SHAIRI: HACHUMI ASIYEPANDA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: HACHUMI ASIYEPANDA (/showthread.php?tid=823) |
SHAIRI: HACHUMI ASIYEPANDA - MwlMaeda - 08-11-2021 HACHUMI ASIYEPANDA Uwe jemedari mwema, na roho isiyodoa, Unapotaka kuchuma, kupanda ni shurutia, Sawa bwana umelima, hukupanda ni udhia, Hachumi asiyepanda, ndiyo mambo ya dunia. Kwanza iweze kumea, mbegu chini ikazama, Hapo huanza kukua, na uwe mti mzima, Mizizi ikatokea, na shina likiwa wima, Hachumi asiyepanda, ndiyo mambo ya dunia. Matawi yakija nyuma, huo mti kupambia, Moyonimwe utasema, kuvuna watarajia, Maua huja chutama, matawini kuchanua, Hachumi asiyepanda, ndiyo mambo ya dunia. Matunda hujichumia, yawivapo ukachuma, Uanze kushangilia, upatapo tunda jema, Ni wapi umesiki, asiyepanda huchuma? Hachumi asiyepanda, ndiyo mambo ya dunia. Unapotaka kuchuma, ndugu yangu nakwambia, Tia mbegu ukilima,nambari wani hatua, Watarajia kuchuma, ndipo utajivunia, Hachumi asiyepanda, ndiyo mambo ya dunia. Beti sita nakimbia, nipande nipate chuma, Ujuzi mekugawia, elimu yenye heshima, Usijekuliwania, usilopanda kuchuma, Hachumi asiyepanda, ndiyo mambo ya dunia. Mtunzi Filieda Sanga MAMA B Mabibo Dsm 0753738704 RE: SHAIRI: HACHUMI ASIYEPANDA - MwlMlela - 08-11-2021 Mashairi mazuri sana haya.Watunzi endeleeni kuonesha kipaji na Mola awatie nguvu |