MRADI WA KUSWAHILISHA PROGRAMU HURIA
WARSHA YA ARUSHA 1-5 NOVEMBA 2004-11-22
MADA YA MAFUNZO
UUNDAJI WA ISTILAHI: UZOEVU WA BARAZA LA
KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA)
na
P.C.K. Mtesigwa
UUNDAJI WA ISTILAHI: UZOEVU WA BARAZA LA KISWAHILI
LA TAIFA
(BAKITA)
1.0 Utangulizi Jukumu kuu ambalo Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) limepewa kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Bunge Na. 27 ya mwaka 1967 iliyoliunda ni kukuza, kuimarisha na kuendeleza Kiswahili hasa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika marekebisho ya sheria hiyo yaliyofanyika mwaka 1983 kwa Sheria ya Bunge Na.
7, BAKITA limepewa uwezo wa kufuatilia na kusaidia ukuzaji wa Kiswahili katika nchi za nje pia. Kwa hiyo kazi zinapokuwa zimethibitishwa na BAKITA huzihusu pia juhudi za uendelezaji wa Kiswahili katika nchi za nje.
Kimsingi ukuzaji au uimarishaji wa lugha maana yake, kwa upande mmoja, ni utumiaji wa lugha hiyo kwa usahihi. Kwa mtazamo huo maana yake ni kuhakikisha kwamba kanuni za sarufi yake zinafuatwa. Lakini pamoja na hilo, kwa upande mwingine kuna suala la kuiwezesha lugha hiyo kukidhi mahitaji ya watumiaji wake wa kila hali na kila uwanja wa matumizi. Kusema kweli mojawapo ya vigezo vinavyotumika kujua kiwango cha kukomaa kwa lugha ni kupima jinsi inavyojimudu katika msamiati wake kukidhi matumizi katika nyanja mbalimbali zikiwemo nyanja maalumu za kitaalamu. Ili kutimiza lengo hilo hapan budi msamiati wake ukuzwe na kusambaa. Kwa mujibu wa Mkude (2004) aina ya msamiati uliosukwa kimkakati na kuratibiwa kwa nia ya kuashiria dhana teule za taaluma fulani huitwa istilahi. Huu ni msamiati maalumu ambao umetokana na msamiati mpana wa lugha na kufanyiwa marekebisho ili kuhakikisha kwamba maana ya neno inaacha au inapanua maana yake ya kawaida na kubeba maana maalumu kwa ajili ya matumizi katika uwanja maalumu.
Ili kutekeleza majukumu yake kama chombo chenye mamlaka ya kukuza na kuimarisha Kiswahili kama lugha ya taifa na mojawapo ya lugha mbili rasmi za Tanzania, BAKITA linayo idara mahususi (Idara ya Kamusi na Istilahi) inayoshughulikia kusanifu istilahi kwa ajili ya kuziba pengo la kukosekana kwa istilahi katika nyanja mbalimbali.
Kazi kubwa inayofanywa na idara hii ni kutafuta visawe vya Kiswahili vya istilahi za Kiingereza zilizopo tayari. Katika kufanya kazi hiyo BAKITA hupokea orodha za istilahi kama hizo baadhi huja tayari na mapendekezo ya visawe vya Kisahili vilivyopendekezwa na mletaji mwenyewe ili yapitiwe na kurekebishwa kama hapana budi au yathibitishwe ili baada ya kukubaliwa rasmi na BAKITA yasambaazwe na kuanza kutmika. Lakini kwa kiasi kikubwa orodha zinazoletwa huwa hazina mapendekezo yoyote ya visawe vya Kiswahili. Idara husika hufanya utafiti kutafuta visawe na kasha Kamati ya kuisanifu istilahi ya BAKITA hukaa na kutumia mbinu mbalimbali ili kuvipitia na kuvisanifu visawe hivyo. Ndipo visawe hivyo vinapowaslishwa katika kikao cha Baraza zima ili kutoa idhini na hatimaye kuvisambaza vianze
kutumika. Mpaka sasa BAKITA limefaulu kusanifu na kusambaza istilahi zipatazo zaidi ya elfu 10 za nyanja maalumu na taaluma mbalimbali zaidi ya 30. Lengo la makala hii ni kueleza misingi na mbinu ambazo BAKITA hutumia katika kuunda istilahi za Kiswahili. Vilevile makala itagusia matatizo yanayojitokeza wakati wa kuunda istilahi na pia baada ya kuunda istilahi.
2.0 Misingi na mbinu za uundaji wa istilahi Shirika la Kimataifa la Viwango (ISO) ambalo miongoni mwa kazi zake ni kuratibu na kusimamia uendelezaji wa istilahi kimataifa, limeorodhesha kanuni zinazopaswa kufuatwa wakati wa kuunda istilahi katika lugha yoyote. Misingi hii imetokana hasa na mtazamo wa wanaisimu wa Vienna – yaani “Shule ya Istilahi ya Vienna (Austria)” iliyoanzishwa na Eugen Wuster. Kwa muhtasari kanuni hizo zinahusu uundaji wa istilahi lugha moja tu inapohusika na pale lugha mbili zinapohusika. Lugha moja inapohusika kanuni zifuatazo hazina budi zizingatiwe:
(1) Istilahi ziundwe baada ya kupata dhana iliyoelezwa kwa ukamilifu na wazi.
(2) Istilahi ziwe fupi kadiri iwezekanavyo lakini zenye kueleweka. Uundaji wa istilahi kwa vifupisho na akronimia uepukwe hasa kama istilahi kamili si ndefu sana.
(3) arufi ya lugha inayohusika lazima itiliwe maanani. Kwa hiyo istilahi ziundwe kwa kufuata mofolojia ya kawaida ya lugha.
(4) Istilahi ziundwe kwa njia ambayo itakuwa rahisi kuunda istilahi nyingine kwa mnyumbuliko.
(5) Uundaji wa istilahi kwa kupanua maana ya neno uepukwe hasa iwapo nyanja zinazotumia maneno hayo zinakaribiana, ili kuepusha utata. Kwa hiyo mfumko wa sinonimia au homonimia (visawe) hauna budi kuepukwa ili watumiaji wasikanganyikiwe.
Lugha mbili zinapohusika kanuni zifuatazo zizingatiwe:
(1) Uundaji wa istilahi kwa njia ya kutohoa maneno ya lugha nyingine uzingatie kuchukua maneno kama yalivyo katika lugha ya asili na kufanya marekebisho machache tu ili kulingana na sarufi na matamshi ya lugha pokezi.
(2) Uundaji wa istilahi kwa kutumia Kigiriki na Kilatini uendelezwe ili kuzingatia uwakilishi sahihi wa dhana hasa za sayansi na pia kupunguza kishawishi cha kupendelea kutumia baaadhi tu yalugha zinazotumika ulimwenguni hivi sasa. Katika uzoevu wa kusanifu istilahi, BAKITA limekuwa likizingatia pia kanuni za nyongeza ili kupata ufanisi zaidi kwa kutilia maanani jamii ya watumiaji wa Kiswahili na utamaduni wake. Kubwa kati ya kanuni hizo za nyongeza ni:
(1)
istilahi ziepuke utusani – yaani zisiundwe kwa maneno ambayo tayari
yanaeleweka
kwamba ni matusi kwa watumiaji. Kwa mfano katika kutafuta
kisawe
cha penis, neno mboo hushitua watumiaji wa Kiswahili wengi na badala
yake
neno dhakari huvumulika na kutumika zaidi. Kadhalika kisawe cha neno
bone
marrow neno uboho ingawa ni sanifu pia lakini huepukwa sana katika
matumizi
na badala yake neno uloto limekomaa sana katika matumizi. Vilevile
katika
kutafuta kisawe cha neno anus, neno mkundu hushitua watumiaji na neno
ngoko
likachukuliwa.
(2)
Istilahi ziwe angavu vya kutosha – yaani istilahi ziweze kudokeza dhana
liliyokusudiwa
kwa kina na usahihi kadiri iwezekanavyo. Wakati wa kutafuta
kisawe
cha neno flip chart kwa Kiswahili kumekuwa na pendekezo la neno
bango
kitita. Katika kulichambua neno hilo imedhihirika ya kwamba ingawa
neno
bango kwa kiasi fulani linawakilisha ukubwa wa chart lakini dhana ya flip
haijidhihirishi.
Hivyo halina uangavu wa kutosha. Pendekezo linaloelekea
kupendelewa
ni chati pindu kwa kuwa neno hilo linawakilisha dhana ya chart
na
pia utumiksji wake wa kupinduliwa wakati chati hiyo inapotumiwa.
(3)
Istilahi ziwe na ulinganifu wa mtiririko ulio katika dhana za kikoa kimoja.
Katika
hili ni muhimu kwa wasanifishaji kukumbuka kwamba istilahi hazikai
pekepeke.
Hazifiki mbali iwapo zitasimama pasipo kuhusisha maneno mengine
yaliyo
katika uga huo. Istilahi ni kama matundu ya wavu ambayo kila moja
sharti
ligusane na lenzake ili hatimaye mfumo mzima wa wavu uweze
kutengenezwa.
Kwa hiyo istilahi moja iwe chanzo cha kupata istilahi zingine
kutokana
na kuinyumbulisha na kuunda istilahi zinazohusiana katika uwanja
ule.
Kwa mfano: Sumaku (magnet), Usumaku (magnetism), Sumakisha
(magnetise),
Jisumakisha (auto magnetise), Usumakishaji (magnetization, nk.
(4)
Istilahi zilizozoeleka au kukomaa kutokana na kutumika kwa muda mrefu
zisibadilishwe.
Kanuni hii ni muhimu sana katika ukubalifu wa istilahi
zinazoundwa.
Ni muhimu kabla ya kuunda istilahi mpya kuchunguza iwapo
hakuna
istilahi inayotumika tayari ambayo inawakilisha kw usahihi dhana
inayokusudiwa.
Uzoevu wa BAKITA umeonyesha kuwa ni vigumu kwa istilahi
mpya
kukubaliwa na kushamiri pale ambapo tayari kulikuwa na istiahi
zilizokuwa
zikitumika, hasa zile za muda mrefu. Kwa mfano neno Ovataimu
(overtime)
lililokuwa limezoeleka kwa muda mrefu limeendelea kutumika
badala
ya neno ajari. Vivyo hivyo neno Mdai (creditor) limeendelea kutumika
badala
ya neno Mwia. Maneno yote mawili ni ya siku nyingi lakini neno mdai
limezagaa
zaidi katika matumizi kuliko neno mwia.
3.0
Vyanzo vya istilahi
BAKITA
linafuata utaratibu ufuatao ili kupata istilahi sanifu:
(a)
Hazina ya Kiswahili chenyewe
Hazina
ya Kiswahili chenyewe huhusisha Kiswahili na lahaja nyingine za Kiswahili.
Kwa kawaida kabla ya kutafuta kisawe cha
Kiswahili cha istilahi iliyo katika lugha ngeni,
wataalamu
wa uwanja husika huhusishwa kikamilifu ili kueleza kwa ukamilifu dhana au
maana
ya istilahi hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya Kusanifu Istilahi. Baada ya hapo
wajumbe
huanza kutafuta iwapo kuna kisawe katika Kiswahili Sanifu cha istilahi
iliyotolewa.
Kama kisawe hakipatikani katika Kiswahili Sanifu wajumbe hutafuta kama
kuna
neno katika lahaja za Kiswahili. Mifano michache jinsi mbinu hii ilivyotumika
ni
istilahi
zifuatazo:
Chovyo
(oedema) kutoka lahaja ya Kipemba
Mbolezi
(elegiac poetry) kutoka lahaja ya Kimvita
Ng’ozi
(leaf curl) kutoka lahaja ya Kimtang’ata
Kisabeho
(breakfast) kutoka lahaja ya Kipemba (kutokana na Kitenzi kusabehe)
Kiangata
(hob) kutoka lahaja za Kiamu na Kisiu
Hazina
ya Kiswahili chenyewe pia huhusu mbinu mbalimbali zinazoweza kuunda
maneno
ya Kiswahili kwa njia ya kunyumbulisha mzizi waneno, kufinyaza maneno au
kwa
njia ya kuunganisha maneno:
Finyazo
Chakula
cha jioni = Chajio
Chemchemi
ya maji moto = Chemimoto
Mfupa
wa paja = Fupaja
Hati
ya kukataza kuiga = Hataza
Bara
lililozama = Barazama
Matuta
kama ngazi = Matungazi
Huduma
hadi bandarini = Huhaba
Huduma
hadi melini = Huhame
Utando
mwembamba wa ogani = Utandogani
Teknolojia
ya habari na mawasiliano = Teknohama nk.
Jambo
la kuzingatia ni kwamba mbinu hii inapaswa itumiwe kwa uangalifu sana ili
istilahi
itakayotokana nayo iwasilishe dhana kwa usahihi na pia iwe na uangavu wa
kutosha
kwa watumiaji. Kama mojawapo kati ya sifa hizo ikipuuzwa istilahi haitakuwa
sahihi
ipasavyo na wala uangavu ukipuuzwa istilahi haitapata nguvu ya kusambaa na
kushika
mizizi baina ya watumiaji.
Muunganiko
wa maneno
Mbinu
hii hutumika hasa kwa lengo la kufupisha istilahi ndefu kwa kuondoa viunganifu
au
umilikaji.
Kipima
pembe kwa ubapa = Kipimapembe ubapa
Doa
la kutu = Doakutu
Nyundo
ya rungu = Nyundorungu
Mwana
+ harakati = Mwanaharakati
Mwendo
wa kasi = Mwendokasi
Nishati
iliyotulia = Nishati tuli
Nishati
yenye mwendo = Nishati mwendo
(b)
Hazina ya lugha za Kiafrika
Lugha
za Kiafrika ni chanzo kingine ambacho husaidia kuunda visawe vya Kiswahili.
Hazina
hii hutumiwa pale hazina ya Kiswahili chenyewe inaposhindwa kukidhi haja ya
kupata
istilahi mwafaka inayoweza kuwakilisha dhana inayoshughulikiwa. Upendeleo
hutolewa
kwanza kwa lugha za Kibantu kwa sababu Kiswahili chenyewe ni mojawapo
kati
ya lugha za kundi hilo. Kwa hiyo maneno yanayotoka katika lugha za kundi hili
hata
yachukuliwapo
katika Kiswahili yatakuwa na uangavu wa kutosha kwa watumiaji wa
Kiswahili.
Kwa sasa BAKITA limekuwa likitafuta maneno yaliyo katika lugha za
Kibantu
za Tanzania kuliko za nchi zingine. Jambo la kuzingatia kamam ilivyokwisha
kudokezwa
katika kanuni ya kukopa au kutohoa ni kwamba maneno yanayochukuliwa
kutoka
huko hurekebishwa ili yatii kanuni ya muundo wa Kiswahili hasa katika maumbo
yake
na pia jinsi yanavyopaswa yapatanishwe yatumikapo katika sentensi. Mifano
michache
kutoka hazina hii ni kama ifuatayo:
Neno
la asili Istilahi Kisw) Umoja (Kisw) Wingi Upatanisho
Lishiganga
(Kisukuma) Shiganga (boulder) Ø Ma- li- yaAkasoko
(Kinyakyusa)
Kasoko (cardella) N- N- I- ziOlweya
(Kihaya)
Lweya (plain land) N- N- I- zi
Itepo
(Kimwera) Tepo(clone) Ø Ma- A- wa-
au pia N- I- ziUlugiligili
(Kinyakyusa)
Giligili (synovial fluid) N- N- I- zi-
Lugha
zingine za Tanzania ambazo si za Kibantu pia zimetoa mchango wa kupata istilahi
za
Kiswahili. Utaratibu unaofuatwa umekuwa ni uleule wa kuchukua neno la asili na
kulirekebisha
ili lichukue umbo na kanuni za sarufi ya Kiswahili. Mifano michache
iliyotokana
na hazina hiyo ni kama ifuatayo:
Embuti
(Kimasai) Mbuti (Kiswahili) duodenum
Engalem
(Kimasai) Ngalemu (Kiswahili) carving knife
Kamongo
(Kijaluo) Kamongo (Kiswahili) cat fish nk
Hazina
ya lugha za Kiafrika pia imehusisha lugha zisizo za Kibantu zinzazotumiwa nje
ya
Tanzania. Mpaka sasa mchango uliopatikana umetoka katika baadhi ya lugha za
Afrika
Magharibi. Mifano michache iliyotokana na lugha hizo ni kama ifuatayo:
Kola
(Kihausa, Kiibo, Kiyoruba) Kola (Kiswahili) kola nut
Rara
(Kiyoruba) Rara(Kiswahili) ballad
Dyeli
(Kimaninke, Kisusu) Yeli (Kiswahili) griot
Juju
(Kiyoruba, Kiibo, Kipijini) Juju (Kiswahili) complex witchcraft nk
©
Lugha za Kigeni
Sehemu
kubwa sana ya istilahi za Kiswahili imetokana na Kiingereza na Kiarabu. Lugha
zote
hizi mbili zimekiathiri sana Kiswahili katika uwanja huu na msamiati kwa jumla
kutokana
na sababu za kihistoria kwamba pamekuwa na uhusiano wa kutawala na
kutawaliwa.
Maneno mengi mno ya Kiingereza na Kiarabu yametoholewa katika
Kiswahili,
hata pasipokuwa na sababu za kutosha, kiasi kwamba baadhi ya wataalamu
hushuku
kwamba lazima Kiswahili kiachane na tabia hiyo kwa kujitahidi kutazama
hazina
iliyo ndani ya Kiswahili chenyewe au katika lugha za Kiafrika.
Kama
ilivyokiwsha kudokezwa kinachofanyika wakati wa kutumia hazina kutoka
lugha
hizi mbili ni kurekebisha maneno ya lugha hizo ili yakubaliane na mfumo wa
matamshi
na othografia ya Kiswahili. Mifano michache kati ya mingi tuliyo nayo ni
kama
ifuatayo:
Psychology
= Saikolojia
Commissioner
= Kamishena
Oxygen
= Oksijeni
Hormone
= Homoni
Element
= Elementi
Vitamin
= Vitamini
Uterus
= Uterasi (Mji mimba)
Chocolate
= Chokoleti/ chakleti
Chlorine
= Klorini nk.
Kwa
kuchunguza orodha ya istilahi za Kiswahili iliyopo inaelekea utohoaji wa maneno
ya
Kiingereza na Kiarabu ndicho chanzo kikuu cha istilahi za Kiswahili badala ya
kwamba
hazina ya Kiswahili chenyewe inapaswa kuwa ya kwanza ikifuatwa na hazina ya
lugha
za Kiafrika.Ziko sababu nzuri tu wakati mwingine wa kuhitaji kuendeleza
ukubalifu
wa istilahi kimataifa. Yako maneno ambayo kwa mfano majina ya waasisi wa
uvumbuzi
Fulani ndiyo pia istilahi ya kitajwa kinachohusika. Lakini maneno hayo si
mengi
sana katika maarifa ya utaalamu wenyewe. Waswahili hawana budi kuchungua
vyanzo
vyao kikamilifu kwanza kabla ya kukkimblia kutohoa. Kanuni za unyambulishaji
wa
maneno, uhusianishaji wa dhana katika kikoa kimoja uwe ndilo jambo la
kuzingatia
awali
ya yote katika usanifishaji wa istilahi.
4.0
Matatizo
Ingawa
misingi na mbinu zilizotajwa zimesaidia sana kupata na kusanifisha visawe vingi
vya
Kiswahili lakini yapo matatizo yaliyojitokeza katika kutekeleza kazi hiyo. Hapa
yataelezwa
machache angalau kwa kifupi ili inapobidi hadhari ichukuliwe. Kimsingi
matatizo
haya yanagusia utumiaji wa hazina ya Kiswahili chenyewe na lahaja zake na
hata
lugha za Kiafrika, suala la kutumia finyazo kama mbinu ya kuunda istilahi na
utusaji.
Hazina
ya Kiswahili na lugha za Kiafrika
Kwa
utaratibu ambao BAKITA limejiwekea ili kupata istilahi, Kiswahili chenyewe na
lahaja
zake ndiyo hazina ya kwanza. Lakini hazina hii haijatumika kikamilifu
inavyopaswa
kwa sababu mbalimbali. Lugha za Kiingereza na Kiarabu zimetagaa sana
katika
uundaji wa istilahi kwa sababu lugha hizi ziliwahi kuwa lugha za watawala
nchini
mwetu
na zikapata hadhi ya pekee. Waundaji wa istilahi huziona kama kimbilio ili
kurahisisha
kazi yao kwa kutohoa istilahi zinazoletwa katika orodha. Laiti utafiti wa
kutosha
katika uwezekano wa kunyumbua maneno ya Kiswahili chenyewe, au
kuchekecha
msamiati ulio katika lahaja za Kiswahili ingeshangaza jinsi hazina ya
Kiswahili
ilivyo pana na ilivyo na uwezo wa kuziba mapengo yaliyopo ya istilahi.
Kadhalika
hazina kubwa bado inalala tuli katika lugha za Kiafrika hasa zikichambuliwa
kwa
kuzingatia mazingira ya kijiografia au shughuli za kiuchumi katika maeneo
zinamozungumzwa.
Mbinu
ya kutumia finyazo
Kama
ilivyokwisha kudokezwa, uundaji wa istilahi kwa kutumia finyazo hauna budi
ufanywe
kwa makini sana ili istilahi iwakilishe kwa usahihi dhana inayokusudiwa na
wakati
huohuo iwe angavu ili watumiaji waweze kupata angalau fununu ya dhana hiyo.
Baadhi
ya mifano tuliyoitoa awali katika kueleza mbinu hii yaweza ktumika hapa ili
kudhihirisha
ugumu wa kuitumia.
Chemchemi
ya maji moto = Chemimoto (Je, dhana ya maji imewakilishwa?)
Huduma
hadi bandarini = Huhaba (Je, istilahi hii ni angavu vya kutosha kuwapa
watumiaji
fununu ya dhana inayowakilishwa?)
Utando
mwembamba wa ogani = Utandogani (Je, dhana ya mwembamba imewakilishwa
katika
istilahi hii?)
Ushiriki
katika hali ya mtu mwingine (empathy) = Ushirikali (Je, istilahi hii
inazingatia
hali
ya mtu mwingine? Je, inao pia uangavu unaokusudiwa?)
Pengine
jambo la msingi ni kuzingatia kwamba istilahi ni neno maalumu kwa dhana
maalumu
na hivyo suala la uangavu halipaswi kutiliwa mkazo sana. Lakini kama hivyo
ndivyo,
basi ni bora kuepuka finyazo na kutafuta mbinu nyingine itakayoweza kukidhi
haja
hiyo kwa ukamilifu zaidi.
Utusani
Sayansi
inataka dhana iwakilishwe kikamilifu bila hoja ya mzungukozunguko. Koleo
liitwe
koleo na si kitu kingine. Hali hiyo inadai utamaduni wa watumiaji wa lugha,
wakiwemo
watumiaji wa Kiswahili, wasiyaonee aibu maneno ambayo yanaweza kuwa
matusi
katika matumizi ya kawaida. Zaidi ya hayo ili kutimiza lengo la kuunda istilahi
maneno
ambayo pengine ni matusi katika lugha ambayo si Kiswahili hayapaswi
kutazamwa
kama matusi katika lugha hiyo au katika Kiswahili chenyewe.
MAREJEO
BAKITA
(1974 – 1983). Istilahi Sanifu (Namba 1 – 5)
BAKITA
(1979). KAKULU (Kamati ya kusanifu Lugha) Na.3
ISO
(1968). R 704-1968. Naming Principles
Kiingi,
K. B. (1981). Swahilization of International Scientific Vocabulary (Mimeo)
Mkude,
D. J. (2004). “Usuli na Umuhimu wa Istilahi katika Maendeleo ya Jamii” Makala
iliyowasilishwa
katika Warsha ya Mafunzo ya Uundaji wa Istilahi za Mradi wa
Istilahi
za Mikrosofti, Juni 2004, Dar es Salaam. Haijachapishwa
Mtesigwa,
P.C.K. (1983). Ethnolects as a source of Swahili technical terms: A case of
Kikerewe
fisheries terminology. Tasnifu ya MA (Linguistics), Chuo Kikuu cha Dar
es
Salaam. Haijachapishwa
Mwansoko,
H. J. M. (2004). “Misingi ya Uundaji wa istilahi” Kitini kilichowasilishwa
katika
Warsha ya Mafunzo ya Uundaji wa Istilahi za Mradi wa Istilahi za
Mikrosofti,
Juni 2004, Dar es Salaam. Haijachapishwa
]]>