Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'ARKISUSU/ARKASUSU/URUKUSUSU'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ARKISUSU/ARKASUSU/URUKUSUSU'

Neno arkisusu/arkasusu/urukususu katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya dawa ya kutibu kikohozi inayotokana na miti shamba.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili arkasusu/arkisusu/urukasusu linatokana na nomino ya Kiarabu irqusuus (soma: irqusuusi/irqasuusi/irqisuusi  عرق السوس/عرقسوس)  lenye maana mmea kutokana na familia ya corneas ambao kinywaji chake kina manufaa anuai mwilini na poda yake hutumiwa katika matibabu ya ngozi.
Waingereza huuita mmea huu licorise/liquorice .

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu irqusuusi/irqussuusi lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno arkasusu/arkisusu/urukususu lilichukua maana mpya ya dawa ya kutibu kikohozi inayotokana na mitishamba.
TANBIHI:
Dawa hii ni maarufu sana katika uwanja wa tiba na hutumiwa kutibu uzito wa ulimi kwa aliyepatwa na ugonjwa wa kiharusi.
Pia hutumiwa kwa kuchangamsha mwili na kuimarisha misuli. KHAMIS S.M. MATAKA.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)