MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SIMULIZI : MAPIGO YA MOYO *SEHEMU YA 03* - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SIMULIZI : MAPIGO YA MOYO *SEHEMU YA 03* - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48)
+---- Thread: SIMULIZI : MAPIGO YA MOYO *SEHEMU YA 03* (/showthread.php?tid=953)

SIMULIZI : MAPIGO YA MOYO *SEHEMU YA 03* - MwlMaeda - 08-20-2021

SIMULIZI : MAPIGO YA MOYO       *SEHEMU YA 03*
 
Maelfu ya watu walikaa kimya huku wakishangaa kile kilichokua kinatokea kwa wakati ule, “Namuomba bwana harusi amvalishe pete bibi harusi ” ,Mchungaji aliongea huku akiwa hajui kati ya mtoto wa raisi bwana Jacob na mimi, ni nani kati yetu alikuwa anahusika na ndoa ile kutokana na muonekano wetu kufanana kwa kila kitu ……huku pia kukiwa na tetesi za Jacob kutohusika na ndoa hiyo.
…………………………………
“Sniper” (mlenga shabaha) akiwa anajiweka tayali kwa kunifyatulia risasi aliendelea kujiweka tayali huku akisubilia kushuhudia kati yangu na Jacob ni nani alikuwa muhusika wa ndoa ile. “Leo ni mwisho wako mpuuzi wewe, nimekuonya sana hutaki kunisikia “, baba yake Rose alizungumza kwa sauti ya chini sana huku akiangalia juu kabisa ya uwanja uelekeo ambapo mlenga shabaha alipo kwa ajili ya kutekeleza mauaji yangu.
Mzee Jastini aliamua kuandaa mtu kwa ajili ya kuniua kutokana na tetesi alizozisikia kuwa, kuna mipango ya siri iliandaliwa ili mimi nifanikiwe kumuoa Rose.”Sitaki aibu, Kijana huyu fukara hawezi kumuoa mwanangu ……nitaiweka wapi sura yangu?? ……mungu wangu kashakua kilema, na ulema huo ndo kabisaaa nitaaibika zaidi siwezi mruhusu amuoe binti yangu labda niwe nimekufa ” mzee Jastini aliongea huku akiwa amepaniki na kutoka sehemu waliyokuwa wameketi wageni rasmi, baada ya kushuhudia nikiingia uwanjani huku Jacob akiskuma kibeskeli changu. “Nimeamini hapa kuna kitu siyo bure, ngoja nimkomeshe kijana huyu kabla mambo hayajaharibika “,mzee Jastini alielekea faraghani na kumpigia moja ya vijana wake aliowatumia katika kutekeleza matukio mbalimbali ya mauaji ili ajaribu kuniua kwa mara nyingine tena.
…………………………………
“Paaaaaah, paaah ……paaah “mlio wa risasi tatu zilizopigwa mfululizo ulisikika na kujikuta nikiishiwa nguvu na kudondoka chini mara nilipotoa pete mfukoni na kumvalisha Rose katika kidole chake. “Jacob my son don’t die ” ,( mwanangu Jacob usife)  niliiskia sauti ya mheshimiwa raisi kwa mbali sana akimsihi mwanae asife japo alikuwa tayali ameshachelewa, Jacob aliamua kunikinga na risasi baada ya kushuhudia nikipigwa  risasi ya kwanza tumboni.”Aaaaah ……”Jacob alipiga kelele na kisha kupoteza maisha baada ya kupigwa risasi mbili kifuani huku akiwa amenikumbatia.
“Robert usife Robert, Jacob rudi Jacob ……fumbua macho angalau uniage……hukustahili kifo hiki Jacob ,bora ningekufa mimi wewe huna hatia. Rudi Jacob rudi ……” sauti ya huzuni ilisikika kutoka kwa Rose, huku akiwa ameshikilia miili ya watu wawili katika mikono yake.
…………………………………
Askari waliendelea kuzunguka kila kona ili kumnasa muhusika wa mauaji ya Robert na kunijeruhi vibaya,huku wakishirikiana na wananchi walioshuhudia tukio lile. “Unatakiwa uondoke Dar es salaam haraka iwezekanavyo  kabla hujakamatwa, kukamatwa kwako kutaniweka sana matatizoni “,bwana Jastini alimsihi kijana wake aliyehusika na shambulio lile, wakiwa ndani ya gari kuelekea katika maficho yao ya siri yaliyoko nje ya mji.
Baada ya jambazi yule kutekeleza shambulio lile, aliiacha bunduki ile aina ya Semi_automatic machine gun (smg) mahali pale, na kisha kujichanganya katikati ya watu waliokuwa wakikimbia bila utaratibu ili kuokoa maisha yao. Jambazi hili lilitoroka kirahisi na kushindwa kukamatwa na askari na wala kujurikana hata sura yake.
“Aliyehusika na haya yote lazma atalipia, “raisi aliongea huku akinitazama nikipatiwa matibabu na kutolewa risasi, machoni alionekana kuwa na huzuni sana huku hasira ikiipamba sura yake kutokana na mwanae kupoteza maisha na muuaji kushindwa kufahamika.