SHAIRI: PUA UTAANGUKIA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: PUA UTAANGUKIA (/showthread.php?tid=775) |
SHAIRI: PUA UTAANGUKIA - MwlMaeda - 08-05-2021 PUA UTAANGUKIA Chambililecho Waswahili, lihiswaha cholembicha, Nisikilize rijali, hata Kama umechacha, Si Leo toka awali, walisema magalacha, Mpenda Cha bure boza, jiangalie kijana. Jiangalie kijana, kwa macho ya kupikicha, Nakumbuka mwakajana, yaliyomkuta Chacha, Alidhani amevuna, kumbe kazoa makucha, Mpenda Cha bure boza, jiangalie kijana. Unasema utajiri, wa kuzoa na kuacha, Tuambie hiyo siri, masikio kupekecha, Mimi naona hatari, hata Kama wewe ticha, Mpenda Cha bure boza, jiangalie kijana. Hamu imekuishia, beti chache ninaacha, Si kwamba nimefulia, Mimi bado nipo chicha, Kichwa kimeniregea, naona Bora kuacha, Mpenda Cha bure boza, jiangalie kijana. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |