Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
FAHAMU MAJINA YA SEHEMU ZA MIJI MAARUFU TANZANIA NA MAANA ZAKE
#1
FAHAMU MAJINA YA SEHEMU ZA MIJI MAARUFU TANZANIA NA MAANA ZAKE

1. KOLOMIJE.
Inasemekana mahali hapo alifika Mzungu aliyeitwa James, hivyo huyu Mzungu akataka watu wamwite "J" badala ya kutamka jina lote. Hivyo akawaambia CALL ME J, wabantu wakatamka KOLOMIJE na kutengeneza jina la eneo hilo.

2. KARIAKOO
Hii ilitokana na neno Carrier_crop ambalo lilikuwa ni jina la wabeba mizigo wa eneo hilo la sokoni, lakini Waswahili walishindwa kulitamka jina hilo hivyo wakasababisha kutokea kwa jina la Kariakoo.

3. MSASANI.
Hili jina lililotokana na Bwana mmoja aliyeitwa Musa Hassan ambaye alikuwa ni Mnyapara aliyekuwa akisimamia mashamba ya katani ambaye asili yake ni Mtwara, wamakonde wengi wakaamua kuja kumuomba kazi na kwa kwa kuwa walikuwa hawajui anapoishi waliuliza kwa Mucha Hachani, na wakaendelea kuunga unga mpaka kusababisha kutokea kwa jina la Msasani.

4. KAWE.
Hili lilitokana na neno Cow_Way, barabara maarufu kwa kuswagwa ng'ombe kufikishwa hapo Tangaynyika Packers kwa machinjo.

5. KIGOGO
Ilitokana na kigogo halisi kabisa cha kuvuka pale kigogo mwisho kila jumamosi walikuwa wanakusanyika kukiweka "jamani leo siku ya kigogo" (leo pamejengwa daraja).

6. TABATA
Palikuwa na Muarabu aliyekuwa ananunua korosho kwa mali kauli na kuwaahidi wachuuzi waje siku fulani watalipwa kwa kuwaambia "hapana tabu tabata (utapata pesa yako) akabatizwa jina la Mwarabau Tabata, na mwishowe mahali hapo napo pakaanza kuitwa Tabata.

7. ILALA
Jina hili linatokana na makaburi ya pale Karume ambako hakukuwa na mengine hivyo kila alasiri watu walikuwa wakienda kuzika na wimbo wa Haila Illallah! na mwishowe mahala hapo pakaanza kuitwa Ilala.

8. UBUNGO
Majina yafuatayo: bungoni, mikoroshini, na mabibo yote haya yalitokana na uwepo wa miti mingi ya matunda hayo kupatikana maeneo hayo.

9. KIBORILONI
Kiboriloni ni neno lililotokana na maneno mawili KIBO na ALONE. Hii ilikuwa sehemu ambapo wazungu walisimama na kuona kilele cha Kibo pekee bila kukiona kilele cha Mawenzi, Kibo na Mawenzi ni vilele vya Mt. Kilimanjaro.

10. KIBOSHO
Lilitokana na maneno KIBO na SHOW, hii ni sehemu ambapo Kibo kilionekana vizuri zaidi.

11. MWANANYAMALA
Hapo kitambo mitaa ya Mwananyamala kulikuwa na mapori na Simba, kwa hiyo kina mama wa kizaramo walipokuwa wakifika mitaa hiyo wakawa wanawaambia watoto wao  wanapolia usiku"Mwana Nyamala" maana yake "Mtoto Nyamaza" ili wasisikiwe na Simba.

12. TABORA
Kambi ya Wafanyabiasha. Walikuwa wakipita na bidhaa zao wanakuta viazi vitamu vilivyopikwa na kukatwakatwa vipande na kuanikwa. Hapo huliwa makavu (Chewing gum) au kupikwa na kuliwa. Haya huitwa Matobolwa au Matovola. Hivyo wakapaita kambi ya Matobolwa au Matovolwa. Hii ilikuwa kugeuka na kuwa Tabora.

13. SUMBAWANGA
Wenyeji wa maeneo hayo walikerwa na vitendo vya ushirikina (tofauti na mtazamo wa watu wengi kwamba wenyeji wanaendekeza ushirikina). Kutokana na kero hiyo waliamua kuwapiga mkwara watu wanaoingia katika mji huo kwamba kama unataka kuja huku, basi Tupa Uchawi i.e Sumba (Tupa) Wanga (Uchawi), ukitupa na kuuacha uchawi wako huko uliko unaruhusiwa kuja hapo Sumbawanga.

14. MTONI KWA AZIZ ALI.
Mtoni kwa Aziz Ali pamepata jina kutokana na mkazi mmoja aliyekuwa maarufu (alwatani) sana marehemu Aziz Ali. Mzee huyu alifariki miaka kadhaa iliyopita.

15. KWA BIBI NYAU.
Kwa Bibi Nyau kulikuwa na ajuza mmoja alikuwa anafuga paka wengi sana.

16. NEWALA.
Waingereza walipofika Mtwara walikuta kisima kilichojengwa na wajerumani ambacho kilikuwa cha kizamani kwa wakati Huo , Hivyo walijenga kisima kipya na kukiita NEW WELL, watanganyika wakatamka NEWALA, hatimaye likawa jina la ile sehemu.

17. CHEKERENI[MOSHI].
Hili ni eneo ambapo barabara inakatiza kwenye reli.Sasa wazungu waliweka alama ya bararani ya tahadhari kabla ya kuvuka reli CHECK THE LINE, watu wakatamka CHEKERENI na kuliita hivyo lile eneo hadi leo.

18 . MAKONGOLOSI
Inatokana na neno la kiingereza MAKING LOSS - Zamani waingereza walipata hasara kutokana na shuguli za uchimbaji wa madini eneo la Makongolosi wilaya ya Chunya mbeya ndipo eneo hilo kubatizwa jina hilo .

19 . GODIMA
Ni kijiji kimoja wapo kilichopo wilaya ya Chunya ambacho jina lake lilitokana na kiingereza ambalo ni GOLD MINE ( Mgodi wa Dhababu

20. MATOMBO
Matombo kwa kiluguru ni matiti. Eneo hilo kuna jiwe lenye mwonekano wa mwanamke mwenye matiti. Ndicho chanzo cha kuitwa matombo.

21. KIPONZERO
Kijiji kilichopo barabara ya Iringa kwenda mbeya ndani ya mkoa wa Iringa.Wakati wa ujenzi wa barabara wapimaji walitumia sana neno KEEP ON ZERO kitu kilichofanya wenyeji wafikiri wale wazungu wanapaita pale keep on zero ambayo wao waliitamka kiponzero.

22.MKONGOTEMA
Kijiji kipo baraba ya Njombe to songea. MKONGO ni mti ,Tema walikuwa na maana ya litema/ matema mashamba ya mazao kama ulezi yanayokuwa milimani. Sasa kutokana na watu kukata miti kwaajili ya matema basi ikawa ukitaka kumwelekeza mtu aliko. Unamweleza " kwavudumula mikongo ya matema kola" kingoni. Basi likaja neno MKONGOTEMA.

23. MBAMBA BAY
Kuna mlima upo hapo unaitwa mlima Mbamba. Kwa kilugha mbamba ni radi. Mlima ule ulikuwa na kawaida ya kupiga sana radi nyakati za masika. Hivyo ukaitwa mlima mbamba. Na kutokana eneo hilo lina ghuba katika ziwa nyasa ( bay) ndipo lilipozaliwa jina Ghuba ya Mbamba yaani MBAMBA BAY.

24. KILOMENI ilitokana na maaguzo wakati wa mapigani mzungu aliagiza askari wakifika pale waue wanaume wote yaani KILL ALL MEN wabongo wakashindwa kutamka ndipo wakaishia KILOMENI

25 GONGO LA MBOTO hili lilitokana na mzee mmoja aliyekuwabakiitwa mzee Mboto alikuwa na kirungu kile chenye kichwa. Alipoenda kuwinda maeneo yale ambayo wakati huo yalikuwa ni porini hakuruni. Wakamtafuta sana lakini hawakumpata mpaka leo isipokuwa waliliona rungo au gongo lake. Ndipo walio liona wakati wa kutafuta wakasema jamanj GONGO LA MBOTO hili hapa. Kuanzia siku hiyo eneo hilo limaitwa GONGO LA MBOTO

26 MIKOCHENI lilitokana na duka la kubadilisha pesa MICRO CHANGE

27 KILIMANJARO limetokana na wazungu kushindwa kutamka KILIMA CHA RUWA

27 MBEZI INN MAGARI SABA ilitokea ajali iliyohusisha magari saba kwa wakati mmoja hapo

28 KIBAHA PICHA YA NDEGE jamaa alitengeneza sanam ya ndege na kuiweka hapo paka pta jina.

29. Sehemu nyungine zinabebe majina ya watu kutokana kwamba wao ndiyo walikuwa maarufu wakati huo au walikuwa wa kwanzq kuhamia maeneo hayo. Mfano Mbezi, Mbezi kwa Yusufu, Kwa Msuguli, kwa Ally Maua, Kwa Tumbo alikuwa na tumbo kubwa, kwa Semangube, kwa Shemsa, Kwa bastola, kwa mfuga mbwa, tegeta kwa ndevu nk

Na wewe ongezea mengine
Mwl Maeda
Reply


Messages In This Thread
FAHAMU MAJINA YA SEHEMU ZA MIJI MAARUFU TANZANIA NA MAANA ZAKE - by MwlMaeda - 01-22-2022, 07:46 PM

Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)