KWA_KUREJELEA_UTENZI_WA_AL_INKISHAFI_ONY.docx (Size: 55.38 KB / Downloads: 0)
]]>
https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1986
Tue, 04 Jan 2022 04:03:30 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1986CHIMBUKO LA VINA NA MIZANI KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI
Mazrui na Syambo (1992:43) wanadai kuwa utafiti katika fasihi ya Kiswahili unadhirisha ya kwamba ushairi umeanza na zile nyimbo za kale.…….. nyimbo hizi ni zile zilizokuwa zikiimbwa katika hafla mbalimbali: harusini, unyagoni, mavunoni, pungwani na kadhalika na inaonekana hazikuwa na utaratibu wa vina na mizani.
Sitaki kuchimba sana kuhusu chimbuko la ushairi wa Kiswahili kwani lengo ni kuchunguza na kubaini vina viliibukaje au vilitokea wapi mpaka kuwepo katika ushairi wa Kiswahili.
VINA NA MIZANI.
TUKI (2003:94) wanadai mizani ni jumla ya silabi zilizomo katika kila msitari wa ubeti. Wanaendelea kwa kusema, hizi ndizo zileatazo urari wa mapigo, kwani kila msitari watakiwa uwe na mizani sawa na mistari mingine (au wakati mwingine ule msitari uwe nusu ya mizani ya msitari mmoja).
Nao Mazrui na Syambo (1992:40) wanasema mizani ni hesabu au idadi ya silabi katika neno au katika kifungu cha maneno (kama mshororo wa ubeti).
Kabla ya kuchambua fasili hizo za mizani, ni vema tukaitizama pia dhana ya vina kisha tuvitazame kwa pamoja.
Mazrui na Syambo (1992:40) wanafasili vina kama sauti au silabi za aina moja zinazopatikana mwisho wa kipande au mwisho wa mshororo wa kila ubeti.
Aidha, kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili Sanifu ya TUKI (2004), kwa kuegemea katika nyanja ya fasihi, mizani ni idadi ya silabi katika msitari wa shairi na utenzi.
Kwa ujumla, vina ni ufanano wa silabi za sauti za mwisho wa kila msitari (mshororo) wa ubeti wa shairi au utenzi (utendi). Ufanano huu waweza kujitokeza katikati kwa maana katika kila kipande kwa shairi lenye vipande viwili au mwishoni au vyote kwa pamoja (yaani kati na mwisho).
Kwa mfano:
Kijana sina maisha, magenge yanishawishi,
Ukata taniuisha, tuibe ili kuishi,
Arobaini zikisha, kipigo mwisho kuishi,
Maisha haya ni kifo, kifo si kukata roho.
Katika ubeti huo, kina cha kati ni –sha na kina cha mwisho ni “-shi”; lakini kuna uwezekano shairi la vipande viwili likawa na vina mwishoni lakini lisiwe na vina katikati.
Mizani ni idadi ya silabi katika mshororo (msitari) wa shairi au utenzi. Idadi hiyo inaweza kuwa na ulinganifu au isiwe na ulinganifu kwa kila mshororo au ubeti kutegemeana na bahari husika.
Kwa mfano:
Alibino kauwawa,
Mwuwaji ana kiganja,
Maswali kaelemewa,
Adai kweli kachinja,
Uchunguzi wendelea.
Katika ubeti huo, kila mshororo (msitari) una mizani nane.
CHIMBUKO LA VINA NA MIZANI KATIKA USHAIRI
Mazrui na Syambo (1992:43), wakiitetea hoja yao kuwa ushairi umetokana na nyimbo, wanataja mambo makuu matatu yaliyopelekea kuibuka kwa mbinu ya vina na mizani katika ushairi wa Kiswahili; nayo ni: mdundo katika nyimbo, methali za Kiswahili na athari za kigeni. Baada ya kuyachambua mawazo yao nimebaini kuwa, mambo wanayoyataja kama sababu za kuzuka kwa vina na mizani ni mitazamo mitatu tofauti katika kujadili na kuchunguza chimbuko la mbinu hizi za utunzi, kwa kuwa wao hawathibitishi moja kwa moja kuwa zote zilipelekea, tuzitazame hoja hizo.
Hitaji la kuongeza ladha ya mdundo katika nyimbo
Mazrui na Syambo (1992:43) wanasema kuwa pole pole, manju wa Kiswahili, katika kujaribu kuongeza ladha katika nyimbo zao walianza kutumia mbinu za vina na baadaye mizani. Huo ukawa mwanzo wa elimu arudhi, (elimu ya kanuni na kawaida za ushairi zilianza kuwa na nguvu).
Nakubaliana na wataalamu hawa kwa kuwa ili wimbo usisimue ni sharti uwe na mdundo mzuri, kwa hivyo, katika uboreshaji wa mdundo, kuna uwezekano mkubwa kwamba manju walizidi kutia vionjo katika nyimbo kiasi cha kufikia kuweka vina na mizani, nyimbo zikanoga na msisimko ukashamiri na kwa hivyo ndio kikawa chanzo hasa cha vina na mizani katika ushairi wa Kiswahil.
Athari ya methali za Kiswahili
Utanzu wa methali unaaminika kuwa ni mkongwe na yawezekana ndio ulioasisi matumizi ya mbinu za vina na mizani. Mazrui na Syambo (1992:43) wanatoa mifano mitatu ya methali ambazo zimezingatia mbinu hizi zote.
(1) Haraka haraka
Haina baraka.
(2) Haba na haba
Hujaza kibaba
Methali zote mbili zimezingatia mbinu ya vina kwa kuwa silabi za mwisho katika methali (1) zinafanana, zote ni “ka” na katika methali (2) kuna ufanano wa silabi “ba” inayojitokeza katika kila msitari.
Hali kadhalika, katika methali (1) kuna ulinganifu wa idadi ya silabi katika kila msitari (mizani) kama inavyodhihirika hapa chini.
(1) Ha-ra-ka ha-ra-ka (mizani sita)
Ha-i-na ba-ra-ka. (mizani sita).
Kutokana na uhalisia wa baadhi ya methali kutumia mbinu hizi, na kwa ukweli kwamba methali zimekuwepo siku nyingi; kuna uwezekano mkubwa kwamba washairi walioanza kutumia vina na mizani waliathiriwa na tabia ya baadhi ya methali kwa kuwa methali pia zina mchango mkubwa katika suala la maudhui na na kuchopekwa kama zilivyo katika mashairi mbalimbali.
Athari za kigeni
Hii inaelezwa kuwa sababu nyingine iliyoleta vina na mizani katika ushairi wa Kiswahili. Wageni hawa hasa Waajemi na Waarabu walipokuja (kuhamia) mwambao wa Afrika ya Mashariki waliathiri utunzi wa ushairi wa Kiswahili kwa kuwa wao walianza kutunga mashairi yaliyokuwa na arudhi na miundo yao waliyokuja nayo. Mazrui na Syambo (1992) wao wanawataja baadhi ya watunzi waliotunga mashairi yaliyokuwa na vina na mizani hapo zamani. Nao ni Fumo Liyongo ambaye mashairi yake yaliimbwa katika ngoma za “gungu” na ‘kisarambe”. Kadhalika alitunga mashairinmengine mengi tu ya tumbuizo na ukawafi.
Mwingine ni Aidarusi, huyu alipata kuishi karne ya 17; Aidarus alitafsiri wasifu wa Mtume Muhammad uliokuwa umeandikwa kwa lugha ya Kiarabu (yeye aliutafsiri kwa mfumo wa ushairi). Inadaiwa kuwa tafsiri hii ilitumia Kiswahili cha kale sana, nayo iliitwa, Hamziya.
Mnamo karne ya 18, uliibuka utenzi au utendi, utenzi huu ulikuwa na vina na mizani; miongoni mwa tenzi (tendi) za kale ni Chuo cha Utendi au Utendi wa Tambuka, au Utendi wa Herekali uliotungwa na Bwana Mwengo wa Athumani; utenzi huu unasimulia vita vilivyotokea baina ya majeshi ya Mtume Muhammad na yale ya mfalme Herakliosi wa Wayunani.
Utenzi mwingine ni ule uliotungwa na mtoto na mrithi wa Bwana Mwengo wa Athumani, huyu aliitwa Bakari wa Mwengo, nazo ni Utenzi wa Katirifu na Utenzi wa Mwana Fatuma.
Utenzi wa Inkishafi wa Sayyid Abdalla ni utenzi mwingine uliopata kutungwa ukizingatia vina na mizani.
Washairi waliotajwa wote ni wakazi wa sehemu ya Pate na ushairi wao ulikuwa na vina na mizani.
Nako Lamu kulikuwa na watunzi kama Zahindi Mgumi, Muhammad al- Lami, Mwenye Shehe Ali na Mtunzi wa Kike Saada (kwa uchache). Hawa, utunzi wao ulichochewa na na vita baina ya Mombasa na Lamu na Oman hali iliyopelekea kutungwa kwa mashairi ya Kisiasa.
Inasemekana kuwa Lamu iliathiri maeneo mengine jirani ikiwemo Pemba, Unguja, Mombasa, Tanga na kusambaa zaidi katika maeneo mengine.
Watunzi wote wa wakati huo waliathiriwa na utunzi wa Kiarabu ulioenea hasa kupitia dini ya Uislamu na hivyo washairi wa ushairi wa Kiswahili wakaanza kutumia kawaida za wageni hawa ikiwemo vina na mizani.
Athari nyingine ni ile ya ujio wa wakoloni wa Kiingereza ambao waliathiri utamaduni wetu, miongoni mwa athari zake kuhama kwa hati ya maandishi kutoka hati ya Kiarabu kwenda hati ya Kilatini. “Cheche” za ukoloni ziliposhamiri, washairi wa Kiswahili kama Shaaban Robert na wengine kama Kaluta Amri Abeid, na Mathias Mnyampala (kwa uchache), walianza kutunga wakiutetea Uafrika huku wakiulaani ubaya wa ukoloni na mkoloni mwenyewe na wakati huu kulishakuwa na mwamko wa kujua kusoma na kuandika kwa mwafrika.
HITIMISHO
Kwa ushahidi wa wazi kabisa, chanzo cha ushairi ni mahitaji ya jamii kutumia lugha kwa ajili ya mawasiliano, kwa hivyo ni sahihi kuwa kwa vyovyote vile ushairi wa awali haukuwa na vina wala mizani bali maendeleo ndiyo yaliyoleta kaida hizi. Kwa hivyo, ushairi wa mwanzo haukuwa na vina na mizani bali kawaida hizo ziliibuka mbele ya safari ndefu ya ushairi wa Kiswahili kama ilivyoelezwa katika hoja za utetezi.
Bibliografia
Mazrui, A. M. na Syambo, B. K. (1992). Uchambuzi wa Fasihi. Nairobi: East African Educational Publishers.
Mulokozi, M. M. na Sengo, T. S. Y. (2005). History of Kiswahili Poetry: A.D. 1000 – 2000. Dar es Salaam: Institute of Kiswahili Research, University of Dar es Salaam.
TUKI. (2003). Makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili (III): Fasihi. Dar es Salaam: TUKI.
TUKI. (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Nairobi: Oxford University Press.
]]>CHIMBUKO LA VINA NA MIZANI KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI

https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1935
Mon, 03 Jan 2022 03:41:33 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1935KWA KUREJELEA UTENZI WA AL-INKISHAFI, ONYESHA NI VIPI HISTORIA HUCHANGIA KATIKA KUIBUA KAZI YA FASIHI
Ni kweli kila jamii ina fasihi simulizi yake tofauti na jamii nyingine. Utofauti huo unatokana na mambo mbalimbali kama vile:
- Mila na desturi
- Mazingira
- Amali
- Historia ya jamii husika
- Misingi ya asili ya jamii husika
Misingi ya jamii ndio msingi wa fasihi ya jamii husika na utofauti wa misingi hiyo ya kila jamii hufanya kila jamii iwe na fasihi simulizi yake.
2. “Fasihi simulizi iko Afrika tu! Ulaya hakuna fasihi simulizi!” Jadili kauli hii.
MAJIBU
Jamii za ulaya haziamini juu ya kuwepo kwa fasihi simulizi, wao wanaamini kuwa maandishi “Litera” ndiyo fasihi pekee. Fasihi za Kiafrika huchukuliwa kuwa ni ushenzi (kutostaarabika) na ushamba. Fasihi simulizi ya Afrika kwa asili haiwekwi katika maandishi kutokana na uwasilishwaji wake na umuhimu wake. Miongoni mwa fasihi simulizi za Afrika ni:
Jando na Unyago, haya ni mafundisho ambayo hutolewa kwa vijana wa kiume na wa kike mtawalia. Mafundisho haya humjenga kijana wa kiafrika kuwa mchapakazi, muadilifu na mtetezi wa jamii yake.
Matambiko, ni ibada zinazowapa waafrika fursa ya kuwasiliana na Mungu wao na kuelezea mahitaji yao ili kupata ufumbuzi. Matambiko husaidia jamii kudumisha umoja na mshikamano na kutatua changamoto zao za kiimani. Jamii za ulaya huona matambiko kuwa ni dhambi.
Ngoma, ni fasihi simulizi ya kiafrika ambayo hutumiwa kuburudisha, kuelimisha na kuleta jamii pamoja katika matukio mbalimbali ya kijamii yafuraha au huzuni. Kila jamii huwa na ngoma yake na hutambulishwa kwa hiyo.
Hadithi za kimapokeo, hutumiwa kupitishia maarifa ya kijamii kwa vizazi vijavyo kupitia masimulizi ya mambo hayo kwa vijana na watoto. Hadithi kama ngano, vigano, tarihi na visasili hubeba amali mbalimbali za jamii.
Miviga, ni fasihi simulizi ya kiafrika ambayo hufanyika msimu wa mavuno na huambatana na sherehe za kijamii kama kusimika viongozi, kumtoa mwari au kuwapeleka vijana jandoni. Miviga hutumiwa pia kuwaleta watu pamoja na kuwasahaulisha watu madhila mbalimbali yanayowakabili.
Kwa ujumla fasihi simulizi inapatikana Afrika kwa kiasi kikubwa kutokana na mazingira na mahitaji ya jamii husika.
3. “Wa mbili havai moja na maskini akipata matako hulia mbwata.” Eleza maana na dhima ya semi hizi.
MAJIBU
Katika maisha kila mtu amepangiwa bahati yake. Kuna ambao kupata ni kawaida na kuna wale ambao kupata sio kawaida. Makundi haya mawili ya watu yanazaa methali mbili ambazo ni “Wa mbili havai moja” na “Maskini akipata matako hulia mbwata.” Methali hizi zinafafanuliwa kama ifuatavyo:
Wa mbili havai moja, methali hii inamaana kuwa alichopangiwa mtu na mola ndicho atakachopokea hata kama patatokea watu wenye chuki na husuda dhidi yake. Kuna watu huwa hawafurahishwi na mafanikio ya watu wengine kiasi cha kufanya mipango ya kukwamisha mafanikio ya mtu mwingine.
Dhima ya methali hii ni kuwahamasisha watu kuongeza bidii katika kutafuta mafanikio yao badala ya kuhangaika kuzuia mafanikio yaw engine ambayo hasa ni mipango ya Mungu.
Maskini akipata matako hulia mbwata, methali hii inaelezea tabia ya baadhi ya watu kuonesha ufahari na kujitapa pindi wanapopata mafanikio kidogo maishani mwao. Watu hawa hasa ni wale ambao hawaamini kama wanastahili kufanikiwa ndio maana wakipata kila mtu atajua na wanaona fahari.
Dhima ya methali hii ni kuwatahadharisha watu kutoonesha ufahari wanapofanikiwa kwa kujua kuwa mafanikio huweza kuwa ya muda nay a kupita lakini utu na uhusiano mwema hudumu daima.
Kwa ujumla methali ni kipengele muhimu cha semi chenye kuhifadhi na kurithisha hekima na busara za jamii.
Chapuzo ni fasihi simulizi itumiwayo sana kuchochea na kuhimiza kazi katika jamii. Nyimbo za kuchapuza hutofautiana kulingana na kazi husika, kwa mfano.
Chapuzo za wakulima, hizi huitwa wawe na huimbwa wakati watu wakiwa shambani. Wawe huimbwa kufuatana na mapigo ya zana, mathalan kupanda na kushuka kwa jembe wakati wa kulima. Nyimbo hizi ni maarufu sana kwa jamii ya wasukuma.
Chapuzo za wavuvi, hizi huimbwa na wavuvi wawapo majini katika shughuli zao hasa usiku. Nyimbo hizi huitwa kimai. Hutumika kuwaondolea wavuvi ukiwa na unyonge.
Nyimbo za vita, hizi huimbwa na wanajeshi msimu wa vita ili kuwapa morali wanajeshi wawapo vitani. Chapuzo huwafanya wanajeshi wasiwaze sana kuhusu madhara ya vita na kujiondolea woga na hofu ya kufa.
Kwa ujumla kazi yoyote huwa nyepesi sana iwapo itaambatana na chapuzo kama kiburudisho cha mfanyaji kazi hiyo.]]>
1. Kila jamii ina fasihi simulizi yake tofauti na jamii nyingine. Kwa vipi?

https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1887
Wed, 29 Dec 2021 08:04:23 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1887Eleza mawazo makuu yanayojitokeza katika nadharia ya Umarx kisha hakiki Tamthilia ya Kwenye Ukingo wa Thim kwa kutumia nadharia ya Ki-Marx
Sarufi ni taaluma ya lugha inayochunguza na kuchanganua vipashio na kanuni mbalimbali zinazotawala muundo wa lugha, (Matinde, 2012.
Sarufi ni utaratibu wa kanuni ambazo humwezesha mtumiaji wa lugha kutunga tungo sahihi zinazoeleweka mara zinapotamkwa. (Kapinga, 1983).
Dhana ya sarufi inatafsiriwa katika mitazamo tofauti lakini yenye kuhusiana. Mtazamo wa kwanza tunaweza kusema Sarufi ni taaluma ya uchambuzi walugha inayojumuisha viwango vyote vya uchambnuzi yaani kiwango cha umbo sauti (fonolojia), kiwango cha umbo neno (fonolojia), kiwango cha miundo maneno (sintaksia) na kiwango cha umbo maana(semantiki), (Massamba, 1999).
DHANA YA SARUFI MIUNDO VIRAI
Sarufi muundo virai ni mkabala wa kimapokeo ambao haujihusishi na sarufi miundo katika marefu na mapana yake, ambapo zilijihusisha sana na sentensi sahili, (Massamba 1999).
Sarufi muundo virai ni kitengo cha sarufi geuza maumbo zalishi, ambacho hujikita katika matumizi ya sheria chache kuzalisha sentensi nyingi zisizo na kikomo, ambazo zina usarufi na hata zile ambazo hazijawahi kutungwa, ( Matinde, 2012).
Sarufi muundo virai ni mpangilio wa vitu vidogo vilivyowekwa pamoja na kujenga kitu kikubwa zaidi. Sarufi miundo virai ni mkabala wa kuchambua lugha kwa kuigawa sentensi katika virai vinayoiunda na kasha kuvichanganua zaidi hadi kufikia neno mojamoja lililokiunda kirai, (Massamba, 2001).
DHANA YA SARUFI GEUZI
Ugeuzi ni utaratibu unaotumiwa kubadili umbo la tungo kuwa umbo jingine kwa kutumia kanuni maalumu. Kwa hiyo ugeuzi ni mbinu ya kisarufi ambayo hutumiwa katika sarufi geuza maumbo zalishi kuzalisha sentensi lukuki kwa kufuata sheria mahususi, (Matinde, 2012).
Sarufi geuzi hueleza ujuzi wa lugha ambao msemaji mzawa anao ujuzi anaomwezesha kutumia lugha (Habwe na Karanja,2007).
Sarufi geuzi maumbo ni utaratibu wa kubadili maumbo kuwa maumbo meng kwa kufuata kanuni maalumu (Matinde,2012).
Zifuatazo ni tofauti kati ya sarufi miundo virai na sarufi geuzi:
Hutofautiana katika lengo. Lengo la sarufi muundo lilikuwa halifahamiki zaidi ya kutumia taratibu za kijarabati zinazohusu ukusanyaji wa data na kuzichambua pamoja na kuunda kanuni kwa kutumia data hizo. Lakini,
Lengo la sarufi geuzi liko bayana, hujitokeza dhahiri. Lengo la sarufi hii ni kufafanua umilisi wa ujuzilugha ambao huwa mwanalugha anao. Umilisi huo humfanya mwanalugha kutambua viambajengo kati ka tungo, katika mtazamo wa ndani yaani muundo wa ndani.
Hutofautiana katika miundo. Sarufi miundo virai, hii huwa inajikita katika miundo ya nje, ambayo huchunguza na kuchambua sentensi katika umbo la nje.
Mfano; Mama anakula ugali
Hivyo huonyesha tu aina ya maneno husika katika sentensi au tungo kama vile: Mama- Nomino, Anakula- Kitenzi, na Ugali- Nomino. Ilihali,
Sarufi geuzi, hii huwa imejikita katika kuchungaza sentensi kama umbo la ndani na umbo la nje. Muundo wa ndani ni uchopekwaji katika miundo hiyo ambapo muundo wan je lazima upitie katika muundo wa mofofonemiki na kuweka katika kitengo cha fonolojia.
Hutofautiana katika vitengo. Sarufi geuzi ni sarufi ambayo inafumbata vitengo vyote vya lugha ambavyo ni fonolojia, sintaksia, semantiki, na mofofonemiki ambapo kitengo cha fonolojia hushughulikia sauti za lugha, kitengo cha kisintaksia hushughulika na uundaji wa sentensi, kitengo cha semantiki hushughulika na ufasili wa maana, na kitengo cha mofofonemiki huwa na kazi ya kuibadili njeo za wakati. Ilihali
Sarufi miundo virai hufumbata kitengo cha mofolojia ambapo sentensi iligawanywa katika kiunzi cha aina za maneno kama Nomino, Kitenzi, Kivumishi, Kielezi na kihunzi hicho kilijulikana kama utaratibu wa uchanganuzi wa viambajengo.
Hutofautiana katika uhusiano wa sentensi. Sarufi geuzi ilipiga hatua kubwa, kwanza huonyesha uhusiano uliopo kati ya maumbo mbalimbli ya sentensi au tungo. Na pia kuonyesha uhusiano unaoweza kuwepo baina ya sentensi moja na sentensi nyingine.
Mfano: (1) Mtoto mrefu anacheza, na si kusema kuwa Mtoto anacheza mrefu
Huu ni uhusianao kati ya maumbo.
Mfano: (2) Juma alipiga mpira
Mpira ulipigwa na Juma
Huu ni uhusiano wa sentensi moja na sentensi nyingine. Ilihali
Sarufi miundo virai haionyeshi uhusiano kati ya sentensi moja na sentensi nyingine.
Hutofautiana katika uwazi. Sarufi geuzi huonesha sentensi sahihi na ambazo sio sahihi pia huonesha sentensi ambazo zinakubalika na sentensi zisizokubalika kwa msemaji mzawa. Ilihali
Sarufi miundo virai yenyewe haina uwazi huo.
Hitimisho ni kwamba, Sarufi geuzi ilianzishwa kutokana na mapungufu katika sarufi muundo virai. Sarufi iliyokuwepo, sarufi miundo virai, ilishindwa kuonyesha mahusiano yaliyokuwepo baina ya sentinsi zinazo husiana kimaana. Hivyo kutokana na upungufu huo kulikuwa na haja ya kuonyesha uhusiano huo.
MAREJELEO
Kapinga,M.C.(1983). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA). Dar-es-Salaam:
TUKI.
Massamba, D.T., Kihore,M.Y.& Hokororo.(1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu
(SAMIKISA). Dar-es-Salaam: TUKI.
Matinde,S.R.(2012). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia. Mwanza: Serengeti Educational
Publishers (T) LTD.
]]>Swali: Sarufi miundo virai inatofautianaje na sarufi geuzi?
DHANA YA SARUFI

https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1641
Thu, 02 Dec 2021 16:57:23 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1641SWALI: Eleza kwa mifano Kiima na Kiarifu na vijenzi vyake.
James, J na Faustino, M (2014) wanasema Kiima ni kipashio ambacho, aghalabu hutokea kabla ya kitenzi. Kipashio hiki hutaja mtenda au mtendwa wa jambo linaloelezwa kwenye tungo.
Hao hao Oxford wanasema Kiarifu ni sehemu kkatika sentensi inayotoa taarifa kuhusiana na kiima. Ni sehemu inayoeleza kiima kimetenda nini, kimetendwa nini au kikoje.
Mdee, J. S (1999) anaeleza kuwa Kiima ni sehemu ya sentensi ambayo hutaja mtenda wa jambo linaloelezwa. Kiima aghalabu hutokea kushoto kwa kitenzi katika tungo.
Mdee anaeleza Kiarifu kuwa ni sehemu inayojazwa na neno au maneno yanayoarifu tendo. Kiarifu ndiyo sehemu muhimu zaidi katika tungo ambayo wakati mwingine huweza kusimama pekee bila kiima kwani huchukua viambishi viashiria kiima.
Vipashio vya Kiima
Mdee anafafanua kuwa Kiima kinaweza kujengwa na vipashio mbalimbali kama vifuatavyo:
Nomino
Mfano:
Mtoto anasoma
Juma anakimbia
Kiwakilishi
Mfano:
Yeye haishi hapa
Sisi tutaondoka pamoja
Yule hataki kuondoka
Wangu wanifuate
Nomino na Kivumishi
Mfano:
Watoto wote wameondoka
Wasichana wazuri wamewasili
Kitabu kidogo kuliko vyote kimeuzwa
Nomino na kishazi tegemezi kivumishi
Mfano:
Mtoto aliyeingia hapa amefiwa
Kisu kilichopotea kimeonekana
Kalamu iliyoisha wino imetupwa
Kitenzi nomino na Kivumishi
Mfano:
Kuimba kwenu kulitufurahisha
Kuja kwao kulitutia faraja
Vipashio vya Kiarifu
Kwa mujibu wa James Mdee Kiarifu kinajengwa na prediketa, kijalizo au chagizo kama ifuatavy:
Prediketa
Hii ni sehemu ya sentensi ambayo hujazwa na aina yoyote ya kitenzi (kishirikishi, kisaidizi au kitenzi kikuu). Prediketa ndiyo sehemu muhimu ambayo sentensi inapaswa kuwa nayo.
Mfano:
Juma ni mwanangu
Ali anasoma kitabu
Maria alikuwa anapika chakula jikoni
Asha yupo chumbani
Kijalizo
Hii ni sehemu ya sentensi ambayo hujazwa na nomino au kikundi nomino katika kiarifu. Nomino au kikundi nomino hiki huwakilisha mtendwa, mtendea au kitendea. Kijalizo hufuata kitenzi katika sentensi iliyo nacho. Kijalizo ni kipashio kisichojitokeza katika kila sentensi. Hutokea katika sentensi yenye kitenzi kinachohitaji kukamilishwa na nomino au kikundi nomino.
Mfano:
Baba analima shamba
Watalii wanaangalia nyumba mpya zilizojengwa
Malima ni mwalimu mpole
Nimempatia rafiki yangu kalamu
Chagizo
Hii ni sehemu ya sentensi inayojazwa na kielezi au kikundi kielezi cha aina yoyote kama vile vielezi vya idadi, namna, wakati au mahali kitendo kilipofanyika. Chagizo huweza kutokea mara baada ya kitenzi au kijalizo kutegemeana na muundo wa sentensi inayohusika, na vipashio vilivyomo.
Mfano:
Mama anasoma barua kimya
Mama anasoma kimya
Tutaondoka alfajiri na mapema
Watoto wanacheza uwanjani
Nimeondoa vitabu vyote mezani
Kwa ujumla Kiima na Kiarifu ni istilahi za sarufi mapokeo ambayo huitazama sentensi na vipashio vyake kiuamilifu (kikazi). Kwa wanamapokeo kila istilahi katika tungo ina kazi maalumu ambayo huitambulisha istilahi husika.
MAREJELEO
James, J na Faustino, M (2014) Kiswahili Kidato cha Tano na Sita. Oxford University Press. Dar es Salaam.
James, J. S (1999) Sarufi ya Kiswahili: Sekondari na Vyuo. DUP. Dar es Salaam.
]]>SWALI: Eleza kwa mifano Kiima na Kiarifu na vijenzi vyake.

https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1639
Thu, 02 Dec 2021 16:42:32 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1639(a) Tathmini dhana ya sintaksia kwa ujumla au fasili ya sintaksia kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali
(b) Eleza jinsi sintaksia inavyohusiana na viwango vingine vya sarufi
Jibu
Katika kujadili mada hii, kwanza tuangalie fasili ya sintaksia kwa mujibu wa wataalam mbalimbali, fasili ya lugha, tutafafanua uhusiano uliopo kati ya sintaksia na vitengo vingine vya lugha na mwisho tutatoa hitimisho juu ya mjadala wetu.
Kwa mujibu wa Massamba na wenzake (1999) Sintaksia ni utanzu wa sarufi unaojihusishana uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipashio vyake. Wanaendelea kusema, utanzu huu huchunguza sheria au kanuni zinazofuatwa katika kuyapanga maneno ili yalete maana inayokubalika na kueleweka katika lugha husika.
Habwe na Karanja (2004) wanasema Sintaksia ni utanzu wa isimu unaoshughulikia muundo wa sentensi na elementi nyingine zinazounda sentensi kama vile kategoria za maneno, vikundi na vishazi.
TUKI (2004) wanasema “sintaksia ni tawi la isimu linaloshughulikia uchanganuzi wa taratibu na kanuni za mahusiano baina ya maneno katika tungo” kwa ufupi sintaksia ni tawi la isimu ambalo linachunguza muundo wa tungo pamoja na uhusiano wa vipashio hivyo vinavyounda tungo ambayo ni nukta pacha, neno, kirai na kishazi.
Radford (1981) anasema isimu miundo au sintaksia ni taaluma inayojishughulisha na namna maneno yanavyoweza kupangwa pamoja kutoa muundo wa sentensi. Radford anaangalia jinsi neno moja linavyoweza kujihusisha na neno lingine na kutathmini muundo uliosahihi.
Kutokana na fasili hizi inaonekana kuwa Massamba na wenzake wamefafanua zaidi kwa kuonesha kuwa licha ya kuzingatia kanuni na sheria za kupanga maneno lakini pia ni lazima maneno hayo yawe na uhusiano. Kwa upande mwingine Habwe na Karanja wameshindwa kuelezea suala hili, wao wanaona sintaksia inashughulika na muundo wa sentensi na vipashio vyake.
Kwa mantiki hii tunakubaliana na fasili ilyotolewa na Massamaba na wenzake kuwa Sintaksia ni utanzu wa sarufi unaojihusisha na uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipashio vyake, kwa kuzingatia sheria na kanuni za lugha husika ili kuleta mawasiliano.
Katika fasili ya lugha, wataalam wengi wanakubaliana kuwa lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao. Baadhi ya wataalam wanao kubaliana na fasili hii ni Massamba na wenzake (Wameshatajwa).
“Kitengo” kwa mujibu wa TUKI (2004) ni mahali pateule palipotengwa kwa shughuli maalum. Tunaporejea katika muktadha wa lugha tunaweza kusema kuwa vitengo vya lugha ni vipengele muhimu vinavyounda maarifa ya lugha kwa ujumla. Kwa fasili hii, vipengele vinavyounda maarifa ya lugha ni fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki.
Kwa hiyo kutokana na kwamba sintaksi pia ni kitengo kimojawapo kinachounda maarifa ya lugha, tunakubali kwamba, sintaksia haiwezi kutenganishwa na vitengo vingine vya lugha kutokana na uhusiano mkubwa uliopo baina ya vitengo hivi. Vitengo hivi hutegemena na kuathiriana. Hivyo basi tunaweza kuonesha jinsi sintaksia isivyoweza kutenganishwa na vitengo vingine vya lugha yaani fonolojia, mofolojia na semantiki kama ifuatavyo:
Uhusiano baina ya fonolojia na sintaksia.
Massamba na wenzake (Wameshatajwa) wanafasili fonolojia kuwa ni uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha mahususi. Wanaendelea kusema ni jinsi ambavyo vitamkwa au sauti za lugha zinavyoungana ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha.
Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa kuungana kwa vitamkwa ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha fulani hutegemea mpangilio sahihi wa vitamkwa. Na kwa kuwa neno ni kiwango cha msingi cha uchambuzi katika sintaksia basi fonolojia ina uhusiano wa moja kwa moja na sintaksia. Mifano ifuatayo huthibitisha hoja hii:
Mfano 1.“Anapika”. Hili ni neno lakini pia ni sentensi, hivyo huweza kuchanganuliwa kifonolojia kama ifuatavyo: a|n|a|p|i|k|a|, mpangilio wa sauti umeunda neno “anapika”.
Mfano 2. (a) baba. Limeundwa na (KIKI).
(b). abab. Limeundwa na (IKIK).
Katika mfano 2(a) tunaona neno “baba” lina maana na limefuata kanuni na mpangilio unaokubalika wakati mfano 2 (b) neno “abab” halina maana katika lugha ya Kiswahili kwa sababu halina mpangilio mzuri wa fonimu.
Kwa mifano hii tunaona kwamba hatuwezi kuwa na miundo mikubwa katika sentensi bila kuwa na mpangilio sahihi wa sauti katika lugha. Kwa hiyo sintaksia haiwezi kukamilika bila fonolojia.
Uhusiano baina ya mofolojia na sintaksia.
Mofolojia ni kitengo kingine cha lugha ambacho kwa mujibu wa Rubanza (1996) ni taaluma inayoshughulikia vipashio vya lugha katika kuunda maneno. Kutokana na fasili hii, kipashio cha msingi katika uchambuzi wa kimofolojia ni neno ambalo ndilo hutumika kuunda darajia ya sintaksia.
Vilevile maumbo ya kimofolojia huathiri vipengele vingine vya kisintaksia, kwa mfano, sentensi zifuatazo hufafanua zaidi:
Mtoto anacheza.
Watoto wanacheza.
Katika mifano hii tunaona kwamba mofimu m- na wa- katika upande wa kiima zimeathiri utokeaji wa mofimu a- na wa- katika upande wa kiarifu.
Pia kanuni za mfuatano na mpangilio wa mofimu au viambishi zikifuatwa huunda maneno katika miundo ya kisintaksia. Mfano:
Alicheza = a-li-chez-a
Anaimba = a-na-imb-a
Kwa ujumla kipengele cha umoja na wingi katika maumbo ya kimofolojia ndicho kinachoathiri umbo linalofuata jina na kuathiri muundo wa sentensi nzima. Mfano:
Mwalimu alikuwa anafundisha.
Walimu walikuwa wanafundisha.
Tunaona katika mifano hii maumbo ya umoja na wingi ya maneno Mwalimu na Walimu yameathiri mpangilio mzima wa sentensi.
Uhusiano baina ya semantiki na sintaksia.
Habwe na Karanja wakimnukuu Richard na Wenzake (1985) wanasema Semantiki ni stadi ya maana. Semantiki ni utanzu unaochunguza maana katika lugha ya mwanadamu. Wanaendelea kusema semantiki hutafiti maana za fonimu, mofimu, maneno na tungo.
Kwa hiyo kutokana na fasili hii maana hushughulikiwa katika vitengo au viwango vyote vya lugha ambavyo ni fonolojia, mofolojia na sintaksia. Mfano:
a) Paka mweusi amepotea.
b) Mweusi paka amepotea.
c)Amepotea mweusi paka.
Katika mifano hii tunaona kwamba sentensi (a) ina maana kutokana na kwamba imefuata mpangilio sahihi wa maneno katika tungo na sentesi zilizobaki hazina maana kutokana na sababu kwamba hazijafuata mpangilio ulio sahihi.
Kwa mantiki hii, kwa kuwa semantiki hushughulikia viwango vyote vya lugha, basi hushughulikia pia kiwango cha sintaksia ambapo huangalia maana za tungo. Tungo yoyote ni lazima ilete maana inayokubalika na wazungumzaji au watumiaji wa lugha husika, kama itakuwa kinyume basi haitakuwa tungo bali ni orodha ya maneno tu.
Mfano:
Mtoto anacheza mpira uwanjani.
Mtoto uwanjani mpira anacheza.
Tukiangalia mifano hii tutagundua kwamba katika sentensi ya kwanza mpangilio wake wa vipashio unaleta maana lakini sentensi ya pili haina maana kutokana na kuwa na mpangilio mbaya wa maneno.
Kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa sintaksia haiwezi kutenganishwa na vitengo vingine vya lugha kwa kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya vipengele hivi vya lugha na kwa hiyo hutegemeana kati ya kipengele kimoja na kingine. Kwa mfano, huwezi kupata mofolojia (neno) bila kupitia ngazi ya fonolojia na pia huwezi kuwa na ngazi ya sintaksia (sentensi/tungo) bila kupitia ngazi ya fonolojia na mofolojia lakini vitengo vyote hivi hutawaliwa na kitengo cha semantika ili kuleta mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji.
MAREJELEO
Habwe, J na P. Karanja (2007). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.
Massamba, D.P.B na wenzake (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu: Sekondari na Vyuo. Dar essalaam: TUKI.
Rubanza, Y.I (1996). Mofolojia ya Kiswahili. Dar es salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
TUKI (2004).Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es salaam: TUKI.
]]>(a) Tathmini dhana ya sintaksia kwa ujumla au fasili ya sintaksia kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali

https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1593
Sun, 28 Nov 2021 07:31:31 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1593SWALI:
Kitezi cha kiswahili Mara nyingi hakiwezi kukaa peke yake kufuatana na viambishi vyenye uamilifu wa aina kadhaa, fafanua kauli hii kwa mifano ya kutosha.
Kiswahili ni lugha ambishi kama zilivyo lugha nyingine za Kibantu. Neno kiambishi lina maana ya kipashio chenye maana ambacho hufungiliwa kwenye mzizi wa neno ili kuletaKiswahili ni lugha ambishaji kama vile zilivyo lugha nyingine za Kibantu. Neno kiambishi lina maana ya kipashio chenye maana ambacho hufungiliwa kwenye mzizi wa neno ili kuleta maana inayokusudiwa. maana inayokusudiwa.
Tofauti na lugha zisizotumia viambishi kwa wingi kama vile Kiingereza ambapo msemaji huhitajika kubadilisha neno zima au kulazimika kutumia maneno mengi kwa nia ya kubadilisha kidogo tu maana iliyobebwa na kitenzi fulani, katika Kiswahili, msemaji hubadilisha tu viambishi katika kitenzi hicho hicho. Hebu tutazame mifano ifuatayo kuthibitisha madai haya. ‘He comes’ {Kiingereza} – ‘huja’ (Kiswahili); ‘He would have come’ (Kiingereza)- ‘Angalikuja’ (Kiswahili); ‘He who comes’ (Kiingereza) – Ajaye (Kiswahili) miongoni mwa mengine.
Lugha ya Kiswahili ina viambishi vya aina mbili ambavyo ni awali na tamati. Viambishi awali huwakilisha dhana tofauti za kisarufi ambazo ni pamoja na nafsi , ngeli, umoja na wingi, nyakati au njeo, urejeshi, mahali, wakati miongoni mwa nyingine. Viambishi tamati navyo huwakilisha mahali, wakati, rai na mnyambuliko.
Nafsi
Katika lugha ya Kiswahili, vambishi vya nafsi hutokea kabla ya mzizi wa neno. Viambishi hivyo ni vya aina sita: nafsi ya kwanza (umoja na wingi) nafsi ya pili (umoja na wingi), nafsi ya tatu ( umoja na wingi). Mifano : Mimi ninaimba wimbo mzuri, Wewe unatoka wapi? Yeye atakuja kesho. Tofauti inayojitokeza baina ya Kiswahili na Kihispania ni kuwa, viambishi vya nafsi vya Kihispania huja mwishoni mwa kitenzi ilhali vile vya Kiswahili hutokea kabla ya mzizi wa kitenzi. Tutaangazia mifano ifuatayo ili kuthibitisha jambo hili. Ninasoma(Kiswahili)- Leo (Kihispania), Unasoma (Kiswahili)- Lees (Kihispania), Tunasoma (Kiswahili)- Leemos (Kihispania). Herufi zilizokolezwa rangi zinawakilisha nafsi katika lugha zote mbili.
Ngeli
Tofauti na ilivyokuwa zamani, ambapo upangaji wa ngeli ulizingatia viambishi awali vya nomino, mtindo mpya unaojulikana kama upatanisho wa kisarufi unazingatia viambishi awali vya vitenzi katika kuziweka nomino katika makundi tofauti. Mifano: Kijiko kimevunjika- Vijiko vimevunjika, Uji umemwagika- Uji umemwagika.
Nyakati/Hali
Kiswahili kina nyakati tatu ambazo ni wakati uliopo, ujao na uliopita , tofauti na Kihispania ambacho kina takriban nyakati kumi na tano na Kiingereza ambacho kina nyakati mbili tu – wakati uliopo na wakati uliopita. Pamoja na nyakati hizo tatu, Kiswahili kina viambishi vya hali ambavyo pia hujulikana kama wakati kadiri ya hali. Hivi ni pamoja na: ki, ka, a, hu, me, ngali na kadhalika. Viambishi vya ( a) huwa havionyeshi wakati maalum wa kutendeka kwa kitendo kifanyavyo kiambishi (na) cha wakati uliopo. Waama, matumizi ya viambishi hivyo huwa hayaonyeshi mwanzo au mwisho wa kutendeka kwa kitendo. Mifano katika sentensi: Mama apika chakula; Wanafunzi hawa wajitahidi ; Tunda laanguka kutoka mtini; Maziwa yamwagika
Urejeshi
Huitwa viambishi vya urejeshi kwa sababu hutuarifu nomino inayorejelewa inapatikana katika ngeli gani. Vinaweza kuja kabla au baada ya mzizi. Vijapo kabla ya mzizi , huitwa ‘o’ rejeshi awali. Vitokeapo baada ya mzizi, huitwa ‘ o’ rejeshi tamati. Mifano: Jambo unalolifanya ni kinyume cha sheria (‘o’ rejeshi awali); Jambo ulifanyalo ni kinyume cha sheria (‘o’ rejeshi tamati). Muundo wa virejeshi hutofautiana kulingana na ngeli.
Mahali
Hivi huwakilisha ngeli ya mahali ya pa-ku-mu. Mifano katika sentensi: Ulipoketi pana siafu, Ulikoketi kuna siafu, Ulimoketi mna siafu. Zaidi ya kiambishi ‘po’ kutumiwa kuwakilisha mahali maalum, kinaweza kuonyesha wakati. Mfano: Utakapokuja utanikuta nikisoma. Hata hivyo, ‘po’ huwa haionyeshi wakati kamili wa kutendeka kwa kitendo hadi pale itakapoandamana na viambishi vingine; ‘napo’- wakati uliopo, ‘takapo’ – wakati ujao, ‘lipo’-wakati uliopita. Mifano katika sentensi: Anapokula hazungumzi; Atakapofika tutamlaki kwa shangwe; Alipomwona alimfanya tambiko la risasi.
]]>SWALI:

https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1535
Sun, 21 Nov 2021 11:20:47 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1535SWALI: Kujadili historia ya tamthilia ya Kiswahili nchini Tanzania tangu kuanza kwake hadi hivi sasa.
Maana ya tamthilia
Tamthilia ni utungo wa kisanaa ambao huweka wazo fulani katika matendo na mazungumzo (TUKI, 2004).
Hivyo basi tunaweza kusema kuwa tamthilia ni utungo au mchezo wa kuigiza matendo au mawazo fulani yaliyopo katika jamii, ambapo huwa ni majibizano baina ya watu wawili au zaidi.
Historia ya tamthilia nchini Tanzania
Historia ya tamthilia nchini Tanzania inaelezwa kwa kurejelea vipindi vitatu yaani kabla, wakati na baada ya ukoloni.
Kabla ya ukoloni
Kwa mujibu wa Mulokozi (1996:203), katika kitabu chake cha “Fasihi ya Kiswahili”, anaeleza kuwa kabla ya ukoloni tamthiliya zilizoandikwa ili ziigizwe jukwaani hazikuwepo , badala yake, zilikuwepo tamthiliya zisizoandikwa, zilizogezwa au kufaraguzwa kwa ajili ya kuonyeshwa kwenye shughuli maalumu, kwa mfano sherehe za jando na unyago, mazishi, kutawazwa kwa Mtemi, arusi na michezo ya watoto. Tamthilia hizo zilikuwa na sifa kadha za tamthilia yaani hadithi, vitendo, wahusika na waigizaji wao na dayolojia. Hata hivyo tamthilia hizo hazikuwepo na ploti ya K – Aristotle wala matini yaliyoandikwa na kuwa tamthilia simulizi.
Mfano mzuri wa tamthilia hizo awali ni maigizo ya watoto wakati wanapocheza mfano A, B, C na D ambapo A huwa ni baba, B huwa ni mama na C na D huwa ni watoto ambao ni msichana na mvulana ambapo mchezo huanza kwa A kumwambia B aandae chakula, B hufanya hivyo na C anakwenda kuchota maji mtoni na D anapeleka mbuzi malishoni”.
Hivyo basi kabla ya ukoloni hakukuwa na tamthilia zilizoandikwa ili ziigizwe badada yake kulikuwa na sanaa za maonyesho ambazo zilikuwa zikitumika katika shughuli maalumu mfano sherehe, michezo ya watoto wadogo pamoja na jando na unyago.
Kipindi cha ukoloni, (1890 – 1960’s)
Katika kipindi hiki jamiii nyingi za Kiafrika (Tanzania), zilikuwa zikitawaliwa na watawala kutoka nchi za Kimagharibi. Hivyo basi kazi ya tamthilia iliegemea katika utawala wa kikoloni na kupelekea kuibuka aina kuu mbili za tamthilia mpya (zisizokuwa za kijadi) yaani hazikuwa na utamaduni wa Kiswahili ambazo ni tamthilia za Kizungu na tamthilia za vichekesho. Mnamo mwishoni mwa miaka 1950 paliongezeka aina nyingine ya tamthilia ambayo ni tamthilia ya Kiswahili na kupelekea kufikia idadi kuwa tatu (Mulokozi 1996:204).
Tamthilia za Kizungu
Tamthilia hizi ni tamthilia ambazo ziliandikwa kwa lugha ya kizungu (Kiingereza) na zilizojikita katika utamaduni wa kizungu. Lengo kuu za tamthilia hizi zilikuwa ni kuburudisha Maofisa na Masetla wa Kizungu ama kufunza Biblia na imani ya Kikristo.
Katika Tanzania tamthilia za Kiingereza zilianza kuingizwa miaka ya 1920, nyingi zilichezwa mashuleni na zilitungwa na Waingereza, kwa mfano Shakespare na baadhi zilikuwa ni za dini ya Kikristo. Tamthilia hizi zilikuwa zikiunga mkono mfumo wa ubepari na ukoloni. Vilevile katika kipindi hiki kulikuwa na tamthilia chache sana zilizotafsiriwa kwa Kiswahili. Mfano tamthilia ya “Moliere Le Medecin Malge Lui” (Kifaransa “Tabibu Asiyependa Utabibu” (Kiswahili) iliyoandikwa na Morrison 1945 na kuchapwa na E.A.S huko Nairobi.
Baadaye katika kipindi hiki viliibuka vikundi viwili vya kuigiza, ambavyo ni Dar es salaam players mwaka 1947 na Arusha Little Theatre mwaka 1953. Kuanzia wakati huo tamthilia ya Kiswahili ilianza kuhusishwa katika mashindano na hivyo kuchochea utunzi wa tamthilia ya Kiswahili.
Vichekesho
Ni aina ya tamthilia – gezwa zilizotungwa papo kwa papo bila ya kuandikwa zilizokuwa na lengo la kuburudisha wenyeji, na ziliwasuta watu waliofikiriwa kuwa “Washamba” wajinga au wasiostarabika. Tamthilia hizo zilimwonyesha mhusika anayetoka shamba na kwenda kuzuzuka mjini.
Tamthilia – andishi ya Kiswahili
Tangu miaka ya 1920 mpaka 1960 mambo yaliyowakabili wanaotawaliwa yalikuwa ardhi na kujipatia uhuru. Hata hivyo tamthilia zilizoandikwa wakati huo na Watanzania hazikujishughulisha na mambo haya matatu. Katika kipindi hiki kabla ya kuchapishwa vitabu vyote, ilibidi vipitiwe kwenye Kamati ya lugha ya makoloni ya Afrika Mashariki. Hiki kilikuwa chombo cha mtawala cha kusimamia ukuzaji wa lugha ya Kiswahili. Kutokana na hali hii maandishi yoyote yale ambayo ni kinyume na ukoloni hayangeweza kuchapishwa.
Tamthilia za wakati huo zilihusu mambo ambayo kwa kiasi fulani yalisababishwa na tabaka tawala lakini hayakuchambuliwa kwa kina kuweza kutoa mwanga wa kuyatatua. Tamthilia hizi zililenga kwenye masuala yanayohusu rushwa, mapenzi, ukabila na migongano ya utamaduni. Iwapo tamthilia hizi zingegusia uondoaji wa ukabila, bali zingeweza kuchangia kuleta Umoja ambao ungetumika kunyakua ardhi ambayo ilikuwa imechukuliwa na mkoloni na hatimaye kuleta vuguvugu la kumtoa kabisa mkoloni.
Tamthilia andishi zilizoandikwa kwanza kabla ya kuingizwa jukwaani zimeanza kutokea miaka ya 1950. Tamthilia za mwanzo zilikuwa za kidini mfano tamthilia ya “Imekwisha” iliyoandikwa na C. Frank mwaka 1951 (Mulokozi 1996).
Kipindi cha Uhuru
Tanzania kuwa jamhuri mwaka 1962 kuliashiria mambo mapya kwenye tamthilia. Kwanza usomi ulipiga hatua kutokana na siasa mpya ya wananchi kujitawala wenyewe. Chuo Kikuu cha kwanza nchini kilianzishwa mwaka 1961. Serikali pia ilianzisha Wizara ya Utamaduni wa Taifa mwaka 1962. Katika kipindi hiki cha uhuru palikuwepo tamthilia za kizungu, vichekesho na tamthilia ya Kiswahili.
Katika kipindi hiki cha Uhuru Tanzania ilikuwa huru katika uendeshaji wa mambo yake hata hivyo aina kuu tatu za tamthilia ambazo zilitumika kipindi cha ukoloni ziliendelea kuwepo.
Tamthilia za kizungu
Kutokana na uhuru waliokuwa nao waandishi, tamthilia muhimu za kizungu zilianza kutafsiriwa na kuigizwa kwa lugha ya Kiswahili ili zilieleweka zaidi kwa wananchi. Mfano wa tamthilia hizo ni Juliasi Kaisari ya Shakespare na Mabepari wa Venisi iliyotafsiriwa na J. K. Nyerere kutoka lugha ya Kiingereza yaani “Julias Caesar” na “Merchants of Venis”.
Hata hivyo tamthilia zilizotafsiriwa hazikuwa za kizungu tu bali hata zile za Kiafrika zilizoandikwa kwa lugha za kigeni na lugha zingine za Kiafrika zilitafsiriwa kwa Kiswahili. Mfano; Mtawa mweusi kilichoandikwa na Ngugi wa Thiong’o, Masaibu ya ndugu Jero kilichoandikwa na Soyinka (Mulokozi, 1996, uk. 205-207).
Vichekesho navyo vilichukua sura tofauti kidogo, ambapo badala ya kuwasuta washamba zilianza kuwasuta wazungu weusi, waafrika wanaoringia elimu, vyeo na kudharau utamaduni wao. Vichekesho hivyo vilibeba ujumbe uliohusu matatizo katika jamii na matukio ya wakati huo. Baadhi ya vichekesho hivyo ni Mahoka, (1974), Pwagu na Pwaguzi (1978) vilivyokuwa vikirushwa katika Radio Tanzania kwa dhumuni la kukemea tabia mbovu za baadhi ya watu. Hata sasa vipo baadhi ya vipindi ambavyo husuta tabia hizo kama vile Futuhi (Star TV), Komedi (East Africa TV), Fataki (TBC).
Tamthilia Andishi Ya Kiswahili
Baada ya Uhuru waandishi wengi chipukizi wa tamthilia ya Kiswahili walipata hamasa ya kuandika kuhusu jamii zao. Mfano E. Hussein, Penina Muhando (Mlama), na Ngahyoma na G. Uhinga waliandika kwa kutumia foni za sanaa za maonyesho. Hivyo basi hii ilipelekea waandishi wengi kuandika juu ya hali halisi iliyopo katika jamii husika (Mulokozi, 1996).
Hitimisho
Kwa ujumla historia ya tamthilia ya Kiswahili nchini Tanzania imekuwa chachu ya mabadiliko ya kijamii ambapo waandishi wengi wamekuwa wakiandika kazi zao kutokana na mambo yanayoikumba jamii kwa ujumla kama vile rushwa, migongano ya kiutamaduni, matabaka, ugonjwa na dini ambapo imepelekea kukua kwa utanzu wa tamthilia ya Kiswahili nchini Tanzania.
MAREJELEO
Mulokozi, M. (1996), Fasihi ya Kiswahili, Dar es salaam. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
TUKI, (2004). Kamusi ya Kiswahil Sanifu. Dar es salaam. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.
]]>SWALI: Kujadili historia ya tamthilia ya Kiswahili nchini Tanzania tangu kuanza kwake hadi hivi sasa.

https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1300
Wed, 06 Oct 2021 14:38:29 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1300
Kusoma ni nini?
Kusoma kunaelezwa katika ngazi nne
(i) uwezo wa kutambua maandishi katika maumbo yake mbalimbali kwa kuyahusisha maumbo hayo na kitu, jambo au tendo.
(ii) Uwezo wa kuyakabili maandishi kwa kasi na wepesi bila kupoteza kiini chake.
(iii) Uwezo wa kuelewa maana iliyomo bila vipingamizi.
(iv) Uwezo wa kuyahusisha maandishi na uzoefu wake wa kila siku.
(v) Uwezo wa kuzingatia na kuyatumia yale yote yaliyo muhimu na kuyafanya sehemu ya maisha.
kwa kifupi kusoma ni ufumbuzi wa maandishi anaofanya msomaji. Katika mawasiliano maandishi (fumbo) – kusoma ni mawasiliano na kikomo ni macho (mapokeo), utambuzi, tafsiri, maana, uzingatiaji kumbukumbu na kadhalika wa msomaji.]]>

https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1292
Sat, 02 Oct 2021 14:24:06 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1292Ni tofauti zipi zilizopo kati ya fonimu irabu za Kiswahili na fonimu irabu za Kiingereza?
MAJIBU
Irabu ni aina ya sauti ya lugha inayotamkwa bila kuwapo na kizuizi chochote kwenye mkondo wa hewa kutoka mapafuni kupitia kinywani na puani.
Irabu za Kiswahili na zile za Kiingereza hutofautiana katika vipengele anuai kama ifuatavyo.
·Kiswahili kina irabu tano wakati Kiingereza kina irabu 20
·Kiswahili hakina irabu za kati lakini Kiingereza kina irabu za kati
·Kiswahili hakina mwambatano wa irabu mbili kwa moja lakini Kiingereza kina mwambatano wa irabu mbili kwa moja
·Katika Kiswahili irabu haiwezi kusimama peke yake lakini kwenye Kiingereza irabu huweza kusimama peke yake mf. A man
·Katika Kiswahili irabu haziwezi kutokea zaidi ya mbili zikifuatana lakini katika Kiingereza huweza kutokea mf. Lawyer /lɔia/, buyer /baia/
]]>Ni tofauti zipi zilizopo kati ya fonimu irabu za Kiswahili na fonimu irabu za Kiingereza?
MAJIBU
Irabu ni aina ya sauti ya lugha inayotamkwa bila kuwapo na kizuizi chochote kwenye mkondo wa hewa kutoka mapafuni kupitia kinywani na puani.
Irabu za Kiswahili na zile za Kiingereza hutofautiana katika vipengele anuai kama ifuatavyo.
·Kiswahili kina irabu tano wakati Kiingereza kina irabu 20
·Kiswahili hakina irabu za kati lakini Kiingereza kina irabu za kati
·Kiswahili hakina mwambatano wa irabu mbili kwa moja lakini Kiingereza kina mwambatano wa irabu mbili kwa moja
·Katika Kiswahili irabu haiwezi kusimama peke yake lakini kwenye Kiingereza irabu huweza kusimama peke yake mf. A man
·Katika Kiswahili irabu haziwezi kutokea zaidi ya mbili zikifuatana lakini katika Kiingereza huweza kutokea mf. Lawyer /lɔia/, buyer /baia/
]]>
https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1224
Fri, 10 Sep 2021 11:55:36 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1224FASIHI ni sanaa inayotumia maneno ili kutoa picha halisi ya mwanadamu akiwa maishani mwake; mahusiano yake na viumbe wengine, migogoro yake na mazingira, shida zake, raha zake, matumaini yake na jinsi anavyopiga hatua katika taratibu za maendeleo yake.
Ni sanaa inayodhihiri ubunifu, inayotumia maneno kama mtambo na malighafi ya kuwasilisha mawazo na ambayo hulenga binadamu kama kiini chake.
Mtazamo huu unaiona fasihi kama kazi inayoendelezwa kwa maneno, iwe ama andishi au simulizi. Kuandika na kusimulia ni mtambo tu wa kuiwasilisha kazi hiyo. Kuandika sawa na kuchonga, kushona, kufinyanga au kuchora ni njia ya kueleza dhana tu, na jinsi ambavyo mchoraji hutumia rangi katika kazi yake, mtunzi wa kazi ya fasihi pia hutumia maneno au lugha kueleza dhana na hisia zake. Maneno hayo huenda akayaandika, akayaimba au akayazungumza.
Matumizi ya lugha kisanaa kwa njia ya kibunifu ndiyo maneno ya msingi ambayo huifanya fasihi kuwa aina ya sanaa. Usanii huo ndio unaofanya maneno ya fasihi yawe tofauti na maneno ya kawaida hata kama fonolojia au maumbo yake (mofolojia) ni sawa.
Kwa hivyo, si kila masimulizi au maandishi yanayofuzu kuwa fasihi, ila tu yale yatumiayo ubunifu wa kisanaa katika kuwasilisha matukio ya kila siku katika maisha ya binadamu.
Ingawa hivyo, fasihi andishi imeathiriwa pakubwa na fasihi simulizi kimaudhui na kifani kadri inavyobainika katika vipengele vifuatavyo: DHAMIRA
Kuna mfanano mkubwa kati ya maudhui katika fasihi andishi na fasihi simulizi. Masuala mengi yanayoshughulikiwa na fasihi andishi yamekwisha kujadiliwa na fasihi simulizi. Kile ambacho fasihi andishi hufanya ni kuongezea masuala mapya kutokana na jamii ya kisasa.
Kwa mfano, asasi ya ndoa na nafasi ya mwanamke katika jamii ni maudhui ya tangu jadi katika fasihi simulizi. Maudhui haya pia yameangaziwa katika kazi mbalimbali za fasihi andishi. Riwaya ya Utengano
(Said A. Mohammed) imeangazia suala la nafasi ya mwanamke katika jamii ambapo kiumbe huyo amesawiriwa kuwa chombo cha starehe, anayekandamizwa na asiye na sauti mbele ya mwamamume.
Dhana ya majaaliwa katika tamthilia ya Mfalme Edipode hujitokeza sana katika kazi za kinathari za fasihi simulizi. Katika baadhi ya ngano, kuna watu ambao kupitia kwa majaaliwa, wanatajirika kimiujiza baada ya kuwa maskini. Majaaliwa ni uwezo wa Mungu.
Jukumu kubwa la fasihi simulizi kijamii ni kuadilisha. Ngano, semi, nyimbo na mawaidha ni baadhi ya tungo za fasihi simulizi zilizotekeleza wajibu huu. Kwa mfano, ngano inayohusu kisa cha fisi kumkosa ndama kwa kuila kamba iliyokuwa imemfunga ndama, ni mfano wa ngano inayotahadharisha kujiepusha na tamaa na ujinga.
Dhamira hii ya kuadilisha inajitokeza katika tungo za fasihi andishi kama vile riwaya ya Adili na Nduguze (Shabaan Robert) ambapo ndugu zake Adili wanageuzwa kuwa nyani kwa adhabu kwa kumdhulumu Adili.
NYENZO NA MALIGHAFI
Fasihi simulizi na fasihi andishi hutumia lugha kuwasilisha mawazo ya binadamu. Fasihi simulizi ndiyo ya kwanza kutumia lugha kiufundi kama malighafi yake. Lugha ilitumiwa kwa njia ya methali, na fani nyingine kama vile nyimbo na maghani. Vivyo hivyo, fasihi andishi kama vile tamthilia na riwaya iliibuka kimaandishi kutumia lugha kwa ufundi kama malighafi. Tanzu za kimaandishi kama vile tamthilia, riwaya, hadithi fupi na hata mashairi hutumia tamathali za usemi kama vile methali, nahau, tashbihi na jazanda.
USIMULIZI
Msingi wa fasihi simulizi ni usimulizi. Tanzu nyingi za fasihi simulizi huwasilishwa kwa masimulizi kama vile tendi, majigambo na rara. Riwaya ya Lila na Fila na Kipendacho Roho zimeandikwa kwa mtindo wa ngano za kimapokeo; hali inayoonyesha athari za tanzu za fasihi simulizi. Katika tungo za fasihi simulizi, fanani husimulia hadithi katika nafsi ya tatu. Kazi nyingi za fasihi andishi pia hutumia nafsi hiyo ya tatu.
UTENDAJI
Fasihi simulizi ni tendi. Vivyo hivyo, upo uwezekano wa kutenda fasihi andishi. Kwa mfano, tamthilia huigizwa jukwaani huku ngonjera zikiambatanishwa na vitendo. Tamthilia za Kifo Kisimani na Mstahiki Meya zimeigizwa pakubwa jukwaani kama ilivyo katika fasihi andishi.
]]>FASIHI ni sanaa inayotumia maneno ili kutoa picha halisi ya mwanadamu akiwa maishani mwake; mahusiano yake na viumbe wengine, migogoro yake na mazingira, shida zake, raha zake, matumaini yake na jinsi anavyopiga hatua katika taratibu za maendeleo yake.

https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1222
Fri, 10 Sep 2021 11:41:11 +0000MwlMaeda]]>https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1222a)Hadhira ya fasihi simulizi huweza kuwasiliana moja kwa moja na fanani ilhali ile ya fasihi andishi sio lazima iwasiliane na mwandishi.
b)Hadhira huchangia katika uwasilishaji wa fasihi simulizi k.v kwa kuimba, kupiga makofi n.k (hadhira tendi/hai) ilhali hadhira ya fasihi andishi haichangii katika uandishi.
c)Hadhira ya fasihi simulizi huonana na mwasilishaji ilhali ile ya fasihi andishi si lazima ionane na mwandishi.
d)Hadhira ya fasihi simulizi ni kubwa kuliko ile ya fasihi andishi kwani huhusisha hata wasiojua kusoma na kuandika.
e)Hadhira ya fasihi simulizi ni hai yaani inajulikana na fanani ilhali ile ya fasihi andishi si hai yaani haijulikani na mwandishi.
f)Hadhira ya fasihi simulizi hainunui kazi ilhali ile ya fasihi andishi hununua kazi.
g)Hadhira ya fasihi simulizi yaweza kumiliki kazi ya fanani lakini ile ya fasihi andishi haiwezi kumiliki kazi ya mwandishi.
h)Hadhira ya fasihi simulizi huchagua kwa kulenga watu wa rika fulani lakini ile ya fasihi andishi hailengi watu wa rika yoyote.
]]>a)Hadhira ya fasihi simulizi huweza kuwasiliana moja kwa moja na fanani ilhali ile ya fasihi andishi sio lazima iwasiliane na mwandishi.