SHAIRI: ALWATANI WA MJINI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: ALWATANI WA MJINI (/showthread.php?tid=794) |
SHAIRI: ALWATANI WA MJINI - MwlMaeda - 08-07-2021 ALWATANI WA MJINI Walozaliwa mjini, na wakakulia huko, siye wana wa shambani, tunayo mengi kuliko. Tunayo mengi kuliko, tuzidiyo wa mjini, haswa tufikapo huko, tunapotoka porini. Tukiwasili mjini, ushamba twaacha huko, ya kwenu twayajueni, kuongezeya ya huko. Ila nyie wanamji, mnalo tu moja shiko, ilhali wa shambani, tuna mawili mashiko. Kwetu siye ni shambani, na twajua kwenu huko, huku nyie wa mjini, hamwelewi kwetu huko. Alwatani wa mjini, twawazidi mengi huko, ingawa tuko shambani, tunayo mambo kuliko. Mjitapapo wa huko, eti mi aluwatani, mji ndio langu shiko, uhishimu wa shambani. Wengi wenu wa mjini, mwakufahamu tu huko, wengi tulio shambani, twajua huku na huko. Mkifika kwetu huko, mkapotea porini, vigumu kutoka huko, wa mjini alwatani. ?Rwaka rwa Kagarama, Mzee wa shamba.?? |