SHAIRI: HAKI ZETU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: HAKI ZETU (/showthread.php?tid=774) |
SHAIRI: HAKI ZETU - MwlMaeda - 08-05-2021 HAKI ZETU Acha watoto wadogo, waje kwangu Yesu Bwana, Watoto sio mzigo, muanze kututukana, Pia ukali wa mbogo, unatuumiza sana, Sisi watoto wadogo, zetu haki tupatiwe. Kwanza haki ya malazi, yawe Safi na salama, Pia na yetu mavazi, Yale yenye sia njema, Chakula enyi Wazazi, katu msijetunyima, Sisi watoto wadogo, zetu haki tupatiwe. Ulinzi na usalama, hivyo ni muhimu kwetu, Tuwe na afia njema, na matendo yenye utu, Tuoneeni huruma, jueni sisi ni watu, Sisi watoto wadogo, zetu haki tupatiwe. Kingine kitu elimu, tutieni darasani, Na mahitaji muhimu, ya shule tupatieni, Mfanowe yunifomu, na viatu mguuni, Sisi watoto wadogo, zetu haki tupatiwe. Twataka kusikilizwa, yetu mawazo watoto, Tumechoka kuumizwa, kwa majeraha ya Moto, Na bakora kuchakazwa, twangalieni watoto, Sisi watoto wadogo, zetu haki tupatiwe. Ubakaji ulawiti, siku hizi vimezidi, Hutukuta umaiti, kwa mambo ya kigaidi, Nchi inatusaliti, kuteseka tuna budi, Sisi watoto wadogo, zetu haki tupatiwe. Nyumbani tunanyanyaswa, hatuna raha jamani, Malezi tunayopaswa, Leo hayaonekani, Taabini tumenaswa, twendeni wapi jamani, sisi watoto wadogo, zetu haki tupatiwe. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 RE: SHAIRI: HAKI ZETU - John John - 09-02-2021 (08-05-2021, 08:11 PM)MwlMaeda Wrote: HAKI ZETU Safi sana mtunzi |