabaka dogo tu la watu?
(h) Je, suala la watu wengi katika jamii, yaani ni tabaka kubwa la watu?
(i)  Je, suala la watu wote katika jamii?
(j)  Je, suala linalojadiliwa lina umuhimu gani kwa jamii kwa wakati huu?
(k) Je, mwandishi amewatumia wahusika wake ipasavyo katika kuliweka bayana wazo kuu kwa hadhira husika, na uwe mfano bora kwa hadhira kuwaiga au kutowaiga kwa vile alivyowamulikia kwa undani maisha yao kwa vitendo na maneno yasemwayo mchezoni?
19.5.5 Uhakiki wa Kichwa cha Mchezo
Kichwa cha mchezo ni kama nembo. Kwa hiyo, nacho pia inafaa kihakikiwe. Maswali ya kujiuliza kuihusu ni kama ifuatavyo:
(a)   Je, kichwa kilichowekwa kweli kinawakilisha wazo kuu, au
         kiini cha habari?
(b) Je, ni wazo mojawapo tu linalojitokeza katika mchezo huu katika jumla ya mawazo?  au
© Ni neno tu la kuamsha udadisi wa msomaji na labda la kuwavutia wanunuzi wa kitabu chake?

]]>
ODC : MUHADHARA WA KUMI NA TISA: UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI

<![CDATA[ODC: MADA YA 2: FONETIKI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1598 Sun, 28 Nov 2021 07:59:31 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1598 ODC:  MADA YA 2: FONETIKI
5.1 UTANGULIZI
5.2  Maana Ya Fonetiki
Hyman (1975) kama alivyonukuliwa na Method (2009) anaeleza kuwa fonetiki ni taaluma ambayo hususani huchunguza sauti ambazo hutumiwa na wanadamu wakati wanapowasiliana kwa kutumia lugha. Anaendelea kueleza kuwa uchunguzi wa kifonetiki huwa hauhusishwi na lugha yoyote maalumu na kutokana na hali hiyo kipashio cha msingi cha fonetiki ni foni. Hyman anaendelea kwa kueleza kuwa foni ni kipande kidogo kabisa cha sauti kisichohusishwa na lugha yoyote.
Naye Massamba na wenzake (2004) wanaeleza kuwa fonetiki ni tawi ambalo hujishughulisha na uchambuzi wa taratibu zote zinazohusiana na utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikiaji na ufasili wa sauti za lugha za binadamu kwa ujumla. Kinachozingatiwa hapa ni kuchunguza maumbo mbalimbali ya sauti zinazoweza kutolewa na ala sauti, namna ambavyo maumbo hayo yanavyoweza kutolewa, yanavyoweza kumfikia msikilizaji (yaani yanavyosikika) na yanavyofasiliwa na ubongo; bila kujali sauti hizo zinatumika katika lugha gani.
Kwa kusikiliza sauti wanafonetiki wanaweza kuzipanga sauti hizo katika makundi na kuzitolea sifa zinazotofautisha sauti moja na nyingine.
Madhumuni ya Muhadhara
Baada ya kusoma huhadhara huu utaweza:
(i)     Kueleza kwa ufasaha maana ya fonetiki.
(ii)    Kufafaua matawi ya fonetiki
(iii)  Kueleza makundi makuu ya sauti za lugha yaani: irabu na konsonanti.
(iv)  Kufafanua kwa ufasaha sifa bainifu za irabu na konsonanti.
5.3  Matawi ya Fonetiki
Fonetiki ina matawi kadhaa kama ifuatavyo:
i. Fonetiki Matamshi
ii.  FonetikiAkustika
iii . Fonetiki Masikilizi/Masikizi
iv. Fonetiki Tiba matamshi.
Fonetiki Matamshi. Massamba na wenzake (2004) wanaeleza fonetiki matamshi kuwa ni tawi linalojishughulisha na jinsi sauti mbalimbali zinavyotamkwa kwa kutumia zile ala sauti. Kinachoangaliwa hapa ni jinsi ya utamkaji wa sauti hizo (kama sauti ni kikwamizi), mahali pa matamshi (kama sauti hizo ni midomo) na hali ya mkondo hewa (kama ni ghuna au si ghuna).
Fonetiki Akustika. Tawi hili la fonetiki huchunguza jinsi mawimbi sauti yanavyosafiri kutoka katika kinywa cha msemaji hadi kufikia sikio la msikilizaji.
Fonetiki Masikizi. Ni tawi la fonetiki linaloshughulikia jinsi mawimbi sauti yanavyoingia katika sikio la msikilizaji na kutafsiriwa na ubongo wake hata kupata maana. Method (2009).
Fonetiki Tiba matamshi. Tawi hili kama linavyoitwa na Massamba (2004) pia linaitwa na Mgullu (1999) kuwa ni fonetiki majaribio na linajishughulisha na matatizo yanayoambatana na usemaji na jinsi ya kuyatatua. Tawi hili ni jipya zaidi na limeibuka hivi karibuni.
Kwa minajili ya kozi hii tutajikita zaidi kwenye fonetiki matamshi.
Fonetiki Matamshi
Fonetiki matamshi kama ilivyoelezewa hapo awali kuwa ni tawi linaloshughulikia jinsi sauti zinavyotolewa na ala sauti. Swali la msingi ala sauti ni nini? Na ni zipi?
Ala sauti ni viungo vya mwili wa binadamu vinavyotumika kumwezesha binadamu kutoa sauti. Viungo hivi pia vina kazi nyingine za kibiolojia. Kwa mfano:
  • Mapafu – hupeleka hewa kwenye damu katika koromeo
  • Nyuzi sauti –hufunga koo wakati wa kula hivyo huzuia chakula kisipite kwenye viribahewa.
  • Ulimi – kuonja
  • Meno – kutafuna
Viungo vifuatavyo ni ala za sauti zinazoshiriki utoaji wa sauti: meno, ufizi, kaa kaa gumu, kaa kaa laini, kidaka tonge/uvula, pua, ncha ya ulimi, pembeni, nyuma, shina la ulimi, koromeo, chemba cha pua, chemba cha kinywa, nyuzi sauti.
Makundi ya ala sauti.
i. Ala Sogezi. Hizi ni vile viungo vya binadamu ambavyo hujisogezasogeza wakati wa utamkaji wa sauti. Ala hizi ni pamoja na midomo, ulimi  n.k
ii. Ala Tuli.  Ala hizi huwa hazisogei wakati wa utamkaji. Zipo kinyume na ala sogezi. Mfano wa ala tuli ni kaa kaa gumu, kaa kaa laini n.k
Meno. Ni ala tuli ambayo hutumika kutamka sauti kadhaa za lugha. Hewa huweza kuzuiwa kati ya meno na kuachiwa na hivyo kutoa sauti Fulani. Kwa mfano: f, v, /s/, /z/ n.k
Midomo. Kwa kawaida binadamu ana midomo miwili. Mdomo wa juu na mdomo wa chini, na midomo hii ni ala sogezi. Ina jukumu kubwa katika utamkaji. Baadhi ya sauti za midomo ni /b/, /p/, /m/ n.k
Ufizi. Ala tuli.Hizi ni ala ambazo zinashikilia meno ya juu nay a chini. Baadhi ya sauti za ufizi ni /n/, /t/, /d/, /s/ n.k
Kaa kaa gumu. Ala sauti hii hupakana na ufizi. Mfano wa sauti za kaa kaa gumu ni: ch, y n.k
Kaa kaa laini. Sehemu hii huanza mara baada ya kaa kaa gumu. Mfano wa sauti za kaa kaa laini ni:k, g, ny, kh, ng’ n.k
Ulimi. Ni ala sauti muhimu sana kwani husaidia utamkwaji wa sauti nyingi sana. Irabu zote hutegemea ala hii katika utamkaji wake. Mfano wa irabu ni: a, e, i, o, u. ulimi umegawanyika katika sehemu kuu tatu.
  1. Ncha ya ulimi. Hutamka vitamkwa mbalimbali kama vile n, t, d.
  2. Sehemu ya kati. Hutamka vitamkwa kama ch, j.
  3. Sehemu ya nyuma. Huenda juu au chini, mbele au nyuma katika kutamka sauti mbalimbali. Kusogea huko kwa sehemu ya nyuma ya ulimi huathiri umbo la chemba cha kinywa.
Nyuzi sauti.Ni misuli miwili yenye uwezo wa kunyambulishwa ambayo huwepo kwenye koromeo. Nyuzi sauti zina mchango mkubwa sana katika katika utoaji wa sauti. Nyuzi sauti zinapotikiswa hutoa mghuno na hivyo hutoa sauti ziitwazo ghuna, kwa mfano b, g, d n.k. Nyuzi sauti zisipotikiswa hazitoi mghuno hivyo hutoa sauti ziitwazo si ghuna. Mfano: p, k, t n.k
Chemba ya pua. Hii hutoa sauti ziitwazo nazali. Wakati wa utamkaji wa sauti hizo hewa hupitia katika chemba ya pua. Mfano wa nazali m, n, ny n.k
Glota. Ni uwazi uliopo kati ya nyuzi sauti. Uwazi huu hubadilikabadilika kutegemeana na kinachotamkwa. Sauti ya glota ni h.
5.4 Uainishaji wa Sauti
Makundi makuu ya sauti za lugha ni: irabu na konsonanti.
5.4.1   Irabu
Ni sauti za lugha ambazo wakati wa kutamkwa hewa haizuiwi wala kuzibwa mahali popote, hewa hupita kwa urahisi bila kizuizi chochote.
Tofauti kati ya irabu na konsonanti ipo katika utamkaji.
Irabu huainishwa kwa kutumia vigezo vitatu: mahali pa kutamkia, mwinuko wa ulimi na hali ya mdomo.
Mahali pa kutamkia
Irabu huweza kutamkwa katika sehemu tatu za ulimi: sehemu ya mbele ya ulimi, sehemu ya kati ya ulimi na sehemu ya nyuma ya ulimi.
Mfano:
–        ,[e]- Hutamkiwa sehemu ya mbele ya ulimi hivyo huitwa – Irabu za mbele
–        [u],[o]- Hutamkiwa  sehemu ya nyuma ya ulimi hivyo huitwa – Irabu za nyuma
–        [a] – Hutamkiwa sehemu ya kati ya ulimi hivyo huitwa –Irabu ya kati
Mwinuko wa ulimi
Wakati wa utamkaji wa irabu ulimi huwa juu, kati au chini. Ulimi huwa umenyanyuka au umeshuka.
Irabu zimegawiwa katika makundi matatu (3). Nayo ni haya yafuatayo :
i. na [u]- Ulimi umenyanyuka juu.
ii. [e] na [o]- Ulimi umeinuka mpaka katikati.
iii. [a]- Ulimi ukiwa chini kabisa.
Hali ya mdomo
Wakati wa utamkaji mdomo unaweza kuwa umeviringwa au haukuviringwa. Tunapata irabu viringo na irabu si viringo. Irabu viringo ni [o] na [u]. irabu si viringo ni , [e] na [a]
Uainishaji wa Irabu
– irabu ya mbele, juu, si viringo.
[e] – irabu ya mbele kati, si viringo.
[a] – irabu ya kati, chini, si viringo.
[u] – irabu ya nyuma, juu, viringo
[o] – irabu ya nyuma, kati, viringo.
5.4.2  Konsonanti
Konsonanti ni aina ya sauti katika lugha ambazo wakati wa utamkaji wake mkondo wa hewa huzuiwa katika sehemu mbalimbali kinywani. Wakati mwingine hewa huzuiwa kabisa, wakati mwingine hewa huzuiwa kiasi mahali fulani baada ya kupita kongomeo. Mfano wa konsonanti ni [p], [g], na [h].
Ili uweze kuzitambua konsonanti ni lazima ufahamu sifa bainifu za konsonanti. Zifuatazo ni sifa maalumu za utambuzi wa konsonanti :
i. Namna ya utamkaji
ii. Mahali pa kutamkia
iii. Ghuna au si ghuna
Namna ya Utamkaji
Kigezo cha kwanza cha kuainishia konsonanti ni namna ya utamkaji. Katika namna ya utamkaji tunarejelea jinsi ambavyo mkondo hewa unavyozuiwa katika sehemu mbalimbali za bomba la sauti wakati wa kutoa sauti za lugha.
Kama tulivyotaja hapo awali mkondohewa unaotoka mapafuni huweza kuzuiwa na vizingiti vya ala sauti kwa namna tatu kimsingi :
  1. Mkondohewa unaweza kuzuiwa kabisa.
  2. Mkondohewa unaweza kuruhusiwa upite katika mwanya mdogo kwa shida.
  3. Mkondohewa unaweza kuruhusiwa upite bila kuzuiwa.
Kwa kutumia hali hizi za mkondohewa, konsonanti huainishwa katika makundi yafuatayo :
  1. Vipasuo/ Vizuiwa
  2. Vipasuo – kwamiza
  3. Vikwamizi/Vikwamizwa
  4. Nazali
  5. Vitambaza
  6. Vimadende
  1. Vipasuo/Vizuiwa
Ni konsonanti ambazo wakati wa utamkaji wake mkondohewa kutoka mapafuni hubanwa kabisa wakati wa kutamkiwa kisha huachiwa ghafla.
Sauti hizi zimeitwa vipasuo kutokana na kuachiwa ghafla kwa mkondohewa. Sauti zitokeazo zina mlio wa kupasua. Ifuatayo ni mifano ya vipasuo :
  • Vipasuo vya midomoni : [p], , [m].
  • Vipasuo vya ufizi: [t], [d], [n].
  • Vipasuo vya kaakaa gumu : …….
  • Vipasuo vya kaa kaa laini : [k], [g], [ ]
  1. Vipasuo – kwamiza

[*]Ni konsonanti ambazo wakati wa utamkaji wake ala sauti huwa zimefungwa kabisa  na kasha kuachiliwa hewa ipite ghafla kwa mlipuko  lakini ala sauti haziachani kabisa; huacha mwanya mdogo na kuruhusu mkondo hewa kupita kwa shida kati yao na kusababisha sauti inayotoka kuwa mkwaruzo. Mifano ya vipasuo- kwamiza ni:
  • Vipasuo-kwamiza vya ufizi: [ts],[dz].
  • Vipasuo-kwamiza vya kaakaa gumu: [t ], [d ]
  1. Vikwamizi
[*]

[*]Sauti hizi hutamkwa wakati ala sauti zinapokaribiana na kupunguza upenyo wa bomba la sauti kiasi cha kufanya hewa ipite kwa shida na hivyo kusababisha mkwaruzo. Sauti za vikwamizi zaweza kutamkwa mahali popote kwenye bomba la sauti.
[*][*]

[*] 
[*][*][*]

[*]Weka picha kutoka Habwe J(2004 :34)
[*][*][*][*]

[*] 
  1. Nazali
[*][*][*][*][*]

[*]Ni sauti ambazo hutamkwa kwa kuruhusu mkondo hewa kupitia kwenye chemba cha pua. Mifano ya sauti nazali ni:
  • Nazali yam domo: [m].
  • Nazali ya ufizi: [n].
  • Nazali ya kaakaa gumu: [  ]
  • Nazali ya kaakaa laini: [  ]
  1. Vitambaza
[*][*][*][*][*][*]

[*]Ni sauti ambazo wakati wa kutamka ulimi hutandazwa na kuruhusu hewa ipite pembeni ya ulimi bila mkwaruzo mkubwa sana. Mfano wa kitambaza ni [l].
  1. Vimadende
[*][*][*][*][*][*][*]

[*]Ni sauti ambayo wakati wa utamkaji wa sauti ncha ya ulimi inakuwa imegusa ufizi lakini kutokana na nguvu ya mkondo hewa inayopita kati ya ulimi na ufizi, ncha ya ulimi hupigapiga kwa haraka haraka kwenye ufizi. Mfano wa kimadende ni [r].
[*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Mahali pa kutamkia
[*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Kigezo cha pili cha kuainisha konsonanti ni mahali pa kutamkia. Wakati wa utamkaji ala sogezi na ala tuli hukaribiana na kugusana. Mara nyingi huwa kuna ala sogezi ambayo husogea kuelekea kwa ala tuli ingawa kuna hali ambayo ala sogezi mbili huhusika. Kwa mfano mdomo wa juu unahusiana na wa chini katika kutoa sauti.
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Konsonanti hugawanywa katika makundi makuu saba.
  1. Midomo
  2. Midomo na meno
  3. Meno
  4. Ufizi
  5. Kaakaa gumu
  6. Kaakaa laini
  7. Koromeo
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Midomo
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Konsonanti zinazotamkwa kwenye midomo huhusisha utatizwaji wa hewa katika midomo yote miwili. Mdomo wa chini huelekeana na ule wa juu. Hapa midomo yote miwili huwa ni ala sogezi. Sauti zitolewazo kwenye midomo ni [m], [p] na .
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Midomo na Meno
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Sauti zitamkiwazo hapa huhusisha mdomo wa chini na meno ya juu. Hapa mdomo wa chini huwa ala sogezi na husogea kuelekea meno ya ju ambayo ni ala tuli. Mfano wa sauti hizo ni [f], [v].
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Meno 
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Sauti za meno hutamkwa kwa ncha ya ulimi ikiwekwa katikati ya meno ya juu na ya chini. Mfano wa sauti hizo ni: [  ], [   ]
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Ufizi
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Sauti za ufizi huhusisha bapa la ulimi kama ala sogezi na mwinuko wa ufizi ulio nyuma ya meno ya juu ukiwa ndio ala tuli. Mifano ya sauti za ufizi ni: [t], [d], [n], [r], [l], [s] na [z].
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Kaakaa gumu
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Sauti za hapa hutamkwa kwa kuhusisha bapa la ulimi na kaakaa gumu. Mfano wa sauti hizo ni : [ch], [j], [sh], na [ny].
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Kaakaa Laini
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Sauti za hapa hutamkwa kwa kutumia sehemu ya nyuma ya ulimi ambayo hugusana au kukaribiana na kaakaa laini. Mfano :  [k], [g], [gh] na [ng].
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Koromeo
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Sauti ya koromeo hutamkiwa kwenye tundu la glota. Mfano wa sauti hiyo ni [h].
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Muhimu
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Kuna sauti ambazo siyo konsonanti wa irabu huitwa viyeyusho/ nusu irabu. Mfano [w] na [y].
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*][w]
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]–        Mahali pa kutamkia ni kwenye mdomo
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]–        Namna ya utamkaji mdomo huvirigwa wakati wa utamkaji wake.
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*][y]
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]–        Mahali pa kutamkia  ni kwenye kaakaa gumu
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]–        Namna ya utamkaji, kutandaza midomo na sehemu ya kati ya ulimi hukaribiana na kaakaa gumu.
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Jedwali la namna ya utamkaji na mahali pa kutamkia
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Ghuna au si ghuna
[*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*][*]

[*]Sauti ghuna ni sauti ambazo wakati wa utamkaji wake nyuzi sauti hurindima au kutetema. Sauti ghuna pia huitwa sauti za kandamsepetuko.

[*]Sauti ambazo si ghuna hazina mrindimo wa nyuzi sauti wakati wa utamkaji wake. Sauti si ghuna pia huitwa sauti za kandatuli au sauti hafifu. Mifano ya sauti ghuna ni : [ b, d, g, v, dh, z] na nazali. Mfano wa sauti si ghuna : [p, t, k, f, s]]]>
ODC:  MADA YA 2: FONETIKI

<![CDATA[ODC : MHADHARA WA TISA: Mawanda ya Sintaksia]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1597 Sun, 28 Nov 2021 07:47:13 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1597 Muhadhara 9:
MHADHARA WA TISA: Mawanda ya Sintaksia
9 .1  Utangulizi
Katika taaluma inayochunguza lugha, ambayo hujulikana kama isimu, lugha hugawanywa katika Nyanja kuu nne ambazo ni fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki. Hivyo, sintaksia ni nyanja mojawapo ya isimu ya lugha. Sintaksia ni nini?
9.2  Fasili ya Sintaksia
Kwa mujibu wa Harper (2001-2010) Online Etymology Dictionary, neno sintaksia liliibuka takribani miaka ya 1600 na linatokana na neno la Kifaransa syntaxé au la Kilatini au Kigiriki syntaxis ambalo maana yake ni kupanga au kuweka vitu pamoja katika mpango. Hata hivyo, wataalamu wengi wa masuala ya sintaksia wanakubaliana kuwa neno hili lina asili ya Kigiriki kwa kuwa Wagiriki ndio wakongwe katika taaluma mbalimbali hapa duniani, ikiwa ni pamoja na taaluma ya lugha. Hata hivyo historia ya isimu inaonesha kuwa, uchunguzi wa kwanza wa lugha ulianza na Wamisri mnamo karne ya 5 Kabla ya Kuzaliwa Kristo (KK), Wagiriki ndio walioweka msingi wa taaluma ya lugha tuijuavyo hivi leo (Khamis & Kiango, 2002: 1).
Katika taaluma za sayansi ya kompyuta, sintaksia ni kanuni zifafanuazo jinsi alama zitumikazo katika lugha ya kikompyuta zinavyounganishwa pamoja kwa mpangilio unaokubalika kuwa ni muundo sahihi katika lugha hiyo ya kikompyuta (Programming Language).
Katika kozi hii hatutahusika na mpango wa vitu kwa ujumla wake wala kanuni fafanuzi za matumizi ya maneno na virai katika lugha ya kikompyuta, bali tutajikita zaidi katika taaluma ya isimu. Kwa hiyo, sintaksia ni nini katika taaluma ya isimu?
Besha (1994: 84), sintaksia ni taaluma inayojihusisha na uchambuzi na ufafanuzi wa muundo wa sentensi za lugha; kwa mujibu wa O’Grady (1996: 181), sintaksia ni taaluma inayochunguza jinsi maneno yanavyounganishwa ili kuunda sentensi. Sintaksia kwa mujibu wa Massamba na wenzake (2009: 34) ni, “Utanzu wa sarufi unaojishughulisha na uchanganuzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipashio vyake.” Wanaendelea kusema kuwa katika utanzu huu kinachochunguzwa ni zile sheria au kanuni ambazo hazina budi kufuatwa katika kuyapanga maneno ya lugha katika mfuatano (neno moja baada ya jingine) kwa namna ambayo itayafanya maneno hayo yalete maana inayokubalika na kueleweka katika lugha husika.
Fasili hizi chache tumezitoa kama mifano tu ya kushadidia hoja ya kwamba kuna fasili nyingi za sintaksia. Pamoja na kuwapo kwa fasili nyingi, mtu akichunguza atagundua kwamba fasili takriban zote zinabainisha kuwa sintaksia ni tawi la isimu linalojihusisha na uchunguzi wa:
(a) Jinsi maneno yanavyopangwa katika tungo
(b) Kanuni au taratibu za lugha zinazotumika na zinavyotumika katika kuyaweka maneno hayo pamoja
Kwa hiyo, sintaksia inaweza kufasiliwa kuwa ni taaluma inayochunguza miundo ya tungo na kanuni mbalimbali za lugha zinazotawala miundo hiyo. Katika uchunguzi huo, sintaksia huhusika na mpangilio wa maneno katika miundo mitatu iliyopangwa kidarajia, yaani jinsi maneno yanavyopangwa ili kuunda virai, vishazi na sentensi.
9.3 Malengo ya Ufafanuzi wa Kisintaksia
Lengo kuu la ufafanuzi wa kisintaksia ni kupata sarufi inayotosheleza kwa usahihi miundo ya lugha. Hivi ni kusema, wanasintaksia hufafanua miundo ya sintaksia wakiwa na shabaha ya kupata njia sahihi na toshelevu zitakazosaidia kupata miundo sahihi na kukataa miundo isiyo sahihi katika lugha.
Tangu awali taaluma ya lugha ilipoanzishwa, enzi za Wagiriki na Walatini, kumekuwa na mbinu mbalimbali za uchanganuzi wa mfuatano wa vipashio katika muundo wa mlalo. Kwa mfano, sentensi:
  1. Mtoto ana bahati
Ni sentensi sahili ambayo ni sahihi. Ni utungo ambao una maneno yaliyopangwa kimlalo kwa kufuata sulubu maalumu. Maneno hayohayo yaliyotumika katika sentensi (1) yanaweza kupangwa vinginevyo na kutupatia miundo mbalimbali sahihi na isiyo sahihi. Mathalan:
  1. Bahati ana mtoto
  2. Ana bahati mtoto
  3. *Mtoto bahati ana
  4. *Ana mtoto bahati
Vivyo hivyo, sentensi:
  1. Tukiwa tunakula, nitakwambia vitu
Kimsingi hii, ni sentensi changamano, ni utungo ambao una maneno yaliyopangwa kwa kufuata sulubu maalumu. Maneno hayohayo yaliyotumika katika sentensi (6) yanaweza kupangwa vinginevyo na kutupatia miundo mbalimbali sahihi na isiyo sahihi kama vile:
  1. Tukiwa tunakula vitu, nitakwambia
  2. Nitakwambia, tukiwa tunakula vitu
  3. *Tunakula vitu, nitakwambia tukiwa
  4. *Tukiwa nitakwambia vitu tunakula
Sentensi zisizo na alama ya kinyota zimefuata sulubu inayokubalika katika lugha ya Kiswahili na kwa hiyo ndizo sentensi sahihi na zile zenye alama hiyo hazikufuata sulubu hiyo na kwa hiyo si sahihi. Je, tunajuaje kuwa sentensi hizi sahihi ni sahihi na nyingine zisizo sahihi si sahihi?
Tukitaka kujua usahihi na utosahihi wa tungo hizo, tunahitaji njia za uchanganuzi zitakazotupatia mbinu ya kujua mfuatano fulani wa vipashio katika tungo sahihi na zisizo sahihi kuzikataa. Lengo la wanasintaksia, ambalo hasa ndilo lengo la ufafanuzi wa kisintaksia, siku zote limekuwa ni kutafuta njia hizo za kuzikubali sentensi sahihi na kuzikataa sentensi zisizo sahihi. Njia hizo za kufanyia uchanganuzi wa sentensi ndizo huitwa sarufi (kwa maana yake finyu). Je, mwanasintaksia anafikiaje hatua ya kupata sarufi ya lugha inayohusika?
Kwanza, mwanasintaksia huchambua na kueleza maarifa aliyo nayo mjua lugha kuhusu miundo ya lugha yake. Na pili, huunda nadharia kulingana na ugunduzi wake kuhusiana na maarifa hayo ya mjua lugha.
]]>
Muhadhara 9:

<![CDATA[ODC : MUHADHARA WA KUMI : Kategoria za Kisintaksia na Ushahidi wa Kuwepo Kwazo]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1596 Sun, 28 Nov 2021 07:45:29 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1596 Muhadhara 10: 
Muhadhara  wa Kumi
 Kategoria za Kisintaksia na Ushahidi wa Kuwepo Kwazo
10.1 Utangulizi
Katika mhadhara uliopita tulipokuwa tunafasili dhana ya sintaksia tulidokeza kuwa sintaksia huchunguza jinsi maneno yanavyopangwa katika tungo. Jambo hili linatuambia kuwa katika lugha kuna maneno. Maneno hayo katika kila lugha hayajakaa kivoloya bali huwa yanahusiana kiasi cha kuweza kuwekwa katika makundi madogo. Akishadidia hoja hii, O’Grady, (1996: 182) anaeleza kuwa Ukweli wa msingi kuhusu maneno katika lugha zote za binadamu ni kwamba yanaweza kuwekwa katika makundi madogo zaidi yajulikanayo kama kategoria za kisintaksia. Kauli hii ya O’Grady inatuingiza katika udadisi wa kutaka kujua maana ya kategoria. Hivyo, tunajiuliza, “Kategoria ni nini?” Kusudi la muhadhara huu ni kujaribu kufasili dhana ya kategoria na kuangalia kama kweli kategoria zipo au la.
Madhumuni ya Muhadhara
Baada ya kusoma muhadhara huu unatarajiwa kuweza:
(i)     Kufafanua dhana ya kategoria
(ii)    Kutaja kategoria za kisintaksia
(iii)  Kueleza ushahidi wa kuwepo kwa kategoria za kileksika
10.2 Dhana ya Kategoria
Kwa mujibu wa Khamisi na Kiango (2002: 9) dhana ya kategoria ilitumiwa na wanasarufi mapokeo kwa namna tofauti na inavyotumiwa na wanasarufi mamboleo. Neno kategoria kama lilivyotumika katika sarufi mapokeo ya akina Aristotle limetokana na neno la Kigiriki na kutafsiriwa kama uarifu (predication). Wao walitumia dhana ya kategoria kuwa ni sifa bainifu, yaani zile sifa zinazoambatana au zinazoambikwa kwenye aina za maneno kama vile idadi, nafsi, kauli, ngeli, njeo, dhamira na uhusika.
Kategoria kwa mtazamo wa kisarufi mamboleo ni jamii, seti, kundi au makundi ya maneno yanayofanya kazi ya kufanana. Aidha, darajia yoyote ya vipashio inayotambuliwa katika uchambuzi wa lugha fulani huitwa kategoria.
Kwa sasa kategoria zipo katika viwango au darajia tatu: kiwango cha neno, kiwango cha kimuundo au kirai na kiwango cha kidhima. Kategoria hizi tatu zinajulikana kwa majina ya:
  • Kategoria za kileksika
  • Kategoria za virai
  • Kategoria za kidhima
10.2.1 Kategoria za Kileksika
Kategoria za kileksika ni kategoria za kiwango cha neno moja moja. Wataalamu mbalimbali wametofautiana katika idadi na istilahi za kategoria hizo. Kuna wanaotaja kategoria nne (tazama O’Grady, 1996: 182), saba (tazama Nkwera, 1978; Kapinga, 1983) na nane (tazama Kihore, 1996). Kategoria za kileksika zilizoainishwa mpaka sasa ni hizi zifuatazo:
Kategoria Mifano
(a) Nomino (N): Masanja, kijana, mtu, kitabu, vumbi, maziwa, utoto, ugonjwa n.k.
(b) Kitenzi (T): tembea, sema, totoa, ugua, kuwa n.k.
© Kivumishi (V): (-)dogo, -eusi, (-)zito, zuri n.k.
(d) Kihusishi (H): cha, katika, la, tena, hadi n.k.
(e) Kielezi (E): kijinga, vizuri, kabisa, sana, hasa, wima n.k.
(f) Kiwakilishi (W): mimi, wao n.k.
(g) Kiunganishi (U): na, lakini, ila, au, ama n.k.
(h) Kibainishi (B): yule, huyu, hawa n.k.
(i) Kiingizi/Kihisishi (K): abe!, naam!, hebu! n.k.
Kama tulivyobainisha kuhitilafiana kwa wataalamu juu ya ukategorishaji wa maneno, O’Grady (1996: 182) anaona kuwa kategoria za kileksika ni (a) mpaka (e) tu na kategoria zinazobaki ni kategoria zisizo za kileksika au ni kategoria za kidhima kwa kuwa maana za vipashio hivyo si rahisi kufasilika au kuelezeka. Aidha, katika kategoria za virai, ni kategoria za (a) mpaka (e) tu ndizo hutokea kama maneno makuu ya virai husika.
Kuna mkanganyiko unaoweza kujitokeza kuwa kuna maneno yanayoweza kuwa katika kategoria zaidi ya moja. Je, ni vigezo gani vinatumika ili kubaini kategoria za maneno? Vigezo vinavyotumika kubaini kategoria za maneno ndizo hutumiwa pia kama ushahidi wa kuwapo kwa kategoria katika lugha.
10.3 Ushahidi wa Kuwapo kwa Kategoria za Kileksika
Ushahidi unaounga mkono kuwapo kwa kategoria za kileksika ni wa kifonolojia, kimofolojia, kisintaksia na kisemantiki.
10.3.1 Ushahidi wa kifonolojia
Katika ushahidi huu kigezo kinachotumiwa ni mkazo au shadda. Neno moja linakuwa katika kategoria tofauti kutokana na uwekaji wa mkazo. Tutazame mifano ifuatayo:
1) Wafanyakazi wote wamejenga baraBAra
2) Kazi zote zimefanyika baRAbara
3) We need to imPORT new technology
4) We need an IMport of new technology
Katika mifano hiyo hapo juu, neno la mwisho katika sentensi 1) ni nomino na katika sentensi 2) ni kielezi. Katika sentensi 3) neno la nne ni kitenzi na neno hilohilo katika sentensi 4) ni nomino. Maneno ni yaleyale lakini yamekuwa katika kategoria tofauti kutokana na uwekaji wa mkazo mahali tofauti. Kwa hiyo, mkazo unathibitisha kuwapo kwa kategoria za kileksika. Unathibitisha kuwa kuna kategoria mbili za neno moja. Hapa tunaona kuwa kanuni fulani za kifonolojia lazima zijue taarifa za kikategoria kabla ya kutumika. Kwa hiyo, tunahitimisha kwa kusema kwamba lile dai la O’Graddy (1996) la kwamba maneno yamegawanyika katika makundi mbalimbali lina ukweli ndani yake.
10.3.2 Ushahidi wa kimofolojia
Katika ushahidi huu kinachoangaliwa ni uambikatizi. Viambishi fulani vya kisarufi huweza kuambikwa kwenye maneno yaliyo katika kategoria fulani tu na haviwezi kuambikwa kwenye maneno ya kategoria tofauti.
Kwa mfano, O’Graddy (1996) anasema katika lugha ya Kiingereza kiambishi cha wingi –s huambikwa kwenye maneno ya kategoria ya nomino, kiambishi cha njeo iliyopita –ed na cha hali ya kuendelea huambikwa kwenye vitenzi, na viambishi vya ukadirifu -er, -est huambikwa kwenye vivumishi. Vivyo hivyo, katika lugha ya Kiswahili, viambishi vya idadi na ngeli huambikwa katika nomino na vivumishi, viambishi vya njeo, kauli, na usababishi huambikwa katika vitenzi n.k.
10.3.3 Ushahidi wa kisintaksia
Hapa kigezo kinachotumika na ambacho yasemekana ndicho kinachoaminika zaidi (O’Grady, 1996: 184) ni kile cha mtawanyo. Tunaangalia nafasi ambayo maneno yanachukua katika tungo.
Kwa mfano, maneno ya kategoria ya nomino ndiyo yanayoweza kuchukua nafasi iliyo wazi katika utungo ufuatao:
__________ anaweza kuwa mnyama hatari sana.
Simba
Chui
Nyoka n.k.
10.3.4 Ushahidi wa kisemantiki
O’Grady (1996: 183) anasema kuwa kigezo kinachohusika hapa ni maana. Kwa maneno mengine, tunajua kuwa neno fulani liko katika kategoria fulani kutokana na linavyofasiliwa. Kwa mfano:
Nomino: maneno yanayotaja vitu
Vitenzi: maneno yanayotaja vitendo
Vivumishi: maneno ambayo hutaja sifa za nomino
Vielezi: maneno ambayo hueleza namna ambavyo tendo linafanyika
Vihusishi: maneno yanayohusisha
Vibainishi: maneno ambayo huweka vitu bayana
Tutakubaliana sote kuwa kigezo hiki hakiwezi kuwa cha kuaminika sana. Kunaweza kuwa na mapungufu mengi mtu akitumia fasili katika kuchanganua kategoria za maneno. Tuangalie mifano michache ya maneno kutoka lugha ya Kiingereza.
  • “Assasination” linaonyesha hali ya kutenda lakini ni nomino
  • “Fast food” katika neno ambatano hili, neno “fast” linadokeza namna ambavyo chakula kinavyotengenezwa (haraka haraka). Kwa jinsi hii neno fast linaonekana kuwa ni kielezi ilhali ni kivumishi.Aidha, kategoria ya vivumishi inaweza kuwa ngumu kuibainisha ikiwa peke yake kwa sababu Huweza kuwa kiwakilishi.
Kigezo kizuri kinachofaa kutumika katika ushahidi wa kisemantiki ni utata. Utata ndicho kigezo kizuri cha kuonyesha kuwa maneno yana kategoria mbili au zaidi. Utata ni kipengele kinachodhihirisha tafsiri zaidi ya moja. Yaani ni hali ya kipashio kimoja kuwa na maana zaidi ya moja. Upo utata wa kileksia na wa kimuundo. Katika utata wa kileksia, leksimu au neno moja linakuwa na maana zaidi ya moja. Kwa mfano:
Kaa 1. Mnyama wa majini, gegeleka (Nomino)
  1. Kijinga cha moto (Nomino)
  2. Keti (Kitenzi)
Panda 1. Tia mbegu ardhini (Kitenzi)
  1. Jamiiana (Kitenzi)
  2. Kwea (Kitenzi)
  3. Njia iliyogawantika (Nomino)
Katika utata wa kimuundo, tafsiri zaidi ya moja zinaibuka kutokana na jinsi utungo ulivyotungwa. Kwa mfano:
Hali halali
N V: Hali ambayo si haramu; ile inayoturuhusu kufanya jambo fulani
T T: Hawezi kula wala kulala
10.4 Hitimisho
Kutokana na ushahidi wa kifonolojia, kimofolojia, kisintaksia na kisemantiki, ni dhahiri kuwa maneno hugawika katika makundi mbalimbali madogo zaidi kama ilivyodaiwa na O’Grady (1997).
]]>
Muhadhara 10: 

<![CDATA[Kutumia michezo ya watoto katika kujifunza]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1501 Thu, 18 Nov 2021 02:45:10 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1501
.pdf   Sehemu ya 3.pdf (Size: 143.01 KB / Downloads: 0) ]]>

<![CDATA[ODC : MUHADHARA WA KUMI NA SABA : FASIHI YA KISWAHILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1245 Wed, 15 Sep 2021 03:20:01 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1245
.pdf   MUHADHARA WA KUMI NA SABA.pdf (Size: 139.06 KB / Downloads: 0) ]]>

<![CDATA[UFUNDISHAJI WA LUGHA YA PILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1173 Mon, 06 Sep 2021 14:02:56 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1173
Kuna mikabala/ mikondo mbalimbali katika historia ya ufundishaji wa lugha ya pili  ambayo  imewahi  kutumiwa.  Baadhi  ya  mikabala  hiyo,  mpaka  sasa  imeendelea kuathiri ufundishaji wa lugha ya pili. Ujuzi wa mikabala hiyo ni jambo muhimu kwa mwalimu wa Kiswahili kwa sababu unaweza kumsaidia kupata fununu kuhusu asili ya mbinu  tofauti  tofauti  zinazotumiwa  kufundisha  lugha  ya  pili. Hapo  awali  mbinu  hizi zililenga hasa ufundishaji wa lugha ya Kingereza kama lugha ya pili. Hata hivyo, baadhi ya  mambo  ambayo  hupendekezwa  katika  mbinu  hizo  yanaweza  kumsaidia  mwalimu ambaye anajishughulisha na ufundishaji wa Kiswahili kama lugha  ya pili.
Madhumuni Ya Somo
Kufikia mwisho wa somo hili utaweza kutoa mifano ya mbinu za kufundishia lugha na kueleza jinsi kila mojawapo ya mbinu hizo inaweza kutumiwa katika ufundishaji wa Kiswahili.
Mbinu Ya Kimapokeo
Hii ni mbinu ambayo hapo awali ilitumika kama njia ya kufundishia lugha za kijadi  kama  vile  Kiyonani  na  Kilatini.  Ilitawala  ufundishaji  wa  lugha  za  kizungu  na kigeni kati ya miaka 1840 na 1940. Lengo kuu la mbinu hii ni kufanikisha ufahamu wa sarufi  pamoja  na  uwezo  wa  kuandikia  kwa  usahihi  katika  lugha  inayolengwa.  Pia inalenga kuwezesha mwanafunzi kuwa na upeo mpana wa msamiati unaotumika sana katika lugha ya uandishi katika lugha husika, ili hatimaye aweze kuthamini umuhimu pamoja na thamani ya nakala zinazohusika.
Katika mazingira ya darasani, mwalimu anatazamiwa kutekeleza malengo haya kwa kushirikisha wanafunzi katika kazi ya kutafsiri mara kwa mara kutoka lugha zao hadi  katika  lugha  inayofunzwa.  Kabla  ya  kutafsiri,  wanafunzi  wanapaswa  kwanza kijifunza maneno ya lugha inayolengwa ili waweze kutafsiri katika lugha mpya. Pamoja na  hayo,  wanafunzi  wanapewa  maelezo  marefu  kuhusu  sheria  za  kisarufi.  Kisha wanapewa zoezi la kutunga sentensi ili kubainisha ufahamu wao wa sheria hizo. Uwezo wa  mwanafunzi  katika  kutafsiri  huwa  ndicho  kigezo  muhimu  kinachotumiwa  kama chombo cha kupima ustadi wake katika kipengele cha sarufi na msamiati.
Udhaifu hasa wa mbinu hii ni kwamba haitilii mkazo juu ya matamshi sahihi pamoja na stadi za kimawasiliano. Inasisitiza sana ujuzi wa sheria za kisarufi bila kupatia wanafunzi nafasi ya kutosha kujieleza kutokana na nafsi zao. Matokeo ya kujishughulisha sana na ufundishaji wa kanuni na vighairi ni kwamba waalimu huishia kwa kufundisha wanafunzi lugha ya ulimwengu wa vitabu, lugha isiyokuwa na uhai, na ambayo mara nyingi haina manufaa katika ufanikishaji wa mawasiliano ya kawaida.
Utumiaji wa mbinu hii unalifanya somo la lugha kukosa ubunifu unaotakikana. Wanafunzi hawapati nafasi ya kutumia lugha kama chombo wanachoweza kukitegemea kutekeleza mahitaji yao ya kimawasiliano. Shughuli ya kujifunza lugha inageuka kuwa zoezi la kukariri maneno chungu nzima na kanuni kemkem za kisarufi. Hakuna hakikisho kwamba baada ya kukariri maneno na kanuni wanafunzi watakuwa na uwezo wa kutumia kanuni  na  maneno  vilivyokaririwa  katika  mawasiliano  ya  nje  ya  darasa.  Shughuli  ya kufundisha na kujifunza lugha inakuwa kama zoezi la kuchemsha bongo tu.
Mbinu Ya Moja Kwa Moja
Hali ya kutoridhika na mbinu ya kimapokeo ni miongoni mwa mambo ambayo yalichangia kuibuka kwa mbinu ya moja kwa moja. Iliibuka katika karne ya 19 kuchukua mahali  pa  mbinu  ya  kimapokeo.  Wanaopendelea  mbinu  hii  hushikilia  kwamba  njia mwafaka ya kujifunza lugha ya pili ni kukabiliana nayo moja kwa moja na kuitumia kama vile mtoto mdogo anavyofanya anapojifunza lugha ya mama. Kulingana na mbinu hii ni marufuku kutumia lugha ya wanafunzi au lugha nyingine yo yote ile.
Mbinu hii husisitiza umilisi wa lugha bila tafsiri wala maelezo rasmi juu ya sheria za kisarufi. Wanafunzi wanatakiwa kijifunza lugha kwa kushirikishwa kikamilifu kama wahusika watendaji katika matumizi tofauti tofauti ya lugha. Inasisitizwa kwamba ikiwa maana inaweza kuwasilishwa moja kwa moja kwa kushirikisha maono au vitendo hakuna haja ya kutafsiri.
Kwa upande wa sarufi, mbinu hii inashikilia kwamba njia bora ya kuendeleza ufahamu wake ni kutokana na uzoefu wa kutumia mara kwa mara lugha inayohusika. Mwanafunzi akipewa fursa ya kutosha kukumbana na matumizi ya lugha, itakuwa rahisi kwake kutambua na kujifunza sheria zinazotawala sarufi ya lugha hiyo. Mbinu hii inasisitiza haja ya kutoa nafasi kwa mwanafunzi ya kujifunza lugha kama vile mtoto anavyojifunza lugha yake ya kwanza. Mtoto anajifunza na kuimudu lugha kwa kukumbana nayo moja kwa moja katika mkutadha maalum wa mawasiliano.
Hakuna mtu anayemfafanulia kanuni za kisarufi za lugha yake. Hata hivyo anazing’amua kanuni hizo yeye mwenyewe baada ya kushuhudia matumizi yake katika vielelezo vya sentensi. Huwa anajifunza lugha ya jamii yake katika mazingira yanayoshirikisha vitendo na maono. Ushirikishaji wa maono na vitendo unachangia kujenga hali ambayo husaidia mtoto  kukisia  maana  ya  kile  kinachosemwa. Anajifunza  lugha  ya  jamii  yake  kwa kusikiliza kwanza na baadaye kuigiza yale anayosikiza.
Kwa mujibu wa mbinu hii mwalimu anapofundisha lugha ya pili anashauriwa kutotegemea  tafsiri.  Anashauriwa  vile  vile  kutofundisha  moja  kwa  moja  sheria  za kisarufi.  Ana  wajibu  wa  kuambatanisha  ufundishaji  wake  na  vitendo,  uigizaji  na mazungumzo. Lakini ikiwa mwalimu hana budi kufundisha sarufi, inafaa ufundishaji wa sarufi uzingatie kiwango cha matumizi ya lugha huko mkazo ukitiliwa juu ya madondoo ya kisarufi yanayotumika sana sana hasa katika mazungumzo.
Kwa mujibu wa mbinu hii, dhima ya mwalimu ni kupanga na kufanikisha utumizi wa lugha badala ya kujishughulisha na ufafanuzi pamoja na uchambuzi wa kanuni za kisarufi. Ili mwalimu aweze kufaulu kutumia mbinu hii anapaswa kuwa na ujuzi wa kiwango cha hali ya juu katika lugha anayofundisha. Ni lazima pia awe na ubunifu wa kumwezesha kuwasilisha maana bila kutumia lugha nyingine yo yote zaidi ya ile ambayo anafundisha.  Anatarajiwa  pia  kujitahidi  kujenga  mazingira  ya  kufundishia  ambayo yanakaribia kufanana yale ya lugha ya kwanza. Mazingira hayo yanatarajiwa kufanikisha ufahamu wa lugha kupitia mazoezi ya kusikiliza pamoja na mazungumzo. Lazima yawe mazingira   ambayo   yanaweza   kuchangia   katika   kuhamasisha   mwanafunzi   kutaka kujifunza lugha inayohusika.
Kwa kawaida mtoto anapojifunza lugha yake ya kwanza anakuwa na hamu ya kujifunza lugha hiyo ili aweze kutangamana na jamii ya watu wanaomzunguka. Jamii hiyo pia humsaidia kuendelea kwa kumtia shime. Pamoja na hayo mtoto huwa na muda mwingi wa kusikia na kutumia lugha hiyo. Lugha inakuwa sehemu ya maisha yake ya kila siku.
Mbinu Ya Uzungumzi
Mbinu hii ilizuka na kukita mizizi katika miaka ya 1950 kutokana na mwamko mpya nchini Amerika wa kujishughulisha na ufunzaji wa lugha za kigeni. Tukio muhimu ambalo lilichangia pakubwa kuamsha ari ya Wamerika katika lugha za kigeni ilitokea mnamo mwaka wa 1957. Mwaka huo Warusi walifaulu kupeleka chombo chao (sputnik) angani. Jambo hili lilikuwa changamoto kubwa kwa taifa la Amerika. Kufuatia tukio hilo, serikali ya Amerika iliamua kujishughulisha kikamilifu katika ufundishaji wa lugha za kigeni ili isiachwe nyuma katika maendeleo ya kisayansi. Jambo ambalo linapewa kipaumbele katika mbinu hii ni ufasaha wa kuzungumza.
Ufasaha unaotarajiwa unahusu matamshi bora, sarufi, pamoja na uwezo wa kuitikia upesi na kwa urahisi katika hali tofauti zinazohusisha utumizi wa lugha katika mazungumzo.
Ufahamu  sikizi,  matamshi,  sarufi  na  msamiati  vinapofundishwa  huwa  kama  njia mojawapo   ya      kufanikisha ufasaha       wa     kuzungumza. Vilevile wanafunzi wanaposhirikishwa katika kuandika na kusoma mambo haya yanaambatanishwa na ustadi wa kutumia lugha ya mazungumzo. Kulingana na mbinu hii, stadi za lugha zinastahili kufundishwa kwa kuzingatia mfuatano huu: Kusikiliza, Kuongea, Kusoma na Kuandika.
Katika hatua za mwanzo mwanzo, kusoma na kuandika vinachukuliwa tu kama mambo  ambayo  yanaweza  kuchangia  kuimarisha  ustadi  wa  kusikiliza  na kuongea.
Vinatiliwa mkazo zaidi katika viwango vya juu wakati ambapo wanafunzi wana uzoefu unaofaa ili kuweza kukabiliana na mitindo zaidi ya lugha ya kimaandishi. Madondoo ya lugha yanapofundishwa kwa   kutumia      mbinu         hii      huwa yanawasilishwa  kupitia  mjadala  ambao  ni  chombo  muhimu  cha  kutoa  mkutadha  wa kufundishia  kile  kinacholengwa.  Zaidi  ya  kushiriki  katika  mjadala,  wanafunzi  huwa wanatakiwa, mara kwa mara, kukariri vielelezo vya sentensi.
Mbinu Ya Mawasiliano
Msingi  wa  mbinu  hii  ni  imani  kwamba  kazi  kuu  ya  lugha  ni  kufanikisha maingiliano   pamoja   na   mawasiliano   katika   jamii.   Lugha   ni   chombo   ambacho kinamwezesha binadamu kushirikiana na watu wengine na pia kutekeleza mahitaji ya maisha yake. Kwa hivyo, kulingana na waasisi wa mbinu hii, lengo kuu la kufundisha lugha  ni  kuwezesha  mwanafunzi  kuwa  na  uwezo  wa  kuwasiliana  akitumia  lugha inayohusika.
Njia moja ya kuhakikisha kuwa mwanafunzi anakuwa na uwezo wa kuwasiliana ni, kwanza, kumpa fursa ya kushiriki kama mhusika mpokezi. Mwanafunzi  anapata fursa ya kupanua upeo wake wa lugha kupitia kusikiliza na kusoma. Baada ya kushiriki katika matumizi ya lugha akiwa mhusika mpokezi mwanafunzi anashirikishwa kama mhusika mwanzilishi wa mawasiliano. Kulingana na waasisi wa mbinu ya mawasiliano, lugha ambayo ni ya maana / manufaa kwa wanafunzi inatilia nguvu juhudi za kujifunza. Kwa hivyo ni muhimu kwa walimu kuhakikisha kwamba wanapochagua kazi ya wanafunzi wanatilia  maanani  uwezo  wa  kazi  hiyo  wa  kuwashirikisha  katika  matumizi  ya  lugha yenye maana na uhalisi.
Kwa kawaida, mawasiliano hufanyika katika mazingira ya watu wakiwa katika vikundi. Pia, aghalabu, mawasiliano huchukua mkondo wa mazungumzo (conversation) na  majidiliano  (discussion).  Wakizingatia  ukweli  huu,  wanaounga  mkono  mbinu  ya kimawasiliano wanapendekeza kugawanya  wanafunzi katika vikundi vidogo vidogo. Hii ni njia bora ya kuendeleza uwezo wa wanafunzi wa kuwasiliana kwa kutumia lugha inayofundishwa. Wakiwa katika vikundi vya watu wachache, wanafunzi wanakuwa na fursa bora ya kutumia lugha halisi. Pia wanapata nafasi ya kujieleza kwa ufasaha bila wasiwasi.  Ustadi  katika  kusoma  na  kuandika  unaweza  kukuzwa  kutokana  na  msingi imara wa kutumia lugha kwa uhalisi.
Je  jukumu  hasa  la  mwalimu  ni  nini?  Kwa  mujibu  wa  waasisi  wa  mbinu  hii, jukumu la mwalimu ni kuhamasisha wanafunzi na kutoa kwao nafasi ya kujieleza katika lugha  inayohusika.  Ana  wajibu  wa  kuhamasisha  wanafunzi  kutumia  lugha  kwa  njia mbalimbali. Anapaswa pia kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata fursa ya kujieleza.
Pamoja na hayo, mwalimu ana wajibu kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa vizuri kwa nini wanafundishwa kile wanachofundishwa. Hivi ndivyo watakavyoweza kushiriki kwa  njia  ya  maana  na  manufaa  kwao.  Vilevile  ni  lazima  mwalimu  ahakikishe  kuwa wanafunzi wake wanahusika zaidi kuliko vile anavyohusika mwenyewe.
Aidha,  mwalimu  anashauriwa  kushirikisha  wanafunzi  katika  vitendo  ambavyo vinaweza   kuwalazimisha   kuwasiliana   kwa   kutumia   lugha   inayofaa   kulingana   na mkutadha. Kwa maneno mengine, mwalimu anapaswa kubuni hali na mazingira ambamowanafunzi  hawawezi  kukidhi  mahitaji  na  matarajio  yao  bila  kuwasiliana.  Wakijikuta katika  mazingira  ya  namna  hii  hawatakuwa na  budi  kutafuta  ufumbuzi  kwa  kutumia lugha.  Kwa  ufupi,  mwalimu  anaweza  kusaidia  kuendeleza  uwezo  wa  wanafunzi  wa kuwasiliana wakitumia lugha kwa kuzingatia mfuatano wa hatua zifuatazo:
  1. Mapokezi ya lugha.
  2. Ufafanuzi / Maelezo
  3. Majaribio ya matumizi ya lugha
  4. Mawasiliano huru
Katika hatua ya mapokezi wanafunzi wanashiriki kama wahusika wapokezi. Kazi yao katika hatua hii ni kupokea ujumbe unaowasilishwa na watu wengine na kupata maana  ya  ujunbe  unaowasilishwa.  Wanaweza  kutekeleza  jambo  hili  kupitia  zoezi  la kusikiliza au kusoma. Zoezi la kusikiliza husaidia wanafunzi kupata nafasi ya kupanua upeo  wa  lugha.  Kupitia  zoezi  hili  wanaweza  kujifunza  msamiati  mpya  na  miundo mbalimbali  ya  kisarufi.  Vilevile  wanafunzi  wanaimarisha  ujuzi  wao  wa  yale  ambayo wamejifunza tayari.
Kwa upande mwingine, katika hatua ya ufafanuzi (maelezo) mwalimu anaweza kudondoa madondoo fulani ya lugha ambayo wanafunzi wamewahi kukumbana nayo, katika zoezi la kusikia na kusoma. Kisha anatoa maelezo kuhusu madondoo hayo ili wanafunzi   wayatilie   maanani   zaidi   kuliko   mengine   kwa   wakati   huo.   Baada   ya kuhakikisha   kwamba   wanafunzi   wanafahamu   kiini   cha   somo   mwalimu   anawapa wanafunzi  nafasi  ya  kujaribu  kutumia  madondoo  hayo  katika  vielelezo  vya  sentensi wakizingatia maagizo yaliyotolewa.
Katika hatua ya mawasiliano huru wanafunzi wanapata fursa zaidi ya kujieleza bila kufuata maagizo ya mwalimu. Wanaweza kujieleza kwa njia halisi kulingana na mahitaji  ya  mawasiliano  katika  mkutadha  unaohusika.  Wanafunzi  watateua  lugha kulingana na hali halisi inayowakabili wakati huo. Mawasiliano huru huwapa wanafunzi fursa ya kutambua kuwa lugha siyo somo ambalo linajikita katika mipaka ya mazingira ya  darasani  tu,  lakini  pia  ni  chombo  cha  mawasiliano  nje  ya  mipaka  ya  darasa.
Mawasiliano huria huwapa wanafunzi nafasi ya kutumia lugha kwa njia ya ubunifu katika miktadha tofauti tofauti ya kijamii. Wanatumia lugha bila usimamizi wa mwalimu, lakini kulingana  na  hali  halisi  katika  mazingira  ya  mawasiliano.  Huwa  wajitegemea  wao wenyewe. Kadiri wanavyoshiriki katika mikutadha tofauti ya mawasiliano na kushuhudia jinsi lugha inavyotumiwa, ndivyo wanavyoendelea kukuza na kuimarisha uwezo wao wa kimawasiliano (communicative competence). Uwezo huu ni muhimu kwa mwanafunzi kwa sababu akiwa nao anaweza kufasiri lugha kwa njia iliyo sahihi akizingatia mkutadha unaohusika.  Na  akifanya  hivyo  anaweza  kuitikia  kama  inavyotarajiwa.  Kwa  mfano mwalimu  akiingia  darasani  ambamo  mna  joto  jingi  na  agundue  kuwa  madirisha yamefungwa,  anaweza  akasema:  Mbona  joto  limezidi  sana  humu  ndani.  Mwanafunzi mwenye  uwezo  wa  kimawasiliano  atatambua  kuwa  mwalimu  angetaka  madirisha yafunguliwe, na ataitikia kwa kuyafungua. Yule asiyekuwa na uwezo huo atachukulia usemi wa mwalimu kama kauli ya kawaida tu.
Msingi wa Mbinu ya Kimawasiliano
Asili ya mbinu ya kimawasiliano ni imani inayoshikilia kwamba:
(a) Lugha ni mfumo wa kueleza maana.
(b) Jukumu kuu la lugha ni kufanikisha maingiliano na mawasiliano baina ya watu.
© Shughuli  ambazo  zinachangia  kufanikisha  ufahamu  wa  lugha  ni  zile ambazo  zinatoa  kwa  wanafunzi  nafasi  ya  kushiriki  katika  mawasiliano halisi (real communication).
(d) Vitendo  vinavyohusisha  matumizi  ya  lugha  ili  kutekeleza  shughuli  za maana (meaningful tasks) husaidia kufanikisha ujuzi wa lugha.
(e) Lugha yenye maana kwa wanafunzi inaimarisha hali ya kujifunza.
(f) Mawasiliano hufanyika ikiwa wale wanaohusika wana hamu (motisha) ya
kuwasiliana.]]>

<![CDATA[ODC : HISTORIA FUPI YA KISWAHILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1159 Mon, 06 Sep 2021 08:16:25 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1159
.pdf   HISTORIA FUPI YA KISWAHILI.pdf (Size: 226.56 KB / Downloads: 1) ]]>

<![CDATA[MBINU ZA KUFUNDISHIA KISWAHILI SHULENI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=710 Sun, 01 Aug 2021 12:40:24 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=710
.pdf   MUHADHARA WA 1.pdf (Size: 121.82 KB / Downloads: 2) ]]>

<![CDATA[MWONGOZO WA MBINU ZA KUFUNDISHIA SHULE ZA AWALI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=707 Sun, 01 Aug 2021 10:18:23 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=707
Ikumbukwe kuwa ufundishaji wa watoto wa shule ya awali ni tofauti na ule wa shule za msingi. Mwalimu anatakiwa kuzingatia kuwa mtoto wa umri huu katika shule ya awali hafundishwi masomo kama wale wa shule za msingi, badala yake watoto hawa hujifunza kwa vitendo, vinavyowapa msingi na kanuni mbalimbali za kuwakuza na kuwawezesha kukabiliana na maisha ya kawaida pamoja na kuwatayarisha kuanza elimu ya msingi.
Msisitizo mkubwa kwa mwalimu umewekwa katika matumizi ya mbinu shirikishi ambazo zitawawezesha watoto kushiriki katika kujadili, kuigiza kuwasiliana wao kwa wao, kufanya ziara na uchunguzi.
Mwalimu anatakiwa kubuni na kufaragua zana mbalimbali za kufundishia elimu ya awali. Aidha mwalimu bora wa elimu ya awali anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo;
  1. Awe na mvuto wa kutosha wa kupenda kufundisha shule ya awali.
  2. Ajiamini katika kushughulika na masuala ya elimu ya awali.
  3. Aweze kujiongoza na kuwaongoza wengine kama mtaalamu wa elimu ya awali.
  4. Ajifunze zaidi na kuthamini mawazo ya watu wengine ili kuboresha na kuendeleza shule ya awali.
  5. Apende na kuhimiza ushirikiano na mawasiliano na wadau wengine wa elimu ya awali.
Maswali:
  1. Eleza maana ya Elimu ya Awali
  2. Taja malengo matano (5) ya kufundisha na kujifunza malezi ya Elimu ya Aawali kwa Mwalimu daraja A.
  3. Eleza umuhimu wa Elimu ya Awali.
  4. Nini mtazamo wa Elimu ya Awali kwa jamii ya Tanzania?
  5. Kwa nini ongezeko la shule za awali ni kubwa mno maeneo ya mjini kuliko vijijini ambako kuna ongezeko la watu wengi?
  6. Taja aina kuu mbili (2) za uchunguzi wa mtoto wa Elimu ya Awali.
  7. Kuna aina anuai za kufanya uchunguzi wa mtot. Taja njia tatu (3).
  8. Taja njia nne (4) zinazoweza kueneza magonjwa ya watoto wadogo.
  9. Nchini Tanzania, Elimu ya Awali ilianza Mwaka gani?
  10. Ainisha aina kuu mbili (2) za uchunguzi wa mtoto na kila moja eleza kwa kutumia mifano miwili miwili kwa ufafanuzi.
  11. Watoto wadogo huwa na matatizo wakati wa kula. Je, matatizo hayo husababishwa na nini?
  12. Ni ajali zipi hutokea mara kwa mara katika Shule za Awali na husababishwa na nini?
  13. Taja na kueleza vifaa vinavyopaswa kuwemo katika Kisanduku cha Huduma ya Kwanza.
  14. Nini maana ya adhabu? Eleza faida na hasara za adhabu katika tendo la kujifunza.

<![CDATA[MBINU ZA UFUNDISHAJI WA KISWAHILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=705 Sun, 01 Aug 2021 09:24:22 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=705
.pdf   MBINU ZA UFUNDISHAJI WA KISWAHILI.pdf (Size: 226.06 KB / Downloads: 1) ]]>

<![CDATA[DC : MUHADHARA WA KUMI  NA MBILI: UAINISHAJI WA SENTENSI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=704 Sun, 01 Aug 2021 09:08:16 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=704
.pdf   DC MUHADHARA WA KUMI  NA MBILI UAINISHAJI WA SENTENSI.pdf (Size: 144.36 KB / Downloads: 0) ]]>

<![CDATA[MAANDALIZI YA MWALIMU]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=703 Sun, 01 Aug 2021 08:55:36 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=703
.pdf   MAANDALIZI YA MWALIMU.pdf (Size: 125.02 KB / Downloads: 2) ]]>

<![CDATA[Kusoma na Kuandika kwa madhumuni mbalimbali]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=702 Sun, 01 Aug 2021 08:44:29 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=702 Kusoma na Kuandika kwa madhumuni mbalimbali
Sehemu ya 1: Kuhamasisha na kutathmini usomaji na uandishi
Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuhamasisha ujifunzaji kusoma na kuandika na kutathmini maendeleo?
Maneno muhimu: kujua kusoma na kuandika katika hatua za mwanzo; nyimbo; mashairi; chapa za kimazingira; tathmini; kazi ya kikundi; usomaji wa ushirika.
Matokeo ya ujifunzaji
Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:
  • kutumia nyimbo na mashairi kufundisha wanafunzi wa kiwango cha mwanzo kusoma;
  • kutumia ‘chapa za kimazingira’ na bidhaa za dukani kufundishia usomaji, uandishi na uchoraji;
  • kutalii njia za kuhamasisha ujifunzaji kwa kutumia kazi ya kikundi;
  • kukuza uwezo wako wa kutathmini ujifunzaji.
Utangulizi
Msomaji na mwandishi mfanisi anatakiwa ajue na aweze kufanya nini? Kama mwalimu, unatakiwa uweze kujibu swali hili ili uweze kuwaongoza wanafunzi wako. Kujifunza kusoma na kuandika kwa ufanisi kunahitaji mazoezi. Hivyo, ni muhimu kutumia mikabala na shughuli mbalimbali ambazo zitawafanya wanafunzi wafurahie. Ni muhimu kutathmini maendeleo ya wanafunzi na kujiuliza mwenyewe kama unakidhi matakwa yao. Sehemu hii inatalii mawazo haya kwani inaangalia ujifunzaji kusoma na kuandika katika hatua za awali.
Somo la 1
Kujifunza kusoma na kuandika ni kazi ngumu! Kwa sababu unataka wanafunzi wazingatie masomo ya kusoma na kuandika, ni muhimu ufanye darasa lako –na shughuli ambazo zinahamasisha ujifunzaji kusoma na kuandika –liwe la kusisimua kadiri iwezekanavyo.
Nyenzo Rejea 1: Wanachotakiwa kukijua wale wasomaji na waandishi wafanisi inaeleza kwamba wanafunzi wanahitaji kujua jinsi ya kuhusisha sauti na herufi, herufi na maneno, maneno na sentensi. Nyimbo na mashairi ambayo wanafunzi wanayajua vizuri –na ambayo wanaweza kuyaimba na kuyaghani kwa kuonesha vitendo –yanawasaidia kujenga mahusiano haya. Pia kushirikishana na wanafunzi wako katika usomaji wa kitabu cha hadithi chenye chapa kubwa kunajenga mahusiano. Unapokuwa unasoma, acha kuwaonesha kila picha na waulize wanafikiri kitu gani kitatokea au kitafuata baadaye. Unapokuwa umemaliza, tumia hiki kitabu kwa shughuli za ugunduzi wa herufi na maneno ambazo utawaambiwa wanafunzi wenyewe waonesha na wasome herufi na maneno fulani. Kumbuka kuwapatia wanafunzi fursa nyingi ili wazungumzie kuhusu hadithi hii –wahusika, kilichotokea, wanavyojisikia kuhusiana na hadithi n.k.
Uchunguzi kifani ya 1: Kuwapatia wanafunzi utangulizi kuhusu usomaji
Bibi Nomsa Dlamini anafundisha wanafunzi wa darasa la 1 wa Nkandla, Afrika Kusini, kusoma na kuandika KiisiZulu. Nomsa huwasomea vitabu vya hadithi, kutoka kwenye baadhi ya vitabu alivyoandika na kufafanua mwenyewe kwa sababu vipo vitabu vichache vya KiisiZulu.
Mwanzoni mwa mwaka, anahakikisha kwamba kila mwanafunzi anaelewa jinsi kitabu kilivyotungwa –jalada, jina la kitabu, hadithi ilivyojengwa –kwa sababu anajua kuwa baadhi yao hawakuwahi kushika kitabu kabla ya kuanza shule. Amegundua kwamba utabiri wa shughuli, ambapo wanafunziwanapendekeza kile kitakachofuata katika hadithi, una umuhimu na huchangamsha wanafunzi wake.
Nomsa amegundua kwamba wanafunzi wanahitaji mazoezi mengi ili kuwafanya wajiamini katika usomaji. Hutengeneza nakala nyingi za machapisho ya mashairi au nyimbo za KiZulu ambazo wanazijua vizuri na nyingine ambazo anajua kuwa ni mahsusi kwa ajili ya ufundishaji wa ugunduzi wa herufi-sauti. Wanafunzi huzisema au huziimba na kuonesha vitendo kuhusiana na nyimbo na mashairi hayo (angalia Nyenzo Rejea 1: Mifano ya nyimbo na mashairi ). La muhimu zaidi, aliwaambia wanafunzi wenyewe waguse na kusoma herufi na maneno. Baadhi ya wanafunzi waliona kuwa kazi hii ni ngumu hivyo alinukuu majina yao na herufi au maneno waliyoona yanawapa shida. Aliandaa kadi zenye picha, herufi na maneno ili kuzitumia kwa njia nyingine na wanafunzi hawa, ama kwa mmojammoja au katika vikundi vidogovidogo, wakati wanafunzi wengine wakiwa wanafanya shughuli nyingine. Nomsa anafarijika kuona kuwa zoezi hili lilisaidia katika kuwafanya wanafunzi hawa wajiamini na kusonga mbele.
Shughuli ya 1: Kutumia nyimbo na mashairi katika kufundisha usomaji
Waambie wanafunzi:
Wachague wimbo au shairi wanalolipenda;
wauimbe/waghani;waangalie kwa makini, unaposema maneno na kuyaandika ubaoni (au kwenye karatasi /ubao ili uweze kuyatumia tena);wasome wimbo/shairi ulilonalo (fanya hivi mara nyingi);waoneshe kwa kugusa herufi fulani (mojamoja) au maneno au alama za uandishi (herufi kubwa, kituo, alama ya kuuliza);waamue vitendo mtakavyofanya mkiwa mnaimba wimbo/kughani shairi ; wafanye vitendo hivi mkiwa mnaimba tena wimbo/kughani tena shairi; wakae kwenye vikundi vya wannewanne na mpeane zamu za kusomeana wimbo huu/shairi hili.
Zunguka darasani, ukiangalia wanafunzi wanaopata matatizo katika usomaji.
Malizia kwa kuliambia darasa zima liimbe tena wimbo au lighani tena shairi, na kuonesha vitendo.
Somo la 2
Baadhi ya wanafunzi wanakulia katika nyumba ambazo zina utajiri wa chapa na maumbo: maboksi ya bidhaa za dukani, pakiti na makopo, vitabu kwa ajili ya watoto na watu wazima, magazeti hata kompyuta/ngamizi. Wengine wana vifaa hivi kwa uchache nyumbani kwao. Changamoto yako kama mwalimu ni kulipatia darasa lako mazingira yenye utajiri wa chapa . Njia moja ya kufanya hivi ni kukusanya vifaa vyovyote popote vinapopatikana. Vifaa vya kufungashia (maboksi ya mbao, pakiti na makopo) mara nyingi vinaandikwa sana na hata wanafunzi wadogo mara nyingi hutambua maneno muhimu kwa zile bidhaa ambazo zinatumika sana nyumbani. Kwa wasomaji wazoevu, magazeti ambayo wanajumuiya wameshamaliza kuyasoma yanaweza kutumiwa kwa shughuli nyingi darasani.
Sehemu hii inatalii njia za kutumia chapa kama hizi katika kusaidia kujifunza kusoma.
Uchunguzi kifani ya 2: Kutumia orodha ya vitu vya dukani kwa shughuli za kujifunza kusoma na kuandika
Precious Muhaji hufundisha Kiingereza kwa wanafunzi 45 wa Darasa la 4 lililopo Lushoto katika Milima ya Usambara. Hawajazoea sana Kiingereza lakini wanatambua herufi na baadhi ya maneno ya Kiswahili yaliyopo kwenye vifaa vya kuhifadhia bidhaa ndogondogo za nyumbani.
Precious alimwomba jirani yake maboksi/makasha, pakiti na makopo matupu. Alivileta vitu hivi shuleni ili kuvitumia katika shughuli za kujifunza kusoma na kuandika.
Mchezo unaopendwa na wanafunzi wake ni mchezo wa ‘ugunduzi wa maneno’. Precious alilipanga darasa katika vikundi tisa vya wanafunzi watanowatano na kukipa kila kikundi boksi, pakiti au kopo lilelile. Aliwaambia wanafunzi waandike namba kuanzia 1 mpaka 5 na kisha aliuliza maswali matano (angalia Nyenzo Rejea 3: Maswali ya mfano ya kuuliza kuhusu vitu vya nyumbani ). Wanafunzi walilinganisha majibu wenyewe na waliamua kuhusu jibu la kikundi. Precious alijadili yale maswali na darasa zima. ‘Mshindi’ alikuwa ni kikundi kilichomaliza cha kwanza na kuweza kutoa majibu sahihi zaidi.
Wakati mwingine Precious alikikaribisha kila kikundi ili kiweze kuuliza swali linalohusiana na ugunduzi wa neno.
Ili kuwahamasisha wanafunzi wafikiri kwa makini, wakati mwingine aliuliza swali kuhusu mchoro wa kifaa kinachohifadhia bidhaa na ujumbe uliopo kwenye tangazo.
Precious aligundua kuwa wanafunzi wengine hawakushiriki, hivyo wakati mwingine walipocheza mchezo huu, alimwambia kila mwanafunzi aandike maneno manne kutoka kwenye kontena la kuhifadhia bidhaa za dukani kabla ya kurudi kwenye viti vyao vya kawaida. Wakiwa wamesharudi kwenye viti vyao alimwambia kila mmoja amsomee mwenzake orodha yake. Aligundua wanafunzi sita ambao walihitaji msaada zaidi na alifanya nao kazi baada ya saa za shule kwa nusu saa, kwa kutumia vitu vilevile na kuwapatia muda wa kufanya mazoezi ya kubainisha herufi na maneno.
Precious aligundua kuwa kuzoea herufi na maneno katika vifaa vya kuhifadhia bidhaa huwasaidia wanafunzi kubainisha herufi na maneno haya katika matini nyingine walizozisoma, kama vile hadithi. Kwa kunakili maneno kutoka katika vitu hivyo, wanafunzi pia hujifunza kuandika herufi na maneno kwa kujiamini zaidi na kwa usahihi zaidi.
Shughuli ya 2: Kutumia orodha ya bidhaa za dukani kwa shughuli za usomaji na uandishi
Leta makopo/mikebe, pakiti au maboksi ya kutosha darasani ili kila kikundi cha wanafunzi watanowatano au sitasita kipate kitu kimojawapo cha kukifanyia kazi au liambie darasa lako likusaidie katika ukusanyaji wa vitu hivi.
Andika maswali ubaoni kuhusu maneno na picha zinazoonekana kwenye pakiti, kopo au boksi ( angalia Nyenzo Rejea 3 ). Ama waambie wanafunzi wayasome au uwasomee.
Ama chezesha mchezo wa ugunguzi wa maneno katika vikundi (angalia Uchunguzi Kifani 2) au waambie wanafunzi waandike majibu wenyewe. Panga muda wa ziada wa mazoezi na wa kutoa msaada zaidi kwa ajili ya wanafunzi ambao hawawezi shughuli hii.
Katika somo linalofuata, waambie wanafunzi wafanye kazi katika vikundi vilevile wabuni maandishi na taarifa zinazoonekana kwa ajili ya kifaa cha kweli au picha ya bidhaa za dukani.
Kiambie kila kikundi kioneshe na kuzungumzia kuhusu ubunifu/mchoro wao kwa wanafunzi wote darasani.
Wanafunzi wamejifunza nini kwa kusoma orodha ya bidhaa za dukani na kwa kuchora na kuonesha vifaa vyao wenyewe vya kuhifadhia bidhaa hizo? Linganisha mawazo yako na mapendekezo yaliyopo katika Nyenzo Rejea 3 .
Somo la 3
Kusoma na kuandika kunaweza kusisimua na kuchangamsha sana, lakini baadhi ya wanafunzi wanajenga mtizamo hasi kuhusiana na shughuli hizi. Sababu inaweza kuwa ni kwa vile wanagundua kuwa kusoma na kuandika ni kugumu, labda kwa sababu wanaweza kuchoshwa na kazi za usomaji na uandishi ambazo zinafuata ruwaza zilezile daima, au labda hawaoni thamani kubwa katika usomaji na uandishi. Moja ya changamoto zako kama mwalimu ni kuamsha ari ya wanafunzi katika usomaji na uandishi na kuwafanya wahamasike.
Uchunguzi Kifani 3 na Shughuli Muhimu vinapendekeza shughuli ambazo zinaweza kuwasaidia wanafunzi wafurahie na wajiamini zaidi katika usomaji na uandishi.
Uchunguzi kifani ya 3: Kusoma alama zinazopakana jirani na eneo lako na kuandika maelezo kuhusiana na alama hizo
Bwana Richard Limbunga hufundisha Kiswahili Darasa la 5 jijini Dar es Salaam. Dar es Salaam ni eneo lenye watu wengi na mifano mingi ya chapa za kimazingira kuzunguka shule –mifano mingi zaidi ni ya Kiswahili lakini pia kuna mifano kutoka katika lugha mbalimbali za asili.
Ili kuongeza kipato watu wameanzisha ‘biashara za uani’ kama vile maduka ya bidhaa ndogondogo za dukani, sehemu za kunyolea, warepeaji magari na vibanda vya simu. Sehemu zote hizi zina alama na baadhi pia zina matangazo ya kibiashara kwa ajili ya bidhaa mbalimbali. Hizi ni shule, kliniki, sehemu na kumbi za kuabudia, ambazo nyingi yazo zina alama na mbao za matangazo. Katika barabara kuu, kuna alama sehemu nyingi, zikiwemo Chuo Kikuu maarufu cha Dar es Salaam.
Bwana Limbunga alipanga safari kuzunguka Dar es Salaam ambayo ingewapatia wanafunzi fursa ya kusoma na kutengeneza kitini na michoro kuhusu mifano mbalimbali ya chapa na maumbo yanayoonekana. Pia aliandaa orodha ya maswali ili kuongozo uchunguzi wao.
Bwana Limbunga anao wanafunzi 58 katika darasa lake, wakiwemo kumi ambao wamewasili hivi karibuni kutoka Burundi. Aliamua kuwaomba wastaafu wawili wanaojua lugha nyingi wamsaidie katika shughuli hii. Mmoja anaongea Kirundi, lugha ya wanafunzi kutoka Burundi. Vikundi vitatu vya darasa lile vilikwenda safari.
Marafiki wa Bwana Limbunga walishiriki katika mjadala darasani na kwenye shughuli zilizofuata za usomaji na uandishi. Kufikia mwishoni mwa wiki, watu wale watatu walikubali kuwa wanafunzi wamejua zaidi jinsi taarifa inavyoweza kuwasilishwa kwa njia mbalimbali na kwa lugha mbalimbali na baadhi walionekana wamefurahia zaidi usomaji na uandishi kuliko hapo awali.
Shughuli muhimu: Kusoma Alama
Kabla ya somo, soma Nyenzo Rejea 4: Kujiandaa kwa matembezi ya kijumuiya ili kupanga matembezi na kuandaa maswali yako. Andika maswali ubaoni.
Ili kuanza somo, waambie wanafunzi kuhusu matembezi na, kama wanaweza, waambie wanakili yale maswali kutoka kwenye ubao. Kama hawawezi, andaa orodha ya maswali kwa kila kiongozi wa kikundi kwa ajili ya kuwauliza katika matembezi.
Wachukue kwa ajili ya matembezi yaliyopangwa mpaka kwenye jumuiya yenu mnayokaa.
Wakiwa wanatembea, lazima watoe au waandike majibu ya maswali na wachore mifano ya chapa au picha wanazoziona.
Baada ya muda, waambie wanafunzi kwenye vikundi washirikishane kile walichokiona, walichokiandika na walichokichora. Liambie darasa zima liripoti na lirekodi pointi muhimu ubaoni.
Kiambie kila kikundi kichore, kiandike jina na kichore alama, ilani au tangazo wanalofikiri ni muhimu kuwapo katika jumuiya zao. Wasaidie katika maneno yoyote magumu. Watoto wadogo wanaweza kuhitaji kufanya kazi kwenye vikundi vidogo vyenye mtu mzima wa kuwasaidia.
Kiambie kila kikundi kioneshe mchoro wao darasani kisha kieleze uteuzi wa lugha, maumbo na taarifa.
Onesha michoro hii darasani ili wanafunzi wote waisome.]]>
Kusoma na Kuandika kwa madhumuni mbalimbali