MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
OSW 123/133: FASIHI YA KISWAHILI NADHARIA NA UHAKIKI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
OSW 123/133: FASIHI YA KISWAHILI NADHARIA NA UHAKIKI
#1
SWALI: Fasihi ya jamii yako ndogo ina nafasi gani katika kuimarisha na kuendeleza fasihi ya kitanzania kwa lugha ya Kiswahili?

JIBU
Fasihi ya
kitanzania  kwa lugha ya Kiswahili ni
matokeo ya mchango wa fasihi za jamii ndogondogo zilizokusanywa pamoja kwa
kutumia lugha ya Kiswahili kama kielelezo cha utamaduni wa jamii ya watanzania
kwa ujumla.
Mchango wa fasihi ya
jamii ndogo unajidhihirisha katika fasihi ya kitanzania kwa lugha ya Kiswahili kama
ifuatavyo:
Ngoma, ngoma ni moja ya
vipengele vya fasihi kwa Kiswahili ambavyo hutoka katika fasihi ya jamii
ndogondogo kwa mfano ngoma ya jamii ya wamakonde (sindimba), ngoma ya Wazaramo
(mdundiko), zimechangia kuwepo kwa utanzu wa ngoma katika fasihi ya kitanzania
iliyoandaliwa kwa lugha ya Kiswahili.
Matambiko, ni fasihi ya
jamii ndogo ndogo na kila jamii huwa na kaida zake na mahali maalumu pa
kutendea. Kipengele hiki kinapochambuliwa na kujadiliwa katika fasihi kwa lugha
ya Kiswahili hakiondolewi asili yake wala hakifanywi kuwa kipengele cha jumla
kwa jamii zote.
Hadithi, masimulizi ya
kihadithi katika fasihi kwa Kiswahili hutoka kwenye masimulizi ya jamii ndogo
ndogo zilizopitia matukio mbalimbali yaliyoacha kumbukumbu zenye masimulizi
hayo kwa mfano jamii ya Wahehe inatoa masimulizi ya Mkwawa, jamii ya Wasukuma
inatupa masimulizi ya mtu ajulikanaye kama Ng’wanamalundi lakini pia jamii ya
Wangozi inatupa masimulizi ya Fumo Liyongo. Kwa hiyo masimulizi ya kihadithi
katika fasihi kwa lugha ya Kiswahili ni mchango toka fasihi za jamii ndogo.
Elimu ya jadi,
itolewayo kwa vijana wa kike kama unyago na wa kiume kupitia jando ni mchango
wa fasihi za jamii zenye kutenda mambo hayo, hivyo fasihi ya kitanzania kwa
lugha ya Kiswahili inaposhughulikiwa katika kuchambua masuala ya jando na
unyago ni kwa sababu masuala hayo yapo ndani ya jamii zinazounganishwa kupitia
fasihi kwa lugha ya Kiswahili
Umoja na mshikamano,
katika jamii huimarika na matabaka huondoka pale jamii inaposhirikiana katika
matukio ya furaha au huzuni kwa mfano katika sherehe mbalimbali zenye kukusanya
watu wa jamii tofauti si ajabu kuchezwa ngoma yenye asili ya jamii mojawapo
kati ya jamii zilizokusanyika, mathalani ngoma ya jamii ya Kichaga huweza
kuchezwa hata na watu wasio Wachaga na kufanya ngoma hiyo kuwa ya wote.
Mwingiliano wa kijamii,
kwamba fasihi kwa lugha ya Kiswahili inasababisha mila na desturi za jamii
ndogondogo kuonekana kama kitu kimoja na kuchochea mwingiliano wa jamii hizo
hata kufikia hatua ya kuoana watu wa jamii tofauti kwa kuzingatia utaratibu wa
mila na desturi zilizorekebishwa hata kupunguza athari zilizokuwepo mwanzo.
 
Maendeleo na kuimarika
kwa fasihi ya kitanzania kwa lugha ya Kiswahili ni matokeo ya mchango mkubwa
toka fasihi za jamii ndogondogo zilizojitoa katika upekee na kuleta ujumla wa
kifasihi.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)