MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI : MIMBA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI : MIMBA
#1
Mimba
Umeificha kwa dela, myezi miwili mitatu,
Tumbo lajaa hujala, ndani wameweka kitu,
Mzigo kuvaa ndala, peku wenda hata mwitu,
Yakuwa kama Uyoga, Mimba sio kichuguu.

Mimba sio kichuguu, wapaswa itunza vyema,
Tena sio kitunguu, wende kuungia nyama,
Wataka vunja mguu, kwa kuutaka mnyama,
Yakuwa kama Uyoga, Mimba ni ya myezi tisa.

Mimba ni ya myezi tisa, dada usije itoa,
Wapenda kula anasa, na tabu zipo tambua,
Utavifunga vitasa, funguo zende potea,
Yakuwa kama Uyoga, Mimba utajalilia.

Mimba utajalilia, ukiikosa nasema,
Wakunga watakujia, vijembe visivyo koma,
Nyimbo watakuimbia, asiye mwana dhalima,
Yakuwa kama Uyoga, utazaa chanda chema.

Utazaa chanda chema, kikufae maishani,
Ujana ukisimama, vitoe vya kitovuni,
Usije anza lalama, kwa kukikosa kidani,
Yakuwa kama Uyoga, Mimba y’ondoa sonona.

Faharasa:
Sonona~msongo wa mawazo
Dhalima~dhalimu
©Adabeth Mwanambuu, 2019.
Malenga wa Ufipa
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)