Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
7 JULAI SIKU YA KISWAHILI DUNIANI
#1
Kwa  taarifa zaidi ni kwamba leo,  pendekezo na azimio lililowasilishwa na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania  ya kuwa na Siku ya Kiswahili Duniani itakayosherehekewa kila  tarehe 7 Julai ya kila mwaka, imepitiswa  na Kamisheni ya Masuala ya Utawala, Fedha na Mahusiano ya Kimataifa (The APX Commission). Hivyo, tunasubiri  ipitishwe katika Plenary ya Mkutano Mkuu mwezi huu mwishoni ambayo itatoa  Azimio.

Habari za kutia moyo. Leo UNESCO imepitisha tarehe 7 Julai kuwa ni  siku ya Kiswahili Duniani.

Ni mwanzo mzuri kwa Kiswahili Kimataifa. Baadaye tunaweza kupata wakalimani kwenye vikao vya kimataifa nasi kuwasilisha masuala Kwa Kiswahili!!!
Mwl Maeda
Reply
#2
Safi sana. Kiswahili kinazidi kuwa na mashiko. Sisi ni nani hata tusikitumie kufundishia?
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)