SHAIRI: NIMEKUTUNUKU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: NIMEKUTUNUKU (/showthread.php?tid=809) |
SHAIRI: NIMEKUTUNUKU - MwlMaeda - 08-09-2021 NIMEKUTUNUKU Moyo hivi udundavyo, papasa changu kifua, Na ndivyo hali ilivyo, nisije nikaugua, Lazizi nikupendavyo, nashindwa kumsimulia. Wengine ni majangili, mume wewe peke yako. Wapo wale wanodhani, kupenda ninatania, Nawatia darasani, wajue nimepania, Wote nawaona nyani, viumbe wenye udhia Wengine ni majangili, mume wewe peke yako. Majina nitawataja, wakizidi nisumbua, Wao mmojammoja, kikashani hunijia, Sasa ninasema ngoja, siku nitawaumbua, Wengine ni majangili, mume wewe peke yako. Hawachi nibembeleza, nipendacho watajia, Sanga ninawapuuza, jicho nikawatupia, Hawaachi nichokoza, zote Mara hunijia, Wengine ni majangili, mume wewe peke yako. Kwakowe nimeridhika, tufurahie dunia, Wanipa ninachotaka, ya nini kujisumbua, Waniita malaika, kiumbe kunisifia, Wengine ni majangili, mume wewe peke yako. Beti hizi safusafu, mwendani nakutungia, Wewe ndiwe mausufu, haki vema unajua, Matendo matakatifu, mbinuze unazifua, Wengine ni majangili, mume wewe peke yako. Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |