Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Eleza umuhimu wa kutumia Lugha fasaha katika mawasiliano
#1
Jawabu.
Lugha ni sauti za nasibu zenye kuleta maana ambazo zimekubaliwa na wanajamii kutumika kwa mawailiano miongoni mwao.
Kulingana na tafsiri hii , tunabaini kwamba, sifa mojawapo ya lugha ni kutoa maana ambayo inaeleweka kwa watumiaji wake. Kinyume na hivyo haiwezi kuwa lugha. Ndiyo sababu milio ya viumbe, kama vile wanyama, ndege, na wadudu siyo lugha kwa vile hazitoi maana. Kwa hiyo kama tusingekuwa na lugha wanaadam tusingeweza kuwasiliana kwa maana tunvyofanya sasa. Umuhimu wa kutumia lugha kwa ufasaha katika mawasiliano husaidia yafuatayo;-
1. Hudumisha taratibu za kisarufi za lugha; Lugha ya Kiswahili ina taratibu zake. Mano mtu anapoema “Juma hukuji shuleni leo” anapuuza ufasaha,ingawa maana inaeleweka lakini baadhi ya maneno ya tungo hiyo yana ukakasi kwa yeyote anaejali ufasaha wa lugha.
2. Kuhakikisha kukamilika kwa mawasiliano baina ya watu; Njia moja ya kutekeleza haya ni kukwepa matumizi ya misimu kwa mfano sentensi inayosema “Ukikanyaga miwaya hatima yake ni kifo” sentensi hii itapewa maana tofauti, kama vile kukanyaga waya za umeme au UKIMWI,kwa hiyo sentensi hiyo si fasaha kwa kuwa haitoi maana kwa uwazi.
3. Hudumisha Kaida za lugha kutegemeana na mila na desturi; Lugha ya Kiswahili ina kanuni zake. Mfano mtoto akisema “habari za asubuhi” kwa mtu mzima,anapuuza kaida za Kiswahili. Desturi za Kiswahili zinamtaka mtoto aamkie “shikamoo”
4. Huhakikisha Uwiano; Ufasaha unahakikisha kuwepo kwa uwiano wa maneno kutokana na upatanisho wa kisarufi. Maneno katika sentensi zifuatazo hayana uwiano:
(a) Migonjwa ya UKIMWI imekonda sana

(b) Maradhi ya UKIMWI Unaua

Sentensi fasaha ni:
(a) Mgonjwa wa UKIMWI amekonda sana

(b) Maradhi ya UKIMWI huua

5. Huipa lugha urembo na mvuto: Mfano;Harusi ya dada yangu ilikuwa ya kipekee na sijaona mthili yake mpaka sasa, ilijaa chereko na hoihoi zilizopigiwa mfanokwa muda mrefu. Hoihoi zilifukuza joto na kukaribisha upepo mwanana, nao ndege wa angani waliokuwa karibu waliungana na wale wa mbali wote walijumika kuishangilia nakala hiyo.
6. Huweza kukuza hadhi ya Lugha;

Lugha yoyote, dhamani yake hutegemea namna inavyotumiwa na watumiaji wake walio wazawa na wageni.kutokana na kutumia lugha kwa ufasaha tunaweza kukuza hadhi yake katika jamii dhidi ya lugha nyengine.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)