SHAIRI: DUDU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: DUDU (/showthread.php?tid=744) |
SHAIRI: DUDU - MwlMaeda - 08-03-2021 DUDU Mganga unipe dudu,nikamdhuru Nkwazi Alale asijimudu,nitakupa hata mbuzi Mno amenihusudu,kusema sana siwezi Kumbe ni yeye kikwazo,Filieda hanitaki Fungu lako nitakupa,mroge atapetape Ahame asiwe hapa,tena mtie mapepe Kaja jijini kwa pupa,sasa acheze mahepe Kumbe ni yeye kikwazo,Filieda hanitaki Kwani anampa nini,babu ramli tazama Ashinde majalalani,hadi jua likizama Mimi mwana wa mjini,mwaka huu atakoma Kumbe ni yeye kikwazo,Filieda hanitaki Babu jini jipya tuma,lisiende lilokongwe Asiweze kuchutama,kwenye kiuno agongwe Ashindwe na kula nyama,japo maungo asingwe Kumbe ni yeye kikwazo,Filieda hanitaki Fundi tamati shairi,kama huwezi nambie Kitanzi changu tayari,kamba nijitundikie Maisha kwangu shubiri,afadhali nikimbie Abdul Ndembo Mabibo sekondari |