Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'BIASHARA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BIASHARA'

Neno *biashara* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana ya mchakato wa kununua na kuuza mali au vitu.
*Biashara sukutu*: aina ya uuzaji na ununuaji wa bidhaa bila maongezi.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *biashara* limechukuliwa kutoka maneno mawili ya  Kiarabu  *'bay-un* *(soma: bay-un/bay-an/bay-in  بيع)**  na *'shiraau* *(soma: shiraaun/shiraa-an/shiraain    شراء)**  yenye maana zifuatazo:
*Bay-un* ni:
1. Tendo-jina *Masdar مصدر* ya kitenzi cha Kiarabu *baa-a  باع* chenye maana ya *ameuza* .

2. Kitendo cha kuchukua kitu na kulipa thamani yake.

3. Kitendo cha kutoa kitu na kuchukua thamani yake.

4. Bidhaa za kuuzwa. 

Na *shiraau  شراء* ni:

1. Kitendo cha kutaka kununua kitu na kulipa thamani yake.

2. Mahali pa kuuza na kununua; *suuq سوق*, *soko* .

Kinachodhihiri ni kuwa maneno mawili ya Kiarabu *'bay-un wa shiraa بيع و شراء* yalipoingia katika Kiswahili na yalitoholewa kuwa neno *biashara* na neno hili la Kiswahili halikubadili maana ya msingi ya maneno hayo ya Kiarabu, kuuza na kununua.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)