SHAIRI: KILE KIJUNGU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: KILE KIJUNGU (/showthread.php?tid=750) |
SHAIRI: KILE KIJUNGU - MwlMaeda - 08-03-2021 KILE KIJUNGU Kijungu chafikirisha,nawaza nafika mbali Tena kinanikumbusha,waandishi mbalimbali Kimbunga chapeperusha,kinachoishi kivuli? Nakumbuka babu yangu,maruhumu Haji Gora Ama kijungu ni kile,cha wale wasaka tonge? Tulowasikia kale,ndicho chaleta mazonge Sasa wamekuwa kwale,wanayaunda magenge Ninamkumbuka gwiji,maruhumu Haji Gora Au ni miradi bubu,yao wale wazalendo? Yatuletea aibu,tukwame tukose mwendo Hima mama toa jibu,usipite kandokando Namkumbuka gambera,maruhumu Haji Gora Kama ni ile Fungate,Ya Uhuru imekwisha Twambie tumkamate,uma anaepotosha Sema sisi tukufuate,mama anza kuwanyosha Siwachi kukukumbuka,maruhumu Haji Gora Hivi wamba hili jungu,ni la watoto na mama? Mama ntilie Mungu,alomtwaa mapema Samia hii mizungu,wenzako tumeshakwama Wafumba mithili baba,yule alotoka mbali Kifo kilipomkaba,roho iukache mwili Wanawe wenye mahaba,walimuezeka swali Babu alisema mali,wangeipata shambani Abdul Ndembo(Wingu zito) Mburahati sekondari |