HADITHI FUPI YA KISWAHILI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: HADITHI FUPI YA KISWAHILI (/showthread.php?tid=772) |
HADITHI FUPI YA KISWAHILI - MwlMaeda - 08-05-2021 Wataalamu wengi hasa wale wa awali waliamini kuwa hadithi fupi ni utanzu wa riwaya lakini baadaye mwishoni mwa miaka ya 1990, wataalamu mbalimbali walisema hadithi fupi na riwaya ni vitu viwili tofauti. Mfano: WAMITILA anasema;
Hadithi fupi si sura katika riwaya, tukio au kituko ambacho kimechopolewa katika hadithi fupi au kisa kirefu, bali humvutia na kumleta msomaji na kumfanya aamini kuwa ingeweza kuharibika ikiwa itakuzwa na kuwa ndefu au kama itafanywa sehemu ya kazi kubwa. Naye NGURE, 2003:1-2 anasema; Hadithi fupi ni masimulizi ya kubuni yaliyoandikwa juu ya tajiri na maisha. Sifa yake kuu ni ufupi ambao ni tofauti na riwaya. Hadithi zenye mbano wa wahusika, mbano wa mandhari, mbano wa maudhui ina dhamira moja.
SIFA ZA HADITHI FUPI
1. Mara nyingi ni fupi na huweza kusomeka kwenye mkao mmoja.
2. Ina athari ya aina moja.
3. Inakuwa na ufinyu wa wahusika; wahusika hawafafanuliwi kwa kina
4. Haiwi na uchangamani wa mandhari, muundo na mtindo; sehemu hizo hazielezwi kwa kina.
5. Huishia na taharuki; haimalizi simulizi
|