MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Watunzi wa Kiswahili]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ Sun, 28 Apr 2024 04:47:20 +0000 MyBB <![CDATA[How is Vidalista 10 Mg used?]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2915 Mon, 27 Mar 2023 09:26:58 +0000 Kieth_winsett]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2915 Vidalista 10 Mg is used to treat men's erectile dysfunction. Cialis and Tadalafil are these drugs' generic names. Erectile dysfunction can be temporarily treated with this pill. The FDA has approved these tablets, and many doctors recommend them. This is an oral medication that should be taken with water. The pill doesn't need to be crushed or chewed first. A single Vidalista 10 (Tadalafil 10 mg) pill can induce an erection at any time during the following 24 hours. As a result, the maximum dosage that is suggested is one pill per day. The pill's tadalafil causes PFE- 5 hormone effects after being taken. As a result, an excessive amount of cGMP hormones are released. It causes the penis arteries to receive more blood. A higher blood stream to the course of the penis brings about an erection.
Benefits of Vidalista 10 (Tadalafil 10 mg):
·        Temporary relief from erectile dysfunction
·        Pulmonary Arterial Hypertension
·        Benign Prostatic Hyperplasia
Administration of Vidalista 10 (Tadalafil 10 mg):
Patients are advised to discuss the dosage with their doctors in light of the conditions of their bodies. One tablet per day is the most common dosage. The tablet should be taken at least one hour before having a sexual encounter. It should be consumed whole, with milk or water, as directed. The pill ought not to be bitten or squashed.
You should take the tablet as directed by your doctor. Taking the tablets over an extensive stretch or persistently ought to be kept away from. In the event of an overdose, contact your doctor right away. It is not recommended to take multiple doses to make up for a missed dose. Remember to take the medication before engaging in sexual activity.

Visit: carisoprodol 350 mg tabletpregabalin 200 mg capsule]]>
Vidalista 10 Mg is used to treat men's erectile dysfunction. Cialis and Tadalafil are these drugs' generic names. Erectile dysfunction can be temporarily treated with this pill. The FDA has approved these tablets, and many doctors recommend them. This is an oral medication that should be taken with water. The pill doesn't need to be crushed or chewed first. A single Vidalista 10 (Tadalafil 10 mg) pill can induce an erection at any time during the following 24 hours. As a result, the maximum dosage that is suggested is one pill per day. The pill's tadalafil causes PFE- 5 hormone effects after being taken. As a result, an excessive amount of cGMP hormones are released. It causes the penis arteries to receive more blood. A higher blood stream to the course of the penis brings about an erection.
Benefits of Vidalista 10 (Tadalafil 10 mg):
·        Temporary relief from erectile dysfunction
·        Pulmonary Arterial Hypertension
·        Benign Prostatic Hyperplasia
Administration of Vidalista 10 (Tadalafil 10 mg):
Patients are advised to discuss the dosage with their doctors in light of the conditions of their bodies. One tablet per day is the most common dosage. The tablet should be taken at least one hour before having a sexual encounter. It should be consumed whole, with milk or water, as directed. The pill ought not to be bitten or squashed.
You should take the tablet as directed by your doctor. Taking the tablets over an extensive stretch or persistently ought to be kept away from. In the event of an overdose, contact your doctor right away. It is not recommended to take multiple doses to make up for a missed dose. Remember to take the medication before engaging in sexual activity.

Visit: carisoprodol 350 mg tabletpregabalin 200 mg capsule]]>
<![CDATA[FAHARASA ZA SHAABAN ROBERT NA MCHANGO WAKE KATIKA LEKSIKOGRAFIA YA KISWAHILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2861 Fri, 11 Nov 2022 05:28:11 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2861
.pdf   FAHARASA ZA SHAABAN ROBERT NA MCHANGO WAKE KATIKA LEKSIKOGRAFIA YA KISWAHILI.pdf (Size: 4.63 MB / Downloads: 0) ]]>

<![CDATA[WATUNZI WA FASIHI WANATAFUTWA]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2841 Sat, 08 Oct 2022 18:29:52 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2841
Kampuni ya Uchapishaji ya APE imo katika mradi wa kukusanya simulizi za Watunzi kisha kuzihifadhi zimulizi hizo kwa manufaa ya sasa na ya baadaye.
Mradi huu unahisaniwa na kampuni ya Uchapishaji ya APE ya Jijini Dar es Salaam. Mradi unaratibiwa na Prof. Mulokozi kwa kusaidiwa na ndugu A. A. Majid Mswahili. Safu nzima ya mradi huu ni pamoja na ndugu E. Mshahara na ndugu P. A. Daudi katika sekta ya ufundi.

Mpaka sasa mradi umewafikia Watunzi wa Dar es Salaam na Zanzibar. Ikiwa wewe bado hujafikiwa,  tafadhali tutafute kwa nambari 0715 838480.

Watunzi ambao tayari wameshatoa simulizi zao ni hawa wafutao;

Kutoka  18/7/2022 hadi  7/10/2022 Hawa ndio wamefikiwa:

1. Amiri Sudi Andanenga x2
2. Ikbal Shaaban Robert (Ndugu wa Mwandishi)
3. Iddy M. Mwimbe
4. Prof. Shani Omari
5. Hussein Wamaywa
6. Dkt Elizabeth Mahenge 
7. Prof. Emmanuel Mbogo
8. Shafi Adam Shafi
9. Kevin Mponda
10. Hafidh Kido
11. Bi. Sikudhani Jalala
12. Bi. Shani Kitogo
13. Charles Mloka
14. Amiri Kaluta (Ndugu wa Mwandishi)
15. Hamisi Kisamvu
16. Athumani Mauya
17. Mwafrika Merinyo
18. Ali Athumani Masoud (Zbar)
19. Bi. Saada Kassim Ahmed (Zbar)
20. Ali Mwalim Rashid (Zbar)
21. Rose Mbijima
22. William E. Mkufya
23. Happy Msokile (Ndugu wa Mwandishi)
24. Ismail Himu
25. Esther Mngodo
26. Chambi Chachage (Ndugu wa Mwandishi)
27. Prof. Penina Muhando
28. Richard Mabala
29. Elieshi Lema
30. Mudhihir M. Mudhihir
31. Wakati Mwaruka (Ndugu wa Mwandishi)
32. Abdallah J. Saffari
33. Mugyabuso M. Mulokozi
34. Farouk Topan (Zbar)
35. Ali Mohamed Ali (Zbar)
36. Nassor Hilal Kharusi (Zbar)
37. Bi. Riziki Mohamed Juma (Zbar)
38. Amir Ali Mohamed (Zbar)
39. Ali Abdallah Bahroon  (Zbar)
40. Simba Haji Gora (Zbar) (Ndugu wa Mwandishi)
41. Ally Salehe (Zbar)
42. Bashiru Abdallah (Zbar)
43. Rashid Mbwana (Zbar)
44. Nassor Hilal Kharusi (Zbar)
45. Bi. Sabra Amran (Zbar)
46. Frank Masai
47. Hussein Molito Omari .
48. Dotto Rangimoto
49. Dickson Mtalaze
50. Florida Kezilahabi (Ndugu wa Mwandishi)
51. Abyas Mzigua
52. Godftrey Mishomari
53. Shaaban Mngazija
54. Mudi Mwanaharakati 
55. Latifa Ntanga
56. Nahida Esmail
57. Khadija Jilala
58. Fr Felician Nkwera
59. Primus Karugendo (Ndugu wa Mwandishi)
60. Bi. Pilli Dumea 
61. G.P. Mwamwingila
62. Dkt. Harrison Mwakyembe
63. Bi. Yustar A. Lucas
64. Amiri Sudi Andanenga (mara ya 2)
65. Elias Mutani   
66. Stallone Joyfully
67. Hussein Tuwa
68. Abdullah Saiwaad
69. Suleiman Kijogoo

Karibu sana katika SAUTI YA MTUNZI, tufuatilia kupitia anuani hiyo hapo chini.

Aidha, usipitwe na kipindi cha Siri ya Sifuri kila Jumatano saa 3: 00 usiku Channelten.]]>

<![CDATA[KONGAMANO LA 34 KUMUENZI SHAABAN ROBERT]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2582 Fri, 27 May 2022 03:02:30 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2582
.pdf   KONGAMANO LA 34 KUMUENZI SHAABAN ROBERT.pdf (Size: 1.33 MB / Downloads: 5) ]]>

<![CDATA[Prof. Abdulrazak Gurnah na waandishi]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2581 Wed, 25 May 2022 16:28:59 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2581 ]]> ]]> <![CDATA[SHAABAN ROBERT…..KUSADIKIKA]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1893 Wed, 29 Dec 2021 14:01:06 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1893 SHAABAN ROBERT…….KUSADIKIKA
“…Magharibi ni machweo ya jua na mwezi. Pia ni upande wa dunia wenye giza limezalo nuru zote na ufupishao uoni wa macho. Auni aliyakabili mashaka haya akafanya safari kubwa sana. Baada ya miezi Mingi kupita, siku moja alikutana na vipofu wawili njiani. Vipofu hawa wote walikuwa wanaume. Kipofu mmoja alikuwa mbele na wa pili nyuma. Uso wa kipofu wa kwanza ulikuwa na furaha kama uso wa bwana arusi, akaonekana kama aliyeridhika kabisa. Lakini uso wa kipofu wa pili ulikuwa umeghadhibika na kinywa chake kilijaa manung’uniko mengi kama aliyekuwa hakuridhika hata kidogo. Kila hatua aliyokwenda alibwata akailaani bahati yake. Auni alishangaa sana kwa kuona vile, akasema moyoni mwake kuwa watu hawa wana vilema namna moja, lakini mmoja amekinai na mwingine hakukinai. Ajabu kubwa iliooje hii! Afadhali niulize ili nielewe sababu yake. Baada ya kukusudia hivyo alitamka, “Mabwana, nyinyi ni kina nani, na asili ya upofu wenu ni nini?”
Kipofu wa pili alijibu, “Bwana wangu mwema, mimi naitwa Sapa na mwenzangu ni Salihi. Salihi haombi neno akalikosa. Ameishi maisha haya tangu ujana wake, lakini vitu alivyovipata kwa maombi aliyoyafanya alikuwa hana matumizi navyo. Nilipoona hivyo nilimwambia kuwa niliota ndoto kuwa akiomba kitu chochote tena bila ya kugawana na mimi sawasawa, dua lake halitapokewa hata kidogo. Kwa sababu hii tuliafikiana kushirikiana kila kitu atakachokiomba tukaandikiana hati mbele ya kadhi. Hati ya mkataba wetu ilipokwisha andikwa nilifurahi sana kuwa shauri langu limefaulu, lakini palepale mwenzangu aliinua mikono yake juu akaomba upofu, na kabla sijatanabahi, sisi sote wawili tulikuwa vipofu. Kama yeye anaipenda hali hii, mimi naichukia kabisa. Nilidhani ataomba niwe mfalme nizungukwe na mawaziri na kuheshimiwa na raia, au niwe tajiri ili niwatumie maskini kama nguo mbovu. Fahari ya mambo haya ndiyo iliyonishawishi kufanyiza mkataba na Salihi. Kama angalikataa kushirikiana na mimi katika fahari hii, pasingalikuwa na dawa yoyote kwa sababu nilimdhihaki tu. Sina haja ya upofu huu. Nimemsihi sana aombe nirudi katika hali yangu ya zamani lakini hakubali. Tafadhali nisaidie kumnasihi, bwana.”
Kabla Auni hajalijua neno la kutumia, Salihi alisema, “Mimi naapa kuwa sikujua kama Sapa alitamani ufalme au utajiri wakati aliponiagulia ndoto yake. Laiti ningalijua nia yake ilivyokuwa, hili lisingalitokea. Ningaliomba madua mawili mbalimbali, yaani, moja langu na jingine lake na kila mmoja katika sisi angalipata haja yake. Nilipoona mambo ya dunia yamenichukiza, nilidhani kuwa na mwenzangu yamemchukiza vile vile, na kwa mujibu wa mapatano yetu nikaomba upofu ili tuishi  bila kuyaona tena. Madhali neno nililoliomba nimelipata, wajibu wangu sasa ni kushukuru. Haiwezekani kuomba niyaone tena mambo niliyoyakataa. Nikifanya hivyo, nitafanana na ng’ombe anayeutia ulimi wake puani na kuurudisha tena kinywani. Si laiki ya mwanadamu kuwa kama ng’ombe kwa neno alilolichagua kwa hiari yake mwenyewe…….”
]]>
SHAABAN ROBERT…….KUSADIKIKA

<![CDATA[WAANDISHI WA KIKE WANAVYOMSAWIRI MWANAMKE]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1865 Tue, 28 Dec 2021 04:21:14 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1865 Waandishi wa Kike Wanavyomsawiri Mwanamke
Ipo hoja inayosema kwamba waandishi wa jinsia ya kike ni wachache ikilinganishwa na wale wa jinsia ya kiume. Kutokana na hayo, basi wenye kuwachora wanawake kwa mtazamo hasi zaidi ni wanaume, kwani wao ni wengi zaidi. Madai haya yamebainishwa na Simala (2002:72) alipofanya utafiti wake nchini Kenya. Yeye anasema ni jambo la kushangaza sana ni kwamba, mpaka hivi sasa nchi ya Kenya haina waandishi wengi wanawake wa fasihi ya Kiswahili kama ilivyo katika fasihi ya Kiingereza. Anatoa mfano katika majadiliano na waandishi wa Afrika nanukuu: waandishi wa kike waliohojiwa kutoka Afrika Mashariki (A. Mashariki) ni Grace Ogot kutoka Kenya na Penina Mlama (Muhando) kutoka Tanzania. Mjadala wa mwaka 1990 waandishi Muthoni Likamani na Pamela Kola ndio walihojiwa miongoni mwa waandishi wanawaake kutoka Kenya. Hivyo ni dhahiri kwamba wanawake wengi wasomi wamejikita zaidi katika uwanja wa kuhakiki na kuchambua fasihi kuliko kutunga kazi asilia za kubuni. Hata hivyo ni wazi kuwa fani hizi mbili haziwezi kutenganishwa kwani zinakwenda sambamba.
Mbughuni (1979) anasema kuwa katika riwaya za Kiswahili zipo picha mbili zinazokinzana za mwanamke, picha inayotokea mara nyingi ni mwanamke kama Hawa yaani mghilibu, asiyeweza kutawaliwa na mwanamume, mwanamke aliye chombo cha uovu, fujo na anayevuruga taratibu za jamii. Picha nyingine ni ya Maria yaani mama mtiifu, mwenye nyumba, pambo la mhusika mkuu wa kiume. Mwanamume anawakilisha maadili mazuri na anaokoa wanawake kwa njia ya kuoa. Katika riwaya mwanamke anayefanya mambo ya kujitegemea au anayepigania maslahi yake anaadhibiwa.
Mbughuni (1982) anabainisha kuwa uchorwaji wa wahusika unategemea ufafanuzi wa tabia au dhana fulani. Kwa mfano akielezea uchorwaji wa Rosa katika riwaya Rosa Mistika, anasema kuwa uchorwaji wake unasisitiza jinsi mazingira, silika na malezi vinavyomuathiri msichana Rosa. Rosa anachorwa kuanzia utotoni akinyanyaswa na baba yake hadi anapokuwa shuleni ambako anakutana na mwalimu mkuu.
Balisidya (1982:2) anabainisha taswira kadhaa zinazomhusu mwanamke, Taswira hizo alizoziainisha ni mwanamke kama mama, mwanamke kama chombo cha kumstarehesha mwanamume na mwanamke kama chombo cha kumilikiwa na mwanamume. Taswira hizo alizoziainisha Balisidya, zimeangaliwa na waandishi wengine wengi kwa mitizamo tofauti. Ila yeye Balisidya alimaanisha yafuatayo:
Katika taswira ya u-mama, Balisidya anaona kuwa mwanamke ni mlezi wa familia, hulelewa toka utotoni huku akijua jukumu hili la kulea familia. Haya yana uhalisia wake kwani tunawaona watoto wadogo katika michezo yao ya kitoto, wanawake huonekana wakipika, wakiosha vyombo, wakilea watoto, na kadhalika, ilhali wanaume
wakionekana kwenda shambani, kujenga nyumba, na kadhalika. Kwa upande mwingine,
tunakumbana na ukweli kwamba, mafunzo anayopewa mwanamke unyagoni huhusisha
mambo yote muhimu katika kulea familia, kumtunza, kumnyenyekea na kumtii
mwanamume, shughuli za jikoni, na kadhalika.
Balisidya anaona fasihi
kwamba, nayo hujikita kwa namna fulani katika kumpa mwanamke nafasi ileile ya
ulezi kupitia hadithi, michezo ya watoto na nyimbo. Suala la mwanamke
kumstarehesha mwanamume limebainishwa na kujadiliwa na Balisidya. Ameona kuwa,
taswira hii inamdhalilisha mwanamke kwani inamchora kwa undani  jinsi anavyotumiwa na mwanamume ili kukidhi
utashi wa haja zake za mapenzi. Mwandishi anaona taswira hii hujengwa kwa
mafunzo yanayotolewa katika jamii hususan miviga wawapo mafunzoni ya unyago,
ambapo wasichana hufundwa jinsi ya kukidhi haja za wanaume.
Mafunzo hayo
yamemsukuma mwandishi kuonesha msimamo wake juu ya manju wanaoendesha mafunzo
hayo na kuyapitisha kwa jamii kama kaida za jamii husika. Jamii imeshindwa
kutambua kuwa jukumu la mafunzo ya miviga huzilenga jinsia zote mbili ili
ziweze kuishi pamoja kwa kusaidiana. Huu ni mfano na msimamo wa mwandishi ambao
unaonesha namna waandishi wa kike wanavyoyaandika haya katika muktadha wa kumdunisha
mwanamke mwenzao katika utanzu huo wa fasihi ilhali waandishi wa kike ndio
tegemeo na msaidizi wa kumtetea mhusika wa kike. Hapa inatubidi kutoa wito kwa
wahusika hawa kujizatiti katika kuandika fasihi yenye malengo ya kuumba upya
uhai na taswira ya mwanamke katika kazi za fasihi.
Muhando (1982: 41)
hayupo nyuma katika kuandika kazi za fasihi, Yeye anamtumia mke wa mwanasiasa
kwa lengo la kubainisha uhalisi huu katika jamii. Mhusika huyu anasawiriwa na
mwandishi kuwa ana wajibu wa kumridhisha na kumfurahisha baba watoto, la sivyo
hatapata chakula. Kwa hakika huu ni udhalilishwaji wa hali ya juu unaofanywa na
jinsia ya kiume. Hali hii inasikitisha kwani kila mtu mwenye uwezo wa kufanya
kazi hana budi kula pia. Wapo wanaume wenye tabia za kuwatesa, kuwadhalilisha,
kuwanyima haki zao na kutoa adhabu dhalilishi kwa wanawake wao. Kosa hili
linasababishwa na mambo mengi ambayo tutayajadili katika kipengele kifuatacho.
Kwa upande mwingine
haya yanatokea kwa sababu ya unyonge wa mwanamke kujiona kiumbe dhaifu mbele ya
wanaume na pia hali halisi za kiuchumi, ambazo husababishwa na wanaume
wasiowaruhusu wanawake wao kufanya shughuli za kujiingizia kipato. Kwa kufanya
hivyo, mwanamke anawajibika kumnyenyekea mwanamume ili mradi apate chakula na
kinga.
Mbilinyi na wenzake
(1991) wanabainisha kwamba nafasi ya wanawake inabadilika mara kwa mara, na
hivyo wajibu wao katika jamii hubadilika pia. Kutokana na hayo, picha na
mwonekano wa wanawake unaoonekana unaowakilishwa katika kazi fasihi kuwa
unabadilika. Picha hiyo ya wanawake inayowakilishwa katika tamthiliya leo
ambayo ni aina mojawapo ya fasihi ya Kiswahili anadai kuwa inatokana na kuwepo
kwa uchumi wa aina mbili: uchumi wa jadi na ule wa kisasa. Ili kuendeleza
uchumi aina hizi mbili bila ya kuathiri au kufifia kwa mfumo wa ukabaila ni
lazima kuleta mabadiliko katika sekta ya kazi kwa wanawake. Pamoja na hayo,
kila mtu katika jamii anatakiwa kuwajibika ipaswavyo katika majukumu ya maisha
ya kila siku.
Balisidya (1982)
anasema kwamba “ukandamizaji wa wanawake na wanaume unategemea sana mahusiano
yao ya mapenzi” Yeye anabainisha dhamira tatu kuu za wanawake katika kazi,
hususan fasihi simulizi. Anamwonesha kama mama watoto, chombo cha kumfurahisha
mwanamume na mwanamke kama mali. Hata hivyo wanawake wachache sana
wanajishughulisha na fasihi simulizi na sanaa au sanaa za maonyesho. Hii ni
kwasababu wanawake hawakupata elimu ya kutosha kama au sawa na wanaume. Pia ni
kwa zile sababu tulizokwisha kuzitaja ya kuwa wanabaguliwa katika elimu.
Ubaguzi huo unawazuia wanawake wasipate vyeo vya juu na wengine wanavunjika
moyo na kukataa kujaribu kazi zinazofanywa na wanaume.
Kwa upande mwingine,
wanawake wanasaidia sana katika kujengwa na kuendelezwa kwa taswira na picha
potofu za wanawake wengine. Hii ndio sababu iliyomsukuma Khonje (1979) kuandika
kuwa wanawake wanasaidia kujenga uovu wa wanawake kwa njia mbalimbali.
Akishadidia hayo, ametoa mfano kuwa, katika familia wanawake wanawafundisha
watoto msingi ya uonevu, nafasi tofauti ya wanawake na wanaume na madaraka ya
mwanamume kama mkuu wa familia. Hivyo wanawake hawajaungana pamoja katika
kuendesha mapambano dhidi ya ubaguzi na kubaguliwa kwao. Badala yake wanasaidia
kujenga wazo kwamba mahali pa mwanamke ni nyumbani kulea familia na sio nje ya
nyumba.
Mwanga (1984) amekwepa
kumsawiri mwanamke katika hali ya kudhalilisha akilinganishwa na Balisidya
katika riwaya ya Shida. Pamoja ukwepaji huo, bado kuna taswira kadhaa
zilizojitokeza katika Hiba ya Wivu, zenye vipengele vya kumdhalisha mwanamke.
Taswira hizi ni utegemezi wa mwanamke kwa mwanamume, mwanamke kuwa kitu adhimu
na laghai.
Swila (2000)
ameichunguza nafasi ya mwanamke katika magazeti ya Kiswahili ya Uhuru na
Majira, haya ni magazeti yanayotolewa kila siku nchini Tanzania. Kwenye
magazeti haya aliangalia hadithi fupi, ambazo hupendwa kusomwa na wasomaji wa
fasihi. Katika uchunguzi wake huo, amegundua kuwa karibu robo tatu ya hadithi
hizo zimemchora mwanamke kwa mtazamo hasi hususan katika matumizi ya lugha na
maudhui. Amemalizia kwa kusema kuwa katika usawiri wa mwanamke kwa kiasi
kikubwa ni hasi, wanamchora mwanamke kama mshawishi aliyewekwa kwa ajili ya
kumvutia mwanamume kimapenzi. Masimulizi haya yameonyesha kuwa mwenye akili na
haki pekee ya kifalme ni mwanamume.
 
Momanyi (2001)
anabainisha kuwa wanawake wamepewa taswira za aina mbili: taswira ya kwanza ni
ile ya motifu ya Bikira Maria4 na taswira ya pili inayomsawiri mwanamke kama
motifu ya Hawa.5 Kuna waandishi ambao wamekoleza mielekeo ya kifeministi katika
kazi zao ili waufundishe umma kuhusu usawaq na uwezo wa wanadamu wote. Miongoni
mwao ni Momanyi (2004 na 2006) kama alivyoandikwa na Richard na wenzake (2007).
Manufaa ya nadharia hii inayozungumzia masuala ya wanawake ni kupigania usawa
miongoni mwa wanadamu na kuonesha udhahifu wa mfumo dume6 . Pia kutetea uhuru
wa mwanamke katika kufurahia haki zote za binadamu.  
]]>
Waandishi wa Kike Wanavyomsawiri Mwanamke

<![CDATA[MAISHA YA SHAABAN ROBERT NA MAWAZO YAKE (M.A. Maganga) – 2]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1407 Fri, 29 Oct 2021 11:08:08 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1407
Bila shaka, baada ya kusoma
mawazo mengi ya Shaaban Robert juu ya maisha ya binadamu, mtu atakuwa na hamu
ya kutaka kujua maswali gani yeye mwenyewe alivyoishi. Na pengine atataka
kujiuliza maswali kama haya: Je, yeye mwenyewe Shaaban aliishije na jamaa zake?
Aliishi kwa kupendana, kusaidiana na kwa usawa wa ujamaa, kama ionekanavyo
katika Adili na Nduguze? Hayo ni
kuhusu maisha yake na jamaa yake. Lakini je, yeye binafsi aliishi kwa kufanya
kazi kwa bidii kadiri ya uwezo wake, na alijitegemea kama awaidhivyo katika Wasifu wa Siti Binti Saad? Je, mtu
akiyachunguza maisha yake ataona nini katika uhusiano wa uraia wake nan chi yake?
Majibu ya maswali ya namna hii ndiyo nipendayo tuyapekuepekue katika Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini. Siyo
kwamba mimi nataka kukariri au kufupisha maandishi ya kitabu chake, bali
natarajia kutoa maoni yangu kuhusu maisha yake, na kuyalinganisha na maoni yake
kuhusu maisha ya watu kwa ujumla.
Kama ilivyo sheria ya asili, mtu
huzaliwa na kufa. Na katikati ya hayo mambo mawili ndipo penye maisha ya mtu. Mambo
mengi yanaweza kutokea katika nafasi hiyo. Napenda kutumia neno hili ‘nafasi’
ili kuleta maana halisi kwamba maisha ya mtu ni nafasi hasa ya kutenda mambo
kadha wa kadha. Maisha ya mtu ndiyo nafasi yake, na matendo yote hutegemea
nafasi hiyo. Nafasi hii ina ncha, na kwa hivyo huisha. Kwa sababu hii, maisha
si kitu cha daima na milele. Yana ukomo wake.
Inaelekea kuwa Shaaban Robert
alijivika mawazo haya kichwani mwake. Lakini hapa pana jambo zima: nalo ni
kwamba hakukomea tu kuwaza kwamba maadamu maisha ni nafasi ya mtu basi ni
lazima mtu ayatumie vema kwa ajili yake binafsi. Marehemu aliona kwamba ingawa
mtu ndiye aliyepewa maisha, lakini maisha yenyewe ni kwa ajili ya maendeleo ya
nchi. Ikiwa basi ‘maisha ya mtu ni msingi wa maendeleo ya nchi’ ndiyo kusema
juu ya maisha machafu au mazuri? Maisha ya bidii ya kazi, au ya ulegevu na
uvivu? Maisha yenye mipango maalumu, au yale yajiendeayo yenyewe ovyo ovyo tu? Maisha
ya kibinafsi au maisha ya ujamaa?
Maisha ya marehemu ya miaka
ishirini na sita ya mwanzo hayakuendelezwa katika Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini kwani, kama asemavyo katika
utangulizi, hayo yaliandikwa katika insha ambayo haikupigwa chapa na ambayo
ilikuwa katika mwandiko wa mkono na kisha haikuwa na nakala. Kwa hivyo basi,
katika hiki, mambo hayo hayamo. Baada ya shindano, insha hiyo haikuonekana
tena. Hata hivyo, tuna ufununu kwamba hayo hasa yalikuwa maisha ya mwandishi
wakati wake wa utoto-alivyopenda kucheza na alivyocheza, alivyokwenda vyuoni na
kumbini hadi akawa mtu mzima, akapata kazi na kuoa. Maisha ya kwenda vyuoni na
kupata kazi hatimaye ni maisha ya aina ya siku za kisasa. Lakini hakuna mengi
ya kuyatolea maoni kwani tumepewa hayo kwa muhtasari tu.
Kwa hivyo, tuanzie mwaka wa
ishirini na saba wa maisha yake.
Muhtasari nilioutaja awali
haugusiijambo lolote kubwa ambalo Shaaban alilifanya kabla ya miaka hii
ishirini na saba. Watu wengi, kama hawajafanya lolote katika miaka yao ishirini
na mitano ya kwanza, hakukata tamaa kuwa hawataweza tena kufanya lolote kwa
sababu wamekuwa ‘wazee’ ati! Je, Shaaban Robert alijionaje alipokuwa na umri
huo? Anasema, ‘Maisha yalikuwa bado mapya na matumaini yake yalikuwa mengi sana.’
Alikuwa mzima wa afya na mwenye furaha moyoni. Anasema, ‘Nilikuwa katika mwanzo
tu wa maisha; bado sijafika katikati wala mwisho wake.’ Lakini hakuridhika kwa
zile ‘kurasa’ chache za maisha yake ya nyuma kwani hazikuandikwa yoyote yaliyo
azizi yawezayo ‘kuwatamanisha wengine kuyanakili’ wala mwenyewe hazikumridhisha
kwamba alitarajia maisha yake yawe ni kielelezo kwa wengine na, wawezao,
wayanakili. Hakukata tama kwani aliwaza kuwa pengine ubora wa mtu huwezekana
kuwa katika wakati ujao. Yaliyopita si ndwele; ganga yajayo. Kwa hivyo
alijiandaa kutumia nafasi yake.
Shaaban aliamini kuwa ipo bahati
na huwapata watu, lakini haiji tu hivi hivi-sharti mtu ajikongoje kuiendea
ndipo akutane nayo, au ainyoshee mkono kujaribu kuishika. Kwa kutokufanya hivi
watu wamezichelewesha bahati zao au pengine wamezikosa kabisa. Na bahati
haitokei mara kwa mara. Na hata kama ingetokea mara kwa mara maisha ya mtu ni
nafasi fupi iliyo na mwisho.
Akiwa na mawazo hayo juu ya
bahati, Shaaban akayapata maisha yake mpango maalum na akaweza kuzitandaza
fikra zake zote huku ana picha kamili ya nini atakacho. Katika mpango wa maisha
yake jambo moja alilitilia mkazo vilivyo: hakutaka utajiri au mamlaka juu ya
watu. Ingawa hivi vilileta fahari, lakini kwa wakati ule vitu hivi alivihofu. Msomaji
anaweza kukubaliana naye au kumpinga akijiuliza kuwa ile miaka ya 1936 ilikuwa
ni enzi gani? Jambo alilotarajia maishani mwake ni ‘jina lililo mbali na madoa
katika umaskini na unyonge.’ Kwa hivyo kama jambo hili lilikuwa jepesi au gumu,
zuri au baya, la kumpa mtu moyo au uchovu, heri lilinganishwe nay ale mengine
mawili kwa kufuata mazingira ya nchi ya Tanganyika siku hizo. Na alitarajia
kulipata hilo ‘jina’angalau nusu au hata robo yake.
Hebu sasa tumwangalie Shaaban
Robert akiwa mchumba, mume na mfiwa-kwani jambo la ndoa, ingawa si watu wote
wanaolitekeleza, ni mojawapo ya miinuko ionekanayo katika maisha ya mtu. ‘Kabla
ya kuoa nilitafuta umbo namna yake muda wa miaka kumi!’ Shaaban alikuwa
amemtafuta mke ambaye ‘uzuri wake ulikuwa kamili’ na kwa tabia alikuwa
mwaminifu na mfano wa kuiga katika nyumba. Mchanganyiko huu wa uzuri wa umbo,
pamoja na tabia ndio uliokuwa ‘jembe’ au ‘nyumba’ kwa maongezi ya uchaguzi wa
mke.
Baada ya kumwoa Amina mwenye sifa
zote hizo mbili, Shaaban alimpenda sana na kumshukuru kwamba alimsaidia katika
mambo mengi wakati wa maisha yao pamoja ambayo yeye pekee yangelimshinda
kuyatenda. Na mengi waliyatarajia kuyafanya pamoja, Shaaban na Amina, lakini
ugonjwa ulimnyakua mapema mkewe mpenzi na akamtangulia mumewe. Bwana Shaaban
hakukilalamikia kifo kwani alijua ni lazima kije; alilalamikia kuja kwake
mapema hivyo. Akalia machozi kama alivyomlilia marehemu babake na alizipamba
dua zake kwa shairi aliloombea marehemu mkewe akubaliwe peponi.
Methali yasema ‘akosaye la mama
la mbwa huamwa’. Shaaban alifahamu kuwa mwanawe na binti yake waliyakosa malezi
na adili zote za mama yao, ndipo akawapa usia katika tenzi ambazo zilitarajiwa
kuwaongoza katika maisha yao. Akatarajia kuwalea watoto wake na kuwafundisha
wema wa moyoni. Shaaban hakuwaacha watoto wake wakue tu hivi hivi kama ua mwitu
linalotanda ovyo bila kuongozwa. Yeye aliwatunza kama maua ya bustanini.
Utenzi wa Hati kwa bintiye na Utenzi
wa Adili kwa mwanawe zilikuwa fimbo au kamba zilizo imara na zilizoongoza
kukua  kwao na maisha yao. Alikuwa na
mengi ya kuwausia kuhusu dunia. Urefu wa kila utenzi ulikuwa beti mia moja. Kwa
ufupi alimwandikia bintiye usia wa kumuasa aitunze hiyo hati imsaidie katika
dunia ngumu na ulimwengu wenye adha, asiwasaliti watu, awe na matendo mema
kwani yote hupaazwa kwa Mungu, na hati hiyo iwe mali na nuru kwake, ashike dini
kwani ni mali ya roho, ajifunze elimu awe mtalamu wa kupambanua halali na
haramu, nyumba yake iwe nadhifu, taabu zikimkabili awe amejiandaa, nia ya
maendeleo aitie moyoni, na asingoje bahati imtendee yote, kwani: ‘watu wengi
huchelewa kwa kungoja kutendewa.’ Majivuno hayafai, asishiriki uwongo, masuto
si mazuri, awe na ulimi wa kulainisha na ulio mtamu, awe na cheko na tabasamu,
usoni awe na haya, awapende wote-wenye vyeo na wanyonge-naawe na adabu kwa baba
na mama na walio sawa nao, awe mlezi bora, ajifundishe kukinai, mapato yake
yawe halali, na waijenge dunia nzuri na ya furaha-yeye na mumewe.
Mtoto wake wa kiume vile vile
alimpa maagizo ya adili. Kwanza alimfundisha awe mcha Mungu, Muumba mbingu nan
chi, wanyama na ndege na samaki, na ajuaye yote kwa ghibu bila kusoma kitabu. Ampe
yeyote roho yake ili shetani asiiteke. Pili, amtii mkuu wa Serikali bila ya
kinyume. Tatu, awape taadhima baba na mama, awatendee kila jema. Nne, afanye
taaluma ya lugha. Tano, ajifunze elimu kwani:
‘Maisha bila elimu
Hayafai mwanadamu
Sababu mambo magumu
Mengi sana mbelee.

‘Milango wazi adimu
Kwa asiye na elimu
Kwa mwenye nayo gumu
Hujifungua wenyewe.’

Sita, akioa mke amshike kwa mapenzi bila makeke, awe na
msamaha kwake, ampe heshima kama mama wa watoto wake, awapende watoto wake,
awafunze taalimu na adili, awapende sana nduguze kama alivyofanya Adili,
apatane na masahibu, kwa rafiki zake awe kitu cha makumbuko akiwapo asiwepo,
ajenge matendo mema, awapende watu wote, afiche siri zake ila kwa wachache
wapasao, akiweka ahadi kutimiza ajitahidi, atoe msaada kwa wenye kulemewa,
asiwe mgomvi, awe na uso wenye tabasamu na wenye furaha, afanye kazi kwa bidii
bila uvivu, asahihishe makosa, amwombee dua babake ambaye ni Mwafrika
madhubuti. Hakika huo ndio usia wa kuwapa watoto majumbani kabla hawajaenda
vyuoni, kwani kuna methali isemayo ‘asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na
ulimwengu.’ Maagizo kama hayo ni tunu, ngao na mwangaza katika maisha.]]>

<![CDATA[MAISHA YA SHAABAN ROBERT NA MAWAZO YAKE (M.A. Maganga) – 3]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1406 Fri, 29 Oct 2021 08:06:05 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1406
Baada ya miaka mitano ya ujane, Shaaban Robert akaoa mke wa pili. Ebu kwanza tujikumbushe ni nini aliyoyataja
kuhusu watu kama wajane au watawa katika Wasifu
wa Siti Binti Saad. Aliwapinga kwa kusema kuwa kukaa na kutoolewa kwa ajili
ya fahari ya kutoolewa tu, ni bure. Hakuna maana. Kwa hivyo yeye akaoa ‘msiba
ni tokeo kwa watu wote. Maisha ya ujane yalijaa tuhuma. Heshima yake ilikuwa
ndogo lakini aibu yake ilikuwa kubwa.’ Kifo kilivunja mkataba wa ndoa na akawa
hutu kuoa; akaoa ‘msichana aliyekuwa na nasaba njema na aliyepata malezi mema
vile vile’
Katika kuoa kila mara, Shaaban
alifuata mambo mawili. Kwanza alifuata uzuri wa mwili na wa tabia. Pili, ndoa
zake hakuziharakisha-alichukua muda wa kutayarisha jambo hilo. Yule wa kwanza
alichukua miaka kumi, na huyu wa pili miaka miwili. Alikuwa akimfariji ‘kama
mama na dada akaziba pengo la ujane kama mke halisi.’ Inaelekea wazo la kuoa
zaidi ya mara moja halikuwa la asili yake. Shaaban anaandika kuwa, ‘Wasutaji
wakinidhihaki kuwa nilikuwa mume wa wake wengi na tabia mbaya wakumbushwa kuwa
nilikuwa sina ahadi wala mkataba na msutaji hata mmoja kuwa sitaoa tena hali ya
mambo ikilazimisha jambo hilo.’ Mauti ndiyo yaliyotangua ahadi yake. ‘Isitoshe;
mke wangu wa kwanza aliishi na mimi kwa wakati fulani mbali, na wa pili alikuwa
na wakati wake mbali vile vile. Hawakukusanywa pamoja katika wakati mmoja wala
katika nyumba moja kama mapacha mimbani au wanyama zizini. Ningalipenda niweze
kuishi na mke mmoja tu lakini bahati haikuniamuru nifanye hivyo.’ Hivi ndivyo
alivyowaza na kufanya kuhusu ndoa.
Je, kazini nako? Kwanza inataka
tufahamu kwamba marehemu hakukaa bure bila kazi. Yale aliyowausia wanawe ndiyo
aliyoyatenda. Kwa hivyo alikuwa ni mfanya kazi. Hakuna tusomapo kwamba alikuwa
na mali aliyopenda wanawe warithi kwani alikuwa ni mtu hivi hivi; si tajiri wa
mali. Utajiri wake ulikuwa ni akili zake na nguvu za mwili wake pamoja na
mipango yake. Elimu humwezesha mtu kupata kazi ya aina fulani tu, lakini
pengine elimu pekee siyo aifanyiayo kazi mtu. Mbali na elimu, juhudi na kupenda
kazi ndio mchanganyiko wa rutuba ya mbolea na maji kazini. Matokeo yake huwa ni
matunda mema ya maendeleo kazini. Hii ni siri kubwa ya kazini. Ndiyo yaliyomo
katika kiini cha kazi. Elimu ni mlango tu wa kuingilia kazi fulani.
Katika Wasifu wa Siti Binti Saad,  Shaaban anatoa mawazo yake kuhusu kazi, na
anasema kwamba kazi lazima ipendwe, ifanywe kwa bidii, isibadilishwebadilishwe.
Kwa kufanya hivyo Siti binti Saad aliendelea vyema na kazi yake ya kuimba. Na hata
naye Shaaban hakupenda kubadilisha kazi na, mwaka alipohamishwa kwenda idara
nyingine, anasema kuwa sikuzote angependa kuwa katika idara moja.
Shaaban aliingia kazi ya ukarani
forodhani ambayo aliifanya mpaka ikafikia miaka kumi bila kubadili! Kazi hiyo,
siku za 1926, kianzio chake kilikuwa shilingi sitini kwa mwezi, lakini aliishikilia
tu! Je, hii inaonesha uvumilivu au shida ya ukosefu wa kazi nyingine? Ni wazi
jambo hili linaonesha ule moyo wa ujamaa aliokuwa nao marehemu. Kwa miaka kumi
hiyo nyongeza yake ilikuwa shilingi sitini tu! ‘Lakini, anasema, ‘kila ongezo
la mshahara lilizidisha uzito wa shughuli kulemea juu ya mabega yangu.’ Kama wewe
msomaji ni mmojawapo wa waliofanya kazi za afisi miaka hiyo, jaribu kufikiri
tena jinsi zilivyokuwa kazi nyingi, na linganisha na pato lake. Au, kama wewe
ni mfanyakazi wa siku hizi, hebu angalia jinsi kazi zilivyokatwakatwa ili
kuwepo wafanyakazi wengi wa kazi moja na jinsi ambavyo mshahara wa kazi hiyo
haukukatwakatwa kugawanyiwa hao wanaoifanya, bali kumewekwa mishahara
mbalimbali, kila mtu na wake, tena si shilingi sitini kwa mwezi! Wale ambao
hawajawa wafanyakazi nawajaribu kulinganisha mshahara huo na yale matumaini yao
tu.
Siku hizo za marehemu kulikuwa na
ubaguzi baina ya wenyeji na wageni katika kazi. Kwa wenyeji wenzake alikuwa
mfano wa kuiga. Lakini kwa wageni kazi yake nzuri ilionewa wivu, jambo ambalo
anasema aliliogopa kama alivyoiogopa tauni, na akajaribu kulikimbia kama
ikimbiwavyo njaa. Je, jambo hilo la wivu afisini alilifanyia nini? Hakuacha juhudi
mpaka uadui ukaupisha urafiki.
Mojawapo ya kazi zake ilikuwa ni
upokeaji fedha na utoaji stakabadhi-kazi yenye mtego na hatari ya kutamani
kuiba, hasa kama karani huyo kima chake cha mshahara ki mbali na fedha azionazo
na kuzishikanisha kila siku. Lakini Shaaban alikuwa imara. Anasema, ‘Kosa ni
uanadamu.’ Siku moja, kulitokea kasoro katika kazi yake hiyo: tafauti ya
upungufu wa shilingi sita! Lakini hakuwa ameziiba. Alikuwa ameziweka mahali
pasipo pake tu, na kisha akasahau. Katika kazi yake ya pili alikuwa mkubwa wa
watu wa kabila, dini na madhehebu mbalimbali. Hawa, anasema, alipatana na
kupeana msaada nao kama walikuwa “Mti-pane” usiovunjika.
Shaaban ana mengi ya kutuachia
kama kielelezo. Jinsi alivyopanda cheo ndivyo jinsi alivyoyapanua mawanda ya
jina lake katika Idara, na alijishughulisha pia kuyaswagia moyoni majina ya
wale alioshirikiana nao katika kazi yake. Kuwa hodari wa kazi, kuwa na uwezo wa
kuchukuana vyema na wafanyakazi wote wa chini na wa juu ndio mfano aliotuachia
marehemu, tuwe nao kazini.
Wafanyakazi hutazamia mabadiliko
mara kwa mara. Mabadiliko ya kazi bora ni kuongezwa mshahara na cheo, na wakati
mwingine uhamisho pia. Baada ya miaka kumi na minane forodhani Pangani Shaaban
aliyapata yote hayo mabadiliko matatu. Alipandishwa cheo cha pili katika
makarani, akapata na uhamisho wa Idara-akenda kwenye Idara ya Utunzaji wa
Wanyama huko Mpwapwa ambako alikaa kwa miaka miwili.
Hapa sitahakiki kazi yake huko
Mpwapwa maadamu ilikuwa nzuri kama kawaida yake. Badala yake, nimechagua kutoa
maoni yangu kuhusu taabu na matukio yaliyimpata kuhusu uhamisho huo. Ingawa alisita,
kama wafanyakazi wengi wafanyavyo, baadaye alitambua kuwa uhamisho huwa una
sababu iliyo nzuri. Kwa kuwa alikuwa anapelekwa mahali papya kwa kazi mpya
anasema, ‘Nilijiona kama mtu aliyepewa shoka na mundu kufyeka njia mpya katika
pori kubwa.’ Aliukubali uhamisho huo kwa kutii amri ya wale waliomtunukia cheo:
‘Nilipewa amri sio uchaguzi.’ Kwa hivyo, hata kama ilikuwa ‘mkuku ng’ombe’,
ilimbidi ahame. Na bila shaka kuondoka ilikuwa ni lazima. Ndege mwenye kutua
tawini lazima aruke. Huu ndio moyo ambao marehemu angelifurahi wafanyakazi wote
kuwa nao.
Pia hakukosa shukrani. Alishukuru
kwa kupandishwa cheo bila ya kukiomba. Msomaji akumbuke kuwa mfanyakazi huwezi
kuwa na sifa bora kazini na papo wakuu wake wasimtambue kwa kumpandisha cheo. Kupandishwa
cheo si tukio la binafsi tu bali ni pamoja na cheche nzuri ziwafikiazo wakuu wa
kazi. Kabla hajenda Mpwapwa, Shaaban alirudi kwao Tanga kupumzika kwa siku
ishirini, na huko alishughulika na kuwarithisha warithi wa mali (mashamba ya
minazi) za marehemu mkwe wake na warithi wa mali za mke wake. Ingawa kulikuwa
na mzozano fulani, kama ilivyo desturi katika mambo ya urithi, Shaaban
aliyatuliza yote.
Baada ya mapumziko yake safari ya
uhamisho ikaanza; Shaaban akiwa abiria cheo cha pili kutoka Tanga hadi Mpwapwa
kupitia Korogwe, Morogoro na Gulwe. ‘Kumbe safari kweli taabu’ ni usemi wa
kweli, kama alivyoimba mwimbaji fulani. Lakini safari ya Shaaban ilikuwa ni
taabu zaidi kwa vile alikuwa Mwafrika ingawa alikuwa na cheo cha pili. Korogwe ilitokea
shida, aliposhuka kungoja safari ya lori. Anasema, ‘Karibu ningalilala nje
Korogwe kwa ukosefu wa malazi ya abiria Waafrika.’ Lakini mtu mmoja, bila shaka
ni Mwafrika mwenzake, alimchukua kwake kumpa malazi mema.
Jambo la kusikitisha zaidi
lilifanyika keshoye Asubuhi alipolazimishwa na Mhindi, msimamizi wa safari,
ashuke kutoka lori la abiria wa cheo cha pili apande lile la cheo cha tatu au
la mizigo kuwapisha nafasi Wahindi wane waliochelewa kuja. Yeye na watoto wake
tu ndio waliokuwa abiria Waafrika katika lori hilo la cheo cha pili, tena
walikwisha wahi kukaa mapema. Lakini mhindi yule hakuona mtu mwingine wa
kumshusha ila Shaaban na watoto wake. ‘Baridi ina mzizimo siku zote kwa kondoo
mwenye manyoya haba’, ndivyo Shaaban alivyoandika. Baada ya kumjibu maneno ya
haki, kwamba yeye naye alikuwa ni abiria wa cheo cha pili na mfanyakazi
Serikalini, aliendelea kukaa; na, kwa vile hakuwa na haki ya kutereshwa, Mhindi
aliwaamuru matarishi wamakamate na kumtupa chini kama mtumba. Mungu awaweke
matarishi hao; hawakutii amri! Lakini, kwa kuwa Shaaban hakupenda kuchelewa
bure Korogwe, aliita watu waje kushuhudia atendewavyo. Wengi wakampa sahihi za
mikono yao na, ingawa yule Mhindi alikataa kuandika stakabadhi ya kuonesha
namna Shaaban alivyosafiri kutoka Korogwe, Shaaban aliwapisha wale Wahindi wane
naye akapanda juu ya gari la mizigo. Lakini hatupati tena habari hii.
Kisa cha tatu ni kile cha
Mpwapwa, Kikombo. Kwa kuwa walifika saa kumi za usiku, aliambiwa akae juu ya
gari hadi saa moja Asubuhi ‘wakati mwendeshaji wetu alipoingia nyumbani mwake
kulala.’ Mpwapwa ni pahali penye baridi kali sana hasa, huo mwezi wa Julai
alipofika Shaaban. Mimi ni mzaliwa na mkulia wa huko; kwa hivyo nafahamu. Lakini
licha ya kumwacha kupigwa na baridi, kumwacha nje mtu mgeni kaka yeye, tena
mahali kama hapo, si uungwana. Na pia, kulikuwa na shida ya nyumba. Hata hivyo,
jambo kuu la Shaaban ni kwamba hakuziacha shida hivi hivi tu bila ya kutafuta
sababu zake. Na, ingawa alikuwa mfanyakazi wa ‘cheo cha juu, hakupigapiga
kelele. Alivumilia.
Katika mwaka huo huo Shaaban
akahamishwa kurudi tena Tanga. Safari hii uhamisho wake ulisababishwa na ombi
lake mwenyewe la kutaka kumwezesha bintiye aendelee na masomo ya juu huko
Tanga. Na hakuomba kwenda Tanga tu, bali kokote kwingine ambako bintiye
angeweza kusoma. Kisomo cha bintiye ni mwangwi wa mawazo yaliyomo katika tenzi
zake za usia. Shaaban anaona kuwa ni sharti watoto wapelekwe skuli;
wote-wavulana kwa wasichana. Anasema, ‘Wakati tulionao sisi sasa, kosa la
kumwelimisha mtoto haliwezi kusameheka hata kidogo pasipo mapatilizo. Mtoto yeyote
anyimwaye makusudi nafasi ya kujifunza matumizi yak soma, kuandika na hesabu
ana haki ya kuwalaumu wazazi wake katika maisha yake atakapojiona kuwa
amefungiwa milango yote ya kusitawi baadaye.’ Haya, sikieni wazazi!
‘Bahati ilinifanya mshairi tangu
1932.’ Hivi aanzavyo kusema juu ya ushairi wake. Mbali na kazi yake maalumu,
Shaaban alikuwa mshairi mashuhuri. Mashairi yake bado yanasomwa sana shuleni,
vyuoni na hata majumbani kwa sababu yanafunza na kutia moyo katika kupambana na
maisha ya dunia hii. Watu wengi husahau kwamba wanaweza kufanya mambo zaidi ya
moja kwa wakati mmoja, kama vile Shaaban alivyokuwa mfanyakazi na mshairi pia. Leo
tuna mfano mzuri wa Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius K. Nyerere. Yeye ana
kazi kemkem za Uraisi na uongozi wan china, pamoja na hayo, anatoa mawazo yake
vitabuni. Mpaka sasa hivi ameandika vitabu vimgi sana ambavyo ni msingi wa
maendeleo ya nchi yetu. Hali kadhalika Shaaban naye, katika enzi zake alijishughulisha
na maandiko au fasihi. Ameandika mawazo yake kwa njia za hadithi na mashairi. Kama
Mheshimiwa Waziri wa Elimu wa mwaka 1966, Bwana Solomon N. Eliufoo, alivyosema
katika dibaji ya kitabu hiki hiki tukizungumzacho, ‘Alikuwa mshairi maarufu…..na
kila aliyewahi kusoma tungo zake…hakukosa kupata fundisho fulani…Mbinu ya
kalamu yake mpaka dakika ya kufa kwake ilikuwa ya hekima tupu (au kwa kileo
tusemavyo ya Folosofia).’ Huo ni mfano kwa wale wenye mawazo mazuri ya
kuendelezea nchi na wenye kipawa cha kuandika, waandike ili mawazo yao yasomwe
na wana wao na wa wenzi wao na vizazi hata vizazi.
Yeyote anayeipenda nchi yake
haitumikii tu bali huwa kama kipima-joto cha mahospitali. Huweza kuona hali ya
nchi ilivyo, akafanya kila bidii ili kuleta maendeleo. Kufanya hivyo
kunategemea wakati na mazingira yenyewe. Shaaban anaonesha kuwa aliipenda sana
nchi yake Tanganyika. Kwanza aliitumikia bila manung’uniko na kwa bidii zake
zote, kisha akaipigania kuikomboa iwe huru. Lakini vipi? Alikuwa na ari ya
siasa. Anasema, ‘Alivyokuwa kila mtu ndivyo nilivyokuwa mimi vile vile. Nilitekwa
na uzalendo….Sikupenda kuwa mgeni katika nchi ya asili na uzazi wangu. Sikutaka
kuwa mtazamaji wakati wananchi wengine walipokuwa wachezaji, nikajiunga na
chama….cha siasa cha Waafrika kilichoundwa…1929.’ Hiki ndicho chama kilichokuwa
asili ya TANU ambacho kilizaliwa 1954 kikawa na wanachama wengi zaidi na
kupigania uhuru na utawala chini ya uongozi wa Julius Nyerere.
Serikali haikupenda wafanyakazi
wake wawe wafuasi wa chama cha 1929, kama ambavyo vile vile haikupenda wawe
wafuasi wa kile cha 1954. Kwa hivyo ilijitahidi kila mara kuwawekea vipingamizi
na hatimaye ikawazuia kabisa kuwa wanachama. Mawazo yake Shaaban juu ya Rais wa
chama na wakuu wenzake ambao kazi zao zilikuwa ni za kujitolea yalikuwa ni
kuwaonea huruma na kuwatia moyo kupigana vita hivyo.
Huku kazi, huku siasa, na huku
uandishi. Yote haya aliyafanya Sheikh Shaaban. Katika fasihi yake Shaaban
alichukua wazo juu ya ujane kwa kufikiria ubora na ubaya wake kwa nchi yake
yenye eneo la maili mraba 365,000 iliyokuwa na jumla ya watu chini ya milioni
10. Ushairi ndio sanaa aliyoitumia kutolea mawazo yake juu ya ujane, akasema, ‘Ujane
una matata si jambo la kutumia.’ Mara dhoruba ya ukinzani ikaanza, huyu akisema
hivi na yule hivi hata magazeti mazuri yakachafuka. Lakini, hata hivyo, alipata
watetezi wengi walioandika kutetea ujane, nay eye mwenyewe binafsi alipenda
nchi ijae watu-lakini sharti watu hao wawe wamezaliwa kwa ndoa ya halali. Ndipo
aliposema:
‘Mume ni
mume, ingawa gumegume, ana sifa ya Mtume;
Na mke ni
mke, ingawa kikwekwe, ana manufaa yake.’
Katika mwaka 1959 ikambidi kuacha
kazi. Akawa amefanya kazi miaka 33, na umri wake miaka 57. Kwa kazi zote
alizozifanya, pamoja na dhiki za mahamisho mengi, cheo chake hakikupanda zaidi
ya ukarani! Mtu kama yeye, kama ingekuwa anaacha kazi leo, angepewa zawadi
nyingi-kiinua mgongo. Angefanyiwa karamu na kuletewa kalamu mbalimbali za
shukrani kwa kazi alizofanya, na pia kumtakia heri kwa siku zake za usoni. Lakini
haya Shaaban hakuwa na bahati nayo. Mzungu mmoja tu ndiye aliyempelekea zawadi.
Hata hivyo Shaaban hakunung’unika. Kwake yeye ushairi na kalamu ya kuandika
ndivyo vitu vilivyokuwa bora zaidi! Anasema, ‘Mbinu hufuata mwendo. Mwendo niliopenda
kabisa maishani ulikuwa huu.’ Kisha baada ya kustaafu, Shaaban alimshukuru
Mwenyezi Mungu aliyemlinda na kumwendeleza kazini, na kuwa naye siku zote
katika miaka yote ile 33 ya usumbufu.
Jambo moja zaidi, ambalo hakuna
aliyelitazamia, lilitokea. Alidaiwa kurudisha gharama ya usafiri iliyotolewa
idhini na Mudir  wa Idara alipostaafu. Sababu?
Waliokuwa wakipata usafiri wa bure ni wale waliokuwa wakirudi kazini au makwao
nje ya Tanganyika! Yeye Mwafrika Mtanganyika safari ya kurudi nyumbani kwao
ilionekana kama ambaye anakwenda ‘Uingereza au Bara Hindi.’
Shaaban Robert hakuwa mzalendo
mwenye kuipenda, kuitumikia, na kuipigania Tanganyika tu, bali pia alikuwa na
ule moyo wa kutaka kuwaona binadamu wote ni sawa. Kwa hivyo, mawazo yake
yalivuka mpaka wa shida za Tanganyika, akalifikiria bara zima la Afrika. Jicho lake
la mawazo likatua huko Afrika Kusini ambako Kaburu hadi leo bado anawanyonya na
kuwabagua watu weusi ambao ndio wananchi halisi. Shaaban hakuvumilia ukatili
uliotendeka huko na uliutia moyo wake machungu. Maoni yake kuhusu usawa wa
binadamu wote ni hivi: ‘Wajibu wa watu katika maisha ni kuwiana hisani, usawa,
adabu, heshima na mapenzi…Katika Afrika Kusini wajibu huu ulimezwa na ubaguzi
wa kutisha. Watu waliusiana chuki, kiasi na makanio. Pumzi ya kila mmoja ilijaa
hofu, kutoridhika na manung’uniko, sumu juu ya sumu.
Shaaban alifurahi kuona Serikali
ya Tanganyika huru ikivunja uhusiano wa Kibiashara na Afrika Kusini ‘mpaka
tabia yake itakapokuwa imebadilika kuwa njema na ya amani kwa watu wa rangi
zote.’ Na ndivyo Serikali yetu ilivyofanya hadi leo hii. Biashara nyingi
ziliathirika kwa msuso huo. Hata yeye Shaaban, baadhi ya kazi zake za sanaa ya
ufasihi-zilizokuwa zinapigwa chapa na Chuo Kikuu cha Witwatersrand, kama Kielezo cha Insha ambacho sasa
kinachapwa na Oxford University Press-ziliathirika. Mawazo yake juu ya athari hiyo
ni haya: ‘Walakini, ikiwa change ndogo kama ilivyokuwa yangu mimi ya sadaka,
ilisaidia kupatikana kwa ufanifu wa uhuru na amani kwa watu katika Afrika Kusini,
hasara hii ilikuwa si kubwa ilinganishwapo na furaha ya ushindi uliotazamiwa
kuja kwa watu mwisho; ushindi uliokuwa si wa mweupe, mwekundu wala mweusi,
lakini uliokuwa wa wote; na fahari ya kila taifa katika dunia.’ Yeye alikuwa na
nia moja tu: kukomboa utukufu wa mwanadamu, hata kama ilikuwa kwa kujitoa
mhanga.
Kazi za uandishi za Shaaban ni
nyingi, nazo zilipata neema kwa vile baadaye vitabu vyake vilipata kupigwa
chapa hapa hapa Tanzania. Pia huko Kenya kazi zake nyingi zilipigwa chapa, na
Julai 1960 duka lake likafunguliwa. Alipoona wengi hawanunui vitabu vyake
aliwapa bure. Wakamshukuru, naye akafurahi kwa mara nyingine tena kwa change ya
namna hii. Kutoa misaada kwa namna hii ni tendo la kiujamaa. Hivyo ndivyo
alivyojaribu kuitenga nafsi yake kando ili awatumikie watu. Kama alivyomuusia
mwanawe, mwenye msaada ampe asiye nao. Shaaban alitoa alichokuwa nacho.
 Hivi nivyo alivyoishi mtu aliyetoa mawazo yake
katika Wasifu wa Siti binti Saad na Adili na Nduguze na mahali pengi
pengine. Je alitimiza lengo lake la kuwa na ‘jina’ ulimwenguni? Msomaji utaweza
kulijibu swali hilo wewe mwenyewe. Mimi naona maisha yake ni kielelezo kikubwa,
na yalikuwa ni msingi mkubwa wa maendeleo ya nchi yetu.
Katika kuhakiki vitabu viwili vya
kwanza nilisema lengo kuu la Shaaban kuandika ni kutaka watu waishi kwa
kupendana. Huu ndio msingi wa kuishi kwa Kujitegemea
na kuishi kwa ujamaa. Tumemwona alivyoishi
na wakeze, wanawe, wafanyakazi wenziwe, wananchi wa Tanganyika, na hata jinsi
alivyotandaza mawazo yake kwa wanaadamu wote. Matendo yake yatakamilisha mawazo
yake.
Maisha ya Shaaban Robert, kama
yalivyoandikwa katika Maisha Yangu na
Baada ya Miaka Hamsini, yameandikwa na Shaaban mwenyewe. Wengine wanaweza
kusema kwamba hakujiweka kwenye mizani na kujiandika bila kujipendelea. Mimi naona
amejiandika bila kujipa jambo lolote lisilo lake, wala hakujirefushia jambo
lolote ambalo ni fupi. Amekuwa na kiasi. ‘Maisha yalikuwa matendo, siyo
usingizi,’
 
Na sasa tumeona kwamba ingawa
maisha ya mtu yanafungamana na pengine huongozwa, na mazingira yake-binadamu
wenzake, mahali alipo, na wakati wenyewe aishio-yeye mwenyewe ndiye mwenye
jukumu lote kwa yale ayajazayo katika nafasi ile. Mawazo ya kujitegemea, kama
ayatoavyo Shaaban katika Wasifu wa Siti
Binti Saad, na mawazo ya ujamaa yaliyomo katika Adili na Nduguze na popote pale, yamo tena katika Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini.

<![CDATA[SAA NNE MAALUM NA MWANDISHI ADAM SHAFI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1404 Thu, 28 Oct 2021 04:57:12 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1404 [Image: adam-shafi.jpg?w=500]

Nimepokea simu. Simu ya maana. Adam Shafi yuko Majuu. Kaja kikazi Uholanzi. Yeye mtaalamu wa lugha ya Kiswahili. Baada ya kumaliza kapitia Uingereza katika mji mmoja wenye wakazi wengi wa Kitanzania, yaani Milton Keynes. Ni wastani wa saa moja kwa treni toka London.  Mrefu, mchangamfu, mzungumzaji aliyesheheni “mastore” kibao. Nishakutana na waandishi wa kila sampuli. Wanaojificha: wakimya, wasioongea sana, wapole wanaokaa chumbani kati kati ya watu ukadhani hawapo. Wanaopiga kelele, wakijafaragua; ama wenye aibu…
Shafi ni mtu wa kawaida kabisa, naweza kuiita hulka, tabia na namna yake “Mfurahia Maisha” : kachangamkia  uhai, haswa. Kaishi, anaishi…hamalizi. Kila mara atasema ana mikakati ya kufanya jambo fulani, kuandika kitabu kingine kipya, kuendeleza fasihi na Kiswahili….
 
Katika saa nne zote nlizokuwa naye ananikumbusha moja. Ikiwa umewahi kuvisoma vitabu vyake utagundua huchanganya kila kitu: furaha, simanzi, vita, amani, mapenzi, karaha, starehe, maonyo, mandhari, elimu na mengine tele. Ukiongea naye yuko hivyo hivyo. Mastore kibao. Anaelezea namna wachapishaji waliotafsiri moja ya vitabu vyake walivyotaka kumrusha fedha. Akawafungia safari hadi Paris kudai haki hiyo. Au alivyofiwa na mpenzi wake wa ujanani zamaaaani…pamoja na mtoto. Alivyotiwa jela ugenini ujanani (anamalizia kitabu kipya kuhusu kisa hiki, soma mbeleni); alivyofungwa Unguja baada ya mauaji ya Rais Karume. Hadi leo mguu wake wa kushoto ananionyesha bado una dosari (“pana ganzi pajani shauri ya kulala sakafuni”); alifungwa miaka miwili. Visa, kibao. Vyote vimepenyezwa angalau kiduchu ndani ya vitabu vyake. Vingine vishatafsiriwa lugha za kigeni. Kimoja kilishinda tuzo. Niko naye. Tunakula ubwabwa  uliopikwa vizuri na binti yake kwa nyama za kukaanga…huku tukila huku tukiongea. Mazungumzo hayaishi. Ingawa masaa manne mengi kukaa na mtu (kwa huku Ulaya ambapo muda ni dhahabu) nahisi itabidi nipewe miezi ili kujua mengi zaidi ambayo nataka kuyafahamu. Anachonifurahisha ni hii picha akiwa na mjukuu wake wa miaka minne. Huyu ni mtu aliyeshaishi. Akaona mengi. Akazaa. Akalea. Aka…mcheki.
[Image: shafi-w-lowell-grandson.jpg?w=500]
Waandishi ni watazamaji na wasikilizaji wakubwa wa jamii. Waandishi ndiyo hutukumbusha yaliyotokea. Kusingekuwepo waandishi tusingefahamu yaliyopita. Kila mmoja wetu kila siku anahangaika na maisha. Tunaamka, tunakula, tunakwenda kazini au masomoni. Tunarudi , tunalala, kesho yake hayo hayo: kila kukicha na kuchwa tunaona mengi, tunayapita, tunayasahau. Ila waandishi? Wasanii? Kazi yao kuweka kumbukumbu ya haya mambo. Kuyahadithia. Wapo waandishi wa aina nyingi. Wana habari. Waandishi wa elimu na historia. Washairi. Watunzi wa muziki na nyimbo. Sinema. Tamthiliya.Wapo waandishi wa fasihi kama Adam Shafi. Shafi alianza na kitabu cha “Kuli”, kinachoelezea mgomo maarufu wa wafanyakazi maskini , Unguja mwaka 1948. Anasema alikuwa na miaka minane tu. Na ingawa anakumbuka juu juu  tukio hilo utotoni, alikuja kuhaditihiwa na mtu akaweka kumbukumbu na baadaye maandishini. (Unaona waandishi walivyo watu muhimu, kutukumbusha?)
“Kuli” kilichapishwa na Tanzania Publishing House (TPH) miaka ya Sabini. Lakini awali  alichapisha “Kasr ya Mwinyi Fuad” ambacho kimeshatafsiriwa  lugha tatu za kizungu: Kijerumani, Kifaransa na Kirusi.
Miaka ya karibuni, Shafi kaibuka na “Vuta Nkuvute” kilichopata Tuzo kwenye tamasha la vitabu, Dar es Salaam, mwaka 1998. Ni kisa cha mapenzi, tena mapenzi makali na mazito kati ya msichana wa Kihindi na Mwafrika. Humo mna siasa na harakati za uhuru na mengi mengine. Mseto mkubwa wa mapenzi na siasa, ambao si waandishi wengi wa KIswahili wamemudu kuuchanganya.
“Vuta Nkuvute” kilichapwa na Mkuki na Nyota. (Soma habari zao hapa : http://www.mkukinanyota.com) .
Mwaka 2003 mwanafasihi huyu alitoka na “Haini” ambacho kama anavyosema mwenyewe kiliogopwa na wachapishaji wengi nchini. “Haini” si mchezo. Kitabu cha moto, cha kuchachafya. Soma ukurasa  wa kutisha wa mfungwa mmoja akipambana na chatu, ukurasa wa 172:
“Anaiangalia dunia kwa hofu na kukata tamaa, anachungulia kaburi. ..Alipomtazama yule chatu alimwona anaanza kujinyumbua, ananyeka, kichwa amekiinua,kama anayezindukana kutoka usingizini. Chakula chake amekwisha andaliwa, hana wasiwasi. Tayari kimo mle chumbani.”
Kama  desturi  visa vyote vya Shafi hujaa mateso, shida, majonzi, taabu za Mwafrika;  lakini haviishii na hisia hizi za kukata tamaa na kutokwa machozi. Wahusika wake huteseka lakini mara wakaibuka, wakaamka na kupambana na matatizo yao. Matumaini ndiyo rangi ya suluhisho lake.
“…Moyo wa ujabali ukamjaa tele akahisi na nguvu kama za simba yuko tayari kuvaana na chatu yule kwa mikono yake miwili. Chatu naye amenyanyua kichwa anajiramba midomo. Huutoa ulimi wake halafu akaurudisha  ndani na pale anapoutoa utadhani  anatoa miali ya moto kutoka mdomoni. Wanatazamana. “Nani atakayeanza kushambulia?” Haramia anajuliza.”
Msomaji sin’takueleza yaliishia wapi. Maana ukijua hutatamkiwa kitabuni. Nnachokumbuka sikulala baada ya kusoma sura hii. Inatisha. “Haini” ni kitabu kinachosisimua sana. Kilinikumbusha visa vya mwandishi wa Kimarekani Stephen King, ambaye karibu vitabu vyake vyote vishafanywa sinema. Sinema yake maarufu ni ile ya kutisha sana iitwayo The Shining. Sidhani ntakosea nikisema maandishi ya Shafi hayapishani na waandishi wa aina hii hata kidogo. Vikitafsiriwa vitapendwa ulimwenguni kote. “Haini” yahusu namna Shafi alivyofungwa jela miaka miwili akiwa bado mwandishi wa habari (taaluma yake kikazi)…akifanya kazi gazeti la “Uhuru” ambalo enzi za miaka ya Sabini (alipowekwa kizuizini) visiwani liliitwa “The Nationalist.” Ubaya,walakini, mmoja. Kitabu hiki kimechapishwa Kenya na Longhorn (http://www.longhornpublishers.com). Bongo hakipatikani kirahisi bali duka moja tu mitaa ya Kinondoni.
Vitabu vyake vyote Shafi vinaonyesha maisha ya sasa na yale yaliyopita. Anapenda kuhusisha historia ya jamii. Kwa hivyo mbali na kustareheshwa unafahamishwa mambo yaliyopita ya zamani. Hali hiyo imo pia katika muswada wake mpya “Mbali na Nyumbani” ambao unaelekeza maisha ya ujanani wa mwandishi.
[Image: page-from-manuscript.jpg?w=500]
Namsikiliza mwanafasihi huyu aliyezaliwa Unguja mwaka 1940 akinisomea: “Mbali Na Nyumbani.” Anasema huchukua wastani wa miaka mitano kumaliza kitabu kimoja. “Huwa sina haraka hata kidogo…” Huandika kwanza kwa mkono halafu ndiyo akachapa katika tarakilishi (kompyuta)….”Mbali na Nyumbani”  anafafanua, kinasimulia ujana wake kati ya mwaka 1960 na 1967 …akijaribu kuvuka Afrika kwenda Ulaya. Hapa alipo ukurasa wa 427 (cheki picha juu)anasimulia akiwa mpakani Sudan kuingia Misri. Anaposoma ananikumbusha mwaka 1978 nilipojaribu na mimi kustoawei kwa meli. Vijana enzi hizo tulitaka sana kupanda meli. Ubaharia ulikuwa kazi ya kutamanika, kutafutwa na kuotea. Miaka hiyo imepita. Leo Vijana bado wanaotea kuingia nchi zilizoendelea. Nchi za Magharibi. Maisha yalikuwa magumu enzi zile, bado magumu leo, miaka arobaini na sita baada ya Uhuru. Lakini Wazungu wamefunga mipaka. Hawataki wageni. Enzi hizo ilikuwa vile vile.  Kupata “kitabu”ilikuwa kazi; leo pia iko kazi. Kupata visa ilikuwa kazi; leo pia iko kazi.
Miaka kumi na mitano iliyopita mtindo uliibuka kwa Mwafrika kujifanya mkimbizi. Hiyo ziku hizi imeshatafutiwa ufumbuzi. Wazungu washajua. Washajua mathalani kuwa Bongo hakuna vita. Yalipokuja mauaji na machafuko ya Burundi na Rwanda wengi tukaanza na sisi kujifanya wakimbizi kutoka sehemu hizo. Ujanja huo ulifaa hadi miaka michache iliyopita. Leo yamegeuka. Wahusika washagundua. Ukimbizi leo haufai tena kama sababu. Yuko jamaa kanieleza ujanja mpya. Kujifanya junya au firauni. Si mnajua tena kuwa jadi hii nchi za Kizungu inaruhusiwa? Mwanaume kuoa mwanaume au mwanamke kumwoa mwanamke mwenzako?
Mwezi jana ilipitishwa sheria Uingereza kuwa ukishtakiwa kuwa umemtania msenge au firauni unakwenda jela miaka Saba. Vituo mbalimbali vya polisi vina vitengo maalum vya kutetea maslahi ya wasenge, na vinaongozwa pia na polisi wasenge. Basi kusikia hayo walala hoi nao wamegundua mpya. Afrika tabia hii hairuhusiwi wala si mila yetu. Basi ukitoka kwenu ukisema umeteswa kwa kuwa wewe msenge, ah unakaribishwa mikono miwili. “Kwani watakucheki?” anauliza mpambe aliyenieleza. “Watakucheki vipi? Watakufungua makalio?”
Basi, ndoto na njozi za kutoka Afrika kwenda Majuu hazikuanza leo. Kitabu kipya cha Mzanzibari Shafi, kitaonyesha harakati hizo miaka ya zamani kabla wengi hatukuzaliwa. “Mbali na Nyumbani” anasema kimeshauliziwa na wachapishaji kadhaa hapa Bongo na Kenya. Pichani chini Adam Shafi akinisomea muswaada.
[Image: shafi-reads-2.jpg?w=500]
Lakini swali niulize. Wangapi wanamfahamu Adam Shafi? Kwa wasomaji wa vitabu vya hadithi na fasihi, jina hili ni la kusisimua na kuvutia. Kwa wapenzi wa lugha yetu tukufu ya Kiswahili huyu ni mjumbe. Walii. Tarishi. Al Watan. Mpiganiaji. Mbunge wa lugha hii. Ndugu msomaji nikupe mfano? Hebu kumbuka Wabongo wangapi wanaodai eti hawana msamiati wa kutosha kujielezea Kiswahili. Utamsikia mtu kasoma, ana shahada, ana ujuzi na utaalam wa hali ya juu akisema : “Ah siwezi kuandika barua kwa Kiswahili…” Ilhali (lakini) anaongea Kiswahili fasaha lakini kuandika anashindwa. Anatumia Kiingereza. Kiingereza chenyewe marea nyingi kibovu. Afadhali hicho Kiingereza kingekuwa kizuri. Msikilize babu na gwiji wa fasihi ya Kiswahili, Ustaadh Shaaban Robert akituasa katika Utenzi wa Adili:
“…Lugha humpa hadhi
Kutumia ajuaye.”
Kisa cha kusema haya yote nini?
Ukitaka kuboresha lugha, ( yeyote ile) soma vitabu. Soma hadithi. Soma mashairi. Kama vile ambavyo wanamuziki hujiendeleza kwa kusikiliza miziki ya aina mbalimbali, msamiati, lahaja na lugha huendelezwa kwa kusoma vitabu. Kwako msomaji unayegomba huwezi kujieleza vizuri kwa Kiswahili, au kuandika Kiswahili…katafute vitabu  vyake Adam Shafi, utafaidika na kustareheka.
Watanzania tunasemwa hatusomi. Baa ziko nyingi kuliko maduka ya vitabu na maktaba. Taifa lenye watu wasiosoma linajichimbia kaburi la ujinga.
[Image: freddy-with-a-shafi.jpg?w=500]
Nikiwa na Shafi, mjini Milton Keynes alipopitia juma lililopita. Picha imepigwa na Hawa Yaxley.
Hebu onja (kidogo) baadhi ya ubingwa wake wa matumizi ya lugha katika nukuu zifuatazo (hapa ni vitabu viwili tu):
“Alihisi Shihab alikuwa kama aliyemtupia mshipi akaumeza pamoja na ndoana, chambo na chubwi.” (Vuta Nkuvute).
“Aziz alitaka kuibusu midomo ya Khadija. Amemwinamia, uso umembadilika, uchu wa mwanamke umemtawala akili zake zimehama kutoka kichwa cha juu zimehamia kichwa cha chini. Alipotaka kumbusu Khadija alimtemea mate yakamtapakaa uso mzima. Alimwachia mkono mmoja ili ajipanguse yale mate,  Khadija akaukamata mkono wake akaung’ata, Aziz akasikia maumivu makali yakipanda mpaka utosini.” (Haini).
“Midomo aliitafuna tafuna nakuimungunyua mungunyua kama mtafuna tambuu…” (Vuta Nkuvute).
“Tokea siku ile aliposokomekwa ndani mle, furaha kwake ilikuwa adimu na huzidi kugubikwa na majonzi pale anapowaza kwamba kosa alilolifanya ni kule kuchinja jogoo lake mwenyewe…” (Haini)
“Amle Mbiza, amle Mboza? Aliwaona kama wote wawili wamemsimamia mbele ya macho yake, achague mmoja. Huyu mmoja keshaolewa, mke wa watu, amemfungia safari kutoka Mombasa mpaka Unguja. Akimwoa kitakuwa chuo chake cha pili. Huyu mwingine bado mbichi, mwari, bikira, atakapomwoa itabidi arusi aijibishe mwenyewe. Arusi ijibu; yeye ajithibitishe urijali wake na mwenzake athibitishe ubikira wake.” (Vuta Nkuvute).
Je unataka kuwasiliana naye Shafi? Mwandikie barua pepe: ashafi40@yahoo.com
CHANZO>>>>
]]>
[Image: adam-shafi.jpg?w=500]

<![CDATA[MAISHA YA SHAABAN ROBERT NA MAWAZO YAKE (M.A. Maganga) – 1]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1398 Wed, 27 Oct 2021 03:49:55 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1398
Makala haya yamegawika sehemu
mbili. Sehemu ya kwanza inachungua mawazo ya Shaaban Robert aliyoyatoa katika
vitabu vyake viwili: Adili na Nduguze
na Wasifu wa Siti Binti Saad. Sehemu ya
pili yatumia mawazo hayo kupimia vitendo na maisha ya Shaaban kama
alivyotueleza yeye mwenyewe katika vitabu viwili vingine vilivyokusanywa
pamoja: Maisha Yangu na Baada ya Miaka
Hamsini.
Nionavyo mimi, Shaaban Robert
amechukua nafasi ya kuandika vitabu vyake hivi viwili vya mwanzo ili aweze
kutoa mawazo na maoni yake kuhusu mambo mabaya na mazuri, yapi ya kufuata na
yapi ya kuepuka katika dunia yenye maisha mbalimbali. Baada ya kuvisoma vitabu
hivyo kwa makini, nimekatikiwa kuwa Shaaban alikuwa na mawazo yasiyo tafauti na
siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Amefikiria kuishi kwa ujamaa katika kitabu
chake cha Adili na Nduguze na katika Wasifu wa Siti Binti Saad ametoa mawazo
yake kuhusu maisha ya kujitegemea; na bila shaka ana lengo halisi katika kutoa
mawazo hayo. Pengine alipenda kueleza na kufafanua, au kupanua zaidi, yasemwayo
katika Injili Takatifu, yaani ‘umpende jirani yako kama nafsi yako’, na mapenzi
hayo ndiyo msingi wa wema, matendo safi, na juhudi ya kazi ziletazo faida kwa
watu wote.
Kwa kuwa vitabu viwili hivi
vimetumiwa kama vyombo vya kuelezea aina mbili za mawazo na maoni ya mtungaji,
naona ni vema nisivichanganye katika uchambuzi huu bali nivichukue kimoja
kimoja. Ebu nianze na kile kilichotangulia kutoka. Kimoja kilitoka mara ya
kwanza katika jarida la 1958 (Nambari 28/1) la Kamati ya Kiswahili ya Afrika
Mashariki, na kingine kilitoka mara ya kwanza kama kitabu kamili mnamo 1952,
nacho ni Adili na Ndiguze ambacho
ndicho tutakachoanzia.
Nimesema kwamba mawazo ya Shaaban
Robert yana lengo au kiini fulani. Katika Adili
na Nduguze lengo lake ni upendo, yaani watu wapendane na kuishi kiujamaa-na
upendo huo ndio alioufungulia kitabu chenyewe alipoandika mwanzoni:
‘Kwa marafiki zangu
Wazawa wa Afrika
Pamoja na Wazungu
Wapendao afrika’.
Shaaban Robert amekianza kitabu
chake kwa maelezo juu ya Mfalme Rai. Mawazo yenyewe, nionavyo mimi, ni sawa nay
ale yasemwayo na Azimio la Arusha kwamba, ili kuleta mafanikio na maendeleo ya
nchi, vihitajiwavyo ni ardhi, watu, uongozi bora na siasa safi.
Kiini cha kumuanzia Rain i kutaka
kueleza kwamba, hata kama ardhi na watu wapo, jambo la kwanza linalotakiwa ni
uongozi bora wenye msingi ufananao na tabia ya Rai. Pengine ardhi na watu wa
Ughaibuni walifanikiwa na kuendelea kwa sababu ya uongozi mzuri wa Rai. Mawazo ya
Shaaban ni kuwa uongozi mzuri wa nchi ni kama ule wa Rai ambao kiini chake
kilikuwa upendo. Alikuwa na mapenzi na wanaadamu, nao wakampenda;alifuata
msingi wa kidini wa zamani ambapo Daudi aliwapenda wanyama na Sulemani akatiiwa
na majini.
Mawazo ya Shaaban juu ya kiongozi
bora wa nchi yoyote yameelezwa katika wasifu wa Rai, ukurasa wa pili. Hapo uongozi
bora unaonekana unahitajia uadilifu, wema, kufanya kazi ndogo na kubwa au kutoa
amri zifanywe, kusaidia na kushiriki katika maendeleo ya nchi, kutolazimisha
watu mambo bali kuwashawishi tu (kama uhitajivyo ujamaa wa kweli), kuvuta mioyo
ya watu ili kusiwe na wavivu, magoigoi wala waoga.
Kwa namna hii Shaaban Robert atoa
mawazo kwamba viumbe wote wangefurahia sifa ya kiongozi wa namna hiyo-tangu
malaika mbinguni hadi ndege angani, watu duniani, samaki majini, na hata majini
na mashetani popote pale wafikiriwapo wapo. Upendo na ujamaa wa kweli ni
kufanya urafiki na viumbe mbalimbali pamoja na kuwajali watu wote. Baada ya
upendo ni matendo. Na hapa ndipo Shaaban aliposema: ‘Tendo hukidhi haja
maridhawa kuliko neno.’ Yaani, tendo huleta haja upesi lakini neno huichelesha;
na neno tu si njia ya kuleta mapinduzi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Katika kuhukumu mwandishi
aonekane ana machache ya kueleza. Itolewapo hukumu inatakikana kiongozi awe
imara, asipendelee bali watu wote wawe sawa mbele ya sheria. Hiyo ndiyo
demokrasi halisi-demokrasia ya kiujamaa. Uongozi bora ni ule ufuatao haki ya
watu na wanyama pia, na ule ufanyao uchunguzi wa matukio yote-mazuri na
mabaya-kwa raia. Na, katika uchunguzi wa Rai kuhusu kasoro iliyotokea Janibu,
ndimo Shaaban Robert anamoeleza mawazo yake kuhusu tabaka kwa tabaka za maisha
ya kiujamaa nay ale yasiyo ya kiujamaa. Na juu ya huo uchunguzi Shaaban
anasema, ‘Mambo katika maisha yambo katika mwnedo huu siku zote. Hayajulikani mpaka
yamechunguzwa na kuthibitishwa kwanza.’ Kiongozi bora kama Rai huwa mtu arifu
wa mwendo huu!
Tunaambiwa vile vile kuwa si
kiongozi tu atakikanaye kuwa mtu wa kufaa bali watu wote walio na wajibu na
mamlaka chini yake, kama vile Rai alivyokuwa na Maarifa (Waziri Mkuu) na
Ikibali (Mshauri). Na kazi lazima ipokezanwe kwani kiongozi hawezi kufanya kazi
zote peke yake. Juu ya Ikibali, ambaye alikuwa na wajibu wa kwenda Janibu
kuchungua mambo ya kodi, tunayaona mawazo mengi ya mwandishi kuhusu njia nzuri
ya mtu kuiweza kazi yake kwa urahisi. Zaidi ya kuwa na maarifa mengi, kuchuana
na watu kwahitaji tabia njema ambayo
ndiyo inayomkamilisha mtu. Tabia njema kwa viongozi wa nchi ndiyo alama ya ‘jembe’
au ‘nyumba’ ambayo Shaaban anataka watu waiangalie wanapoteua viongozi wao, na
ndiyo sifa inayowapa watu kuwaamini na kuwapenda.
Sura ya kwanza ni fupi; lakini
mwandishi ameitumia kutolea mawazo mengi kuhusu uongozi bora wa watu na utumiaji
bora wa ardhi, kuhusu raia, serikali, mawaziri, siasa safi na mifano bora ya
viongozi. Sehemu yote iliyosalia-na ni kubwa-anaitumia kutolea mawazo yake
kuhusu umma na jinsi ya kuishi kwa mapenzi na ujamaa. Na sura zote kumi na nne
zifuatazo, hadi kufikia mwisho, ni maoni juu ya ‘machimbo na hazina zake’, ‘biashara
na faida yake’, ‘safari na manufaa yake’, ‘utajiri na Baraka yake’, ‘hali na
heshima yake’ na juu ya ndugu, watu, jamaa na matendo yao-mambo yahsuyo dunia
nzima. Kwanza kabisa amekwisha kutoa maoni yake kuhusu ardhi na mimea yake na
mifugo na mazao yake, kwamba ni hazina za urithi wa watu wote. Hebu basi
tuangalie ni nini awazacho mtungaji huyu juu ya ujamaa na upendo kati ya watu.
Katika sura ya pili, mwandishi
anatoa maoni yake kuhusu mgeni Ikibali aliyekuwa na hulka ya kuwapendeza watu
waliokutana naye na ambaye usoni aling’aa kwa kicheko; na aliyekuwa na fadhila
na shukrani. Katika kwenda kwake Janibu, Ikibali anakutana na Adili, Liwali wa
mji huo ambaye mtungaji anamtumia kuelezea mawazo yake kuhusu namna nzuri na
mbaya ya kuishi na ndugu na watu mbalimbali. Ikibali alipotaka kurudi
Ughaibuni, Adili alimwomba akae Janibu kwa muda wa siku tatu zaidi ili wazidi
kutafaraji pamoja. Ikibali akakubali, kwani ‘waungwana hawanyimani neno’. Kwa hiyo
tunaona vile vile kuwa penye upendo pana kujitolea na subira pia.
Twafahamu kwamba subira mara
nyingi huvuta heri, basi Ikibali naye katika kusubiri kwake alivuna heri-na heri
yenyewe ilikuwa ni kule kuona kuwa kuna kitu fulani kibaya ambacho ilimlazimu
Adili kukitenda bila furaha. Juu ya habari hii ya Adili, Shaaban
anatutanabahisha tusimchukulie mtu kwa hali yake ya nje tu, tukafikiri yakuwa
mtu kama Adili-Liwali mzima-ati hana jambo linalomuondolea furaha. Mtu kama
huyo, tunapogundua ana tatizo, inafaa tumsaidie-si katika mambo ya kikazi tu
bali hata mambo yake mwenyewe binafsi. Hii ndiyo sababu Ikibali akaazimia
kumsaidia mwenziwe ingawa hilo jambo la kusaidiwa lilikuwa ni la siri: siri ambayo
ilibidi ifichuliwe ili msaada upatikane. Ndipo Ikibali akaitoboa siri hiyo, ya
Adili na manyani wake, na baadaye akenda naye mbele ya Rai, si kwa ajili ya
kumuaibisha bali kumfanya Rai ayasikilize maelezo ambayo huenda yakawa ndio
ufunguo wa furaha. ‘Aonae kosa akitoa hana lawama’, ndivyo asemavyo mwandishi. Na
kusaidiana ni dalili ya upendo nan i ujamaa.
Katika sura ya tatu, mawazo ya
mwandishi ni kuwa vitendo ni mapinduzi. Tunaambiwa kwamba busara nyingi humjia
mtu baada ya jambo kufanyika. Hivyo, Adili hakumkasirikia Ikibali kwa kumtolea
siri yake kwa Rai. Inaonekana kwamba wazo la mtungaji ni kusema kuwa itukiapo
ajabu, au jambo la kushangaza, huenda kukawa na sababu maalumu na kwamba, jambo
lenyewe likichunguzwa, huenda sababu yenyewe ikaonekana. Ajabu ya wale manyani
waliopanda farasi na kumfanyia mfalme ishara inapochunguliwa ndipo sababu yake
inapofahamika. Katika kusikiliza shauri la Adili na manyani kuna wazo kwamba ‘waungwana
hawasemi uongo’. Kwa hivyo ingawa Adili ameshtakiwa kwamba anawatesa manyani,
tunaona anawageukia manyani wale wale na kuwataka wayathibitishe ayasemayo.
Kuhusu malezi ya Hasidi, Mwivu na
Adili, mtungaji atoa wazo kwamba kumlea mtoto ni kumtunza mwili, kumfundisha
mawaidha na kuzipanua fikra zake, na zaidi ya yote ni kumfundisha ‘wema’ wa
moyoni. Moyo ndio makao ya upendo ambao ndio msingi wa ujamaa.
Kuhusu madeni inaonekana kwamba,
ili kutengeneza maisha ya upendo na kujitegemea, kukopa si jambo zuri na
kwamba, kama imekuwa lazima kulipa kabla ya kudaiwa. Na yule anayekukopesha
naye asiwe na lazima ya kudai kwa kero au inda.
Shaaban anamtumia Adili kueleza
kuwa, ingawa yeye alikuwa kitinda mimba, aliweza kuwa na busara na subira zaidi
ya wakubwaze. Busara yake ilimfanya afaulu katika biashara kwani aliweka
daftari ya mapato, kwa hivyo mali yake haikupotea bila ya kuelewa vile
ilivyopotea. Wazo la mtungaji ni kuwa biashara au shamba lahitaji mpango ambao
usipokuwepo patapatikana hasara. Kwa kuwa ndugu zake Adili hawakuwa na mpango
walifilisika baada ya mwaka mmoja tu. Na hivi ndivyo watu wengi duniani
wafanyavyo: hupata mali wakafanyia pupa kwa kutaka kuchuma zaidi bila mpango,
mara wakapata hasara. Lakini mtu kuvumilia na kusamehe ndugu zake ndilo jambo
linalohitajia, na hapa mtungaji anazidisha sana wazo lake la ukarimu. Kwa ajili
ya upendo, Adili aliwagawia tena mali nduguze ili wafanye tena biashara na
wajitegemee, wasimnyonye. Katika safari waliyoifanya wote watatu, Shaaban
anachukua nafasi ya kueleza faida za safari kwa kusema kuwa safari huleta ‘kufarijika
kkatika hamu, kujua namna ya kuendesha maisha, kupata elimu mpya, kuelewa tabia
za watu mbalimbali, kukutana na marafiki wa kweli kushinda ndugu, na mtu mwenye
bahati mbaya kwao huweza kupata bahati njema ugenini.’
Katika sura ya sita mwandishi
aeleza tena kwamba upendo ndiyo jambo muhimu duniani, kwani Adili ‘aliwapenda
ndugu zake kama pumzi ya maisha yake mwenyewe’. Pendo huleta huruma, na huruma
hii ndiyo iliyomwezesha Adili kumwokoa yule tandu aliyetaka kuangamizwa na
nyoka. Jambo la kukumbuka hapa ni kwamba jema hulipwa na jema. Yule tandu,
ambaye alijigeuza msichana, aliahidi kumlipa wema Adili na akamwombea dua
njema. Sura hii inaonesha kwamba ujasiri unatakiwa sana katika kufanya mambo
yaonekanayo kuwa magumu. Kwa ujasiri wake, Adili alipata maji, na safari ya
pili akajitolea peke yake kwenda mji wa Mawe kutafuta tena maji ya kunywa.
Sura ya saba haina mawazo mengi
ya mtungaji ila kusema kwamba duniani kuna mali nyingi lakini ni vigumu mtu
kuipata ikiwa amejificha. Watakaoipata ni wale wajasiri tu wenye nia ya
kuipata. Sura ifuatayo yasema hivyo hivyo: bahati ya turufu humwendea mchezaji,
na ndivyo ilivyokuwa bahati ya Adili, hata sasa akawa na bahati ya kukaribishwa
humo mjini na msichana mrembo.
Mawazo ya uongozi bora yarudiwa
tena katika sura ya tisa. Katika ukurasa wa 35, tunaelezwa jinsi kiongozi
ahitajiwavyo kuwa katika maingiliano yake na watu na vile vile na dini ya kweli
ya Mungu. Mrefu alimwangamiza Mfalme Tukufu na enzi yake yote (ila bintiye,
Mwelekevu) kwa sababu kiongozi huyo alimdharau Mungu akawa anaamini mizimu na
uimamu wa Kabwere. Rehema za Mungu huwafikia wanaomtii, na hivi ndivyo
Mwelekevu alivyojaaliwa kukipata kile kitabu kitakatifu pamoja na ule
mkomamanga. Mizimu na kutomjali Mungu ni kinyume cha ustawi wa moyo.
Maelezo yafuatayo yanahusu wivu. Mtungaji
anatwambia kwa njia hii hii ya hadithi kuwa wivu haufai. Mwenye kupata kitu kwa
jasho lake aachwe kufurahia mapato yake. Katika ukurasa wa 40, mtungaji
anahubiri juu ya mambo machafu na hila mbovu kama za wale ndugu zake Adili
ambao kila mmoja wao aling’ang’ania kutaka kumwoa Mwelekevu na baadaye
wakaonelea kuwa yule binti awe mke wa wote-jambo ambalo ni chafu sana. Na hapo
ndipo atoapo mawazo yake kuhusu ndoa yenye msingi kamili, kuwa ndoa si jambo la
watu wote; ni la watu wawili tu-mume na mke. ‘Mwanamume hakukusudiwa kuwa
fahali wa kila mtamba, wala mwanamke kuwatembe wa kila jogoo’. Mafanikio ya
Adili yaliwakata maini nduguze, kwa hivyo maoni ya Shaaban hapa ni kwamba watu
wafanikiwao ni lazima wawe macho, watahadhari na kijicho wanachoonewa, kwani si
watu wote wapendao au wanaofurahia mafanikio yao. Tena nduguze Adili, waliokuwa
hawapendi Adili, wakamtosa majini kwa wivu. Tunaoneshwa kuwa, kwa upande
mwingine, pendo likitoka upande mmoja tu katika maisha ya ujamaa basi huwa
halina msingi imara, na maisha yake huwa si marefu. Pendo lazima litoke pande
zote mbili sawa kwa sawa.
Adili alitoswa majini lakini ile
dua ya msichana-tandu ikamuokoa. Mtenda mema mara ntingi hulipwa mema, na
mtenda mabaya naye pia hupata kadiri ya ule ubaya wake. Basi Adili akapata mali
zaidi, na nduguze walio na wivu wakaadhibiwa wakageuzwa manyani na kupigwa
mijeledi kila siku.
Sura ya kumi na nne na ya mwisho
zaonesha mambo mawili hasa: wajibu wa kiongozi kuwaangalia wafuasi wake kwa
shida zao-kama vile Rai alivyojishughulisha kumpatia Adili ushahidi kutoka kwa
babake Huria, Kisasi-na mafundisho kuhusu hali ya binadamu na vitendo vyake. Mawazo
haya ya Shaaban yasemwa na Rai kuwaambia nduguze Adili: ‘Weavivu walijitahidi
kuwa hodari, ilikuwa kinyume hodari kuwa wavivu; kama waovu walitaka kuwa wema,
ilichukiza wema kuwa waovu; kama maskini walitafuta utajiri, ilikuwa ujinga
matajiri kufuja walichokuwa nacho; kama mbegu kidogo iliongezwa mchanga,
ilikuwa uharabu mtu kuua ndugu yake; pia ilikuwa aibu kubwa sana kwa wazuri
kutenda maovu.’
Kwa hiyo, ni dhahiri yakuwa
katika Adili na Nduguze Shaaban
afundisha watu waishi kwa kupendana chini ya uongozi bora, na wajisaidie
kiujamaa badala ya kujiangamiza na kuoneana wivu ambao hauna faida-si kwa hao
wenye wivu tu, bali kwa nchi nzima. Vile vile anawaambia wale wenye busara na
werevu kwamba dunia ni kubwa na imejaa mali na vitu vizuri ambavyo vitakuwa ni
vya kila avitoleaye jasho na mwenye wema moyoni na akili kichwani.
Wasifu wa Siti Binti Saad zaidi unaonesha pendo kuliko ujamaa,
lakini kiini chake ni ‘kujitegemea’. Kama Bwana Waziri Juma asemavyo katika
dibaji ya kitabu hicho (uk. vii), ni sawa kama mwandishi awatia moyo wasichana
na wanawake wengi wa Kiafrika wanaojibidiisha kwa shughuli mbalimbali kwa ajili
ya maisha yao.
Shaaban Robert ana nia ya kueleza
kwamba ni lazima mtu ajitegemee kwanza ndipo atakapofanikiwa kupata yale
ayatakayo. kule kuwa mwanamke, au kutosoma, au kutokuwa na fedha, au kutozaliwa
na kukaa mjini, au kutokuwa na sura nzuri, hayo yote si kitu kwani kujiamini,
kuwa na nia, na kuwa na subira na juhudi kunaweza kuleta mafanikio mengine
makubwa yasiyoweza kufikiriwa hata kidogo hapo mwanzoni. karibu kitabu chote
kinazungumza habari za mtu mmoja tu, na hakisemi mengi juu ya watu wengine ila
kuonesha tu yakuwa wapo wengine waliomuonea wivu Siti wakastahili kupewa jibu
la kuwatia vidaka vya midomo. kwa hivyo inaonekana kwamba maelezo yaliyomo humu
ni kama safari ya barabara moja yenye vipingamizi, na mtungaji anaonesha vile
msafiri mmoja anavyoendelea na safari yenyewe. na hata huyu msafiri mwenyewe, Siti,
ametumiwa na mtungaji ili awe mfano kwa wanawake wengine wanaojidharau na kuona
kwamba hakuna lolote hapa duniani wawezalo kulifanya. Lakini hivyo sivyo;
ulimwenguni ni mpana.
Shaaban Robert anataka kuonesha
kuwa katikati ya vizuizi mtu anaweza kusimama na kufanya kazi kwa bidii hata
akajipatia sifa. Siti hakuwa na bahati njema ya kuviepuka ‘vipingamizi’ vile vilivyotajwa
hapo juu (kutokuwa na sura nzuri na kadhalika), lakini vivyo alianza safari
yake katika maisha. alijua kuwa wazazi wake ni maskini, kwa hivyo aliendelea na
biashara yao ya kuuza vyungu. hakuna mtu aliyepata vyote au aliyekosa vyote. Mtumwa-jina
la Siti la hapo mwanzo-alikosa sura nzuri, lakini alifadhiliwa sauti ya kuvutia
kweli kweli. Fimbo iliyo mkononi ndiyo iuayo nyoka; kwa hivyo Siti aliifanya
sauti yake ndiyo fimbo yake, na akaitumia vilivyo. Hapa Shaaban anachukua
nafasi ya kutueleza kuwa sura nzuri si kitu cha kukiangalia sana maishani mara
kwa mara, wala si kizima kiu cha mapenzi. Mawazo yake ni kuwa inambidi mtu aikubali
hali yake kwanza, kisha ndipo atakapoweza kuona ni wapi anapofaa ili aweze
kufanya jambo atakalo kwa kadiri ya uwezo wake. na haya yote yawezekana, si ya
ajabu.
Lakini, katika kukata shauri juu
ya jambo la kutekeleza, mtu mara nyingi humbidi kuyatoa mhanga mambo yake
fulani aliyokuwa nayo kama vile Siti ilivyombidi kukiacha kijiji chao Fumba,
mumewe, mtoto wake na maisha ya utulivu yasiyo na ghasia, akakata shauri
kukidhihirisha kipawa chake kwa kuimba katika taarab mjini Unguja. Alihitajia
sana subira, juhudi, kujiamini na kujitegemea katika maisha mapya ya mjini
yaliyokuwa na vipingamizi vingi. kimojawapo cha vipingamizi hivyo kilikuwa ni
kushindwa kuimba siku ya kwanza alipotokea hadharani. Alikuwa hajazoea. Lakini
baadaye alifaulu kwani ‘alishikilia kazi yake kwa bidii’, akawa na dhamira na
nia ya kufaulu.
Kipawa bila ya ujasiri, dhamira
na nia ni bure tu. Maisha ya mjini ni magumu na hasa kwa mwanamke ambaye ni
mgeni tena ni mtu mzima ambaye hapo alipokuwapo hakuwa na mume. Lakini Siti
hakuwa muhuni. Aliweza kukaa imara kwani alikwenda mjini kwa kusudi maalumu; na
palimfaa kwalo. Hakwenda mjini kutafuta fedha, kwani tunaambiwa yakuwa Siti
hakupenda fedha, lakini kazi yake ilikusudiwa kumletea sifa na umaarufu. Hakuwa
mnyang’anya watu fedha kwa sababu ‘alikuwa mcha Mungu wa sala na saumu. Alisali
vipindi vitano kila siku, akafunga faradhi na suna katika maisha yake yote’.
Maoni ya mwandishi hapa ni kuwa mtu awe wa ibada saa za ibada, na mlimwengu
wakati wa mambo ya kilimwengu.
Pia inaonekana mwandishi
anafikiri kwamba Siti alifanikiwa kwa sababu ya ukarimu wake na Baraka kuliko
kuwa ni kwa sababu ya masharti ya mikataba na mapatano katika kazi yake.
Mafanikio, kwa wale wajuao wayafanyayo ni kama moto wa mbugani. Mara watu
wakawa wanamfuatafuata Siti, watribu wakamzunguka kwa vinanda ili awaimbie,
wapiga picha na wapiga chapa nao wakamwendea, watu wa santuri pia wakawa
wanamfuata, na kwa njia hii sifa za mwanamke huyu zikatapakaa hata nje ya Afrika
Mashariki. Mafanikio mengi ya Siti, asema Shaaban, ni kwa sababu alikuwa
mtanashati, hana majivuno, mwenye adabu na mlahaka kwa watu wote.
Ni kweli kabisa kwamba ‘jina
kubwa lolote halipatikani duniani bila vizuizi kadha wa kadha’ kwa maana kuna
mfano wa Siti ambaye, mara tu alipoanza kupata sifa kwa kuimba, watu walianza
kumwonea wivu na kumdharau na hata kumtukana. Kuhusu mambo haya yote, maoni ya
mwandishi ni haya: mtu lazima awe na subira, bidii na uvumilivu katika kazi
yake; aende mbele bila ya kuangalia nyuma.
Safari ya Siti katika maisha
ilifanikiwa kwa ramani ya maneno. Mwenye busara hujiwekea maneno ya kumwongoza.
Katika kuwajibu waliokuwa wakimtia ila na kumtukana, Siti alisema:
Si hoja uzuri, na sura jamali
Kuwa mtukufu, na jadi kubeli
Hasara ya mtu, kukosa akili

Huu ndio wimbo uliowakomesha
wapinzani wake. Na yaonesha kwamba mtu yambidi kujitetea anaposhambuliwa na
binadamu wenziwe, lakini si kujitetea kishenzi kama mnyama wa porini.
Kama kawaida, mwandishi
anajiuliza kwa nini Siti alifanikiwa hivyo? Maoni yake ni kwamba, kwanza, Siti
alifahamu sana tabia za watu, alikuwa na adabu na alijua kuchukuana nao (wazo
lililomo katika kitabu cha Adili na
Nduguze pia); na pili aliwapenda sana wasikilizaji wake. Hapa upendo
waonekana kuwa ndio msingi wa mafanikio. Hata hivyo, Siti hakujisifu mwenyewe.
Baada ya kueleza kwamba Siti
alizidi kusonga mbele, na kuviruka vipingamizi vingi, mwandishi anatoa mawazo
yake kwamba hayo hayakuwa mambo ya ajabu; matendo yake yanaweza kuigwa. Siti
alikuwa ni mtu kama watu wengine. Katika ukurasa wa 49 yapo mawazo mazuri ya
Shaaban yanayosema:
‘Fikiri kama na wewe umepata
kutenda neno lolote la fadhili kwa watu au nchi yako. Kama hujalifanya bado,
lifanye sasa. Yamkini una marafiki. Wafurahishe kwa fadhili yoyote uwezayo
kutenda. Haikosi una washindani. Wape sababu ya kukuajabia kwa unyofu ulio nao….Maisha
yalikuwa matendo, sio usingizi’.
Tangu mwanzo mpaka mwisho wa sura
ya nane Shaaban ameacha kutuzungumzia mtu wake. Hapa anasimama na kutoa mawazo
yake juu ya jambo moja muhimu sana kwa wanaadamu. Nalo ni tabia njema. Anasema
tabia njema imo katika ukweli na mapenzi ya moyoni. Tabia njema haifuati elimu,
wala utajiri, wala kuwa na cheo. ‘Tabia ilikuwa kama njia panda kuu katika
maisha yaliyogawa watu kwenda pande mbalimbali za dunia.’ Watu hutengana kadiri
ya tabia. Hata Mungu anawagawa watu kwa kufuata tabia zao. Ni vizuri kuwa na
tabia nzuri ambayo Shaaban Robert anafikiri ina amani na upole, saburi na
unyenyekevu, uungwana na uaminifu kwa watu wote-hiyo ni johari. Mwandishi
anahubiri juu ya tabia njema itakiwayo, akitoa mfano wa Siti, na anamalizia
kitabu chake vizuri sana kwa kutaja waziwazi kiini hasa cha mawazo na maoni
yake juu ya maisha.
Kama nilivyosema hapo awali,
Shaaban Robert katika Wasifu wa Siti
Binti Saad anaonesha jinsi mtu, hata akiwa katika hali ya chini, awezavyo
kujitahidi hadi akaweza kustawi na kujitegemea. Sura ya mwisho inatilia mkazo
neno kuu la kitabu hiki, ‘kujitegemea’. ‘Kujikimu ni kujiruzuku. Kujiruzuku ni kujitegemea kwa chakula, nguo na
masurufu mengine katika maisha.’ Na hapa ndipo tutakapokomea kutoa mawazo ya
mtungaji wa kitabu hiki.
 
Baada ya kuhakiki Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad, na pia nikiyapima mawazo ya marehemu
Shaaban Robert katika fasihi zake nyingine kama mashairi yake Masomo Yenye Adili, Kusadikika, na Kufikirika, naona vigumu sana kuuepa
ukweli kwamba marehemu aliandika vitabu vyake kwa nia ya kufundisha watu;
alitoa fasihi yake iwe kioo cha watu kujiangalia ili waone jinsi wanavyoishi na
wanavyotaka kusihi, na vile vile waone jinsi ambavyo yeye mwenyewe Shaaban
Robert angependelea watu waishi. Kwa sababu hii, maandishi yake yote yanang’aa
kwa ilani isemayo, ‘Maisha ya mtu ni msingi wa maendeleo ya nchi.’ Maneno haya
ndiyo ufunguo uliomo mwanzoni kabisa mwa Maisha
Yangu na Baada ya Miaka Hamsini-kitabu ambacho kwacho Shaaban ametueleza na
kutuonesha sehemu ya maisha yake. 

<![CDATA[Waandishi wa zama zetu na dhana ya ‘kuiafrikanisha’ fasihi ya Afrika]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1389 Tue, 26 Oct 2021 03:26:34 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1389 Boris Boubacar Diop ana msimamo kuwa: “huwezi kuwa wa kimataifa kama huna uthubutu wa kuwa wa kwenu”, lakini Patrick Mudekereza anasema katika maeneo mengi barani Afrika ukweli ni kuwa waandishi wanafikiri kwa lugha za kigeni kukiwemo kwao, Kongo, na Nuruddin Farahanasema kilichomfanya kuelekea kwenye uandishi wa Kiingereza ni kuwa lugha yake ya Kisomali haikuwa na hati za maandishi yake yenyewe.
Wote hawa ni waandishi mashuhuri wa fasihi ya Kiafrika, ambao wameandika sehemu kubwa ya kazi zao kwa kutumia lugha za kigeni, hasa Kifaransa na Kiingereza, jambo ambalo bado – kwa wengi – ni dalili ya doa kwenye utukufu wa bara la Afrika, ambalo lina lugha zake lenyewe zinazokisiwa kufikia 2000.
Lakini je, kuna haja ya ‘kuiafrikanisha’ fasihi ya Kiafrika, kwa maana ya kusimulia na kuandika kazi za kifasihi kwa kutumia lugha halisi za Kiafrika? Na, hata pale panapoonekana haja hiyo, je upo uwezekano wa kufanya hivyo katika ulimwengu huu unaoitwa wa utandawazi, ambapo lugha zinazoitwa za kimataifa zinajilazimisha zenyewe kuwa ndizo nyenzo za maisha ya  walimwengu wote? Kwani matumizi ya lugha za kigeni kusimulia hekaya za Kiafrika zinamtenga mwandishi mbali na hadhira yake?
[/url]
[Image: dsc0816.jpg?w=840&h=559]
Mwandishi wa fasihi wa Senegal, Boris Boubacar Diop.
Ndiyo maswali niliyokuwa nayo kichwani wakati nikihudhuria kongamano la shirika la Wakfu wa Kwaninchini Kenya mwanzoni mwa mwezi Disemba 2015, ambako fursa ilinikutanisha na wanafasihi bingwa kutoka kote barani Afrika.
“Nchini kwangu Kongo, wakati najifunza, nilijifunza kwa Kifaransa, na hakuna namna ambapo Kiswahili kinaweza kikashika kwenye fikra zetu, bali kinabakia kuwa cha mazungumzo ya kawaida tu. Ile lugha ya kufikiri hasa, bado ingali Kifaransa,” aliniambia Patrick, ambaye ingawa chuoni alisomea kemia, mwenyewe ni msanii, mwandishi na mpigapicha, akiwa anajishughulisha na kazi za kisanii na kifasihi tangu utotoni mwake. Pia ni mhariri wa jarida la masuala ya utamaduni liitwalo Nzenze.
Hoja hii ya kuwepo kwa mafungamano makubwa sana baina ya uwasilishwaji wa fasihi ya Kiafrika na lugha za kigeni, ndiyo pia hoja ya Boubacar Diop, mwandishi mashuhuri wa riwaya kwenye mataifa yanayozungumza Kifaransa. Lakini yeye anakwenda mbali zaidi na kuhusisha ukweli huo na historia ya ukoloni barani Afrika.
“Kwa watu wengi, huwezi kuzungumzia fasihi ya Kiafrika ikiwa huzungumzii uzoefu wetu wa kikoloni. Kuna uhusiano kati ya uzoefu huo na kwamba tunaandika riwaya, tathmilia na ushairi.”
Ukweli wa Kihistoria?
Ukweli huu wa kihistoria, ungawa mchungu kama ulivyo, ndio unaoiandama fasihi ya Kiafrika. Kwa hakika, kwa kuwa ndani ya kazi za kifasihi kama vile riwaya, tamthilia na ushairi ndimo munapopatikana mawazo na maono ya kimaisha kwa wasomaji wake, ambao wengi ni vijana, basi matokeo yake huakisika kwenye maisha, hata kwa mambo ya ndani kabisa, kama vile hisia za kimapenzi.

[Image: dsc0732.jpg?w=840&h=559]
Msanii Patrick Mudekereza kutoka Lubumbashi.
Katika riwaya ya Nyota ya Rehema, kwa mfano, mwandishi anasimulia jinsi muhisika wake Karim alivyokuwa akiamini kuwa mapenzi kwa mkewe yanakuwa na ladha tamu sana pale anapotumia Kiingereza kumuita [i]“my wife”[/i] badala ya mke wangu, ama [i]“my darling”[/i] badala ya mpenzi wangu. Na hii ni alama kubwa ya historia ya ukoloni ndani ya fasihi na hivyo hata damu yetu, kama anavyosema David Caeser, mshairi na mhakiki wa kazi za fasihi nchini Uganda.
“Ni mchakato wa historia, na ni tatizo la historia, kwamba tayari tunaishi kwenye dunia hii mpya ya kikoloni, ambamo wenyewe tunazidi kuwa watu wa wapya. Mimi napenda kuandika kwa Kiingereza kwa sababu najiona kuwa naijuwa lugha hii, lakini huandiki kwa kuwa tu unafurahia kuyapanga maneno, bali kwa kuwa unataka kuwasiliana kuhusu kitu fulani, lakini ninagundua kuwa ninachokiandika kikiwa kitu kigeni kwa watu.”
Hata hivyo, watetezi wa kutumia lugha za kigeni katika kazi za kifasihi za Afrika wana hoja zao. Mojawapo ni kwamba Afrika, bara lenye wakaazi wapatao bilioni moja na milioni mia mbili, lina lugha zaidi ya 2000, na wakati mwengine ndani ya taifa moja muna, kama ilivyo Tanzania kwa mfano, muna lugha zaidi ya 100. Hivyo ni shida kuwaunganisha watu hawa wenye lugha nyingi kwa lugha zao, hivyo lugha ya kigeni inapotumika kusimulia fasihi yao ni sahihi.
Boubacar Diop, ambaye mbali ya kuwa mwanafasihi pia ni mwanahabari akiwa mwanzilishi wa gazeti huru nchini kwake liitwalo Sol, anasema hoja hii inapingana na fahari ya Afrika kuwa bara kongwe, kwani “unaposema kuwa fasihi kwenye nchi za Kiafrika zinazozungumza Kifaransa kwa mfano ilianza 1926 kwa kazi kama za Bakari Diallou, unamaanisha kuwa tulikuwa kimya kwa mamilioni ya miaka, nami naamini hilo si jambo linaoingia akilini.”
Uhalali wa kutumia lugha za kigeni?
Kuna sababu nyengine pia kukazia hoja ya wale wanaoamini kuwa ni sahihi kwa fasihi ya Kiafrika kuandikwa kwa lugha ya kigeni. Nayo ni kwamba wakati waandishi wa mwanzo mwanzo wa Kiafrika walipoanza kusimulia hekaya ya Kiafrika kwa maandishi, lugha za Kiafrika zilikuwa hazijakuwa na herufi zake zenyewe. Ndio mazingira aliyojikuta, kwa mfano, Nurdin Farah, mwandishi bingwa wa riwaya kutokea Somalia, ambaye amekuwa akiandika kwa lugha ya Kiingereza.

[Image: dsc0951.jpg?w=840&h=559]
Mshairi na mhakiki wa fasihi David Caeser kutoka Uganda.
Katika mazungumzo yake na Binyavyanga Wainaina, bingwa huyu wa fasihi ya Somalia anayezungumza kwa ufasaha lugha nne, anasema hakuweza kuandika kwa Kisomali maana Kisomali hakikuwa na hati za maandishi. “Sikutaka kuandika kwa Kiamhara kwa kuwa tulilelewa tukifahamu kuwa hiyo ni lugha ya adui yetu. Ningeliweza kuandika kwa Kiarabu na kwa kweli niliandika hadithi chache kwa Kiarabu, lakini tatizo lilikuwa mashine ya kuandikia. Nilipoanza kuandika kwa Kitaliano nikakuta tatizo hilo. Ndipo nilipopata mashine ya Kimarekani ambayo ilikuwa madhubuti zaidi, rahisi zaidi na nzuri zaidi na hapo nikasema sasa nitakuwa naandika kwa Kiingereza. Na hiyo ndiyo sababu ya kuanza kuandika kwa Kiingereza.”
Na baada ya kuselelea sana na kwenye Kiingereza, waandishi kama Nurdin Farah hawaoni haja ya kutumia lugha ya Kiafrika kusimulia hekaya ya Kiafrika.
Katika ulimwengu wa Waswahili pia kuna mifano kadhaa ya waandishi kama hao – Abdulrazak Gurnah kutoka Zanzibar na Ngugi wa Thiong’o kutoka Kenya, wakiwa mifano yao. Lakini je, hata kwa mtu aliyeimiliki lugha ya kigeni kwa kiwango kikubwa, bado anaweza hasa kuelezea kila kitu kwa kutumia lugha isiyokuwa ulimi wake wa kuzaliwa nao?
David Caeser amekuwa akiandika kazi zake kwa lugha ya Kiingereza anayoimudu vyema, lakini bado anaamini kuwa ni mateso kwake kuandika kwa lugha hiyo ya kigeni. Anasema huwa anajihisi kama vile amebanwa na jinamizi, maana “ninapoandika kwa Kiingereza kwenyewe ni kama kutafsiri. Ninapoandika kuhusu mahala au watu fulani, kwa mfano, hao hawazungumzi Kiingereza, hawatendi kwa mujibu wa Uingereza, hivyo kwangu kitendo cha kuandika ni kama niko kwenye mchakato wa mateso.”
Kiswahili ni mfano mwema
Hata hivyo, kinapolinganishwa na lugha nyengine za Kiafrika, bado Kiswahili kina bahati ya kuwa na waandishi wengi Waswahili walioandika fasihi ya Kiswahili kwa kutumia Kiswahili – Said Ahmed Mohammed, Mohamed Said Abdullah, Shaaban Robert, Ken Walibora, na orodha inaendelea. Wengi wa waandishi hawa wameandika kazi zao zote takribani kwa lugha ya Kiswahili pekee na zikajizolea sifa kubwa ulimwenguni kote, nyengine zikitafsiriwa kwa lugha za kigeni, kama ilivyo riwaya ya Kuli ya Shafi Adam Shafi.

[Image: nuda-diin.jpg?w=840]
Nuruddin Farah, mwanafasihi wa Kisomali anayetumia Kiingereza.
Hata mwandishi Boubacar Diop ilimchukuwa muda kuamini kuwa anaweza kutoka nje ya lugha ya Kifaransa anayotumia kuandikia kazi zake na kugeukia lugha yake ya kuzaliwa nayo. “Nilipoanza kuandika, kamwe sikuwahi kufikiria kuwa kuna siku nitaweza kuandika riwaya kwa Kiwolof, kwa sababu nilikuwa siwezi. Siwezi tu. Ingawa nilifikiria kuwa ni jambo zuri kufanya, lakini mimi nisingeliweza. Kisha nikaamua kujaribu na nikaweza.”
Hivyo, tunaporejea lile swali la awali la ikiwa kuna haja ya ‘kuiafrikanisha’ fasihi ya Kiafrika, pamoja na yote, jibu hadi sasa ni kwamba haja hiyo ipo, maana Waafrika wana utamaduni na hivyo fasihi yao ambayo ni tafauti kabisa na wengine, baadhi ya wakati haiwezi hata kusimulika kwa kutumia lugha isiyokuwa yao, maana fasihi ni pamoja na kuzielezea hisia za ndani mno za kibinaadamu.
Manu Chandaria, mwanzilishi na mwenyekiti wa makampuni ya Safal, ambayo kupitia kampuni yake tanzu ya Mabati Rowlings inashirikiana na Chuo Kikuu cha Cornell cha Marekani kutoa [url=http://kiswahiliprize.cornell.edu/]tuzo kwa waandishi wa Fasihi ya Kiswahili, anaamini kuwa Kiswahili kinaweza kuinuliwa na kujisimamia wenyewe.
“Tunataka kukisambaza Kiswahili. Ndilo jambo ambalo tunapaswa kulifikiria. Ndiyo lugha yetu ya kuelezea hisia zetu. Hatuwezi kuzielezea kwa namna nyengine. Unaweza kujaribu lugha zote, lakini hutaweza. Na kuumiliki utamaduni na fasihi yetu, lazima tuijuwe lugha hii.”
Na, kwa hakika, njia ziko nyingi ambazo lugha za Kiafrika zinaweza kutumiwa na Waafrika kusimulia fasihi yao wenyewe. Mojawapo ni tafsiri baina ya lugha moja ya Kiafrika kwenda nyengine na pia kwa waandishi wenyewe waliozowea kuandika kwa lugha za kigeni kuandika kwanza kazi hiyo hiyo kwa lugha ya Kiafrika.
Na kwa wale ambao bado wanaamini kuwa kuandika kazi za fasihi ya Kiafrika kwa lugha ya kigeni ndiko kunakowafanya wawe wa kimataifa na wasomi zaidi, mwandishi gwiji wa fasihi kutoka Senegal, Boubacar  Diop, anawataka afikirie upya.
“Watu wanadhani ni rahisi kusahau asili yangu. Nakwenda tu moja kwa moja tu kuwa mtu wa ulimwengu na inakuwa hivyo. Nadhani ni sisi peke yetu tunaofikiria hivyo. Tuwe wakweli, tuna tatizo la kukosa kujiamini wenyewe.”    Chanzo >>>>>>]]>
Boris Boubacar Diop ana msimamo kuwa: “huwezi kuwa wa kimataifa kama huna uthubutu wa kuwa wa kwenu”, lakini Patrick Mudekereza anasema katika maeneo mengi barani Afrika ukweli ni kuwa waandishi wanafikiri kwa lugha za kigeni kukiwemo kwao, Kongo, na Nuruddin Farahanasema kilichomfanya kuelekea kwenye uandishi wa Kiingereza ni kuwa lugha yake ya Kisomali haikuwa na hati za maandishi yake yenyewe.

<![CDATA[UFUNDI WA M.S. ABDULLA (E. N. Hussein)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1384 Mon, 25 Oct 2021 11:26:42 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1384 ‘Viti vilikuwa viwili tu – kimoja
kimesukumwa chini ya mvngu wa meza iliyokuwepo chini ya ukuta baina ya
mashubaka mawili yaliyojazwa vitabu; cha pili kimekaa ovyo tu, katikati ya
chumba. Hapana picha hata moja juu ya kuta zote; ila katikati ya ukuta wa
mezani ilikuwapo saa nyeusi ya Japani imetundikwa kwa juu, na chini yake
ilikuwapo rafu iliyojaa vitabu.’
 
Hebu tuuchungue ustadi alioupitisha Bwana Muhammed Said Abdulla katika maandishi haya kutoka ukurasa wa kwanza wa Mzimu wa Watu wa Kale.
Jambo la kwanza ni hakika aliyonayo ya chumba hiki. Ni kama kwamba Bwana Muhammed anakiona chumba chenyewe mbele yake na huku anaandika, na siyo kuwa anakibuni kutoka akilini. Hakika hii inamfanya msomaji vile vile ‘akione’ chumba hiki mbele yake. ‘Kweli, ama hiki chumba!’ anaamini. Imani hii ndiyo inayomfanya ajihisi kuwa yumo katika chumba hiki. Pale akijihisi kuwa yumo katika chumba cha Musa kilichomo ndani ya ulimwengu wa kubuni, ndipo msomaji anapokuwa ameshaukimbia kwa nafsi yake ulimwengu huu wetu – ulimwengu wa hakika, ulimwengu wangu na wako – na kuingia ulimwengu wa kubuni.
Kukimbia huku kwa nafsi, kutoka ulimwengu wa hakika kwenda
ulimwengu wa kubuni, ndio msingi war aha ya usomaji, nan i moja katika malengo ya maana ya msomaji wa maandishi ya kubuni.
Jambo la pili ni tabia ya Musa. Katika kutuchorea chumba cha Musa, mwandishi anatuchorea tabia ya Musa. Madhumuni mawili yamechanganywa – kutupa picha ya chumba na kutupa picha ya mwenye chumba. Huu ndio ustadi. Bwana Muhammed anapoongea juu ya chumba anaongea juu ya mambo mawili – chumba na tabia ya mwenye chumba bilakutaja tabia zake. Kwa mfano, ‘Viti vilikuwa viwili tu – kimoja kimesukumizwa chini ya mvungu wa meza…..’ Kuna uchache wa vitu: viti viwili tu. Bwana Musa si mtu mwenye kupenda fanicha ya kitajiri na mazulia ya kifalme. Kwake yeye, fanicha sip ambo la nyumba bali ni kitu cha matumizi. Kiti ni kitu cha kukalia tu, si cha kujisifia. Yeye hajali nidhamu ya viti na vitu kama hivi. Viti vimekaa ovyo tu- ‘kimoja kimesukumwa’. Neno ‘kimesukumwa’ hapa laonesha kutokujali kwake. Maana jambo linaloingia fikirani katika kusoma maneno haya ni kuwa Musa, bila ya kujali chochote, na si kwa makusudi, kakisukuma hiki kiti bila ya kujali tena kukiweka sawa. Hata kwa mfano ingalikuwa sio yeye aliyekisukuma, lakini madhali yeye hakukirudisha mahali pake, madhali yeye hakukiweka katika mpango fulani, yaonesha kuwa yeye mwenye chumba hiki hajali habari ya nidhamu.
Tunaambiwa kuwa kuna uchache wa fanicha lakini kuna wingi wa vitabu – vitabu juu ya meza, vitabu katika rafu, vitabu katika mashubaka mawili. Bwana Musa apenda vitabu na ana kiu cha elimu. Uandishi ni jambo la uchaguzi kwa vile mwandishi huchagua kuandika neno hili na kuacha neno hili. Kwa vile uchaguzi huu hufanywa kwa sababu maalumu, basi kila kinachoandikwa nacho huwa na sababu maalumu. Juu ya msingi wa makala haya nimejenga uchambuzi huo hapo juu. Kwani sikubali kuwa maneno kama (kiti) ‘kimoja kimesukumwa….’ ni maneno tu. Maneno haya yameandikwa kutoa picha fulani kwa ubingwa. Ikiwa tunakubaliana kuwa katika maandishi ya kubuni kila linaloandikwa lina sababu, basi ni nini sababu ya maneno, Hapana picha hata moja juu ya kuta zote tatu? Kwa nini mwandishi anatwambia hivi? Maana katika chumba hiki viti vingi vimetoweka, havipo.
Lakini mwandishi ametaja habari ya picha tu, yakuwa hakuna picha yoyote viambazani. Tena anasisitiza ‘hata moja’. Nitalijibu swali hili
kwa kusema kuwa huo ni ufundi. Katika kutwambia nini hakipo, anatwambia nini kipo; katika hali ya kutoweka, kuna kuwako. Nini kimetoweka? Picha zimetoweka. Hakuna picha. Lakini kuna nini? Vipo ‘vitu’ hivi bali bila ya kutajwa: Ni kawaida katika nchi hii, yaani Unguja, kuweka picha viambazani. Huu ni utamaduni na ustaarabu wa watu hawa. Kama ingalikuwa kuweka picha si jambo la kawaida, mwandishi asingalistaajabu juu ya ukosefu wa picha hizo. Imekuwa kama mwandishi anatwambia: ‘Kwa kawaida chumba kama hiki hapa petu huwa na picha. Lakini katika chumba hiki hapana picha hata moja juu ya ukuta.’ Kwa hivyo tunaelewa juu ya utamaduni.
Jambo la pili ni kuuliza: hizi picha ni picha gani? Mwandishi hatwambii. Jambo jema hivyo kutotwambia. Jema kwa sababu fikra za msomaji Zapata mawanda makuu ya kuchagua.
Mimi niliposoma kitabu hiki nilifasiri kuwa picha hizi ni za rafiki, jamaa au mke. Mara nilipofikiri hivi picha niliyoipata ya Musa ni kuwa Musa ni mtu pweke; hana jamaa, hana mke wala hana rafiki! Lakini nikasema kuwa lakini Najum ni rafiki yake! Nikabadilisha mawazo pale pale. Hana rafiki wengi, hana jamaa kabisa wala hana mke. Lakini si lazima, anaweza kuwa ana jamaa lakini haweki picha zao kama wanavyofanya watu wote. Mbona hakuweka picha ya Najum? Musa, kwa hiyo, si mtu kama watu wengine wa Unguja; ni mtu asiyependa kufanya mambo kama wanavyofanya watu wengine. Vile vile Bwana Musa ni mtu pweke. Haya yote nimeambiwa kwa ufundi, kwa mstari mmoja tu: ‘Hapana picha hata moja juu ya kuta zote tatu….’
Mstari huu umenieleza habari kadha wa kadha. Kunieleza huku siyo kwa kawaida, bali kwa ubingwa. Mstari huu unazitekenya fikra za msomaji na kuziachia ziende zinapopelekwa na shauku zake. Bila shaka kila mtu atafasiri atakavyo, lakini kule kufunguliwa mawanda ambapo fikra zetu zaweza kutimka zitakavyo ni jambo la ustadi.
Katika kitabu chake, Bwana Muhammed Said Abdulla ametumia ufundi kama huu pahala pengi. Hivyo sitaweza kuonesha pahala pote hapo katika kurasa chache hizi, lakini tunaweza kuonesha maandishi ambayo yamepitishwa kidogo na ufundi wa namna nyingine. Najum yupo ndani ya mzimu, kashikwa na woga. Mbele yake anamwona mtu wa kutisha- miguu yake ameinyosha mbele, kichwa chake amekipakata. Mwandishi anatusimulia (uk. 37): ‘ Najum aliduwaa na kutumbua macho. Miguu yake haikuweza kusimama sawasawa kwa ajili ya hofu. Alitamani kurudi nyuma, lakini hofu ilimzidia. Alipozunguka kumtazama Bwana Musa….wapi? Bwana Musa hayupo!’ Maandishi haya yanaweza
kusomwa namna mbili. Mtu anaweza kuyasoma kama maelezo. Mwandishi anamwona Najum fikrani mwake, naye anatueleza vitendo vya Najum kama avionavyo humo. Utaratibu unamtenga mwandishi na ‘kiumbe’ chake-Bwana Muhammed, mwandishi, na Bwana Najum ni watu wawili tafauti. Bwana Muhammed ni mtoaji habari tu na msimulizi way ale yanayomfika Bwana Najum. Yeye hayahisi yale anayoyahisi Najum.
Tunaweza kufasiri namna nyingine tena. Mwandishi na kiumbe chake katika maarifa haya huwa kitu kimoja. Kwanza Bwana Muhammed anatueleza yale yanayomkuta kiumbe chake-Najum. Lakini kwa vile yeye na kiumbe chake wameambatana sana, hawezi kujizuia kueleza bila kuyahisi yeye mwenyewe yale anayoyahisi Najum. Kwa mfano. Toka mstari ‘Najum aliduwaa…’ mapaka… ‘Alipozunguka kumtazama Bwana Musa….’ (uk. 37) mwandishi yu mbali na kiumbe chake. Anatoa ripoti tu. Lakini kiumbe, yaani Najum, anageuka. Anapogeuka anahisi ‘kitu’ fulani. Bwana Muhammed hawezi kungojea kutueleza kile anachohisi Najum. Yeye na Najum wanakuwa kitu kimoja. Bwana Muhammed anayahisi anayoyahisi kiumbe chake. Hawezi tena kukaa na kutueleza kwa utulivu kama vile anavyofanya mwanzo wa maelezo. Kwa hivyo…. ‘wapi? Bwana Musa hayupo!’ Hofu na ajabu, yote yamemuelemea Najum. Anayeona ajabu na hofu hapa ni Najum. Lakini kitambo kidogo alikuwa ni Bwana Muhammed aliyekuwa akituongelea. Sasa ni Najum anayetuongelea. Mabadiliko yamefanyika kufumba na kufumbua. Maandishi haya yanaonesha maendeleo ya uandishi na kitendo.
Bila shaka Bwana Muhammed ni fundi wa usimulizi. Lakini mimi nina malalamiko mawili makubwa. Kwanza, hajaudhibiti kamili ufundi huu. Kwa mfano, baada ya Musa kumaliza maelezo yake, mwandishi anatwambia (uk. 79): ‘Kiasi dakika kumi zilipita, kimya kilitawala ukumbi mzima wa Baniani. Husikii kitu ila labda tik tik ya saa ikitokea upande wa ndani tu.’ Ni wazi kuwa haiwezekani kuweko dakika kumi za ukimya mahali kama hapa. Kwani kimya hiki si kimya cha kawaida, ni kimya chenye mivumo ambayo haiwezi kukaa kwenye ukimya au katika hali ya wasiwasi kama hiyo kwa muda mrefu kama huo. Mwandishi kajiandikia tu bila ya kufikiri.
Maelezo kama haya yamo mengi katika kitabu hiki. Vilevile tukiangalia mikogo ya Musa inayovuka mpaka katika sehemu ya mwisho ya kitabu, twaona kwamba Musa anajikwatua na kiko chake na kujipanua mpaka msomaji akawa hapendezwi tena.
Lalamiko la pili linahusu msingi wa hiki kitabu. Hiki kitabu kimetawaliwa na kimejengwa juu ya mithali ya Sherlock Holmes. Sherlock Holmes na Watson-Musa na Najum. Kuiga si
jambo baya, lakini kuna miigo ya namna mbalimbali. Inapokuwa kuiga ni
kubadilisha majina na mahali, basi kuiga huko ni kubaya. Mwigo huu ndio mwigo
alioufanya Bwana Muhammed. Badala ya Sherlock Holmes ametafuta jina
jingine-Musa. Akambadilisha rangi. Sherlock Holmes akaweka Unguja. Akamwita Musa,
Mwafrika. Tukisoma kitabu hiki inakuwa vigumu sana kukubali kuwa yeye ni mtu wa
Unguja. Nalo hilo si ajabu. Kwani yeye ni Mzungu mweusi. Kumpa mtu jina la
Kiafrika na rangi nyeusi na umbile la Kiafrika siyo kumfanya kiumbe huyo awe
Mwafrika hasa katika ulimwengu wa kubuni. Kwani fikra na thamani, na utamaduni
wa mtu vile vile ni sehemu kuu ya kiumbe. Musa anaonekana Mwafriks. Lakini utamaduni
wake na ustaarabu wake ni wa kigeni. Yeye ni Mzungu mweusi.
Sina shaka yoyote kuwa
Bwana Muhammed anataka sisi tumpende Musa. Lakini kioo cha tabia alichotuwekea
kina kasoro fulani kama nilivyoonesha hapo juu. Fikra za Mzungu mweusi si fikra
njema za kuiga.
Hoja inatolewa kuwa
Bwana Muhammed hakuandika kitabu hiki kama mafunzo juu ya tabia. Yeye kataka
kuandika hadithi ya upelelezi. Lengo lake si kuhutubia bali kufurahisha. Maoni yangu
juu ya hoja kama hizi ni haya.
Ikiwa lengo ni
kufurahisha na kuandika hadithi ya upelelezi, mwandishi anaweza kuandika
hadithi ya upelelezi yenye mizizi ya hapa hapa Tanzania. Hapa upelelezi
unafanywa sana na polisi lakini sio upelelezi namna hiyo. Habari hii ya
mpelelezi wa siri (private detective), mwaka 1957, katika kisiwa cha Unguja ni
habari ngeni, tena ni vigumu kusadikika.
Haikubaliki kuwa wakati
huo, mwaka 1957, walikuwapo wapelelezi wa siri wa namna hii. ‘Mpelelezi wa siri’
ni mtu mwenye kuuza uwezo wake wa upelelezi kwa wale wanaouhitaji. Ni jambo la
kuuza na kununua. Mpelelezi huyo anauza. Hivyo lazima awepo mnunuzi wa
upelelezi huo. Lazima iwepo haja ya upelelezi kama huo kabla ya kuwepo
mpelelezi kama huyo. Haja hii hutokeaje? Nchi huwa na mauaji au maasi mengine
ambayo polisi peke yao hawawezi kuyachunguza. Pengine watu wanataka kupelelezi
mambo fulani fulani kwa siri. Haya yanasababisha haja ya mpelelezi wa siri. Mauaji
mengi au maasi mengine ni alama ya miji mikubwa kama London, New York,
Johannesburg, au hata Nairobi. Ukubwa wa nchi, wingi wa watu, mandeleo na
ustaarabu wa kisasa-haya yote yanasababisha maasi. Na maasi nayo yanasababisha
haja ya mpelelezi wa siri.
Unguja, mwaka 1957,
haikutimiza sharti hizi. Sisemi kuwa Unguja kulikuwa hakuna maasi, bali
haukuwapo wingi wa maasi hata ukasababisha haja ya kuwapo mpelelezi kama huyu.
Hebu tujiulize huyu
Musa anafanya kazi gani (pale anapokuwa hapelelezi)? Anapataje chakula chake? Je,
analipwa kwa upelelezi aufanyao? Hii ni kazi inayompa fedha ya kuendesha
maisha? Maswali haya hayajibiwi. Tunaambiwa tu kuwa Musa ni mpelelezi hodari. Na
sisi lazima tuamini.
Kwa ufupi maoni yangu
juu ya maandishi ya Bwana Muhammed Said Abdulla ni haya. Bwana Muhammed ni
mwandishi mwenye ustadi na ubingwa wa kuandika. Lakini ubingwa wake bado
hajaumiliki sawa sawa. Tena ni jambo la kusikitisha kuwa ufundi huu umejiruhusu
kutawaliwa moja kwa moja na mithali ya kigeni.
REJEA
Uchambuzi wa Maandishi
ya Kiswahili (1996) Dar es Salaam. DUP. Kimehaririwa na Farouk. M. Topan.
]]>
‘Viti vilikuwa viwili tu – kimoja

<![CDATA[BEN R. MTOBWA ALISTAHILI ‘ZAWADI YA USHINDI’]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1369 Mon, 25 Oct 2021 05:48:49 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1369 Kwa ufupi
Ni kweli ‘Tutarudi na Roho Zetu? au hizi ni ‘Salamu Toka Kuzimu’. Pengine hii ni ‘Roho ya Paka’ lakini inawezekana hawa ni ‘Malaika wa Shetani’ wanaotaka kumuweka ‘Mhariri Msalabani”. Hapana nadhani ‘Najisikia Kuua Tena’.
Na Florence Majani ,Mwananchi

Naam, kwa wasomaji wa vitabu hasa riwaya pendwa, aya hii ya kwanza haina mushkeli kwao.
Kwa wewe ambaye pengine hujaielewa, maneno yote yaliyo katika fungua na funga semi ni vitabu vilivyowahi kuandikwa na Ben Mtobwa aliyefariki dunia mwaka 2008.
Nimeishika kalamu yangu kumkumbuka kutokana na umahiri wake wa uandishi wa vitabu ambao naweza kusema umechochea mimi kuwa mwandishi leo.
Nilianza kusoma kazi za Mtobwa nikiwa darasa la tatu, nakumbuka nilikuwa sijali kama hakuna umeme nyumbani. Nilikaa pembeni ya taa ya kandili usiku na kukisoma kitabu chake cha Tutarudi na Roho Zetu hadi usiku wa manane.
Mtobwa atakumbukwa kwa umahiri wake katika uandishi. Uandishi ulioweza kumfanya msomaji asikiweke kitabu chini.
Alikuwa ni mwandishi aliyeweza kutunga hadithi inayofanana na ukweli kiasi cha msomaji kuamini yupo mtu anayeitwa Joram Kiango ambaye siku zote huwa ni mhusika mkuu wa kazi zake.
Aliwaumba wahusika wake na kuwapa sifa ambazo msomaji angedhani ni kweli wanaishi au ni binadamu wa kweli.
Kwa mfano, Mtobwa alimuumba Joram Kiango kama kijana mtanashati, hodari na mwenye mapenzi tele kwa nchi yake.
Tofauti na waandishi wengine, Mtobwa hakuwa msahaulifu, bali alizitumia tabia zile zile za Joram Kiango katika kila kitabu.
Kadhalika alimjenga Nuru kama msichana mwerevu, mzalendo na mwenye uzuri wa kipekee. Fasihi ya aina hii ilimfanya msomaji aamini Nuru na Joram ni watu wanaoishi, lakini kumbe walikuwa ni wahusika wa kubuniwa tu.
Pamoja na umahiri wa kuwaumba wahusika, Mtobwa alikuwa ni mwandishi aliyekuwa akijidhatiti kwa kusoma, kwani kazi zake nyingi zilihusisha taarifa na mada za kitaalamu.
Mwandishi huyu atakumbukwa kwa uwezo wake wa kuunganisha matukio katika mtiririko unaomfanya msomaji aendelee kusoma, na si hivyo tu bali si ajabu msomaji akarudia vitabu mara kadhaa bila kuvikinai.
Mwanafasihi huyu hakuwaegemea riwaya za mapenzi tu, kazi zake nyingi zilihusisha upelelezi, uzalendo na harakati za ukombozi wa Afrika na hata kufichua ufisadi.
Tutampata wapi Ben Mtobwa mwingine ambaye atakuwa na kipaji cha uandishi kiasi hiki? Nchi imepoteza waandishi wa riwaya pendwa, kuanzia Elvis Musiba na Willy Gamba wake hadi Ben Mtobwa na Joram Kiango!
Siwezi kuisahau riwaya ya Zawadi ya Ushindi. Riwaya hii, niliisoma nikiwa shule ya sekondari na mpaka sasa nimerudia kuisoma mara mbili.
Katika riwaya hii, Mtobwa anaonyesha vita vya Kagera, anaonyesha uzalendo aliokuwa nao msichana Russia kwa nchi yake hata akamshawishi, mchumba wake Sikamona akapigane vita vya Kagera.
Mtobwa alionyesha jinsi Watanzania walivyohamasishwa wakati ule kujumuika na kumng’oa Iddi Amin.
Miaka nane sasa imepita tangu Ben Mtobwa afariki dunia, kilichobaki ni kumpa ‘Zawadi ya Ushindi’ kwa kuzisoma kazi zake zilizofichua mafisadi waliofanana na ‘Malaika wa Shetani’ na wahujumu uchumi wenye ‘Roho ya Paka’.
Waandishi wajifunze kutoka kwake kwa kufichua yale yaliyo ‘Nyuma ya Pazia’ kwa kuwa kalamu ya mwandishi lazima itatufanya ‘Turudi na Roho Zetu’ Ben Mtobwa hakika unastahili ‘Zawadi ya Ushindi’
fmajani@mwananchi.co.tz
0715-773366
]]>
Kwa ufupi

<![CDATA[REJEA ZA KISWAHILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1368 Mon, 25 Oct 2021 05:43:40 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1368 Abdalla, A., 1973. Ushairi wa Kiswahili na Uhuishwe Usiuliwe Zinduko. Idara yaKiswahili, Chuo Kikuu. 

Abdallah, A., 1977. Mashairi ya Miaka Kumi ya Azimio la Arusha UKUTA, Dar es Salaam.
Abdallah bin Ali bin Nasir,Sayyid, 1972. Al-Inkishafi. Oxford University Press, Nairobi.
Abdallah, H., 1960. Utenzi waVita vya Wadachi Kutamalaki Mrima. East African Library Bureau, EALB, Dar es Salaam.
Abdulaziz, M., 1979. Muyaka: 19th Century Swahili Popular Verse. Kenya Literure Bureau, Nairobi.
Abedi, A., 1983. ( lst ed. 1954) Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri. East African Library Bureau, EALB, Nairobi.
Abedi, A., 1971. ‘Utangulizi’ wa Waadhi wa Ushairi. (M. Mnyampala 1971). East African Library Bureau, EALB, Nairobi.
Allen, J. de V., 1982. Review of Four Centuries of Swahili Verse (J. Knappert). RAL 13/1: 141147.
Allen, J.de V., 1982a. ‘Traditional History and African Literature The Swahili Case.’ JAH23: 227-236,
Allen, J.W.T. 1971. TendiHeinemann, London
Arnold, R,. 1973. ‘Swahili
Literature and Modern History: A Necessary Remark on Literary Criticism.’
Kiswahili Vol. 42/1 & 43/1, Institute fot Kiswahili Research, Dar es
Salaam. , pp. 68 73.
Buettner. C.G, 1894. Anthologie
der Suaheli Literature. Berlin.
Chiraghdin, S., 1971, ‘
Utangulizi wa Mhariri’ katika Nassir,A Mal enga wa Mvita. Oxford University
Press, Nairobi.
Chiraghdin, S., Nabhany, A. S. na
Baruwa, A., 1975. ‘Tarehe ya Ushairi wa Kiswahili.’ Mulika 7: 59-67.
Chiraghdin, S., 1987. Malenga wa
Karne Moja. Longman, Nairobi.
Chiraghdin, S. and Mnyampala,
1977. Historia ya Kiswahili. Oxford University Press, Nairobi.
Dammann, E., 1940. Dichtungen in
der Lamu Mundart des Suaheli Hamburg.
Dammann, E, 1942. ‘Muhammed bin
Abubekr bin Omar Kidjumwa Masihii.’ Afrika und uebersee 52:315-21.
Dammann, E., (ed) 1993.
Afrikanische Handschriften Teil 1: Handschriften in Swahili und anderen
Sprachen Afrikas. Franz Steiner Verlag, Stuttgart.
Dumila, F., 1971, Wasifu wa
Kenyatta. Jomo Kenyatta Foundation, Nairobi.
Farsy, M. S., 1960, Kurwa na
Doto. East African Library Bureau, EALB, Nairobi.
Gerard, A., 1982, African
Language Literatures. Three Continents Press Longman: London and
Washington.
Ghaidam, U., 1975. Lamu: A Study
of the Swahili Town. Kenya Literature Bureau, Nairobi.
Gibb, H. A. R., 1963. Arabic
Literature. Oxford University Press, London.
Gibbe, A., 1978. ‘Fasihi na
Jamii: Baadhi ya Washairi wa Kiswahili, 1960-77’. Kiswahili 48/1, March 1978: 1
– 25
Gibbe, A.G., 1980. Shaaban Robert
Mshairi. Tanzania Printing House (TPH), Dar es Salaam
Gwassa, G. C. K., 1967.
kwnbukumbu ya Vita vya Maji Maji. East African Printing House (EAPH),
Nairobi.
Harries, L., 1962. Swahili
Poetry. Oxford University Press, London
Harries, L., (ed) 1971. ‘ ‘Dunia
Imezungukuka’: Mashairi ya Ali Koti.’ Kiswahili41/2: 56-59.
Harries, L., 1972. ‘Poetry and
Politics in Tanzania.’ Ba Shiru 4: 52-54.
Hichens, W. (ed) 1934. Diwani ya
Muyaka. Witwatersrand Press, Johannesburg.
Hichens, W. (ed) 1939. Al
Inkishafi. Sheldon Press, London (See also Abdallah bin Ali bin Nasir,
1972).
Hichens, W 1962/3. Swahili
Prosody. Swahili No 33/1, I.K.R Dar es Salaam (Written in 1941).
Hinawy, M. A., 1958. Al-Akida and
Fort Jesus, Mombasa. Macmillan, London.
History Dept., University of Dar
es Salaam. (UDSM), 1968. ‘Maji Maji Research Project.’ Mimeo, University of Dar
es Salaam Library.
Honero, L. N., Sengo, T. S. Y na
Ngole, S. Y., 1980. Matunda ya Azimio. Institute fot Kiswahili Research, Dar es
Salaam.
Jamaliddin, A., 1957. Utenzi wa
Vita vya Maji Maji Supplement to Swahili 27. Institute fot Kiswahili Research,
Dar es Salaam.
Kahigi, K. K., 1976. ‘Ushairi:
Mtazamo wa Kisayansi,’ KiswahiliTol. 45/1. Institute fot Kiswahili Research,
Dar es Salaam.
Kandoro, S., 1978, Ushahidi wa
Mashairi ya Kiswahii na Lugha Yake. Longman, Dar es Salaam.
Kandoro, S. A., 1978a, Liwazo la
Ujamaa. Tanzania Printing House (TPH), Dar es Salaam.
Karama, S 1981 Urembo wa
Kiswahili Evans, London.
Karama, S 1986 Utunzi Wenye
Fahari. Macmillan, Nairobi.
Kezilahabi, E 1973 ‘The
Developmentof Swahili Poetry 18 – 20 Century.’ Kiswahili Vol. 42/2, 43/1
Institute fot Kiswahili Research, Dar es Salaam. pp. 62- 67.
Kezilahabi, E., 1976. Ushairi wa
Shaaban Robert. East African Library Bureau, EALB, Nairobi.
Kezilahabi, E., 1983, ‘Uchunguzi
katika ushairi wa Kiswahili’, Institute fot Kiswahili Research, Makalaza
Seminalll: 144 – 163
Kezilahabi, E., l988. Karibu Ndani
Dar es Salaam University Press, DUP, Dar es Salaam.
Khatib, M. S. l975. Utenzi wa
Ukombozi wa Zanzibar. Oxford University Press, Dar es Salaam.
Kibao, S. A , 1975. Utenzi wa
Uhuru wa Kenya. Oxford University Press, Nairobi.
Kijumwa, M, 1973. (lst ed. l911).
Utenzi wa Fumo Liyonga. Institute fot Kiswahili Research, Dar es Salaam.
Kija, P. M., 1987. Wimbo wa
Kandambili B. P. Ndanda, Peramiho.
Knappert, J., 1967. Traditional
Swahili Poetry. G. J. Brill, Leiden
Knappert, J., 1979. Four
Centuries of Swahili Verse. Heinemann, London.
Lesso, Z. A., 1972. Utenzi wa
Zinduko la Ujama . East African Library Bureau, EALB, Nairobi.
‘Mashairi ya Watu wa Lamu’ (Ms).
Lamu Museum Library.
Massamba, D. P. B., 1983, ‘Utunzi
wa Ushairi wa Kiswahili.’ Makala za Semina va Kimataifa ya Waandishi wa
Kiswahili 111: Fasihi Institute fot Kiswahili Research, Dar es Salaam 55 –
95.
Mayoka, J., 1986. Mgogoro wa
ushairi na Diwani ya Mayoka. Tanzania Printing House (TPH), Dar es
Salaam.
Mazrui, A., 1988. Chembe cha
Moyo. Heinemann, Nairobi.
Mbaabu, I., 1978. Kiswahili Lugha
ya Taifa Kenya Literure Bureau, Kenya Literure Bureau, KLB, Nairobi.
Mbaabu, I., 1988. Utamaduni wa
Waswahili. Kenya Publishing & Marketing Co. Ltd., Nairobi
Mbaabu, I 1991 Historiaya
Usanifishaji wa Kiswahili. Longman Kenya, Nairobi.
Mbele, J 1986 ‘The Fumo Liyongo
Epic and the Scholars.’ Kiswahili 53/1 & 53/2, pp 128- 145.
Mgeni bin Faqihi, 1978. Utenzi wa
Ras’lGhuli (ed. Leo van Kessel). Tanzania Printing House (TPH), Dar es
Salaam.
Mkelle, M.B. 1976. ‘Hamziyya, the
Oldest Swahili Translation.’ Kiswahi1i 46/1, Institute fot Kiswahili Research,
Dar es Salaam.
Mnyampala, M., 1970. Ngonjera za
UKUTA 1. Oxford University Press, Dar es Salaam.
Mnyampala, M., 1971. Ngonjera za
UKUTA 2. Oxford University Press, Dar es Salaam.
Mohamed, M., 1967. Utenzi wa
Uhuru wa Tanganyika. Wizara ya Habari, Dar es Salaam.
Mohamed, S.A., 1980. ‘Sikate
Tamaa. Longman Kenya, Nairobi.
Mulokozi, M. 1975.’Maudhui ya
Ushairi wa Shaaban Robert.’ Umma 5/2: 172-187.
Mulokozi, M. 1982. ‘Protest and
Resistance in Swahili Poetry.’ Kiswahili 49/1: 25 – 54
Mulokozi, M and Kahigi, K.,1982.
Kunga za Ushairi na Diwani Yetu. Tanzania Printing House (TPH), Dar es
Salaam.
Mutiso, K., 1985. ‘Kasida ya
Hamziya’ (Tafsiri na Maelezo yake) (Ms).
Mutiso, K., 1986. Mizani Yangu.
Kenya Literure Bureau, KLB, Nairobi.
Mutiso, K. (19??).’Utenzi wa Fumo
Liyongo’
Muyaka bin Haji al-Ghassaniy 1940
Diwani ya Muyaka bin Haji al-Ghassaniy (Mh. W. Hichens). Witwatersrand
University Press, Johannesburg.
Mwana Kupona, 1962. Utendi wa
Mwana Kupona in Harries, L.
Nassir, A., bin Juma Bhalo, 1977.
‘Muyaka wa Muhajina Ushairi wa Kiswahili.’ Mulika 10:1-14.
Ndulute, C. L. 1985. ‘Politics in
a Poetic Garb: The Literary Fortunes of Mathias Mnyampala.’ Kiswahili
52/1&2: 143-160.
Nicholls, C. S. 1971. The Swahili
Coast. Gerge Allen & Unwin Ltd., London.
Nyaigotti-Chacha, C., 1992.
Ushairi wa Abdilatif Abdalla: Sautiya Utetezi. Dar es Salaam University Press
(DUP), Dar es Salaam.
Ohly, R., 1973. ‘Historical
Approach to Swahili Literature as Heretofore an Open Question.’ Kiswahili Vol.
43/2, Institute fot Kiswahili Research, Dar es Salaam. pp. 79-87
Ohly, R.,1980. ‘The Bitter
Attraction of the Bourgeoisie’ in Schild, U (ed) East African Experience:
Essays on English and Swahili Literature. D. Reimer Verlag, Berlin
Ohly, R., l985. ‘Literature in
Swahili,’ in Andrzejewski, B.W, Pilaszewicz, S and Tyloch, W (ed) Literatures
in African Languages: Theoretical Issues and Sample Surreys. Wiedza Powszechna,
Warszawa/Cambridge Univ.Press,
Ridhiwani, P. (Mnukuzi), 1987.
‘Utenzi wa Vita vya Badru’ (Mswada). Institute fot Kiswahili Research, Dar es
Salaam.
Ridhiwani, P (Mnukuzi) (Ms)
‘Shairi la Fumo Liyongo’ (Kumsifu Yanga). Transcription of Manuscript No.577.
KR.
Robert, S. 1969. (1st ed. 1945?)
Koja la Lugha Oxford University Press, Nairobi.
Robert, S. l 947. Pambo la Lugha.
Witwatersrand University Press.
Robert, S. 1960. Almasi za
Afrika. Art and literature, Tanga.
Robert, S. 1966. Maisha Yangu na
Baada ya Miaka Hamsini Nelson, Dar es Salaam.
Rozensztroch, M., 1984. ‘Liongo
Fumo Legende et Signification Politique.’ These pour le
Doctorat de Troisieme cyle.
Universite Paris III (a copy of this thesis is available at Lamu Museum
Library).
Ruo, Kimani R. 1983. ‘Suala la
Ushairi wa Kiswahili, Makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili
III: Fasihi. Institute fot Kiswahili Research, 127 – 143.
Ruo, K. R., 1989. Nguzo za
Ushairi wa Kiswahili. Macmillan, Nairobi
Salim, A. I., 1973.
Swahili-Speaking Peoples of Kenya’s Coast. East African Printing House (EAPH),
Nairobi.
Sengo, T. S. Y., 1976. Shaaban
Robert: Uhakiki wa Maandishi Yake Longman, Dar es Salaam.
Sengo, T. S .Y. and Mulokozi, M.
M., 1993. ‘Kiswahili Poetry in Tanga Region During the Colonial Period’ (Field
Research Report). Institute fot Kiswahili Research, Dar es Salaam.
Sengo, T. S. Y. and M. M.
Mulokozi, 1993. ‘Research on the History of Kiswahili Poetry: A.D. 1000-2000.’
(Progress Report, Nov. 1993). Institute fot Kiswahili Research/OSSREA, Dar es
Salaam.
Shariff, A, 1987. Slaves, Spices
and Ivory in Zanzibar. Tanzania Printing House (TPH), Dar es Salaam.
Shariff, I. N., 1984. ‘Review of
Four Centuries of Swahili Verse’ (J. Knappert). Kiswahili Vol.
51:156-196.
Shariff, I. N., 1988. Tungo Zetu.
The Red Sea Press Inc. Trenton, N. Jersey
Steere, E., 1867. Swahili Tales.
Bell and Daldy, London.
Taylor, 1891 and 1924 . ‘African
Aphorisms’ (Unpublished Papers, SOAS). S.P.C.K. London,
Topan, F. M. (ed), 1971.
Uchambuzi wa Maandishiya Kiswahili. (Analysis of Swahili Writings). Oxford
University Press, Nairobi
Institute fot Kiswahili Research,
1983. Makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili: II Fasihi,
Institute fot Kiswahili Research, Dar es Salaam.
Velten, C,. 1907. Prosa und
Poesie der SuaheL Berlin.
Werner, A,. 1926. ‘The Swahili
Saga of Liyongo Fumo.’ Bulletin of SOAS 4 / 28: 247 – 55.
Werner, A., 1918. ‘Swahili
Poetry.’ Bulletin of SOAS 1/II: 113-127.
Whiteley, W., 1969. Swahili: The
Rise of a National Language Methuen, London.
Zani, Z. M. S., 1953. Mashairi Yangu. TMP, Tabora.Msururu wa PTE Kiswahili – Suleiman A. Mirikau –
]]>
Abdalla, A., 1973. Ushairi wa Kiswahili na Uhuishwe Usiuliwe Zinduko. Idara yaKiswahili, Chuo Kikuu. 