MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'AMARI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'AMARI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AMARI' 

Neno *amari*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana ya mnyororo au kamba inayofungia nanga katika chombo cha baharini/majini; *kamba ya kufungia nanga.* 

Katika lugha ya Kiarabu neno *amari* linatokana na neno la Kiarabu *ammaar (soma: ammaarun/ammaaran/ammaarin  عمار)* lenye maana  zifuatazo:

1. Mmea wa harufu nzuri uliokuwa unawekwa kama  ishara ya kuwaamkia wafalme. 

2. Mmea wa harufu nzuri huwekwa ili  kupendezesha kikao cha kunywa vinywaji.

3. Maamkizi, salamu.

4. Kila kinachovaliwa kichwani kama vile kilemba, kofia au chochote kile.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *ammaar عمار*  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno *amari* lilichukua maana mpya ya *kamba ya kufungia nanga* na kuacha maana zake katika lugha ya asili - Kiarabu.

Istilahi wanayoitumia Waarabu kwa kamba ya kufungia nanga ni *hablul mirsaat  حبل المرساة*; *silsilatul mirsaat سلسلة المرساة*  na pia neno *alkaabil الكابل* lililochukuliwa na kutoholewa kutoka neno la Kiingereza ' *cable* '

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)