SHAIRI: MPENZI NIMEKUOTA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: MPENZI NIMEKUOTA (/showthread.php?tid=848) |
SHAIRI: MPENZI NIMEKUOTA - MwlMaeda - 08-15-2021 MPENZI NIMEKUOTA tulikuwa ufukweni, mimi na wewe wawili, Tulivaa dizaini, yale mavazi ya mbali, Mpenzi ulishaini, uzuri kila mahali. Mpenzi nimekuota. Wavyele nawaamini, kweli mapenzi ajali, Basi tulikaa chini, pale palipo kivuli, Nikalala kifuani, kifua chako rijali, Mpenzi nimekuota. Ukaniuliza swali, ukitazama usoni, Hivi wanipenda kweli, hutanitenda mbelini? Hapa nakujibu swali, sikutendi asilani, Mpenzi nimekuota. Nikwambie wangu honey, Mimi nakupenda kweli, Naomba uniamini, ujue sili silali, Ninaomba ubaini, bado tungali awali, Nimekuota mpenzi. Ninakuomba rijali, hebu nitie moyoni, Penzi ulipe sahali, kupenda nijiamini, Mambo yawe wastani, Filieda nikubali, Nimekuota mpenzi. Hivi nimelala chali, nakuwaza mjuani, Hebu unipe sahali, inipate afueni, Ninaomba unijali, nipate yako jubuni, Nimekuota mpenzi Nimefika ukingoni, nimekupenda rijali, Ujue nakutamani, tupendane si wawili, Hivi raha yako nini, nilivyo sili silali, Nimekuota mpenzi. Mtunzi Filieda Sanga Mam B Mabibo Dsm 0753738704 |