MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: KUKU USIMCHUNGUZE - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI: KUKU USIMCHUNGUZE - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI: KUKU USIMCHUNGUZE (/showthread.php?tid=849)

SHAIRI: KUKU USIMCHUNGUZE - MwlMaeda - 08-15-2021

Si nia niwaumize,kwa hili langu suala
Kuku usimchunguze,kama wataka kumla
Mengi usijiulize,zikajakukifu hila
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla

Utengewapo minofu,na michuzi dikodiko
Zifute dhana potofu,kukumbuka atokako
Ukayawaza machafu,kwa yake michakarimo
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla

Ni ada kiumbe huyu,kudonoa kuchakua
Kuku sio mbayuwayu,yakupasa kutambua
Mkuyu uwe mbuyu,hapo utajisumbua
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla

Shukuru wako Manani,riziki kukupatia
Mkono kwenda kinywani,hii dunia ni njia
Japo atoke jaani,epuka kufuatilia
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla

Nyongeza haiwi fungu,hapa mwisho nafikia
Kama hutaki machungu,kaa hili zingatia
Kuku ukimchunguza,abadani hutomla

Abdul Ndembo
Mburahati Sek