MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

<![CDATA[JIFUNZE KISWAHILI - Maendeleo ya Kiswahili]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/ Sat, 27 Apr 2024 20:38:21 +0000 MyBB <![CDATA[MAENDELEO YA KISWAHILI BAADA YA UHURU NA CHANGAMOTO ZAKE]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2783 Fri, 15 Jul 2022 07:35:56 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2783
.pptx   ppt.pptx (Size: 958.52 KB / Downloads: 11) ]]>

<![CDATA[HISTORIA YA LUGHA YA KISWAHILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2640 Sun, 03 Jul 2022 14:51:07 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2640 Lugha ya Kiswahili imeanza takriban miaka 1000 iliyopita kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki. Neno Swahili lina asili ya Kiarabu: Sahil ina maana ya pwani; sawahil ’’ a-sawāhilī’’ ni wingi wake kwa kumaanisha yote yanayohusiana na pwani, watu au utamaduni na lugha ya eneo la pwani. Kiswahili kilianza kama lugha ya miji na bandarini wakati wa biashara ya kimataifa kwenye pwani ya Afrika ya mashariki.

Tuna historia jinsi gani miji kama vile Kilwa, Lamu na mingine kadhaa iliyoanzishwa na wafanyabiashara Waarabu au Wajemi waliooa wenyeji. Idadi ya wahamiaji kutoka Uarabuni haikuwa kubwa sana, hivyo lugha ya wenyeji ilitumika kila mahali ila tu maneno mengi yameingia kutoka katika lugha ya Kiarabu. Utamaduni mpya ulijitokeza uliokuwa wa Kiafrika Kiswahili kilizaliwa kuwa lugha ya Kibantu kilichopokea maneno mengi ya asili na ya nje.

Kiswahili kiliandikwa muda mrefu kwa herufi za Kiarabu kama inavyosomeka kwenye sanamu ya askari huko Dar es Salaam, Tanzania. Maandishi Yanasema: "Huu ni ukumbusho wa askari wenyeji Waafrika waliopigana katika Vita Kuu."

Lugha iliandikwa kwa herufi za Kiarabu tangu karne ya 13 kabla ya kristo. Kwa bahati mbaya leo hatuna tena maandiko ya kale sana, kutokana na hali ya hewa kwenye pwani isiyosaidia kutunza karatasi na kurasa zenyewe zinaweza kuoza kutokana na unyevu hewani pamoja na wadudu wengi walioko katika mazingira ya pwani ya Tanzania.

Kuna Maandiko ya kale yanayopatikana kutoka karne ya 17 huonyesha ya kwamba tenzi na mashairi vinafuata muundo uliotangulia maandiko yenyewe kwa karne kadhaa. Sehemu kubwa ya maandiko ya kale ni tenzi yaani mashairi yenye aya maelfu. Tenzi ndefu kabisa inahusu kifo cha Mtume Muhamad ikiwa na aya 45,000.

Kiswahili kilipokelewa kirahisi na wenyeji kwa sababu walikosa lugha ya pamoja kati yao, lugha za Kibantu ziko karibu sana na athira ya Kiarabu ilikuwa kilekile kote pwani. Haya yote yalisaidia kujenga umoja wa Kiswahili katika eneo kubwa la pwani ya Afrika ya Mashariki. Kiajemi pia kilichangia maneno mbalimbali, kama vile "bibi" na "cherehani".

Kufika kwa Wareno huko Afrika ya Mashariki kuanzia mwaka 1500 kulileta athira mpya ikiwa maneno kadhaa ya Kireno yameingia katika Kiswahili kama vile "bendera", "gereza" na "meza".

Kuwepo kwa wafanyabiashara Wahindi katika miji mikubwa ya pwani kuliingiza pia maneno ya asili ya Kihindi katika lugha kama vile "lakhi", "gunia" n.k. Athira ya lugha za Kihindi iliongezeka kiasi baada ya Waingereza kutumia Wahindi wengi kujenga reli ya Uganda.

Kiswahili kama Lugha ya biashara.

Kiswahili kilitumika kama lugha ya biashara baina ya watu wa pwani na bara katika kanda ndefu sana kutoka Somalia hadi kasikazini mwa Msumbiji,

Wafanyabiashara Waswahili waliendeleza biashara ya misafara hadi Kongo. Kiswahili kiliendelea kuenea kwenye njia za misafara hii. Kila msafara ulihitaji mamia ya watu hadi maelfu wa kubeba mizigo ya biashara kutoka pwani hadi pale msafara ulipolenga Ziwa Tanganyikan. katika mkoa wa Kigoma.

Watu hawa wote walisambaza matumizi ya Kiswahili katika sehemu za ndani ya Tanzania.

Kiswahili wakati wa ukoloni
Karne ya 19 ilileta utawala wa kikoloni. Wakoloni walitangulia kufika katika bandari za pwani wakatumia makarani, askari na watumishi kutoka eneo la pwani wakijenga vituo vyao Pwani wakitumia lugha ya kiswahili. Watu hao walipeleka

Kiswahili pande za bara.
Wajerumani waliamua kutumia Kiswahili kama lugha ya utawala katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hapo waliweza kutumia kazi ya wamisionari Wakristo wa awali, hasa Ludwig Krapf, waliowahi kufanya utafiti wa lugha na kutunga kamusi na sarufi za kwanza mwaka 1879 na kuchapishwa Jijini London Uingereza Mwaka 1882 pamoja na kuunda mfumo wa kuandika Kiswahili kwa herufi za Kilatini.

Utawala wa kikoloni ulirahisisha mawasiliano kati ya wenyeji kwa kuzungumza Kiswahili wakati wote wa Ujenzi wa Reli ya kati ilijengwa na wafanyakazi kutoka makabila mbalimbali wakishirikiana.

Waafrika walilazimishwa kulipa kodi kwa wakoloni, hivyo walitafuta kazi ya ajira katika mashamba makubwa yaliyolimwa mazao ya biashara na katika migodi ya madini huko Kongo ambako watu wa makabila mengi walichanganyikana wakitumia Kiswahili kama lugha ya mawasiliano.

Namna Lugha ya Kiswahili ilivyoenea zaidi.
Waingereza baada ya kuchukua Tanganyika kutoka kwa Wajerumani waliendela kutumia Kiswahili kama lugha ya utawala. Kuanzia mwaka 1930 waliunda kamati yenye shabaha ya kuunganisha lahaja mbalimbali na kuunda Kiswahili cha pamoja kwa ajili ya Afrika ya Mashariki (Inter-territorial Language (Swahili) committee for the East African Dependencies).

Mwenyekiti alikuwa Frederick Johnson, makatibu R. K. Watts, P. Mzaba na Seyyid Majid Khalid Barghash. Kamati hiyo iliamua kutumia lahaja ya Kiunguja kuwa msingi wa Kiswahili cha pamoja kilichoendela kufundishwa shuleni. Leo hii ndicho Kiswahili rasmi kinachofunzwa na wanafunzi na kuandikwa magazetini na vitabuni.

Miaka ya ukoloni ilisababisha kupokelewa kwa maneno mapya katika Kiswahili. Kijerumani kiliacha maneno machache kama "shule" (Kijerumani Schule) na "hela" (Heller) lakini maneno mengi sana ya asili ya Kiingereza yalipokelewa.

Kiswahili kimeonyesha uwezo mkubwa wa kupokea maneno kutoka lugha tofauti, kikitumia maneno haya kufuatana na sarufi ya Kibantu ya Kiswahili.

Mwalim Nyerere alivyochangia kukua kwa Kiswahili
HAYATI Mwalimu Julius Nyerere, ni miongoni mwa viongozi wanaokumbukwa kwa kuwa watetezi wa lugha na falsafa za Kiafrika, akiheshimika kwa juhudi kubwa za kukuza na kuendeleza Kiswahili katika jitihada za kuwaunganisha Watanzania na Waafrika pia.

Mchango wake ulianza wakati wa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Hii inajidhihirisha kwa kuangalia jinsi alivyotumia lugha ya Kiswahili kama chombo muhimu cha mawasiliano ambacho kiliwaunganisha Watanganyika kupigania na kudai uhuru.

MWALIMU Nyerere alitumia Kiswahili katika kampeni za kisiasa ambapo siasa na sera za TANU zilienezwa sehemu mbalimbali nchini kwa kutumia kiswahili. Matumizi ya lugha ya Kiswahili ni sababu mojawapo ya Tanganyika kupata Uhuru mapema na bila vikwazo vingi wale waliokuwa hawaifahamu na waliokuwa hawajui kusoma walipata nafasi ya kujifunza na kuelewa hatua za kudai uhuru zinavyokwenda na zilipofikia. Baada ya Uhuru,

Mwalimu Nyerere akiwa Waziri Mkuu wa kwanza alitangaza Kiswahili kuwa Lugha ya Taifa na kuagiza itumike katika shughuli zote rasmi za umma. Kwa kuonyesha msisitizo wa matumizi ya lugha hii, Nyerere alitoa hotuba ya kusherekea sikukuu ya Jamhuri tarehe 10, Desemba 1962, kwa Kiswahili.

Hatua hiyo ilidhihirisha na kukionyesha Kiswahili kama lugha asilia ambayo ilitumika ili kuondoa uwezekano wowote wa mafarakano yanayohusiana na mitafaruku ya kimatamshi.

Aidha, Mwalimu Nyerere alihutubia hafla nyingi kwa Kiswahili, hatua ambayo ilifanya kila mwananchi kuelewa mipango na mikakati ya serikali katika kuwaletea maendeleo yao. Kuanzia wakati huo Kiswahili kilianza kutumika katika shughuli zote za nyanja mbalimbali nchini kwa kuimarisha mahusiano ya makabila na kuifanya nchi kuwa kama kabila moja licha ya kuwa na zaidi ya makabila 120.

Hatua ya pili iliyochukuliwa na Mwalimu Nyerere ilikuwa ni kupitisha Azimio la Arusha mwaka 1967, aliposema kuwa ni mfumo wa “ujamaa na kujitegemea ndiyo sera ya taifa, hii ilikuwa ni njia muhimu ya kuwaunganisha Watanzania wote.

Matumizi ya Kiswahili yaliendelea kupanuka ambapo mnamo 1962, lugha hii ilianza kutumika rasmi bungeni na kwa upande wa elimu kilianza kutumika kufundishia masomo yote katika shule za msingi nchini huku Kiingereza kikibaki kufundishwa kama somo.

Mwalimu Nyerere alianzisha mpango wa Elimu ya Watu wazima, waliofundishwa kusoma na kuandika kwa Kiswahili, pia alianzisha maktaba za vijiji ambazo zilitumia vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Aidha kampeni mbalimbali za kitaifa zilizotangazwa na viongozi na kutekelezwa na wananchi zilitumia kaulimbiu za Kiswahili.

Mfano wa kampeni hizi ni ‘Siasa ni Kilimo’, ‘Mtu ni Afya’, ‘Kilimo cha Kufa na Kupona’ na ‘Madaraka Mikoani’.

Mwalimu Nyerere aliandika vitabu kwa Kiswahili, baadhi ya vitabu hivyo ni ‘TANU na Raia’ ‘Elimu Haina Mwisho’ na ‘Tujisahihishe’. Pia Mwalimu Nyerere alitafsiri kitabu cha ‘The Merchant of Venice’ cha William Shakespear kama ‘Mabepari wa Venis’ kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili.

Juhudi za Mwalimu Nyerere katika kukiendeleza Kiswahili zilikwenda mbali kwa kutoa idhini ya kuanzishwa kwa asasi mbalimbali za kushughulikia maendeleo ya Kiswahili nchini, zikiwamo Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (Tuki), Baraza la Kiswahili Tanzania (Bakita) na Umoja wa Kiswahili na Ushauri Tanzania (UKUTA).

Kiswahili leo Nchini Tanzania Kiswahili lugha rasmi ya serikali na taifa. Shule za msingi hutumia. Kiswahili lakini shule za sekondari na vyuo bado zinaendelea kufundisha kwa Kiingereza. Kiswahili kimezidi kuenea sehemu mbalimbali duniani na kuongeza idadi ya watumiaji. Juhudi za kukiendeleza zinapata msukumo kutoka marais walioongoza Tanzania baada ya Mwalimu kwa kusisitiza matumizi ya Kiswahili.

Kiswahili kwa sasa kinatumika katika nchi za Afrika Mashariki, kati na pembe ya Afrika. Baadhi ya nchi zinazotumia lugha hiyo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi Msumbiji, Zambia, Visiwa vya Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Kiswahili ni miongoni mwa lugha zinazozungumzwa sana hata Mashariki ya Mbali, na Ulaya na Marekani. Kiswahili barani Afrika ni lugha ya pili ya Kiafrika inayotumiwa na watu wengi ikitanguliwa na Kiarabu. katika eneo kubwa la Afrikakiswahili ina utajiri mkubwa wa misamiati, misemo, methali, mashairi, mafumbo, vitendawili na nyimbo. Kiswahili kinatumika kufundishia shuleni na kuna vitabu vingi vilivyotungwa kwa lugha ya kiswahili, vikiwa pamoja na vile vya hadithi, hekaya na riwaya.

Kiswahili ni lugha ya utawala serikalini Tanzania na mahakamani amabko mashauri yote husikilizwa kwa lugha ya Kiswahili,

Kiswahili kinatumika kote nchini, makanisani, misikitini, redioni, kwenye runinga na idadi kubwa ya magazeti.

Nchini Kenya:
Sera ya elimu ya mwaka 2015 imechagua Kiswahili katika miaka 10 ijayo kiwe lugha ya kufundishia katika ngazi zote, ikiwemo ile ya chuo kikuu Kenya: ni lugha ya taifa tena lugha rasmi, sawa na Kiingereza, baada ya rasimu ya katiba mpya kupitishwa tarehe 4 Agosti 2010;

Kiswahili ni lugha ya kwanza ya mawasiliano kati ya wananchi wakikutana nje ya eneo lenye kabila moja tu; ni lugha inayofundishwa lakini si lugha ya kufundisha mashuleni; ni lugha inayotumika na polisi na jeshi, ni lugha ya kuhutubia wananchi mjini na kitaifa; sehemu za ibada makanisani zinatumia Kiswahili; kuna gazeti moja tu la Kiswahili; sehemu za vipindi redioni na kwenye runinga ni kwa Kiswahili. Hata hivyo mara nyingi, lugha ya Kiswahili inachanganywa na Kiingereza na lugha za maeneo au za kikabila.

Nchini Uganda:
Kiswahili kimetangazwa kuwa lugha ya taifa tangu 2005; iliwahi kuwa lugha ya taifa wakati wa utawala wa Idi Amin; wakati wa ukoloni ilifundishwa mashuleni ikaelekea kuwa lugha rasmi pamoja na Kiingereza lakini matumizi haya yalipingwa hasa na Waganda hivyo Waingereza waliacha mipango hiyo.

Ni lugha ya polisi na jeshi, hali ambayo imeleta ugumu kwa lugha kukubalika na wananchi wengi kutokana na historia ya utawala wa kijeshi Uganda; watu wengi bado hukumbuka hasa matusi ya wanajeshi waliowatesa wakizungumza Kiswahili. Lakini kuna maeneo ya Uganda ambako Kiswahili kinatumiwa na watu wengi kama lugha ya sokoni na barabarani. Wona UBC, WBS tv.

Mwaka 2005 bunge lilipiga kura kukifanya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya pili kwa kuwa kinazungumzwa zaidi (nje ya Buganda).

Nchini Rwanda:
Tarehe 8 Februari 2017 bunge la Rwanda lilifanya Kiswahili lugha rasmi ya nne baada ya Kinyarwanda, Kifaransa na Kiingereza.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo:
Kiswahili ni kati ya lugha nne za kitaifa (pamoja na Kilingala, Kiluba na Kikongo), pia lugha ya jeshi. Kiswahili kilifika mashariki ya nchi ya DRC kupitia misafara ya wafanyabiashara ya watumwa na pembe za ndovu kutoka Zanzibar na pwani ya Tanganyika. Imeenea zaidi kati ya mchanganyiko wa wafanyakazi kwenye migodi ya Shaba.

Kimataifa
Lugha hii leo imekuwa na umuhimu mkubwa duniani kwa jumla, hasa Afrika, kwa sababu ya kuenea kwake nchi mbali mbali za ulaya zimeanzisha idhaa mbalimbali za Kiswahili zinazorusha matangazo yake Dunia nzima kwa lugha ya Kiswahili. ambazo zinachukuwa mahala pa lugha za kigeni za Wakoloni, kama Kiarabu, Kiurdu, Kiebrania, Kireno na kadhalika.

Leo Kiswahili kimekuwa kinatumiwa katika kusambaza habari katika vituo mbali mbali ulimwenguni kama vile Sauti ya Amerika, BBC, Deutsche velle, Monte Carlo, RFI, na nchi nyinginezo kama vile Uchina, Urusi, Irani.

Kiswahili kimekuwa ni mojawapo ya lugha muhimu zinazofundishwa katika vyuo vikuu nchini Marekani, Uingereza, Ulaya bara, Urusi, Uchina, na Nchi nyingi barani Afrika.

Maendeleo ya Kiswahili
Lugha ina maendeleo: inaweza kukua, kukwama au kufa. Athira nyingi hutokea bila mpangilio pale ambako wasemaji wanapokea maneno mapya, wanaacha kutumia maneno mengine au hubadilisha kawaida ya matamshi au sarufi. Haya yote hutokea pia katika uwanja wa Kiswahili.

Taasisi zinazokuza Kiswahili Tanzania
Kuna taasisi zinazolenga kukuza na kuimarisha Kiswahili kama vile Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na idara za Kiswahili katika vyuo vikuu vingine vya Kenya na pia Uganda.

Nchini Tanzania kuna Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) ilhali nchini Kenya kuna Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA). BAKITA na CHAKITA pamoja na wawakilishi kutoka Uganda wanaandaa kuundwa kwa Baraza la Kiswahili la

Afrika Mashariki (BAKAMA)
Uchunguzi wa Kiswahili huendelea pia katika idara za vyuo vikuu vingi duniani, kwa mfano katika Institute National des Langues et Civilisations Orientales, jijini Paris, Ufaransa. Matumizi yake ni kwa njia ya lahaja za Kingwana.

Faida za kutumia lugha ya Kiswahili zinatajwa kama ifuatavyo:

1. Husaidia kuleta umoja wa bara zima.

2. Hudumisha utamaduni wa Kiafrika kuliko kufuata kasumba.

3. Hufanya Waafrika waamini zaidi mambo yao kuliko kutegemea tu ya kigeni.

4. Hurahisisha mawasiliano baina ya watu wa Afrika Mashariki.

5. Husaidia kuwa na mahusiano ya kibiashara na watu mbalimbali.

6. Ni ishara ya kuwa huru na kushikamana.

7. Ni utambulisho wa jamii husika (utaifa).

8. Husaidia kukuza na kuendeleza sanaa.

9. Husaidia kuimarisha ulinzi na usalama katika taifa husika.

10. Husaidia kupata ajira katika vyuo na shule mbalimbali zinazofundisha lugha ya Kiswahili hata nje ya nchi.

11. Husaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wa lugha hiyo watakaofanya vizuri katika masomo kwa kuyaelewa zaidi.

12. Husaidia kuikuza na kuieneza ndani na nje ya jamii.

Kamusi za Kiswahili
Kati ya shughuli muhimu za taasisi hizo, mojawapo ni kazi ya kukuza misamiati ya Kiswahili yaani kutafuta maneno mapya au kupanua matumizi ya maneno yaliyopo ili kutaja mambo ya maisha ya kisasa yaliyobadilika. Utunzi wa kamusi za Kiswahili hupanua elimu hiyo.

Zifuatazo ni baadhi ya Kamusi za lugha ya Kiswahili
  • Kamusi ya Kiswahili ya Kwanza ya mwaka 1882

  • Kamusi ya Kiswahili Sanifu (imetungwa na TATAKI, awali TUKI)

  • Kamusi la Kiswahili Fasaha (KKF), (imetungwa na BAKIZA

  • Kamusi ya Karne ya 21 (KK21). Nairobi, Kenya

  • Kamusi Teule ya Kiswahili (KTK).

  • Kamusi Kuu ya Kiswahili (KKK). (imetungwa na BAKITA)

  • Kamusi Sanifu ya Kompyuta (KSK),

  • Kamusi Sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia

  • Kamusi ya Tiba (KyT),

  • Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha

  • Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha,

  • Kamusi ya Tashbihi, Vitendawili, Milio na Milingano,

  • Kamusi ya Fasihi. Istilahi na Nadharia,

  • Kamusi ya Historia - TUKI,

  • Kamusi ya Methali,

  • Kamusi Fafanuzi ya Methali,

  • Kamusi ya Biashara na Uchumi

  • Kamusi ya Tiba (TUKI)

  • Kamusi ya Ndege kwa Picha, TUKI

  • Kamusi ya Wanyama - TUKI

  • Kamusi ya Semi,

  • Kamusi ya Semi,

  • Kamusi ya Visawe,

  • Kamusi ya Ukristo, Mkuki na Nyoka,

  • Kamusi ya Kiswahili - Kiingereza

  • Kamusi Awali ya Sayansi na Tekinolojia (

  • A Standard Swahili-English Dictionary
Mafanikio ya Kiswahili nchini yametokana na juhudi kubwa za Mwalimu Nyerere ambaye mpaka leo anakumbukwa kwa kukienzi. Katika kuunga mkono jitihada zake, Watanzania wanapaswa kujivunia juhudi hizi na kuwa mstari wa mbele katika kukiendeleza na kukitumia kama utambulisho wao ili kukieneza pamoja na kutangaza utamaduni wa taifa. Lugha ya Kiswahili.

Rais wa Tanznaia Dkt John Pombe Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha matumizi ya lugha ya Kiswahili Afrika na Duniani. Akitambua kwamba Tanzania ndipo Kiswahili kilipoanzia na asili ya Kiswahili ni nchini Tanzania.

MWISHO ]]>
Lugha ya Kiswahili imeanza takriban miaka 1000 iliyopita kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki. Neno Swahili lina asili ya Kiarabu: Sahil ina maana ya pwani; sawahil ’’ a-sawāhilī’’ ni wingi wake kwa kumaanisha yote yanayohusiana na pwani, watu au utamaduni na lugha ya eneo la pwani. Kiswahili kilianza kama lugha ya miji na bandarini wakati wa biashara ya kimataifa kwenye pwani ya Afrika ya mashariki.

<![CDATA[Maneno ya Kiswahili yaliyotoholewa kutoka Lugha mbalimbali za kigeni]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2527 Tue, 26 Apr 2022 10:07:22 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=2527
Kiingereza

Oveni, Soseji, Supu, Chizi, Shati, Sketi, Pini, Hereni, Herini, Burashi, Brashi, Stovu, Mota, Muoki, Kisi, Televisheni, Basi, Plastiki, Injini, Kangaruu, Kalenda, Koti, Buti, Helmeti, Skuli, Skrubu, Sukurubu, Namba, Nambari, Bumarengi, Redio, Savana, Daktari, Bia, Kola, Taulo, Bili, Baisikeli, Mashine, Hospitali, Benki, Sinki, Buluu, Bluu, Familia, Nta Ya Sikio, Gauni, Soksi, Glavu, Glovu, Blangeti, Blanketi, Plau, Sepetu, Sepeto, Reki, Ekseli, Faini, Betri, Polisi, Peremende, Pipi, Bomu, Filamu, Muziki, Gazeti, Sleji, Motokaa, Eropleni, Treni, Fanya Mapenzi, Gluu, Feni, Dansi, Kona, Wiki, Jaji, Jela, Jagi, Leseni, Skii, Kadi, Gamu, Breki, Stempu, Mota, Chokaa n.k

Kihindi:

Duka, Rangi, Sanduku, Bakuli, Jangili, Bata, Barafu, Kaka, Babu, Bibi, Mbuzi, Beberu, Kasuku, Goti, ****, Shela, Bangili, Bungalow, Bangiri, Dirisha, Taa, Ngano, Mwanzi, Muwa, Gundi, Bati, Patasi, Gari, Meli, Nanga, Rangi, Manjano, Namna, Godoro, Bisibisi, Dafu, Hodari, Ngalawa, Jina, Khaki, Kama, Cheti, Pesa, Kodi, Baba, Bahari, Bahati (Njema), Bandari, Barabara, Bunduki, Chai, Chokaa, Chapati, Pilau, Biriani, Dawa, Desturi, Dini, Duka, Dusumali, Hakimu, Hewa, Hori, Jahazi, Kahaba, Kahawa, Karakana, Kazi, Kiberiti, Kufuli, Lozi, Mashua, Meza, Msala, Msumari, Ndimu, Njaa, Pilipili, Popoo, Sabuni, Sanamu, Serikali, Sherisi, Sonobari, Sultani, Suruali, Tayari, Tufani, Tumbaku, Valanda, Wakati, Wazi, Waziri.

Kiarabu:

Aljebra, Alogarithim, Alkali, Karatasi, Dunia, Bara, Bahari, Rasi, Radi, Soda, Sofa, Spinachi Tufani, Giza, Kiza, Umande, Hewa, Theluji, Kiberiti, Arusi, Harusi, Talaka, Baba, Dada, Yatima, Jamaa, Fahali, Farasi, Baghala, Bata, Tai, Samaki, Papa, Simba, Dubu, Ngamia, Mdudu, Damu, Titi, Jasho, Jamii, Hai, Maiti, Kaburi, Swahili, Dhaifu, Afya, Homa, Usaha, Dawa, Sumu, Njaa, Kaba, Birika, Bakuli, Sahani, Tasa, Gudulia, Tini, Zabibu, Lozi, Zeituni, Pilipili, Asali, Sukari, Jibini, Siagi, Sufu, Gitaa, Futari, Afriti, Yasmini, Kitani, Hariri, Maharazi, Joho, Suruali, Kofia, Hema, Sakafu, Dohani, Mshumaa, Rafu, Hori, Tofali, Bustani, Mfereji, Nafaka, Shayiri, Tumbaku, Ndizi, Kazi, Kamba, Kemia, Kata, Mkasi, Makasi, Seremala, Msumari, Subu, Dhahabu, Fedha, Shaba, Risasi, Kikapu, Zulia, Sanamu, Rudi, Daraja, Nira, Kafi, Usukani, Bandari, Miliki, Haribu, Tafuta, Sarafu, Tajiri, Dai, Deni, Ajiri, Mshahara, Soko, Duka, Bei, Ghali, Baada, Kabla, Mahali, Kilele, Karibu, Mashariki, Magharibi, Kaskazini, Kusini, Kulabu, Msalaba, Mraba, Mstari, Sifuri, Sita, Saba, Tisa, Ishirini, Mia, Elfu, Hesabu, Zaidi, Umati, Sehemu, Nusu, Jozi, Wakati, Umri, Sasa, Haraka, Tayari, Abadani, Tena, Asubuhi, Adhuhuri, Alasiri, Saa, Juma, Alhamisi, Ijumaa, Majira, Ladha, Tamu, Laini, Baridi, Safi, Roho, Bahati (Njema), Furahi, Tabasamu, Busu, Huzuni, Wasiwasi, Juta, Huruma, Kasirika, Aibu, Thubutu, Jasiri,

Kiajemi

Mama, Tandu, Kasa, Paja, Chungu , Haragwe, Pamba, Sindano, Chana, Barabara, Gurudumu, Bwana, Malaya, Boma, Balungi, Bandari, Baba, Babu, Bahari, Bahati (Njema), Bara, Barabara, Barafu, Barakoa, Bata, Bibi, Bunduki, Bustani, Chai, Cheti, Dada, Desturi, Dirisha, Duka, Dusumali, Gari, Hodari, Jahazi, Jamvi, Joho, Kahaba, Kaka, Kamba, Karakana, Kazi, Kilele, Kitani, Mbuzi, Mdudu, Meza, Msikiti, Msumari, Namna, Nanga, Ndimu, Ngano, Ngano, Ngano, Njaa, Pilipili, Popoo, Rangi, Serikali, Sherisi, Simu, Siwa, Stadi, Suruali, Tasa, Tayari, Tofali, Tufani, Tufe, Tumbaku, Wazi, Waziri, Kodi, Tasa, Joho, Dirisha, Bustani, Bandari, Bahati (Njema), Desturi, Serikali, Karakana, Dusumali, Barabara, Stadi]]>

<![CDATA[NADHARIA MBALIMBALI KUHUSU HISTORIA YA KISWAHILI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1751 Thu, 16 Dec 2021 03:28:29 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1751
  Kiswahili Asili Yake ni Kongo
Baadhi ya wataalamu hudai kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni huko Kongo ambayo baadaye iliitwa Zaire na sasa inaitwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Dai hili linaimarishwa na wazo lingine linalodai kwamba katika vipindi kongwe vilivyopata kuwako, sehemu za Pwani ya Afrika mashariki hazikuwa zimekaliwa na watu. Kutokana na hali ya vita, uchungaji na biashara, inadaiwa kuwa Wabantu walitoka sehemu za Kongo walisambaa na kuja pwani ya Afrika mashariki kupitia Kigoma. Baadhi ya wabantu hawa walipitia sehemu za Uganda. Wakati wa kusambaa kwao, walieneza pia lugha zao ikiwemo hii ya Kiswahili.

Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba, madai ya kuwa asili ya Kiswahili ni Kongo hayana msingi kwani mpaka sasa wataalamu wanaodai hivi hawajaweza kueleza na kuthibitisha kisayansi ama Kihistoria juu ya lini hasa watu walianza kuishi pwani ya Afrika mashariki.

  Kiswahili ni Ki-Pijini au ni Ki-Krioli

(i)    Kiswahili ni Ki-Pijini
Baadhi ya wataalamu hudai kuwa Kiswahili ni Ki-Pijini. Wataalamu hawa hudai kwamba Ki-Pijini ni lugha ambayo huzaliwa kutokana na kukutanika  kwa makundi mawili (A) na (B) yanayotumia lugha mbili tofauti. Ili makundi haya yaweze kuwasiliana kunaundwa lugha ambayo kitabia ni tofauti  na zile zinazozungumzwa na makundi yanayohusika. Lugha hii inaweza kuwa na msamiati mwingi kutoka lugha kati ya zile mbili, au inaweza kuwa na msamiati wenye uzito sawa. Lugha hiyo ndiyo inayoitwa Ki-Pijini. Mazingira yanayosababisha kuwepo Ki-Pijini ni kama vile biashara, utumwa, ukoloni, nk.

Kwa mantiki ya nadharia hii, wataalamu hawa hukiona Kiswahili kuwa kilianza kama Ki-Pijini kwani ni tokeo la mwingiliano baina ya wenyeji wa pwani ya Afrika Mashariki na wageni wa kutoka Mashariki ya Kati, hususan Waarabu. Aidha, husisitiza kuwa lugha ya Kiswahili haikuwepo kabla ya hapo.

(ii)    Kiswahili ni Ki-Krioli
Wataalamu hawa wanadai kwamba watu wanaozungumza Ki- Pijini wanaweza kuishi pamoja kwa muda wa karne nyingi na kwa hiyo wakaweza kuzoeana na hata kufikia hatua ya kuoana. Wakioana watoto wao huikuta lugha ya ki-Pijini ama lugha yao ya kwanza. Inapofikia hatua ya aina hii kwa watoto wanaozungumza lugha hiyo, wao husemekana sasa  wanazungumza lugha ya Ki-Krioli, lugha ambayo ni hatua ya juu ya Ki-Pijini, yaani Ki-Pijini kilichokomaa.

Nadharia hii hutumia kigezo cha msamiati wa Kiswahili kuonesha uhusiano uliopo kati ya Kiswahili na Kiarabu. Wanadai kuwa, msamiati mwingi wa Kiswahili unatokana na Kiarabu. Hivyo huhitimisha kuwa hapana shaka Kiarabu kimehusika katika kuizalisha na kuikomaza lugha ya Kiswahili.

Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba hutumia kigezo cha msamiati tu bila kuzingatia vipengele vingine vya lugha kama vile matamshi, maumbo ya maneno au muundo wa sentensi za Kiswahili. Aidha, wataalamu hawa hawakuhoji suala la kufanana kwa Kiswahili na lugha jirani katika hayo yaliyotajwa hapo juu na katika eneo la Kijografia ambamo Kiswahili na lugha hizo nyingine hujikuta zikizungumzwa. Vigezo hivi ni ushahidi tosha unaoonesha kuwa Kiswahili SI Ki-Pijini wala SI Ki-Krioli, bali ni lugha kama zilivyo hizo lugha jirani.

  Kiswahili ni Lugha ya Jamii ya Vizalia
Kundi la kwanza la wataalamu wa nadharia hii, Bishop Edward Steera, Bwana Taylor, Dkt. R. Reusch, (Katika Maganga, 1997)  hudai kwamba:

·        Waarabu na Waajemi waliohamia pwani ya Afrika ya Mashariki waliwaoa wanawake wa  ki-Afrika.

·        Watoto wao walijifunza maneno ya Kiarabu na ki-Ajemi kutoka kwa baba zao.

·        Aidha, watoto hao wakajifunza maneno ya ki-Bantu kutoka kwa mama zao.

·        Katika jitihada zao, watoto hao walijirekebisha kutokana na  tamaduni za wazazi wao ambazo ni tafauti: utamaduni wa Kiarabu na utamaduni wa ki-Bantu.

·        Vizalia hawa wakaanza kutumia lugha mpya ya mseto wa Kiarabu, Kiajemi na lahaja mbalimbali za ki-Bantu.

·        Kwa kiasi kikubwa, lugha mpya ya mseto ilikuwa ni upotoshaji wa lugha ya Kiarabu na Kiajemi.

·        Mwarabu au Mu-Ajemi alikuwa muumini wa dini ya Uislamu.

·        Umo humo, vizalia hawa wakayaingiza maneno ya Kiarabu, Kishirazi na Kihindi katika hii lugha mpya.

·        Pamoja na kuyaingiza maneno ya kigeni, lugha-mpya yao hii (Kiswahili), ilikithiri vionjo vingi vya lugha mbali mbali za ki-Bantu.

·        Ndipo baadaye, lughampya yao hii ikajulikana au kuitwa Kiswahili.

·        Kwa maoni ya wataalamu hawa, sehemu mbili kati ya tano (2/5) ya maneno yanayotumika katika lugha hii mpya ni ya ki-Bantu.

·        Sarufi ya lugha mpya hii ni mseto wa ki-Bantu (chenye utata na kisicho na mpangilio maalumu) pamoja na Kiarabu (chenye mantiki na kilichokomaa).
         
Kundi la pili la wataalamu wa nadharia hii, B. Krumm na F. Johnson lina mawazo yanayodai kwamba:
·        Kiswahili kilitokana na visiwa vya Lamu, Kilamu/Kiamu.

·        Wageni kutoka Ghuba ya Ushirazi/Uajemi na Arabia ya Kusini walikuja katika Pwani ya Afrika ya Mashariki na lugha tofauti.

·        Lakini kutokana na kuoana kwao na wenyeji, wageni hawa wakaichukua lugha ya hapo walipofikia, wakaikuza kwa maneno kadhaa na sentensi kadhaa kutoka lugha zao za asili, yaani Kiarabu, Kiajemi na Kihindi hususan katika masuala ya  biashara, ubaharia, vyombo vya kazi zao na nguo.

·        Aidha,  utumwa na tabia ya kuoa wake wengi ilisaidia kutoa kundi kubwa la masuria. Hali hii ikaondosha hisia za ugeni katika lugha zao; na maneno yote yakabatizwa kuwa ya ki-Bantu, na hata kupoteza kabisa sura ya ugeni.

  Kiswahili ni Kiarabu
Kuna hoja kuu tatu ambazo baadhi ya wananadharia hii huzitumia kutetea nadharia hii kuwa Kiswahili asili yake ni Kiarabu.
(i)          Inadaiwa kuwa maneno yenye asili ya Kiarabu yaliyomo katika Kiswahili ni ishara tosha kwamba lugha hii ilianza kama Pijini ya Kiarabu.

(ii)      Inahusu neno lenyewe Kiswahili ambalo asili yake ni Kiarabu. Neno Kiswahili linatokana na neno “sahili” (umoja) na “swahil” (wingi) lina maana ya pwani.

(iii)    Inadaiwa kwamba kwa kuwa Kiswahili kilianza pwani, kwa kuwa idadi kubwa sana ya wenyeji wa pwani ni waislamu, na kwa kuwa uisilamu uliletwa na Waarabu, basi Kiswahili nacho kililetwa na Waarabu.

  Kiswahili si Kiarabu
Madai kwamba Kiswahili si Kiarabu yanathibitishwa na hoja kinzani zifuatazo:

Tukianza na dai la kwanza ‘kwamba maneno yenye asili ya Kiarabu yaliyomo katika Kiswahili ni ishara tosha kwamba lugha hii ilianza kama pijini ya Kiarabu’ tunaona wazi kwamba madai haya hayana mashiko. Lugha ya Kiswahili imetokea kuwa na maneno ya mkopo yenye asili ya Kiarabu (na kwa hakika yapo yenye asili ya Kiajemi, Kireno, Kihindi, Kijerumani, Kiingereza nk.) kutokana na ukweli kwamba kulikuwa na mawasiliano ya karne na karne baina ya wenyeji wa pwani na wafanyabiashara wa Kiarabu. Wasemaji wa lugha mbili tofauti wanapokutana hawaachi kuathiriana kilugha. Kwa hiyo lugha kuwa na maneno mengi ya mkopo kutoka lugha nyingine, haifanyi lugha hiyo isemekane kuwa imetokana na hiyo lugha nyingine.

Pili wataalamu hawa wanadai kwamba neno lenyewe Kiswahili lina maana ya Kiarabu.

Kwani linatokana na neno “sahili” (umoja) na “swahil” (wingi) lina maana ya pwani. Hapa ingetupasa tuelewe kwamba kila mtu binafsi au jamii binafsi aghalabu hajiiti mwenyewe jina lake, yeye huitwa kwa hilo jina alilopewa na wengine: Jamii yake au wageni waliomtembelea kwake. Na hivi ndivyo ilivyojitokeza kwa upande wa jamii ya watu wa pwani ya Afrika mashariki, yaani Waswahili,  walipotembelewa na Waarabu na kuitwa As-Sahilyy au As-Sawahiliyy, na nchi yao kuitwa sahil (wingi wake Sawahil), yaani pwani (upwa), ufuo. Kwa mantiki hii, dai hili halina mashiko !

Kigezo cha dini nacho hakikubaliki lugha haiwi lugha kwa sababu ya imani. Hata hivyo lugha ya Kiarabu yenyewe ilikuwepo karne nyingi kabla ya kufunuliwa dini ya Uislamu. Hali kadhalika, lugha nyingine za Kimagharibi zilikuwepo karne nyingi kabla ya kufunuliwa imani ya ukristo. Kama ilivyo kwamba Kiingereza au Kijerumani si ukristo, basi ndivyo vivi hivyo ilivyo kwamba Kiswahili hakiwezi kuwa dini ya uislamu, aslan! Wala Kiarabu nacho si uislamu. Tunachoweza kufanya ni kuitumia lugha kuifasili dini, lakini hatuwezi kuitumia dini kuifasili lugha.

  Kiswahili ni Kibantu
Vipengele vinavyotumika katika kuihalalisha nadharia inayodai kwamba Kiswahili ni Kibantu ni ushahidi wa ki-Isimu, ushahidi wa ki-Historia na kuichunguza lugha ya Kiswahili katika mfumo mzima wa historia ya mgawanyiko wa kusambaa kwa lugha za ki-Bantu. Wataalamu wa nadharia hii wanahitimisha kwa kudai kwamba Kiswahili ni mojawapo kati  ya lugha katika jamii kubwa ya lugha za ki-Bantu.

Baadhi ya wataalamu muhimu wanaoiunga mkono nadharia hii ni Prof. Malcon Guthrie, Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl na Prof. Clement Maganga.

Profesa Malcom Guthrie ni mtaalamu (mwanaisimu) mashuhuri kutoka Chuo Kikuu cha London, Uingereza. Alitumia miaka 20 kuchunguza uhusiano uliopo baina ya lugha za Kibantu zilizoko katika eneo lote ambalo hukaliwa na wabantu. Sehemu hii ni ile ambayo inajulikana kama Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Alifanya uchunguzi wa mashina/mizizi (viini) ya maneno 22,000 kutoka lugha 200 za Kibantu. Katika uchunguzi wake alikuta mizizi (mashina) 2,300 imezagaa      katika lugha mbalimbali za Kibantu na Kiswahili kikiwemo. Mashina/mizizi 500          yalilingana katika lugha zote 200. Mashina haya yalipatikana katika lugha zote za Kibantu. Mashina haya yalikuwa ya asili moja. Baadhi ya lugha hizo 200 zilizofanyiwa uchunguzi Kiswahili kilionesha kuitikia ulinganifu sawa na Kikongo kwa asilimia arubaini na nne (44%).

Katika kuchunguza ni asilimia ngapi za mashina hayo 500 yaliyomo katika kila lugha, mgawo uliojitokeza ulikuwa kama ifuatavyo:

Kiwemba kizungumzwacho Zambia        -          54%
Kiluba kizungumzwacho Katanga            -          51%
**Kikongo kizungumzwacho Zaire          -          44%**
**Kiswahili kizungumzwacho Afrika Mashariki            44%**
Kisukuma kizungumzwacho Tanzania                41%
Kiyao kizungumzwacho Tanzania/Msumbiji -  35%
Sotho kizungumzwacho Botswana                        -          20%
*Kirundi kizungumzwacho Burundi        -          43%*
Kinyoro kizungumzwacho Uganda          -          37%
Kizulu kizungumzwacho Afrika Kusini  -          29%

Baada ya kupata matokeo haya, Profesa Malcom Guthrie anaiunga mkono nadharia hii ya kwamba Kiswahili ni ki-Bantu kwa kudai kwamba:
(i)    Kiswahili kilikuwepo kabla ya ujio wa wageni;
(ii)    Anaonyesha kwamba Kiswahili kina uhusiano mkubwa na lugha za Kibantu;
(iii)  Mwisho anasema Kiswahili kilianzia Pwani ya Afrika Mashariki.
         
Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl: Wataalamu hawa wanaamini kwamba:
(i)                Wakati wa utawala wa Shirazi katika upwa wa mashariki ya Afrika kulikuwa na kabila la Waswahili;

(ii)            Kabila hili ni dhuria ya Wazaramo wa leo.

(iii)          Kwa kuwa hawa Wazaramo walikuwa wamezaliwa katika harakati za kibiashara, kwa hivyo wakafuata nyayo za wazazi wao.

(iv)          Lugha yao ilikuwa ya aina ya ki-Bantu.

(v)              Kwa kuwa Wabantu ni wengi zaidi kuliko jamii ya makabila mengine, lugha yao ya Kiswahili ikaanza kutumika na kuenea katika makabila mengine, hususan katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki.

(vi)          Baadaye, Waswahili hawa hawa wakafanya biashara na wageni waliokuja kuvinjari Afrika Mashariki, hususan Waarabu, Washirazi, Wamalaysia, Wahindi na Wareno ambao tayari walikuwa wamefurika katika pwani hii ya Afrika Mashariki miaka kadhaa kabla.
(vii)        Vifaa na majina ya vitu vya biashara vya wageni hao vikaselelea na kuingizwa katika mfumo wa lugha hiyo ya Waswahili ambayo ni ki-Bantu.

Madai ya nadharia hii yakichunguzwa, tunagundua kwamba inazingatia mitazamo miwili yaani, mtazamo wa ki-Isimu na mtazamo wa ki-Historia. Kwa mantiki hii, nadharia hii inaelekea kukubalika na wataalamu wengi kuwa ndiyo sahihi kuhusu asili au historia ya Kiswahili.

Profesa C. Maganga, na uthibitisho wake kwamba Kiswahili ni ki-Bantu. Kama tulivyoona, lugha ya Kiswahili ilifanyiwa utafiti na uchambuzi na wanataaluma kadhaa kwa madhumuni ya kuiainisha kama ilikuwa yenye misingi ya ki-Bantu au la. Prof. Maganga alifanya uchambuzi wa ki-Isimu na wa ki-Historia kuhusu lugha hii. Matokeo ya utafiti wake wa ki-Isimu kuhusu lugha ya Kiswhili (au lugha kwa ujumla) unadhihirisha mambo mengi, mojawapo ni asili ya lugha hiyo. Amethibitisha kwamba Kiswahili ni lugha ya Kibantu; na kwa hivyo, kuthibitisha kwa ushahidi thabiti hoja ya Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl kama  tulivyoieleza hapo juu.

(i)        Ushahidi wa Kiisimu
(a)      Msamiati
Matokeo ya utafiti alioufanya kuhusu msamiati wa Kiswahili ulibaini kwamba 60% ya maneno yote yanayoweza kuandikwa na kutamkika katika lugha ya Kiswahili asili yake ni lugha za Kibantu, 30% ni lugha ya Kiarabu na 10% ni lugha nyingine za kigeni kama vile Kiingereza, Kireno, Kijerumani, Kihindi, Kiajemi, Kifaransa, nk. Kinyume chake ni kwamba msamiati wa Kiswahili na ule wa Kibantu hautofautiani.

Mfano:
            Kiswahili  Kindali  Kizigua  Kijita  Kikurya  Kindendeule         
            Mtu          Umundu    Mntu      Omun      Omontu      Mundu
            Maji        Amashi      Manzi    Amanji    Amanche    Maache
            Moto        Umulilo    Moto        Omulilo  Omoro        Mwoto

(b)      Tungo (Sentesi) za Kiswahili
Miundo ya tungo (sentesi) za maneno ya Kiswahili zinafanana sana na miundo ya tungo za maneno ya ki-Bantu. Sentesi za Kiswahili na za lugha za ki-Bantu zina kiima  na kiarifu.

Mfano:
Lugha za Kibantu              Kiima                        kiarifu
Kiswahili                              Juma                          anakula ugali.
Kizigua                                  Juma                          adya ugali.
Kisukuma                              Juma                          alelya bugali
Kindali                                  Juma                          akulya            ubbugali.
Kijita                                      Juma                          kalya  ubusima.
Kindendeule                        Juma                          ilye ughale.
©      Ngeli za Majina
Wanataalamu wanakubaliana kuhusu ngeli za majina kwa mujibu wa:
maumbo ya nomino (umoja na wingi wa majina) pamoja; na
upatanisho wa kisarufi katika sentesi.

Kigezo cha maumbo ya majina: Kigezo hiki hufuata maumbo ya umoja na uwingi katika kuyaainisha majina. Majina yaliyo mengi katika lugha ya Kiswahili na lugha za ki-Bantu hufuata mkondo wa umoja na uwingi. Majina ya lugha ya Kiswahili na lugha za ki-Bantu yaliyo mengi yana maumbo dhahiri ya umoja na uwingi.

Mfano:
Lugha za Kibantu              Umoja                        Wingi
Kiswahili                              mtu                -          watu
                                                mtoto              -          watoto
Kikurya                                  omanto          -          banto (abanto)
                                                omona                        -          bana    (abana)
Kizigua                                  mntu              -          bhantu
                                                mwana            -          bhana
Kindali                                  mundu            -          bhandu
                                                mwana            -          bhana
Kindendeule                        mundu            -          βhandu
                                                mwana            -          βhana

Kigezo cha upatanisho wa kisarufi katika sentesi: Katika kigezo hiki tunaangalia uhusiano uliopo kati ya kiima (jina na viambishi awali vya nafsi) na vivumishi katika vitenzi vya Kiswahili na ki-Bantu. Vivumishi, majina pamoja na viambishi hivyo vya vitenzi hubadilika kutokana na maumbo ya umoja na uwingi.

Mfano:
Lugha za Kibantu      Umoja                    -                      Wingi
Kiswahili                      Baba analima        -                      Baba wanalima
Kindali                          Utata akulima        -                      Abbatata bbakulima
Kikurya                        Tata ararema          -                      Batata(Tata)bararema
Kijita                            Tata kalima                        -                      Batata abalima
Kindendeule                Tate ilima              -                      Akatate βhilima

(d)      Vitenzi vya Kiswahili na Kibantu
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vitenzi vya Kiswahili na vile vya lugha zingine za ki-Bantu. Vipengele vinavyothibitisha uhusiano huu ni: Viambishi, mnyumbuliko, pamoja na mwanzo au mwisho wa vitenzi, kama ifuatavyo:

Viambishi: vitenzi vya lugha ya Kiswahili na vya lugha zingine za ki-Bantu hujengwa na mzizi (kiini) pamoja na viambishi vyake vya awali na vya tamati.

Mfano:

Kiswahili      -          analima          =          a – na – lim -  a
Kiikuyu          -          arerema          =          a  –  re –  rem–a
Kindali          -          akulima          =            a  - ku  –  lim – a
                                                                          1  -  2  -  3  -  4
Sherehe:
1  -    Kiambishi awali kipatanishi cha nafsi.
2  -    Kiambishi awali cha njeo (wakati uliopo).
3  -    Mzizi/Kiini.
4  -    Kiambishi tamati.

Mnyambuliko wa vitenzi: Mnyumbuliko wa vitenzi vya Kiswahili hufanana na ule wa vitenzi vya lugha za ki-Bantu.

Mfano:       

Kiswahili      -          kucheka        -          kuchekesha  -          kuchekelea.
Kindali          -          kuseka            -          kusekasha      -          kusekelela.
Kibena          -          kuheka          -          kuhekesha    -          kuhekelea.
Kinyamwezi  -          kuseka            -          kusekasha      -          kusekelela.
Kikagulu        -          kuseka            -          kusekesha      -          kusekelela

Mwanzo wa vitenzi: Vitenzi  vyote vya Kiswahili na vile vya lugha za ki-Bantu huanza na viambishi ambavyo ni viwakilishi vya nafsi, kama ifuatavyo:

Mfano:

Kiswahili      -          Ni-nakwenda
Kihaya          -          Ni-ngenda
Kiyao            -          N-gwenda
Kindendeule -          Ni-yenda

Mwishilizo wa vitenzi: Vitenzi vya lugha za ki-Bantu na Kiswahili huishia na irabu –a.

Mfano:

Kiswahili      kukimbi-a      -          kuwind-a      -          kushuk-a
Kindali          kukind-a        -          kubhing-a      -          kukol-a
Kisukuma      kupil-a          -          kuhwim-a      -          Kutend-a
Kisunza          kwihuk-a      -          kuhig-a          -          kising-a
Kindendeule kuβhutuk-a    -          kuhwim-a      -          kuhuk-a

tafiti wa Prof. Maganga kuhusu ushahidi wa ki-Isimu wa kuthibitisha kama Kiswahili ni ki-Bantu au la ungeweza kuelezwa kimuhtasari kwa mifano mingine ifuatayo:

Mfano wa 1:

Lugha
Sentesi
Kiswahili
Kipare
Kindamba
Kichaga
Kihaya
Kikaguru
Kindendeule 
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
anafuga
erisha
kafugha
nao he
n’afuga
kachima
ifuga
mbuzi
mbuji
mene
mburu
embuzi
m’ehe
mbuhi
kuku
nkuku
nguku
nguku
enkoko
ngu’ku
nguku
na
na
na
na
n’
na
na
ng’ombe
ng’ombe
senga.
umbe
ente
nn’ombe
ng’ombe

Katika mfano huu inaonekana kwamba mpangilio wa maneno katika sentesi una ufanano kwa sababu katika kila sentesi kuna kiima na kiarifu. Katika kiima kuna nomino, yaani jina la mtenda (Jongo) na katika kiarifu kuna kitendo kinachofanyika na nomino mtendwa. Pia nafasi ya viunganishi ni ile ile kwa lugha zote zilizoonyeshwa katika mfano huu.

Kuna mfano mwingine wa ufanano wa mpangilio huu.

Mfano wa 2:

Lugha
Sentesi
Kiswahili
Kihaya
Kisukuma
Kinyaturu
Kipare
Kizigua
Sitamkuta kesho
Timushangemu nyenkya
Natusanga intondo
Tumuhanga fadyu
Nesikemkiche yavo
Sirambila luvi

Katika sentensi hizo mpangilio wa maneno una ufanano kwa sababu kila sentensi ina kiima na kiarifu chenye kitenzi na kielezi. Pia kiambishi cha nafsi cha nomino ya mtenda kinajitokeza mwanzoni mwa neno la kwanza la kila sentesi.
Sitamkuta;    Timushangemu;        Natusanga;                                                                            Tumuhanga;            Nesikamkiche;                      Sitambila.

Viambishi hivyo vya nafsi ya mtenda pia vinaonyesha hali ya ukanushi katka kila sentesi na nafasi yake ni ile ile kwa kila sentesi.

Viambishi vya urejeshi navyo vinajitokeza katika kitenzi cha kila sentesi.

Viambishi {m}, {m}, {ti}, {tu} sitamkuta, timushangemu, natusanga, tumuhanga, nesikamkiche, na sitambwila ni vya urejeshi; vinawakilisha nomino mtendwa.

Kwa hivyo, hali hii inadhihirisha kwamba miundo ya sentensi hizi inafanana na vitenzi vyake vina tabia mbalimbali, kama vile:

(i)        kubeba viambishi vya nafsi, mtenda na mtendwa,

(ii)      kuonyeshga hali ya ukanushi njeo za wakati na kitendo kinachofanyika.

Mfano wa 3:

Lugha                 
Sentesi
Kiswahili
Kizigua
Kihaya
Kisukuma
Kinyaturu
Kipare
Kindendeule
Akija mwambie anifuate
Akeza umugambe anitimile.
Kalaija omugambile ampondele
Ulu nahali anikubije
Newaja mwele ang’onge.
Ekiza umti aniratere
Anda ahikite n’nongerera angobhekeraye

Katika sentesi hizo inaonekana kwamba sentesi zote zinafanana  kimpangilio. Pia maneno yake yanakubali uambishaji, kwa mfano:

(i)        Katika maneno ya mwanzo:
            akija, akeza. kalaija, akuja, newaja, ekiza, herufi zilizopigiwa vistari ni viambishi vya nafsi vinawakilisha dhana ya mtenda.

(ii)      Vivyo hivyo katika maneno:
anifuate, ampondele, anitimile, ang’nge, aniratere, angobhekeraye, viambishi vilivyoko katika viarifu vya sentesi hizo vinawakilisha nafsi za watenda.

(iii)    Pia vitenzi vya sentesi hizo vina tabia ya kubeba virejeshi vya nafsi kama ilivyo katika, mwambie, omugambile, nahali,mbwele na umti, vinaonyesha njeo na hali ya uyakinifu- hali inayoonyesha ufanano wa maumbo ya maneno.

(iv)      Licha ya kuwa na mpangilio unaofanana na wa lugha nyingine za kibantu, kwa mfano, katika mifano tuliyoiona hapo juu, baadhi ya maneno yanafanana: tazama maneno:
            kafugha (Kindamba); nafuga  (Kihaya);
            nifuga (Kindendeule); anafuga  (Kiswahili).

Pia maneno:

            nkuku  (Kipare);                  nguku (Kindamba);
            nguku  (Kichaga);              enkoko  (Kihaya);
            ng’uku  (Kikaguru);                        nguku(Kindendeule);
            nguku    (Kindendeule)

Katika mfano wa 3, maneno yafuatayo yana ufanano:

Akeza  (Kizigua);                kalaija  (Kihaya);    alize  (Kisukuma),
newaja  (Kinyaturu);          ekiza  (Kipare);      anda ahikite,... (Kindendeule);
akija,  (Kiswahili.)

Pia maneno;

umugambe  (Kizigua);        omugambile  (Kihaya);      unongeraye (Kindendeule);  na mwambie (Kiswahili).

Ufanano huu wa msamiati, maumbo ya maneno pamoja na wa mpangilio wa maneno katika sentesi, vyote vinathibistisha kwamba lugha ya Kiswahili ni ya kibantu kama zilivyo nyingi nyinginezo.

(ii)    Ushahidi wa Kihistoria Kwamba Kiswahili ni Kibantu
Baada ya kuangalia ushahidi wa kiisimu kuhusu asili ya Kiswahili, katika sehemu hii Maganga (1997) aliendelea kuchambua ushahidi wa Kihistoria unaothibitisha kuwa lugha ya Kiswahili ilizungumzwa katika upwa wa Afrika Mashariki hata kabla ya ujio wa wageni kama vile Waarabu na Wazungu. Ushahidi huu ulitolewa na wageni mbalimbali waliofika hapa Afrika Mashariki. Wote wanathibitisha kuwa lugha ya Kiswahili ilizungumzwa hapa Afrika Mashariki kabla ya ujio wa wageni.

(a)    Ugunduzi wa Ali-Idris (1100-1166)
Ugunduzi huu yasemekana ulifanywa huko Sicily yapata mwaka 1100-1166. Kwenye mahakama ya mfalme Roger II. Licha ya kufahamika kuwa Kiswahili, kilipata kuandikwa kabla ya 10BK. Ali-Idris alikuwa wa kwanza kugundua jina la zamani la Zanzibar kuwa ni Unguja. Katika maelezo yake anaandika pia majina kama vile kikombe, mkono wa tembo, muriani, na kisukari, ambayo ni ya ndizi mbalimbali zilizokuwa zikipatikana huko.

(b)    Ushahidi wa Marco Polo
Huyu ni mzungu ambaye alijishughulisha sana na masuala mbalimbali ya kijiografia na alisafiri sehemu nyingi duniani. Marco Polo aliandika hivi:

“Zanzibari ni kisiwa kizuri ambacho kina ukubwa wa mzunguko wa maili 200. Watu wote wanaabudu (Mungu), wana Mfalme na wanatumia lugha yao, na hawalipi kodi (ushuru) kwa mtu.” Safari za Marco Polo 1958:301

Marco Polo anasemekana aliandika pia kitabu cha jiografia ambacho hakikupata kuchapishwa lakini sehemu zake zimepata kufasiriwa kwa Kirusi na Kifaransa. Mfano mmojawapo ni huu unaofuata:

“Katika visiwa vya Sjawaga vilivyoshughulikiwa katika sura hii, ni kile kisiwa cha Andjaba ambacho mji wake mkuu unaitwa katika lugha ya kwao. Zanguabar/Ungudya, na wakazi wake, japokuwa ni mchanganyiko, kwa sasa wengi wao ni Waislam…chakula chao kikuu kikiwa ndizi. Kuna aina tano ambazo zinajulikana kama kundi, fili, ambazo uzito wake waweza kuwa wakia 12, Omani, Marijani, Sukari....”

Maelezo haya ya Marco Polo yanathibitisha mambo ya msingi kuhusu wakazi wa Pwani ya Afrika ya Mashariki na lugha yao; mintarafu ya dini, chakula na utamaduni wao kwa ujumla.

©    Ushahidi wa Al-Masudi (915 BK)
Katika moja ya maandiko yake, Al-Masudi anazungumzia juu ya wakazi wa mwambao ambao walijulikana kwa jina la “wazanji”. Kwa dhana hii, neno Zanzibar linatokana na Zenzibar yaani “Pwani ya Zenji”. Katika maelezo yake Al-Masudi anaonyesha kwamba Wazenji walikuwa  “Watawala Wakilimi” ambao waliaminiwa kuwa walitawala kwa nguvu za Mungu. Kuna maelezo kuwa huenda neno “wakilimi” lina maana ya “wafalme”. Al-Masudi alisisitiza katika maelezo yake kuwa Wazenji walisema lugha kwa ufasaha na walikuwa na viongozi waliowahutubia kwa lugha yao. Kutokana na neno “zenji” kuna uwezekano kuwa kabla ya majilio ya Waarabu, Kiswahili kiliitwa “Kiazania” au “Kizanji” na wageni waliofika pwani.

(d)    Ushahidi wa Ki- Historia wa Mji wa Kilwa
Kimsingi habari zinazoeleza historia ya mji wa Kilwa katika karne ya 10-16BK zinataja majina ya utani kama vile: mkoma watu, nguo nyingi, nk. ambayo walipewa Masultani wa kwanza wa Kilwa Ali Ibn Hussein na mwanae Mohamedi Ibn Ali. Kutokana na habari hizi huenda lugha ya Kiswahili ilishaanza kusemwa mnamo karne ya 10 au ya 11 BK. Maelezo ya kihistoria yanaeleza juu ya Sultani aliyeitwa Talt Ibin Al Husaini ambaye alipewa jina la utani “Hasha Hazifiki”.
(e)      Utenzi wa Fumo Liyongo (13 BK) kama Ushahidi
Shairi la zamani kabisa lililopata kuandikwa la Kiswahili, linalojulikana ni lile la Utenzi wa Fumo Liyongo. Utenzi huu inasemekana uliandikwa karne ya 13BK. Kuweko kwa shairi hili kunadhihirisha kuwako kwa lugha ya Kiswahili kabla ya karne hiyo, na kwa hivyo, huenda Kiswahili kilianza kutumika kabla ya karne ya 10BK. Baadhi ya beti za utenzi wa Fumo Liyongo ni hizi zifuatazo:
Ubeti  6:        Liyongo Kitamkali,
                        Akabalighi vijali
                        Akawa mtu wa kweli
                        Na hiba huongeya.

Ubeti 7:          Kilimo kama mtukufu
                        Mpana sana mrefu
                        Majimboni yu maarufu
                        Watu huja kwangaliya.

Ubeti 10:        Sultani pate Bwana
                        Papo nae akanena
                        Wagala mumemwona
                        Liyongo kiwatokeya.

(Kutoka E.A. Swahili Committee 1973)

Lugha hii ndio mfano wa lugha iliyokuwa ikitumika kunako karne ya 13BK. Ni wazi kuwa lugha hiyo ilianza kusemwa mapema kabla ya muda huo. Hoja za kihistoria inaelezea historia ya lugha ya Kiswahili toka karne ya 10BK hadi karne ya 18BK. Kutokana na ushahidi huu ni dhahiri kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni Wabantu wa Afrika ya Mashariki.

MAREJELEO

Maganga (1997), OSW 102: Historia ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Masebo, J. A. Nyengwine, N. (2002), Nadharia ya Lugha ya Kiswahili, Kidato cha 5 na 6.  Aroplus Industries Ltd: Dar es Salaam.
Nkwera, Fr. F. V. (2003), Sarufi, Fasihi na Uandishi wa Vitabu, Sekondari na Vyuo. Creative Prints Ltd: Dar es Salaam.

Soma zaidi>>>>>>http://petermwiza.blogspot.com/2014/03/nadharia-mbalimbali-kuhusu-historia-ya.html]]>

<![CDATA[HISTORIA YA KUSAMBAA KWA WABANTU AFRIKA]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1559 Fri, 26 Nov 2021 16:20:15 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1559 SWALI: Thibitisha kauli kuwa kusambaa kwa wabantu kulianzia Afrika ya Magharibi hadi Pwani ya afrika Mashariki kwa kuelezea hatua nne za kusambaa kwa wabantu hao.
Utangulizi:
Ushahidi wa kihistoria unatueleza kuwa lugha za kibantu zilienea kutoka Afrika Magharibi eneo la kaskazini magharibi ambako ni makazi ya wabantu mpaka sasa. Kutoka eneo hilo ndicho chanzo cha kuwa na wabantu katika upwa wa Afrika Mashariki.
Kiini
Hatua za kusambaa kwa wabantu ni kama zifuatazo
(a) Wabantu walianza kuondoka katika eneo lao la asili (Kameruni) katika karne ya 10-40 BC wakielekea upande wa Kusini - Mashariki kupitia kingo za misitu ya Kongo na wengine walielekea Kusini karibu na visiwa vya Fernando.
(b) Wabantu walitawanyika kutoka Kusini mwa misitu ya Kongo kuanzia mwaka 100 BC na kuelekea maeneo ya Afrika baada ya idadi yao kuwa kubwa na kukumbwa na upungufu wa ardhi kwa ajili ya kilimo na maeneo ya kulisha wanyama wao.
© Wabantu walitawanyika kutoka eneo la Kusini Mashariki ya Kongo na kuelekea ukanda wa Afrika ya Mashariki mnamo karne ya 1 - 2AD katika makundi madogo madogo ambayo yalitofautiana katika lugha na ada zao. Tofauti hizi zilisababisha kuibuka kwa makabila ya kibantu ya Afrika Mashariki na kwingineko ambako ndio chanzo cha lahaja mbalimbali ikiwemo lahaja ya Kiunguja iliyotumika kusanifisha Kiswahili.
(d) Mnamo karne ya 3 - 4AD wabantu walielekea katika nyika tambarare za Pwani ambako walifanya maskani katika mabonde yenye rutuba yaliyo kando kando ya mto Tana na kuanzisha makazi katika maeneo ya Shupate na Shungwaya ambako ndiko chimbuko la waswahili wa leo.
Hitimisho
Upungufu wa ardhi yenye rutuba na malisho ya wanyama ndicho chanzo cha kuendelea kusambaa kwa wabantu kutoka Afrika ya Magharibi hadi Afrika ya Mashariki na hatimaye katika upwa wa Afrika Mashariki hadi bar]]>
SWALI: Thibitisha kauli kuwa kusambaa kwa wabantu kulianzia Afrika ya Magharibi hadi Pwani ya afrika Mashariki kwa kuelezea hatua nne za kusambaa kwa wabantu hao.

<![CDATA[KISWAHILI NA MIAKA 60 YA UHURU]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1438 Wed, 10 Nov 2021 13:04:19 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1438 ]]> ]]> <![CDATA[LAHAJA ZA KIARABU]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1315 Thu, 14 Oct 2021 06:40:37 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1315 Waarabu wana lugha za kijamii zipatazo 30 ambazo 'International  Organisation for Standardization wanaziona ni lugha zenye kujitegemea wakati 'Library of  Congress' wanaziona ni lahaja za Lugha ya Kiarabu.
Kuna lahaja inayowaunganisha Waarabu wote (Wana uwezo wa kuifahamu) inaitwa 'Lahaja ya Umoja /Allahjatul Muwahhidat - اللهجة الموحدة) na hii ndiyo lahaja ya Kiarabu cha Qur'aan Tukufu na sasa huitwa Kiarabu Fasaha/ Al-Arabiyyatul Fusw-haa العربية الفصحى).
Lahaja nyingine za Kiarabu zinakaribiana na kuachana hapa na pale.
Kwa mfano, tuliangalie neno Kayfa كيف Vipi (Kiswahili), How (Kiingereza) katika lahaja mbalimbali za Kiarabu:
1. Kiarabu Fasaha: KAYFA كيف.
2. Saudia: KAYFA/SH-LOON كيف/ شلون.
3. Libya: KAYFA  كيف
4. Morocco: KIIFASH كيفاش
5. Algeria: KIIFASH كيفاش
6. Misri: IZAAY إزاي
7. Jordan: KAYFA/SH-LOON كيف/شلون
8. Shaam (Syria): KAYFA/SH-LOON كيف/شلون
9. Iraq: SH-LOON شلون
10. Sudan: KAYFA كيف
11. Yemen: KAYFA كيف
12. Kuwait: KAYFA/SH-LOON كيف
13. Imaraat (Falme za Kiarabu - UAE): SHAQAA/SHAQAAIL شقى/شقايل
14. Bahrain: SH-LOON/CHIIFAT شلون/جيفة
15. Oman: KAYFA كيف.
TANBIHI: Neno KAYFA baadhi ya Waarabu hulitamka KEEF.

Na:
Khamis Mataka
+255 713 603 050]]>
Waarabu wana lugha za kijamii zipatazo 30 ambazo 'International  Organisation for Standardization wanaziona ni lugha zenye kujitegemea wakati 'Library of  Congress' wanaziona ni lahaja za Lugha ya Kiarabu.
Kuna lahaja inayowaunganisha Waarabu wote (Wana uwezo wa kuifahamu) inaitwa 'Lahaja ya Umoja /Allahjatul Muwahhidat - اللهجة الموحدة) na hii ndiyo lahaja ya Kiarabu cha Qur'aan Tukufu na sasa huitwa Kiarabu Fasaha/ Al-Arabiyyatul Fusw-haa العربية الفصحى).
Lahaja nyingine za Kiarabu zinakaribiana na kuachana hapa na pale.
Kwa mfano, tuliangalie neno Kayfa كيف Vipi (Kiswahili), How (Kiingereza) katika lahaja mbalimbali za Kiarabu:
1. Kiarabu Fasaha: KAYFA كيف.
2. Saudia: KAYFA/SH-LOON كيف/ شلون.
3. Libya: KAYFA  كيف
4. Morocco: KIIFASH كيفاش
5. Algeria: KIIFASH كيفاش
6. Misri: IZAAY إزاي
7. Jordan: KAYFA/SH-LOON كيف/شلون
8. Shaam (Syria): KAYFA/SH-LOON كيف/شلون
9. Iraq: SH-LOON شلون
10. Sudan: KAYFA كيف
11. Yemen: KAYFA كيف
12. Kuwait: KAYFA/SH-LOON كيف
13. Imaraat (Falme za Kiarabu - UAE): SHAQAA/SHAQAAIL شقى/شقايل
14. Bahrain: SH-LOON/CHIIFAT شلون/جيفة
15. Oman: KAYFA كيف.
TANBIHI: Neno KAYFA baadhi ya Waarabu hulitamka KEEF.

Na:
Khamis Mataka
+255 713 603 050]]>
<![CDATA[UKUAJI NA UENEAJI WA KISWAHILI KATIKA ENZI ZA WAINGEREZA]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1203 Thu, 09 Sep 2021 03:42:09 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1203 Ukuaji na ueneaji wa Kiswahili umepitia hatua mbalimbali, kuanzia enzi za waarabu hadi wa kati wa ukoloni. Waingereza walipochukua koloni la Tanganyika kutoka kwa Wajerumani walikuta Kiswahili kimeimarika na kinatumika katika maeneo mengi ya nchi. Katika mada hii utaweza kujifunza mambo mbalimbali yaliyofanywa na Waingereza na ambayo yalichangia kukua na kuenea kwa Kiswahili.
Mambo yaliyosaidia ukuaji wa Kiswahili enzi za utawala wa Waingereza
Waingereza walipochukua koloni la Tanganyika kutoka kwa Wajerumani walikuta Kiswahili kimeimarika na kinatumika katika maeneo mengi ya nchi. Kwa kuwa nao walihitaji kutawala hawakupuuzia matumizi ya Kiswahili katika utawala wao japo hawakutumia Kiswahili kwa lengo la kukikuza lakini walijikuta wanakieneza na kukikuza bila ya wao kukusudia.
Waingereza walitumia Kiswahili kama nyenzo ya kusaidia shughuli zao za kiutawala. Hata hivyo kuna mambo waliyofanya waingereza yaliyosaidia kukua na kuenea kwa Kiswahili, mambo hayo ni kama yafuatayo:
Shuguli za kiuchumi
Shuguli za kiuchumi wakati wa Waingereza zilihusisha kilimo na biashara. Kwa upande wa klimo, Waingereza waliendesha kilimo cha mazao mbalimbali, na walitumia mfumo wa kuajiri vibarua kutoka sehemu mbalimbali za nchi. Vibarua hao walijulikana kwa jina la manamba.
Katika mkusanyiko wa vibarua hawa waliokuwa na usuli wa makabila tofautitofauti, lugha pekee iliyoweza kuwaunganisha ni Kiswahili ikizingatiwa kwamba Kiswahili kiliteuliwa kuwa lugha rasimi katika mawasiliano ya kiutawala. Walilazimika kuzungumza Kiswahili kwani bila hivyo mawasiliano yasingeweza kufanyika kwa urahisi.
Hata hivyo kupitia shuguli za kilimo maneno mapya ya Kiswahili yaliweza kuzaliwa, kwa mfano: yadi, belo, belingi, bani, mtama n.k, kwa hiyo kupitia shughuli hizi Kiswahili kilizidi kukua.
Shuguli za kiutamaduni
Shughuli hizi ni kama vile uigizaji wa tamthiliya za kigeni, uchezaji wa mziki wa kigeni hususani twisti. Tamthiliya za kigeni zilikuwa zikiigizwa majukwaani kwa lugha ya Kiswahili na hivyo ikasaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili.
Shughuli za kidini
Wakati wa utawala wa mwingereza pia kuliambatana na ujio wa wamishonari waliokuwa na lengo la kueneza dini ya kikristo.
Katika harakati hizi walitumia lugha ya Kiswahili ili kufanikisha malengo yao ikizingatiwa kwamba Kiswahili kilikuwa kimeshaenea vya kutosha wakati wa utawala wa Mjerumani, kwa hiyo wamishonari wa Kiingereza waliendelea kukiimarisha zaidi.
Pia shughuli za kidini zilipelekea kutafsiriwa kwa vitabu mbalimbali vya kidini kama vile Biblia na vitabu vingine. Tafsiri ya vitabu hivi ilikuwa ni kutoka katika lugha ya kiingereza kwenda katika lugha ya Kiswahili. kwa kufanya hivi Kiswahili kiliweza kuingiza msamiati mwingi sana na hivyo kukuza lugha ya Kiswahili.
Wamishonari walilazimika kujifunza Kiswahili hukohuko kwao ili wanapokuja huku Afrika Mashariki wasipate tabu ya kujifunza Kiswahili. Kwa sababu hii wamishonari waliokuwa wamekwishajifunza lugha ya Kiswahili walitunga kamusi za Kiswahili – Kiingereza   ili kuwasaidia wenzao pia kujifunza Kiswahili; kwa njia hii waliweza kukikuza Kiswahili.
Shughuli za kisiasa
Shughuli za kisiasa hasa katika uanzishwaji wa vyombo mbalimbali vya kiutawala, jeshi, polisi, mahakama, boma n.k. Kufuatia uanzishwaji wa vyombo hivi msamiati mwingi wa Kiswahili uliweza kuzuka na hivyo kukuza Kiswahili.
Shughuli za kiutawala
Makampuni ya uchapishaji yalianzishwa (East African literature Bureau), na kamati ya lugha iliundwa (Interterritorian language committee). Hatua hii iliimarisha matumizi ya lugha ya Kiswahili hali iliyosaidia kukua kwa lugha ya Kiswahili.
Shuguli za ujenzi wa reli na barabara
Shughuli hizi pia zilisaidia kuibuka kwa msamiati mpya kama vile, reli, stesheni, tiketi n.k.
Usanifishaji wa Kiswahili
Usanifishaji wa lugha ya Kiswahili pia lilikua ni jambo jingine muhimu sana lililosaidia kukua kwa msamiati wa Kiswahili. Lengo la usanifishaji wa Kiswahili lilikuwa ni kuleta ulinganifu wa matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ukanda wa Afrika Mashariki.
UENEAJI WA KISWAHILI
Ukuaji na Ueneaji ni maneno mawili yenye maana zinazokaribiana lakini zinazotofautiana. Ukuaji humaanisha ongezeko la msamiati katika lugha na ueneaji ni uongezekaji wa matumizi ya lugha kieneo. Kwa hiyo hapa tutaangalia yale mambo yaliyosababisha Kiswahili kitumike katika eneo kubwa. Mambo hayo ni haya yafuatayo:
Vyombo vya habari
Vyombo vya habari vilivyokuwepo kwa wakati huo ni redio, magazeti na majarida mbalimbali. Kwa upande wa redio kulikuwepo na redio Tanganyika iliyoanza kurusha matangazo yake kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Na magazeti yaliyokuwa yakichapishwa wakati huo ni pamoja na: Mambo leo, Sauti ya Pwani, Kiongozi na Habari za leo. Magazeti haya yote yalikuwa yakichapishwa kwa lugha ya Kiswahili. Kwa hiyo kwa kutumia vyombo vya habari (redio na magazeti) kiswahili kiliweza kuenea.
Kilimo
Kupitia kilimo watu waliweza kukutana pamoja, watu wa makabila tofautitofauti. Kwa hiyo katika kipindi chote walichokaa kwenye makambi ya mashambani waliweza kujifunza Kiswahili na walipomaliza muda wao walirudi nyumbani wakiwa wamejifunza lugha mpya na hivo kwa njia hii waliweza kuieneza lugha ya Kiswahili.
Muundo wa jeshi la kikoloni (KAR)
Jeshi la KAR liliundwa na watu kutoka makabila mablimbali, na lugha iliyokuwa ikitumika jeshini ni Kiswahili, askari hawa walisaidia kueneza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi kwani kila walipokwenda walikuwa wakizungumza Kiswahili.
Mfumo wa elimu
Chini ya utawala wa Waingereza Kiswahili kilitumika katika masomo yote kwa ngazi ya shule ya msingi, na pia kilitumika kama somo kwa ngazi ya shule za sekondari. Kwa hiyo hii pia ilichangia kuenea kwa lugha ya Kiswahili.
Harakati za kudai uhuru
Chama cha TANU kilianzisha harakati za kudai uhuru, harakati hizo ziliendeshwa kwa lugha ya Kiswahili. Kwa hiyo kupitia harakati hizo Kiswahili kiliweza kuenea kwa kiwango kikubwa.
Tathimini ya maendeleo ya Kiswahili wakati wa Waingereza
Licha ya maendeleo ya lugha ya Kiswahili katika utawala wa Waingereza, pia kulikuwa na changamoto zilizoikabili lugha ya Kiswahili katika kupiga hatua ya maendeleo. Changamoto hizo ni kama zifuatazo:
Kutofundishwa kwa Kiswahili shule zote nchini
Wakati wa utawala wa Waingereza Kiswahili kilifundishwa katika shule za watoto wa kiafrika tu, wakati katika shule za watoto wa kizungu Kiswahili hakikufundishwa. Kwa hiyo suala hili lilifanya Kiswahili kipewe msukumo mdogo sana na hivyo kuhafifisha ukuaji wake.
Kutotumika kwa Kiswahili kama lugha ya kufundishia
Lugha ya Kiswahili ilitumika kufundishia katika shule za msingi pekee ilihali lugha ya kiingereza ilitumika kuanzia shule za sekondari hadi elimu ya juu. Hali hii ilisababisha watu kujitahidi sana kujifunza kiingereza; kwa kuzungumza kiingereza ilikuwa na ishara kwamba wewe ni msomi, na hivyo kutokana na hali hii Kiswahili kilendelea kukua polepole sana.
Kukosekana kwa vyombo vya kizalendo vya kukuza Kiswahili
Vyombo vilivyokuwa vinahusika na masuala ya ukuzaji wa Kiswahili wakati wa ukoloni vilikuwa vimeanzishwa na wakoloni wenyewe, kwa mfano Kamati ya Lugha ya Afrika Mashariki (Inter-Territorial Swahili Language commitee) na Shirika la maandiko la Afrika Mashariki (East African Literature Bureau). Katika hali kama hii ukuzaji wa Kiswahili ulikosa msukumo mkubwa wa kizalendo.
Kasumba ya kuthamini Kiingereza
Wananchi walikuwa na kasumba kwamba mtu anayezungumza Kiingereza alichukuliwa kuwa ni mtu mwenye maendeleo na msomi, kwa hiyo hali hii ikapelekea watu kutothamini Kiswahili na hivyo Kiswahili kudharaulika.
]]>
Ukuaji na ueneaji wa Kiswahili umepitia hatua mbalimbali, kuanzia enzi za waarabu hadi wa kati wa ukoloni. Waingereza walipochukua koloni la Tanganyika kutoka kwa Wajerumani walikuta Kiswahili kimeimarika na kinatumika katika maeneo mengi ya nchi. Katika mada hii utaweza kujifunza mambo mbalimbali yaliyofanywa na Waingereza na ambayo yalichangia kukua na kuenea kwa Kiswahili.

<![CDATA[LUGHA YA KISWAHILI (VIDEO)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1202 Thu, 09 Sep 2021 03:36:40 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1202 ]]> ]]> <![CDATA[Mzee Mwinyi ni mwalimu ‘darasa maalumu la Kiswahili’]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1201 Thu, 09 Sep 2021 03:25:42 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1201 Kwa ufupi
Mzee Mwinyi ni mtumiaji mzuri wa lugha fasaha. Matumizi yake ya lugha hayana ubanangaji wa taratibu za lugha. Yeyote anayemsikiliza, huvutiwa na jinsi anavyotamka maneno kwa vituo na lafudhi yenye mvuto kiasi cha kumfanya kila mmoja aweze kuelewa ujumbe anaoutoa.
Na. Erasto Duwe
Lugha ya Kiswahili ni tunu iliyositirika kwetu, haina budi kuenziwa. Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, ni mfano mzuri na wa kuigwa katika kukienzi Kiswahili.

Apatapo nafasi ya kuongea na wadau wa Kiswahili, amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha matumizi ya Kiswahili fasaha. Katika Uzinduzi wa machapisho ya TATAKI, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 19. Machi 2015 , alibainisha kuwa vijana ndilo kundi litumialo ovyo Kiswahili. Hivyo, akawasihi vijana na wadau wa Kiswahili kukitumia kwa ufasaha.
Amekuwa akitumia Kiswahili na kukipamba kwa semi na tamathali za semi. Pindi anapotoa hotuba au ufafanuzi wa mambo, aghalabu hutumia semi na tamathali zake. Matumizi ya aina hii huufanya ujumbe wake uwe mzito, hivyo kuwafanya wasikilizaji kumakinika zaidi.
Apatapo nafasi kuwa mgeni rasmi au kutoa neno katika mikusanyiko ihusuyo Kiswahili, Mwinyi hutoa ‘darasa’ kwa hadhira yake kuhusu Kiswahili.
Katika uzinduzi alitoa ‘darasa’ lililowavutia wengi. Katika kufundisha kwake, alisisitiza kuacha ‘kukinyofoa’ Kiswahili. Hapo alimaanisha kuwa baadhi ya watumiaji wa Kiswahili, hawatumii maneno halisi ya Kiswahili badala yake huchukua maneno ya kigeni na kuyapachika katika Kiswahili bila sababu za msingi.
Alitoa mfano wa neno ‘wiki’ ambalo wengi hupenda kulitumia badala ya ‘juma’ likimaanisha siku saba za juma.
Akiendelea kukosoa matumizi mabaya ya msamiati, alisema maneno “tahadhari” na “hadhari” hubanangwa na watumiaji wa lugha. Neno ‘tahadhari’ linapaswa kutumika kama kitenzi na ‘hadhari’ kama nomino. Vilevile, katika utamkaji wa tarehe, alirekebisha na kusisitiza kuwa, mtumiaji wa lugha hapaswi kusema tarehe moja au “tarehe mbili bali tarehe mosi na tarehe pili.
Katika mkutano wa mwaka wa Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (Chaukidu), uliofanyika Maryland, Marekani hapo Aprili 2015; akiongea na wadau alisisitiza ufasaha wa Kiswahili katika matumizi.
Alisema kutumia neno “nawaahidini” (kwa watu ambao wapo karibu nawe na unawaahidi wao) ni makosa makubwa, kwani kiambishi awali ‘wa’ kinasimama kuwakilisha nafsi ya tatu ‘wao’ yaani watu wanaozungumziwa. Kama ahadi hiyo unaitoa mbele ya watu walio karibu yako, basi unapaswa kusema “nakuahidini”.
Maneno mengine ambayo Mwinyi amewahi kuyatolea ‘darasa’ ni pamoja na ‘onya’ na ‘ona’. Kitendo cha kutaka mtu aone kitu fulani ni ‘onesha’ na siyo ‘onyesha’ neno linatokana na ‘onya’ likimaanisha ‘kataza kwa konesha hatari itakayojitokeza.’
Huu umekuwa mtindo wake Rais Mstaafu Mwinyi apatapo nafasi za namna hiyo. Kwa njia hii huwafungua masikio wengi na kutanabahi makosa yao katika Kiswahili.
Mmahiri huyu wa Kiswahili si mpenzi wa lugha mseto kama walivyo baadhi ya watumiaji wa Kiswahili. Pamoja na kuzifahamu lugha za kigeni, hasikiki akichanganya ovyo maneno ya Kiswahili na lugha nyingine, labda kwa sababu maalumu za kiufundishaji.
Wapenzi wa Kiswahili, tuige mfano wa Mzee Mwinyi katika kuwafundisha wengine Kiswahili.
]]>
Kwa ufupi

<![CDATA[Historia ya mswahili wa Zanzibar (VIDEO)]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1199 Thu, 09 Sep 2021 03:04:34 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1199 Historia ya mtu anayeitwa Mswahili inaonekana kutotiliwa maanani sana na wataalamu wengi kiasi cha kuibua hofu miongoni mwa waswahili kuwa pengine ipo njama ya kuwameza na kuwapoteza waswahili katika historia ya jamii za Mwambao.

]]>
Historia ya mtu anayeitwa Mswahili inaonekana kutotiliwa maanani sana na wataalamu wengi kiasi cha kuibua hofu miongoni mwa waswahili kuwa pengine ipo njama ya kuwameza na kuwapoteza waswahili katika historia ya jamii za Mwambao.

]]>
<![CDATA[UHAKIKI WA SERA YA LUGHA KATIKA ELIMU YA TANZANIA]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1198 Wed, 08 Sep 2021 12:55:37 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1198
Uhakiki wa Sera ya Lugha Katika Elimu Tanzania
Z.S.M. Mochiwa katika Kioo cha Lugha 2,1996/97:41-58
Z.S.M.Mochiwa katika kuhakiki sera ya elimu katika Tanzania anaeleza yafuatayo:
Utangulizi
Katika wimbo wa Taifa la Tanzania, hekima, umoja na amani hutamkwa kuwa ngao za Watanzania. Aidha, nembo ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam imesogeza falsafa hii hatua moja mbele kwa kutangaza kuwa: Hekima ni uhuru. Hainipitii akilini mwangu kuwa kuna mtu-hadhiri wa nafsi yake anayeweza kusema matamko haya ni mufilisi. Mimi, binafsi yangu, ninayahesabu kuwa miongoni mwa vito vichache tulivyo navyo katika taifa hili.
Kwa bahati mbaya, sijapata kusikia majadiliano yanayomulika jinsi vito hivi vinavyorutubishwa ndani ya jamii. Penyenye peke yake niliyoona ni ile inayotokana na matumizi ya kito kimoja ndani ya nembo ya Chuo Kikuu. Kwa kuwa Chuo Kikuu ni taaisis ya elimu, hapana shaka kuwa nemno ile inahusisha elimu na hekima. Kwa maana hiyo, ndani ya elimu, hekima hukua na inapokua, hekima humpa aliye nayo uhuru.
Tukiyaondoa hayo yote, bado taifa halielekei kujiuliza kwa dhati kabisa, hekima, umoja na amani hukuzwa na kuendelezwa vipi. Hata wataalamu wa Chuo Kikuu, pamoja na kudai kuwa hekima ni uhuru, hawaelekei kuionesha imani hii kwa vitendo kwa kubainisha na kutumia mbinu zinazokuza hekima. Aidha, mtu anapohakiki safari ya taifa hili tangu lizaliwe hadi hivi leo, na hususan miaka kumi hivi iliyopita, inadhihirika wazi kuwa kuna kupuuzwa kwa virutubisho vya vito hivi.
Inawezekana kuwa mwenendo wa kupuuzwa kwa virutubisho hivi si wa makusudi. Linaloelekea kuwa dhahiri kwangu, ni kule kutotambua vizuri virutubisho hivyo ni vipi na vina umuhimu gani. Mathalan, baada ya uhuru, Tanzania ilianzisha wizara ya Utamaduni-kirutubisho cha kwanza cha hizo ngao za taifa-lakini wizara hii haikuweza kudumu na nafsi yake. Kisa cha kupachikwa pachikwa kwa wizara hii kila mahali-mara utamaduni ni sehemu ya Wizara ya kazi, mara vijana, ningethubutu kusema, ni taswira yake yenye uvumilivu mbele ya wahandisi wanaoanzisha wizara katika Jamhuri. Hali hii ya uvumilivu wa taswira ya wizara huakisika pia katika mgao wa mafungu ya fedha. Hali hii hujirudia kwenye taasisi za wizara hii, kama vile, BAKITA. Kwa ufupi taifa halijapambaukiwa kwamba utamaduni ndiyo nyenzo pekee ya kurutubishia vito vya taifa.
Katika makala haya ninakusudia kudai kuwa Tanzania haikupiga hatua kubwa kielimu na kimaendeleo kwa ujumla kwa sababu ya kuweka kipaumbele chake katika mambo ambayo, kwa maoni ya makala haya, si ya msingi. Kuitelekeza lugha ya Kiswahili ikabaki kuwa lugha ya kuuzia nyanya sokoni, kumeleta maafa makubwa kielimu, kijamii na kiuchumi, ima kwa neno moja kiutamaduni. Ikisemwa vinginevyo, kwa kupuuza lugha ya Kiswahili na kuikumbatia ya Kiingereza, Tanzania imekubali kujiweka katika hali ya kutojitegemea. Matokeo ya mwenendo huu ni kwamba kila kinachofanyika ni maigizo tu. Hali hii hailiruhusu taifa kuishi kwa nafsi yake isipokuwa kwa nafsi ya kuazima. Kabla ya kuanza mjadala huo hapana budi kuelekeza makini yetu kwenye dhana muhimu, nazo ni taifa, utamaduni, maendeleo ya kijamii, elimu na lugha.
 
Taifa
Inaposemwa kwamba Tanzania ni taifa, ina maana ni kundi la watu ambao wana nduni mahususi. Kwanza kundi hilo lina kipande cha ardhi ambacho wote kwa pamoja wanadai kuwa ni chao; ni nchi yao. Watanzania, kwa mfano, huishi Tanzania, na Wakenya huishi Kenya. Pili, ili wawe taifa, ni lazima watu hao wawe na mambo kadhaa yanayofanana. Miongoni mwa mambo hayo ni historia, mila na desturi. Tunaposema, mila na desturi, tunasema taifa haliwezi kuwa taifa bila ya kuwa na utamaduni wake. Nduni hizi ndizo zinzorutubisha umoja wao.

Watu wenye mila na desturi au, kwa neno moja, utamaduni unaofanana wana kongamano kubwa la rai, mtazamo na hisia. Hukumu zao kuhusu masuala na matukio mbalimbali hufanana. Kwa misingi hii watu wa namna hii wana umoja wa aina fulani katika mienendo na hukumu kuhusu vilivyo na visivyo. Pamoja na kuzikubali nduni hizi, Gerth na Mills (1954:197) wanaongeza kuwa kundi hilo lina uwezo wa kujiundia chombo cha uongozi kikawa serikali yao. Kwa kuwa moja ya nduni za taifa ni utamaduni wake, tujipe wasaa wa kuifasili dhana hii.

Utamaduni
Kwa watu wa kawaida, utamaduni unafasiliwa kwa namna nyingi kwa kutegemea muktadha. Utamaduni unanasibishwa na uganga au mazingaombwe, uchawi, michezo au ngoma au mambo yote ambayo, kwa macho ya sasa, yamepitwa na wakati. Mifano halisi ya mikanganyiko hiyo ni pamoja na jina la wizara yenyewe inayosimamia masuala ya utamaduni nchini ambayo inaitwa Wizara ya Elimu na Utamaduni. Kutenganisha Elimu na Utamaduni ni kudai kuwa Elimu huweza kuangaliwa pekee bila ya kuhusisha Utamaduni. Jina la Wizara halidokezi kuwa Utamaduni ni elimu na elimu ni utamaduni. Aidha, inapotokea kuwa watu huiita Wizara hii kuwa ya michezo, kwa sababu tu wao ni washabiki wa michezo, hii ni dalili ya ufahamu nusu nusu wa dhana nzima ya utamaduni. Hali hii, kwa maoni yangu, inatia hofu kwa sababu utamaduni, kwa sehemu kubwa, unaonekana kuwa mambo ya jana na si ya leo. Ni mambo ambayo hayana mchango wa moja kwa moja katika uhai wa jamii hivi leo. Aidha, fasili hizi zinaelekea kudokeza uwezekano wa utamaduni kuwa kikwazo katika maendeleo ya jamii badala ya kuwa suluhu au mashine yenyewe ya maendeleo hayo.

Chanzo cha mikanganyiko hii ni upana wa dhana yenyewe. Karibu kila kitu katika jamii kinanasibika na utamaduni. Kutokana na mikanganyiko hii, hata wataalamu wameelekea kufasili dhana hii kwa kutaja ‘orodha’ ya vitendo, matukio na mienendo ya jamii. Goodenough (1957:167), kwa mfano, anasema:

Quote:Utamaduni wa jamii ni mkusanyiko wa yote ambayo mwanajamii ni lazima ajue au aamini kama sharti la kukubalika kwa mwenendo wake kwa wanajamii wenzake…..(tafsiri ya mwandishi).
Maneno ‘mkusanyiko wa yote’ katika fasili husisitiza kuwa dhana ya utamaduni ni ‘kapu’ la kubebea yote yaliyo ndani ya jamii. Pamoja na upana wake, fasili hii ni maarufu kwa wataalamu wengi kama Wardhaugh (1992) na Baker (1995). Baker, kwa mfano, zaidi ya kutumia mkusanyiko wa yote, anaorodhesha vipengee kama fasili yake inavyoonesha:
Quote:Utamaduni ni mwenendo mzima wa maisha ya jamii, maono ya jamii, mpangilio wao wa uzoevu, taratibu za matazamio, mahusiano ya kijamii, kaida za mienendo, sayansi na teknolojia, n.k (uk. 28) (tafsiri ya mwandishi)
Udhaifu wa fasili hizi ni kwamba unaifanya dhana hii iwe ngumu kufumbatika kiakili. Aidha fasili hii inashindwa kuhusisha channzo na matokeo na badala yake kushikilia matokeo. Mienendo ya jamii, mpangilio wa uzoevu, matazamio na mahusiano kati ya wanajamii, ngoma, michezo n.k. peke yake si utamaduni. Utamaduni ni muunganiko wa haja ya jamii kupata nusura na jitihada zao za vitendo vya kuipatia nusura hiyo. Yote yanayoorodheshwa yanatokana na haja iliyo ndani ya nafsi ya kila mwanajamii ya kutaka kunusurika. Nusura hii ndiyo inayofasilika kuwa mfumo wa maitikio yote ya wanajamii katika kukabiliana na changamoto zilizomo ndani ya mazingira ya jamii yenyewe. Mbinu za kujiruzuku, kujihami, kujifurahisha, kujenga mahusiano kati ya wanajamii ni mkusanyiko wa jitihada za wanajamii ambazo zinakidhi haja ya kupata nusura.
Fasili hii, inatuwezesha kuona nafsi ya kubadilikabadilika kwa michomozo ya nusura. Ingawa haja ya kunusurika haibadiliki lakini mbinu zinazotumika ili kuipata hubadilika kutokana na mabadiliko ya mazingira. Tuchukue mfano wa burudani. Kuburudika ni kipengee muhimu kinachodhihirisha utashi wa mwanajamii wa kujipatia nusura. Lakini kwa kadiri miaka inavyobadilika jamii imeshuhudia kuingia na kutoka kwa aina mbalimbali za burudani. Ni nani, kwa mfano anajua Mserego au beni ni nini hivi leo? Kutoweka kwa ngoma kama hizi hakuna maana ya kupotea kwa haja ya burudani. Kilichotokea ni kwamba wanajamii hupata burudani wanayohitaji kutokana na ngoma, michezo au shughuli nyingine mpya.
Fasili kama hii inatusaidia kuusawiri mwanzo wa utamaduni ndani ya heba ya mwanajamii badala ya kuuona kuwa nje ya heba hiyo. Aidha fasili hii itatuzuia kuuona utamaduni kuwa gwanda ambalo mtu anaweza kuvaa au kuvua. Ingawa mtu hazaliwi nao, lakini mbegu ya utamaduni imo ndani ya nafsi yake. Utamaduni kwa mtazamo huu ni mfungamano wa nafsi ya mwanadamu ya kutaka nusura na maitikio yake ya changamoto za mazingira yake. Kutokana na mfungamano huo, utamaduni huifumbata heba yake. Kwa vyovyote itakavyofasiliwa, hapana budi dhana ya utamaduni iungane na heba ya jamii. Utamaduni ndiyo nafsi; ni dhati ya jamii.
Mjadala huu unatufanya kuuona utamaduni kuwa na nyuso mbili. Uso mmoja ambao umo ndani ya heba ya mwanajamii katika sura ya utashi wake wa nusura. Utashi huu wa nusura ndio unajidhihirisha katika mkusanyiko wa mbinu mbalimbali za kuutafutia nusura. Uso huu ulio ndani ya heba ndio unaoukilia vipengele vyote vinavyoorodheshwa. Aidha, uso huu ndio unaomsukuma mwanajamii mpya kufanya jitihada ya kujifunza huu uso wa nje. Uhusiano wa usababisho kati ya utashi wa nusura na mbinu za maisha zinazodhihirika ni kitu cha msingi katika kuchochea, kuimarisha na/au kuhamasisha maendeleo ya jamii. Kwa maneno mengine, ncha mbili hizi zinazokamilisha fasili zinasaidia kuona uhusiano wa karibu kati ya utamaduni na maendeleo ya jamii.
Maendeleo ya jamii
Tunapochukulia kuwa utamaduni una nyuso mbili, yaani utashi wa nusura na mbinu za kuipata nusura hiyo, inawezekana kusema maendeleo ya jamii yoyote ni mabadiliko ya utamaduni wake, na hasa, kwa usahihi zaidi, ni  mabadiliko ya mbinu za kupatia nusura. Mabadiliko ya mbinu hizo huanzia kwenye utashi. Huanza na hisia za kutosheleza kwa mbinu hizo za kuipatia jamii nusura yake. Baada ya kuridhika kuwa mbinu zinazotumika zina udhaifu, jamii hufanya bidii ya kuondoa zile zilizochakaa na kuingiza mpya. Mbinu mpya zinapoingia katika jamii, ndipo jamii inayohusika inasemekana kuwa imepiga hatua ya maendeleo.Kwa maana hii, jitihada zozote za kuiletea jamii maendeleo huanza na tathmini ya kina ya utamaduni wa jamii inayohusika, hususan, mbinu za maitikio ya changamoto za mazingira zinakidhi kwa kiasi gani haja ya jamii hiyo ya kujitafutia nusura. Tathmini hii itaelekeza ni vipengee gani katika ‘mashine’ ya maendeleo vimechakaa na kwa hivyo vinahitaji kubadilishwa. Mbinu mpya za utunzaji wa mazingira, kwa mfano, huibukia ndani ya utamaduni wa jamii kuhisi kuwa maitikio ya zile za zamani ya changamoto hizo hayaleti tija inayolingana na mahitaji.
Jambo la msingi hapa ni kwamba ni lazima jamii ihisi kwamba kuna tatizo. Endapo jamii, kwa macho yake ya utamaduni, haihisi kuwa liko tatizo, jitihada zote za kuleta maendeleo hukwama. Mathalan, sina hakika kama heba ya Tanzania inahisi kuwa uzazi wa watoto wengi ni tatizo. Mradi wa Uzazi wa mpango utafanikiwa ikiwa heba ya jamii itagundua na kukubali kuwa, kuwa na watoto wengi katika familia ni tatizo.
Umuhimu wa kuangalia maendeleo ya jamii kwa mwanga huu umetiliwa mkazo katika Mkutano Mkuu wa sera za utamaduni ulimwenguni (1982). Mkutano huo wa Mexico ulidhihirisha kwa kauli moja haja ya kuweka mnasaba kati ya maendeleo na utamaduni. Mkutano ulizingatia na kutangaza kwamba:
Quote:Maendeleo ya kweli ni yale yanayotokana na hisia na dhamira za mabadiliko za wanajamii. Kwa maana hiyo maendeleo ya jamii yatakuwa matokeo ya juhudi za wanajamii. (uk. 18). (Tafsiri ya mwandishi)
Kwa kuangalia kampeni nyingi za nchi, ni rahisi kuona kuwa, yaliyo matatizo kwa wenzetu, yamefanywa kuwa matatizo kwetu. Aidha, kwa kuwa suala la utamaduni halina kipaumbele, nchi imejitumbukiza katika miradi mbalimbali ambayo mara nyingi haielekei kukabili changamoto halisi za mazingira ya jamii. Kampeni kama Twende na wakati na Uzazi wa mpango, zinafungamana zaidi na heba za jamii za nje kuliko heba ya Tanzania Ni dhahiri kuwa, Tanzania haitafuti maendeleo ya kijamii kwa kurekebisha heba yake bali kwa kujilinganisha na kujifananisha na heba nyingine. Kujiangalia na kujirekebisha kwa kioo cha nje, au tuseme, kwa kutumia vigezo vya tamaduni za nje, kuna matokeo ya kutelekeza utamaduni wetu ambao, ndio mashine ya maendeleo ya kweli.
Elimu na lugha
Zinapokubalika, fasili za utamaduni na maendeleo ya jamii zinadokeza kwa nguvu, umuhimu wa elimu na lugha katika maendeleo. Ikiwa ndani ya utamaduni mna mfumo wa maarifa au mbinu mbalimbali zinazoleta arabuni ya utashi wa nusura ya jamii, na ikiwa maendeleo ya jamii ni mabadiliko ya utamaduni, ni dhahiri kuwa elimu na lugha ni muhimu katika uhai wa mfumo wenyewe pamoja na maendeleo ya jamii. Mfumo huo hauwezi kuendelea kuwako bila ya kuwako kwa taratibu za kuurithisha kwa kizazi kipya. Taratibu hizo za kuurithisha mfumo wa maarifa na mbinu za nusura ndizo zinazoingia katika ajenda ya elimu.

Elimu kwa rai ya makala haya, iwe ya asili au ya kisasa, ina kazi kuu mbili. Zaidi ya kuwa mchakato wa kurithishia vipengee mbalimbali vya mfumo wa nusura ya jamii, lakini pia, mchakato huu humpatia kila mwanajamii fursa ya kugundua na kukuza vipawa vyake. Ni mfumo unaokuza akili ya mpokeaji hadi imepata uwezo wa kutanzua tata, kudadisi na/au kupata stadi za ubunifu. Elimu hii ndiyo ile ile inayofasiliwa na Nyerere (1967) kuwa mchakato wa kukuzia udadisi na wa kujengea fikra angavu.

Freire (1970) anaifasili elimu hii kuwa kitendo cha kitamaduni chenye kumleta mpokeaji kwenye uhuru. Kauli ya Freire inaobesha wazi kuwa Elimu ni utamaduni na utamaduni ni elimu. Tanzania kuwa na Wizara ya Elimu na Utamaduni ni kuonesha kuwa dhana ya utamaduni haijaeleweka. Aidha, kwa mujibu wa Freire, kitendo hicho cha kitamaduni kitakuwa hakina maana ikiwa hakimpi mpokeaji kujua na badala yake humpa kukariri mambo tu.

Elimu, na hasa ile ambayo ni chipukizi la utamaduni wa jamii, ni mchakato muhimu na wenye nguvu za kusukuma gurudumu la maendeleo. Lakini kama wanavyodai Costa na Garmston (1994) elimu hiyo ni sharti iwe na makusudi mahususi. Hapana budi iwe na ‘mtu wa ndoto’ anayeaniwa nayo;

Quote:Ni lazima elimu ikuze uwezo wa kufikiri kwa unyofu na uangavu. Impe mpokeaji uwezo wa kuunganisha chanzo na sababu za matukio na kutoa maamuzi razini (uk 77) (Tafsiri ya mwandishi)
Haya, kwa kiasi kikubwa, ndiyo yanayotajwa na Nyerere anapofafanua mtu wake wa ndoto kielimu (mtajwa). Yeye pamoja nao wote wanasisitiza kuwako kwa falsafa ambayo itaongoza mchakato mzima wa elimu. Kutokuwako kwa falsafa ya elimu iliyo hai nchini kumesababisha matatizo ya aina mbalimbali ambayo yanaelekea kuunyima mchakato wa elimu Tanzania uwezo wa kumuumba mtu wa ndoto tuliyemtaja.
Mchakato wa elimu wenye uwezo wa kutoa bidhaa ya aina iliyoelezwa, ni ule ambao unatumia lugha inayoruhusu makusano (interaction) baina ya walimu na wanafunzi, walimu na walimu na wanafunzi na wanafunzi. Matumizi ya lugha ya Kiingereza katika elimu ya sekondari yametunyima bidhaa hii. Walimu na wanafunzi hawaonani kifikra, hawakusani wala hawajadiliani. Kwa miaka mingi, Kiswahili kwa macho ya serikali Tanzania hakistahiki na wala hakiwezi kumudu mawasiliano ya kitaalam. Viongozi na watu wengine wanalitamka jambo hili bila ya ‘ashakum’ wala ‘astaghafiru’. Kinachoumiza roho ni kwamba, kama tutakavyoona hivi punde, dai hili si sahihi kabisa. Aidha, hata kama lingalikuwa kweli, lisingalitangazwa kwa mikogo hiyo. Kwa kuwa lugha huakisi akili ya jamii nzima, inaposemwa lugha yake haimudu hili au lile ni kifani cha kusema akili ya jamii hiyo ni ndogo kuliko ya jamii nyingine. Sina hakika kama jamii hii iko tayari kujipuuza hivi ili iendelee kupuuzwa. Vinginevyo tunajitia katika ushahidi kuwa mnyonge huanza kujinyonga mwenyewe.
Lugha ya kufundishia

Kwa muongo mzima huu, kuanzia 1987 hadi 1997, taifa kwa sehemu kubwa, limeendelea kutoelewa vipengee vya msingi vinavyosukuma mbele gurudumu la maendeleo. Hakuna dalili zozote zinazoonesha nafasi ya utamaduni, na hususan lugha, katika kurutubisha vito vya taifa kwa upande mmoja na kwa maendeleo ya taifa kwa upande wa pili. Taifa limeshindwa, hadi sasa, kugundua ubadhirifu wa vipawa vya taifa shuleni. Ingawa Kiingereza hakijulikani, bado serikali imeshikilia kidinindi kiendelee kuwa lugha ya kufundishia elimu ya sekondari. Inatia huzuni, na pengine aibu, kuona kuwa Tanzania inaamini kuwa mtoto wa nchi hii atakuwa amesharabu Kiingereza baada ya kupewa saa 800 za kujifunza lugha hiyo katika shule ya msingi (ang. Mochiwa 1991).

Kutojulikana kwa Kiingereza si suala la utafiti tena. Wataalam mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wamelieleza taifa hili kwamba lugha hii haijulikani kwa kiwango cha mawasiliano katika elimu ya sekondari (ang. Mlama na Matteru, 1977, Criper & Donald 1984, Rubagumya 1990). Isitoshe, tume ya Rais (1982) ilipendekeza kitumike Kiswahili badala ya Kiingereza lakini, serikali ililifumbia macho pendekezo hilo.

Hali hii inaonesha kuwa serikali ya Tanzania haiendeshi mambo yake kisayansi badala yake inafuata ushauri wa kihisia usiozingatia hali halisi. Ushauri huo wa kihisia unaelekea kuitisha serikali kwa kutangaza matatizo makubwa yatakayoikumba nchi endapo itaamua kuingiza Kiswahili ndani ya madarasa ya sekondari. Baadhi ya matatizo ni ya hhakika na mengine ni ya kufikirika. Tujipe fursa ya kuyaangalia.

Matatizo ya kutumia Kiswahili

Matatizo au vikwazo vinavyotajwa sana tunaposhauri kuongezeka kwa matumizi ya Kiswahili katika uhai wa taifa hili ni mengi. Aidha, sababu za kushikilia matumizi ya Kiingereza katika shule za sekondari ni nyingi. Lakini Maghimbi (1995) angepata nafasi ya kutangaza sababu za kushikilia Kiingereza na kutupilia mbali Kiswahili – mwenyewe sababu hizo anaziita Tasinifu – ametaja 25. Baadhi ya tasnifu hizo ni: kuogopa kuwa wa kwanza katika mabadiliko, ukosefu wa vitabu vya taaluma, gharama, kuanguka kwa viwango vya elimu nchini, kuvunjika kwa mashirikiano ya kitaalam na uchanga wa Kiswahili. Kwa makusudi ya makala haya matatizo haya yatawekwa katika matapo makuu mawili: nafsi ya lugha yenyewe na utekelezaji wa sera ya Kiswahili sekondari. Tutaanza na nafsi ya lugha.

Nafsi ya lugha
Hofu kubwa ambayo inasambazwa na washauri ina mwega ndani ya Kiswahili chenyewe. Kiswahili, inadaiwa, hakina msamiati. Ingawa dai hili ni kweli lakini inasaliti udhaifu wa aina tatu. Mosi, inaelekea wanaotangaza dai hili kwa pumzi zote, hawajui lugha ni nini. Kwa nafsi yake, lugha ni sarufi yake na si msamiati wake. Hawajui kwamba asilimia kubwa ya msamiati wa Kiingereza – lugha inayotukuzwa kupita kiasi – si wake; ni wa kusharabu. Hivyo basi, matumizi ya Kiswahili katika nyanja za elimu hayawezi kuleta matatizo kwani, ikiwa kitapungukiwa na msamiati, Kiswahili kinaweza kuchukua/kutohoa maneno kama ilivyofanyika katika ukuaji wa Kiingereza. Kinachotakiwa kubadilika si msamiati bali sarufi. Wanafunzi shuleni hawashindwi kwa sababu ya msamiati mgumu bali wanashindwa na sarufi ngumu ya Kiingereza.
Pili, njia ya kuondoa tatizo la msamiati, washauri wanasema, ni kuahirisha kwanza matumizi ya Kiswahili ili uundwe msamiati kwanza, Ushauri huu hudhihirisha kutojua kuwa lugha, kama ulivyo utamaduni, hujirekebisha kwa kulingana na mahitaji mapya. Isitoshe, maana ya ushauri huu ni kutaka Tanzania itayarishe Kiswahili kwa matumizi yatakayotangazwa baadaye. Ushauri huu, zaidi ya kuhuzunisha, unapingana na maumbile. Maneno na semi hujengwa na wazungumzaji wenyewe katika hizo shughuli zao. Mkemia atazua maneno kwa kulingana na kile anachokiona akilini mwake au tuseme katika taaluma yake. Wasio na utaalamu wa kemia hawawezi kuratili hali halisi ya taaluma hiyo. Kwa maana hii, tunapozungumzia mabadiliko ya lugha ya kufundishia, tunatangaza changamoto kwa wataalamu wote – wakemia, wafizikia, wahandisi n.k – wajenge msamiati na semi mwafaka kwa taaluma zao. Kwa mantiki hii hata kesho Kiswahili kingeweza kuingia katika maabara ya shule ya sekondari maadam walimu ni Watanzania.
Tatu, washauri hao wanasahau kuwa vinavyoelea vimeundwa. Ikiwa lugha yetu ina kasoro zozote ni juu yetu sote kusimama kidete kuirekebisha katika hima ya kujiletea maendeleo yetu. Kuijenga lugha hii ikawa chombo chenye uwezo wa kuchanuza mikondo yote ya fikra za wanajamii ni hatua muhimu katika maendeleo.Aidha, ikiwa lugha ni miongoni mwa mbinu za jamii za utashi nusura, kwa kufanya hivyo, jamii hujijengea mtandao wa mawasiliano utakaolea changilizi ya maarifa. Taifa ambalo watu wake wamegawanyika kimawasiliano hawana changilizi ya maarifa. Maana, inagawa Kiswahili kinazungumzwa na wote, lakini fikra na mijadala ya kitaalamu, hivi sasa, haina mikondo katika lugha hii. Hivyo, kama Waaarabu wa Pemba, Kiingereza ndicho kilemba cha wasomi na asiye na kilemba hicho hafaidiki na mazungumzo yao.
Hofu nyingine maarufu iliyoenea na inaendelea kusambazwa na washauri inahusiana na kukosekana kwa vitabu vya kitaaluma. Wataalamu wetu – pengine pamoja na sisi wenyewe – wanagwaya wanapoichungulia maktaba ya Kiswahili ilivyosinyaa. Wanadai kwamba, vitabu vyote vya kitaaluma vimeandikwa kwa Kiingereza. Hivyo haitakuwa busara wala kwa faida yetu endapo tutaacha Kiingereza kitoke madarasani mwetu. Hofu hii nayo ni imara kwa kiasi fulani cha masafa. Lakini ikiangaliwa kwa jicho la karibu, itaonekana kuwa hoja hii inalegalega na inatia kiinimacho katika tatizo. Hii, kwa upande mwingine, ni hoja inayodai kuwa jambo linalotafakariwa haliwezekani mpaka Kiswahili kiwe na vitabu vyake vya kitaaluma. Kila mtu anajua kuwa kutokuwako kwa vitabu vya taaluma ni jambo la hakika. Lakini kama ilivyokuwa katika suala la msamiati, matatizo ya kukosekana kwa vitabu ni changamoto kwa wataalamu wetu. Wataalamu wetu wataanza kuandika vitabu vya taaluma zao baada ya kujua kuwa kuna wasomaji na/au wanunuzi.
Utaratibu wa kuanza kutumia Kiswahili katika sekondari, ninathubutu kusema, ndio ambao utajenga mwega wa usomi wenye manufaa. Sasa hivi wasomi wengi hawafikirii kuandika vitabu kwa sababu wanaweza kufanya kazi zao kwa kutegemea vitabu vya jamii nyingine. Hivyo kitendo cha kuanzisha mijadala ya kitaalam kwa Kiswahili kitaanza kutengua mihimili ya utegemezi wa kisomi.
Swali ambalo linakuja akilini haraka ni lile linalohusu vitabu vya kutumiwa wakati vya Kiswahili vinaandikwa. Aidha, kutokuwako na vitabu vya taaluma si suala la kuzua au la kukichukia Kiswahili. Namna ya kulikabili suala hili ni kukifanya Kiswahili kifundishie kwa sauti, Kiingereza kifundishie kimya kimya. Maana ya tamko hili ni kwamba Kiswahili kiendeshe majadiliano darasani na Kiingereza kiwapatie wasomi wetu maarifa kutoka vitabuni. Kwa maneno mengine Kiingereza kiendelee kuwa lugha ya maktaba. Utaratibu huu usiwe wa muda bali uwe wa kudumu katika jamii. Utaratibu huo utawataka wanafunzi wasome vitabu na marejeo mbalimbali kwa Kiingereza lakini ufundishaji, majadiliano, mazoezi na tathmini vifanyike kwa Kiswahili. Aidha, huu ndio utaratibu unaotumika katika ufundishaji wa Isimu katika Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu.
Utaratibu wa kumlazimisha mwanafunzi aeleze maarifa yake kwa lugha asiyoijua, kama ilivyo sasa, hutupotezea watu wengi wenye vipawa. Katika makala fulani, (Mochiwa 1991:15) niliuliza swali: ikitokea kwamba mwanafunzi ameulizwa: What is ice? na akajibu kwa Kiswahili: ni maji yaliyoganda: tutasema amekosa au amepata? Tukisema amekosa, amekosa nini? Haya ni miongoni mwa matatizo yanayodhihirisha udhaifu wa sera yetu ya lugha katika elimu. Kwa sera hii wasio na vipawa vya kujifunza lugha hupotea hata kama wanavyo vingine ambavyo vingeleta tumaini jipya katika jamii. Kwa hekima ya Tanzania, mpaka sasa, kujua ni kujua Kiingereza na /au kwa Kiingereza.
Suala lililojadiliwa hivi punde ni suala la uhusiano wa lugha na elimu. Tumezoezwa kuchanganya elimu na lugha. Mtu anayemwaga Kiingereza vizuri hufikiriwa kuwa ana akili, tena amesoma sana. Maana, kama Whiteley (1971) alivyopata kutamka, kwetu, Kiingereza ni elimu, na elimu ni Kiingereza. Katika miaka kumi hii iliyopita, kigezo kikuu cha tathmimi ya watu ya kuanguka kwa kiwango cha elimu nchini ni udhaifu wa wanafunzi katika Kiingereza. Inadaiwa kuwa, watoto wanafika kidato cha nne bila uwezo wa kuandika barua ya mistari miwili ya Kiingereza. Kitu ambacho wangezingatia ni kwamba Kiingereza kimemzuia mwanafunzi asikuze uwezo wake wa kufikiri na kutanzua tata. Lakini badala ya kulizingatia tatizo hili wazazi wengi wanasikitika kuwa watoto wao wanajua Kiswahili tu, eti hii ni hasara!Wazazi wanaosema kuwa watoto wao wamepata hasara kwa kujua Kiswahili wanaendeleza fikra ya usawa wa Kiingereza na elimu. Lakini kinyume cha bahati, watoto wao hata hicho Kiswahili hawakijui! Aidha, kujua Kiingereza fasaha si usomi wala akili. Lugha ni suhula tu (facility) ya kuchanuzia yale tunayofikiri. Hivyo, katika tathmini ya elimu haitoshi kupima uwezo wa kusema tu bila ya kupima uzito wa lile linalosemwa pia. Tathmini sahihi ya viwango vya elimu ni lazima izingatie jinsi Kiingereza kilivyosahilisha au kuleta pingamizi katika uelewa wa wanafunzi. Kiingereza ni chanzo cha kuanguka kwa viwango vya elimu kwa sababu hakifai kwa matumizi ya lugha ya kufundishia.
Gharama
washauri wetu wameshikilia kidinindi kuwa kukiingiza Kiswahili katika madarasa ya sekondari kuna gharama kubwa na za namna mbalimbali. Miongoni mwa gharama hizo ni ile ya matayarisho. Watu wengi wanafikiri au ni ubinu wao wa kuchelewesha utekelezaji wa matumizi ya Kiswahili sekondari – ni lazima vitabu vyote, vya kiada na ziada, vifasiriwe kwa Kiswahili. Mradi huo utaligharimu taifa mabilioni ya fedha. Baadhi ya washauri, Maghimbi (1995) kwa mfano, wanatangaza kwa midomo mipana kwamba Kiswahili hakiwezi kuwa lugha ya kufundishia mpaka vitabu vyote vya kitaaluma vimefasiriwa na kuchapishwa. Kwa kweli ikiwa Tanzania inafikiri haiwezi kutumia Kiswahili katika shule za sekondari mpaka vitabu vyote vya taaluma vifasiriwe ni kana kwamba inasema Kiswahili hakitafundishia elimu ya sekondari.
Kwa nchi maskini kama yetu, kuamua kubadilisha lugha ya kufundishia ni ujuba ikiwa, mradi wa kufasiri vitabu ni muhimu kiasi hicho. Ilivyokuwa hakuna haja ya kufasiri kitabu chochote, hakuna sababu ya kuchelewesha hatua ya kukiingiza Kiswahili katika madarasa ya sekondari. Mabadiliko ya lugha ya kufundishia ni hatua muhimu na ya kwanza kabla ya kuingia katika mchakato wa maendeleo ya kijamii. Kwamba hadi leo tumo katika majadiliano ni dalili kuwa bado hatujapafahamu pa kuanzia safari yetu ya maendeleo.
Gharama nyingine kubwa iliyojizonga akilini mwa washauri wetu ni ule uwezekano wa kutoka kwenye kambi ya wasema Kiingereza. Itakumbukwa kwamba nchi za Kiafrika zimo katika makambi ya lugha za wale waliozitawala. Tanzania na nchi nyingine zilizotawaliwa na Waingereza ni za kambi ya Anglophone. Zilizotawaliwa na Wareno zimo katika kambi ya Lusophone na za Wafaransa ni za kambi ya Francophone. Kwa mtazamo huo washauri, kama Maghimbi (1995) wanafikiria haitakuwa salama kama tutatoka kwenye kambi ya Waingereza. Msingi wa rai hii uko mara mbili. Kwa upande mmoja, washauri wanalinda mazoea na kwa upande wa pili wanafirki kwamba Watanzania watakuwa wameandalika kwa masomo nchi za nje. Pengine inasemekana kuwa kuendeleza mtindo huu kunawapatia Watanzania uwezo wa kuwasiliana na watu wa nje.
Tathmini yagharama hizi inaonesha kuwa ushauri unaelekeza kwenye haja ya uanachama wa u-anglophone bila kujiuliza kama upo uwezekano wa kuupata. Isitoshe ushauri haukuzingatia kwamba kazi kubwa ya lugha katika elimu si kutufutia uanachama. Ushauri umeendelea kulifumbia macho suala la kutojulikana kwa Kiingereza nchini Anayetumia lugha kwa masomo au kutafuta urafiki ni yule anayejua lugha yenyewe. Je, ni nani ambaye, hadi sasa, hajui kwamba Kiingereza hakijulikani nchini kwa kiwango cha kuendeshea mawasiliano yanayoweza kuonesha fikra pevu?
Zaidi ya kufumbia macho suala la kutojulikana kwa Kiingereza, kuna ule ushauri wa kuwaandaa Watanzania kwa masomo ya nje ambao ni dhaifu. Hii ni kwa sababu, kwa hali ilivyo sasa hivi, si sahihi kufikiri kila penye asasi ya elimu patazungumzwa Kiingereza. Watanzania wamekwenda  China, Japani, Ujerumani na sehemu nyingine nyingi mbalimbali ambazo hazitumii Kiingereza. Ke bado watu wale wamesoma. Pengine ingekuwa bora kwa Mtanzania kujifunza lugha yoyote kule inakozungumzwa na wazawa wake kuliko tunavyofikiri tunajifunza Kiingereza hapa ambapo hakina wazungumzaji wazawa.
Hasara ya kung’ang’ania Kiingereza
Baada ya mjadala wa ushauri wa kutelekeza Kiswahili, kikabakia lugha ya kuuzia karanga kwa muda wote huu, ni vyema tutafakari kidogo hasara au tuseme, gharma ya kung’ang’ania Kiingereza. Gharama kubwa tunayobeba ni kuendeleea kwa kutenguka kwa elimu. Kiingereza kinaendelea kuzuia makusano kati ya walimu na wanafunzi na kwa hivyo umaizi wa ubongo wa mtoto haupati nafasi ya kuongezeka. Kwa maana hii, mchakato wa elimu mpaka sasa haujaweza kuwasaidia wanafunzi kujifunza kufikiri, na hasa kufikiri haraka haraka. Ingawa sina ushahidi wa kisayansi kuhusu jambo hili, lakini ninahisi kwamba, kwa kuwa hatukimiliki ipasavyo, tunapokitumia, Kiingereza kinapunguza kasi ya kufikiri. Kama Powell (1997) anavyosema, kujifunza lugha ni kupata mamlaka ya kutawala mazingira na kutawala ulimwengu wa uzoevu. Wanafunzi wasiojua Kiingereza watatarajiwa vipi kutawala mazingira yao au taaluma zao?
Kung’ang’ania Kiingereza katika kuendeshea maisha ya taifa hili kunawanyima wanajamii haki za msingi za binadamu. Nitachukua mifano kutokana na kuchungua sehemu tatu. Sehemu ya kwanza inahusu haki ya kuishi duniani. Hospitali zimesambazwa nchini kuhakikisha kuwa kila mwanajamii anapata huduma anapougua ili apone. Wahudumu wetu wamejifunza huduma hiyo kwa Kiingereza. Ikiwa sote tunajua kuwa Kiingereza hakifahamiki vizuri, tuna hakika gani kuwa Madaktari na Manesi wao wanaelewana? Lini taifa litagundua hatari ya unasibu wa lugha? Unasibu wa lugha ndio uliosababisha neno moja la Kiarabu lipokewe kwenye Kiingereza kuwa ‘risk’ kitu au tukio la hatari na katika Kiswahili ‘riziki’ kitu cha kukidhi haja! Ingawa sina takwimu,- na si rahisi kuzipata-lakini kuna uwezekano mkubwa wa kuwako kwa vifo ambavyo vimetokana na mawasiliano butu kati ya Daktari na Nesi, au kutoiva kikamilifu kwa Daktari au Nesi mwenyewe.
Sehemu ya pili inahusu sheria. Ninaambiwa mpaka leo, waheshimiwa wanasheria huweka kumbukumbu zao kwa lugha ya Kiingereza, hata kama washitaki na washitakiwa wametumia Kiswahili au lugha nyingine. Wao wameaminiwa kuwa ‘wafasiri’ wasiojikwaa! Lakini kwa mujibu wa ninavyojua dhati ya lugha, unasibu wake pamoja na matatizo yanayofafanuliwa katika nadharia za tafsiri (ang. Nida 1964), ninahisi kwa nguvu kuwa wako watu ambao wamezama magerezani kwa kutokana na mabadilikobadiliko haya ya lugha. Kosa la tafsiri linaumba hatia ya mshitakiwa. Jambo kama hili linapotokea, kuna mwanajamii mmoja ambaye atakuwa amenyimwa haki yake ya kimsingi. Ni dhahiri kwamba jamii inashindwa kulinda haki za watu.
Sehemu ya tatu inahusu haki ya kujiendeleza. Tanzania ilikuwa maarufu duniani kwa kuweka kipaumbele katika maendeleo ya elimu ya watu wazima. Kinyume cha bahati, jitihadi za mtu anayeanza kujielimisha haziwezi kuvuka elimu ya msingi. Hii ni kwa sababu akipita kiwango cha shule ya msingi hawezi kusonga mbele kwa kuwa hajui lugha ya Kiingereza. Jambo hili linazidi ugumu kwa kuwa mhitimu wa kisomo chenye manufaa atajiendeleza nje ya mazingira ya shule. Sasa ikiwa wanafunzi wa kidato cha kwanza, wenye miaka kumi na nne au kumi na tano, wanashindwa kujifunza Kiingereza mbele ya mwalimu wao, mtu aliyeanza kisomo cha manufaa na miaka arobaini ataweza kujifunza Kiingereza chini ya mwembe? Ikiwa hana Kiingereza, mwanakisomo atajiendelezaje? Kwa utaratibu wa sasa, matumizi ya Kiingereza yanazuia mienendo ya elimu nchini. Hivyo elimu si ya wote bali ni haki ya wachache, tena, wenye kipawa madhubuti cha lugha.
Suala hili lililojadiliwa hivi punde halimwathiri mtu mmoja mmoja tu, bali jamii nzima. Jamii inawazuia watu ambao, kama wangepata nafasi ya kujiendeleza, wangekuwa wabunifu na watundu wa manufaa kwa taifa. Ama, hali hii nayo inahuzunisha. Huenda taifa halipati wasiwasi kwa imani kuwa wavumbuzi au wagunduzi watapatikana Chuo Kikuu. Lakini, kwamba rai hii imepotoka, inaonekana kwa kusoma kwenye magazeti kuwa kuna watu vijijini wanaweza kutengeneza vitu vya kisasa kama silaha. Aidha, labda kwa sababu ya imani ileile ya wavumbuzi kuwa watu wa Chuo Kikuu, watu hawa wanapogundulika hupata misukosuko. Isingekuwa hivyo, watundu hawa wangepewa kipaumbele. Watu hawa, kwa kuonekana umuhimu wao kwa taifa, wangeengwaengwa na kubembeslezwa wajiunge na jeshi ili taifa lifaidike.
Makusudi yangu hapa ni kwamba si siku zote wavumbuzi watatoka vyuoni. Kuendelea na matumizi ya Kiingereza katika elimu ya juu ni kuziba uwezekano wa kupatikana kwa watu walio na vito muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Pamoja na umaarufu wake – kwa herufi na harufu-Tanzania haiwezi kukipa Kiingereza kiti kikakaa hapa nchini kwa makusudi ya kuongeza ukuzaji wa umaizi wa Watanzania. Hii haina maana kuwa Kiingereza hakifai au hakitakiwi nchini. Haya si makusudi ya makala. Bali kinachokusudiwa hapa ni kwamba, kwa mazingira tuliyo nayo, upeo wa ufundishaji, muda na mbinu za ufundishaji, si rahisi kukifundisha kikajulikana ganda na kiini. Aidha, wataalamu wengi (Qorro, et al 1987, Trappes – Lomax et al (eds) 1982) wameonesha wazi kuwa Kiingereza hakiwezi kufundishwa hadi aliyefundishwa akafikia kiwango cha umilisi wa kuchambua fikra au viumbile dhahania. Ziko sababu nyingi zinazosababisha hali hii, lakini hapa tutachambua mbili: Muda na mazingira. Tutaanza na muda.
Muda
Tanzania haina budi kuelewa kuwa kufundisha na hasa kujifunza lugha kunataka muda mrefu. Kujua kuwa hivyo ndivyo, tujiulize mtoto mchanga anayejifunza lugha yake ya maziwa anahitaji muda gani. Mtaalam mmoja (ang. Hammerly 1982) alidai kuwa mtoto anatumia saa 18,000 za kujifunza lugha hiyo ya kwanza. Kwa kuwa suala hili halikutiwa ndani ya mizani zetu sawasawa, Tanzania inaona kuwa saa 800 za kujifunza Kiingereza (soma. Mochiwa 1991) katika shule ya msingi zinatosha. Baya zaidi ni kwamba, ilihali anapojifunza lugha ya kwanza mtoto anakutana nayo kwa wakati mwafaka, wakati ambao ubongo na hisia havijui kukataa wala kudharau, lakini mtoto wa shule ya msingi anakutana na Kiingereza kwa wakati usio mwafaka. Anakuwa amekwisha vuka umri wa kawaida wa kujifunza lugha.
Tunapoendelea kuwalinganisha watoto wawili hawa, tunaona kwamba anayejifunza lugha ya mama hana ratiba yoyote ya shughuli. Yeye hatumwitumwi na wala halazimishwi kujifunza kipengee fulani kilichomo mwenye muhtasari. Lakini huyu aliye shuleni hupewa hizo saa 800 za Kiingereza ndani ya ratiba ya masomo mengine. Kana kwamba hii haitoshi, hizo saa mia nane zimetawanywa kwa kipindi cha miaka mitano, kuanzia darasa la tatu hadi la saba. Yule mtoto aliye nyumbani ana saa nyingi na haziingiliwi na mambo mengine isipokuwa usingizi tu.
Tunapolinganisha muda huu mrefu wa kusharabu lugha, itakuwa hatuangalii mambo kiuhakikifu (objectively) kama tutatarajia Kiingereza kijengeke katika akili ya mtoto kwa muda huu mfupi. Ikiwa tunataka Kiingereza kijengeke basi inabidi ratiba ya shule isogelee hizo saa 18,000. Lakini hii ina maana kwamba, kwa muda wa miaka isiyopungua mitatu, Watanzania hawana budi wazamishwe kwenye programu ya Kiingereza. Kwa rai yangu hatua ya namna hii haiwezekani kwa sababu nyingi, lakini kubwa, ni gharama yake ya mali na muda.
Mazingira
Mtoto anapojifunza lugha ya kwanza anafunikwa na lugha anayojifunza. Mtoto anayejifunza Kiingereza shuleni hana bahati hiyo. Kwake, Kiingereza hakisikiki, maana hakitumiki kuongoza maisha ya kila siku. Hivyo, dafaa za kukisikia Kiingereza ni chache sana. Ni lugha ambayo itasikika darasani na si muktadha utakaomfanya mtoto aone jinsi lugha yenyewe inavyofanya mambo yaende.
Mazingira ya ufundishaji wa Kiingereza ni ya kuigiza heba ambayo haipo katika jamii. Maadamu ‘Kiingereza’ maana yake ni ‘kwa namna’ au kwa ‘mila ya’ au ‘mwenendo wa’ Waingereza, Kiingereza ndani ya mazingira ya Kiswahili kinahitaji jitihada kubwa za kukifanya kimee. Kujifunza namna au mwenendo wa Kiingereza kunahitaji uamuzi na nidhamu ya kisaikolojia. Heba hiyo hiyo iliyosisitizwiwa umuhimu wa kujivunia. Uswahili, Uafrika ndiyo hiyo hiyo inayoingizwa katika majaribu ya kuenenda naau kujifasili kwa Kiingereza. Migongano ya aina hii ndiyo inayosababisha elimu nchini Tanzania kuwa maigizo na si maisha.
Mwisho
Mchakato wa elimu katika Tanzania hauna tofauti na maigizo kwa sababu mbili. Kwanza, ingawa unatakiwa umfanye mpokeaji awe ‘huyo mtu wa ndoto’ lakini kwa kutokana na sera ya lugha iliyopo, mchakato wa elimu unamfanya mpokeaji awe KAMA ‘huyo mtu wa ndoto’ Mtu huyo wa ndoto si Mtanzania bali ni Mwingereza. Ilivyokuwa haiwezekani, Mngoni kuzaa Mzigua, vivyo hivyo Mtanzania hawezi kuzaa Mwingereza. Kwa mantiki hiyo, mchakato wa elimu unampeleka mtanzania kuzaa ‘Kizuu cha Mwingereza’ au Mmarekani, mpokeaji wa elimu ya Tanzania atakuwa anaingiza heba ya Kiingereza na/au Kimarekani kwa mwenendo wa fikra na msemo. Mpokeaji huyo hataishi kwa heba ya kwao bali ataishi kwa heba ya kuazima.
Pili, mpokeaji wa elimu hii atakuwa ana utapia elimu mkubwa kwa sababu ya pingamizi la lugha ambalo humkabili katika mchakato mzima. Hatapata kiwango cha weledi sawa na mtu wa ndoto ambaye Tanzania imemwekea. Katika mazingira haya, mfumo wa elimu unakuwa mchakato wa kuingia utumwani na si wa kumpatia uhuru kama unavyotarajiwa na Nyerere na Freire (op.cit). Anapoumaliza mfumo wa elimu, mpokeaji hatalingana na Mwingereza kwa uwezo wa kuchambua, kuwaza, kusasanya mambo wala kusasanyua. Kutokana na kuung’amua ukweli huu, mhitimu atasema moyoni mwake ‘Wazungu,wazungukeni!’
Zaidi ya kuufanya kuwa mchakato wa kuvuruga mfumo wa kujiamini wa mpokeaji sera ya lugha inamnyima mpokeaji haki za msingi za kibinadamu. Haki hizo ni pamoja na ya kujielimisha, ya mazingira ya kupata tiba isiyo na madhara kwake na ya kupata haki mbele ya sheria. Watanzania hawana hakika ya kukuza akili zao, ya kupata matibabu sahihi wala ya kutendewa haki wanapokabiliwa na daawa. Yote haya ndiyo matokeo ya maigizo ya kielimu yanayosababishwa na matumizi ya Kiingereza katika elimu. Wanaonufaika katika vurumai hii ni watu wenye kipawa cha lugha tu. Aidha vurumai hii hunufaisha sana mataifa ya nje kwa sababu kwao Watanzania ni ‘wateja’.

<![CDATA[NAFASI YA KISWAHILI KATIKA JAMII YA AFRIKA MASHARIKI, KATI NA KUSINI]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1197 Wed, 08 Sep 2021 12:47:46 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1197 Massamba, D.P.B na wenzake (2001:26-28) Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu. TUKI.Dar es Salaam
Katika sehemu ya 1.1 tulisema kwamba lugha ya Kiswahili ndiyo lugha muhimu sana katika eneo lote la Afrika Mashariki na kati. Tulisema vile vile kwamba lugha hii ina nafasi ya pekee katika nchi ya Tanzania na Kenya. Hii ni kwa sababu lugha hii ni lugha ya taifa na pia lugha rasmi katika nchi zote mbili. Wananchi wengi wa Afrika mashariki wanajua na huitumia lugha ya Kiswahili katika mawasiliano yao. Kwa hiyo ina maana kwamba lugha hii ina nafasi ya pekee katika mambo muhimu kama utamaduni, siasa na uchumi. Pengine yafaa kufafanua kidogo jambo hili.
Wataalamu wengi wa masuala ya utamaduni hukubaliana kwamba kwa kiasi kikubwa lugha ni kielelezo cha utamaduni. Ukweli huo hujidhihirisha katika lugha yenyewe. Ukiichunguza kwa makini lugha yoyote iwayo utagundua kwamba ina vipengekele mbalimbali vya utamaduni vya wasemaji wa lugha hiyo ambavyo vinajitokeza ndani mwake. Mfano mdogo tu ni kwamba wakati kwa Mswahili ndugu wa kiume wa baba ni baba na ndugu wa kike wa mama ni mama kwa mzungu sivyo, kwani Mzungu ana baba (father) mmoja tu na mama (mother) mmoja tu; Mzungu ana dhanna za half-brother (nusu-kaka?) na half-sister (nusu-dada?), ambazo hazimo katika lugha ya Kiswahili. Mswahili akiamua kutumia lugha ya Kiingereza atashindwa kuvieleza vipengele hivi vya utamaduni; hivyo itakuwa njia moja wapo ya kumomonyoa utamaduni. Kwa hiyo basi, matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Afrika Mashariki yataendelea kuudumisha utamaduni wetu.
Nafasi ya lugha ya Kiswahili katika masuala ya siasa ni jambo ambalo halihitaji kupigiwa ngoma. Tumekwishaona jinsi lugha hii inavyotumika kama chombo muhimu sana cha kuunganisha watu na kuleta umoja, Kwa kuwa lugha hii ndiyo itumiwayo na watu wengi katika Afrika mashariki ndiyo lugha peke yake inayoweza kuleta uelewano katika masuala ya kisiasa kwa wananchi wa eneo hili, siyo lugha nyingine. Aidha, lugha ya Kiswahili ndiyo lugha muhimu iwaunganishayo wananchi wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini. Kwani katika maeneo haya kuna lugha mbalimbali zinazotumika, lugha peke yake inayotumika kote ni Kiswahili.
Lugha ya Kiswahili ni lugha muhimu sana katika Afrika Mashariki kwa upande wa masuala ya uchumi. Lugha ambayo inafahamika kwa watu wengi ndiyo lugha ifaayo kutumiwa katika mambo na mawasiliano ya kibiashara. Tangu zamani wananchi wa Afrika Mashariki wamekuwa wakiitumia lugha hii katika shughuli zao za kibiashara. Kiswahili kinamwezesha Mkenya kwenda Tanzania, hata vijijini akafanya biashara bila wasiwasi wowote; halikadhalika Mtanzania anaweza kwenda Kenya vijijini akaendesha shughuli zake za kibiashara bila tabu ya kutafuta mkalimani. Na kwa hakika hii si kwa Tanzania na Kenya tu; hali ni hiyo hiyo kwa upande wa mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kwa kiasi fulani hata katika Rwanda na Burundi pia.
Kwa ujumla lugha ya Kiswahili ni lugha muhimu katika harakati zozote za wananchi wa sehemu za Afrika Mashariki na Kati. Kwa misingi hiyo, lugha hii haina budi kukuzwa na kuendelezwa zaidi ili matumizi yake yazidi kuwa mapana na toshelevu kwa kiwango kinachotakiwa katika sehemu zote hizi.
]]>
Massamba, D.P.B na wenzake (2001:26-28) Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu. TUKI.Dar es Salaam

<![CDATA[KISWAHILI NI LUGHA YA AFRIKA]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1196 Wed, 08 Sep 2021 12:34:14 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1196 Kiswahili ni kati ya lugha nne za taifa la DRC. Rais wa DRC, Joseph Kabila, anaongea Kiswahili sanifu. Kwa vile rais wa nchi anaongea Kiswahili sanifu, hii itakuwa chachu ya kukiboresha Kiswahili cha DRC, na kukieneza kwenye nchi zinayoizunguka DRC, kwa upande wa kaskazini. Kiswahili ni lugha ya taifa la Tanzania, Uganda na Kenya. Ingawa Kiswahili, si lugha ya taifa la Rwanda na Burundi, lakini vita vya maziwa makuu vimekifanya Kiswahili kuzungumzwa karibu na watu wote wa Rwanda na Burundi. Mipango iko mbioni kukifundisha Kiswahili kwenye shule za msingi za Rwanda na Burundi. Msukumo huu unatokana na nchi hizi mbili kuomba kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Kwenye miaka ya themanini, Kenya ilifanya jitihada nyingi kukiendeleza Kiswahili. Kiswahili lilifanywa somo la lazima kwenye shule za sekondari. Matokeo yake yameanza kujitokeza miongoni mwa kizazi kipya cha Kenya, kwa kuongea Kiswahili sanifu kuliko kile Kiswahili cha kizazi cha miaka ya nyuma. Pia ongezeko la vyuo vikuu nchini Kenya vimeongeza ufanisi wa Kiswahili, kila mwaka zaidi ya vijana 2000 wanaokifahamu vizuri Kiswahili wanahitimu vyuo vikuu. Hii itachangia kuwapata walimu wazuri wa kufundisha lugha ya Kiswahili na wataalamu wazuri wa lugha ya Kiswahili. Ingawa magazeti ya Kiswahili hayajaongezeka kwa kasi kubwa, lakini uchapishaji wa vitabu vya Kiswahili uko juu zaidi nchini Kenya kuliko Tanzania. Kenya inatoa vitabu vingi vya Kiswahili na usambazaji wake ni mzuri kuliko wa Tanzania. Pia Wakenya wanasoma vitabu kuzidi watanzania. Bidii ya Kenya, katika kukikuza Kiswahili itachangia kwa kiasi kikubwa kuieneza lugha hii katika nchi zinazopakana nayo upande wa kaskazini, kama vile Somalia, Sudan na Ethiopia. Tukizingatia kwamba wakimbizi wengi kutoka katika nchi hizi wamekuwa wakiishi nchini Kenya. Hizi ni dalili za kukipanua Kiswahili kuwa lugha ya Afrika nzima!
Tofauti na Tanzania, ambapo Kiswahili, karibu kinatumika kila sehemu katika jamii, Kenya Kiswahili kinatumika kama lugha ya siasa, dini na wasomi. Ingawa hii inaonyesha picha hasi ya kukiendeleza Kiswahili katika jamii nzima ya Wakenya, lakini pia kwa njia hii Kiswahili kinaweza kuongeza kasi ya kuongea lugha ya kisayansi na kiteknolojia na kujikita katika utandawazi kwa haraka zaidi ya Tanzania.
Kwenye miaka ya Sabini, Iddi Amin, alikitangaza Kiswahili kuwa lugha ya taifa ya Uganda. Lakini waganda na hasa “Baganda” hawakukipokea Kiswahili kwa vile wanaipenda sana lugha yao ya “Luganda”. Sababu nyingine ni kwamba wanajeshi wa Iddi Amin, walitumia Kiswahili kama lugha ya jeshi. Matendo maovu ya jeshi la Iddi Amin na mauaji yaliyofanywa na jeshi hilo, yalikipaka matope Kiswahili na kuwafanya watu wa Uganda, kukichukie. Pia waganda walimchukulia mtu anayeongea Kiswahili kuwa ni “Mswahili” mjanja mjanja na mtu asiyeaminika. Lakini pia waganda wengine walikihusisha Kiswahili na Uislamu, maana Waislamu walikitumia kama lugha ya dini kwa kukichanganya Kiswahili na Kiarabu, au kutafsiri Kiarabu katika kistahili. Kwa nchi kama Uganda, ambayo imepitia migongano na michafuko mikubwa ya kidini, kujifunza Kiswahili ilikuwa ni sawa na kuamsha vita kati ya Wakristu na Waislamu.
Jeshi la Museveni, na Museveni mwenyewe walitumia Kiswahili. Hadi leo hii Kiswahili ni lugha ya jeshi la Uganda. Hii haikuwavutia waganda waliokuwa wamechoka na utawala wa kijeshi. Hivyo Kiswahili ilibaki ni lugha ya jeshi na biashara ya magendo kati ya Uganda, Tanzania na Kenya.
Kwa sababu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, ambayo waganda wanaiona ina faida kubwa kuliko hasara, wameanza kuwa na hamu ya kujifunza Kiswahili. Serikali ya Uganda imepitisha kwamba kuanzia mwaka kesho Kiswahili litakuwa somo la lazima katika shule za msingi na sekondari. Huu utakuwa ni msaada mkubwa wa kukikuza Kiswahili na kukipatia picha ya kuwa lugha ya Afrika ya Mashariki na hatimaye Afrika nzima.
Kwenye makala iliyopita nilielezea jinsi Tanzania, ilivyofanikiwa kukisambaza Kiswahili nchi nzima na kuifanya lugha hii kuwa ya taifa ingawa haikutangazwa kisheria. Hivyo sirudii haya kwenye makala hii. Labda kutaja tu hapa kwamba Mwalimu Nyerere, kukubali Dar-es-Salaam, kuwa kitovu cha mapambano ya uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika, kulisaidia kukisambaza Kiswahili katika nchi hizo za Kusini mwa Afrika.
Mpango wa IPP Media Group wa kuanzisha gazeti la Kiswahili liitwalo Afrika ya Mashariki, utakuwa mchango mkubwa katika kukifanya Kiswahili lugha pana inayoweza kukubalika Afrika nzima. Huu unaweza kuwa uwanja wa kuzua malumbano na majadiliano ya kuelekea kukikomaza Kiswahili kama enzi zile washairi wa Afrika ya Mashariki walivyokuwa wakijibizana na kulumbana katika uwanja wa ushairi. Bado kuna ushahidi wa kutosha jinsi mashairi yalivyosaidia kukikuza Kiswahili.
Vita vya ukombozi kusini mwa Afrika, vimekifanya Kiswahili isiwe lugha ngeni katika nchi za Zimbabwe, Namibia, Angola, Msumbiji na Afrika ya kusini. Lakini pia wakimbizi wa Sudan, Somalia na Ethiopia, walioishi Kenya na Uganda wamesaidia kukisambaza Kiswahili hadi kwenye nchi zao. Wafanyabiashara wa Kisomali ambao hufanya kazi ya kusafirisha mizigo kwenye magari ya mizigo kwenye maeneo yote ya Afrika ya Mashariki, Kati na kusini wamekuwa mabalozi wa kuisambaza lugha ya Kiswahili.
Ingawa kuna lugha zingine za Afrika zinazozungumzwa na watu wengi kama Kihausa. Kiswahili kinachomoza zaidi kwa sababu si lugha inayofungamana na kabila au taifa Fulani. Mfano ni tofauti na Kihausa. Ingawa Kihausa kinazungumzwa na watu wengi wa Afrika ya Magharibi, kinafungamana na kabila kubwa la Wahausa ambalo limekuwa kwenye migogoro na mapigano na makabila mengine kwa muda wa miaka mingi. Lengo lolote la kutaka kukifanya Kihausa kuwa lugha ya Afrika nzima, ni lazima litaamsha chuki miongoni mwa makabila makubwa ya Afrika magharibi ambayo nayo yangependa lugha zao zichukue nafasi ya kwanza.
Profesa Mulokozi, kwenye mada yake: “Kiswahili as a National and International Language” Anaelezea kisa alichosimuliwa na Kanyama Chiume, pale Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, mwaka 2002; kwamba mwaka 1959, wapigania uhuru wa Afrika walikuwa na mkutano ulioitishwa na Sekou Toure, katika mji wa Conakry, Guinea, ili kupanga harakati za kudai uhuru. Mkutano huu ulihudhuriwa na watu kutoka nchi zilizokuwa zikiongea Kiingereza na Kifaransa. Tatizo kubwa lililojitokeza katika mkutano huo ni lugha ya kutumia. Wajumbe walikaa wakitafakari zaidi ya masaa mawili juu ya lugha ya kutumia katika mkutano huo ili wote waweze kusikilizana na kuchangia hoja. Waliotoka kwenye nchi zilizokuwa zikiongea Kiingereza hawakufahamu Kifaransa na wale waliotoka kwenye nchi zilizokuwa zikiongea Kifaransa hakukifahamu Kiingereza. Huu ulikuwa mtindo wa wakoloni, wakutaka kufundisha lugha zaidi ya lugha yao. Baada ya muda mrefu wa kutafakari namna ya kuendesha kikao hicho kigumu, Kanyama Chiume, ndiye aliyeokoa jahazi. Alipendekeza: Kwa vile yeye alifahamu Kiswahili na Kiingereza, na Patrice Lumumba, alifahamu Kiswahili na Kifaransa, mkutano ungeweza kuendelea kwa wajumbe waliokuwa wakitumia Kiingereza, kuongea kwa Kiingereza na Kanyama Chiume, kutafsiri yote kwa Kiswahili ili Patrice Lumumba, aweze kutafsiri Kiswahili kwa Kifaransa. Vilevile na wale wa upande wa Kifaransa waliongea kwa Kifaransa na Patrice Lumumba, alitafsiri kila kitu kwa Kiswahili ili Kanyama Chiume, aweze kutafsiri kwa Kiingereza.
Kufuatana na maelezo ya Kanyama Chiume, mkutano huo uliendelea kwa ufanisi mkubwa ingawa ulikuwa wa kuchosha. Lakini wajumbe walielewana vizuri kwa msaada wa Lumumba na Kanyama Chiume waliokuwa wakikifahamu Kiswahili. Ndiyo kusema Kiswahili kiliwaunganisha Waafrika katika mkutano huo. Na kama nilivyosema hapo juu, ni kwamba Kiswahili ni tofauti na Kihausa au lugha nyingine maana si lugha ya Kabila Fulani au taifa Fulani. Mfano katika mkutano huu wa Conakry wa mwaka 1959, Patrice Lumumba alitokea Congo na Kanyama Chiume, alitokea Malawi! Kiswahili, haikuwa lugha ya kabila la Lumumba na wala haikuwa lugha ya kabila la Kanyama Chiume. Tunaweza kusema Kiswahili ilijitokeza kama lugha ya Waafrika katika mkutano huo. Huu ulikuwa ni mwanzo mzuri, kama si uvivu na kutojali kwa watu wanaojiita chimbuko la Kiswahili, kama vile watanzania, leo hii Kiswahili, kingekuwa kimepiga hatua kubwa katika Bara zima la Afrika na duniani kote.
Mfano mwingine anautoa Profesa Mulokozi, ni ule wa mwanamapinduzi Che Guevara, wakati akiongoza harakati za mapambano ya vita vya msituni kuikomboa Congo, akiwa bega kwa bega na Laurent Kabila, alilazimika yeye na wapiganaji kutoka Cuba, kujifunza Kiswahili, hadi yeye Che Guevara, akabatizwa jina la Kiswahili la Tatu! Waligundua kwamba hii ndio lugha pekee iliyoweza kuwaunganisha Waafrika waliokuwa wakipigana msituni na kwamba adui aliyeongea Kiingereza na Kifaransa asingeweza kufuatilia nyendo zao katika mawasiliano. Che Guevara, ni mwanamapinduzi anaheshimika duniani kote na historia yake imejaa mvuto wa pekee na kati ya mvuto huu ni lugha ya Kiswahili!
Lakini kitu kinachokifanya Kiswahili kionekane kuwa ni Lugha ya Afrika, wale wanaoisukuma mbele si watu wa Afrika Mashariki na wala si watu wanaotoka kwenye nchi ambazo zinaaminika kuwa ni nchi za Kiswahili kama Tanzania na Kenya. Tumeona mfano wa Kanyama Chiume na Lumumba. Mfano mwingine ni wa Chisano kutoka Msumbiji kwenye nchi inayoongea Kireno, na lugha nyingine za Kiafrika ambazo ni kubwa pia, kuwa rais wa kwanza wa Afrika, kuhutubia Umoja wa nchi za Afrika, kwa lugha ya Kiswahili.
Mkutano wa viongozi na wataalam wa maziwa makuu uliofanyika Aprili 2002 kwa kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere, ulitoa mwito wa kukifanya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya mataifa ya maziwa makuu.
Katika miaka ya sitini Mwandishi Maarufu wa Nigeria Wole Soyinka , alitoa mwito wa kukitangaza Kiswahili kuwa ni lugha ya Afrika nzima. Nigeria, kuna lugha kubwa za Kiafrika, lakini Wole Soyinka, aliguswa na lugha ya Kiswahili! Baadhi ya vitabu vyake vimetafsiriwa katika lugha ya Kiswahili.
Mwito huu ulirudiwa tena na mwandishi mwingine wa Ghana, Ayi Kwei Armah, mnamo mwaka wa 1985, yeye alikiona Kiswahili kama lugha ambayo inaweza kuingiza maneno mengi kutoka kwenye lugha nyingine za Kiafrika na kukifanya Kiswahili kuwa tajiri kwa msamiati. Ayi Kwei Armah, aliishi na kufanya kazi Tanzania. Alifundisha kwenye Chuo cha Walimu Chang’ombe. Kitabu chake “Te Beautiful Ones Are Not Yet Born” kimetafsiri katika Kiswahili: “Wema Hawajazaliwa”.
Kiswahili kilitumika kwenye mkutano mkuu wa UNESCO, Parish, Ufaransa. Hizi ni dalili kwamba Kiswahili kinatambulika kuwa ni lugha kubwa kutoka Afrika.
Mwanzoni mwa miaka ya themanini, UNESCO iliamua juzuu nane (8-volume) za historia ya Afrika zitafsiriwe kwenye lugha zaidi ya tatu za Kiafrika, Ukiondoa Kiarabu, lugha nyingine zilizopendekezwa ni Hausa,Fulfulde na Kiswahili. Juzuu za Kiswahili zimekamilika na kuchapishwa. Huu ni mchango mkubwa wa lugha ya Kiswahili katika historia ya Afrika. Kwa wale wanaofikiri kwamba Kiswahili si lugha ya kisomi, juzuu hizi ni changamoto kubwa kwao. Na huu ni ushahidi kwamba Kiswahili ni lugha ya Afrika.
Kwa vile utandawazi unatishia kuzimeza nchi za ulimwengu wa watu na hasa Afrika, kwa karibu kila kitu, ni vyema na Afrika itafute kitu cha kuuza kwenye utandawazi. Tukishindwa kuuza vitu vingine kama utamaduni, kazi za mikono na bongo zetu, basi tuuze lugha zetu na hasa zile zinazoelekea kukubalika Ulimwengu mzima kama vile Kiswahili.
Na,
Padri Privatus Karugendo.
]]>
Kiswahili ni kati ya lugha nne za taifa la DRC. Rais wa DRC, Joseph Kabila, anaongea Kiswahili sanifu. Kwa vile rais wa nchi anaongea Kiswahili sanifu, hii itakuwa chachu ya kukiboresha Kiswahili cha DRC, na kukieneza kwenye nchi zinayoizunguka DRC, kwa upande wa kaskazini. Kiswahili ni lugha ya taifa la Tanzania, Uganda na Kenya. Ingawa Kiswahili, si lugha ya taifa la Rwanda na Burundi, lakini vita vya maziwa makuu vimekifanya Kiswahili kuzungumzwa karibu na watu wote wa Rwanda na Burundi. Mipango iko mbioni kukifundisha Kiswahili kwenye shule za msingi za Rwanda na Burundi. Msukumo huu unatokana na nchi hizi mbili kuomba kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

<![CDATA[Katiba itambue Kiswahili kuwa Lugha ya Taifa]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1195 Wed, 08 Sep 2021 12:26:05 +0000 MwlMaeda]]> https://jifunzekiswahili.co.tz/showthread.php?tid=1195 [Image: katiba.jpg]
Mjumbe wa Tume ya Katiba, Mohamed Yusuf Mashamba akifafanua jambo wakati wa ukusanyaji wa maoni katika Kijiji cha Kitere, Halmashauri ya wilaya ya Mtwara mkoani hapa juzi.Kushoto ni Mjumbe mwingine wa Tume hiyo, Dk.Sengondo Mvungi. Picha na Abdallah Bakari
Kwa ufupi
“Wenyeviti wa vijiji, vitongoji walipwe mishahara, wazee umri wa miaka  60 walipwe posho ya uzeeni kila siku” alisema Singa.
Abdallah Bakari, Mtwara
DIWANI wa Kata ya Ziwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, mkoani hapa, Mohamedi Mkiwa (72) amependekeza katiba ijayo itamke kuwa Kiswahili ndiyo lugha ya Taifa na shughuli zote za nchi zitaendeshwa kwa lugha hiyo.Akitoa maoni yake juzi mbele ya Tume ya Katiba ilipofanya mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi hao katika kijiji cha Madimba, Ziwani na Msangamkuu, diwani huyo alisema katiba ya sasa haitambui Kiswahili kama lugha ya Taifa.
Alisema kukosekana kwa kipengele hicho kunasababisha kupuuzwa kwa lugha ya Taifa na watendaji wa serikali wanaotumia lugha za kigeni katika shughuli za kila siku za utendaji wa serikali.
“Katiba itambue kuwa Kiswahili ni lugha ya Taifa na itamke wazi kuwa shughuli zote za kiserikali zitaendeshwa kwa kutumia lugha ya Kiswahili” alisema Mkiwa.
Aidha diwani huyo alipendekeza Rais kuongezewa madaraka kwa kuitwa Rais mtendaji badala ya sasa ambapo shughuli za kiutendaji zipo chini ya Waziri Mkuu.
Mkazi mwingine wa Ziwani Hassan Singa (76), alipendekeza viongozi wa vitongoji na vijiji walipwe mishahara kwa kuwa wanatumia muda wao mwingi kuhudumia wananchi.

Naye Mkazi wa Madimba,Abdallah Lina (54) alipendekeza siku ya kupiga kura wapiga kura wote walipwe posho kwa sababu wanatumia muda wa siku nzima kushinda kwenye foleni wakisubiri kupiga kura.
Maoni hayo yalihojiwa na Mjumbe wa Tume hiyo, Mohamedi Mashamba, aliyehoji iwapo haoni kwa kufanya hivyo wananchi watakuwa wameuza haki yao, swali ambalo lilijibiwa na Lina kuwa “Viongozi wamegeuza uongozi kuwa mtaji basi ni heri na sisi tukaambulia japo kidogo”
Mashamba alimweleza Lina kuwa iwapo maoni yake yatapitishwa kutakuwa na hatari kubwa ya nchi kutawaliwa na mafisadi, kwa kuwa wataweza kuwalipa wapiga kura.
Awali Mwenyekiti wa mkutano huo, Dk. Sengondo Mvungi  aliwataka wananchi hao kuwa wawazi kutoa maoni yao ili watunge Katiba itakayoondoa matatizo yao.
Mvungi alisema ni vema kwa wananchi wakaelewa kuwa Katiba waitungayo itadumu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo na kwamba ni muhimu matatizo yao wakayapa kipaumbele ili yapatiwe ufumbuzi na katiba yao.
“Katiba ndiyo maisha yako ya kila siku, sema unataka iweje, msiwe na hofu maoni yote yatachukuliwa, kwa maandishi, vinasa sauti na video” alisema Dk. Mvungi. Chanzo>>>>>
]]>
[Image: katiba.jpg]