MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'MSHAHARA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'MSHAHARA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'MSHAHARA' 

Neno *mshahara*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: u-/i-, wingi: mishahara]* yenye maana zifuatazo:

1. Malipo ya mwezi anayopewa mwajiriwa kwa kazi aliyofanya. 

2. Ujira anaolipwa mtu na mwajiri wake kila baada ya kipindi fulani kwa kazi aliyotumikia.

Katika lugha ya Kiarabu neno *mshahara* linatokana na neno la Kiarabu  *shahru (soma: shahrun/shahran/shahrin شهر)* lenye maana zifuatazo:

1. Mwezi, sehemu moja ya sehemu kumi na mbili za Kalenda ya mwaka unaozingatia  mzunguko wa Mwezi *As-Sanatul Qamariyyatu السنة القمرية* au mwaka unaozingatia mzunguko wa Jua *As-Sanatush Shamsiyyatu السنة الشمسية*.

2. Mwezi Mwandamo.

3. Ulimwengu.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *shahrun  شهر* lilipoingia katika Kiswahili lilitamkwa *shahara* kisha likaingia katika ngeli ya *m-/mi* - na kupatikana neno *mshahara* lililochukua maana mpya ya *ujira anaolipwa mtu na mwajiriwa wake kwa kazi aliyoifanya katika kipindi maalumu.*

*TANBIHI* :
Maneno ya Kiarabu yenye maana ya ujira anaolipwa mtu na mwajiri wake mwishoni mwa mwezi ni *raatibun shahriyyun راتب شهري* mshahara wa mwezi au *badalun shahriyyun بدل شهري* posho ya mwezi.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)