MISEMO YA VYOMBO VYA USAFIRI (1) - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Semi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=49) +---- Thread: MISEMO YA VYOMBO VYA USAFIRI (1) (/showthread.php?tid=732) |
MISEMO YA VYOMBO VYA USAFIRI (1) - MwlMaeda - 08-02-2021 Misemo yenye Ujumbe kuhusu Imani za Dini
1. “Mungu tu hana wivu”
Maana:
· Viumbe wote ulimwenguni wana uwezekano wa kuwa
na wivu, isipokuwa Mwenyezi Mungu. · Binadamu huwa na kawaida ya kumwonea gere
mwenzake hasa anapopata mafanikio katika kazi au biashara. · Mungu humjalia kila mja wake/kila mtu.
· Mungu hana upendeleo, choyo, wala aina nyingine
yoyote ya tabia mbaya. 2. “Mungu ni mmoja”
Maana
· Mungu ni yuleyule anayempa huyu na kumnyima
mwingine. · Mungu ni wa watu wote.
· Sote twamuabudu Mungu huyohuyo ijapokuwa
tunatofautiana kiimani na kimadhehebu. 3. “Aliyekupa wewe ndiye aliyeninyima mimi”
Maana
· Riziki hugawiwa na Mwenyezi Mungu, sio binadamu.
· Usimcheke wala kumdharau mwenye hali duni ya
kimaisha, kwani ndivyo alivyojaaliwa na Mungu. · Wenye hali nzuri ya kimaisha (kipato) wasijione
kuwa wapo hivyo kwa jitihada zao pekee, kwani Mungu ndiye aliyewajaalia. 4. “Mungu asamehe ndimi zetu”
Maana
· Mungu asamehe kauli zetu.
· Huwa tunajinenea mengi mabaya au kuwanenea
wengine mabaya kwa kujua au bila kujua, hivyo, Mungu asamehe yale mabaya tunayoyanena. · Mungu awe na huruma kwa waja wake.
5. “Mungu akiendesha, shetani haombi lifti”
Maana
· Nguvu ya Mungu ni ya kipekee, haina mshindani.
· Mungu akisimamia jambo, shetani hana nafasi.
· Mtu akimwamini Mungu, hawezi kughilibiwa na
shetani. 6. “Silaha yangu msalaba”
Maana
· Imani kuwa hakuna jambo lolote linaloweza kufanyika
bila nguvu ya msalaba. · Alama ya kuwa na imani thabiti ya Kikristo.
7. “Nina furaha kuzaliwa Mwislam”
Maana
· Anaona fahari kuwa Muislamu
· Anaipenda dini ya Kiislamu.
8. “Shukuru kwa kila jambo”
Maelezo:
Msemo huu,
aghalabu, hutumiwa katika mazingira ya kitanzia; yaani, pale ambapo mtu hukutwa na jambo lenye kuumiza, kutia majonzi au simanzi. Maana
· Tunatakiwa kushukuru pale tupatapo mafanikio au
matatizo. · Mtu anapaswa kushukuru hata kwa tatizo au janga linalomtokea. Hutakiwa kushukuru hata janga au tatizo hilo kwa sababu huenda
angepatwa na kubwa zaidi ya hilo, lakini Mungu akaamua alipitishe mbali kupitia hilo dogo. · Binadamu anapaswa kuwa na moyo wa kuridhika na
kila alichonacho, akipatacho au kimtokeacho. 9. “Allah Akbar”
Tafsiri:
Huu ni msemo ulio katika lugha ya Kiarabu. Maana yake ni Mwenyezi Mungu (ni) mkubwa.
Maana
· Mungu ndiye Mkuu wa viumbe wote duniani.
· Mungu ndiye Muweza wa kila jambo.
10. “Asante Mungu”
Maana
· Shukrani zote anastahili Mungu (kwa yote
ayatendayo kwa viumbe wake). · Tunapaswa kushukuru kwa kila jambo (liwe zuri
lenye kufurahisha au baya lenye kuhuzunisha au kuumiza). 11. “Allah Karim”
Maana
· Mwenyezi Mungu
ni mkarimu kwa kila kiumbe. 12. “Acha pupa, Mungu atakupa; kama si nyama,
hata mfupa” Maana
· Mja yeyote anapaswa kumtegemea Mungu katika
upatikanaji au ukosekanaji wa riziki yake. · Kutafuta maisha kwahitaji uvumilivu na imani ya Mungu.
· Mtua anatakiwa awe tayari kupokea chochote
ambacho Mungu anampa. · Kupata ni kupata, kiwe kidogo au kikubwa; muhimu
kuvumilia. 13. “In God we trust”
Tafsiri:
Huu ni msemo
ulio katika lugha ya Kiingereza. Maana yake ya jumla ni ‘Tunamwamini Mwenyezi mungu’. Maana
· Mungu pekee ndiye wa kuaminiwa na kutegemewa.
· Mungu ndiye Muweza wa kila jambo.
14. “Kwa Mungu hakuna rushwa”
Maana
· Mungu ndiye pekee anayetenda haki.
· Mungu hamwonei mja wake.
· Kwa Mungu kuna haki.
· Duniani hakuna haki.
· Mungu ndiye anayehukumu viumbe wake wote.
15. “Kwa Mungu si kwa mzungu”
Maana
· Hata mtu awe bora kiasi gani hawezi kufanana na Mungu.
· Mungu hafananishwi na kiumbe yeyote.
· Mungu ndiye mfalme wa ulimwengu mzima.
16. “Bwana awe nanyi”
Maana
· Mungu awe pamoja nanyi.
· Salamu kwenu.
17. “Kwa rehema zake Mungu”
Maana
· (Mafanikio niliyonayo) ni matokeo ya upendo au Baraka
kutoka kwa Mungu. · Mungu ndiye anayetoa riziki.
· Mungu hutenda mema kwa waja wake.
18. “Yesu ni jibu”
Maana
· Yesu pekee anastahili kuabudiwa.
· Yesu ndiye mwokozi.
19. “Heri wenye moyo safi”
Maana
· Ni vema mwanadamu akatenda matendo mema maana
huwa na malipo hapa duniani na akhera. 20. “Kazi na sala
Maana
· Haya mambo mawili (kufanya kazi na kumwabudu Mungu)
ndio msingi wa mafanikio ya wanadamu. · Kufanya kazi peke yake hakuwezi kumletea mtu
ustawi kamili. Chanzo:
Ponera, A. S na Kikula, I.S, (2017) Misemo ya Vyombo vya Usafiri. UDOM. Afroplus Industries, Ltd. |