Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
MAKIWA MAMA - KISWAHILI!
#1
MAKIWA MAMA - KISWAHILI!
Mama yetu - Kiswahili anayetulea kwa hali na mali amepata pigo kwa kufa mmoja wa watoto wake - Profesa Pete Mhunzi.
Nilifahamiana na Profesa Pete Mhunzi, aliyelibadili kuwa la Kiswahili jina Peter Smith zaidi ya miaka 30 pale alipozuru Tanzania na kutembelea ofisi ya Waswahili - Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania (UKUTA), eneo la Anartoglo, Mnazimmoja, Dar es Salaam mwishoni mwa miaka ya 80.
Hiyo ilikuwa ni mara ya pili kumuona Mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyempenda Mama Kiswahili na kumtendea haki baada ya kukutana na John Mtembezi (Bwana Punda).
Profesa Pete Mhuzi alipenda sana kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Kiswahili na Taaluma zake na tulikuwa  na vikao maalum, tukiwa na gwiji la Kiswahili Marehemu Mzee Hamis Akida (Allaah Amrehemu), pale nyumbani kwa mwanadada (bila shaka sasa ni Bibi mwenye wajukuu) Irene (aliyekuwa mfanyakazi wa Kampuni ya TPH - Tanzania Publishing House, eneo la Kota za Misheni, Kariakoo, Dar es Salaam.
Anapofika Profesa Pete Mhuzi huwa ni hekaheka nguo kuchanika kwa waswahili waliokuwa na raghba ya kufanikisha ziara yake ya utalii wa Kiswahili.
Hapa namkumbuka Kaka Mswahili Mohamed Mwinyi (Bwana Jasho), Marehemu Ramadhani Stumai (Allaah Amrehemu), Marehemu Sihiyana Swalehe Mandevu (Mtenda Mema) na mradi wake wa alfabeti za Kiswahili zinazowakilisha vinavyopatikana Uswahilini kama upawa, mwiko, chungu na kadhalika.
Huchoki unapomsikiliza Mswahili Pete Mhunzi na juhudi zake za kumuenzi Mama Kiswahili.
Kuondoka kwake ni pigo kubwa kwa Mama yetu na ukoo mzima wa Mama Kiswahili.
Mama Kiswahili ana huzuni kubwa anapokumbuka maumivu ya tumbo la udele linalouma mno.
Makiwa Mama Kiswahili!
Makiwa watoto wa Mama Kiswahili!
Tunamuomba Mola wetu Ampokee.
Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, jina la  Bwana lihimidiwe.
Na:
Khamis Mataka
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)