MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ Sat, 27 Apr 2024 17:24:40 +0000 MyBB <![CDATA[NINAMUENZI MWALIMU NYERERE KWA KULIA NA MTANZIKO WA LUGHA NCHINI TANZANIA]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2843 Fri, 14 Oct 2022 17:12:29 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2843
Uzoefu na Tajiriba ya Mwandishi

*1.0 UTANGULIZI*
Ninayeandika makala hii ni Mwalimu na Mtafiti wa lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kwa hiyo, sauti yangu katika uga huu wa lugha (ya Kiswahili na Kiingereza) inaweza ikawa na uzito mkubwa kuliko sauti yangu katika nyuga nyingine za kitaaluma. Msingi wa uchambuzi wa makala yangu umejikita katika uzoefu na tajiriba katika lugha hizi mbili. Ijapokuwa hoja nyingi katika makala hii hazijashadidiwa kwa kurejelea tafiti au maandiko mbalimbali, ninaomba uamini kwamba ni uchambuzi wa mambo wenye ukweli. Lengo langu ni kuwa na makala rahisi fupi isiyochosha kusomwa.

Mwalimu Nyerere ndiye anaweza kutajwa kuwa msingi wa kukifikisha Kiswahili leo hii kilipo. Nyerere alitumia njia nyingi sana za kukikuza, kukieneza na kukiendeleza Kiswahili ikiwemo kukipa hadhi kubwa ya kimatumizi nchini Tanzania. Kiswahili kimekuwa lugha ya kufundishia katika shule za msingi nyingi za Serikali na baadhi ya shule Binafsi huku Kiingereza kikifundishwa kama somo.

Kiingereza, kama tunavyojua, ni lugha iliyotufikia kwa njia ya ukoloni (Waingereza). Ni lugha ambayo ina nafasi kubwa sana kidunia; hii ni lugha ya kufundishia katika ngazi ya elimu ya sekondari na chuo kikuu nchini mwetu ambapo katika ngazi hizo, Kiswahili kinafundishwa au kumakinikiwa kama somo.

*2.0 UFANISI WA LUGHA ZA KUFUNDISHIA*
_2.1 Elimu katika Shule za Msingi_
Katika ngazi ya shule za msingi ambako Kiswahili ni lugha ya kufundishia, ufanisi wa matumizi ya lugha hiyo ni mkubwa kwa maana walimu wanaweza kuitumia lugha hiyo vema kuwafundisha wanafunzi, na wanafunzi wanaweza kuwasikiliza vema walimu wao. Kwa ujumla, majadiliano baina ya walimu na wanafunzi hufanyika vema bila shida yoyote.

Aidha, shule nyingi za msingi (idadi kubwa ikiwa shule za binafsi) zinazotumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia, nazo zimekuwa zikifanya vema pia katika kutumia lugha ya Kiingereza katika masuala mbalimbali ya kishule.

_1.2 Elimu katika Sekondari na Vyuo Vikuu_
Ufanisi wa matumizi ya lugha ya kufundishia ambayo ni Kiingereza katika ngazi za elimu tajwa si mzuri hata kidogo. Wanafunzi wengi wameripotiwa na tafiti mbalimbali kuwa hawawezi kufuatilia, kujadili na kujielezea kwa lugha ya Kiingereza. Cha kushangaza, tafiti zimebaini kwamba hata baadhi ya walimu hawana uwezo wa kufundisha na kufanya majadiliano na wanafunzi kwa kutumia Kiingereza muda wote. Kinachotokea ni kwamba walimu wamepitisha utaratibu wa kuchanganya msimbo, yaani wanatumia Kiingereza na Kiswahili wanapofundisha na kujadiliana na wanafunzi wao darasani, ofisini au katika vyumba  semina (kwa vyuo vikuu).

*2.0 MTANZIKO WA LUGHA NCHINI TANZANIA*
Kama ambavyo umeona hali halisi katika kipengele cha kwanza hususani 1.1 na 1.2 kinavyoeleza hali ya ufanisi wa lugha za kufundishia nchini Tanzania. Kwa ujumla, ufanisi wa lugha ya kufundishia upo katika ngazi ya elimu ya msingi tu. Hapo ndipo mtanziko wa lugha unapoanzia. Mtanziko huu wa lugha upo kwa mapana yake; ambapo unaweza kujidhihirisha katika aina tatu: mtanziko wa lugha ya kufundishia; mtanziko wa lugha ya mawasiliano katika taasisi, asasi na vyama vya kitaaluma; na mtanziko wa matumizi ya lugha rasmi.

_2.1 Mtanziko wa Lugha ya Kufundishia_
Kama ambavyo imeelezwa vema katika 1.2; ijapokuwa sera ya lugha imebainisha wazi kwamba shule za sekondari na vyuo vikuu vitumie Kiingereza kama lugha ya kufundishia, walimu na wanafunzi wanachanganya karibia nusu kwa nusu Kiingereza na Kiswahili katika majadiliano kwa njia ya mazungumzo ya mdomo katika mada mbalimbali. Hii hali imeshamiri na inazidi kuota mizizi sekondarini na vyuoni. Na tusipochukua hatua za makusudi, Tanzania litakuwa Taifa la kwanza linalotumia mfumo wa peke yake wa matumizi ya lugha ya kufundishia ambao ni kuchanganya msimbo ( _code-switching/code-mixing_ ).

_2.2 Mtanziko wa Lugha ya Mawasiliano katika Taasisi, Asasi na Vyama vya Kitaaluma_
Taasisi, asasi, na vyama mbalimbali vya kitaaluma vimekuwa katika mtanziko mkubwa wa matumizi ya lugha. Nyaraka nyingi katika taasisi hizi huandikwa kwa Kiingereza lakini majadiliano hufanywa kwa Kiswahili au kwa kuchanganya Kiswahili na Kiingereza.

Hata vyuo vikuu na vyama vya kitaaluma, ambako watu wanategemea mtanziko huu usiwepo, nako bado vikao mbalimbali na mawasiliano ya kiofisi ambayo yameagizwa kisera/kiutaratibu yafanyike kwa Kiingereza, vinafanywa kwa kuchanganya msimbo. Mathalani, kikao kinaweza kufunguliwa kwa lugha muafaka (Kiingereza) kwa dakika kadhaa kisha lugha inabadilika na kuwa ama Kiswahili au kuchanganya msimbo, kwa maana ya kutumia Kiswahili na Kiingereza kwa wakati mmoja.  Cha kushangaza  zaidi, hata katika makongamano na midahalo iliyoandaliwa na wanataaluma na kujadiliana miongoni mwao, nyaraka huandikwa kwa Kiingereza lakini majadiliano kwa mazungumzo ya mdomo hufanyika ama kwa Kiswahili au kuchanganya msimbo (Kiswahili na Kiingereza). Hapo sasa unajiuliza: wanataaluma hawa hawajui Kiingereza?

_2.3 Mtanziko wa Matumizi ya Lugha Rasmi/Sanifu_
Hii ni aina nyingine ya mtanziko ambapo Watanzania wengi hawana weledi wa lugha hizi mbili (Kiswahili na/au Kiingereza) wanazotumia. Licha ya wengi wao kufuzu au kumaliza elimu ya sekondari na/au vyuo vikuu ambako walijifunza na/au kufundishwa (kwa) lugha hizi mbili vema, hawana weledi wa matumizi ya lugha hizo katika misingi yake ya urasmi na usanifu. Wengi wao wanabanga tu lugha hizo pale wanapotakiwa kuzitumia kwa kufuata misingi yake sanifu na rasmi.  Mtanziko huu umekithiri pia katika vyombo vya habari. Hali ni tete! Ina maana kwamba Watanzania wengi hawakijui Kiswahili sanifu/rasmi wala Kiingereza sanifu (standard British English). Ushahidi wa haya mambo upo wazi kabisa.

Kwa ujumla, jambo ambalo nimelibaini ni kwamba kadiri muda unavyozidi kwenda mbele, weledi wa matumizi ya lugha (na hata katika masuala mengine mengi) miongoni mwetu unapungua kwa kasi sana. Ninafikiri upo ulazima wa kufanya utafiti ili kujua sababu ya jambo hili.

*3.0 SABABU ZA MTANZIKO WA LUGHA*
Sababu za mtanziko huu ni:
(a) Kukosekana kwa muumano wa lugha ya kufundishia kati ya ngazi moja na nyingine ya elimu. Suala la kutumia Kiswahili katika ngazi ya shule ya msingi kisha kutumia Kiingereza katika sekondari na vyuo, linamvuruga mwanafunzi kwa kiasi kikubwa sana. Ikumbukwe kwamba binadamu huamilia lugha ( _a person acquires language_ ) pasi kutumia nguvu akiwa mdogo sana, na akishakuwa mkubwa, uwezo wa kuamilia unakufa na kuhamia katika kujifunza lugha ( _to learn language_ ) na hapo sasa nguvu kubwa hutumika. Kwa hiyo, wakati mwanafunzi huyu ni mtoto mdogo akiwa shule ya msingi anatumia lugha X (Kiswahili) ambapo lugha hiyo inakuwa imeshaota mizizi kichwani mwake; akishakua anajiunga na sekondari, anakutana na lugha X (Kiingereza), inakuwa ni vigumu sana kuingiza misingi mipya ya lugha akilini mwake. Matokeo yake, anabakia na mtanziko wa lugha katika msingi kwamba anakosa fursa ya kuimarisha lugha iliyoota mizizi kichwani mwake na analazimika kuingiza lugha mpya katika kichwa  ambacho kinatakiwa sasa kitumie nguvu nyingi kuipokea lugha hiyo na kujiimarisha nayo. Matokeo yake ni kwamba mwanafunzi anakuwa na kazi mbili: kwanza, kujifunza lugha ngeni ambayo haijaimarika kichwani mwake, na pili, kujifunza maarifa husika. Je, unadhani mwanfunzi huyu anaweza kujenga maarifa muafaka pamoja na fikra tunduizi kichani mwake?

(b) Baadhi ya walimu (wa masomo ya lugha na wa masomo mengine)  kutokuwa weledi. Ualimu unachukuliwa kama fani ya watu wenye ufaulu  duni (wa chini);

© Kukosekana kwa mbinu changamani nzuri za kufundisha na kujifunza somo la Kiingereza; mfano, kukosekana kwa midahalo (debates), kukosekana kwa mashindano ya usomaji wa hadithi na vitabu vya Kiingereza, kukosekana kwa mashindano mbalimbali ya uandishi kwa lugha ya Kiingereza, n.k. ;

(d) Kukosekana kwa usimamizi madhubuti wa matumizi ya lugha yaliyopitishwa kisheria/kisera katika ngazi fulani ya elimu, taasisi, au katika muktadha fulani; na

(e) Mazingira magumu na maslahi duni kwa walimu hasa wa sekondari na shule za msingi.

*4.0 NINI KIFANYIKE KUONDOKANA NA MTANZIKO WA LUGHA?*
Jibu ni rahisi: kutatua changamoto na matatizo yaliyobainishwa katika sehemu ya 3.0

*5.0 HITIMISHO*
Licha ya kwamba ni kweli ili kuondokana na mtanziko huu wa lugha nchini Tanzania, kwa kiasi kikubwa tunategemea mchakato usimamiwe na Serikali; bado mtu binafsi au taasisi inaweza kuwa na mikakati ya kupunguza au kuondokana na kiwango fulani cha mtanziko wa lugha. Kwa hiyo, ninatoa wito kwa watu wote hususani waliobahatika kusoma elimu ya sekondari na/au chuo wafanye jitihada za makusudi za kujikwamua katika mtanziko huu. Yafuatayo ni mambo unayoweza kuyafanya au kuyazingatia ili kuondokana na mtanziko wa lugha:

(a) Kujifunza au kujiimarisha katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili; jipige msasa katika sarufi ya lugha hizo, kama una shida ya kuongea Kiingereza vema; jenga utamaduni wa kusikiliza sana Kiingereza, kusoma &  kuandika sana habari za Kiingereza, na kujenga mazoea ya kuongea Kiingereza; na

(b) Jenga nidhamu ya kuheshimu lugha iliyopitishwa kutumika katika miktadha fulani; kama ni Kiingereza, tumia Kiingereza, kama ni Kiswahili, tumia Kiswahili; achana na habari za kuchanganya msimbo bila ulazima wowote.

*Dkt. Issaya Lupogo*
Chuo Kikuu Mzumbe
lupogoissaya1@gmail.com
0712-143909

_#TumuenziBabaWaTaifaKwaKuitumikiaNchiYetuVema#_

14/10/2022]]>

<![CDATA[ETIMOLOJIA YA NENO "DAHALIA'']]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2842 Wed, 12 Oct 2022 13:29:20 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2842
Neno *dahalia* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana zifuatazo:

1. Jengo wanamolala wanafunzi wasomao kwenye shule au vyuo vya bweni *(Kamusi Kuu ya Kiswahili*).

2. Bweni la wanafunzi wa kike.( *Kamusi Teule ya Kiswahili*).

Neno hili *dahalia* linatokana na neno la Kiarabu *daakhiliyyat  داخلية*  lenye maana zifuatazo:

1.  Shule ya bweni, *madrasatun Daakhiliyyat مدرسة داخلية.*

2. Kivumishi *-a ndani*, *mushkilatun daakhiliyyat مشكلة داخلية* tatizo la ndani, *malaabisun daakhiliyyat  ملابس داخلية* nguo za ndani, *wizaaratun daakhiliyyat وزارة داخلية* wizara ya mambo ya ndani. 

Kinachodhihiri ni kuwa neno *daakhiliyyat داخلية* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *dahalia* maana yake ya bweni katika lugha ya asili - Kiarabu (cha zamani)  haikubadilika.

Neno la Kiarabu Sanifu linalotumika kwa maana ya bweni ni *mahjau مهجع (umoja) na mahaajiu مهاجع (wingi).* 

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*]]>

<![CDATA[ETIMOLOJIA YA NENO "DAFTARI'']]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2840 Fri, 07 Oct 2022 20:06:06 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2840
Neno *daftari* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: li-/ya-*] yenye maana zifuatazo:

1. Kitabu kinachotumiwa na wanafunzi kuandikia masomo ya darasani na kufanyia mazoezi  *(Kamusi Kuu ya Kiswahili*).

2. Kitabu cha kutunzia kumbukumbu za miamala ya kifedha; leja.( *Kamusi Kuu ya Kiswahili*).

Neno hili *daftari* linatokana na neno la Kiarabu *daftarun  دفتر*  lenye maana zifuatazo:

1.  Karatasi zilizofungwa pamoja ambazo wanafunzi huandikia masomo yao darasani kama vile hesabati na kadhalika.

2. Daftari la kumbukumbu kwa ajili ya kuandikia matukio, fikra muhimu na kadhalika.

3. Kitabu cha hundi za benki,  brosha.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *daftarun دفتر* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *daftari* maana zake katika lugha ya asili - Kiarabu  hazikubadilika.

<![CDATA[ETIMOLOJIA YA NENO "DAFRAO'']]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2838 Wed, 28 Sep 2022 02:01:32 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2838
Neno *dafrao* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana zifuatazo:

1. Tukio la kugongana uso kwa uso kwa vyombo vinavyotembea.

2. Chuma kigumu kinachofungwa Mbele ya gari ili kuzuia uharibifu wakati magari yanapogongana.

Neno hili *dafrao* linatokana na neno la Kiarabu *dafraau دفراء* na lenye maana zifuatazo:

1.  Kilichodhalilika.

2. Kitu kilichooza, kikanuka na kutoa wadudu.

3. Aina ya mmea wa kitropiki. Kwa Kiingereza huitwa *scoparia.*

Kinachodhihiri ni kuwa neno *dafraau  دفراء* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *dafrao* maana yake kati lugha ya asili - Kiarabu ilibadilika na kupata maana mpya zilizotajwa.

<![CDATA[ETIMOLOJIA YA NENO "FURUTU'']]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2836 Sun, 25 Sep 2022 05:54:22 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2836
Neno *furutu (furut.u)* katika lugha ya Kiswahili ni *kitenzi si elekezi* chenye maana ya 'zidisha kufanya jambo fulani kuliko kawaida'.

*Mfano:* Kati yenu, Mwanakibibi anafurutu kwa kupenda kujiremba.

Neno hili *furutu*,linatokana na neno la Kiarabu *furtwun فرط* na lenye maana zifuatazo:

1. Kuchupa mpaka, kuzidisha kufanya jambo fulani kuliko kawaida.

2. Kitu kilichoachwa au kutelekezwa.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *furutwun  فرط* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *furutu* maana ya kuzidisha kufanya jambo fulani kuliko kawaida haikubadilika na maana ya Kitu kilichoachwa au kutelekezwa iliachwa.

<![CDATA[ETIMOLOJIA YA NENO "SARUFI'']]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2829 Wed, 14 Sep 2022 17:51:14 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2829
Neno *sarufi* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana zifuatazo:

1. Mfumo na muundo wa lugha ambao mtu akiufahamu humwezesha kuizungumza kwa ufasaha.

2. Taaluma ya isimu inayotafiti na kubainisha kanuni za vipengele mbalimbali vya lugha kwa mfano fonetiki, fonolojia, mofolojia, semantiki au sintaksia, *mfumo wa lugha.*

Neno hili *sarufi* linatokana na neno la Kiarabu *swarf* lenye maana zifuatazo:

1. Matukio ya zama, *swarfud  dahri صرف الدهر.*

2. Kiuchumi, ni kubadilisha fedha ya nchi kwa fedha ya kigeni; kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni.

3. Kilugha, ni taaluma inayohusika na kutambua vijenzi vya maneno na minyumbuliko yake; *mofolojia.*

4. Kisarufi, ni uwekaji wa herufi nuun (ن) mwishoni mwa neno ili kulitambulisha kuwa kwake katika kundi la nomino.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *swarfu صرف* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *sarufi* liliacha maana yake ya *mofolojia* katika lugha ya Kiarabu na kuchukua maana mpya pana ya kanuni, sheria au taratibu zinazotawala lugha  katika viwango yote vya uchambuzi wa lugha yaani kiwango cha sarufi matamshi (fonolojia) sarufi maumbo (mofolojia) sarufi miundo (sintaksia) na sarufi maana (semantiki).

Neno lenye maana ya tawi la isimu ya lugha linalojihusisha na fonolojia, mofolojia, semantiki na sintaksia, katika lugha ya Kiarabu, ni *Qawaaidul Lughatil Arabiyyat قواعد اللغة العربية* misingi ya lugha ya Kiarabu.

<![CDATA[ETIMOLOJIA YA NENO "BURUDAI'']]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2826 Sat, 10 Sep 2022 13:41:56 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2826
Neno burudai katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana zifuatazo:

1. Kisomo maalumu cha kumsifu Mtume Muhammad (Swalla Llaahu Alayhi Wasallama/Allaah Amrehemu na Ampe Amani); maulidi      ( Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili).

2. Jina la kasida mojawapo ya kumsifu Mtume Muhammad (S.A.W) na kueleza maisha yake; maulidi (Chanzo:Kamusi ya Kiswahili Sanifu - TUKI).

3. Wimbo wa kasida ambao ni mashairi ya kumsifu Mtume Muhammad (S.A.W) (Chanzo: Kamusi ya Kiswahili ya Karne ya 21).

Neno hili burudai linatokana na neno la Kiarabu burdah ( soma: burdatun/burdatan/burdatin بردة) lenye maana zifuatazo:

1. Mharuma (Kitambaa chembamba kirefu kinachotupiwa shingoni au begani).

2. Kasida ya kumsifu Mtume Muhammad (Allaah Amrehemu na Ampe Amani) iliyotungwa na Kaab bin Zuheir. Na imeitwa kwa jina hilo kwa kuwa Kaab bin Zuheir alipomaliza kuiimba Mtume alivua mharuma wake na kumtunza.

3. Kasida ya kumsifu Mtume Muhammad (S.A.W) iliyotungwa na Imam Al-Buswiriy.

Kinachodhihiri ni kuwa neno burdatun  بردة lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno burudai halikubadili maana yake ya kasida ya kumsifu Mtume Muhammad (S.A.W) katika lugha ya asili - Kiarabu.

TANBIHI:
Burudai mashuhuri, kwa Waswahili wa Afrika ya Mashariki, ni ile kasida iliyotungwa na mwanachuoni mshairi wa Misri aitwaye Muhammad bin Said bin Hamad  bin Abdillaahi Al-Sanhajii Al-Buswiiriy maarufu kwa jina la Al-Imaam Al-Buswiiriy (Amezaliwa tarehe Mosi Shawwal Mwaka 608 Hijiriyyah sawa na tarehe 7 Machi Mwaka 1213 Miladiyya).

Al-Imaam Al-Buswiiriy ndiye mtunzi wa kasida ya Hamziyya iliyotafsiriwa kwa Kiswahili na Sharif Aidarus na kuitwa Utendi wa Hamziyya.

Al-Imaam Al-Buswiiriy amesimulia kuwa alitunga kasida hii iitwayo ' Burdatu Al-Madiih بردة المديح'  alipopatwa na ugonjwa wa kupooza, akaomba uombezi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumsifu Mtume  Muhammad (S A.W) kwa kutunga kasida hii.

Alipolala alimuona Mtume Muhammad (S.A.W) ndotoni, akimfuta mwili wake kwa mkono wake uliobarikiwa na akapata nafuu.

Kulipokucha alipotoka nje ya nyumba yake alikutana na  baadhi ya watu masikini, na mmoja akasema: Ewe Bwana, nataka unipe shairi ulilomsifu Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Akamuuliza: shairi lipi? Akasema: Shairi linaloanza na: “ Amin tadhakuri jiiranin..../Je, ni kwa kuwakumbuka majirani…” (Ubeti wa kwanza wa shairi la Burdatu Al-Madiih, ambalo hakumwambia siri yake yeyote), basi akampa.

Habari ya kupona kwake ikaenea na watu wakaanza kutafuta baraka na uponyaji kwa kuisoma kasida hii.

Imesimuliwa kuwa burdah/burudai ni mharuma ambao Al-Imaam Al-Buswiiriy alimuona Mtume Muhammad ndotoni akiutumia kumpagusa mwilini na akaamka hali amepona kabisa maradhi ya kupooza yaliyokuwa yakimsumbua.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.]]>

<![CDATA[ETIMOLOJIA YA NENO "BURIANI'']]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2825 Thu, 08 Sep 2022 18:08:58 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2825
Neno *buriani* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana zifuatazo:

1. Maagano yanayoonesha kuwa wanaoagana wataachana kwa muda mrefu au kutoonana kabisa.

2. Salamu za kutakiana heri ambayo watu hupeana wanapoagana.

3. Msamaha au radhi ambayo watu hutakiana huku wakiagana.

*Nahau:*
*Peana buriani:* agana.

Katika lugha ya Kiarabu, hakuna neno *buriani* na neno lililo karibu ni neno *barawah*, neno la msimu lililotumika katika baadhi ya nyimbo za Kiarabu likiwa na maana zifuatazo:

1. Neno la kushukuru; ahsante.

2. Hali ya kukamilika; timamu.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *buriani* halina asili ya Kiarabu kinyume na madai yaliyosajiliwa makamusini.

<![CDATA[ETIMOLOJIA YA NENO "BURUJI'']]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2822 Mon, 05 Sep 2022 08:44:35 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2822
Neno buruji katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] na pia [Ngeli: a-/wa- kwa mtu]* yenye maana zifuatazo:

1. Ngome iliyo na kuta zenye uwazi juu, boma la ngome lenye kuta zilizo na mapengo kwa juu; sera      ( Vyanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu - TUKI).

2. Jengo au kitu kirefu kinachowekwa au kujengwa kwa ajili ya kuadhimisha au kuashiria tukio fulani; mnara (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu-TUKI ).

3. Chombo cha muziki aina ya tarumbeta ambacho mabadiliko ya sauti yake hutokana na kubonyeza vali, tarumbeta ndogo inayopigwa na askari. (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu-TUKI ).

4. Njia au mashukio ya nyota.(Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu-TUKI ).

5. Nafasi zilizoachwa chini ya ua uliojengwa kwenye maji machache na ambayo nyuma yake huwekwa mitego ya samaki, nafasi inayoachwa katika uzio uliojengwa majini kwa ajili ya kuwekea  mitego ya kunasia samaki. (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili Sanifu-TUKI ).

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili buruji linatokana na neno la Kiarabu buruuj ( soma: buruujun/buruujan/buruujin بروج) wingi wa neno la Kiarabu burj (soma: burjun/burjan/burjin برج) lenye maana zifuatazo:

1. Mnara wa kuongozea meli au ndege.

2. Kibanda cha askari kinachojengwa juu aghalabu katika ukuta wa kuingia kwenye mji, kwenye gereza, ukuta au ngome kwa ajili ya kufuatilia kwa mbali.

3. Kasri yenye kulindwa kwa ulinzi madhubuti.

4. Njia ya kushukia nyota 12 katika elimu ya Falaki.

5. Jengo refu kama vile Burju Al-Khalifa nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E).

Kinachodhihiri ni kuwa neno buruujun  بروج lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno buruji lilichukua kutoka Kiarabu baadhi ya maana, kuziacha nyingine na kuchukua maana mpya za nafasi inayoachwa katika uzio uliojengwa majini kwa ajili ya kuwekea  mitego ya kunasia samaki na chombo cha muziki kiitwacho tarumbeta.

<![CDATA[ETIMOLOJIA YA NENO "BURUNUSI'']]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2821 Mon, 05 Sep 2022 08:43:12 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2821
Neno burunusi katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya vazi zito lililounganishwa na kofia.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili burunusi linatokana na neno la Kiarabu burnus ( soma: burnusun/burnusan/burnusin برنس) lenye maana zifuatazo:

1. Vazi lenye mikono miwili linalounganishwa na kofia aghalabu huvaliwa baada ya kukoga.

2. Mji wa mimba.

Kinachodhihiri ni kuwa neno burnus  برنس lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno burunusi halikubadili maana ya vazi linalounganishwa na kofia, katika Kiarabu na liliacha maana ya mji wa mimba.

<![CDATA[ETIMOLOJIA YA NENO "UJUMI'']]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2819 Sat, 03 Sep 2022 06:30:16 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2819
Neno *ujumi* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: u-/u-*] yenye maana zifuatazo:
1. Kanuni zinazohusu ubora na ubaya wa kazi ya sanaa.(Vyanzo: *Kamusi ya Karne ya 21* na *Kamusi ya Kiswahili Sanifu - TUKI*).

2. Tathmini inayobainisha ubora au ubaya wa kazi za sanaa. (Chanzo: *Kamusi Kuu ya Kiswahili*).

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ujumi* linatokana na neno la Kiarabu *ujmu* ( *soma: ujmun/ujman/ujmin عجم*) wingi wa neno la Kiarabu *a-ajamiyyu (a-ajamiyyun/a-ajamiyyan/a-ajamiyyin اعجمي)* lenye maana zifuatazo:

1. Mtu asiye fasaha katika kuzungumza aghalabu lugha ya Kiarabu hata kama ni mwarabu.

2. Asiye mwarabu, mtu wa Uajemi (Iran); muajemi.

3. Mtu asiyeweza kusema; bubu.

4. -siyo na mlio/sauti aghalabu mawimbi au bunduki.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *ujmun  عجم* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *ujumi* lilichukua maana mpya *kanuni zinazohusu ubora na ubaya wa kazi ya sanaa, tathmini inayobainisha ubora au ubaya wa kazi za sanaa* na kuacha maana za neno hili katika lugha ya Kiarabu.

<![CDATA[ETIMOLOJIA YA NENO "BULIBULI'']]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2815 Sun, 28 Aug 2022 04:22:51 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2815
Neno *bulibuli* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana ya mtindo mmojawapo wa kofia nyeupe yenye nakshi (viua) inayovaliwa hasa mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki, kofia ya kazi.

Pia ni kivumishi kwa maana ya: -zuri, -a kupendeza, bambam, -ema.

Mwanafunzi mwenye tabia bulibuli hufaulu vizuri katika mitihani yake.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *bulibuli* linatokana na nomino ya Kiarabu *bulbulu بلبل* yenye maana zifuatazo:

1. Ndege mdogo aina ya kunega maarufu kwa kuimba vizuri.

2. Sehemu ya kumiminia maji katika birika.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *bulbulu  بلبل* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bulibuli* lilichukua maana mpya ya (nomino) kofia yenye viua inayovaliwa pwani ya Afrika Mashariki na maana ya (kivumishi): -zuri, -a kupendeza, bambam, -ema.

<![CDATA[ETIMOLOJIA YA NENO "MAHABA'']]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2810 Tue, 23 Aug 2022 05:59:57 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2810
Neno mahaba katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: ya-/ya-] yenye maana zifuatazo:

1. Hisia za mvuto zinazojengeka kwa mtu mwengine kutokana na kupendezwa naye. (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili).

2. Hali ya kuvutiwa na kitu au mtu kutokana na uzuri wake ambao huingia moyoni na kumfanya ampende. (Chanzo: Kamusi ya Karne ya 21).

3. Hali ya kuingiwa moyoni na mtu au kitu na kukuthamini zaidi ya vingine; mapenzi .(Chanzo: Kamusi ya Kiswahili Sanifu - TUKI).

4. Matandu ya wali yaliyoandaliwa maalumu kama tunu kwa mume.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili mahaba linatokana na neno la Kiarabu mahabbah محبة  ( soma: mahabbatun/mahabbatan/mahabbatin محبة) lenye maana zifuatazo:

1. Kupendana na kuthaminiana moyoni.

2. Ashiki inayojenga ubinafsi wa pendo na wivu.

3. Kinachotakiwa na moyo.

4. Ki-Falsafa, mahaba ni sababu inayoleta pamoja vitu mbalimbali.

Kinachodhihiri ni kuwa neno mahabbatun  محبة lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno mahaba lilichukua maana jumla ya mapenzi na kuleta maana mpya ya matandu ya wali yaliyoandaliwa kama tunu kwa mume.

<![CDATA[ETIMOLOJIA YA NENO "BUGHUDHA'']]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2809 Tue, 23 Aug 2022 05:59:17 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2809
Neno bughudha katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya mambo yanayomkasirisha au kumuudhi mtu, maneno na vitendo vinavyomfanya mtu audhike.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili bughudha linatokana na tendo-jina la Karabu bugh-dhwun بغض lenye maana ya chuki linalotokana na kitenzi cha Kiarabu baghadhwa (soma: baghadhwa/yabghadhwu/bugh-dhwan بغض، يبغض، بغضا)  chenye maana zifuatazo:

1. Kuchukia.

2. Kuchukiza.

3. Kuchukiwa.

Kinachodhihiri ni kuwa neno bugh-dhwun  بغض lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno bughudha lilichukua maana mpya ya maneno na vitendo vinavyomfanya mtu audhike, mambo yanayomkasirisha au kumuudhi mtu.

<![CDATA[ETIMOLOJIA YA NENO "BUDI'']]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2806 Sun, 21 Aug 2022 10:38:53 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2806
Neno budi katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana zifuatazo:

1. Jambo la lazima.
Msemo:
Sina budi kusafiri: lazima nisafiri. (Kamusi Kuu ya Kiswahili).

2. Suala linalomlazimu mtu kulitimiza.
Msemo:
Sina budi kuwasilisha mada yangu leo. (Kamusi ya Karne ya 21)

3. Nomino (Msemo) Sina budi kuja kesho: Lazima nitakuja kesho; Hapana budi : lazima. (Kamusi ya Kiswahili Sanifu-TUKI).

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili budi linatokana na neno la Kiarabu buddun (soma: buddun/buddan/buddin بد)  lenye maana zifuatazo:

1. Sehemu ya kitu, mbadala, kutengana.
Waarabu hulitumia neno hili pamoja na herufi laa (لا), yaani: Laa budda لا بد  kwa maana ya: hakuna mbadala, hakuna hiari, hakuna pa kukimbilia.

2. Sanamu, nyumba ya kuhifadhi sanamu.

Kinachodhihiri ni kuwa neno buddun  بد lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno budi lilichukua maana ya Laa budda inayoashiria  'ulazima'  katika Kiarabu lakini wakalipa neno lenyewe ' budi ' maana ya 'lazima' ambayo ikitanguliwa na neno ' hapana ' linaleta maana kinyume na kilichokusudiwa.
Neno ' budi ' lilipaswa kupewa maana ya hiari au kitu mbadala ili linapotanguliwa na neno ' hapana/sina' lilete maana ya ulazima. 