MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Taasisi za kukuza lugha]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ 2024-12-21T11:54:57Z MyBB MwlMaeda]]> 2022-04-11T18:41:25Z 2022-04-11T18:41:25Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2508 <![CDATA[HISTORIA YA UKUTA KWA UFUPI]]>
                       

                            Makala
HISTORIA KWA UFUPI YA UKUTA (USANIFU WA KISWAHILI NA USHAIRI TANZANIA) MALENGO YAKE NA UMUHIMU WAKE

Mada iliyowasilishwa na Ndugu Abdallah Ahmad Seif (Ngome Imara) katika kongamano la CHAWAKAMA lililofanyika Tarehe 30/8/2012 – 01/09/2012
Ngozi, Burundi

Chama au chombo cha UKUTA (Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania), kiliasisiwa Tarehe 29/3/1959 Mjini Dar es salaam na wapenzi wa Lugha ya Kiswahili pamoja na Ushairi, Mwenyekiti wa chama Taifa akiwa marehemu Mahamoud Hamdouny (Jitukali), aliyekuwa mshairi maarufu katika ukanda huu wa Afrika ya mashariki na pia mjuzi mkubwa aliyebobea wa lugha ya Kiswahili ambaye maskani yake yalikuwa mjini Dodoma.

Watu wengine maarufu ambao walikuwa ni waasisi wa chombo hichi UKUTA, ni akina Mzee Mathias Mnyampala, Shaaban Robert, Sheikh Kaluta Amri Abeid, Mzee Akilimali (Snow white), Mzee Mwinyikhatibu Mohammed, Mzee Said Shomari Kaniki na wengineo wengi.

Mara baada ya Tanzania (Tanganyika) kupata Uhuru, UKUTA ulipata nguvu zaidi baada ya kuongezeka wadau wengi wapenzi wa Lugha ya Kiswahili, akiwemo Rais wa kwanza wa Tanzania marehemu Mwl. Julius Kambarage Nyerere, ambae alikuwa mdau mkubwa wa Lugha ya Kiswahili na pia Mshairi alieumudu vema Ushairi.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati huo ndiye aliyekuwa mlezi wa chama cha UKUTA, na kwa nafasi yake alitoa chumba kimoja katika jengo la Anatouglo Dar es salaam ili kitumike kama ofisi kuu ya UKUTA. Ofisi hiyo ipo mpaka leo na inaendelea kutumika kwa kazi mbalimbali za kiofisi za UKUTA.

UKUTA ilifungua matawi Mikoani, na hivyo kuwa chombo kilichokuwa karibu na wananchi, na hivyo hamasa ya watu kukienzi Kiswahili ikawa iko juu kutokana na mipango madhubuti iliyokuwepo wakati huo.

MALENGO YA UKUTA
Malengo ya UKUTA ni kama yalivyoainishwa katika katiba yake ambayo ni pamoja na:-
i)          Kulinda, kuhifadhi na kustawisha Lugha ya Kiswahili, Ushairi na Utamaduni wake.
ii)        Kufanya kazi zitakazostawisha Ushairi kuwa sehemu ya mitaalaa ya Kiswahili nchini na nje ya nchi na kukuza Kiswahili kwa kuzingatia Lugha za kibantu.
iii)        Kuhamasisha na kuamsha ari na kuwasaidia watu wanaotaka kuwa mafundi wa lugha ya Kiswahili katika taasisi za elimu na jamii kwa ujumla.
iv)      Kuhamasisha na kuamsha ari za wale wanaotaka kutunga vitabu vya fani mbalimbali za elimu kwa lugha ya Kiswahili na vya Ushairi na kutafuta njia za kuchapisha kazi zao.
v)        Kutunza, kulinda na kutangaza kazi za Kiswahili zilizotungwa na watunzi waliokwisha kutangulia mbele ya haki.
vi)      Kusisimamia matumizi sahihi na sanifu ya Lugha ya Kiswahili na kukosoa na kuelekeza pale Lugha ya Kiswahili inapokosewa ili matumizi sahihi ya Kiswahili yabaki katika unyoofu wake.
vii)      Kufasiri matangazo, maandishi, vitabu, filamu, kazi za sanaa kutoka Lugha za kigeni, Asili kwenda Lugha ya Kiswahili.
viii)    Kutoa huduma ya ufasiri na ukalimani katika mikutano ya Kitaifa na kimataifa.
ix)      Kushirikiana na taasisi nyingine za ndani na nje ya nchi yetu katika kukiendeleza Kiswahili.

UMUHIMU WA UKUTA
UKUTA ni chombo muhimu kutokana na malengo kiliyonayo katika uendelezaji wa Lugha ya Kiswahili na sanaa ya Ushairi.

Hivyo ni muhimu kwa wadau wa Kiswahili kujiunga na chombo hichi, kuanzia wanafunzi wanavyuo, na watu wengine wa kada mbalimbali.

Kwani mnapokuwa katika chombo kilichosajiliwa na kutambulika na chenye historia adhimu katika Tasnia ya Kiswahili, inakuwa ni rahisi kuunganisha nguvu zenu kupitia chombo hicho na kuweza kuyafikia malengo yenu.

Kwa kuzingatia changamoto nyingi zinazowakwaza wadau wa Lugha ya Kiswahili kutokana na kukosa msukumo kutoka Serikalini, ni vyema wadau wa Kiswahili wakiunganisha nguvu kupitia katika chombo, wanaweza kuyafikia malengo yao, tofauti na mtu ukiwa mmoja mmoja, siyo rahisi kusikika na kutekelezewa jambo lako hata kama hicho unachokidai kina mantiki ndani yake.

CHANGAMOTO ZILIZOIKUTA UKUTA
Changamoto zilizoikuta UKUTA na kusababisha kulegalega, kwa sehemu kubwa zilichangiwa na viongozi wenye mamlaka katika utawala wa nchi kutokipa uzito Kiswahili katika umuhimu wake, na hivyo kusababisha hata zile taasisi zilizokuwa zinasimamia malengo ya kukiendeleza Kiswahili zipoteze mwelekeo.

Taasisi hizo kama UKUTA zilizokuwa na umuhimu mkubwa katika maendeleo ya Lugha ya Kiswahili, zilishindwa kujiendeleza kwa ufanisi kwa sababu ya kukosa nyenzo muhimu, ikiwa ni pamoja na fedha.

Serikali iliyopaswa kuzisaidia taasisi hizi kwa maendeleo ya lugha adhimu ya Kiswahili, haikuchukua wajibu wake huo muimu, na hivyo kuziacha taasisi hizi katika hali ngumu, zikikabiliwa na ukata, na hivyo kukwamisha malengo ambayo taasisi hizi zilikuwa zimejiwekea.

Lakini kwa kuwa UKUTA ni taasisi yenye malengo mazuri kwa mustakabali endelevu wa lugha ya Kiswahili, WANAUKUTA waliendelea na juhudi zao. Pamoja na kukosa uungwaji mkono kutoka katika mamlaka za utawala, juhudi za kukiendeleza Kiswahili pamoja na sanaa ya utunzi wa Mashairi ziliendelezwa hadi kufanikisha kuchapisha vitabu kadhaa vya mashairi na hata vitabu vingine vya Kiswahili vyenye maudhui mbalimbali yenye kuifaidisha jamii.

Mfano wa vitabu hivyo ni, DIWANI YA MLOKA ambayo kwa miaka mingi kuanzia 1998 hadi mwaka 2008 ilitumika kufundishia shuleni. Pia kuna vitabu kama ADHA YA UKIMWI, ELIMU YA JAMII NA CHEMSHA BONGO na vingine vilivyotungwa kwa Lugha ya Kiingereza vyenye maarifa ya kutosha, vilivotungwa na MWANAUKUTA ambaye ni Katibu wa UKUTA tawi la Dodoma, ndugu Charles Mloka.

Vingine ni BAHARI YA HEKIMA YA USHAIRI kilichotungwa na Mshairi maarufu nguli, Amiri Sudi Andanenga.

Kwa kuwa juhudi za kuliendeleza jambo lolote, huwa zipo kwa wahusika wenyewe wenye jambo lao hilo. Wadau wa Kiswahili Dodoma tuliamua mwaka 2000, kukutana na kulihuisha tena wa tawi la UKUTA kwa malengo ya kuendeleza Lugha yetu ya Kiswahili na sanaa ya utunzi wa Mashairi baada ya tawi hili lililoanzishwa mwaka 1960 kusuasua hasa mwishoni mwa mwaka 1990.

Hivyo Januari mosi mwaka 2000, tawi la UKUTA Dodoma llilifanya uchaguzi na kupata viongozi wapya kama ifuatavyo:-

Mwenyekiti                  -        Mariam Ponda
Makamu/M/Kiti          -        Ramadhani Nyembe
Katibu                        -          Charles Mloka
Katibu Mwenezi          -        Abdallah Hancha
Mwenezi Msaidizi        -        Abdallah Seif
Mweka Hazina            -        Saleh Seif
Mohammed Kajembe  -          Mjumbe
Halidi Jumanne          -          Mjumbe
Mohamed Kiwipa        -          Mjumbe
Ayoub Seif                  -          Mjumbe
Zainabu Issa                -          Mjumbe
Said Yasini                  -          Mjumbe
Hamisi Biliyetega          -        Mjumbe
Justina Mwaja              -          Mjumbe
Mussa Kazimiri            -        Mjumbe
Juma Kidogo              -          Mjumbe
Said Kaniki                  -        Mlezi

Kwa sasa angalau, kuna mwangaza unaojitokeza wa Lugha hii ya Kiswahili na hata Sanaa ya Ushairi kupata msukumo kutoka kwa viongozi wenye mamlaka ya utawala. Kwani kongamano la UKUTA lililofanyika Mjini BUKOBA, Mkoani KAGERA, Tarehe 31 Machi hadi Tarehe 01 Aprili mwaka 2012, mkuu wa Mkoa huo Mheshimiwa FABIAN MASSAWE alibeba jukumu la kuufadhili mkutano huo kwa juhudi zake, na hivyo kuonesha angalau sasa viongozi wameanza kutambua umuhimu wa uwepo wa taasisi za uendelezaji wa Lugha ya Kiswahili na kuelewa kwamba zinahitaji kuwezeshwa na kuungwa mkono ili kufikia lengo la Kiswahili kufahamika vyema kwa wadau kitaifa na kimataifa ili kiwe hazina kwa maendeleo endelevu.

UKUTA Dodoma imejipanga kutumia fursa zitazojitokeza za uungwaji mkono kwa umakini na ufanisi. Tayari tuna mipango ya kutoa vitabu vya mashairi na vitabu vingine vya Kiswahili vyenye maarifa na maelimisho kwa kushirikiana na vyuo vikuu vya Dodoma (UDOM) na St. John, na tayari maandalizi ya kazi hizo yameshaanza kufanywa.

Hivyo tunawakaribisha wote walio tayari katika kuliendeleza jahazi letu la Kiswahili, kuungana nasi ili kufanikisha malengo yetu ya kukifanya Kiswahili kuwa kweli ni hazina ya Afrika kwa maendeleo endelevu.

SANAA YA USHAIRI
Sanaa ya Ushairi ni katika tanzu za fasihi za Lugha ya Kiswahili. Ushairi ni Sanaa yenye historia ndefu na inaenda sanjari na historia ya Lugha ya Kiswahili.

Ushairi umeanza chungu ya miaka, kwa ushahidi wa tungo za mashairi za Bwana Muyaka bin Haji.

Kwamba Ushairi umeanza miaka mingi kabla ya wageni kuja katika janibu yetu ya Afrika Mashariki. Hivyo basi Ushairi umeanza kuwepo kabla wageni kutuijia kwenye pande zetu hizi na hivyo kuwa ushahidi tosha, kuwa ushairi asili yake inaenda bega kwa bega na Lugha ya Kiswahili ambayo asili yake ni Kibantu. Hivyo Sanaa ya ushairi tunapaswa kujivunia nayo kwani inatokana na sisi wenyewe. Ushairi kwa miaka mingi umetumika katika kuielimisha jamii kwa maswala mbalimbali pia kuiburudisha.

Katika Tanzania, washairi waliandika mashairi mbalimbali katika kuhamasisha kudai uhuru wa Tanganyika na hivyo kuwa na mchango mkubwa katika harakati hizo. Hata baada ya Uhuru mashairi yalitumika katika kuwajenga watu kuwa na uzalendo na nchi yao, na kuhamasisha watu kufanya kazi kwa bidii ili taifa liweze kupiga hatua za maendeleo kwa haraka.

Itoshe kusema, ushairi una faida kubwa katika jamii, kwani unaonya, unaelimisha, unahamasisha mambo mazuri na pia kuburudisha. Hivyo ni muhimu watu kujifunza Ushairi ili waweze kutunga mashairi na pia kuyasoma na kusikiliza, kutokana na faida lukuki zilizosheheni katika sanaa hii ambayo huwa imepangwa katika mpango unaovutia na kusisimua.

Ni vizuri sanaa hii ikarithishwa na kuendelezwa vizazi hadi vizazi kwa kuwafundisha watu waijue na waipende kutokana na umuhimu na uadhimu ilionao, ukizingatia ina mchango mkubwa katika uendelezaji wa Lugha ya Kiswahili.

Shairi hupangwa kwa urari wa mizani na vina, huku maudhui yaliyotawala katika shairi yakiwa na mvuto na msisimko mkubwa kutokana na mpangilio wa maneno yenye kufanana katika miishilio yake. Ama hakika Sanaa hii ya Ushairi tunapaswa KUIDUMISHA.

Nimalizie kwa kusoma shairi hili nililolitunga ili kumpongeza na kumuusia mshairi mwezetu ndg Mohamed Mkagile Mandai baada ya kufunga ndoa “MAISHA YA NDOA YA MKAGILE” lililotoka katika gazeti la Uhuru Februari mwaka 1993 kama mfano wa shairi zuri la kuvutia na lenye kudhihirisha uzuri na uadhimu wa Sanaa ya Ushairi.

MAISHA YA NDOA YA MKAGILE

1.      Mkagile wa mandai, umeshaoa kijana,
Usia ninatumai, huu nitaounena,
Najua huukatai, nawaombea rabana,
      Maisha yawe mwanana, Mkagile wa Mandai.

2.      Ndoa natoa madai, ni safari ndefu sana,
Epukeni ulaghai, dunia ulojazana,
Mpende wako nisai, nae akupende bwana,
      Hili jambo la maana, Mkagile wa Mandai.

3.      Tamaa ni haifai, hiyo ni kuepukana,
Ridhini Siwahadai, kitakacho patikana,
Mwenda pole hajikwai, faraja huja kufana,
      Tamaa heri haina, Mkagile wa Mandai.

4.      Dhana kamwe haizai, jambo lenye muamana,
Muwe hilo hamtwai, la mambo kudhaniana,
Penye dhana hapang’ai, ushwari huwa hamna,
      Mzingatie kwa kina, Mkagile wa Mandai.

5.      Dhana kama hamwambai, nayo mkiambatana,
Welewano haukai, kutadumu kuzozana,
Itazuka jitimai, msisikizane tena,
      Hatima mtaachana, Mkagile  wa Mandai.

6.      Maisha nawapa rai, muishi kwa kupatana,
Kama maji na karai, kama nywele na kitana,
Ni kama suti na tai, daima mkirandana,
      Mambo mkiridhiana, Mkagile wa Mandai.
7.      Kamwe msijikinai, mdumu kuelewana,
Furaha haisinyai, mkiwa mmeshibana,
Faraka haiwavai, kama mkishikamana,
      Katika zote namna, Mkagile wa Mandai.

8.      Nasi panapo uhai, tutakuja kuwaona,
Mje tukirimu chai, na vitu vya kutafuna,
Mikate jamu mayai, na  vingi vyenye kunona,
      Tukija kwenu bayana, Mkagile wa Mandai.

9.      Atowapa vurumai, Mungu ampe laana,
Afe kwa kizaizai, na maitiye kuchina,
Kisha iliwe na tai, kuzikwa iwe hakuna,
      Ataeleta fitina, Mkagile wa Mandai.

10.  Beti kumi baibai, kwa nguvuze Rahmana
Mpewe mengi malai, neema kila aina,
Muishi hamfubai, muwapate wema wana,
      Kwaheri ya kuagana, Mkagile wa Mandai.

Muwasilishaji – Abdallah Ahmad Seif  - 0754  - 870196 au 0716 - 903355
Katibu  Mwenezi Msaidizi    UKUTA – Dodoma

Don Bosco – Ngozi – Burundi
31/8/2012

Umuhimu wa Kiswahili katika jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMA)

Mada hii iliwasilishwa katika kongamano la Kiswahili lililoandaliwa na CHAWAKAMA na CHAWAKIRWA lililofanyika  mjini Kigali Novemba 12-16 2008. Imeandikwa na Cyprian Niyomugabo, PhD katika Sayansi za Kiisimu (Lugha za Kafrika). Mhadhiri wa Kiswahili katika chuo kikuu cha Kigali-Rwanda (KIE).

UTANGULIZI
Si rahisi kuzungumzia umuhimu wote wa jambo lolote lile, na hivi ni vigumu kutaja umuhimu wote wa Kiswahili mnamo dakika hizi 15 ninazopewa, lakini nitajaribu. Kiswahili ni lugha ya kiafrika ambayo  ni maarufu sana humu Afrika na nje ya bara la Afrika. Asili ya lugha hii ni Afrika ya mashariki sehemu za mwambao au upwa (pwani) wa Afrika ya Mashariki kando kando ya bahari ya India. Kiswahili ni lugha yenyewe na watu wake ni Waswhili na utamaduni na utu ni Uswahili.

1.      FASILI YA KISWAHILI
Kiisimu, lugha ni mfumo wa sauti nasibu za binadamu (sauti hizo ni herufi: vokali/irabu na konsonanti). Kiisimu jamii, tutasema ya kwamba lugha ni chombo cha mawasiliano katika jamii za binadamu. Kuwasiliana kwenyewe ni kupashana habari kwa kutumia maneno yaani lugha.
ü      Kiswahili ni lugha: ni mfumo wa sauti nasibu, vilevile chombo cha mawasiliano kama lugha yoyote ile.
ü  Asili ya Kiswahili ni Afrika ya Mashariki: Ingawa kitovu cha Kiswahili ni Afrika ya Mashariki, kiwakati uliopo Kiswahili ni cha sisi sote.
ü  Kiswahili ni lugha ya Kiafrika. Namba yake ni G40 katika tipolojia/ uainishaji wa lugha ya AE Meeussen.
ü  Kiswahili ni lugha ya taifa nchini Tanzania, nchini Kenya na katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
ü  Kiswahili ni lugha rasmi nchini Tanzania, nchini Kenya, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika umoja wa Afrika ( na bado haijawa lugha rasmi katika JAMA).
ü  Kiswahili ni lugha ya umahiri maana lugha iliyovuka mipaka ya kitaifa na kuwa lugha ya kimataifa. Kama asemavyo Calvet (1988:14), “lugha inayozidi kuongeza idadi ya wazungumzaji wake na idadi ya dhima zake ni jumuia lugha inayotapakaa”. Leo Kiswahili kinasemekana kuwa ni lugha ya saba katika lugha za ulimwengu na ni lugha inayoongewa na takribani watu zaidi ya milioni 100.

2.      DOKEZO LA KIHISTORIA: MUHTASARI WA HISTORIA YA KISWAHILI KATIKA JAMA
Nianzie labda kwa porojo isemayo ya kwamba Kiswahili kilizaliwa Unguja (Zanzibar), kikakulia na kulelewa Tanganyika (Tanzania Bara), kikapatwa na ugojwa huko Kenya, kikalazwa hospitali na kufia Uganda na kuzikwa Zaire (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya sasa hivi) na tuongeze labda kikafufukia hapa Rwanda leo hii. Ni porojo ambayo inaukweli wake kihistoria.
Wakati wa harakati za uhuru wanasiasa walijaribu sana kutumia Kiswahili kama kiungo kati yao na wananchi.
TANZANIA: TAA (Tanganyika African Association) chama hiki kilianzishwa DSM na kusambaa nchi nzima. Chama hiki kilikuwa na katiba yake katika Kiswahili. Kiswahili kikatiliwa mkazo sana. Mnamo mwaka 1954 TAA kikabadiliswa na kuwa TANU (Tanganyika African National Union) na kiongozi akawa Mwalimu J.K Nyerere. Mara nyingi mikutano yake ya hadhara alitumia Kiswahili bila ya mkalimani katika juhudi zake za ukombozi. Mnamo mwaka wa 1955 kiswahili kilianza kutumiwa Bungeni na 1961 TANU kikafanya Kiswahili kuwa lugha ya Taifa. TANU kilijaribu sana kukikuza na kukitumia Kiswahili na watu wakaanza kujivunia lugha hii. Wakati wote huu Kiswahili kilikuwa ni chombo muhimu cha ukombozi wa kisiasa nchini KENYA:
Nchini Kenya Kiswahili kilipigwa vita sana na magavana wa kizungu, mathalani 1900 Sir Charles Elist aliyekuwa Gavana alihimiza lugha za makabila mengine na hakutaka Kiswahili kitumiwe. Lengo lake kubwa ni kuifanya Kenya iwe chini ya wazungu na kusiwe na kiungo chochote cha lugha ya kiafrika. Na hali hii ya kukipiga vita iliendelea sana na mnamo mwaka wa 1935 Kiingereza kikawa ndiyo lugha ya mitihani katika shule ya msingi. Hata hivyo wanasiasa walijaribu sana kukitilia mkazo Kiswahili toka awali na polepole kikaanza kuwaunganisha wananchi katika harakati za ukombozi. Kumbukeni kazi ya Mhe. Rais Jomo Kenyatta, kumbukeni kazi ya MAUMAU n.k.
UGANDA: Kiswahili ni lugha ya kwanza ya kigeni kutumiwa nchini Uganda. Kiswahili kilianza kupendelewa na wakoloni hapo awali  japo Ukristo ulikipinga maana ulikinasibisha na Uislamu. Mathalan Gavana wa Uganda, W.F Gowers, 1927 alihimiza Kiswahili kitumiwe Kiswahili kitumiwe Uganda huku akipingana sana na mfalme Kabaka Daudi wa Uganda ambaye alitaka Kiganda kitumiwe, Kiswahili hata hivyo kilifahamika bila kupata nguvu sana. Na hata katika harakati za ukombozi Kiswahili hakikutumika sana ukilinganisha na nchi nyenzake za Afrika Mashariki.
RWANDA-BURUNDI nchini Rwanda, Kiswahili ndiyo lugha rasmi ya kwanza ya kigeni. Mtawala Mjerumani, mfanyabiashara wa kiarabu, dini ya Islamu na Wamisionari wa kizungu, kati ya hawa wanne si rahisi kusema ni nani ameleta au ametumia kwanza Kiswahili nchini. Kazi nyingi zilizogusia mada hii hazikutoa mwanga wa kutosha juu ya swali hili. Ukweli wa mambo ni kwamba Kiswahili kiliingia rasmi Rwanda mwishoni mwa karne ya 19 wakati wa utawala wa Mjerumani. (Taz. NIYOMUGABO C. 1992). Burundi Kiswahili kiko kwani historia ya Rwanda na burundi wakati wa ukoloni si tofauti.
ZAIRE (DRC), Kiswahili kilisambazwa mashariki mwa Zaire na Tiputipu (Mtipura) kabla ya 1860 akifanya safari za biashara na Kiswahili chake kule kinajulikana kwa jina la Kingwana na ni lugha ya Taifa tena ni lugha rasmi nchini humo.

3.      UMUHIMU WA KISWAHILI KATIKA JAMA
Katika Isimujamii, lugha haichukuliwi kama mfumo unaotenganishwa na mazingira yake ya matumizi; ndiyomaana hapa tutaona jinsi lugha inavyofanyakazi katika jamii ya wazungumzaji wake. Kuhusu rai hii tunasema ya kwamba luha haiwezi kuchunguzwa nje ya wale wanaoitumia kwa sababu ni sehemu muhimu ya maisha ya watu. Mabadililko katika lugha ni sehemu moja ya mabadiliko katika jamii nzima yaani katika utamaduni wake. Dhima ya madhumuni ya lugha katika jamii yatakuwa mengi. Yanayojitokeza kuwa muhimu sana ni haya yafuatayo: kusudi la kwanza la lugha katika jamii ni kuwa chombo cha mawasiliano. Kuwasiliana kwenyewe kunatarajia kuleta uelewano na ujirani mwema kati ya watu wa jamii au` kati ya jamii na nyingine. Waishio katika hali ya usalama  katika jamii, maendeleo yanawafikia haraka haraka.
·        Kiswahili ni chombo cha kujenga uhusiano, ujirani mwema  na urafiki kati ya watu na watu. Kujua lugha nyingi ni kujiongezea uwanja wa kujipatia marafiki na kuweza kujifunza mengi kutoka kwao. Ni chombo cha kuleta amani na utulivu kwani na amani ni mojawapo ya msingi wa maendeleo katika jamii yoyote ile. Na kama tunaoimba katika Kanisa ni kwamba kunako urafiki, upendo na uhusiano Mungu yupo. Sasa Mungu yu hapa katika kongamano hili.
·        Kiswahili ni chombo cha elimu: kwa kupitia mfumo wa elimu za kijadi au za kisasa.
·        Kiswahili ni chombo cha starehe na burudani: nyimbo zinazopendwa katika Kiswahili, kuweza kufanya utalii kwa kutumia Kiswahili.
·        Kiswahili ni silaha ya ukombozi na kitambulisho cha Waafrika: Tazama kazi iliyofanywa na TANU, MAUMAU, maandishi ya Shaaban Robert katika pambo la lugha, “Titi la mama ”. titi hilo ni lipi? Ni Kiswahili.
·        Kiswahili ni kiungo cha Waafrika: Kwa Waafrika kusini mwa jangwa la Sahara, matumizi ya lugha za kigeni yamekuwa yakikuzwa kwa sababu mbalimbali mojawapo ni kukosekana lugha ya kuunganisha watu wengi wa makabila tofauti.
·        Kiswahili lugha isiyo na ukabila: Ukabila, maana , matendo au mawazo ya mtu yaliyotawaliwa na kuthamini kabila lake tu na kubagua makabila mengine, ni kizuizi kikubwa sana kwa maendeleo ya Afrika. Kwa hiyo Kiswahili kimekuja kama lugha ambayo haina mwenyewe kiukabila kwani ni ya sisi sote.
·        Kiswahili hupatia watu kazi: wakalimani wa Kiswahili katika UA, walimu, wauza vitabu, wanahabari.
·        Kiswahili chombo cha maendeleo: Sheila Ryanga Kenyatta University amesema: “Kila lugha yoyote ile katika kila taifa iwe ni ya umahiri, iwe inatumika kwa uchache inadhima yake na nafasi yake kama chombo cha maendeleo ya nchi upande wa uchumi uongozi bora…..”. Hadhi na thamani ya lugha hutokana na hadhi ya wazungumzaji wake. Lugha ya watu maskini hadhi yake itakuwa ya  umaskini. Lugha ya watu tajiri kimaendeleo, kiutamaduni, kiteknolojia,….itakuwa ni lugha yenye hadhi kubwa. Kwa hiyo ili tuendeleze Kiswahili ipasavyo lazima sisi wanachi wa JAMA tufanye kazi, tutumie bidii sana kwa kusoma hasahasa nyie vijana kwani ukesho wa JAMA ni nyie. Kama asemavyo Mnyarwanda utakachokula kesho unakitayarisha leo.

4.      MIKAKATI YA KUKUZA KISWAHILI KATIKA JAMA
Taasisi za dola zinazohusika na ukuzaji wa Kiswahili katika JAMA inapaswa kukutanika pamoja kwa shuguli ya kueneza lugha ya Kiswahili na huu ni wakati mzuri wa kuchunguza sera za JAMA kiwakati uliopo katika harakati za utapakazaji wa Kiswahili. Hatua ya kwanza ya kuweza kufikiri juu ya ukuzaji wa lugha fulani ni kujua waziwazi umuhimu wake. Umuhimu wa Kiswahili katika JAMA unajulikana kinagaubaga. Yafuatayo ni kama mapendekezo:
·        Kiswahili kiwe chombo cha kisiasa cha kweli: Utambulisho wa Waafrika: Mhe. Rais Joaquim Chissano wa Msumbiji (Rais mstaafu) ndiye Rais wa kwanza kuhutubia kikao cha wakuu wanchi wanamemba wa Umoja wa Afrika (AU) katika Kiswahili. Wakati huo alikuwa mwenyekiti wa umoja huo. Niwakumbushe ya kwamba kabla ya hotuba yake katika Kiswahili, lugha rasmi za UA zilikuwa Kiarabu, Kifaransa, Kingereza na Kireno. Alipozungumza katika Kiswahili na alikuwa anafanya ukalimania yeye mwenyewe. Wakati Rais Chissano alipozungumza Kiswahili kwa mara ya kwanza viongozi wengi na hata mabalozi walipatwa na mshangao na tangu wakati huo azimio likachukuliwa ili Kiswahili kiwe mojawapo ya lugha rasmi za umoja huo. Na sasa hivi Rais Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amabaye amechukua uenyekiti wa UA kutoka kwa mwenyekiti aliyemaliza muda wake Rais John Kufor wa Ghana aliwahutubia wakuu wenzake katika Kiswahili mnamo kikao cha mwisho cha mwezi Januari 2008. Hatua za Marais hawa zilikanganya wenzao kwani ilkuwa mazoea kwa wakubwa wa Afrika kutumia lugha za kigeni na kuonyesha umahiri na ubingwa wao katika lugha hizo za kigeni. Nikumbushe kwa kupitia ya kwamba mpaka sasa hivi kwa mujibu wa katiba ya JAMA lugha ya Kiingereza ndiyo lugha rasmi inayotumiwa na Kiswahili kimeelekezwa kutumika kama lugha ya mawasiliano, ambapo jitihada za kukifanya kiwe lugha rasmi zinaendelea. Hapa kuna maoni tofauti: (a) Kiswahili kiwe lugha ya JAMA peke yake tu. (b) Kiingereza kiwe peke yake lugha rasmi katika JAMA. © Kiswahili na Kiingereza, lugha hizi mbili zichukuliwe kama lugha rasmi za JAMA. Hali ya uwili lugha (hali ya ulugha mbili) au ulumbi (ulugha nyingi) iingizwe katika JAMA (mfano Kiswahili-Kiingereza-Kifaransa/Kiswahili-Kiingereza/Kiarabu….). Nyie mnaonaje? Mnipashe. Mimi maoni yangu ni yafuatayo:
·        Sera ya lugha na upangaji wa lugha: Sera ya lugha ni taratibu mbalimbali za kuratibu matumizi ya lugha katika jamii. Upangaji wa lugha ni jitihada za kuweka sera mbalimbali za lugha ambao husaidia kutatua tatizo la mawasiliano katika jamii. Tunajua ya kwamba mradi wa upangaji wa lugha si jambo rahisi. Kwani kweli sera ya upangaji wa lugha katika jamii/jumuia fulani huonekana mara nyingi kama jaribio gumu kwani inazingatia uteuzi wa kiitikadi na kutilia maanani maoni ya kijamii, kistadi na kiutekelezaji. Wakati umefika ili kuwepo sera ya nafasi ya kila lugha katika JAMA maana kuonyesha nafasi ya kila lugha kufuatana na umuhimu au dhima zake katika jamii. Kudhihirisha nafasi za lugha za kiasili (makabila/makundi), lugha za taifa, lugha za ukanda, lugha za kimataifa. Ingawa Kiswahili kimefikia hatua ya lugha inayozungumzwa na wengi na yenye dima nyingi katika JAMA, si kumanisha kuwa hakuna vipingamizi vya uenezaji wake. Kizuizi chake cha kwanza ni mapambano ya kilugha. Taasisi za dola zinazojihusisha na ukuzaji wa lugha ya kiswahili zifanye kazi bega kwa began a ACALAN (African Academy of Languages) maana Akademia ya lugha za Afrika ya UA.
·        Kiswahili kiwe chombo cha elimu cha kweli: Kiswahili kiwe chombo cha kufundishia katika viwango vyote vya masomo lakini tusisahau na lugha nyingine. Taz. Upangaji lugha.
·        Kufuta kasumba za ukoloni: kasumba ni mabaki ya fikra za kikoloni kichwani mwa mtu. Kuna waafrika wengi sana ambao wanafikiri ya kwamba kujua au kuzungumza lugha za kiafrika, lugha za kishenzi, lugha duni, lugha za akinayake, lugha ambazo ndani yake kuna umasikini… ni aibu na ni kukosa akili. Mhe George Mkuchika (Mb), Waziri wa Habari utamaduni na michezo, Tanzania, akizungumzia kuhusu ukuzaji wa lugha ya Kiswahili na lugha za kiafrika kwa ujumla amesema “Mada hii ni mada muhimu sana hasa katika kipindi hiki ambacho nchi zetu za kiafrika zimekwishajipatia uhuru wa kujitawala na kujiamulia mambo yetu wenyewe na kwamba kazi kubwa iliyoko mbele yetu kwa sasa ni  kuelekeza jitihada zetu katika kujikomboa kifikira, kiutamaduni na kiuchumi mambo ambayo yalikandamizwa na kudidimizwa wakati wa kipindi cha ukoloni, kwa hiyo kwa kupitia dini na utawala walijitahidi kuwatia wenyeji kasumba ili waone kila walichonacho ni cha kishenzi; kuanzia lugha, dini, utamaduni, teknolojia, dawa na mengineyo. Somo hili walilotoa lilifanikiwa sana na likawa ni sehemu au viambajengo vya ukoloni”. Kwa wakati mwingi mradi wa kukuza lugha za kiafrika kwa jumla na kiswahili hasahasa hupingwa kwa sababu idadi ya watu wengi wanaochukua madaraka katika nyanja mbalimbali za taifa walisomea katika mfumo wa ufundishaji wa kikoloni. Baadhi ya hawa ni watu ambao machoni mwao kuwa na mradi wa kukuza lugha ya kiafrika ni upotezaji wa wakati na pesa.
·        Kutafsiri vitabu na maandishi mengine katika Kiswahili: Ili Waafrika wa kila kiwango cha ujuzi wanufaike na maendeleo ni lazima ujuzi wote (teknolojia, sayansi, falsafa…) viwekwe katika Kiswahili kutoka lugha ambazo jamii zake zimepiga hatua kimaendeleo kama Kiingereza, Kifaransa, Kichina, Kidachi, Kijapani n.k. Vilevile ni lazima kazi za uandishi na utangazaji wa vitabu na utafiti wa kila aina katika Kiswahili yatiliwe maanani. Kwani kama asemavyo Senkoro (1987) “elimu na maarifa mbalimbali ni mali ya watu wote duniani”.
·        Kuweka nguvu zaidi katika utungaji kamusi na ukuzaji wa istilahi. Ili lugha iwe na uhai lazima iweze kutafsiri dhana zote na fikra zote katika lugha hiyo ili iweze kuwa chombo cha kweli cha maendeleo ya kila aina. Kwa upandea wa Kiswahili tunapongeza sana kazi iliyofanywa na TUKI pamoja na BAKITA.
·        Kufungulia milango “viswahili” vingine. Kiswahili sanifu lazima kifungulie milango launi nyingine ya Kiswahili hasahasa cha Afrika ya Kati.
·        Kuongezeka idadi ya makongamano kuhusu ukuzaji wa Kiswahili kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa.

ASANTENI NYOTE!
 
MAREJELEO
Calvet, L.J. Les langues vehiculaires, PUF, Paris, 1981.
Chimerah, R.M. Kiswahili past present and future Horizons, Nairobi 2009.
Kagabo, J.H.L. Islam et les “Swahili” au Rwanda, Paris, 1988.
Khalid Abdallah, the liberation of Swahili, Nairobi, 1977.
Massamba, D.P.B. Historia ya Kiswahili 50BK hadi 1500 BK, Nairobi, 2002.
Mmallavi, A.P.W. Lugha katika jamii, EAPH, DSM, 1977.
Niyibizi, S. Le Swahili au Rwanda: Aspects historique, linguistique et sociolinguistique, Butare      1980.
Niyomugabo, C. Nafasi ya lugha ya Kiswahili katika uwanja wa dini nchini Rwanda: Mkabala wa kiisimujamii, Ruhengeri 1992.
Senkoro, F.E.M.K. Fasihi na jamii, DSM, 1987.
Shihabudin Chiragdin na M. Mnyampala (1977) Historia ya Kiswahili OUP, Nairobi.
Tuli R.S.K. (1985) Chimbuko la Kiswahili kukua na kuenea kwake, Arusha Tanzania.s]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-12-16T03:26:38Z 2021-12-16T03:26:38Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1750 <![CDATA[NAFASI YA VYAMA NA TAASISI MBALIMBALI KATIKA MAKUZI YA KISWAHILI]]>
Kwa Mukhtasari

IKIWA idara ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI), awali
ikiitwa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) ni miongoni mwa taasisi kongwe
zaidi za lugha nchini Tanzania na Afrika Mashariki. Madhumuni yake ni kusimamia
usanifishaji na maendeleo ya Kiswahili.

Japo Kiswahili
kimeendelea kubaki nembo ya Afrika, mjadala usio na mwisho kuhusiana na ni ipi
lugha ya kufundishia katika shule na vyuo nchini Tanzania ni ithibati kwamba
Kiswahili hakijapokezwa hadhi inayostahiki katika mengi ya mataifa ya Afrika
Mashariki na Kati.

TUKI, kwa sasa TATAKI,
ilianzishwa mnamo 1930 ikijulikana kama International-Territorial Language
(Swahili) Committee kwa nchi tatu za Afrika Mashariki na baadaye ikaitwa Kamati
ya Kiswahili ya Afrika Mashariki.

Mnamo 1964, kamati
ilifanywa kuwa sehemu ya UDSM na baadaye ikaitwa Chuo cha Uchunguzi wa
Kiswahili. Tangu 1970 kimepewa jina la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili
(TUKI). Mwaka 2009, TUKI iliungana na iliyokuwa Idara ya Kiswahili ya UDSM na
kuunda taasisi kubwa zaidi inayoitwa TATAKI.

Majukumu ya taasisi hii
awali yalikuwa ni kutafiti nyanja zote za lugha ya Kiswahili, fasihi na
utamaduni na kuchapisha matokeo ya utafiti huo.

Hivyo pamoja na Baraza
la Kiswahili Tanzania (BAKITA), TUKI ni mlinzi wa usanifu wa lugha ya Kiswahili
katika Tanzania. Baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili, sasa TATAKI
inafundisha Isimu, Fasihi na Historia ya Lugha ya Kiswahili.

Inafundisha Kiswahili
kama lugha ya pili hasa kwa wageni kutoka nje ya ulimwengu wa Waswahili na
kuendeleza utungaji wa kamusi mbalimbali zinazohusiana na Kiswahili.

BAKITA

Ni taasisi ya serikali
iliyoundwa kwa sheria ya Bunge Na.27 ya mwaka 1967 kwa madhumuni ya kukuza
Kiswahili. Kutokana na sheria hii, Baraza ndilo mratibu wa kusimamia asasi zote
na mawakala wote wanaokuza Kiswahili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

BAKITA imekuwa na
mchango mkubwa katika ukuzaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili kupitia
majukumu yake.

Miongoni mwa majukumu
ya Baraza hili kama yalivyofafanuliwa katika sheria hiyo ni kuratibu na
kusimamia maendeleo na matumizi ya Kiswahili nchini pamoja na kushirikiana na
vyombo vingine vinavyojihusisha na maendeleo ya Kiswahili.

Huhimiza matumizi ya
Kiswahili katika shughuli rasmi na za kawaida, huandaa vipindi mbalimbali
redioni ili kuhimiza matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili, hushirikiana na
mamlaka zinazohusika kuthibitisha tafsiri sanifu za istilahi, hutoa huduma za
tafsiri na ukalimani kwa serikali, mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali
na asasi nyingine pamoja na kuidhinisha vitabu vya Kiswahili vitakavyotumika
shuleni na vyuoni kabla havijachapishwa.

TAKILUKI

Taasisi ya Kiswahili na
Lugha za Kigeni (TAKILUKI) ilianzishwa mnamo 1979 kwa lengo la kukuza na
kueneza Kiswahili ndani na nje ya Zanzibar.

Inajishughulisha na
kuratibu, kuendesha mafunzo ya Kiswahili visiwani Zanzibar, kuhariri miswada
mbalimbali ili kuthibitisha ufasaha wa Kiswahili na kufanya tafiti za Kiswahili
katika nyanja zake zote, hususan sarufi na fasihi.

TAKILUKI inatoa ushauri
wa kitaaluma kwa watunzi wa vitabu ili waweze kuandika kazi zenye ubora, na
kushirikiana na wadau wengine wa Kiswahili kuandaa na kuendesha semina, warsha
na kozi fupifupi za Kiswahili.

CHAUKIDU

Chama cha Ukuzaji wa
Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) kina makao makuu katika Chuo Kikuu cha
Wisconsin-Madison, Marekani.

Madhumuni yake ni
kuwajumuisha pamoja wakuzaji wa Kiswahili duniani kote kwa lengo la kuchochea
kasi ya malengo mahususi kama vile kukuza Kiswahili katika nyanja zote ambamo
lugha hii inatumika na kuongeza ufanisi wa mawasiliano katika ufundishaji na
utafiti wa maarifa ya aina zote mathalan uandishi na utangazaji wa habari,
uandishi na uchapishaji wa vitabu na majarida pamoja na utayarishaji wa safari
za mafunzo katika Afrika Mashariki na Kati.

Husambaza habari na
matokeo ya utafiti kwa kutumia machapisho mbalimbali na teknolojia ya mtandao
wa kompyuta kuhusu vipengele mbalimbali vya Kiswahili na masuala yanayohusiana
na Kiswahili. CHAUKIDU inaelimisha umma juu ya umuhimu wa kujivunia,
kuendeleza, na kuheshimu Kiswahili.

Vilevile inashauri ama
kushinikiza serikali za nchi ambamo Kiswahili kinazungumzwa kutambua thamani
iliyobebwa na maliasili hii ili kuunda sera mwafaka za kukiendeleza kadri ya
uwezo wake kwa manufaa ya maendeleo ya serikali na watu wake kijamii, kisiasa,
kiuchumi, kiutamaduni na kielimu.

CHAWAKAMA

Chama cha Wanafunzi wa
Kiswahili katika vyuo vikuu vya Afrika Mashariki (CHAWAKAMA), kilianzishwa
mnamo 2004 kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili katika eneo lote la Afrika
Mashariki kupitia kwa wanafunzi wanaosoma Kiswahili vyuoni.

Wanachama wa chama hiki
ni wale wanaosomea taaluma za Kiswahili ila wapenzi wa Kiswahili pia wanaweza
kujiunga nacho.

Mara kwa mara,
CHAWAKAMA huandaa makongamano kwa lengo la kuwapa wanachama nafasi ya kujadili,
kuimarisha, kuendeleza na kukuza vipawa vyao vya lugha na fasihi ya Kiswahili,
kuamsha ari ya mapinduzi ya utamaduni wa Kiswahili, kueneza Kiswahili ndani na
nje ya nchi, kushirikiana na vyama vingine katika juhudi za kuendeleza na
kuimarisha Kiswahili ndani na nje ya nchi wanachama, kuwaunganisha wanafunzi wa
Kiswahili Afrika Mashariki na Kati katika kukikuza Kiswahili pamoja na
kushirikiana na asasi mbalimbali zinazojihusisha na ukuzaji na uenezaji wa
Kiswahili.

CHAKAMA

Chama cha Kiswahili
Afrika Mashariki (CHAKAMA) ndicho cha tatu kwa umaarufu zaidi miongoni mwa
wasomi, wataalamu na wahadhiri wa vyuo vikuu baada ya CHAUKIDU na Chama cha
Walimu wa Lugha za Kiafrika (ALTA) ambacho haundaa makongamano yake jijini
Bayreuth, Ujerumani.

Kwa pamoja na Chama cha
Kiswahili cha Taifa (CHAKITA), CHAKAMA huchapisha jarida la chama na machapisho
mengine ili kusaidia kueneza taaluma za Kiswahili.

Aidha, huhifadhi
kumbukumbu za wataalamu wa Kiswahili kwa nia ya kutumia katika kufanikisha
malengo ya chama na wadau wa Kiswahili pamoja na kuratibu makongamano na
mijadala mbalimbali inayohusiana na taaluma za Kiswahili.

Chama huandaa
makongamano kila mwaka ambalo linawakutanisha wanachama wote katika vyuo
mbalimbali katika nchi husika.

Katika makongamano
hayo, mada mbalimbali zinazohusu Kiswahili na mustakabali wake hujadiliwa
lakini pia maazimio mbalimbali huchukuliwa kuhusu maendeleo ya chama. Makala
mbalimbali huandikwa na kuchapishwa kwa minajili ya kusomwa na watu mbalimbali.]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-11-17T02:16:48Z 2022-01-21T16:23:41Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1499 <![CDATA[KISWAHILI NA WASWAHILL]]>
Kodoa macho na tega sikio umsikilize aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania (UKUTA) Marehemu Mzee Salim bin Ali bin Hemed (Kibao) bin Abdallah bin Ali Albuhury ndugu halisi wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania (UKUTA) Marehemu Sheikh Mohamed Ali Albuhury, akimwaga lulu za Kiswahili.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-11-10T08:43:59Z 2021-11-10T08:43:59Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1431 <![CDATA[MRADI WA KUSWAHILISHA PROGRAMU HURIA]]> MRADI WA KUSWAHILISHA PROGRAMU HURIA
WARSHA YA ARUSHA 1-5 NOVEMBA 2004-11-22
MADA YA MAFUNZO
UUNDAJI WA ISTILAHI: UZOEVU WA BARAZA LA
KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA)
na
P.C.K. Mtesigwa
UUNDAJI WA ISTILAHI: UZOEVU WA BARAZA LA KISWAHILI
LA TAIFA
(BAKITA)
1.0 Utangulizi Jukumu kuu ambalo Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) limepewa kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Bunge Na. 27 ya mwaka 1967 iliyoliunda ni kukuza, kuimarisha na kuendeleza Kiswahili hasa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika marekebisho ya sheria hiyo yaliyofanyika mwaka 1983 kwa Sheria ya Bunge Na.
7, BAKITA limepewa uwezo wa kufuatilia na kusaidia ukuzaji wa Kiswahili katika nchi za nje pia. Kwa hiyo kazi zinapokuwa zimethibitishwa na BAKITA huzihusu pia juhudi za uendelezaji wa Kiswahili katika nchi za nje.
Kimsingi ukuzaji au uimarishaji wa lugha maana yake, kwa upande mmoja, ni utumiaji wa lugha hiyo kwa usahihi. Kwa mtazamo huo maana yake ni kuhakikisha kwamba kanuni za sarufi yake zinafuatwa. Lakini pamoja na hilo, kwa upande mwingine kuna suala la kuiwezesha lugha hiyo kukidhi mahitaji ya watumiaji wake wa kila hali na kila uwanja wa matumizi. Kusema kweli mojawapo ya vigezo vinavyotumika kujua kiwango cha kukomaa kwa lugha ni kupima jinsi inavyojimudu katika msamiati wake kukidhi matumizi katika nyanja mbalimbali zikiwemo nyanja maalumu za kitaalamu. Ili kutimiza lengo hilo hapan budi msamiati wake ukuzwe na kusambaa. Kwa mujibu wa Mkude (2004) aina ya msamiati uliosukwa kimkakati na kuratibiwa kwa nia ya kuashiria dhana teule za taaluma fulani huitwa istilahi. Huu ni msamiati maalumu ambao umetokana na msamiati mpana wa lugha na kufanyiwa marekebisho ili kuhakikisha kwamba maana ya neno inaacha au inapanua maana yake ya kawaida na kubeba maana maalumu kwa ajili ya matumizi katika uwanja maalumu.
Ili kutekeleza majukumu yake kama chombo chenye mamlaka ya kukuza na kuimarisha Kiswahili kama lugha ya taifa na mojawapo ya lugha mbili rasmi za Tanzania, BAKITA linayo idara mahususi (Idara ya Kamusi na Istilahi) inayoshughulikia kusanifu istilahi kwa ajili ya kuziba pengo la kukosekana kwa istilahi katika nyanja mbalimbali.
Kazi kubwa inayofanywa na idara hii ni kutafuta visawe vya Kiswahili vya istilahi za Kiingereza zilizopo tayari. Katika kufanya kazi hiyo BAKITA hupokea orodha za istilahi kama hizo baadhi huja tayari na mapendekezo ya visawe vya Kisahili vilivyopendekezwa na mletaji mwenyewe ili yapitiwe na kurekebishwa kama hapana budi au yathibitishwe ili baada ya kukubaliwa rasmi na BAKITA yasambaazwe na kuanza kutmika. Lakini kwa kiasi kikubwa orodha zinazoletwa huwa hazina mapendekezo yoyote ya visawe vya Kiswahili. Idara husika hufanya utafiti kutafuta visawe na kasha Kamati ya kuisanifu istilahi ya BAKITA hukaa na kutumia mbinu mbalimbali ili kuvipitia na kuvisanifu visawe hivyo. Ndipo visawe hivyo vinapowaslishwa katika kikao cha Baraza zima ili kutoa idhini na hatimaye kuvisambaza vianze
kutumika. Mpaka sasa BAKITA limefaulu kusanifu na kusambaza istilahi zipatazo zaidi ya elfu 10 za nyanja maalumu na taaluma mbalimbali zaidi ya 30. Lengo la makala hii ni kueleza misingi na mbinu ambazo BAKITA hutumia katika kuunda istilahi za Kiswahili. Vilevile makala itagusia matatizo yanayojitokeza wakati wa kuunda istilahi na pia baada ya kuunda istilahi.
2.0 Misingi na mbinu za uundaji wa istilahi Shirika la Kimataifa la Viwango (ISO) ambalo miongoni mwa kazi zake ni kuratibu na kusimamia uendelezaji wa istilahi kimataifa, limeorodhesha kanuni zinazopaswa kufuatwa wakati wa kuunda istilahi katika lugha yoyote. Misingi hii imetokana hasa na mtazamo wa wanaisimu wa Vienna – yaani “Shule ya Istilahi ya Vienna (Austria)” iliyoanzishwa na Eugen Wuster. Kwa muhtasari kanuni hizo zinahusu uundaji wa istilahi lugha moja tu inapohusika na pale lugha mbili zinapohusika. Lugha moja inapohusika kanuni zifuatazo hazina budi zizingatiwe:
(1) Istilahi ziundwe baada ya kupata dhana iliyoelezwa kwa ukamilifu na wazi.
(2) Istilahi ziwe fupi kadiri iwezekanavyo lakini zenye kueleweka. Uundaji wa istilahi kwa vifupisho na akronimia uepukwe hasa kama istilahi kamili si ndefu sana.
(3) arufi ya lugha inayohusika lazima itiliwe maanani. Kwa hiyo istilahi ziundwe kwa kufuata mofolojia ya kawaida ya lugha.
(4) Istilahi ziundwe kwa njia ambayo itakuwa rahisi kuunda istilahi nyingine kwa mnyumbuliko.
(5) Uundaji wa istilahi kwa kupanua maana ya neno uepukwe hasa iwapo nyanja zinazotumia maneno hayo zinakaribiana, ili kuepusha utata. Kwa hiyo mfumko wa sinonimia au homonimia (visawe) hauna budi kuepukwa ili watumiaji wasikanganyikiwe.
Lugha mbili zinapohusika kanuni zifuatazo zizingatiwe:
(1) Uundaji wa istilahi kwa njia ya kutohoa maneno ya lugha nyingine uzingatie kuchukua maneno kama yalivyo katika lugha ya asili na kufanya marekebisho machache tu ili kulingana na sarufi na matamshi ya lugha pokezi.
(2) Uundaji wa istilahi kwa kutumia Kigiriki na Kilatini uendelezwe ili kuzingatia uwakilishi sahihi wa dhana hasa za sayansi na pia kupunguza kishawishi cha kupendelea kutumia baaadhi tu yalugha zinazotumika ulimwenguni hivi sasa. Katika uzoevu wa kusanifu istilahi, BAKITA limekuwa likizingatia pia kanuni za nyongeza ili kupata ufanisi zaidi kwa kutilia maanani jamii ya watumiaji wa Kiswahili na  utamaduni wake. Kubwa kati ya kanuni hizo za nyongeza ni:
(1)
istilahi ziepuke utusani – yaani zisiundwe kwa maneno ambayo tayari
yanaeleweka
kwamba ni matusi kwa watumiaji. Kwa mfano katika kutafuta
kisawe
cha penis, neno mboo hushitua watumiaji wa Kiswahili wengi na badala
yake
neno dhakari huvumulika na kutumika zaidi. Kadhalika kisawe cha neno
bone
marrow neno uboho ingawa ni sanifu pia lakini huepukwa sana katika
matumizi
na badala yake neno uloto limekomaa sana katika matumizi. Vilevile
katika
kutafuta kisawe cha neno anus, neno mkundu hushitua watumiaji na neno
ngoko
likachukuliwa.
(2)
Istilahi ziwe angavu vya kutosha – yaani istilahi ziweze kudokeza dhana
liliyokusudiwa
kwa kina na usahihi kadiri iwezekanavyo. Wakati wa kutafuta
kisawe
cha neno flip chart kwa Kiswahili kumekuwa na pendekezo la neno
bango
kitita. Katika kulichambua neno hilo imedhihirika ya kwamba ingawa
neno
bango kwa kiasi fulani linawakilisha ukubwa wa chart lakini dhana ya flip
haijidhihirishi.
Hivyo halina uangavu wa kutosha. Pendekezo linaloelekea
kupendelewa
ni chati pindu kwa kuwa neno hilo linawakilisha dhana ya chart
na
pia utumiksji wake wa kupinduliwa wakati chati hiyo inapotumiwa.
(3)
Istilahi ziwe na ulinganifu wa mtiririko ulio katika dhana za kikoa kimoja.
Katika
hili ni muhimu kwa wasanifishaji kukumbuka kwamba istilahi hazikai
pekepeke.
Hazifiki mbali iwapo zitasimama pasipo kuhusisha maneno mengine
yaliyo
katika uga huo. Istilahi ni kama matundu ya wavu ambayo kila moja
sharti
ligusane na lenzake ili hatimaye mfumo mzima wa wavu uweze
kutengenezwa.
Kwa hiyo istilahi moja iwe chanzo cha kupata istilahi zingine
kutokana
na kuinyumbulisha na kuunda istilahi zinazohusiana katika uwanja
ule.
Kwa mfano: Sumaku (magnet), Usumaku (magnetism), Sumakisha
(magnetise),
Jisumakisha (auto magnetise), Usumakishaji (magnetization, nk.
(4)
Istilahi zilizozoeleka au kukomaa kutokana na kutumika kwa muda mrefu
zisibadilishwe.
Kanuni hii ni muhimu sana katika ukubalifu wa istilahi
zinazoundwa.
Ni muhimu kabla ya kuunda istilahi mpya kuchunguza iwapo
hakuna
istilahi inayotumika tayari ambayo inawakilisha kw usahihi dhana
inayokusudiwa.
Uzoevu wa BAKITA umeonyesha kuwa ni vigumu kwa istilahi
mpya
kukubaliwa na kushamiri pale ambapo tayari kulikuwa na istiahi
zilizokuwa
zikitumika, hasa zile za muda mrefu. Kwa mfano neno Ovataimu
(overtime)
lililokuwa limezoeleka kwa muda mrefu limeendelea kutumika
badala
ya neno ajari. Vivyo hivyo neno Mdai (creditor) limeendelea kutumika
badala
ya neno Mwia. Maneno yote mawili ni ya siku nyingi lakini neno mdai
limezagaa
zaidi katika matumizi kuliko neno mwia.
3.0
Vyanzo vya istilahi
BAKITA
linafuata utaratibu ufuatao ili kupata istilahi sanifu:
(a)
Hazina ya Kiswahili chenyewe
Hazina
ya Kiswahili chenyewe huhusisha Kiswahili na lahaja nyingine za Kiswahili.      
 Kwa kawaida kabla ya kutafuta kisawe cha
Kiswahili cha istilahi iliyo katika lugha ngeni,
wataalamu
wa uwanja husika huhusishwa kikamilifu ili kueleza kwa ukamilifu dhana au
maana
ya istilahi hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya Kusanifu Istilahi. Baada ya hapo
wajumbe
huanza kutafuta iwapo kuna kisawe katika Kiswahili Sanifu cha istilahi
iliyotolewa.
Kama kisawe hakipatikani katika Kiswahili Sanifu wajumbe hutafuta kama
kuna
neno katika lahaja za Kiswahili. Mifano michache jinsi mbinu hii ilivyotumika
ni
istilahi
zifuatazo:
Chovyo
(oedema) kutoka lahaja ya Kipemba
Mbolezi
(elegiac poetry) kutoka lahaja ya Kimvita
Ng’ozi
(leaf curl) kutoka lahaja ya Kimtang’ata
Kisabeho
(breakfast) kutoka lahaja ya Kipemba (kutokana na Kitenzi kusabehe)
Kiangata
(hob) kutoka lahaja za Kiamu na Kisiu
Hazina
ya Kiswahili chenyewe pia huhusu mbinu mbalimbali zinazoweza kuunda
maneno
ya Kiswahili kwa njia ya kunyumbulisha mzizi waneno, kufinyaza maneno au
kwa
njia ya kuunganisha maneno:
Finyazo
Chakula
cha jioni = Chajio
Chemchemi
ya maji moto = Chemimoto
Mfupa
wa paja = Fupaja
Hati
ya kukataza kuiga = Hataza
Bara
lililozama = Barazama
Matuta
kama ngazi = Matungazi
Huduma
hadi bandarini = Huhaba
Huduma
hadi melini = Huhame
Utando
mwembamba wa ogani = Utandogani
Teknolojia
ya habari na mawasiliano = Teknohama nk.
Jambo
la kuzingatia ni kwamba mbinu hii inapaswa itumiwe kwa uangalifu sana ili
istilahi
itakayotokana nayo iwasilishe dhana kwa usahihi na pia iwe na uangavu wa
kutosha
kwa watumiaji. Kama mojawapo kati ya sifa hizo ikipuuzwa istilahi haitakuwa
sahihi
ipasavyo na wala uangavu ukipuuzwa istilahi haitapata nguvu ya kusambaa na
kushika
mizizi baina ya watumiaji.
Muunganiko
wa maneno
Mbinu
hii hutumika hasa kwa lengo la kufupisha istilahi ndefu kwa kuondoa viunganifu
au
umilikaji.
Kipima
pembe kwa ubapa = Kipimapembe ubapa
Doa
la kutu = Doakutu
Nyundo
ya rungu = Nyundorungu
Mwana
+ harakati = Mwanaharakati
Mwendo
wa kasi = Mwendokasi
Nishati
iliyotulia = Nishati tuli
Nishati
yenye mwendo = Nishati mwendo
(b)
Hazina ya lugha za Kiafrika
Lugha
za Kiafrika ni chanzo kingine ambacho husaidia kuunda visawe vya Kiswahili.
Hazina
hii hutumiwa pale hazina ya Kiswahili chenyewe inaposhindwa kukidhi haja ya
kupata
istilahi mwafaka inayoweza kuwakilisha dhana inayoshughulikiwa. Upendeleo
hutolewa
kwanza kwa lugha za Kibantu kwa sababu Kiswahili chenyewe ni mojawapo
kati
ya lugha za kundi hilo. Kwa hiyo maneno yanayotoka katika lugha za kundi hili
hata
yachukuliwapo
katika Kiswahili yatakuwa na uangavu wa kutosha kwa watumiaji wa
Kiswahili.
Kwa sasa BAKITA limekuwa likitafuta maneno yaliyo katika lugha za
Kibantu
za Tanzania kuliko za nchi zingine. Jambo la kuzingatia kamam ilivyokwisha
kudokezwa
katika kanuni ya kukopa au kutohoa ni kwamba maneno yanayochukuliwa
kutoka
huko hurekebishwa ili yatii kanuni ya muundo wa Kiswahili hasa katika maumbo
yake
na pia jinsi yanavyopaswa yapatanishwe yatumikapo katika sentensi. Mifano
michache
kutoka hazina hii ni kama ifuatayo:
Neno
la asili Istilahi Kisw) Umoja (Kisw) Wingi Upatanisho
Lishiganga
(Kisukuma) Shiganga (boulder) Ø Ma- li- yaAkasoko
(Kinyakyusa)
Kasoko (cardella) N- N- I- ziOlweya
(Kihaya)
Lweya (plain land) N- N- I- zi
Itepo
(Kimwera) Tepo(clone) Ø Ma- A- wa-
 au pia N- I- ziUlugiligili
(Kinyakyusa)
Giligili (synovial fluid) N- N- I- zi-
Lugha
zingine za Tanzania ambazo si za Kibantu pia zimetoa mchango wa kupata istilahi
za
Kiswahili. Utaratibu unaofuatwa umekuwa ni uleule wa kuchukua neno la asili na
kulirekebisha
ili lichukue umbo na kanuni za sarufi ya Kiswahili. Mifano michache
iliyotokana
na hazina hiyo ni kama ifuatayo:
Embuti
(Kimasai) Mbuti (Kiswahili) duodenum
Engalem
(Kimasai) Ngalemu (Kiswahili) carving knife
Kamongo
(Kijaluo) Kamongo (Kiswahili) cat fish nk
Hazina
ya lugha za Kiafrika pia imehusisha lugha zisizo za Kibantu zinzazotumiwa nje
ya
Tanzania. Mpaka sasa mchango uliopatikana umetoka katika baadhi ya lugha za
Afrika
Magharibi. Mifano michache iliyotokana na lugha hizo ni kama ifuatayo:
Kola
(Kihausa, Kiibo, Kiyoruba) Kola (Kiswahili) kola nut
Rara
(Kiyoruba) Rara(Kiswahili) ballad
Dyeli
(Kimaninke, Kisusu) Yeli (Kiswahili) griot
Juju
(Kiyoruba, Kiibo, Kipijini) Juju (Kiswahili) complex witchcraft nk
©
Lugha za Kigeni
Sehemu
kubwa sana ya istilahi za Kiswahili imetokana na Kiingereza na Kiarabu. Lugha
zote
hizi mbili zimekiathiri sana Kiswahili katika uwanja huu na msamiati kwa jumla
kutokana
na sababu za kihistoria kwamba pamekuwa na uhusiano wa kutawala na
kutawaliwa.
Maneno mengi mno ya Kiingereza na Kiarabu yametoholewa katika
Kiswahili,
hata pasipokuwa na sababu za kutosha, kiasi kwamba baadhi ya wataalamu
hushuku
kwamba lazima Kiswahili kiachane na tabia hiyo kwa kujitahidi kutazama
hazina
iliyo ndani ya Kiswahili chenyewe au katika lugha za Kiafrika.
Kama
ilivyokiwsha kudokezwa kinachofanyika wakati wa kutumia hazina kutoka
lugha
hizi mbili ni kurekebisha maneno ya lugha hizo ili yakubaliane na mfumo wa
matamshi
na othografia ya Kiswahili. Mifano michache kati ya mingi tuliyo nayo ni
kama
ifuatayo:
Psychology
= Saikolojia
Commissioner
= Kamishena
Oxygen
= Oksijeni
Hormone
= Homoni
Element
= Elementi
Vitamin
= Vitamini
Uterus
= Uterasi (Mji mimba)
Chocolate
= Chokoleti/ chakleti
Chlorine
= Klorini nk.
Kwa
kuchunguza orodha ya istilahi za Kiswahili iliyopo inaelekea utohoaji wa maneno
ya
Kiingereza na Kiarabu ndicho chanzo kikuu cha istilahi za Kiswahili badala ya
kwamba
hazina ya Kiswahili chenyewe inapaswa kuwa ya kwanza ikifuatwa na hazina ya
lugha
za Kiafrika.Ziko sababu nzuri tu wakati mwingine wa kuhitaji kuendeleza
ukubalifu
wa istilahi kimataifa. Yako maneno ambayo kwa mfano majina ya waasisi wa
uvumbuzi
Fulani ndiyo pia istilahi ya kitajwa kinachohusika. Lakini maneno hayo si
mengi
sana katika maarifa ya utaalamu wenyewe. Waswahili hawana budi kuchungua
vyanzo
vyao kikamilifu kwanza kabla ya kukkimblia kutohoa. Kanuni za unyambulishaji
wa
maneno, uhusianishaji wa dhana katika kikoa kimoja uwe ndilo jambo la
kuzingatia
awali
ya yote katika usanifishaji wa istilahi.
4.0
Matatizo
Ingawa
misingi na mbinu zilizotajwa zimesaidia sana kupata na kusanifisha visawe vingi
vya
Kiswahili lakini yapo matatizo yaliyojitokeza katika kutekeleza kazi hiyo. Hapa
yataelezwa
machache angalau kwa kifupi ili inapobidi hadhari ichukuliwe. Kimsingi
matatizo
haya yanagusia utumiaji wa hazina ya Kiswahili chenyewe na lahaja zake na
hata
lugha za Kiafrika, suala la kutumia finyazo kama mbinu ya kuunda istilahi na
utusaji.
Hazina
ya Kiswahili na lugha za Kiafrika
Kwa
utaratibu ambao BAKITA limejiwekea ili kupata istilahi, Kiswahili chenyewe na
lahaja
zake ndiyo hazina ya kwanza. Lakini hazina hii haijatumika kikamilifu
inavyopaswa
kwa sababu mbalimbali. Lugha za Kiingereza na Kiarabu zimetagaa sana
katika
uundaji wa istilahi kwa sababu lugha hizi ziliwahi kuwa lugha za watawala
nchini
mwetu
na zikapata hadhi ya pekee. Waundaji wa istilahi huziona kama kimbilio ili
kurahisisha
kazi yao kwa kutohoa istilahi zinazoletwa katika orodha. Laiti utafiti wa
kutosha
katika uwezekano wa kunyumbua maneno ya Kiswahili chenyewe, au
kuchekecha
msamiati ulio katika lahaja za Kiswahili ingeshangaza jinsi hazina ya
Kiswahili
ilivyo pana na ilivyo na uwezo wa kuziba mapengo yaliyopo ya istilahi.
Kadhalika
hazina kubwa bado inalala tuli katika lugha za Kiafrika hasa zikichambuliwa
kwa
kuzingatia mazingira ya kijiografia au shughuli za kiuchumi katika maeneo
zinamozungumzwa.
Mbinu
ya kutumia finyazo
Kama
ilivyokwisha kudokezwa, uundaji wa istilahi kwa kutumia finyazo hauna budi
ufanywe
kwa makini sana ili istilahi iwakilishe kwa usahihi dhana inayokusudiwa na
wakati
huohuo iwe angavu ili watumiaji waweze kupata angalau fununu ya dhana hiyo.
Baadhi
ya mifano tuliyoitoa awali katika kueleza mbinu hii yaweza ktumika hapa ili
kudhihirisha
ugumu wa kuitumia.
Chemchemi
ya maji moto = Chemimoto (Je, dhana ya maji imewakilishwa?)
Huduma
hadi bandarini = Huhaba (Je, istilahi hii ni angavu vya kutosha kuwapa
watumiaji
fununu ya dhana inayowakilishwa?)
Utando
mwembamba wa ogani = Utandogani (Je, dhana ya mwembamba imewakilishwa
katika
istilahi hii?)
Ushiriki
katika hali ya mtu mwingine (empathy) = Ushirikali (Je, istilahi hii
inazingatia
hali
ya mtu mwingine? Je, inao pia uangavu unaokusudiwa?)
Pengine
jambo la msingi ni kuzingatia kwamba istilahi ni neno maalumu kwa dhana
maalumu
na hivyo suala la uangavu halipaswi kutiliwa mkazo sana. Lakini kama hivyo
ndivyo,
basi ni bora kuepuka finyazo na kutafuta mbinu nyingine itakayoweza kukidhi
haja
hiyo kwa ukamilifu zaidi.
Utusani
Sayansi
inataka dhana iwakilishwe kikamilifu bila hoja ya mzungukozunguko. Koleo
liitwe
koleo na si kitu kingine. Hali hiyo inadai utamaduni wa watumiaji wa lugha,
wakiwemo
watumiaji wa Kiswahili, wasiyaonee aibu maneno ambayo yanaweza kuwa
matusi
katika matumizi ya kawaida. Zaidi ya hayo ili kutimiza lengo la kuunda istilahi
maneno
ambayo pengine ni matusi katika lugha ambayo si Kiswahili hayapaswi
kutazamwa
kama matusi katika lugha hiyo au katika Kiswahili chenyewe.
MAREJEO
BAKITA
(1974 – 1983). Istilahi Sanifu (Namba 1 – 5)
BAKITA
(1979). KAKULU (Kamati ya kusanifu Lugha) Na.3
ISO
(1968). R 704-1968. Naming Principles
Kiingi,
K. B. (1981). Swahilization of International Scientific Vocabulary (Mimeo)
Mkude,
D. J. (2004). “Usuli na Umuhimu wa Istilahi katika Maendeleo ya Jamii” Makala
iliyowasilishwa
katika Warsha ya Mafunzo ya Uundaji wa Istilahi za Mradi wa
Istilahi
za Mikrosofti, Juni 2004, Dar es Salaam. Haijachapishwa
Mtesigwa,
P.C.K. (1983). Ethnolects as a source of Swahili technical terms: A case of
Kikerewe
fisheries terminology. Tasnifu ya MA (Linguistics), Chuo Kikuu cha Dar
es
Salaam. Haijachapishwa
Mwansoko,
H. J. M. (2004). “Misingi ya Uundaji wa istilahi” Kitini kilichowasilishwa
katika
Warsha ya Mafunzo ya Uundaji wa Istilahi za Mradi wa Istilahi za
Mikrosofti,
Juni 2004, Dar es Salaam. Haijachapishwa
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-11-06T11:12:07Z 2021-11-06T11:12:07Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1415 <![CDATA[JARIDA LA LUGHA YETU (BAKITA)]]>
.pdf   Jarida la Lugha Yetu_3.pdf (Size: 1.12 MB / Downloads: 2) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-09T04:00:02Z 2021-09-09T04:00:35Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1205 <![CDATA[Toka TUKI mpaka TATAKI]]> Leo hii mbalamwezi ya Kiswahili inaangazia historia ya iliyokuwa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (Tuki) ambayo sasa inaitwa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (Tataki) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
MBALAMWEZI ya Kiswahili imekuwa ikipokea maoni mengi kutoka kwa wapenzi wa Kiswahili kuhusiana na mada mbalimbali zinazojadiliwa katika safu hii.
Nyote mnapongezwa kwa maoni yenu na kuonyesha mapenzi makubwa ya lugha ya Kiswahili. Mnapokuwa na maoni na maswali msisite kuyatoa kwani safu hii ipo kwa ajili yenu.
Leo hii mbalamwezi ya Kiswahili inaangazia historia ya iliyokuwa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (Tuki) ambayo sasa inaitwa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (Tataki) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Lengo la kufanya hivi ni kutoa ufafanuzi mintarafu Tuki na Tataki kwa wasomaji wakiwamo walimu, wanafunzi wa shule za sekondari walioomba maelezo kuhusu matumizi ya majina haya ambapo wengine huchukulia kuwa ni taasisi mbili tofauti.
Awali ya yote ifahamike kwamba taasisi hii ni moja na siyo mbili tofauti.
Historia ya Tataki ilianza mwaka 1930 kwa iliyokuwa Kamati ya Lugha ya Afrika Mashariki. Kamati hii ilikuwa na majikumu kadhaa miongoni mwake ni kusanifisha Kiswahili kinachotumika katika shughuli rasmi katika Afrika Mashariki.
Pia kusimamia maendeleo ya lugha hii; kusoma miswada; kusahihisha na kutoa ithibati; kuteua vitabu vya kutumika shuleni; kutafsiri vitabu vya lugha za kigeni kwa Kiswahili; kufanya utafiti katika nyanja za sarufi na fasihi; kuchapisha na kusambaza matokeo ya utafiti unaofanywa.
Mwaka 1961 UDSM ilipoanzishwa kama Chuo Kikuu Kishiriki cha London Kamati ya Lugha ya Afrika Mashariki ilihamishiwa katika Chuo Kikuu cha Makerere , Uganda.
Ilipofika mwaka 1964 kamati ilibadilisha jina na kuitwa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI).
Jina hili limegonga masikio ya wengi na kuganda akilini kutokana na huduma zake.
Majukumu
Aidha, Taasisi hii imekuwa na majukumu mengi ambayo ilikuwa inayatekeleza kama vile kuratibu msamiati, kuunda istilahi mpya za kitaaluma, kufanya utafiti katika nyanja za mofolojia, sintaksia, fonolojia, isimu jamii na dialektolojia; kuratibu na kutafsiri matini za Serikali, viwanda na taasisi binafsi ndani na nje ya nchi.
Kwa nini Tataki?
Akizindua Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (Tataki) Juni 2009 aliyekuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda alilipongeza Baraza la Chuo kwa kusimamia vyema mpango mkakati wa mageuzi ya chuo ambao ulihusisha kuunganisha idara anuwai chuoni hapo kwa lengo la kupanua wigo na kuongeza ubora katika ufundishaji, utafiti na utoaji huduma kwa jamii.
Hivyo, kutokana na mpango mkakati uliowekwa na chuo hicho kwa lengo la kustawisha huduma, iliyokuwa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (Tuki) na iliyokuwa Idara ya Kiswahili chini ya Kitivo cha Fani za Sayansi za Jamii ziliungana na kuwa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (Tataki).
Tangu mwaka huo Tataki imekuwa ikidahili wanachuo wa shahada za awali na umahiri kufundisha na kufanya utafiti. Mwaka 2014 taasisi ilianzisha programu ya shahada ya uzamivu kwa tamrihi na tasnifu.
Wafuatao ni wakurugenzi wa Tuki/Tataki tangu kuanzishwa kwake: G. Mhina (1970 – 1976), A.M. Khamisi (1976 – 1982), C.W. Temu (1982 – 1985), D.P. Massamba (1985 – 1991), S.Y. Sengo (1991 – 1994).
Wengine ni S.A.K. Mlacha 1994 – 2000), M.M. Mulokozi (2000 2006) J. G. Kiango, (2006 – 2009), A.K. Mutembei (2009 – 2013), Murugenzi wa sasa E.S. Mosha 2013 hadi sasa).
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-09T03:49:45Z 2021-09-09T03:49:45Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1204 <![CDATA[VYOMBO VYA UKUZAJI NA UENEZAJI WA KISWAHILI]]> Vyombo vya ukuzaji na uenezaji wa Kiswahili
Ili kuimarisha matumizi ya lugha ya Kiswahili serikali iliamua kuanzisha vyombo mbalimbali vya ukuzaji wa Kiswahili. Katika mada hii utaweza kujua vyombo mbalimbali vya kitaifa na kimataifa vinavyojishughulisha na ukuaji na uenezaji wa Kiswahili. Pia utaweza kujua majukumu ya kila chombo kataka ukuaji na uenezaji wa Kiswahili.
Tangu Tanzania ipate uhuru hadi sasa kuna vyombo kadha wa kadha vilivyoanzishwa kwa ajili ya kukuza na kueneza Kiswahili baadhi ya vyombo hivyo ni hivi vifuatavyo:
BAKITA
Hii ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa sheria ya Bunge Na.27 ya mwaka 1967 kwa madhumuni ya kukuza Kiswahili. Kutokana na sheria hii Baraza ndilo mratibu wa kusimamia asasi zote na mawakala wote wanaokuza Kiswahili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
BAKITA imekuwa na mchango mkubwa sana katika ukuzaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili kupitia majukumu yake. Majukumu ya Baraza kama yalivyofafanuliwa katika sheria hiyo ni haya yfuatayo:
  • Kuratibu na kusimamia maendeleo na matumizi ya Kiswahili nchini kote. Katika kufanya hivi Baraza lina jukumu la kuhakikisha Kiswahili kinaendelea na kuhakikisha kuwa matumizi ya Kiswahili yanakuwa sahihi.
  • Kushirikiana na vyombo vingine nchini vinavyojihusisha na maendeleo ya Kiswahili na kuratibu shughuli zao. Vyama vya Kiswahili kama vile CHAKAMA, CHAWAKAMA vina mchango mkubwa wa kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili kwa kushirikiana na BAKITA. Ushirikiano wa BAKITA na vyama hivi waweza kuwa ni wa kuto ushauri, au msaada wa kifedha, kwa mfano BAKITA imekuwa ikiwasaidia CHAWAKAMA pale wanapokuwa wanataka kufanya makongamano nap engine wanahitaji msaada wa kifedha, kwa hiyo BAKITA imekuwa ikiwasaidia kifedha.
  • Kuhimiza matumizi ya Kiswahili katika shughuli rasmi na za kawaida. BAKITA imekuwa ikiandaa vipindi mbalimbli redioni ili kuhimiza matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili.
  • Kushirikiana na mamlaka zinazohusika kuthibitisha tafsiri sanifu za istilahi. Katiaka uundaji wa istilahi, BAKITA imekuwa ikichapisha vitabu mbalimbali ikionesha istilahi sanifu zilizoingizwa katika lugha ya Kiswahili. kwa hiyo kupitia jukumu hili Kiswahili kimekuwa kinakua.
  • Kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa serikali, mashirika ya serikali na yasiyo yaserikali na asasi nyingine. Kupitia tafsiri zinazofanywa na BAKITA Kiswahili kimekuwa kikikuwa na kuenea.
  • Kuchapisha jarida au toleo linalohusu lugha na fasihi ya Kiswahili. Machapisho haya ya BAKITA yanaendelea kukifanya Kiswahili kukua kwa kuongeza msamiati mpya na hivyo watu wanaposoma machapisho hayo wanajifunza msamiati mpya na hivyo kufanya Kiswahili kukua.
  • Kushirikiana na mashirika ya kitaifa, asasi na watu binafsi, kufuatilia, kushauri na kusimamia shughuli zinazolenga kukuza Kiswahili nchini Tanzania.
  • Kutoa ushauri kwa waandishi na wachapishaji ili watumie Kiswahili fasaha. Kwa kufanya hivi matumizi bora ya Kiswahili yanakuwa yanaimarika.
  • Kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuthibitisha vitabu vya Kiswahili vitakavyotumika shuleni na vyuoni kabla havijachapishwa. Hili pia ni jamabo linaloimarisha matumizi ya Kiswahili sanifu.
TAKILUKI
Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni (TAKILUKI) ilianzishwa mwaka 1979 kwa lengo la kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Zanzibar, ili kutimiza lengo hilo TAKILUKI inajishughulisha na kazi zifuatazo:
  • Kuratibu na kuendesha mafunzo ya lugha ya Kiswahili visiwani Zanzibar, kuendesha mafunzo ya lugha ya Kiswahili kwa wazawa na wageni, kuhariri miswada mbalimbali ili kuthibitisha ufasaha wa Kiswahili na kufanya tafiti za Kiswahili katika Nyanja zake zote, hususani katika uwanja wa sarufi na fasihi.
  • Pia TAKILUKI wana kazi ya kuandaa istilahi za taaluma mbalimbali, kutoa huduma za taaluma mbalimbali, kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa lugha mabalimbali kwa mashirika, idara, wizara, taasisi, kampuni na watu binafsi, kufundisha lugha za kigeni na kuandika vitabu mbalimbali vya Kiswahili.
  • Pia hujishughulisha na utoaji wa ushauri wa kitaaluma kwa watunzi wa vitabu ili waweze kuandika kazi zenye ubora, na kushirikiana na wadau wengine wa Kiswahili kama vile, mashirika, wizara, taasisi, vyuo na watu binafsi katika kuendesha shuguli za ukuzaji wa Kiswahili, mathalani kuandaa na kuendesha semina, warsha na kozi fupifupi za Kiswahili.
  • Vilevile hujishugulisha na usimamizi na ufuatiliaji wa matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili katika vyombo vya habari na katika shughuli mbalimbali za serikali na za kawaida.
TUKI/TATAKI
Majukumu ya TUKI ni pamoja na kuunda sera muafaka za kustawisha Kiswahili na pia kufanya utafiti katika lugha ya Kiswahili.
Majukumu mengine ya TUKI ni kuhariri, kuchapisha vitabu na kutawanya vitabu na majarida ya kitaaluma katika Kiswahili.
Kwa sasa TATAKI inatoa shahada ya awali na uzamili katika lugha ya Kiswahili, kwa njia hii inawaandaa wataalamu wa lugha ya Kiswahili ambao watatumika sehemu mbalimbali za ulimwengu kufundisha lugha ya Kiswahili.
CHAUKIDU
CHAUKIDU ni kifupi cha Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani, makao makuu ya chama hiki kwa sasa yapo chuo kikuu cha Wisconsin-Madison, Marekani.
Madhumuni makuu ya CHAUKIDU ni: Kuwajumuisha pamoja wakuzaji wa Kiswahili duniani kote kwa lengo la kuchochea kasi ya malengo mahususi yafuatayo:
  • Kukuza Kiswahili katika nyanja zote ambamo lugha hii inatumika au inaweza kutumika na kuongeza ufanisi wa mawasiliano katika ufundishaji na utafiti wa maarifa ya aina zote, uandishi/utangazaji wa habari, uandishi wa vitabu, uchapishaji vitabu na majarida, utayarishaji wa safari za mafunzo katika Afrika ya Mashariki na Kati, n.k.
  • Kusambaza habari na matokeo ya utafiti kwa kutumia machapisho mbalimbali na teknolojia ya mtandao wa kompyuta juu ya vipengele mbalimbali vya Kiswahili na masuala yanayohusiana na Kiswahili.
  • Kuwajumuisha wanachama kwa ajili ya kubadilishana mawazo na tajiriba zao katika masuala mbalimbali yanayohusu Kiswahili (k.v. uboreshaji wa ufundishaji, utangazaji, utafiti, uandishi, nk.) kwa njia ya mkutano wa kila mwaka, warsha au semina au kongamano maalumu, na hata kwa njia ya mtandao.
  • Kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kujivunia, kuendeleza, na kuheshimu Kiswahili.
  • Kushauri ama kushinikiza serikali za nchi ambamo Kiswahili kinazungumzwa kutambua thamani iliyobebwa na maliasili hii ili kuunda sera muafaka za kukiendeleza kadri ya uwezo wake kwa manufaa ya maendeleo ya serikali na watu wake kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, kielimu, n.k.
CHAWAKAMA
CHAWAKAMA husimama badala ya Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili vyuo vikuu Afrika Mashariki. Chama hiki kilianzishwa mwaka 2004 kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili katika eneo lote la Afrika Mashariki kupitia wanafunzi wanaosoma Kiswahili vyuoni. Wanachama wa chama hiki ni wale wanosoma Kiswahili na hata wale wenye mapenzi ya lugha ya Kiswahili pia wanaweza kujiunga na chama hiki.
Chama hiki kina utaratibu wa kuandaa makongamano ambapo wanachama wake kutoka nchi zote za Afrika Mashariki hupata fursa ya kukutana mara moja kila mwaka. Pamoja na utaratibu wa chama kuandaa makongamano pia uanzishwaji wake umeambatana na malengo kadhaa ambayo ndiyo dira inayoiongoza chama kwa mujibu wa katiba, malengo hayo ni haya yafuatayo:
  • Kuwapa wanachama nafasi ya kujadili, kuimarisha, kuendeleza na kukuza vipawa vyao vya lugha na fasihi ya Kiswahili.
  • Kuamsha ari ya mapinduzi ya utamaduni wa lugha ya kiswahili.
  • Kueneza lugha ya kiswahili ndani na nje ya nchi.
  • Kushirikiana na vyama vingine katika juhudi za kuendeleza na kuimarisha lugha ya kiswahili ndani na nje ya nchi wanachama.
  • Kuwaunganisha wanafunzi wa kiswahili Afrika Mashariki na kati katika kukikuza kiswahili.
  • Kushirikiana na asasi mbalimbali zinazojihusisha na ukuzaji na uenezaji wa kiswahili ndani na nje ya nchi kama vile BAKITA, TATAKI, TAKILUKI, UWAVITA, CHAKAMA, BAKIZA n.k.
  • Kuchapisha kijarida cha chama na machapisho mengine ili kusaidia kueneza taaluma ya kiswahili.
  • Kuweka kumbukumbu ya wataalamu wa kiswahili kwa nia ya kuwatumia katika kufanikisha malengo ya chama na wadau wa Kiswahili.
  • Kuratibu makongamano na mijadala mbalimbali inayohusiana na taaluma ya kiswahili.
Pamoja na malengo hayo, lengo kuu la chama hiki ni kueneza Kiswahili lakini sasa wanakienezaje? Wanachama wa chama hiki ambao ni nchi wanachama wa jumuia ya Afrika mashariki wanakawaida ya kuandaa makongamano kwa ngazi ya kitaifa na ngazi ya kimataifa.
Kwa ngazi ya kitaifa kila nchi huandaa kongamano kila mwaka ambalo linawakutanisha wanachama wote kutoka vyuo mbalimbali katika nchi husika. Katika kongamano hilo mada mbalimbali zinazohusu lugha ya Kiswahili na mustakabali wake hujadiliwa lakini pia maazimio mbalimbali huchukuliwa juu ya maendeleo ya chama. Sasa katika mijadala kama hii inatoa nafasi ya Kiswahili kukua kwani makala mbalimbali huandikwa ambazo pia husomwa na watu mbalimbali. Makala hizi pia zimekuwa zikichapishwa katika majarida ya chuo husika na pia zimekua zikichapishwa mtandaoni ambapo hutoa fursa kubwa kwa watu wengi zaidi kuzifikia na kusoma, hivyo kwa njia hiyo Kiswahili kinakua kimeenea.
MAFANIKIO NA CHANGAMOTO ZINAZOVIKABILI VYOMBO VYA UKUZAJI WA KISWAHILI
Mafanikio
  • Vyombo vya ukuzaji wa Kiswahili vimejitahidi sana kukuza lugha ya Kiswahili, kwa hali ya Kiswahili ilivyo sasa ni matokeo ya juhudi za vyombo hivyo. Mafanikio ya vyombo hivyo ni pamoja na haya yafuatayo:
  • Machapisho ya lugha ya Kiswahili ni mengi sana nchini na nje ya nchi, kufanya mafunzo ya Kiswahili, kukua kwa matumizi ya Kiswahili na kuongezeka kwa idadi ya watumiaji wa Kiswahili nchini.
  • Matumizi ya lugha ya Kiswahili katika sehemu rasmi hasa katika ofisi za serikali na ofisi za watu binafsi inadhihirisha mafanikio ya jitihada za vyombo hivi kuhimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili.
  • Kufundshwa kwa lugha ya Kiswahili kama taaluma kwa ngazi ya shahada ya awali, uzamili na uzamivu. Hizi ni jitihada za TATAKI katika kuhakikisha kunapatikana wataalamu wa lugha ya Kiswahili, hivi sasa TATAKI wanafundisha lugha ya Kiswahili kwa ngazi ya shahada ya awali, uzamili na uzamivu.
  • Matumizi ya lugha ya Kiswahili katika vyombo mabalimbali vya kimataifa, matumizi ya lugha ya Kiswahili katika vikao vya Umoja wa Afrika na pia ufundishwaji wa lugha ya Kiswahili katika vyo mabalimbali Duniani ni ishara tosha ya kuonesha mafanikio ya jitihada za vyombo vya ukuzaji na uenezaji wa Kiswahili.
Changamoto
Licha ya mafanikio hayo lakini pia kuna changamoto zinazovikabili vyombo hivi vya ukuzaji wa Kiswahili.
  • Vyombo hivi vinakabiliwa na upungufu wa wataalam. Wataalamu wengi waliobobea katika taaluma za Kiswahili wanakimbilia nje ya nchi wakidhani huko ndiko kuna maslahi mazuri zaidi.
  • Upungufu wa fedha za kuendeshea shughuli za ukuzaji wa Kiswahili katika vyombo hivi pia limekuwa ni tatizo sugu. Kwa hiyo shughuli za ukuzaji wa Kiswahili zinakuwa zinakwenda taratibu.
  • Taasisi hizi pia zinashindwa kujitangaza vizuri kutokana na kwamba hazina vyombo vya habari binafsi ambavyo vingeweza kutumika kutangaza shughuli zao. Jambo hili limesababisha vyombo hivi kushindwa kutoa elimu ya Kiswahili kwa kutumia vyombo vya habari kutokana na kwamba gharama za kufanya hivyo ni kubwa.
  • Vyombo hivi baadhi havina ofisi za kudumu, na hivyo kuhamahama jambo ambalo linaathiri utendaji kazi wa vyombo hivyo.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-08T04:57:18Z 2021-09-08T04:57:18Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1190 <![CDATA[KATIBA YA CHAWAKAMA]]>
.pdf   KATIBA YA CHAWAKAMA.pdf (Size: 105.81 KB / Downloads: 1) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-08T04:17:06Z 2021-09-08T04:24:50Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1188 <![CDATA[TAASISI YA TAALUMA ZA KISWAHILI (TATAKI)]]> Taasisi ya Taaluma za Kiswahili
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) ni idara ya Chuo Kikuu cha Dar es SalaamTanzania. Taasisi hii ni miongoni mwa taasisi kongwe za lugha nchini Tanzania. Madhumuni yake yakiwa ni kusimamia usanifishaji na maendeleo ya lugha ya Kiswahili. Hadi mnamo mwaka 2009 taasisi hii ilijulikana zaidi kwa jina la TUKI au “Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili“
Historia yake
Ilianzishwa mnamo mwaka 1930 kama Inter-territorial Language (Swahili) committee ya Nchi za Afrika ya Mashariki, baadaye ikaitwa Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki. Mnamo mwaka 1964 kamati ilifanywa kuwa Sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaamu. Baadaye ikaitwa Chuo cha Uchunguzi wa Lugha ya Kiswahili. Tangu 1970 kimepewa jina la Taasisi ya Uchunguzi wa Lugha ya Kiswahili. Mwaka 2009, TUKI iliungana na iliyokuwa Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuunda Taasisi kubwa zaidi inayoitwa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili – TATAKI
Majukumu
Mwanzoni, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ni taasisi ya utafiti ilipewa jukumu la kutafiti nyanja zote za lugha ya Kiswahili, fasihi na utamaduni, na kuchapisha matokeo ya utafiti huo. Hivyo pamoja na BAKITA (Baraza la Kiswahili Tanzania) TUKI ndiye mlinzi wa usanifu wa lugha ya Kiswahili katika Tanzania. Baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili, sasa TATAKI inafundisha Isimu, Fasihi na Historia ya Lugha ya Kiswahili katika Shahada za Awali, Mahiri na Uzamivu.
Kazi yake
Kutafiti na kuchapisha matokeo ya utafiti katika nyanja mbalimbali za Lugha, Isimu na Fasihi ya Kiswahili, TATAKI inasimamia Tafsiri na Ukalimani. Inafundisha Kiswahili kama lugha ya pili hasa kwa wageni kutoka nje ya ulimwengu wa Waswahili na kuendeleza utungaji wa Kamusi mbalimbali zinazohusiana na Kiswahili. Kati ya kamusi hizi ni
TUKI imehariri toleo la Kiswahili la “Historia Kuu ya Afrika” iliyotungwa na kamati ya wataalamu ya UNESCO

Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ( TATAKI) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni asasi kongwe inayojishughulisha na ufundishaji, utafiti na utoajiushauri wa kitaaluma katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili. TATAKI inadhamana ya kufundisha na kutafiti vipengele vyote vya lugha, kwa kuzigatia vipaumbele vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
HISTORIA YA TATAKI
TATAKI ni Taasisi yenye historia ndefu kuliko Taasisi zote zinazohusika na ukuzaji na uendelezaji wa lugha ya Kiswahili duniani. Historia ya TATAKI inaanzia mwaka 1930 ilipoanzishwa kamati ya lugha (ya Kiswahili) ya Afrika Mashariki. Mnamo mwaka 1961 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilianzishwa kama Chuo Kikuu Kishiriki cha London.
Kuanzia mwaka 1962, viongozi wa kamati waliaza kufikiria kuhamisha shughuli za kamati kwenye Chuo Kikuu kimojawapo. Vyuo vilivyofikiriwa ni Makerere na Dar es Salaam. Mwaka 1963 shughuli za kamati zilihamishiwa katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam na hatimye kamati ilibadili jina na kuwa Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili. Majukumu ya Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili hayakutofautiana na yale ya kamati ya lugha.
Mwaka 1970 baada ya kuanzishwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndipo Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) ikaanzishwa chini ya ibara ya 22(3) ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Katika kipindi hiki ilianzishwa pia idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyokuwa chini ya Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii. Miongoni mwa majukumu ya idara ilikuwa ni kufundisha lugha ya Kiswahili kwa wanafunzi kutoka ndani na nje ya Tanzania. Kuanzia mwanzoni mwa miaka 2000, Chuo Kikuu kilianza kupitia upya muundo wake ili kufanyakazi kwa ufanisi na weledi. Katika mchakato huo yalitolewa mapendekezo mbalimbali ilikiwa ni pamoja na kuunganisha vitengo ambavyo majukumu yake yalionekana kufanana. Kwa kuwa malengo ya idara ya Kiswahili na TUKI yalilenga kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili, mnamo mwaka 2009 iliyokuwa idara ya Kiswahili ikaungana na TUKI na kuunda Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI). Majukumu ya TATAKI sasa yamejikita katika utafiti wa Nyanja mbalimbali zihusuzo lugha na fasihi ya Kiswahili katika ngazi mbalimbali.
TATAKI inaidara mbili ambazo ni idara ya lugha ya Kiswahili na isimu na idara ya fasihi, mawasiliano na uchapaji. Idara hizi kwa pamoja zinashirikiana katika ufundishaji wa programu mbalimbali taasisini kama inavyoainishwa hapa chini:
PROGRAMU ZINAZOFUNDISHWA NA TATAKI
1. B.A. Kiswahili
Ni shahada ya awali ambayo hutolewa katika muda wa miaka mitatu. Katika shahada hii, kozi mbalimbali za Isimu na Fasihi hutolewa. Masharti ya jumla ya udahili ya Chuo Kikuu huzingatiwa. Hata hivyo ili mwombaji adahiliwe katika programu ya B.A (kiswahili) anapaswa, pamoja na masomo mengine, awe amesoma somo la Kiswahili kidato cha tano na sita na kufaulu kwa wastani wa angalau alama D au awe na sifa zinazofanana na hizo.
2. M.A. Kiswahili
Hii ni shahada ua umahiri ambayo hutolewa kwa Tamrini na Tasnifu katika Isimu na Fasihi kwa muda wa miezi 18 (Tamrini na Tasnifu); na miezi 24 (kwa Tasnifu pekee). Ili kujiunga na programu hii mbali na sifa za jumla za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwombaji anapaswa kuwa amefaulu masomo ya Kiswahili katika shahada za awali kwa WAKIA (GPA) isiyopungua 3.0 kwa kozi za Kiswahili.
3.PhD. Kiswahili
Masomo katika programu hii hutolewa kwa namna mbili. PhD kwa Tamrini na Tasnifu.PhD kwa Tamrini hutolewa kwa muda wa miaka minne na PhD kwa Tasnifu hutolewa kwa muda wa miaka mitatu. Ilikudahiliwa katika programu hizi mwombaji anapaswa kuwa amesoma Kiswahili au masomo yanayoendana na umahiri. Lugha inayotumika kufundishia na kuandika ripoti ya utafiti kwa programu zote ni Kiswahili.
VITUO VYA TATAKI
Mbali na idara za ufundishaji, TATAKI pia hufanya kazi za kiutafiti kupitia vituo vya utafiti na ushauri.
KITUO CHA FASIHI YA KISWAHILI NA MAPOKEO YA SIMULIZI YA KIAFRIKA
Miongoni mwa majukumu ya kituo hiki ni kuratibu na kusimamia shughuli zote za utafiti katika nyanja mbalimbali; kuandaa na kuchapisha Makala na vitabu vyo kufundishia kozi za fasihi, mawasiliano na uchapishaji kwa Kiswahili; kutafiti kuhusu kazi za wanafasihi mbalimbali wa zamani na sasa; kukusanya na kuhifadhi data, nyaraka na taarifu muhimuza kifasihi.
KITUO CHA ISTILAHI, TAFSIRI, UKALIMANI NA TEKNOLOJIA YA LUGHA
Jukumu kuu la kituo hiki ni kutoa huduma zinazohusu masuala ya istilahi, tafsiri, ukalimani na teknolojia ya lugha. Kwa kiasi kikubwa kituo hiki hujihusisha na shughuli za tafsiri ya nyaraka mbalimbali kutoka katika asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali.
KITUO CHA KISWAHILI KWA WAGENI
Kituo hiki kinahusika na kuratibu shughuli zote za ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni. Wageni hufundishwa kwa vikundi au mtu mojamoja. Kituo pia kina mpango wa kujiimarisha na kuwa kituo cha weledi wa Kiswahili Ulimwenguni.
KITUO CHA KAMUSI NA SARUFI YA KISWAHILI
Hujishughuliasha na kufanya utafiti wa msamiati mpya unaotumika katika jamii na kuukusanya kwa  ajili ya kuboresha kamusi na vitabu vingine vya sarufi ya Kiswahili. Hivi sasa kituo kimeshatoa kamusi ya Kiingereza-Kiswahili na Kiswahili-Kiingereza kwa njia ya nakala ngumu na kwa njia ya simu ya kiganjani. Aidha kituo kwa kushirikiana na shirika la uchapishaji la OXFORD tawi la Nairobi wametoa matoleo kadhaa ya Kamusi ya Kiswahili Sanifu.
UDAHILI WA WANAFUNZI
Wanafunzi wenye lengo la kusoma programu zinazotolewa na TATAKI hudahiliwa kwa kuzingatia taratibu zote za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
TAARIFA NYINGINE
TATAKI pamoja na kujishughulisha na ufundishaji, utafiti na utoaji ushauri, hujishughulisha pia na shughuli za uchpaji na uchapishaji. Uchapishaji hulenga kazi zilizoandikwa kwa lugha ya Kiswahili na uchapaji hufanywa kwa kazi zote bila kujali zimeandikwa kwa lugha gani ilimradi kazi hizo zizingatiye maadili ya uchapaji wa kitaaluma kama ilivyoinishwa katika Sera ya Uchapaji na Uchapishaji wa TATAKI.
Aidha, TATAKI hutoa huduma ya ushauri wa kitaalamu kwa watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vya ualimu wanaokuja kufanyakazi mradi kwa lengo la kikamilisha matakwa ya kitaaluma katika masomo yao.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-08T04:05:22Z 2021-09-08T04:05:22Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1187 <![CDATA[Katiba ya Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU)]]>
.pdf   Katiba ya Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani.pdf (Size: 95.83 KB / Downloads: 3) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-07T14:11:50Z 2021-09-07T14:11:50Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1185 <![CDATA[NAFASI YA VYAMA NA TAASISI MBALIMBALI KATIKA MAKUZI YA KISWAHILI]]> Kwa Mukhtasari
IKIWA idara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI), awali ikiitwa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) ni miongoni mwa taasisi kongwe zaidi za lugha nchini Tanzania na Afrika Mashariki. Madhumuni yake ni kusimamia usanifishaji na maendeleo ya Kiswahili.
Japo Kiswahili kimeendelea kubaki nembo ya Afrika, mjadala usio na mwisho kuhusiana na ni ipi lugha ya kufundishia katika shule na vyuo nchini Tanzania ni ithibati kwamba Kiswahili hakijapokezwa hadhi inayostahiki katika mengi ya mataifa ya Afrika Mashariki na  Kati.
TUKI, kwa sasa TATAKI, ilianzishwa mnamo 1930 ikijulikana kama International-Territorial Language (Swahili) Committee kwa nchi tatu za Afrika Mashariki na baadaye ikaitwa Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki.
Mnamo 1964, kamati ilifanywa kuwa sehemu ya UDSM na baadaye ikaitwa Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili. Tangu 1970 kimepewa jina la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI). Mwaka 2009, TUKI iliungana na iliyokuwa Idara ya Kiswahili ya UDSM na kuunda taasisi kubwa zaidi inayoitwa TATAKI.
Majukumu ya taasisi hii awali yalikuwa ni kutafiti nyanja zote za lugha ya Kiswahili, fasihi na utamaduni na kuchapisha matokeo ya utafiti huo.
Hivyo pamoja na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), TUKI ni mlinzi wa usanifu wa lugha ya Kiswahili katika Tanzania. Baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili, sasa TATAKI inafundisha Isimu, Fasihi na Historia ya Lugha ya Kiswahili.
Inafundisha Kiswahili kama lugha ya pili hasa kwa wageni kutoka nje ya ulimwengu wa Waswahili na kuendeleza utungaji wa kamusi mbalimbali zinazohusiana na Kiswahili.
BAKITA
Ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa sheria ya Bunge Na.27 ya mwaka 1967 kwa madhumuni ya kukuza Kiswahili. Kutokana na sheria hii, Baraza ndilo mratibu wa kusimamia asasi zote na mawakala wote wanaokuza Kiswahili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
BAKITA imekuwa na mchango mkubwa katika ukuzaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili kupitia majukumu yake.
Miongoni mwa majukumu ya Baraza hili kama yalivyofafanuliwa katika sheria hiyo ni kuratibu na kusimamia maendeleo na matumizi ya Kiswahili nchini pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vinavyojihusisha na maendeleo ya Kiswahili.
Huhimiza matumizi ya Kiswahili katika shughuli rasmi na za kawaida, huandaa vipindi mbalimbali redioni ili kuhimiza matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili, hushirikiana na mamlaka zinazohusika kuthibitisha tafsiri sanifu za istilahi, hutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa serikali, mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali na asasi nyingine pamoja na kuidhinisha vitabu vya Kiswahili vitakavyotumika shuleni na vyuoni kabla havijachapishwa.
TAKILUKI
Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni (TAKILUKI) ilianzishwa mnamo 1979 kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili ndani na nje ya Zanzibar.
Inajishughulisha na kuratibu, kuendesha mafunzo ya Kiswahili visiwani Zanzibar, kuhariri miswada mbalimbali ili kuthibitisha ufasaha wa Kiswahili na kufanya tafiti za Kiswahili katika nyanja zake zote, hususan sarufi na fasihi.
TAKILUKI inatoa ushauri wa kitaaluma kwa watunzi wa vitabu ili waweze kuandika kazi zenye ubora, na kushirikiana na wadau wengine wa Kiswahili kuandaa na kuendesha semina, warsha na kozi fupifupi za Kiswahili.
CHAUKIDU
Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) kina makao makuu katika Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, Marekani.
Madhumuni yake ni kuwajumuisha pamoja wakuzaji wa Kiswahili duniani kote kwa lengo la kuchochea kasi ya malengo mahususi kama vile kukuza Kiswahili katika nyanja zote ambamo lugha hii inatumika na kuongeza ufanisi wa mawasiliano katika ufundishaji na utafiti wa maarifa ya aina zote mathalan uandishi na utangazaji wa habari, uandishi na uchapishaji wa vitabu na majarida pamoja na utayarishaji wa safari za mafunzo katika Afrika Mashariki na Kati.
Husambaza habari na matokeo ya utafiti kwa kutumia machapisho mbalimbali na teknolojia ya mtandao wa kompyuta kuhusu vipengele mbalimbali vya Kiswahili na masuala yanayohusiana na Kiswahili. CHAUKIDU inaelimisha umma juu ya umuhimu wa kujivunia, kuendeleza, na kuheshimu Kiswahili.
Vilevile inashauri ama kushinikiza serikali za nchi ambamo Kiswahili kinazungumzwa kutambua thamani iliyobebwa na maliasili hii ili kuunda sera mwafaka za kukiendeleza kadri ya uwezo wake kwa manufaa ya maendeleo ya serikali na watu wake kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kielimu.
CHAWAKAMA
Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili katika vyuo vikuu vya Afrika Mashariki (CHAWAKAMA), kilianzishwa mnamo 2004 kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili katika eneo lote la Afrika Mashariki kupitia kwa wanafunzi wanaosoma Kiswahili vyuoni. Wanachama wa chama hiki ni wale wanaosomea taaluma za Kiswahili ila wapenzi wa Kiswahili pia wanaweza kujiunga nacho.
Mara kwa mara, CHAWAKAMA huandaa makongamano kwa lengo la kuwapa wanachama nafasi ya kujadili, kuimarisha, kuendeleza na kukuza vipawa vyao vya lugha na fasihi ya Kiswahili, kuamsha ari ya mapinduzi ya utamaduni wa Kiswahili, kueneza Kiswahili ndani na
nje ya nchi, kushirikiana na vyama vingine katika juhudi za kuendeleza na kuimarisha Kiswahili ndani na nje ya nchi wanachama, kuwaunganisha wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki na Kati katika kukikuza Kiswahili pamoja na kushirikiana na asasi mbalimbali zinazojihusisha na ukuzaji na uenezaji wa Kiswahili.
CHAKAMA
Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA) ndicho cha tatu kwa umaarufu zaidi miongoni mwa wasomi, wataalamu na wahadhiri wa vyuo vikuu baada ya CHAUKIDU na Chama cha Walimu wa Lugha za Kiafrika (ALTA) ambacho haundaa makongamano yake jijini Bayreuth, Ujerumani. Kwa pamoja na Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA), CHAKAMA huchapisha jarida la chama na machapisho mengine ili kusaidia kueneza taaluma za Kiswahili.
Aidha, huhifadhi kumbukumbu za wataalamu wa Kiswahili kwa nia ya kutumia katika kufanikisha malengo ya chama na wadau wa Kiswahili pamoja na kuratibu makongamano na mijadala mbalimbali inayohusiana na taaluma za Kiswahili.
Chama huandaa makongamano kila mwaka ambalo linawakutanisha wanachama wote katika vyuo mbalimbali katika nchi husika.
Katika makongamano hayo, mada mbalimbali zinazohusu Kiswahili na mustakabali wake hujadiliwa lakini pia maazimio mbalimbali huchukuliwa kuhusu maendeleo ya chama. Makala mbalimbali huandikwa na kuchapishwa kwa minajili ya kusomwa na watu mbalimbali.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-07T03:33:12Z 2021-09-07T03:33:12Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1177 <![CDATA[NGUVU YA KAMATI YA LUGHA NA ITHIBATI]]>
.pdf   Makampuni ya kuchapisha vitabu hayakusita kuchapisha kitabu baada ya ithibati ya kamati kupatikana.pdf (Size: 530.73 KB / Downloads: 0) ]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-06T05:43:11Z 2021-09-06T05:43:11Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1151 <![CDATA[VYOMBO ( ASASI ) MBALI MBALI VYA KUKUZA NA KUENEZA KISWAHILI NCHINI]]> Baada ya uhuru, serikali imechukua hatua mbali mbali ili kukuza na kueneza Kiswahili . hatua moja wapo ni ile ya kuunda asasi za ukuzaji Kiswahili.  Asasi hizo ni:
  1. UKUTA
 Hiki ni chama cha Usanifu wa Kiswahili na Mashairi . chama hiki kilianzishwa mwaka 1965 na mshairi Mathias Mnyapala kwa lengo la kukuza ushairi wa Kiswahili kwa ujumla.
  Ukuta ilikuwa na malengo yafuatayo:
     a). Kukuza lugha ya Kiswahili na ushairi kwa ujumla kwa njia ya kujishughulisha na kazi tafauti zinazohusiana na maendeleo ya Kiswahili na ushairi kama vile uhariri wa miswada ya Kiswahili, utunzi wa mashairi na uandishi wa vitabu na kutafsiri maandishi mbali mbali katika Kiswahili.
     b).  Kukuza utunzi wa ngonjera na kuhamasisha utunzi wa vitabu katika misingi yenye kuzingatia utamaduni wa Mtanzania.
Mafanikio ya UKUTA.
     c).   Imeweza kuundaa na kuendesha semina na makongamano ya Kiswahili na kutunga kazi za fasihi kwa kushirikiana na vyombo vingine.
     d).   UKUTA imeweza kuandika vitabu mbali mbali vya ushairi hususan vya ushairi, kama vile Ngonjera za  ukuta ( cha kwanza na cha pili – 1968 ), Mashairi ya Azimio la Arusha – 1974 na Mashairi ya miaka kumi ya Azimio la Arusha – 1977.
     e).   Imeweza kutafsiri kwa Kiswahili maandishi mbali mbali . mfano , iliwza kutafisiri majina ya baadhi ya mitaa ya jiji la Dar – es – Salaam kama vile mtaa wa uhuru badala Independence Avenue na mtaa wa Sokoine badala ya Sokoine Drive.
  1. TUKI ( Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ).
     Taasisi hii kihistoria ilianzishwa mwaka 1930 ikiwa kamati ya lugha ya lugha ya Afrika Mashariki na uatwala wa Waingereza , na mnamo mwaka mwaka 1964, ilipandishwa hadhi na kuhamishiwa katika chuo kikuu cha Dar –es – Salaam baada ya kuimarishwa kwa sheria ya Bunge ya mwaka 1964. Na mwaka 1970 kilipoanzishwa chuo kikuu cha Dar –es Salaam taasisi ilikuwa moja wapo wa asasi za utafiti wa chuo, ambapo mpaka leo asasi hii imekuwa ikifanya kazi chini ya Chuo Kikuu,
    Mnamo mwaka 2009, taasisi hii ilibadili jina baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili ya chuo na kujulikana kwa jina la Taasisi ya Taaluma za Kiswahili. ( TATAKI ).
    Malengo ya TUKI ( TATAKI ).
       i).  Kuichunguza na kuiendeleza lugha ya Kiswahili katika fani zake zote ikizingatia mipango ya muda mrefu katika Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Afrika na mashariki na Katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
3.BAKITA ( Baraza la Kiswahili Tanzania).
        Baraza hili liliundwa mwaka 1967 kaw sheria ya Bunge Na. 27. Ya mwaka huo.
        Malengo makuu ya uundwaji wa baraza hili ni kutaka kuwepo kwa chombo nchini cha kusimamia shughuli za ukuzaji Kiswahili.
KAZI ZA BAKITA.
   i). Kuhimiza matumizi ya Kiswahili fasaha, kuandika vitabu vya Kiswahili na taaluma zake hususan fasihi na sarufi.
   ii).  Kutoa huduma za ukalimani kwa serikali na mashirika
   iii). Kuratibu kazi za ukuzaji Kiswahili nchini na zile zinazofanyika nchi za nje.
    iv). Kuchapisha majarida ya Kiswahili yatakayoongoza matumizi sahihi ya maneno na maendeleo yake.
    v). Kuchunguza usahihi wa lugha ya Kiswahili inayotumika katika uandishi wa vitabu mbali mbali vinavyokusudiwa kutumika kufundishia shuleni na vyuoni kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu.
   vi). Hujishughulisha na uthibitishaji wa tafsiri sanifuza isitilahi na kusimamia utafiti wa lugha ya Kiswahili.
   vii). Kutoa ushauri kwa waandishi na wachapishaji kuhusu utumiaji wa Kiswahili fasaha na kuratibu maendeleo ya Kiswahili nchini.
        Katika utekelezaji wa shughuli zake, baraza hilo limeanzisha idara tano za taaluma. Nazo ni:
  Idara ya Uhariri na Uchapishaji.
   Idara hii hujishughulisha na  masuala mbali mbali ya uchapaji wa taarifa za BAKITA na majarida mengine.
Idara ya Lugha na Fasihi.
    Idara hii husimamia matumizi sahihi ya Kiswahili sanifu katika vyombo vya habari  na matumizi rasmi na kutoa ithibati ya vitabu vya Kiswahili vinavyokusudiwa kutumika katika elimu.
Idara ya Tafsiri na Ukalimani.
Idara hii hujishughulisha na kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa lugha ya Kiswahili kwa mashirika,idara,wizara,balozi na watu binafsi.
 Idara ya Istilahi na kamusi.
Hii inafanya kazi ya kufanya tafiti za isitilahi, kuandaa orodha ya isitilahi na kuandaa kamusi kwa matumizi ya asasi, shule na watu wa aina mbali mbali.
Idara ya Uhusiano
Idara hii inafanya kazi ya kutangaza kazi za shughuli za baraza kwa kutumia radio,magazete na majarida na kusimamia vipindi vya Kiswahili katika radio na televisheni, pamoja kuimarisha uhusiano baina ya vyombo vya ukuzaji Kiswahili kwa kuandaa warsha na semina.
MAFANIKIO YA BAKITA
.  Bakita imeandaa isitalahi za taaluma mbali mbali kama vile za Fizkia, Kemia, Uchumi, Ufundi, Bunge , maktaba n.k
.  Bakita inatoa majarida mbali mbali yanayohusu lugha ya Kiswahili kama vile lugha yetu tusome tuijue, jifunze Kiswahili uwafunze wengine , lugha ya kiswahili – fasihi na sarufi yaken.k
.  Bakita huendesha vipindi mbali mbali vya Kiswahili katika radio Tanzania dar es sallam  kama vile lugha yetu, ulimwengu wa Kiswahili, Kiswahili lugha ya taifa n. k
MATATIZO YA BAKITA.
  1. Uhaba wa fedha wa kuendeshea shughuli za bakita, kama vile warsha ,semina,makongamano uchapishaji wa majirida.
  2. Uhaba wataalamu
4). TAASISI YA KISWHILI NA LUGHA ZA KIGENI. ( TAKILUKI ).
    Taasisi hii iliundwa mwaka 1979 ikiwa chini ya Wizara ya Elimu  na Mafuzo ya Amali Zanzibar.
 Lengo kubwa ya kuanzishwa taasisi hii ni :Kusimamia na kuendeaha shughuli za ukuzaji wa kiswahli na lugha za kigeni kisiwani humo.
KAZI ZA TAKILUKI:
  1. Kutoa mafunzo na elimu ya Kiswahili kwa kiwango cha juu kwa watumishi wa serikali na viongozi wa chama ua vyama ili kukuza ujuzi wa Kiswahili  na kuzumgumza Kiswahili fasaha
  2. Kufanya utafiti wa Kiswahili , kuandika vitabu vya taaluma mbali mbali za Kiswahili na kutafsiri katika kisahili maandishi mbali mbali yaliyo katika lugha za kigeni.
  3. Kuhimiza matumizi ya Kiswahili fasaha , kuchapisha vitabu vya Kiswahili  na kuwapa waandishi chipukizi miongozo ya uandishi sahihi wa vitabu.
  4. Kuratibu na kusimamia maendeleo ya Kiswahili visiwani Zanzibar pamoja na kuendesha mafunzo ya lugha ya Kiswahili kwa wazawa na wageni
  5. Kuandaa isitalahi za taaluma mbali mbali pamoja na kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwamashirika ,idara wizara kampuni,na watu binafsi , pia hufundisha lugha za kigeni kama vele GR, PR FR ARB CHINA na kuandika vitabu vya Kiswahili.
  6. Hujishughulisha na ufuatiliaji pamoja na usimamizi wa matumizi sahihi ya Kiswahili katika vyombo vya habari katika shughuli mbali mbali za serkali na za kawaida.
  7. Kufanya utafiti wa lahaja na fasihi simulizi ya Kiswahili.
MAFANIKIO YA TAKILUKI.
Takiluki imepata mafanikio kadhaa yakiwemo haya yafutayo:
  1. Kuchapisha vitabu mbali mbali vya Kiswahili kama vile malenga wapya, na tungo zakale.
  2. Kuandaa na kuendesha semina na makongamano mbali mbali ya Kiswahili.
  3. Kuhimiza ufundishaji wa Kiswahili visiwani Zanzibar.kushirikiana na vyombo mbali mbali vyaukuzaji lugha ya Kiswahili katika kutekeleza mipango mbali mbali ya ukuzaji Kiswahili.
BAKIZA. ( BARAZA LA KISWAHILI ZANZIBAR ).
     Ni chombo chengine ambacho kimesidia kukuza na kustawisha kugha ya Kiswahili visiwani Zanzibar. Baraza hili lilianzishwa mwaka 1983.
KAZI ZA BAKIZA.
  • Kuratibu na kusimamia maendeleo ya Kiswahili visiwani Zanzibar.
  • Kuhimiza matumizi ya Kiswahili fasaha na kufanya utafiti wa Kiswahili kwa kushirikiana na vyombo vingine.
  • Kuendesha semina za Kiswahili na kuwafundisha waandishi misingi ya uandishi.
  • Huratibu maendeleo ya Kiswahili na kutoa ushauri kwa serikali kuhusu namna ya kufanikisha ukuzaji wa Kiswahili ndani nan je ya Zanzibar.
CHAMA CHA KISWAHILI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
           Chama hiki kilianzishwa mwaka 1970 kwa juhudi za mwanzo za wanafunzi walioingia chuo kikuu kusoma Kiswahili katika ngazi ya shahada ya kwanza.
      Chombo hiki kilikuwa na madhumuni yafuatayo:
  • Kuwapa wanachama nafasi ya kuvumbua na kukuza vipawa vyao katika isimu na fasihi ya Kiswahili.
  • Kuamsha ari ya kimapinduzi katika kuendeleza lugha ya Kiswahili kwa njia ya uchunguzi namaandishi.
MAFANIKIO YA CHAMA HIKI.
  1. Kutoa jarida ya kioo cha lugha.
  2. Kutoa nafasi kwa walimu na wanafunzi kujadili na kuhakiki fani mbali mbali za isimu na fasihi.
  3. Kuongoza makongamano ambayo mijadala yake huhaririwa na kutolewa katika kijarida kiitwacho ZINDUKO.
TAASISI YA ELIMU.
    Taassisi hii ilianzishwa mwaka 1966  na ilikuwa na kazi zifuatazo:
  1. Kutayarisha mihutasari ya masomo ya shule za msingi na sekondari  pamoja vyuo vya elimu.
  2. Kutayarisha na kuongoza semina mbali mbali  kwa walimu ili waweze kufundisha vyema lugha ya Kiswahili.
  3. Kutoa muongozo mpya kuhusu utahini wa somo la Kiswahili katika kidato cha tatu na nne wakishirikiana na baraza la mitihani la taifa.
MAFANIKIO YA TAASISI HII.
  • Kuandaa mihutasari ya masomo mbali mbali hapa nchini.
  • Kuandaa vitabu vya kufundishi Kiswahili sekondari kama vile Kiswahili kidato cha 1 – 4 (1996).
TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA.
       Taasisi hii ilianzishwa mwaka 1963. Kama chombo cha kuwasaidia wazelendo  katika stadi za kusoma na kuandika ambao hawakupata fursa ya kupata elimu katika ngazi ya msingi na sekondari.
   Baadhi ya mafanikio ya elimu ya watu wazima ni:
  • Kufanikiwa kutoa elimu ya watu wazima katika stadi za kusoma na kuandika wakati wa jioni kwa lengo la kufuta ujinga .
  • Kutoa masomo kwa njia ya posta kwa kidato cha kwanza hadi cha sita katika somo la Kiswahili.
  • Kuanzisha maktaba makao makuu ambayo huwasidia wanafunzi kupata vitabu na majarida mbali mbali ya Kiswahili.
  • Kunzisha idara ya mafunzo ya elimu ya watu wazima ambapo wanafunzi kutoka ndani na n je ya nchi husomea diploma ya elimu ya watu wazima.
IDARA YA KISWAHILI – CHUO KIKUU DAR ES SALAAM
 Idara hii ilianzishwa mwaka 1970 baada ya kuanzishwa chuo kikuu.
    Kazi kubwa ya idara hii ilikuwa ni:
  • Kutayarisha walimu na wataalamu wenye shahada katika somo la Kiswahili ili waweze kufundisha mashuleni na vyuoni.
  Mafanikio makubwa ya idara hii ni kuweza kutoa walimu wengi wenye shahada  ya Kiswahili wanaofundisha mashuleni mashuleni na vyuoni,
   Pia imeweza walimu wenye shahada ya pili , tatu  na hata uprofesa wa lugha ya kiswahili.
CHAMA CHA KISWAHILI CHA AFRIKA.
     Chama hiki kiliundwa katika semina ya kimataifa kuhusu usanifishaji wa isitilahi za Kiswahili iliyofanyika chuo kikuu dar es salaam mwaka 1978. Ikiwa na wajumbe tafauti waliotoka nchi za Kenya, Tanzania, msumbuji, na Zambia ikiwa na madhumuni yafuatayo:
  • Kukuza kueneza Kiswahili kote afrika.
  • Kuleta umoja katika mataifa ya kiafrika kwa kutumia lugha ya asili.
Pia semina nyengine iliandaliwa tena mwaka 1983 na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka Kenya, Rwanda, Comoro, Uganda, DRC, Zanzibar  na kutoka radio mbali mbali kama vile India, BBC, RTD, Radio Rwanda n.k na waliazimia mambo yafuatayo:
  • Kuandaa mikutano ,semina na warsha  zitakazotumika kuchambua isitilahi za Kiswahili badala ya kawaachia Tanzania peke yake.
  • Kusambaza isitilahi za Kiswahili zitumike na watu wa kawaida na hasa wale wanaojishughuisha na ukuzaji Kiswahili ndani na nje ya mipaka yake.
  • Kupendekeza mpango wa usanifishaji wa isitilahi uwe wa kiwango cha kimataifa.
  • Kuanzisha jarida makhsusi ambalo litajidili masuala ya usanifishaji ili kuimarisha taasisi mbali mbali zinazo jishughulisha na Kiswahili kama vile unesco.
MATATIZO YA CHAKA.
  • Kuachiwa Tanzania peke yake katika usanifishaji wa isitilahi.
  • Kutafsiriwa kwa maneno ya kigeni bila ya utafiti mkubwa ambayo hupelekea kutokuwa na mvuto kwa wasomaji wa kawaida.
  • Kutokuwa na msukumo wa viongozi wa nchi wanachama kwani viongozi wengine walipiga vita shughuli hii badala ya kutoa ushauri na kuhimiza.
UWAVITA. ( Umoja wa waandishi wa vitabu Tanzania ).
   Umoja huu ulianzishwa mwaka 1974 na ulikuwa na madhumuni yafuatayo:
  • Kuwahimiza watu kuandika vitabu mbali mbali vya Kiswahili.
  • Kuwasidia waandishi chipukizi ikiwa ni pamoja kuwafahamisha uandishi wa masuala mali mbali ya fasihi.kujishughulisha na kukikuza na kukitangaza Kiswahili katika vyombo vya habari kama vile radio na magazeti.
  • Kutetea maslahi ya waandishi wa kitanzania ili kuwaunganisha pamoja.
  • Kubuni na kuendesha miradi ya uandisshi, uchapaji na uchapishaji.
  • Kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kusoma, uandishi wa vitabu na Sanaa zinazoambatana nazo kwa njia ya radio na magazeti.
TATHMINI YA MAENDELEO YA KISWAHILI BAADA YA UHURU.
       Lugha ya Kiswahili baada ya uhuru imepata mafanikio kadhaa. Miongoni mwa mafanikio hayo ni:
  1. Uendelezwaji wa Kiswahili.
    Kiswahili kimeweza kuendelezwa kwa njia mbali mbali kama vile kufundisha kama somo moja wapo katika ngazi zote za elimu nchini, kufanyiwa utafiti, kusanifiwa na kutumika kama lugha kuu ya mawasiliano.
  1. Kuongezeka kasi ya ueneaji wa lugha ya Kiswahili.
         Kiswahii kimeweza kuenea hadi nje ya Tanzania katika mataifa mbali mbali na hata kufikia moja wapo lugha ya kimataifa na pia kuongezeka msamiati.
  1. Kuongezeka kwa uundwaji wa vyombo vya ukuzaji Kiswahili.
    Kuendelea kujitokeza vyombo mbali mbali vya ukuzaji wa Kiswahili ndani na nje ya Tanzania  ni mafanikio makubwa kwa upande wa lugha ya Kiswahili kwa sababu vyombo hivyo vimewea kuikuza lugha ya Kiswahili kwa njia mbali mbali.
  1. Kutumika Kiswahili katika vyombo vya habari vya nje.
    Kuendelea kutumika lugha ya Kiswahili katika vyombo mbali mbali vya habari vya nje kama viel BBC. Deutchwelle,radio japani, sauti ya amerika na nyinginezo kumeifanya lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha mashuhuri duniani
CHANGAMOTO ZINAZOATHIRI MAENDELEO YA KISWAHILI.
   Pamoja na mafanikio hayo ,zimekuwapo changamoto kadhaa zinazoathiri maendeleo ya Kiswahili. Baadhi ya changamoto hizo ni:
  • Upotoshwaji wa lugha ya Kiswahili.
       Upotwashwaji wa Kiswahili hutokea kwa namna kadhaa mfano ni wa uchanganyaji wa Kiswahili na kingereza na pia kutumia Kiswahili kwa maneno yasio yanifu na pia utumizi wa Kiswahili ulioathiriwa na sarufi ya lugha za kikabila hususan kimatamshi na kimuundo.
  • Athari za lugha za kigeni.
Tatizo la kutokithamini Kiswahili miongoni mwa wanajamii ni changamoto ya kuathiriwa na kasumba za ukoloni ambapo wanajamii huthamini Zaidi lugha za kigeni hususan kingereza.
  • Kutokuwepo uwiano wa kimatumizi.
Hii ni changamoto nyengine ambapo Kiswahili hakina uwiano wa kimatumizi katika nchi nzima, tofauti hizi zipo kutokana na jamii moja na nyingine kuathiriwa na lugha mama.
  • Utafauti wa sera .malengo na mipango ya vyombo vya ukuzaji Kiswahili.
  Juhudi za ukuzaji Kiswahili zinaonekana hazina mashiko kutokana na kuwepo idadi kubwa ya vyombo vya ukuzaji Kiswahili ambayo havina mshikamano wa pamoja kwani kila chombo kina malengo,sera, na mipango ya yake ya uendeshaji wa Kiswahili.
  • Uhaba wa wataalamu.
  Uhaba wa wataalamu katika vyombo vya ukuzaji wa Kiswahili husababisha vyombo kutofanya  na kutekeleza malengo kwa ufanisi.
  • Kutokwepo mpango wa kukitumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia.
   Ni tatizo jengine linalokwanishwa maendeleo ya Kiswahili kwa kutotekelezwa kwa mpango wa kukitumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika ngazi zote za elimu nchini, na hivyo kutoa mwanya hasa kwa lugha za kigeni kama vile kingereza kustawi zaidi na hivyo kuathiri nafasi ya Kiswahili katika jamii.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-09-06T04:46:53Z 2021-09-06T04:46:53Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1148 <![CDATA[UKUTA]]> Hiki ni chama cha Usanifu wa Kiswahili na Mashairi . chama hiki kilianzishwa mwaka 1965 na mshairi Mathias Mnyapala kwa lengo la kukuza ushairi wa Kiswahili kwa ujumla.
  Ukuta ilikuwa na malengo yafuatayo:
     a). Kukuza lugha ya Kiswahili na ushairi kwa ujumla kwa njia ya kujishughulisha na kazi tafauti zinazohusiana na maendeleo ya Kiswahili na ushairi kama vile uhariri wa miswada ya Kiswahili, utunzi wa mashairi na uandishi wa vitabu na kutafsiri maandishi mbali mbali katika Kiswahili.
     b).  Kukuza utunzi wa ngonjera na kuhamasisha utunzi wa vitabu katika misingi yenye kuzingatia utamaduni wa Mtanzania.
Mafanikio ya UKUTA.
     c).   Imeweza kuundaa na kuendesha semina na makongamano ya Kiswahili na kutunga kazi za fasihi kwa kushirikiana na vyombo vingine.
     d).   UKUTA imeweza kuandika vitabu mbali mbali vya ushairi hususan vya ushairi, kama vile Ngonjera za  ukuta ( cha kwanza na cha pili – 1968 ), Mashairi ya Azimio la Arusha – 1974 na Mashairi ya miaka kumi ya Azimio la Arusha – 1977.
     e).   Imeweza kutafsiri kwa Kiswahili maandishi mbali mbali . mfano , iliwza kutafisiri majina ya baadhi ya mitaa ya jiji la Dar – es – Salaam kama vile mtaa wa uhuru badala Independence Avenue na mtaa wa Sokoine badala ya Sokoine Drive.
  1. TUKI ( Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ).
     Taasisi hii kihistoria ilianzishwa mwaka 1930 ikiwa kamati ya lugha ya lugha ya Afrika Mashariki na uatwala wa Waingereza , na mnamo mwaka mwaka 1964, ilipandishwa hadhi na kuhamishiwa katika chuo kikuu cha Dar –es – Salaam baada ya kuimarishwa kwa sheria ya Bunge ya mwaka 1964. Na mwaka 1970 kilipoanzishwa chuo kikuu cha Dar –es Salaam taasisi ilikuwa moja wapo wa asasi za utafiti wa chuo, ambapo mpaka leo asasi hii imekuwa ikifanya kazi chini ya Chuo Kikuu,
    Mnamo mwaka 2009, taasisi hii ilibadili jina baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili ya chuo na kujulikana kwa jina la Taasisi ya Taaluma za Kiswahili. ( TATAKI ).
    Malengo ya TUKI ( TATAKI ).
       i).  Kuichunguza na kuiendeleza lugha ya Kiswahili katika fani zake zote ikizingatia mipango ya muda mrefu katika Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Afrika na mashariki na Katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
]]>
false
MwlMaeda]]> 2021-06-14T03:19:13Z 2021-06-14T03:19:13Z https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=4 <![CDATA[NAFASI YA VYAMA NA TAASISI MBALIMBALI KATIKA MAKUZI YA KISWAHILI]]> Kwa Mukhtasari

IKIWA idara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI), awali ikiitwa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) ni miongoni mwa taasisi kongwe zaidi za lugha nchini Tanzania na Afrika Mashariki. Madhumuni yake ni kusimamia usanifishaji na maendeleo ya Kiswahili.

Japo Kiswahili kimeendelea kubaki nembo ya Afrika, mjadala usio na mwisho kuhusiana na ni ipi lugha ya kufundishia katika shule na vyuo nchini Tanzania ni ithibati kwamba Kiswahili hakijapokezwa hadhi inayostahiki katika mengi ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.

TUKI, kwa sasa TATAKI, ilianzishwa mnamo 1930 ikijulikana kama International-Territorial Language (Swahili) Committee kwa nchi tatu za Afrika Mashariki na baadaye ikaitwa Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki.

Mnamo 1964, kamati ilifanywa kuwa sehemu ya UDSM na baadaye ikaitwa Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili. Tangu 1970 kimepewa jina la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI). Mwaka 2009, TUKI iliungana na iliyokuwa Idara ya Kiswahili ya UDSM na kuunda taasisi kubwa zaidi inayoitwa TATAKI.

Majukumu ya taasisi hii awali yalikuwa ni kutafiti nyanja zote za lugha ya Kiswahili, fasihi na utamaduni na kuchapisha matokeo ya utafiti huo.

Hivyo pamoja na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), TUKI ni mlinzi wa usanifu wa lugha ya Kiswahili katika Tanzania. Baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili, sasa TATAKI inafundisha Isimu, Fasihi na Historia ya Lugha ya Kiswahili.

Inafundisha Kiswahili kama lugha ya pili hasa kwa wageni kutoka nje ya ulimwengu wa Waswahili na kuendeleza utungaji wa kamusi mbalimbali zinazohusiana na Kiswahili.

BAKITA

Ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa sheria ya Bunge Na.27 ya mwaka 1967 kwa madhumuni ya kukuza Kiswahili. Kutokana na sheria hii, Baraza ndilo mratibu wa kusimamia asasi zote na mawakala wote wanaokuza Kiswahili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

BAKITA imekuwa na mchango mkubwa katika ukuzaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili kupitia majukumu yake.

Miongoni mwa majukumu ya Baraza hili kama yalivyofafanuliwa katika sheria hiyo ni kuratibu na kusimamia maendeleo na matumizi ya Kiswahili nchini pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vinavyojihusisha na maendeleo ya Kiswahili.

Huhimiza matumizi ya Kiswahili katika shughuli rasmi na za kawaida, huandaa vipindi mbalimbali redioni ili kuhimiza matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili, hushirikiana na mamlaka zinazohusika kuthibitisha tafsiri sanifu za istilahi, hutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa serikali, mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali na asasi nyingine pamoja na kuidhinisha vitabu vya Kiswahili vitakavyotumika shuleni na vyuoni kabla havijachapishwa.

TAKILUKI

Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni (TAKILUKI) ilianzishwa mnamo 1979 kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili ndani na nje ya Zanzibar.

Inajishughulisha na kuratibu, kuendesha mafunzo ya Kiswahili visiwani Zanzibar, kuhariri miswada mbalimbali ili kuthibitisha ufasaha wa Kiswahili na kufanya tafiti za Kiswahili katika nyanja zake zote, hususan sarufi na fasihi.

TAKILUKI inatoa ushauri wa kitaaluma kwa watunzi wa vitabu ili waweze kuandika kazi zenye ubora, na kushirikiana na wadau wengine wa Kiswahili kuandaa na kuendesha semina, warsha na kozi fupifupi za Kiswahili.

CHAUKIDU

Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) kina makao makuu katika Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, Marekani.

Madhumuni yake ni kuwajumuisha pamoja wakuzaji wa Kiswahili duniani kote kwa lengo la kuchochea kasi ya malengo mahususi kama vile kukuza Kiswahili katika nyanja zote ambamo lugha hii inatumika na kuongeza ufanisi wa mawasiliano katika ufundishaji na utafiti wa maarifa ya aina zote mathalan uandishi na utangazaji wa habari, uandishi na uchapishaji wa vitabu na majarida pamoja na utayarishaji wa safari za mafunzo katika Afrika Mashariki na Kati.


Husambaza habari na matokeo ya utafiti kwa kutumia machapisho mbalimbali na teknolojia ya mtandao wa kompyuta kuhusu vipengele mbalimbali vya Kiswahili na masuala yanayohusiana na Kiswahili. CHAUKIDU inaelimisha umma juu ya umuhimu wa kujivunia, kuendeleza, na kuheshimu Kiswahili.

Vilevile inashauri ama kushinikiza serikali za nchi ambamo Kiswahili kinazungumzwa kutambua thamani iliyobebwa na maliasili hii ili kuunda sera mwafaka za kukiendeleza kadri ya uwezo wake kwa manufaa ya maendeleo ya serikali na watu wake kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kielimu.

CHAWAKAMA

Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili katika vyuo vikuu vya Afrika Mashariki (CHAWAKAMA), kilianzishwa mnamo 2004 kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili katika eneo lote la Afrika Mashariki kupitia kwa wanafunzi wanaosoma Kiswahili vyuoni.

Wanachama wa chama hiki ni wale wanaosomea taaluma za Kiswahili ila wapenzi wa Kiswahili pia wanaweza kujiunga nacho.

Mara kwa mara, CHAWAKAMA huandaa makongamano kwa lengo la kuwapa wanachama nafasi ya kujadili, kuimarisha, kuendeleza na kukuza vipawa vyao vya lugha na fasihi ya Kiswahili, kuamsha ari ya mapinduzi ya utamaduni wa Kiswahili, kueneza Kiswahili ndani na nje ya nchi, kushirikiana na vyama vingine katika juhudi za kuendeleza na kuimarisha Kiswahili ndani na nje ya nchi wanachama, kuwaunganisha wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki na Kati katika kukikuza Kiswahili pamoja na kushirikiana na asasi mbalimbali zinazojihusisha na ukuzaji na uenezaji wa Kiswahili.

CHAKAMA

Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA) ndicho cha tatu kwa umaarufu zaidi miongoni mwa wasomi, wataalamu na wahadhiri wa vyuo vikuu baada ya CHAUKIDU na Chama cha Walimu wa Lugha za Kiafrika (ALTA) ambacho haundaa makongamano yake jijini Bayreuth, Ujerumani.

Kwa pamoja na Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA), CHAKAMA huchapisha jarida la chama na machapisho mengine ili kusaidia kueneza taaluma za Kiswahili.

Aidha, huhifadhi kumbukumbu za wataalamu wa Kiswahili kwa nia ya kutumia katika kufanikisha malengo ya chama na wadau wa Kiswahili pamoja na kuratibu makongamano na mijadala mbalimbali inayohusiana na taaluma za Kiswahili.

Chama huandaa makongamano kila mwaka ambalo linawakutanisha wanachama wote katika vyuo mbalimbali katika nchi husika.

Katika makongamano hayo, mada mbalimbali zinazohusu Kiswahili na mustakabali wake hujadiliwa lakini pia maazimio mbalimbali huchukuliwa kuhusu maendeleo ya chama. Makala mbalimbali huandikwa na kuchapishwa kwa minajili ya kusomwa na watu mbalimbali.]]>
false