MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

MFANO WA NGONJERA : TUONDOE KUPE

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
MFANO WA NGONJERA : TUONDOE KUPE
#1
 TUONDOE KUPE
Mume
Mke wangu wasikia, yasemwayo redioni?
Wakubwa wahutubia, na kusema hadharani,
Kupe wanatuibia, watutia umaskini,
Kaka yako huyu John, arudi kwao shambani.
 
Mke
Lo! Kaka wamchukia, kisirisiri moyoni?
Hana baya katulia, hana kukuru nyumbani,
Kazi ajitafutia, tamjalia Manani,
Nawe nduguyo yu ndani, vipi haendi shambani?
 
Mume
Hivi waniiga kumbe, vile ndugu yumo ndani?
Hana mke yu msimbe, nitamtupia nani?
Maneno hayo usambe, wanitia ghadhibani,
Kaka yako huyu John, arudi kwao shambani.
 
Mke
Wako si mwana mkembe, ni mkubwa mara thani?
Kila mara umpambe, na chakula kila fani,
Huyu wangu umchimbe, umrudishe nyumbani,
Nawe nduguyo yu ndani, vipi haendi shambani?
 
Mume
Mjumbe wa nyumba kumi, hukumwona jioni?
Alisema kwangu mimi, nitafikishwa bomani,
Kwa siasa ya uchumi, tusiweke watu ndani,
Kaka yako huyu John, arudi kwao shambani.
 
Mke
Hendi aniache mimi, tufukuzwe sote ndani,
Kwa nduguyo hungurumi, kwani ana kazi gani?
Hana kazi na hasomi, kazi yake ukunguni.
Nawe nduguyo yu ndani, vipi haendi shambani?
Mume
Kaka yako ndiyo kupe, anatunyonya nyumbani,
Na kila kitu tumpe, wala hana shukrani,
Madeni mengi tulipe, waleta hawa wahuni,
Heri watoke nyumbani, wote waende shambani.
 
Mke
Na wako pia ni kupe, azimio labaini.
Linasema tuwakwepe, wasio kazi mjini,
Wanyonyaji tuwatupe, wajitegemee nchini,
Heri watoke nyumbani, wote waende shambani.
 
(Ngonjera za Ukuta, uk. 54-55, M. E. Mnyampala)
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)