SHAIRI: MWIZI HUJAMBAINI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: MWIZI HUJAMBAINI (/showthread.php?tid=749) |
SHAIRI: MWIZI HUJAMBAINI - MwlMaeda - 08-03-2021 MWIZI HUJAMBAINI Hai hai majiani, yangu njia kwa mganga, Asitiwe matatani, Nkwazi nguvu kumfunga, Mwizi ukimbaini, tatamani kwenda Tanga, Ni bure wamuandama, mwizi hujambaini. Kunaye kijana Njau, mwangalie mara mbili, Huyo hunijia juu, adai yeye rijali, Analeta madharau, asema wewe tumbili, Ni bure wamuandama, mwizi hujambaini. Unamponza ushenga, Nkwazi si mwizi halali, Ila Njau huyo chunga, asema halali hali, Adai wewe mchanga, hujui lile na hili, Ni bure wamuandama, mwizi hujambaini. Juzi alinipigia, kanambia twende mbali, Wewe tukakukimbia, ulie ukonde mwili, Japo anifwatilia, mwenyewe simkubali, Bure unamuandama, mwizi hujambaini. Sasa mwambie mganga, lile jina kubadili, Na Nkwazi ampe kinga, asije kumtapeli, Asije kutangatanga, akifikia mahali, Bure unamuandama, mwizi hujambaini. Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |