MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

VIFAA VYA MTAALA - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
VIFAA VYA MTAALA - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Zana za kufundishia (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=69)
+--- Thread: VIFAA VYA MTAALA (/showthread.php?tid=706)

VIFAA VYA MTAALA - MwlMaeda - 08-01-2021

VIFAA VYA MTAALA
Mtaala una vifaa vyake maalumu ambavyo vinatakiwa vitumike kwa usahihi ili kutekeleza mtaala kwa ufaninsi. Vifaa hivyo ni;
  1. Muhtasari
  2. Vitabu vya kiada
  3. Kiongozi cha mwalimu
  4. Kitabu cha mwalimu na
  5. Rejea.
MATAYARISHO YA UFUNDISHAJI
Matayarisho ya ufundishaji ni ile hali ya mwalimu kuandaa zana na vifaa muhimu kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia
UMUHIMU WA MATAYARISHO YA UFUNDISHAJI
Kazi ya kufundisha ni kazi ya kitaalamu hivyo inahitaji maandalizi wakati wote. Hivyo basi mwalimu anapaswa kufanya maandalizi ya kutosha kabla ya kuingia darasani kufundisha na kwa mantiki hiyo mwalimu analazimika kujiandaa ili kuepuka matatizo yafuatayo wakati wa kufundisha na kujifunza.
  • Kukosa mtiririko unaofaa wa ufundisahaji
  • Kufundisha kwa kubahatisha au kubabaisha
  • Kuchosha wanafunzi katika kujifunza
  • Uwezekano wa kupotosha maudhui
  • Kushindwa kutunza muda
  • Kushindwa kukidhi matarajio ya somo na ya wanafunzi
  • Kujiamini au kutojiamini kusiko na misingi dhahiri
Kumbuka:
Ili Mwalimu aweze kukamilika katika maandalizi yake ya ufundishaji wa kila siku ni muhimu awe na baadhi ya vifaa ambavyo ndivyo msingi muhimu na muongozo muhimu wa kazi yake. Miongoni mwa vifaa hivyo ni:
  1. Muhtasari wa somo
  2. Azimio la Kazi
  3. Andalio la Somo
  4. Shajara la somo nk.