MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'JABALI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'JABALI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'JABALI'

Neno jabali  katika lugha ya Kiswahili ni Nomino [Ngeli: li-/ya-, wingi: majabali] yenye maana zifuatazo:

1. Mwamba mkubwa uliochomoka juu ya ardhi au maji.

2. Mwinuko mkubwa wa jiwe juu ya ardhi.

Neno jabali  pia ni Nomino [Ngeli: a-/wa-, wingi: majabali] yenye maana zifuatazo:

1. Mtu mwenye umbo kubwa na nguvu nyingi.

2. Mtu aliye gwiji katika jambo.

Msemo: Jabali la muziki: bingwa katika masuala ya muziki. 

Kadhalika, neno jabali ni Nomino [Ngeli: i-/zi] yenye maana ya mshono wa kanzu  uliopo kati ya bega moja hadi jingine upande wa mgongoni.

Katika lugha ya Kiarabu neno jabali linatokana na neno la Kiarabu jabal (soma: jabalun/jabalan/jabalin  جبل) lenye maana  zifuatazo:

1. Eneo kubwa la ardhi lililojitokeza juu zaidi ya sehemu nyingine za ardhi; mlima.

2. Mtu thabiti asiyeyumba katika misimamo  na maamuzi yake.

3. Nyoka, ibnatul jabali  ابنة الجبل.

4. Sauti inayojirudia baada ya mawimbi ya sauti kugonga mahali na kumrudia mzungumzaji aghalabu hutokea pangoni, msituni au kwenye jengo kubwa na tupu; mwangwi .

5. Kundi la watu; umma.

6. Uwanja; uga.

7. Kiongozi wa watu/ukoo.

8. Mwanazuoni.

Kinachodhihiri ni kuwa neno jabalun  جبل  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno jabali lilibeba maana mpya na kuziacha zile maana za neno hili katika lugha ya Kiarabu. 

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply
#2
Safi sana, Uga huu unamaarifa mengi sana
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 2 Guest(s)