MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
UHAKIKI WA TEUZI ZA NAFSI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
UHAKIKI WA TEUZI ZA NAFSI
#1
Francis H.G. Semghanga: Teuzi za Nafsi
SURA YA SITA
Diwani ya Teuzi za Nafsi ni mkusanyo wa tenzi tano: “Ewe Mama Mpenzi”, “Kidani cha Huba”, “Ewe Mwana”. “Siasa Yetu” na “Ujamaa Vijijini.” Kwa vile kwa namna moja ama nyingine tenzi hizi zote zinaingiliana hapa na pale kifani na kimaudhui, tutaziangalia kidhamira kwa jumla badala ya kuzichambua moja moja.
DHAMIRA KUU
Dhamira kadhaa zinajitokeza katika tenzi za diwani hii. Kati ya hizo, kuu ni kama saba hivi:
1. Mapenzi
2. Mila na desturi za jadi
3. Umuhimu wa elimu
4. Ukamilifu wa mtu na ulu wake
5. Ndoa katikajamii
6. Nafasi ya mwanamke katika jamii
7. Siasa.
Mapenzi
Mshairi anajaribu kujibu swali ta maana yu mapenzi halisi. Katika “Ewe Mama Mpenzi,” tunaonyeshwa mapenzi ya mtoto kwa mama yake. Mapenzi haya yamejikita katika “deni” alilonalo mtoto kwa mama yake hasa kutokana na uchungu wa kumbeba tumboni na hatimaye kumzaa na kumlea. Hapa mshairi anaonyesha kuwa mapenzi ya mama hayawezi kulipwa kwani hayakadiriki.
Katika “Kidani cha Huba” mapenzi baina ya mwanamume na mwanamke yanaonyeshwa katika sura zake mbalimbali. Kwa kupitia katika ndoto (beti za 34-61) mwpndishi anatuonyesha mapenzi mabaya yanayofuata sura na vitu kama ile nguo na umbo. Kinyume chake mshairi anascma kuwa mapenzi mazuri ni yale ya labia njema:
63 Ni wewe nakuwazja,
Tabiayo ni murua,
Tena u mwenye kujua,
Wa akili na busuri.
64 Huna ndeo huna hila,
Unenayo ni aula,
Ningakuwa ni muila,
Hunifanyii ghairi.
Katika “Ewe Mwana” tunaonyeshwa mapenzi baina ya baba na mwana; mapenzi ambayo yamejengwa juu ya malezi mema na mawaidha kuhusu umuhimu wa kushika dini (beti za 1-143), umuhimu wa kuwaheshimu wazazi (beti za 144-160), kuheshimu kazi (beti za 144-160), kuepuka uvivu, ulevi, uzembe na ufasiki, na kuwa na heshima kwa watu.
Tenzi za “Siasa Yetu” na “Ujamaa Vijijini” zinaonyesha aina tofauti ya mapenzi: mapenzi ya kijamii na kitaifa yaletwayo na siasa ya ujamaa na kujitegemea. Katika “Siasa Yetu” tumepewa nguzo kuu nane za mapenzi hayo:
1. Usawa wa binadamu
2. Heshima baina ya watu
3. Haki ya kushiriki katika uongozi
4. Uhuru wa kufuata dini yoyote aitakayo mtu
5. Haki ya kuwa na makazi mazuri
6. Haki ya kuwa na kazi na kupata ujira utokanao na jasho la mtu
7. Umuhimu wa kujitegemea
8. Umuhunu wa Serikali kumiliki njia zote kuu za uchumi pamoja na kulinda usawa katika mgawanyo wa mali.
Kwa jumla dhamira hii ya mapenzi imepanuliwa sana katika diwani hii kwa kupewa nyuso hizo tulizozitaja. Hata hivyo, msomaji wa “Ewe Mama Mpenzi” na wa “Kidani cha Huba” huweza kuchoshwa sana na marudiorudio mengi ya kauli zenye kumaanisha jambo moja; na hasa katika “Kidani cha Huba” ambamo kumejaa mapenzi ya “sili silali” pamoja na wingi wa sala ambazo sio za lazima.
Mila na Desturi za Jadi
Baadhi ya tenzi katika diwani hii zinaibusha masuala fulanifulani ambayo yaha umuhimu wa kisosholojia. Mathalani, katika utenzi wa kwanza wa “Ewe Mama Mpenzi,” beti za 72-77 zinaonyesha imani za jamii ya mwandishi kuhu.su “kinga” itokanayo na tunguri, pembe, hirizi na chanja. Baadaye katika beti za “4-181 mila na desluri za jadi kumhusu mtoto mara baada ya kuzaliwa zinajitokeza, na baada ya baba kufariki tunaiona mila imhusuyo mama kuhamia kwa mjomba. Kwa jumla beti hizi zinatuonyesha nguvu za utamaduni wa jadi japokuwa tunaweza kuuliza kama mila na desturi hizi zina nafasi gani katika maisha ya leo.
Utenzi wa mwisho wa “Ujamaa Vijijini” nao unatupa taswira ya mila, desturi na imani za mababu zetu wa zamani:
1. Jamaa zetu zamani
Waliishi na vijijini
Kwa ujamaa yakini
Na bila kujitambua.
Utenzi unatoa picha ya ujima wa awali uliowashirikisha wanajamii wote katika kufanya kazi. Ufanyaji kazi huu uliambatana na haki na usawa wa kugawana mapato:
13. Hitaji za hao watu,
Ziwile “chakula chetu,
Ardhi na ng’ombe wetu.”
‘Ansu’ hawakuiiua.
Katika maisha haya ya ujamaa wa asili tunaonyeshwa kuwa watu waliishi kwa kupendana na kushirikiana (ubeti wa 20); waligawana mali kiusawa (ubcti wa 29); hapakuwa na wizi (ubeti wa 32); na njia kuu za uzalishaji mali zilimilikiwa na umma wote kama ielezwavyo katika beti za 33 na 34. Pia, kaiika jamii hii ya awali kila mtu alifanya kazi, hakuna aliyeishi kwa jasho la mwingine.
Mshairi, hata hivyo, anaikosoa jamii hii ya awali kwa kumgandamiza mwanamke. Hili tutalichambua vizuri zaidi wakati wa kuichunguza dhamira ya nafasi ya mwanamke katika jamii.
Mshairi anatuonyesha, sawa na Mwalimu Nyerere alivyofanya katika andiko lake la Ujamaa Vijijini, kwamba maisha haya ya mababu zetu ndio msingi mkubwa wa siasa ya Tanzania ya ujamaa.
Umuhimu wa Elimu
Katika diwani hii mwandishi anatuonvesha aina mbili kuu za elimu:
1. Elimu itokanayo na shule na vitabu
2. Elimu ya kurithishwa.
Katika beti za 209-213 za “Kidani cha Huba,” mshairi anaonyesha jinsi vitabu vinavyoyapanua mawazo ya mtu, na piajinsi vilivyo “ngazi” ya kumpandisha daraja. Elimu hii imeonyeshwa kuwa ni silaha ya ukombozi wa mtu kikazi, kicheo na pia katika upande wa mapato. Kutokana na elimu aliyo nayo mshairi ya utaalamu wa kilimo, tunaonyeshwa pia faida zake kwa mkulima ambaye huutumia utaalamu huu na kuongeza ufanisi wa kazi yake.
EIimu ya kurithishwa tunaiona ikielelezwa katika sehemu mbalimbali zinazohusu desturi na mila za jadi ambako mtoto anafunzwa na wazazi wake juu ya maisha bora katika jamii.
Ukamilifu wa Mtu na Utu Wake
Mshairi anatupatia taswira ya ukamilifu wa mtu na utu wake kwa kutuorodheshea sifa azionazo kuwa ni muhimu katika maisha ya mtu.
Kwanza, katika tenzi zote Semghanga anasisitiza kuwa ukamilifu wa mtu hutokana na kufuata mafunzo ya dini pamoja na “amri” za Mungu. Wakati ambapo “ukamilifu” huu unakubalika kwa wale ambao bado wanaweka mategemeo na matumaini yao katika nguvu zilizoko nje ya uwezo na mazingira ya mwanadamu hapahapa duniani, kwa wale ambao maisha ya mtu yanaanza na kumalizikia duniani “ukamilifu” huo utaonekana kuwa si wa maana yoyote.
Katika utenzi wa “Kidani cha Huba” tunapewa taswira nyingine ya ukamilifu wa mtu. Zaidi ya kwamba heshima na unyenyekevu ni sehemu ya kukamitika huko, mwandishi pia anaonyesha ukamilifu wa kimaumbile. Mathalani, katika beti za 35 na 36 za “Ewe Mama Mpenzi” twaelezwa haya:
35. Awe mwana sio jitu,
Ambalo halina utu,
Nimzae mwana mtu,
Nisimzae kitishia.
36. Awe mtu wa kamiti,
Aleumbika muili,
Na kuchongoka kauli,
Mengine nipishilia.
Sifa za “kuumbika muili” tunazikuta pia katika utenzi wa “Kidani cha Huba” ambamo mshairi anajieleza kwa mpenzi wake kuhusu ukamilifu wa maungo yake:
171. Umbo langu kawaida,
Kwangu mie laakida,
Sikia hayo muwada,
Uyajue ukariri.
172. Kichwa si kikubwa sana,
Tena kimenilingana,
Wala hakikupitana,
Kimewekwa barabari.
173. Kina sikio za kingo,
Tamthili vile ungo,
Yamekaa kwa mpango,
Kwenye panja za kadiri.
Baada ya sifa zihusuzo viungo mbalimbali vya mwili, mshairi anasema kuwa kakamilika kwani:
186. Muili wote mzima,
Sina mie ukilema,
Ninaketi ninaima,
Tembeo natasawari.
187. Ni wa Manani mpango,
Kunipa hivyo viungo,
Viwe kwangu ni ukingo,
Kuniambaza fakiri.
Labda swali liwezalo kuzuka kuhusu hii dhana ya “kukamilika” kwa mtu kama aitoavyo mshairi ni: je, mazingira ya jamii ya kiuchumi, kisiasa na kitamaduni yana nafasi gani katika dhana hii? Hili ni swali muhimu kwani “kukamilika” kwa mtu na utu wake hutegemea wakati na mahali. Katika jamii ya kibepari kama ya Marekani, kwa mfano, mtu huonekana kakamilika kama ana malimbikizo ya mali nyingi za kibinafsi na pesa nyingi, wakati ambapo dhana ya “ukamilifu” wa mtu si hivyo katikajamii za kijamaa.
“Ukamilifu” mwingine wa mtu ni ule wa kiwango cha jamii ambao unamhitaji ayafuate maadili na amali mbalimbali za wanajamii wenzake. Huu ni wa kisiasa, nao tutaujadili vizuri katika dhamira ya mwisho.
Ndoa Katika Jamii
Kwa mawazo ya Semghanga, taasisi ya ndoa ni jambo la lazima na muhimu katika jamii. Mshairi anatuonyesha kuwa kuoa au kuolewa si jambo la hiari bali ni wajibu wa kila mtu afikiapo makamo yanayoruhusu.
Mshairi anaonyesha jinsi ambavyo kutokana na ndoa mapenzi yanapatikana, kwani katika ndoa kuna kusaidiana, kuheshimiana, kuzaa, pamoja na kulea watoto.
Umuhimu wa ndoa umeonyeshwa hasa katika utenzi wa “Kidani cha Huba’ ambamo beti za 74-99 zinapinga ukapera na upweke wa kutooa au kuolewa:
75. Kupwekeka si auta,
Kwasababisha madhila,
Hata mtu angekula,
Hana raha na sururi.
76. Kupwekeka nuksani,
Alisema Shaabani,
Hukutia aibuni,
Ukavunjiwa suturi.
79. Ujane kitu dhalili,
Kasema Akilimali,
Nayo ndoa nafttdhili,
Ashirafu na fahari.
Majina ya Shaaban (Robert) na Akilimali (Snowhite) yametajwa kwani katika ushairi wao washairi hawa walitetea sana ndoa na kupinga ujane.
Katika kuisifu ndoa mwandishi anatumia tamathali mbalimbali ambazo anatutaka tuzilinganishe na kuzilinganua na zile zinazoonyesha ubaya wa ujane. Kwa hiyo-basi upweke na ujane kauita “nuksani”, “una misiba”, “hauna heba”, “ni mkatili” na ni “kitu dhalili”; wakati ambapo tunaeiezwa yafuatayo kuhusu ndoa:
80. Ndoa pambo la unasi
Ni kidani cha nafsi
Ni kifao kwetu sisi
Kukikosa takiriri
81. Ndoa ni kitu cha hadhi
Hutoa shaka na udhi
Na tena hukuhifadhi
Penye tabu na usiri.
Twaambiwa pia kwamba ndoa ni fadhila ambayo imetoka kwa Mungu.
Wakati ambapo baadhi ya wasomaji watamuunga mkono Semghanga kuhusu ndoa katika jamii, huenda baadhi wasikubaliane naye. Inaelekea kuwa mshairi huyu anaamini kuwa ndoa hutatua matatizo yote baina ya wawili wanaooana. Lakini, hata hivyo ingembidi mshairi ajiulize maswali kuhusu talaka zinavyozidi kuongezeka leo hii si katika jamii za Ulaya tu bali pia katika jamii za Afrika.
Ndoa, kama taasisi zingine zote, ni zao la jamii. “Ukamilifu” na mabadiliko katika taasisi hii hutegemea mfumo mzima wa Jamii pamoja na mtazamo wa wanajamii kiutamaduni, kisiasa na kiuchumi. Leo hii yametokea mabadiliko mengi katika jamii kiasi ambacho taasisi hii si kama ilivyokuwa zamani. Imeingiliwa na nguvu mbalimbali za kijamii kama vile uchumi wa kifedha, kuzuka kwa miji ambayo inavutana na vijiji, na madaraka ya watawala kiasi kwamba wazazi hawana tena kauli juu ya nani amuoe au aolewe na mtoto wao – vjjana wanaweza kwenda kwa mkuu wa wilaya na kuoana bila idhini ya wazazi wao, na mengi mengineyo. Yote haya yameibadili taasisi hii kiasi ambacho kiuhalisi mawazo ya Semghanga yanaeleza ndoa inavyotakiwa iwe na siyo ilivyo. Kulikuwa na haja kwa mshairi kuzingatia athari za kimazingira juu ya taasisi hii ili atupatie taswira sahihi ya ndoa badala ya ile ya “mito ya asali na maziwa” aliyotupatia.
Nafasi ya Mwanamke Katika Jamii
Suala la nafasi ya mwanamke katika jamii limeshughulisha sana kalamu za waandishi wengi wa Kiswahili. Wengi wao wameiona nafasi hii kuwa ni duni ya kuonewa na kunyanyaswa.
Katika diwani hii, mshairi anaangalia masuala matatu kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii. Kwanza kamwangalia mwanamke kama mama. Hili tunaliona katika utenzi wa “Ewe Mama Mpenzi” ambamo jukumu la kubeba mtoto tumboni kwa miezi tisa likiambatana na uchovu na maumivu, halafu uchungu wa kujifungua mtoto huyo – yote haya yanaonyeshwa na mwandishi asemapo:
32. Miezi tisa wandani,
Kijusu bila amani,
Nakanyaga na mbavuni,
Wewe umevumilia.
33. Uchovu kila namuna,
Na umivu na sonona,
Ukivumilia nina,
Huku unaniombea.
Pili, kamwona mwanamke kama pambo au ua zuri – taswira ambayo aghalabu hujitokeza sana katika baadhi kubwa ya kazi za fasihi na hata nyimbo za bendi zetu – kama ionekanavyo katika ubeti wa 161 wa utenzi wa “Kidani cha Huba”
61. Awe kama ua safi,
La urembo na usafi,
Livutivu na nadhifi,
Na nukioja ambari.
Tatu, kama ionekanavyo katika utenzi wa mwisho, mshairi ameikosoa jamii ya zamani kwa kumdunisha mwanamke. Anasema:
56. Japo tulihusiana,
Pia tukaheshimiana,
Mwanamke tunakana,
Hakupata afudhaa.
57. Hakuthaminika mke,
Kwa hali na umbo lake,
Heshima kuwekwa kwake,
Ni ajabu na ajaa.
58. Walifanya kazi mama,
Kama watumwa na uma,
Huku wakishika tama,
Pasina kufurahia.
Beti hizi na zingine zinazoongelea suala la nafasi duni ya mwanamke katika jamii hii ya ujima wa awali, zinafanya kosa moja kubwa la kihistoria. Kosa hilo ni lile la kumpa mwanamke nafasi ambayo hakuwa nayo katika jamii ya awali kabisa ya mtu. Utengano anaouongeiea Semghanga baina ya mwanamume na mwanamke haukuwapo enzi za ujima wa awali. Tujuavyo, bistoria ya jamii ya watu ina hatua kuu tano: ujima wa awali, utumwa, umwinyi, ubepari, na ujamaa ambao hatima yake ni ukomunisti. Mfumo wa jamii ya kiujima haukuwa na matabaka ya watu. Mazingira ya wakati huo yaliyokuwa ya kiuhasama kwa mtu hayakuruhusu “anasa” za mgawanyiko wa watu kwa kufuata tabaka au jinsi ya kike au ya kiume. Yalihitaji watu wote washirikiane kwa pamoja kupambana na mazingira hayo. Ni baadaye sana, baada ya jamii kuanza kuwa na mifumo ya kitabaka na mali au milki za kibinafsi, ndipo suala la kugandamizwa na kuonewa kwa mwanamke linapojitokeza. Hili liliambatana na mambo ya mahari pamoja na kumwona mwanamke kuwa ni moja ya milki hizo za kibinafsi. Hali za namna hii hazikuwapo katika jamii ya ujima wa awali.
Siasa
Katika mkusanyo huu wa tenzi, tenzi mbili za mwisho zinashughulikia masuala ya kisiasa. Kama tulivyokwishaonyesha, “Siasa Yetu” ni utenzi mfupi unaoorodhesha nguzo muhimu za siasa ya Tanzania. Nguzo hizi ndicho kiini cha siasa ielezwayo katika “Ujamaa Vijijini.”
Kama alivyosema mwandishi katika Utangulizi, utenzi wa “Ujamaa Vijijini” ni “kama tafsiri ya kitabu cha Mwalimu Julius K. Nyerere UJAMAA VIJIJINI (uk. iii). Humu, baada ya k’uiangalia jamii ya zamani ilivyoishi kijamaa, mshairi, sawa na Nyerere, ameikosoa jamii ya leo hasa kuhusu maadui kama vile ujinga (ubeti wa 74), tamaa ya kujilimbikizia mali (beti 84-89), kupenda miji na kuchukia vijiji (ubeti wa 90), kukosekana kwa usawa baina ya watu (ubeti wa 106), na kukosekana uongozi bora (ubeti wa 202). Hayo yote mwandishi anahubiri kuwa hatuna budi kuyarekebisha ili kujenga jamii ya ujamaa kamili.
Njia anazozipendekeza mshairi kuwa zitatuletea maendeleo hazitofautiani na za Nyerere, nazo zinahusu mambo kama vile kuwa na usawa wa binadamu, kuunda vyama imara vya ushirika (beti za 109-117), kilimo bora cha shirika (ubeti wa 118), ujenzi wa ujamaa kwa kuzingatia tofauti za mazingira (beti za 141-144), kutumia mali asili ya jamii kwamanufaa yajamii nzima (ubeti 146), kutunza vizuri mahesabu ya mapato na matumizi (ubeti wa 163), uongozi bora (beti za 200-206), kuwa na demokrasia (beti za 235-237), Chama na serikali kuwa na mipango madhubuti ya kusimamia ujenzi wa jamii, pamoja na kujitegemea.
Labda ingefaa ieleweke tu kuwa mshairi hakukusudia kutathmini na kuhakiki siasa ya ujamaa vijijini, bali nia yake kubwa ilikuwa kunakili yale yaliyoelezwa katika kijitabu cha Nyerere. Kwa hiyo, kwa msomaji ambaye alikwishasoma kitabu hicho cha Mwalimu Nyerere, utenzi huu hautoi lolote jipya kimaudhui.
Utatuzi wa Migogoro
Mwandishi ameibusha migogoro ambayo pia amejaribu kuipendekezea masuluhisho. Hata hivyo, mengi ya masuluhisho hayo ni ya kimaadili na kimahubiri, na yamejikita katika udhanifu wa kidini. Kwa mfano, katika Utenzi wa “Ujamaa Vijijini,” baada ya kueleza njia sahihi ya ukombozi wa wanawake mshairi anatoa tu maonyo:
68. Si vyema hata kidogo,
Wake kuwafanya gogo,
La kukalia mzigo,
Huku wakivumilia.
69. Hilijambomnukusi,
Kudunisha mzima nusi,
Ya Tanzania unasi,
Si vyema hili sikia.
Baada ya mahubiri haya, mshairi anadhani amekwishaiteka mioyo ya wanaume wanaowadunisha wanawake, kwa hiyo anatoa utatuzi:
72. Tukitaka wendeleo,
Tuwape wake ufao,
Uhuru na haki zao,
Hapo tutaendelea.
Ni dhahiri kwamba ni kosa kufikiria kuwa kwa kuhubiri tu tutaibadili mioyo ya watu, nao wataziacha dosari zao. Hivi ni kukwepa uhalisi wa nguvu mbalimbali za kimazingira zilizozizaa dosari hizi. Huu ni udhaifu unaojitokeza karibu katika kila dhamira aliyoishughulikia mshairi wa Teuzi za Nafsi. Katika tenzi mbili za mwisho ndimo tu mlimo na utatuzi wa migogoro katika kiwango cha mfumo wa janui, ijapokuwa hapa pia hatuwezi kumsifu mshairi kwani haya si mawazo yake ila kayanakili tu.
Dhamira nyinginezo
Tulizozishughulikia ni baadhi tu ya dhamira muhimu zijitokezazo katika diwani hii. Ziko dhamira zingine ndogo ndogo ambazo msomaji huweza kuzichambua sambamba na hizo tulizoziangalia. Kwa mfano dhanura ya umuhimu wa kazi inaweza kuchambuliwa kipekee na kuonyeshwa jinsi mshairi alivyoiangalia. Kazi za aina zote – za sulubu na za akili zimeonyeshwa zinavyohitaji kuthaminiwa na kuheshimiwa kwani kazi ni msingi wa mapenzi na hata wa ndoa. Mshairi kaonyesha basi, kuwa kazi ni wajibu kwani ndiyo chanzo cha heshima kwa mtu.
Dhamira nyingine ambayo msomaji huweza kuichunguza kipekee ni ile ya nafasi ya dini au Mungu katika maisha ya mtu. Hii imejitokeza sana katika tenzi tatu za mwanzo ambazo zinatuonyesha jinsi mshairi anavyoamini kuwa mtu ni kiumbe dhaifu ambaye hawezi kuishi bila msaada na baraka za Mungu. Ndiyo sababu mshairi ameona heri azinakili Amri Kuu za Mungu pamoja na Amn Sita za Kanisa ili kukamilisha mahuhiri yake. Ni dhahin kuwa katika jamii ya leo ambapo dini inaelekea kupoteza nafasi muhimu iliyokuwa imeishikilia hapo awali, dhamira hii huweza kuzusha mjadala mkubwa wa kuuliza kama dini inayo nafasi yoyote katika maendeleo ya jamii iliyotawaliwa na elimu, sayansi na teknolojia za hali ya juu.
FANI KATIKA TEUZI ZA NAFSI
Kwa msomaji ambaye amekwishasoma kazi nyingi za washairi wengine wa Kiswahili kama vile za akina Muyaka bin Haji, Abdilatif Abdalla, Shaaban Robert. Mathias Mnyampala, Saadani Kandoro, Amri Abedi, Akilimali Snowhite, E. Kezilahabi, M.M. Mulokozi na K.K. Kahigi, miongoni mws wengi wengineo, itadhihirika wazi kuwa Francis HJ. Semghanga bado hajaiva kwa upande wa ufundi wa kisanaa.
Mara nyingi fani ya Teuzi za Nafsi imeonekana kuwa chapwa. Japokuwa mshalri kajitahidi kuzingatia kanuni za tenzi’ za kimapokeo za vina, ulinganifu wa mizani na mpangilib wa beti; kanuni na minyororo hii ya “sheria” imemfunga mno ikamletea matatizo. Kwa vile ilimbidi afuate kanuni za vina na mizani, mara nyingi kutokana na upungufu wa maneno mshairi amerudiarudia msamiati uleule katika beti mbalimbali hadi unamchosha msomaji.
Kurudiarudia huku si kuie tukukutapo katika ubeti wa 110 wa “Ewe Mama Mpenzi” au ule wa neno “mtwae” katika beti za 135-138, kwa mfano. Hapa inajulikana wazi kuwa mshairi anafanya hivyo kama mtindo wa kusisitiza. Mtindo huu wa kusisitiza umejitokeza hata katika beti za 176-181 za utenzi huo huo, beti za 164-167 za “Kidani cha Huba” zinazolirudia neno “japo”, na beti za 78-81 za “Ujamaa Vijijini” zenye kurudia bahari ya “shabaha itatimia.”
Kule kurudiwarudiwa kwa maneno mengi ya hapa na pale ambayo yangeweza kupatiwa mengine ya maana na mizani sawa na yenyewe ndiko kunakomchosha msomaji. Kwa mfano, katika beti za 19 na 20 za “Ewe Mama Mpenzi,” mshairi katumia maneno “na kwisha” ambayo angeweza kuyatumia katika ubeti mmoja tu na kutumia neno kama “baada,” katikaubeti mwingine. Pia, katika beti za 196 na 198 za utenzi wa “Ujamaa Vijijini” tunaona jinsi mshairi alivyokosa msamiati wa kuundia tamathali zake kwa hiyo akatumia ile ya “taji” kwa mambo mawili. Msomaji anaweza kugundua mifano mingine mizun zaidi ya udhaifu huu wa Semghanga.
Pia, mara nyingi mizani imezidi ile ya kanuni za kimapokeo na ni dhahiri kuwa mshairi hakuikusudia iwe hivyo. Mathalani, mstari wa mwisho wa ubeti wa 180 wa “Ewe Mwana,” na wa tatu wa ubeti wa 181 wa utenzi huo huo; mstan wa pili wa ubeti wa 196 wa “Ujamaa Vijijini,” na wa kwanza wa ubeti wa 219 wa utenzi huo huo – yote maonyesha kuwa katika kupungukiwa na msamiati, mshairi alijikuta katumia mizani 9 badala ya 8. Na hata wakati mwingine mshairi katumia mizani kumi katika baadhi ya mistari. Mfano ni mstan wa mwisho wa ubeti wa 252 wa utenzi wa “Ujamaa Vijijim.”
Kwa Jumla, mtu asomapo tenzi hizi, hasa tenzi tatu za kwanza, ataona kuwa mshairi amezirefusha tu bila sababu maalumu. Maudhui ya mawaidha na sala pamoja na dua mzomzo yangeweza kupunguzwa sana, labda kvva zaidi ya nusu, na bado yakaleta maana ile ile aliyoikusudia mwandishi
Ushairi husemwa umeiva kwa matumizi yake ya iugha ya mficho, y kipicha (taswira) na ishara. Lugha ya namna hii ndiyo aghalabu huutofautisha ushairi na tanzu zingine za fasihi kama vile riwaya, hadithi, au tamthilia. Hata hivyo lugha ya aina hii imetumika kwa nadra sana katika Teuzi za Nafsi. Mara nyingi lugha aliyoitumia mwandishi ni ya moja kwa moja ambayo haina ubunifu wa kisanaa ndani yake.
Sehemu tuwezazo kuzitaja kuwa rimetumia lugha kisanaa ni kama vile ubeti wa 26 wa utenzi wa “Ewe Mama Mpenzi” unaotoa taswira ya “zigo” kuwakilisha kazi kubwa ya kumshukuru mama; ubeti wa 126 wa utenzi huohuo utumiao tamathali ya sitiari ya kumwita mama “nyota ya hudumu;” mtindo wa lugha ya majigambo tuuonao katika beti za 244-249 za utenzi huohuo; tamathali zieiezazo maana ya maisha katika beti za 257 na 258 za utenzi huohuo; tamathaii ya kumwita mkosa dini kuwa ni “safura” katika ubeti wa 130 wa “Ewe Mwana;” na ile ya kuuita usawa kuwa ni “taji” ya watu.
Mwisho wa utenzi wa ”Ewe Mwana” ni wa ghafla mno, na kwa baadhi ya wasomaji huu ni udhaifu kwani yaelekea mshairi aliukatisha tu utenzi huu baada ya yeye mwenyewe kuchoshwa nao.
Japokuwa katika utenzi mfupi wa “Siasa Yetu” mshairi kaonyesha mtindo tofauti na ule wa idadi ya vina na hata wa mizani katika mistari ya beti, na japokuwa huenda mshairi akapata sifa za kuwa miongoni mwa “‘wanamapinduzi” wa mwanzo walioutoa utenzi wa Kiswahili kutoka katika silisila za maadili, dini na historia tu na kuungiza katika masula ya mapenzi na mahaba, uzito wa sifa hizo hupungua hasa tuzingatiapo udhaifu wa ufundi wa kisanaa na hata wa kimaudhui kama tulivyouonyesha; udhaitu uonyeshao uchanga wa mshairi huyu katika bahari kubwa ya ushairi wa Kiswahili.
Maswali
1. Ichambue dhana ya “mapenzi halisi” kama ilivyojitokeza katika diwani ya Teuzi za Nafsi.
2. Jadili jinsi mwandishi alivyoiibusha na kuishughulikia dhamira ya mila na desturi za jadi katika jamii katika Teuv za Nafsi. Je, unadhani dhamira hii ina nafasi gani katika jamii ya Tanzania ya leo?
3. Chagua dhamira mbili kati ya zifuatazo ujadili zilivyojitokeza katika diwani ya Teuzi za Nafsi:
1. Umuhimu wa elimu
2. Ukombozi wa mwanamke
3. Nafasi ya dini katika maisha ya mtu
4. Siasa.
4. “Kazi ya fasihi haina budi iwe na uwiano mzuri baina ya maudhui yake na fani”. Ijadili kauli hii ukiihusisha na diwani ya Teuzi za Nafsi.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)