Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA MANENO ' ADA' na 'ADAA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO ' ADA' na 'ADAA'

Neno *ada* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Nomino* : Gharama au karo anayolipa mtu ili apatiwe huduma fulani kwa mfano katika elimu, burudani au kupata uanachama katika chama.

2. *Nomino:* Mila na desturi za jamii fulani. (Mfano: Kila kabila lina ada zake za maziko.)

3. Kawaida katika kufanya jambo. (Kwa mfano: Kunywa chai kila jioni ni ada yake.)

Kuna methali: *Ada ya mja hunena, muungwana ni kitendo.*

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ada* (soma: *aadatun/aadatan/aadatin عادة* ) lina maana zifuatazo:

1. *Nomino* : Jambo ambalo mtu amezoea kulifanya na kulikariri.

2. *Nomino* : Kulitekeleza jambo ipasavyo na ndani ya wakati.

3. *Nomino* : Kutimiza wajibu na kuukamisha.

4. Jambo linalokariri kutokea kila mwezi; ada ya mwezi.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *aadatun/aadatan/aadatin عادة*) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *ada*  maana yake katika Kiarabu haikubadilika na lilichukua dhana mpya ya *gharama au karo anayolipa mtu ili apatiwe huduma fulani a*  dhana ambayo  Kiarabu huitwa *rasmun/rusuumun*  *رسم/رسوم* .

Neno *adaa* katika lugha ya Kiswahili lina maana ya 'ulazima unaompasa mtu kuutekeleza kwa mujibu wa maamrisho ya dini kwa mfano kuswali, kufunga na kutoa Zaka.

Neno hili *adaa* (soma: *adaa-un/adaa-an/adaa-in أداء* ) katika lugha ya  Kiarabu lina maana ya:

1. Kulifikisha jambo na kulitimiza au kulitekeleza kwa namna inavyopasa.

2. Kuzitamka herufi za lugha kwa namna inayopasa.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili *adaa*(soma: *adaa-un/adaa-an,/adaa-in أداء*) lilipoingia katika Kiswahili maana yake katika Kiarabu haikubadilika ingawa lilijifunga katika wajibu wa kutekeleza maamrisho ya dini.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)