MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MISEMO YA VYOMBO VYA USAFIRI (3)

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
MISEMO YA VYOMBO VYA USAFIRI (3)
#1
Misemo yenye Ujumbe kuhusu Maisha kwa Ujumla
      1.     “Dunia tupo stand”
Maana:
· Hapa duniani sote ni wasafiri ingawa kila mtu
ataondoka na gari lake na kwa wakati wake, maana magari yapo kwenye foleni.
·  Hapa duniani kila mtu anapita tu, kila mtu
anayeishi afahamu hilo.
·  Kila mtu atakufa.
·  Tutende mema hapa duniani ili kujiandalia maisha
ya huko tuendako.
·   Maisha ya mwanadamu ni mafupi, muda wowote mtu
anaweza kuaga dunia.
      2.     “Fanya kazi ulioomba”
Maana:
·    Usiingilie kazi ambazo hazikuhusu, hasa kama
hujaombwa kushiriki.
·    Weka bidii kwa kazi inayokupa riziki kwa
kujituma.
·   Acha uvivu na uzembe
·   Jail majukumu yako.
      3.  “Heshima ya mtu kazi”
Maana:
·   Kazi ndiyo msingi wa kupatikana kwa ustawi wa
kila eneo katika maisha ya mtu.
·   Mtu asiye na kazi halali, hukosa heshima katika
jamii.
·   Tuache uvivu na uzembe.
·   Siku zote mtu mwenye kazi ndiye anayeheshimiwa
katika jamii.
            4.  “Heshimu kazi”
          Maana:
·   Kazi yoyote ile unayoifanya hata kama
inakuingizia kipato kidogo iheshimu, kwani ndiyo inayoendesha maisha yako.
·   Jail sana kazi kuliko mshahara.
·  Kazi ndiyo mhimili wa maisha yako.
           5.  “Dunia haina huruma”
     Maana:
·  Maisha ni magumu
·  Ulimwengu ni kama mwalimu afundishaye mambo
mbalimbali ya maisha kutokana na matukio na mikasa inayompata mwanadamu.
         6.  “Askari hachagui msitu”
      Maana:
· Mtu aliye jasiri hana kisingizio katika kufanya analotakiwa kulifanya
         7. “Posho  oya oya”
   Maelezo:
    Dhana ya “oya oya” ni msimu.
    Maana:
·  Malipo hayatoshi
·  Malipo au mshahara unapatikana kwa taabu
· Mshahara unatolewa (na bosi  au mmiliki) kwa malalamiko au manung’uniko.
         8. “Baba hapendi mbio”
    Maana:
·  Wahenga wametufundisha tuwe wastaarabu.
·   Si vyema kuwa na papara tuwapo barabarani,
hususan kwa wanaoendesha vyombo vya moto.
       9. “Dagaa ndo’ mboga, kuku mbwembwe tu!”
      Maana:
· Maisha huendeshwa kwa vitu vya kawaida, visivyo
ghali
·  Maisha hayataki ujivuni
·  Tuepuke uziada katika maisha
·  Kila mtu anatakiwa afanye kitu kilicho ndani ya
uwezo wake
·  Vitu vya ziada huwa na gharama na athari katika
kuyaendesha maisha ya kila siku
·  Mtu hula akipatacho
           10.  “Kufunga siyo kazi, kazi kuilinda swaumu”
    Maana:
·  Kuna tofauti kati ya kushinda na njaa na
kushinda na swaumu
·  Swaumu ina misingi yake ambayo inatakiwa
ifuatwe.
·   Kila jambo linatakiwa lifanywe kwa uhakika
kufuatana na miongozo yake.
·  Kukithiri kwa vishawishi
         11.  “Dah, najuta kuchukua majibu”
    Maana:
·   Nimekutwa na maambukizi (ya UKIMWI) baada ya
kwenda kupima.
         12.  “Fainali uzeeni”
     Maana:
·  Vema tujiandae na maisha ya uzeeni.
·  Maisha ya uzeeni huandaliwa wakati wa ujana na
utu uzima, hivyo, makosa yoyote ayafanyayo mtu katika kipindi  chake cha ujana au utu uzima huweza kumtesa
wakati wa uzee.
         13.  “Iga ufe”
    Maana:
·    Siyo vema kuiga mambo kibubusa (bila
kutafakari).
·    Kuiga au kufuata mkumbo bila kufikiri huweza
kuleta madhara.
·   Fanya jambo kulingana na uwezo wako.
·   Usiige kitu anachofanya mtu mwingine, kwani
baadaye kitu hicho kitaweza kukuletea madhara.
          14.  “Maisha kutafuta, si kutafutana”
      Maana:
·   Kila mtu ajibidiishe kujitafutia ustawi wa
maisha yake
·   Siyo vizuri kuyachunguza maisha ya mtu mwingine
·  Kila mmoja afanye kinachomhusu, na si kutaka
kujua mambo ya mtu mwingine
          15.  “Kifo kiboko ya nyodo”
     Mana:
· Kifo ndicho kinachokomesha maringo ya viumbe hai
wote wanaoringa hapa duniani
Chanzo:
 
Ponera, A. S na Kikula, I.S,  (2017) Misemo
ya Vyombo vya Usafiri. UDOM. Afroplus Industries, Ltd.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)