Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Baba alivyookoa ndoa ya kijana wake
#1
Baba alivyookoa ndoa ya kijana wake
Iko hivi, katika familia moja yenye mabinti watatu na kijana mmoja wa pekee wa kiume siku moja paliingia tafrani. Kijana wa familia alipofikia umri wa kuoa wazazi na dada zake walihakikisha kijana mpendwa wao anapata mke wa ndoto zake lakini jukumu la kumtafuta mke mwenyewe likawa la muoaji.
Kijana hatimaye aliamua kumtambulisha binti mmoja aliyekuwa naye katika mahusiano kwa muda uliotosha kuwashawishi wote kujiona kila mmoja ameumbwa kwa ajili ya mwenzake.
Baada ya kutambulishana hatua za kuhalalisha uhusiano wao zilianza na hatimaye wakafunga pingu za maisha wakawa mke na mume halali. Mungu akawajalia watoto wawili katika ndoa yao.
 Kadiri siku zilivyosonga wakazidi kuzoeana na mauzauza ya ndani ya ndoa yakaanza kujitokeza kama ilivyokawaida ya vijana wengi wakishazoeana katika ndoa. Makandokando huwa hayakoseni. Mume akaanza vituko mara kuchati kwingi, kuchelewa kurudi na mwisho hata mapenzi kwa mkewe yakawa haba tofauti na ilivyokuwa awali. Katika hali hiyo mke akagundua dhahiri kuna jambo zi bure.
Uvumilivu ulipomshinda mke naye akaona isiwe tabu bora ajiliwaze kwa namna inayomfaa. Hapo mke naye akajipatia kiben ten wake akawa wanapeana raha duniani. Mapenzi kama kikohozi huwezi kukificha. Wakanogewa mpaka mume akagundua na hapo mfumo dume ukajidhihirisha waziwazi kuwa kuchepuka achepuke mume si mke.
Mume alipojiridhisha kwa Ushahidi alionao, siku ya siku akaikusanya familia yake na kwenda kwa wzazi wake. Kufika huko tena akaitisha kikao, ndugu wote wakakusanyika kusikiliza neno la kijana wao wa pekee mpendwa.
Hatimaye kijana akatumbua jipu na kumwaga ushahidi alionao licha ya ushahidi kuwa wa maneno matupu. Mama wa kijana na dada wa kijana hawakutaka kusikiliza la mkwezi wala mfua madafu macho na vidole vyao vikawa juu ya mke wa kijana wao huku wakimtuhumu na kumshutumu kwa maneno makali. “Unataka kutuulia kaka yetu, malaya mkubwa wewe.” Binti wa watu hakutia neno akaamua machozi yamtetee tu.
Wakati hayo yote yakiendelea baba wa kijana alikuwa kimyaaaaaa akitafakari nini cha kufanya. Waswahili wanasema utu uzima dawa. Baada ya muda baba akasema, haya tumekusikia kijana wetu hebu na wewe bitni yangu tueleze una lipi la kusema juu ya tulichoelezwa? Binti yule kwa sauti ya chini sana akasema baba kama anayoyasema ni kweli basi Mungu atajua.
Baada ya kimya kirefu baba wa kijana akasema haya sasa naomba mnisikilize. Kwanza, wewe kijana wangu urudi kwako huyu mkeo na watoto wabaki hapa. Pili, leo hiihii nitasafiri kwenda kutafuta dawa ya kumaliza tatizo hili. Kisha kusema hayo baba akaondoka kwenda alikokuita safari. Huku nyuma binti yule aliishi pale kwa mateso makali na manyanyaso mengi lakini alivumilia akisubiri muujiza utakaoletwa na baba mkwe wake.
Baada ya siku mbili kupita baba yule alirejea nyumbani na kuita tena familia yake yote. Hapo akatoa rai kuwa huko alikokwenda amefanikiwa kupata dawa ya kumaliza tatizo la ndoa ya kijana wao lakini dawa yenyewe inatakiwa kuandaliwa na mtu “safi” na hasa ndugu wa damu. Hapo akamuomba mama mzazi atayarishe dawa hiyo. Mama mzazi wa kijana aliruka futi mia moja akikataa kutayarisha dawa hiyo kwa kuhofia masharti ya “usafi” uliosemwa na baba.
Mpira ukarushwa kwa dada mkubwa wa kijana, naye akaruka na kukataa kabisa kuandaa dawa hiyo kwa kuhofia madhara yanayoweza kumkuta kwani naye hakuwa “safi” kama sharti la dawa linavyotaka.
Baada ya ndugu wote wa kijana kukataa kuandaa dawa baba wa kijana akaamuru wote waondoke na wamuache yeye na kijana wake. Walipoondoka wote baba akamgeukia kijana wake na kumuuliza, “Vipi mwanangu umejifunza nini?” Kijana akajibu nimegundua kumbe hata wewe ni uvumilivu tu ndio unakuweka na mama bila, kumbe hata mama anachepuka!
Baba akamwambia kijana wake, “mchukue mkeo mkaendelee na maisha yenu”.
Je, na wewe umejifunza nini?
 
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)