MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

KISASILI CHA JONGOO NA NYOKA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
KISASILI CHA JONGOO NA NYOKA
#1
Tokiani!
Namchai!
Hapo kale mzee Jongoo na NYoka walikuwa marafiki wa kuaminiana sana. Siku moja Jongoo akamwambia Nyoka, “Rafiki yangu, leo kuna ngoma. Twende nasi tukaone jinsi wenzetu wanavyocheza.”
Nyoka akamjibu, “Ningependa sana kwenda huko. Lakini ujuavyo sina macho. Nitaonaje huo mchezo?” Jongoo akasema, “NItakuazimisha macho yangu, nawe utaniazimisha miguu yako kama dhamana.” Wakakubaliana. Basi wakabadilishana viungo: Jongoo alimpa Nyoka macho yake, naye Nyoka akampa Jongoo miguu yake mingi.
wakaenda ngomani. Baada ya ngoma kwisha, Jongoo alimtaka Nyoka macho yake. Lakini Nyoka akajibu, “La, rafiki yangu. Kumbe wenzangu mnafaidi sana kwa macho yenu. Leo nimeona ngoma na moyo wangu umeburudika sana. Kwa hiyo hupati macho haya tena. Jongoo akamjibu, “Lakini werevu siyo kupata!” Kwa hasira Jongoo akaondoka na miguu yake yote huku anapapasa njia kurudi kwake.
Ndicho kisa cha Nyoka kukosa miguu na Jongoo kuwa na miguu mingi bila macho. Ndicho kisa pia cha Jongoo na Nyoka kamwe hawaamkiani hata kama wangekutana njiani.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)