SHAIRI: HATUKUWA BINADAMU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: HATUKUWA BINADAMU (/showthread.php?tid=822) |
SHAIRI: HATUKUWA BINADAMU - MwlMaeda - 08-10-2021 HATUKUWA BINADAMU Enzi zile za mababu, mke alikuwa nyani, Hali tukipata tabu, tukateswa majumbani, Kipigo nazo sulubu, vilikuwa maungoni, Hatukuwa binadamu! Kituona wanawake, meno hatuna vinywani, Ni mangumi na mateke, meno yaanguke chini, Na utake usitake, tulibakwa vitandani, Hakuwa binadamu! Yetu kazi ni uzazi, hatukuwa na thamani, Ni duni yetu mavazi, mapaufu migongoni, Pengine liitwa mbuzi, nayo majina ya nyuni, Hatukuwa binadamu! Mwiko kupata elimu, kutwa twapika jikoni, Cheo hata umakamu, vilibakia ndotoni, Mbaya ule msimu, nimekumbuka zamani, Hatukuwa binadamu! Tuamkeni insia, toka hapo kitandani, Kiti tumekikalia, raia nambari wani, Letu jina Ni Samia, mwenye vazi la kijani, Hatukuwa binadamu! Nashangaa wanawake, wanakiri hadharani, Eti nao watamke afanyacho hatuoni, Wanawake niwatake, Samia mteteeni, Hatuwa binadamu! Vita si lelemama, mke kubaki kitini, Lazima kutuandama, kututia makosani, Kucha wakitusakama, eti tunaweza nini, Hatukuwa binadamu! Semeni oye Samia, wamama tuunganeni, Mwakana tucholilia, twende kule utumwani? Kidete kusimamia, mtieni masifuni, Hatukuwa binadamu! Na huu ndio ushindi, anayebisha ni nani? Wanawake kwa vikundi, imara tusimameni, Tujue siye washindi, tumeshinda utumwani, Hatukuwa binadamu! Niwaamshe fikara, wanawake pulikani, Vita sio masihara, habari hizi shikeni, Japo hatuna vipara, zetu silaha shikeni, Hatukuwa binadamu! Mtunzi Filieda Sanga MAMA B Mabibo Dsm 0753738704 |