MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
ZOEZI LA UTUNGAJI : MASWALI NA MAJIBU

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ZOEZI LA UTUNGAJI : MASWALI NA MAJIBU
#1
ZOEZI LA UTUNGAJI : MASWALI NA MAJIBU
Zoezi la kuandika: Utungaji
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, watunge kifungu cha habari ambacho kinadhihirisha matumizi ya nahau zisizopungua tano.
Mfano wa kifungu chenye kutumia nahau zisizopungua tano
Kulikuwa familia moja ya Baba , bibi na watoto. Wanaishi kijiji Maendeleo. Familia hii ina matatizo ya makao, kupata chakula si kitu rahisi kwao, watoto hupekua….. Kila wakati baba akipata pesa kazi yake ni kuponda raha na kuvaa miwani. Haleti chochote nyumbani.
Kwa ushirikiano wa watoto na mama wao walijijengea nyumba ya mbavu za mbwa na mahali pa kwenda kujisaidia. Baadaye, baba naye alitoa mchango wake na kuepukana na tabia zote mbaya alizokuwa nazo. Walianza kuwa na maendeleo na kuishi kwa amani.
Watoto wao walikomaa na kufika kwa umri wa kujipatia jiko. Msichana wake alipata kijana ambaye alikuwa na nia ya kumuoa. Walikuwa pete na kidole.
Watoto wote walibahatika katika familia zao na baba na mama nao wanashukuru Mungu aliyewasidia. Hivi sasa ni famalia tajiri. 106
MAJIBU KUHUSU TATHMINI YA MADA YA PILI
Sanaa ni ufundi unaowakilisha mawazo na hisia alizo nazo binadamu kwa njia ya ubunifu.
Kuna aina mbalimbali za sanaa kama vile uchoraji, uchongaji, ususi, uhunzi, usonara, fasihi, uashi, sinema, uimbaji, ufinyanzi, ufumaji, upishi, ushonaji, udarizi n.k.
Sanaa ina nafasi kubwa kwa ujenzi wa taifa, kwani hupunguza ukosefu wa ajira na huwezesha jamii kutosheleza baadhi ya mahitaji yao ya kila siku kupita kazi mbalimbali zinazofanywa na wasanii. Wasanii nao hujiendeleza kiuchumi kutokana na pato linalotoka kwenye kazi zao .
Tanzu za fasihi simulizi ni:
Hadithi
Methali
Nahau
Vitendawili
Nyimbo na mashairi
Fasihi ina umuhimu mkubwa katika jamii. Katika jamii fasihi inaweza:
Kuelimisha jamii
Kuburudisha jamii,
Kuhifadhi na kurithisha amali za jamii,
Kudumisha na kuendeleza lugha
Kuunganisha jamii,
Kukuza uwezo wa kufikiri,
Kumtajirisha msanii
Fasihi inaweza kuwa chanzo cha madhara katika jamii inapotumiwa vibaya kupitia nyimbo na methali zinazochochea ubaguzi na uadui baina ya wanajamii. Mfano ni jinsi nyimbo zilivyochochea uhasama baina ya wananchi na kuishia kwenye mauwaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mnamo mwaka wa 1994.
  1. Soga
Huu ndio mwisho wa hadithi au Hadithi inakomea hapa.
“Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo” Methali hii inamaanisha kwamba jinsi unavyomlea mtoto wako ndivyo atakavyokua. Yaani ukimpa malezi mazuri naye atakuwa mzuri, yakiwa mabaya naye atakuwa mbaya vile vile.
Methali hiyo ni “Ahadi ni deni”
  1. kufukuzwa kazini
  2. Kudanganya mtu na maneno matamu
Majibu
hili
yule
hayo
mawili
manane
matatu
langu
hayo
langu
lipi
Majibu
Sisi tuna malengo ya kupambana na majangwa.
Vijana warefu walibeba makasha makubwa.
Mashirika ya reli yaliagiza magarimoshi makubwa.
Madaftari yanapashwa kuhifadhiwa vizuri.
Mambo haya yanawafurahisha wengi
Mawe yangu yana thamani kubwa
Mapapai yapi yameivya ?
Meno yako yameng’oka?
Majaribio ya leo yamesahihishwa.
Majanga makubwa yamesababisha maafa.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)